Saturday, 27 June 2009

Mume Cheated, sasa anadai tupeane nafasi-Ushauri

"Hi, wadau mwenzenu nina shida, mnajua toka mume wangu acheat wakati nina mimba, sijamsamehe. Tunaongea vizuri na tunalea familia vizuri, ila tatizo nikikumbuka maudhi ya mume wangu basi naacha huduma zote na chumba nahama.

Nakaa hata wiki then tunaongea narudi, najaribu kumsamehe na kusahau nashindwa, nakuwa jeuri sana siwajibiki chochote kuhusu mume. Na hii jeuri inakuwepo muda mwingi zaidi kuliko amani.

Sasa eti kaja na solution, eti we need space from each other so mimi nirudi kwetu kwa atleast 3 weeks or 1 month.. Nikamwambia "mie siendi popote coz siwezi kuacha watoto wangu na I dont need any space. Kama he needs hata yeye ana kwao aende tu. Mi mi kama nitaondoka ni 4 good na naondoka na TALAKA yangu mkononi". Akasema hatuachani ila tunarekebishana. Hapo wadau nisaidieni kuna cha kurekebishana au ana yake?"

Dinah anasema:Pole sana Mdada kwa unayokabiliana nayo, watu hawaelewi ni namna gani kuwa cheated on inauma na ni ngumu kiasi gani kusahau. Unaweza kusamehe vema kabisa , well ukadhani umesamehe (huwezi kusamehe kama huwezi kusahau) na ukawa unazungumza na mumeo lakini uhusiano wenu ninyi wawili hautakuwa the same again unless huyo aliyekosa (kwa case yako Mumeo) afanye kazi ya ziada ili wewe uweze kumuamini tena na hatimae kusahau aliyokutenda......hebu bofya hapa kwa maelezo ambayo yanaweza kukusaidia kiasi fulani.

Sio kwamba unakiburi bali unahasira kutokana na kitendo chake kichafu na hujafanikiwa kusamehe kama ulivyodai mwenyewe kitu ambacho kinaongeza ugumu zaidi kwenye kusahau na kuganga ya mbele. Ingekuwa yeye ndio katendwa yaani kama wewe ndio ungekuwa ume-cheat on him sidhani kama angekuwa na wewe by this time.....angekutwanga TALAKA siku hiyo hiyo.

Nimekutana na watu wachache wenye tatizo kama lako na niliwasaidia na wakafanikiwa na sasa wako pamoja wakiendelea na ndoa zao, na huko ndiko nilikopatia uzoefu na hivyo kujiamini ktk kulielezea hili suala la cheating.

Kwa mtu ambae hajawahi kukutwa na tatizo hili ningumu sana kwake kujua ugumu na maumivu yake na hivyo kudhani kuwa wewe unakiburi tu na unachezea shilingi chooni, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa, unampenda mumeo, unataka sana kuendelea kuwa kwenye ndoa lakini hujui how to 4get and move on, kwasababu 1)-huji kwanini alifanya hivyo(cheat), 2)-Je umenusurika dhini ya maambukizo? 3)- Kwanini yeye hana habari na anachukulia kawaida (kwa vile hajaomba msamaha) na maswali mengine lundo.

Wewe kuwa mjamzito ni moja ya sababu kati ya zile nyingi ambazo wanaume huzitumia kama sababu kwa nini hutereza nje a.k.a cheat,.

Tatizo lililopo hivi sasa si yeye ku-cheat japokuwa ndio sababu, ninachokiona hapo ni mume wako kuwa na Majivuno (proud of himself) kwa vile tu yeye ni mwanaume na wewe kuwa needy na muoga kudai haki yako. Kingine ni ukosefu wa maswalisiliano baina yenu.

Mwanaume yeyote ambae hana majivuno na anathamini ndoa yake hawezi kukaa ziku zote hizo bila kuomba msamaha kuhusiana na tabia yake chafu, unless huna uhakika na unahisi tu kitu ambacho kitakufanya ushindwe kuwakilisha hoja.

Kama mgewasiliana kuhusu tukio lililotokea wakati wewe mjamzito na unauhakika kweli alikusaliti ni wazi kuwa angeomba msamaha na kuahidi kuacha hiyo tabia na kubadilika kuwa a loving hubby kwako na a great father kwa watoto wenu.

Cheating sio kitu kizuri na ni sawasawa kabisa na yule muuaji(inategemea na reaction ya mhusika), lakini haina maana kuwa ndio mwisho wa ndoa yenu au mwisho wa uhusiano wenu. Inawezekana kabisa kutokana na tukio hilo mkawa the best couple (am not asking u to cheat on ur lover ili kuwa best...hapana), ila kwa bahati mbaya ikitokea na uko kwenye ndoa kuna hatua za kufuata na kuna njia ya kukabiliana na hilo.

Nini cha kufanya:Kwanza kabisa unatakiwa kujua umesimama wapi na unataka nini out of ndoa yako?
1)- Je unampenda mumeo na ungependa ku-work things aout na mumeo ili ndoa iendelee kuwepo na iwe yenye amani na upendo?(Kuna mengi ya kufanyia kazi ili kufanikisha hilo)

2)-Je Penzi limepauka/chujuka ila unamheshimukwa vile ni baba wa watoto wenu na unahofia watoto wenu wasilelewe na mzazi mmoja ikiwa utatoka ndoani?(Mkiweka mipangilio mizuri watoto watalelewa na ninyi wote, lakini kujilazimisha kukaa kwenye ndoa wakati huna furaha sio afya kwako)

3)-Unahitaji muda zaidi kuponyeka kabla hujafanya uamuzi wa busara? (hapa utahitaji kutengana nae kwa muda ili ku-sort our ur feelings and ur head).

Sasa kutokana na kitendo chake cha kukusaliti unadhani kuwa ukiondoka na kwenda nyumbani yeye atahamishia makazi kwa huyo mwanamke mwingine si ndio? Vipi ikiwa yeye ataondoka nakukuacha hapo nyumbani? Unauhakikahuko aendako ni nyumbani kweli na je itakuwaje kama atabeba na huyo msaliti mwenzie kwenda huko wote? Mana'ke kuna nyumba za wageni na wanaweza kutumia.........

Sulihusho hapa ni kupeana nafasi (kama alivyodai mwenyewe) ili kuona kama kweli bado mnapendana na mnataka ndoa yenu iendelee kuwepo lakini kutokana na hali halisi ya uhusiano wenu itakuwa ngumu kwa vile wewe humuamini tena mumeo.

Mimi nashauri wote wawili msafiri na kwenda mahali ambako hakuna ndugu wala jamaa, mkakae hotelini na huko muende kujaribu kurekebisha mambo baina yenu, kitendo cha kukaa ninyi wawili pakeenu na kuwatumia muda wote pamoja kufanya mambo tofauti ya kufurahi (msihusihe ngono) itasaidia kujua hisia zenu na namna gani mnahitajiana ktk maisha yenu.

Pia itasaidia ninyi wawili kutaka kuzungumza kuhusu maisha yenu, kumbuka siku zote naamini kuwa mwanamke ndio mtu pekee anaweza kubomboa au kujenga ndoa yake......hivyo basi jukumu hili liko mikononi mwako kwahiyo ni wewe pekee ndio uko upande wa kulianzisha na kulizungumzia tatizo lililopo kwenye ndoa yenu hivi sasa.

Lakini je utamuanzaje ili akubali?-Ili kumpata kwanza kabisa muombe msamaha kwa kumtamkia Talaka na kubishia wazo lake la kutengana kwa muda. Mwambie kwa uwazi na kwa upole kuwa hudhani kama ni idea nzuri kutengana na unadhani kuwa mnahitaji kutumia muda mwingi peke yanu bila ndugu, watoto na marafiki ili kusort things out.

Sema kuwa, ikiwa yeye au wewe utasafiri na kuwa mbali mbali itaongeza matatizo badala ya kuyamaliza. Mueleze kuwa mnahitaji muda wa kutosha ili kuzungumza na kurudisha the romance kwenye ndoa yenu kwani unahisi imetoweka ghafla na unadhani inawezekana kabisa ni kutokana na vitendo vyako ambavyo unavifanya kutokana na sababu ambayo utamueleza muda ukifika (hii itampa hamu ya kutaka kujua), na kama kweli alikusaliti atang'amua then na kama hakukusaliti basi atasubiri au anaweza ku-demand umwambie....

Wewe usimwambie mpaka mtakapo safiri nje ya mji au mkoa mwingine.....Kama mnaishi Tz basi Morogoro pale pametulia, Arusha pia kuzuri, Bagamoyo, Kigamboni kule kuna Hotel moja bomba kabisa kwa ajili ya kupumzikia mwisho wa wiki....lakini kuzuri kabisa nadhani ni kwenye Mbuga za wanyama kutokana na asilia ya nchi itawasaidia muwe na mood nzuri zaidi....


Weka wazi hisia zako zilizoumizwa ili mumeo aelewe kuwa bado linakuuma na huwezi kabisaa kusahau (ikiwa unauhakika na usaliti wake). Unajitahidi kusamehe lakini msamaha haukamiliki ikiwa yeye mumeo hajakubali kuwa alikosa na kukuomba msamaha.....kama mwanamke natambua unafanya vyote hivyo kwa kudhani kuwa yeye mumeo atang'amua unataka nini kutoka kwake.

Kwa bahati mbaya hawezi kusoma via vitendo vyako wala hawezi kujua yaliyokichwani mwako isipokuwa pale utakapoamua kuliweka wazi ktk mtindo wa kuwasiliana. Ukiendelea hivyo ataamua kwenda kutafuta amani sehemu nyingine na wewe utabaki unaumia even more.

Ikiwa hunauhakika na usaliti wake pia mueleze kuwa ulipokuwa mjamzito ulikuwa unahisi au kama uliambiwa bsi sema wazi kuwa kuna watu walikuambia kuwa mumeo anatoka na mtu fulani na tangu siku hiyo imani nae mumeo imekutoka na hunashindwa kumuamini tena.

Kama akikana kutokana na tuhuma hizo (ikiwa huna uhakika) then inabidi kuwekeana rules kama inawezekana ili kukuongezea au kukurudishia wewe ile hali ya uaminifu juu yake mume(kwamba uanze kumuamini tena).

Ndoa ni ngumu sana kama hakuna mawasiliano ya kutosha au hujui namna ya kuwasiliana na mwenza wako, ndoa ni ngumu kama hakuna uaminifu baina yenu, ndoa ni ngumu kama hakuna maelewano wala masikilizano, ndoa inaweza kuwa ndoano kama hakuna amani ndani ya nyumba yenu.

Ndoa ni our third job kwa wale wote wenye kazi, watoto na waume/wake pia ni our second job kwa wale wote ambao bado hamjazaa lakini mna wake/waume na kazi. Hivyo tukitaka ndoa zetu ziwe Imara, bora, nzuri, zenye furaha na amani hatuna budi kuwajibika na kuzifanyia kazi kila siku iendayo kwa Mungu kama vile unavyokwenda kazini kila siku ili kulipwa mshahara lakini tofauti ya ndoa ni kuwa haina mwisho wa wiki wala likizo ila malipo yake ni zaidi ya Mshahara ikiwa utawajibika vema.

Nakutakia kila la kheri ktk kurudisha ndoa yake kwenye track kama kweli unataka kuendelea kuwa ndani yake.

Ubarikiwe!

Friday, 26 June 2009

Nilipinduliwa nikaolewa tena ila mume2 simuelewi-Ushauri

"Dear Dinah
Mimi ni mdada wa miaka 28 niliolewa na mume wa kwanza na nilijaliwa kupata nae watoto
wawili.Mume alikua hodari sana kwa kila kitu katika mambo ya ndoa na tulipendana
sana hadi nilipopinduliwa na mwanamke mwenzangu bahati yake sasa ndio anakula raha
zote.

Nilivumilia saana baada ya kupinduliwa kwa vile mwanamme tulipendana saana
na hasa nilizingatia kuhusu watoto kwani alionyesha mapenzi saana pia kwa watoto wetu wa
kinyume na sasa nilivyoachika.

Kama unavyojua ndoa za waislam ni mwaname ndio
anapoama kumuacha mwanamke huwa na haki japo wewe bado unampenda akiamua
kukuacha huwa halazimishwi kuwa na wewe ila mwanamke ni hadi uwe na sababu
ya kimsingi kama vile ametaka tigo au analewa na hakutimizii mahitaji, lakini mambo mengine
huwa huwezi kuachika!

Dinah anasema: Hii wala sio haki, mwanamke unakandamizwa kwa kenda mbele kha! Eti mpaka uwe na sababu. Pole kwa kuachwa ukiwa bado unampenda mumeo wa kwanza.

Anyway hayo yamepita! Nilikaa nimeumia kwa muda wa miaka sita sikutamani tena
mwaname yoyote kwani pale nilipoishi sikupata mwaname aliemfikia ex wangu hata robo
yake kwa hiyo nikaendesha tu maisha yangu mwenyewe na watoto wangu.

Kama unavyojua jinsia hasa mwanamke ukishaolewa na kuonja utamu wa ngono,
nilifanikiwa kumpata mwaname mwingine nchi nyingine lakini alikua na asili ya nchi
yangu lakini tu alizaliwa kule. Sasa tulikubaliana kuowana na tukajaliwa kuishi
nchi ambayo niliishi mimi. Na huyu pia tulipendana sana ila kwa bahati mbaya
hakuweza kupata kazi kwani nchi hiyo ilikua na ubaguzi sana wa wageni!


Nilibahatika kushika mimba na nilitabiriwa kuwa nitazaa mtoto wa kiume
kitu ambacho kilinifanya niende ughaibuni mwa Ulaya kwani ningezaa mtoto
wa kiume nchini mwangu baada ya muda mtoto huyo angelazimika arudi
kwao kwani watoto hawafati mama! Tulikubaliana vizuri na mume wangu
na tulikua tunawasiliana kama kawaida na mapenzi yalikua mazuri tu.

Kitu cha kushangaza niliposettle huko ulaya ughaibuni mwenzangu
kanibadilikia kabisa! Namfahamisha njia za wenzie wanavyofanya
ili tuweze kuishi pamoja lakini haonyeshi interest kabisa kuja kuishi
na mimi na kisingizio eti wenzake wamemwambia maneno mengi kuhusu
mimi eti namsema na kusema namsimanga!

Na kibaya kabisa hata mtoto wake ambae toka azaliwe hajamuona, hamjali kabisa
na sasa ndio hana hata mawasiliano na nikimpigia simu anaongea
kama kalazimishwa! Nikimuandikia email hajibu!

Nimejitahidi kufuata mafunzo yangu niliyofundishwa, kwani na mie pia kabla ya hii blong
yako nilialikwa na hadi nilikua nyakanga nimejitahidi kumfanyiakila aina ya mapenzi ili kuboresha ndoa yetu, ikiweno kumsemesha maneno mazuri vitendo na hata kumvumilia na wakati mwingine hata kujifanya mtumwa kwake pia huchangia mafunzo yote
ninayoyapata kumtumia na yeye pia kama general kwani nahofia yeye ni negative thinking na hapendi kuambiwa.

Eti unamfundisha lakini mwaname habadilika kabisa! Najua ananipenda lakini anapenda kunitesa kwani nimeshadai talaka hadi nimechoka haniachi na huniignore tu pindi nikiomba talaka!

Kibaya zaidi pindi nikimwambia mapenzi au kufanya mambo mazuri huwa
haonyeshi kufurahia kabisa lakini nastahimili na kushindwa, nikilalamika
hapo ndio hujibu Bomu yaani utajuta kuzaliwa na pia mara nyingi hupenda
kujibu urgument than mapenzi.

Imefikia hata hapo nchini kwangu hataki niende na hunipa sababu zake ambazo haziniingii akilini na nikilazimisha kwenda basi atanikimbia akae mbali eti kikazi hadi siku zangu ziishe nisafiri
na nikimpigia simu au kumtext hapokei au harudishi text au kupiga simu.


Alitokea kwenda kwao hata bila ya kuniambia na mimi kwa mapenzi yangu
nilifurahi na kutaka kumfuata lakini alivyojua nataka kwenda kwanza alinambia hakai
sana amekwenda tu kibisahara kidogo, nilivyosema nitakwenda na tutarudi nchi yangu
pamoja alinikatia hata simu akawa hapokei na matokeao nikaambiwa eti
simu niliyokua nampigia imeibiwa nikaona sasa huko ndio kukataliwa.


Nikawa najaribu hadi nikafanikiwa kumpata nchini mwangu nikawa naongea
nae lakini hana mood na hata nikimwambia naumwa au mtoto anaumwa
haonyeshi kutujali kabisa!

Email anasoma lakini hajibu kwani nikimpigia
huzungumzia salam alizozipata lakini hajibu na kila mara mie tu ndio
nimpigie na mara nyingi nikimpigia anakua hana mood ya kuongea na mimi!


Nampenda saana lakini naumia nimejitahidi sasa mwaka wa tatu lakini mwaname
haonyeshi hata dalili ya kubadilika!na anadharau sijapata kuona au kusikia!
naomba ushauri ndugu yenu nifanyaje kwani sipendi kuachika
na hata nikiachika sitamani tena mwanamme kwani wanaume
unakaa nao vizuri baada ya muda wanabadilika kitu kinakufanya
unachukia maisha yako na maisha ya ndoa na mapenzi kwa ujumla!.


Nimekaa kusoma tu za wenzangu huona mengine yanazidiana na yangu
lakini mimi sina raha ya maisha na hata mtoto wangu, na kila kitu kwangu
naona hakina faida ila nasoma dini yangu lakini mara nyingi huwa katika majonzi
na kuona kama mimi sina bahati duniani na leo nimeona na mimi nipate
ushauri kutoka kwako Dinah na wengine.
Ni mimi Salha"

Dinah anasema:Salha mpendwa asante kwa kunivumilia (nimekuwa busy kimtindo).
Ni mwanamke mvumilivu sana na sina budi kukupa hongera kwa hilo. Inasikitisha huyu mume wako wa sasa anasikiliza zaidi marafiki badala ya kujali maisha yake yeye kama yeye na familia yake ambayo ni wewe na mtoto aliyezaliwa.

Kama ulivyosema ndoa ya mwanzo ilikuwa ya kiislamu, sina shaka hata hii ya sasa ni ya kiislamu. Kwa mujibu wa Imani hii ya Dini inasemekana* (usininukuhu) kuwa mwanamke ni mtu wa kukaa ndani tu na mwanaume ndio mtu wa kujishughulisha na kuhakikisha anamtimizia mkewe mahitaji yake yote.

Apart from Imani hiyo ya Dini, utafutaji, uwindaji na kumuangalia mwanamke na kumpa mahitaji yake yote au kujitahidi angalau kidogo sio lazima yawe yote, wanaume wanaamini kuwa ni jukumu lao na hii ni kutokana na EGO zao as men.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa hajisikii vema au niseme hatuko comfortable wewe kumfanyia kila kitu na yeye anakaa tu akisubiri kupewa au kuambiwa nini cha kufanya (ulipokuwa unampa mbinu za kujiunga nawe huko Ulaya) na "mwanamke" si unajua wanaume wengine na dharau zao, wanadhani wanawake zetu ni ku gossip tu na hatuna uwezo wa kujituma na kufanya mambo makubwa kimaisha na kijamii.

Sasa tatizo la huyu mume wako wala sio kubwa sana japokuwa litachukua muda mrefu kidogo kwa yeye kubadilika, tatizo lake ni kutojiamini kama mwanaume na kujishitukia kuwa anapoteza uanamme wake kwa vile wewe ni mwanamke unaejituma na kumuangalia yeye na watoto wako.

Kuna uwezekano mkubwa akawa anadhani kuwa, mumeo wa zamani ambae ni baba wa watoto wawili wa mwanzo ndio anaerekebisha mambo hapo nyumbani na yeye kama mumeo wa sasa anahisi kuwa ni useless na njia pekee ya kuonyesha uanaume wake kwako ni kwa kuwa na kiburi, m-bishi au mkorofi ndani ya uhusiano wenu.

Mwenyewe umekili kuwa anakupenda na wewe unampenda hivyo basi sio mbaya kama mtajitahidi na kuifanya ndoa hiyo kuendelea na pia kuwa bora kwakurekebisha maeneo machache ambayo mimi nadhani ndio chanzo cha yeye ku-withdraw kama mpenzi.


Kitu muhimu hapa ni ninyi wawili kushirikiana na kuwa kitu kimoja kama mke na mume na wakati huohuo wapenzi, na ili kufanikisha hili mumeo anapaswa kuacha tabia ya kusikiliza zaidi watu wengine na kujitahidi kuwaridhisha ili asionekane "anatawaliwa na mkewe".

Wanaume wengine ni wajinga wajinga, wakiona mwanaume mwenzao kapata mwanamke muhangaikaji na anajituma huwa wanapatwa na wivu na kuanza kum-feed mamneno ya uongo ili tu asifanikiwe kimaisha. Nasema hivyo kwa vile umegusia suala ya rafiki zake kusema wewe unamnyanyasa yeye. Hawa marafiki lengo lao ni kuharibu ndoa yenu na kwa vile mumeoo ana-give in upuuzi wao wewe unataeseka ndani ya ndoa yako.

Nini cha kufanya: Kwa vile umefanya yote ( kwa mujibu wa maelezo yako) nakujitahidi kumuonyesha mapenzi nakuongea nae vizuri kwa mapenzi lakini yeye haonyeshi kubadilika. Kuna uwezekano namna unavyowakilisha hoja zako sivyo ambavyo inatakiwa kwa mwanaume wa namna hiyo (asie jiamini,mwenye kiburi na dharau).

Mwanaume kama huyu ukimuibukia na issue inayokutatiza ktk mtindo wa mawasiliano na kumuonyesha mapenzi mara zote anakuona kuwa unajipendekeza kwake na kuwa uko-needy (kumbuka ni ndoa yako ya pili hivyo anadhani kuwa hutokwenda popote na utaendelea kuwa nae milele na kuvumilia upuuzi wake).

Sasa kama inawezekana wee mfuate huko kwenye nchi yake (huko anako ishi), kisha fanya nae mazungumzo kuhusu issues zote zinazokutatiza na zimekuwa zikikunyima raha kwa muda wa miaka mitatu sasa. Wakati unawakilisha hoja zako hakikisha hubembelezi na wakati huohuo humfokei (usiwe na hasira) na badala yake kuwa firm.

PSSST**Kwa vile hamjaonana kwa muda mrefu anaweza kutanga Ngono, hakikisha ukimpa usimfanyie mautundu yako yote au hata kama unavipya na badala yake kuwa mvivu-mvivu hivi, sio sana ila hakikisha unajifikiria wewe zaidi na sio yeye linapokuja suala la kupata utamu/kilele.**

Sasa kuna sheria za kuwakilisha hoja au issues zinazokutatiza kwenye ndoa au uhusiano wa kimapenzi kwa mujibu wa aliyenifunza nayo ni (1)-Vizia siku ambayo mumeo hayuko moody na tengeneza mazingira mazuri (badilisha mpangilio wa vitundani, ongeza/punguza mapembo.

(2)-Anza kwa kuelezea hisia zako juu yake, umuhimu wenu kwa watoto na namna gani basi watoto wote wanavyo muhitaji kama baba (hii itamfanya asihisi kuwa anatengwa na watoto wa ex mumeo)

(3)-Kumbushia maisha yenu ya kimapenzi mlivyokuwa mkianzana na jinsi gani ulikuwa unafurahia na kiasii gani basi unakosa hayo yote. Mueleze namna gani unajisikia kila unapozungumza nae na hisia hizo zinavyozidi kila mnapokuwa pamoja.

Mwambie kuhusu hisia zako dhidi ya marafiki zake, sio kwamba unawachukia lakini unahisi kuwa wanachukua nafasi yako...kwamba mumeo anafanya maamuzi kwa kufuata marafiki zake na sio wewe mkewe.

(4)-Muulize ni kitu gani hasa kinamuudhi kuhusu wewe? na ni kitu gani hakipendi kuhusu uhusiano wenu pia angependa kubadilisha nini ikiwa atapewa nafansi ya kubadili kitu kuhusu uhusiano wenu na ndoa kwa ujumla......mara nyingi hii itamfaya na yeye akuulize maswali hayo hayo kitu ambacho ndio unakihitaji.

(5)-Kumbuka kumpa nafasi ya kujieleza ikiwa anataka kufanya hivyo, usilazimishe aseme kitu kama haonyeshio kufanya hivyo (hapa inamaa unayosema yanamuingia taratibu).

(6)-Fikiri huku unaasikiliza maelezo yake na wakati huo huo kuelewa. Kwamwe usiongee wakati yeye anajieleza na ikiwa yeye ataingilia wakati unajieleza kaa kimya na umsikilize lakini kumbuka kufikiri huku unaongea/sikiliza hii itasaidia kuepusha mabishao.

(7)-Kamwe usionyeshe Kiburi wala usimuonyeshe kuwa unamuhitaji sana hata kama ni kweli unamuhitaji, mdhihilishie kuwa wewe ni mwanamke unaejiamini na unaweza kuendesha maisha bila mwanaume lakini huwezi kuzuia moyo wako kupenda, na mtu pekee unampenda ni yeye mumeo. Hivyo humuhitaji (as in need) bali unataka awepo kwenye maisha yako na watoto wako.

(8)-Sasa mueleze yote yalioujaza moyo wako, kumbuka kutokulalamika, kubembeleza, kulaumu, wala ku-demand na kubwa kabisa hakuna kuonyesha mapenzi.....mpe straight face na tazama macho yake....this is your moment inaweza kubadilisha mwenendo mzika wa ndoa yako.

(9)-Mara tu baada ya maongezi kuisha usionyeshe ile "straight face" na badala yake kuwa more loving na ikitokea anataka mambo fulani huu ndio wakati wa kumuonyesha zile vitu adimu, ambavyo hawezi kuvipata ovyo-ovyo.

(10)-Badilisha mtindo wa maisha yako, you are only 28 hivyo bado mdogo na unaweza kuwa bonge la sista duu kwa maana ya mavazi na kujipenda (sio lazima uvae nguo za ajabu ajabu unawez akuvaa kufuatana na Imani yako ya Dini lakini ukavutia nakupendeza). Hakikisha unavutia kuliko ilivyo sasa.

Ibua interest mpya, mfano kufanya mazoezi ili kuweka mwili wako vema zaidi na utavutia zaidi ukiwa mtupu, valia nguzo za ndani zenye mvuto, ongeza ubunifu kwenye mapishi yako n.k

Endelea namtindo huu mpya wa kimaisha na baada ya wiki chache utaona mabadiliko......lakini kama haitatokea ndani ya wiki chache (nazungumiza kati ya wiki 2-miezi 3) basi itakuwa ni wakati muafaka kupata msaada kutoka kwa wale waliowafungisha ndoa.

Kila la kheri!

Wednesday, 24 June 2009

Siko tayari kumuacha lakini anapenda T-O!

1-"Habari ya kazi ? kwanza nashukuru kwa kutuhabarisha. Mimi ni mwanamke na hivi karibuni natarajia kuolewa na mwanaume ambaye naamini tunapendana sana. Ila naomba ushauri kwani SIKO TAYARI KUMWACHA ila tatizo ni kwamba anapenda nyuma na nilijaribu kumpa siku moja inauma sana mpaka sasa naogopa kurudia tena.

Kila tukikutana anataka nimpe nyuma ila nakataa.Naomba unishauri kuna madhara gani ambayo nitayapata iwapo nitakuwa nampa nyuma? Kwani kwa kutaa kwangu kumpa nyuma kumesababisha yeye kunicheat na wanawake wanaoweza kutoa nyuma nifanyaje na kumwacha siwezi kwanza anahuruma, utu, ananithamini, ananifikisha hapa huwa nachanganyikiwa.
Naomba unishauri"

Dinah anasema: Tafadhali tembelea topic inayosema ngono kusiko au ngono kinyume na maumbile....tumia kibox cha kutafuta topics hapo juu kulia. Asante.

Monday, 22 June 2009

Nilisikia Kwenye KP kuwa shabu....-Msaada!

"Hi dinah, am new to your websyt and i think it will help me a lot. My k ilikuwa so tight na raha ya mapenzi ilikua maximum. Katika kitchen party nlisikia kua ukiosha na shabu (alum salt used to treat water) K inakua haina maji na hunata sana, basi nikaifanyia trial, na tokea hiyo siku kuingiza dick ni kazi kinoma yani am almost as tyt as a virgin ila humo ndani ndo kasheshe, maji kibao halafu mepesi na sioni raha ya sex.


I stopped using it ila problem haijaresolve. One week i had a chest infection nikawa natumia antibiotics na 4 that week my K was perfect as it used to be. Ila i finished them and now maji yamerudi. wat shall i do? A."

Dinah anasema: Hello! Asante kwa mail yako na karibu sana mahali hapa. Sasa Mdada kama ilikuwa inabana kitu gani kilikufanya ukatafute namna ya kuibana zaidi na kuifanya inate? Ngojanikujibu kw akifupi tu hapa kisha nitoe maelezo kidogo kuhusu K mnato.

Tatizo lako wewe nadhani sio matumizi ya Shabu kama Shabu bali ni maambukizo yaliyosababishwa na ukavu wa Uke wako, nasema hivyo kwa vile Shabu ni Tindi kali kama ilivyo ndimu na limau amabzo zote hutumiwa "kubana uke" lakini inachokifanya sio kubana bali kukausha sehemu hiyo isiyo na makosa (uke umekukosea nini mpaka unauadhibu hivyo).

Sasa mimi nahisi ulikuwa na maambukizo huko Ukeni bila wewe mwenyewe kujua na inawezekana kabisa ndio ikawa sababu ya wwe kutokwa na maji mengi na kukosa raha ya tendo. Kinachonipa kiburi cha kusemahivyo ni kwa vile ulipata maambukizo ya Kifua na ukatumia antibiotics.

Kama ujuavyo mara nyingi dawa hizo (antibiotics) huwa na tabia ya kutibu au kuzalisha maambukizo mengine mwili, so inawezekana kabisa zilikuwa zinatibu tatizo lako la Ukeni sambamba kabisa na Kifua lakini kwa vile Dozi haikuwa kwa ajili ya tatizo hilo la ukeni ambali hata wewe hukujua kama ulikuwa nalo ni wazi halijaisha kwa vile dozi imeisha.


Nini cha kufanya-Nenda kwa daktari wa magonjwa ya kike na mpe maelezo kamaulivyonieleza mimi, kama kuna aina yeyote ya madawa ya kuzia mimba umewahi kutumia au unaendelea kutumia pia weka wazi kwa Mtaalam huyo,kisha mwambie kuhusu maambukizo ya kifua na aina ya dawa ulizokuwa ukitumia na tofauti uliyoiona ukeni amabyo ni tofauti na sasa.....yeye atakupa ushauri wa kitibabu na hatimae tiba.

Kidokezo:-(kuna topic ya Mnato namaji mengi ukeni kaisome tafadhali)
Unajua baadhi ya wanawake hudanganyana ili kuharibiana mambo kwa wenzao, kwa vile wao wako hivyo au walijaribu jambo likienda kombo hushauri/shawishi wenzao wakajaribu wakijua kabisa kuwa matokeo ni sivyo ndivyo.....si unajua wanawake tunavyopendana NOT!

Skia sasa, wanaume wanaposema wanapenda K a.k.a Sambusa* mnato haina maana inanata kama udongo wa Mfinyanzi bali ni ile hali ya uke kuibana, kuivuta na kuiachia Mboo a.k.a Mtalimbo*.... kila unapokuwa ndani, na kinachosababisha hayo yote ni misuli yako ya uke na jinsi wewe unavyojua kuitumia ili kumpa umpendae utamu zaidi (Pitia Topiki ya Endiketa) kwa maelezo ya kina.

K inayonata (sio mnato wanaouzungumzi wanaume though) mara nyingi itakuwa haijasafishwa, Mf-kama wewe umewahi kufanya mapenzi/ngono asubuhi mara tu baada ya kuamka utahisi ndani ya uke wako kuna hisia tofauti kidogo na muda mwingine wowote unaofanya Ngono baada ya kujiswafi, unaweza kuhisi u-tight fulani unaoambatana na kijiharufu mwanana hivi hii ni kutokanana Utoko uliojikusanya usiku uliopita.

K-mnato inayozungumziwa na wanaume wengi ni ile safi yenye uwezo wa kubana, kuvuta na kuachia uume a.k.a endiketa wakati wa kufanya mapenzi na sivinginevyo. Hata kama ni kubwa na unahisi kuwa ni pana saaana kama unajua utundu huu mumeo/mpenzi wako hatolalamika hata siku moja na ataipenda hivyo hivyo ilivyo na upana wake....

Natambua kuwa kuna wanawake wengi wanatafuta dawa za kienyeji sio Shabu tu ili kurudisha K zao na kuwa ndogo na wengi wanafanikiwa kama ulivyodai mwenyewe kuwa njia inabana lakini ndani maji debe*......nilikuwa najaribu kuweka hili sawa ili kupunguza idadi ya kinadada wanaotumia Shabu kwani inaweza kukusababishai matatizo ya kiafya.

Hakikisha unafanya uchunguzi unapoambiwa kutumia kitu kama Shabu, jaribu kufahamu madhara yake hapo baade sio unakurupuka tu kutumia kwa vile umesikia Kungwi kwenye KP akisema ukimfanyia hivi mumeo hakuachi......KP ni biashara hivyo kuwa mwangalifu.

Kila lililo jema nakutakia.

Friday, 19 June 2009

Ushuhuda kutoka kwa Asif King!

Habari za saa hizi dada Dinah na wachangiaji wote. Mimi ni Asif King sijui unanikumbuka? nilikuja hapa kuomba msaada wa mawazo na ushauri kuhusu mke wangu ambae anaishi Ughaibuni na watoto wetu wawili. Napenda kusema Mungu awabariki sana kwa kuweza kuokoa ndoa yangu. Kama isingekuwa Blog hii na wachangiaji wake hasa kiongozi wao Dinah basi ndoa yangu ingekuwa historia.

Ni karibu miezi miwili tangu nilipopata ushauri wenu na kuufanyia kazi na ninamshukuru Mungu mke wangu alinisikiliza na kuonyesha kunielewa na kuahidi kurudi nyumbani mara moja ili tuongee vizuri. Kama kawaida nilimtumia tiketi na akaja na sasa ninavyoongea yuko hapa Tanzania na watoto watafuata baada ya kufunga shule kwa ajili ya mapumziko ya summer, hivi sasa wanaangaliwa na Ndugu huko huko Ughaibuni.

Leo hii nimeamua kuja hapa kusema yaliyotokea kwani sasa nina uhakika na maamuzi ya mke wangu kuwa kweli atabaki hapa nyumbani kama mlivyonishauri nimshawishi.

Kwakweli sina jinsi ya kuwashukuru Ndugu zangu kwa wema wenu na muda wenu mliotumia kunishauri kupitia Blog hii, nilikuwa nimekata tamaa kabisa na nikawa tayari kupoteza ndoa yangu lakini Dinah akaniambia kwanini nikimbilie kuoa mwanamke mwingine wakati sijajaribu kuiokoa ndoa yangu? Dada kwa kweli kama ni kipaji basi ni cha pekee, hakuna mtu alinishauri yote niyoyapata hapa kwa Dinah, naahidi kuja tena hapa kama tutatetereka tena kwenye ndoa yetu.

Mungu awabariki sana tena sana wote mliochangia, wote mlionipa ushauri mzuri na kunitaka nisioe, wote mlionipa moyo na matumaini ya kuwa mvumilivu. Nimeamini ukichangia tatizo unapata suluhisho haraka kuliko kukaa nalo moyoni. Ule ukurasa na maoni yake yote nime print na nimeyatuza kwenye faili langu kwa kumbu kumbu.

Nisiwachoshe sana jamani, mke ananisubiri. Kwaherini na endeleeni kuokoa ndoa za wengine kama mlivyo okoa yangu.

Dinah anasema: Habari ni njema tu.
Shukrani kwa kurudi tena mahali hapa, nimesoma wakala wako nikahisi machozi yananilengalenga kwa furaha, D'hicious imeokoa Ndoa nyingine tena!

Hongera sana Asif kwa kufanikiwa kuokoa ndoa yako na hatimae kuvinjari na mkeo. Kusoma Mkasa wa huyu bwana unaweza kubonyeza hapa

Tuesday, 16 June 2009

Sijapata Unyumba mwezi wa 8 sasa-Ushauri

"Habari za kazi dada Dinah, hongera na pole kwa kazi ngumu ya kutuelewesha,
mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 29, niliolewa na kijana mwenye umri wa miaka 33, kwa sasa tunakaa Temeke na hatujajaliwa kupata watoto tunaishi peke yetu tu.

Mume wangu ni mwajiriwa na anafanya kazi katika Bank ya Twiga bancop, elimu yake ni chuo kikuu na mie elimu yangu ni form four. Mimi sifanyi kazi ofisini, ni mama wa nyumbani najishughulisha na vibiashara kidogo kidogo. Ila wakati tunachumbiana nilikuwa nafanya kazi kaniambia kuwa niache niende shule kwa hiyo nasubiria kuanza shule sasa ambayo naanza huu mwaka wa serikali yaani mwezi wa 7.

Swali linakuja hivi wakati tunaoana ilikuwa furaha na shangwe, tulipanga Mungu akijalia tutazaa watoto watatu. Imefikia sasa kwenye matekelezo mwenzangu mara "oh sitaki mtoto sasa hivi", hata tendo la ndoa ni sumu ndani yetu tunalala pamoja kitanda kimoja lakini ukimgusa anasema "unanitekenya usiniguse".

Mara "ohh nimechoka, ukipata mimba itakuwaje na unataka kwenda shule", nikimwambia kwani chuo wanakataza watu wenye mimba? anasema "sitaki uzae sasa", umri unakwenda, hata siku zisizokuwa za mimba hataki kufanya mapenzi. Nikimwambia kama unaogopa basi tumia condom, anasema "sitaki je ikipasuka", yaani hadi ananipa mawazo mabaya kumwazia, au ameathirika? ila tulipima kabla ya ndoa.

Nyumbani anarudi saa za kawaida na akirudi ni kitandani kutandika usingizi, je huu ni ugonjwa au nimakusudi au ni nini? nisaidieni wamama wenzangu, imefikia kipindi nikahisi labda hakuna ladha ile anayoitaka kwenye K yangu au imekuwaje jamani?

Nimeangalia hata katika simu hakuna mwanamke aliyemtumia msg au kumpigia hata akinipa simu yake siku mbili sipati msg wala simu ninayoihisi. Siku moja nikahisi labda huwa akinipa simu yake anawapa taarifa, nikaitoa kisiri kadi yake nikabaki nayo na kumpa yangu na hata hivyo ikawa vilevile sijaona simu wala msg.

Mume wangu hanywi pombe na hatumii madawa ya kulevya , ila anavuta sigara, Tokea mwaka jana mwezi wa 10 hadi leo tumefanya mapenzi mara moja tu, anadai amechoka, kila siku sijui labda nashindwa kumpa staili anayoipenda au inakuwaje, nikijaribu kumuuliza au unamwanamke nje anakataa anasema hana hamu tu.

Nikajaribu kumchunguza labda anasehemu anayo nyumba ndogo sijaona, ila chumbani kwetu kuna meza na hiyo meza kila mara naikuta inamafuta ya mgando, sijui huwa anayafanyia nini? na hata hivyo nilivyomsachi katika mifuko kuna koti la suti kalitundika ndiko anakoficha chupa ya mafuta mazito ya mgando. je anajichua nayo? atakuwa na matatizo au mimi nina matatizo? nifanyeje ili kuweza kuinusuru ndoa yangu changa?

Nisaidie dada Dinah na pia nikipata mawazo ya wengine yatanisaidia zaidi"

Dinah anasema: Habari ni njema tu, vipi wewe? Asante sana Binti kwa kuniandikia, napenda kuchukua nafasi hii kukutaka uwe mvumilivu kutokana na majibu ya wengi ambayo ni wazi yanaweza kukufanya umtazame mumeo kivingine kabisa.

Kabla sijakupa maelezo na mbinu za kufanya, napenda kuweka wazi kidogo kuhusu jambo la mafuta mazito. Inasikitisha kuona kuwa baadhi Wabongo wanaamini kuwa mafuta mzito hutumika kwenye kufanya Ngono kusiko au Kujichua.

Ifahamike kuwa mtu huwezi kujichua kwa kutumia mafuta mazito kwa sababu hayana uterezi wa kutosha kama KY, Sabuni au mafuta ya maji (hasa baby oil) na kama ujuavyo mafuta hayo huganda ngozini badala ya kulainisha.

Hivyo basi mtu kuwa na mafuta mazito sio kithibitisho kuwa yeye ni Shoga, kuna matatizo mengi ya sirini na sehemu za kawaida ambayo yanaweza kuhusisha matumizi ya mafuta mazito.....tatizo kama Constipation (kutokupata choo), Ukavu wa ngozi, ukavu wa midomo ya nje (wanaume hawapaki lipstick au lip bum wengi hupitisha mafuta mazito kwambaali), ukavu wa viganja vya mikono, matatizo mengine ya ngozi maeneo yenye mikunjo n.k.

Unapotoa maelezo kuhusu issue ya mtu unatakiwa kusoma maelezo yake na kuyaelewa kisha una-analyse ili kutoa majibu ya kutosha ambayo yanagusa kila point aliyoigusia ambayo yeye anadhani huenda ikawa ni tatizo...........tuendelee sasa.

Wewe unajua kabisa mumeo alivyokuwa kipindi kile mnachumbiana, ni wazi kuwa ulikuwa ukifurahia tendo na hata mkawa mnapanga masuala ya kuzaa na idadi ya watoto. Kama angekuwa Shoga basi ungeligudua then na angekuwa anakukwepa na kwamwe asingelizungumzia suala la ninyi kufunga ndoa na kuzaa watoto.

Kama ilivyo kwa wanawake, wanaume pia hukumbana na mabadiliko ya miili yao kwa maana ya utendaji wao kingono, kwa bahati mbaya Mwanaume yeyote akipatwa na tatizo hili (huwapata wengi tu) hubadilika sana kutokana na hofu, mawazo na uwoga.

Mf- anawaza itakuwaje kama asipokupa watoto mliopanga, je ukijua tatizo lake utamkimbia ukaolewe na mtu mwingine? vipi kuhusu uanaume wake (Ego), je ataanzia wapi kuliweka wazi hili kwako au hata kwa Daktari n.k

Hivyo vyote vinaweza kumfanya mwanaume huyu akawa mkali na mkorofi au akawa mpole na mwenye mawazo mengi na kutumia muda mwingi kulala au kukaa peke yake hali inayoweza kuharibu hata utendaji wake kazini na pengine kupoteza kazi.

Mwanaume kama huyu anahitaji ushirikiano, kupewa matumaini, kuonyesha kuwa unamjali, unamthamini kama mwanaume na kuelewa tatizo lake. Usitegemee yeye akuambie na badala yake wewe unatakiwa kuvumbua mwenyewe, kumbuka ni mumeo na unamamlaka juu ya mwili wake sasa utumie nguzo ya Mawasiliano, busara na uanamke wako (unafundishwa kabla ya ndoa) ilikujua ukweli na hatimae kumsaidia na hatimae kupata uvumbuzi wa tatizo lake. Hilo moja.


Pili, Inaonyesha wewe ni mwanamke unaependa ku-demand kwa vile tu uliambiwa au mlipanga, kumbuka mipango siku zote hubadilika hivyo basi unatakiwa kujua namna ya kukumbushia badala yaku-demand kupata mtoto wakati mwenzakoa nahisi kutokuwa tayari au (kama nilivyosema) pengine anadhani hawezi kukuzalisha kwa vile Jogoo hawiki kama zamani na anashindwa kukuambia kwa vile anahisi aibu au kudhani kuwa utamdharau.

Tatu, umegusia kitu muhimu sana. Ilifikia mahali ukahisi huenda mumeo ameathirika na HIV na hataki kukuambukiza, lakini ukajima moyo kuwa mlipima kabla ya kufunga ndoa. Huenda ikawa kweli au inaweza ikawa sio kweli. Kama aliwahi kuonja mtu kabla ya ndoa na baadae akajaambiwa kuwa Mtu huyo anaNgoma au amefariki Dunia ni wazi atakuwa anajihisi kuwa na yeye anao na hivyo kuhofia kukuambukiza....fanyia kazi hili.

Nne, Inawezekana kabisa mumeo ana tatizo la akili liitwalo Depression ambalo kwa hapa nyumbani linaweza kuwa geni kuzungumziwa lakini lipo nalinawakumba watu wengi tu sema ni ngumu kugundua kwa mwanaume kwa vile huwa hawalalamiki unless uwe mfuatiliaji sana wa mwenendo wake.

Kutokutaka tendo la ndoa, kulala-lala, kusisitiza kwenye jambo moja, kuwa obsessed na kitu fulani mfano aina fulani ya muziki, Sigara, aina fulani ya pipi, aina fulani ya kinywaji (mf kwa case yako nitasema mafuta mazito) ni dalili chache za ugonjwa huo.

Ugonjwa huu hauponi kabisa kama ilivyo Pumu bali unatulizwa na Dawa hivyo atakuwa akitumia dawa hizo 4 life, na dawa zake kwa bahati nzuri huongeza hamu na nguvu ya kufanya mapenzi kama side effect yake ( Nina uzoefu na mtu wenye tatizo hili ndio maana nahisi linaweza likawa tatizo kwa mume pia), Mara tu akipatiwa matibabu atakuwa mume mwema na utafurahia ndoa yako....lakini je ndio tatizo? fanyia kazi hili pia......

Kutokana na maelezo yako huyu mumeo anamuamko wa hali ya juu kuhusu maendeleo yenu ya kimaisha na ndio maana anataka wewe uendelee na masomo ya juu kitu ambacho ni kizuri na unapaswa kumshukuru Mungu kwa kukupatia mwanaume mwenye kujali maisha yako ya baadae, kwani chochote kikitokea bado utakuwa na Elimu yako ambayo itakusaidia kurekebisha mambo.....sasa hebu focus on that kwanza kwa sasa.

Naja midaz kukupa nini cha kufanya.............

Saturday, 13 June 2009

NINA GONJWA WA HATARI NAOGOPA KUMWAMBIA MUME-Ushauri

"Hi Dinah,
Habari za kazi, pole na kazi ya kuelimisha jamii kuhusu maswala ya uhusiano. Tunafurahia sana blog yako maana ni mengi tunayojifunza. Mimi nimekuwa msomaji mzuri sana wa blog yako nikichangia hapa na pale ila sijawahi kuleta tatizo lolote.


Leo nimeamua kuondoa kigugumizi na kuzungumzia ya kwangu ili wenzangu nao wanisaidie kwa ushauri. Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka thelathini na tano. Nimeolewa na nimejaliwa watoto wawili.


Kabla ya kuolewa miaka saba iliyopita nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na kijana mmoja, ambaye nilifahamiana naye nikiwa chuo kikuu ila kutokana na tofauti mbalimbali hatukuweza kuoana.

Katika mahusiano yetu kijana huyo aliniambukiza ugonjwa unaoitwa kwa kizungu ‘herpes simplex virus’. Kiswahili chake kwa kweli sijui ila ni jamii ya ugonjwa inayofanana kama mkada wa jeshi lakini mkanda wa jeshi ni more severe case na inaambatana na wa watu wenye virusi vya ukimwi.

Nisingependa kuzungumzia kwa kirefu ugonjwa huu, kwa sababu hii si glob ya magonjwa, na wewe aunt Dinah si daktari, ila kwa wanaopenda kufahamu zaidi wajaribu kutafuta katika mtandao.

Ila ambacho ningependa kuwaasa wenzangu ambao hasa wako kwenye mahusiano, jamani tuangalie sana kuhusu hili gonjwa kama una mpenzi ambaye ndio kwanza mnafahamiana usikimbilie kunyonyana ndimi, sehemu za siri au kufanya vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kukuexpose katika ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa hii zinafichika sana na pia mgonjwa anaweza kuwa amerecover from symptoms lakini bado akawa na virusi active kwenye mwili kiasi kwamba akaweza kumuambukiza mtu mwingine.

Pia incubation period ya ugonjwa huu ni miezi mpaka mitatu, na once ukiupata ndo unao maisha hautibiki kabisa unakuwa unaenda ukijirudia angalau mara mbili au tatu kwa mwaka. Kwa hiyo tuchunge sana na hili, wenzetu Ulaya wana matangazo ya wazi kuhusu huu ugonjwa kuwatahadharisha vijana wao wajikinge juu yake. Unapendelea kuattack sehemu za pembe za midomo, kama vipele vya homa hivi au sehemu za siri.

Anyway nikirudi kwenye habari yangu, kama nilivyoeleza ni yule mpenzi wangu wa mwanzo ndiye aliyeniletea, alikoutoa anajua mwenyewe.Tatizo ni kwamba mume wangu sikuwahi kumueleza juu ya tatizo hili miaka yote hiyo ambayo niko naye.

Najitahidi sana kumlinda asiupate, pindi nikiona dalili zinaanza huwa sikubali kabisa kufanya naye mapenzi ntatafuta visingizio vyote duniani mpaka tusifanye. Mume wangu pia ni msafiri sana hivyo mara nyingi hayupo nyumbani wakati ambapo saa nyingine ugonjwa unakuwa umejirudia.

Kuna dawa ambayo natumia kupunguza makali ya ugonjwa nimeificha mbali sana asiione. Nashindwa kumweleza mume wangu kwa sababu sijui reaction yake. Nikimwambia leo anaweza kufikiri ni kitu ambacho nimepata hivi karibuni labda nimetembea nje ya ndoa ndio nikapata.

Ninavyomjua mume wangu hataweza kuamini kuwa ni ugonjwa niliokuja nao kwenye ndoa. Ataenda kuwaeleza ndugu zangu na ndugu zake kuwa mi sio mwaminifu ndio nimepata huo ugonjwa.

Kabla ya kuoana niliogopa pia kumweleza nikihofia kuwa ataniogopa labda asinioe kwa sababu ya huu ugonjwa na mie ndoa nilikuwa naitaka. Ila kama nilivyowaeleza najitahidi kweli kadri ya uwezo wangu nisimwambukize mwenzangu ila naona kwamba inawezekana siku akaja kugundua na ikawa mbaya zaidi.

Hapa nilipo niko njia panda najishauri kama nimwambie au nisimwambie na jinsi gani nitumie kumwambia, naomba mnisaidie wenzangu niko njia panda. "

Dinah anasema: Asante sana kwa uwazi wako na vilevile kuja na jambo zuri ambalo wengi walikuwa hawajui, wengi hudhania kuwa UKIMWI ndio gonjwa hatari pekee la ngono kumbe kuna mengine mengi ila watu huwa hawasemi kama sio hawajui kama wanayo....shukrani sana kwa kuliwek ahili wazi.

Pia mchangiaji alieweka link ya NHC kwa maelezo zaidi na namna ya kukabiliana na Tatizo hilo ubarikiwe sasa (tafadhali msomaji zingatia maelezo ya Kitibabu zaidi via NHS site)....nirudi kwenye suala lenyewe je mwenza wako aambiwe au aendelee kufichwa!

Mimi binafsi siamini ktk uongo au kuficha siri sio tu kwa Mume wangu bali kwa mtu yeyote ambae ni muhimu kwangu hivyo ushauri wangu utakuwa ni wewe kuliweka wazi hilo bila kuzungumzia ulivyolipata (itamtia hasira). Kuna njia nyingi sana za kuliweka wazi tatizo lako kwa mumeo bila kuhusisha yaliyopita kama vile ulivyoupata, unavyomkinga n.k

Kama ulivyodai mwenyewe kutokana na uzoefu wako (umeishi na tatizo hilo kwa muda sasa na unakabiliana nalo kwa kupunguza makali),

Narudi in few minutes.....

Friday, 12 June 2009

Mpenzi hajitumi kabisa, niache au?-Ushauri

"Wana jamvi tusaidiane hii scenario. Nimekua nina mpenzi kwa muda wa miaka 2 sasa huu waenda 3, katika muda wote huo nimekua nikiona mapungufu mengi lakini mengine nimeyamezea na kuyavumilia kwani ndio kwanza tulikua katika take off sasa ndo tuko highway kuelekea kule kwa sahihi yaani Ndoa.


Kinachonitisha kati yangu na huyu mdada ni kua hayuko aggressive kwa maana ya kujituma au upiganaji katika mambo yaani amepoa sana. Yeye kila kitu kinachohitaji effort anakua hawezi au sio makini., Example baada ya kumaliza shule yake amekua katika mchakato wa kusaka ajira lakini cha kushangaza ni kua uombaji wake huambatana na makosa ya hapa na pale mpaka binafsi niamue aidha kuedit au kutuma cv yake kwa kampuni husika.

Dinah anasema: Mwenyewe hapo umesema kuwa amemaliza shule hivi karibuni hivyo basi hana uzoefu na masuala ya kuomba kazi au hata namna ya kuandika hiyo CV, wewe kama mtu wake wa karibu na unajali maendeleo yake ambayo yatakufaidia na wewe unapaswa kumsaidia au hata kumuelekeza. Hivyo hatua uliyochukua ya kuhariri na kumsaidia kuituma ni sahihi kabisa, hapo wala sio uzembe bali ni kutokujua/kutokuwa na uzoefu.

***********************************************************************************

Kwa sasa anafanya kazi katika kampuni moja ambayo kila kukicha analalamika hawajampa ajira nimekua nikijitahidi kumtumia matangazo ya kazi ili awe anaomba lakini amekua haombi hizo kazi kwa kisingizio cha kua amesahau au eti ana mambo mengi kiasi cha kushindwa kuapply.

Dinah anasema: Inawezekana ni kweli kabisa shughuli zimem-bana au ameridhika hivyo haoni umuhimu wa kuandika maombi mengine ya kazi wakati tayari anamahali amejishikiza japokuwa hawajampa ajira ya kudumu.


Kawaida ya sisi wabongo tunapenda sana kuridhika, pamoja na kuwa tunalalama bado huwa waoga kutoka mahali na kwenda kwingine ambako kuna mafao mengi/makubwa....unafanya kazi sehemu moja maisha yako yote kwa vile hujiamini kuwa unaweza kufanya mabadiliko ikiwa tu unataka hivyo.

*********************************************************************************

Kilichoniudhi zaidi ni pale alipofikia hatua ya kupoteza cheti chake cha kuzaliwa wakati ni muhimu sana katika maombi ya fursa mbali mbali. MBAYA ZAIDI haonyeshi kuappreciate kile nikifanyacho ili aweze kupata kazi nzuri anadai siko supportive to her while matangazo yote mie ndo nayatafuta. Kazi zingine mie ndo ninaziomba kwa niaba yake, pia mie ndo natuma appliation zote kwa njia ya posta etc.


Dinah anasema: Inaelekea wewe unatabia ya kusema sema kutokana na "uzito" wake wa kufanya au kuzingatia mambo, na ndio maana akasema hauko supportive kwake. Kitendo cha yeye kupoteza Cheti chake cha kuzaliwa sio kikubwa sana kukufanya uudhike zaidi kwani anaweza kupata kingine as long as alitoa taarifa Polisi, Wazazi wake au ndugu wa karibu/damu wote wapo na anajua wapi, lini alizaliwa. Kama huko alikozaliwa wamefuta kumbukumbu basi anaweza kupatiwa hati nyingine kupitia Mahakamani ambacho kinathamani sawa kabisa na Cheti cha kuzaliwa.

*******************************************************************************
JE HUYU NI MWANAMKE ANAEFAA KWA MTU AMBAE NI AGGRESSIVE KATIKA MAISHA YA KILA SIKU?Kwani haeleweki kabisa kiperformance nikimaanisha kua kila ikiwa nitamuagiza kitu afanye kwa faida yake mwenyewe wasi wasi hunijia kama atafanya kwa usahihi au inavyopaswa. Kwa mfano unamwagiza aombe kazi anaweza tuma cv na covering letter akasahau vyeti.


Je ni sahihi kama nikijitoa katika maisha yake?as tukiachana kwani binafsi ni mtu ambae nahitaji mwanamke ambae ni mpiganaji kweli sio ambae kila kitu anahitaji monitoring au usimamizi.
Wadau nikwamueni."

Dinah anasema: Asante sana kwa mail yako. Nimekujibu hapo juu kulingana na maelezo husika na sasa nakujibu kwa ujumla! Sio sahihi kujitoa kwenye maisha yake kama anakupenda na wewe unampenda, utakuwa unamdhurumu kihisia.

Pamoja na kuwa mpenzi wako anakuudhi kutokana na yeye kuwa slow ninauhakika anavitu vingine vingi tu ambayo vinakufurahisha, Mf-Tabia yake kama mwanamke, Heshima yake kwako, Uzuri wake kama mwanamke nakadhalika......

Kutokana na maelezo yako nimegundua kuwa kuna tatizo la mawasiliano, ushirika na usaidizi. Hizi ni nguzo tatu kati ya zile tano ambazo ni kuu ktk kuboresha uhusiano wa kimapenzi ukiachilia mambo mengine madogo madogo ambayo pia ni muhimu.

Ikiwa u-slow wake unakuudhi ulipaswa kuliwakilisha hili kwake ktk mtido wa kuongea (wasiliana nae) na sio kulalamika na kushupalia kuwa yeye ni "mzembe", "mvivu", "hajali" hajitumi n.k huenda hutumii haya maneno kama nilivyoweka hapa lakini huwa unayatumia.

Ushirikiano unampa na pia unamsaidia kama ulivyojieleza mwenyewe, lakini hailete maana halisi ninayoijua mimi ktk mahusiano ya kimapenzi kwani unalalamika kuwa anadai huwa humpi support wakati wewe unamfanyia kila kitu, hata kazi aliyonayo ni wewe ndio ulisababisha......sasa hayo yote yanabadilisha maana ya Ushirikiano na Usaidizi na kuzaa masimango.....unamsimanga kitu ambacho hakisaidii kwani kitamfanya asijiamini tena kama mpenzi wako.

Binaadamu wote tumetofautiana na sote tunakasoro zetu ambazo wapenzi wetu hutuvumilia kwa vile tu wanatupenda. Ukilinganisha kasoro nyingi tulizonazo wanaadamu hiyo aliyo nayo mpenzi wako ya kutokuwa na habari au sio mzingatiaji/tia maanani (sio anafanya makusudi ila akili haiko sharp) au yuko slow ktk utendaji na ufanyaji wa maamuzi sio kitu kabisa na inaweza kubadilishwa na pengine hata kuvumilika.

Nini cha kufanya:
Naja kumaliza......

Tuesday, 9 June 2009

Nahisia zaidi ya za Kirafiki, nimwambie?-Ushauri

"Hi Dinah,
Nilikuwa natembela blogs nikaona ya kwako, imenivutia na nikaona hapa naweza pata ushauri.

Mimi ni mdada wa miaka 34, nina binti wa miaka 8. kwa hivi sasa mie nipo single sina mume. Ninachoomba ushauri ni hiki.

Nilikutana na mkaka mmoja baada ya yeye kupewa contacts zangu na rafiki yangu ambae alikuwa amenitumia zawadi kutoka nyumbani. Baada ya hapo tulipanga kukutana na tukakutana, ikatokea kwamba tumelewana na tukawa marafiki sana.

Kila siku lazima tuongee katika simu na pia sms, muda ulivyoenda ikawa kama vile lazima tuwasiliane kila siku isipokuwa hivyo huwa najihisi kuna jambo limepungua. Nae baadae akakiri kwamba inakuwa hivo kwake.

Ikafika likizo ya Christimas akanialika kwa wazazi wake mimi pamoja na mwanagu, tukaenda tukafurahi na kurudi. SASA tangu kipindi hicho nimekuwa napata hisia tofauti kimapenzi na za kirafiki kwake.

Yeye ananiambia ananimiss anatamani kuniona lakini hasemi kama hisia zake zimekuwa zaidi ya Urafiki. Nitakutanae week mbili zijazo anakuja kwangu je nimwambie how I feel? lakini pia sitaki kupoteza rafiki....

Nifanyeje? nisaidie jamani i dont want to loose a friend and I also want to know what we feel for each other.

Thanks
Jenifer"

Dinah anasema:Shukrani kwa kustop mahali hapa na kuniandika maelezo haya. Huyo mwanaume anajua kabisa kuwa unampenda au unamtaka zaidi ya urafiki lakini hana uhakika kama utamkubali awe kama "mpenzi" kutokana na urafiki wenu.


Wengi huamini kuwa hakuna urafiki wa watu wa jinsia mbili tofauti ukaishia urafiki tu unless wewe na yeye muwekeane mipaka na kuidumisha vinginevyo ile kitu inaitwa "chemistry" inaweza ikabadili urafiki na mkawa wapenzi.


Naelewa hofu yako ya kupoteza urafiki na huyo Kijana iwapo utaweka wazi hisia zako lakini ukweli ni kuwa wanaume huwa hawana hizo hisia za "akinikataa nitamuangalia vipi usoni kama rafiki", hivyo mwanaume ambae ni rafiki yako akikutaka huwa anafocus kwenye hisia na anajua kabisa ukimtosa ataendeleza urafiki japokuwa wewe kama mwanamke utashindwa kutokana na aibu au kujisikia vibaya kwavile umemtolea nje ,pengine unaweza kudhani kuwa amekushushia heshima hasa kama huna hisia nae.


Lakini kwa case yako, wewe mwanamke ndio mwenye hisia kali za kimapenzi juu yake hivyo basi hakuna ubaya kama utaziweka wazi hisia zako hizo na yeye akajua wazi kuwa umemzimia, sio lazima sana umwmabie kwa maneno unaweza kutumia uanamke wako na ukafanya kwa
vitendo zaidi, wanaume ni waelevu sana na hunyaka chapchap ile "lugha ya machoni".

Nafurahi kusema kuwa hakuna mapenzi matamu kama yale yalioanza na kuegemea kwenye urafiki, mara nyingi mapenzi ya namna hii huwa hayana kukinahi wala kupauka kwa vile wote wawili mnafahamiana vema kama marafiki hivyo mnakuwa tayari mmeweka msingi mzuri kabisa wa maisha yenu ya baadae kama wapenzi.

Ni matumaini yangu utayafanyia kazi yale yote yaliyoelezwa na wachangiaji, mimi kama Dinah nasema dada, go for it....muonyeshe tu kuwa safari zako zooote hapo umefika na mabegi umeshusha....

Kila lililo jema.

Monday, 8 June 2009

Nifanye nini kupata mtoto wa Kiume-Msaada

"Mimi na mume wangu tumejaaliwa mtoto wa kike miaka miwili na miezi saba sasa. Tunaomba mungu sana hapo baadae tupate mtoto wa kiume hebu nipe darasa najua unaelewa haya mambo kuwa pamoja na kusali upate wa kiume je Kitaalam unataimu vipi ili iwe kweli wa kiume dear?Pia kama nataka twins pia nafanyaje?

Nitashukuru sana ukinipa data kwani ndio nataka kujiandaa kumtafutia Bridgitte mdogo wake baada ya miaka miwili. Naomba nisikuchoshe nikutakie siku njema na baraka msalimie baby wako Conso a.k.a mama Bridgitte"

Dinah anasema: Dada Conso na Shamimu asanteni kwa ushirikiano wenu, hakika suala hili ni common sana miongozi mwa wazazi wengi wanaopenda kuwa na pea za watoto weye jinsia tofauti.

Natambua kuwa mtoto yeyote akizaliwa upendo, hali ya kujali na furaha ni ileile bila kujali jinsia yake, lakini kama ingewezekana basi wengi tungependa kuwa na mchanganyiko wa jinsia...namna gani basi utafanikisha hilo ndio mbinde!

Kupata mtoto wa kiume inategemea zaidi familia zenu ninyi wawili, kwa maana kuwa kwenu kuna wanaume na wanawake kiasi gani hali kadhalika upande wa familia ya mume wako, ikiwa wanawake ni wengi zaidi kwenu na kwa mumeo pia wadada wengi basi utazaa watoto wakike tu au wengi (inategemea unataka kuzaa wangapi).

Lakini kama kwao mumeo wanawake wengi na kwenu wanaume wengi basi mtoto wa kiume kupatikana ni rahisi zaidi, ila ikiwa kwa mumeo kuna wanaume wengi na kwenu wanawake wengi bado uwezekano wa wewe kuzaa wa kike tu au wengi ni mkubwa.

Hivyo basi, ili kupata mtoto wa kiume inategemea zaidi na upande wako wewe mwanamke, nikiwa na maana kwenu kuna wanaume wangapi kwa maana ya wajomba, kaka zako, baba wakubwa na wadogo n.k. (ila binamu hawahesabiki).

Nini cha kufanya kupata mtoto wa kiume.
Kuna njia kuu mbili nizijuazo mimi ambazo zinaweza kusababisha wanandoa kupata mtoto wa kiume na njia hizo ni zile za Kisasa/Kitaalamu na asilia....nitafafanua kidogo asilia ambayo ndio naijua zaidi na ile ya kitaalamu ni straight foward.....lakini kabla napenda ufahamu yafuatayo;-

(1)-Mbegu zinazosababisha mtoto wa kiume hutoka haraka na kwa speed kubwa sana ili kuungana na Yai vilevile hufa haraka (hufa ndani ya masaa 3 ya mwanzo).

(2)-Mbegu zisababishazo mtoto wa kike hujivuuuta sana (maringo ya wanawake yanaanza b4 hata hatujawa viumbe kha! hihihihi) na hubaki hai kwa zaidi ya masaa 72 (zaidi ya siku tatu).

(3)-Bao zito na lenye afya ndio muhimu kusababisha mtoto wa kiume (mlishe mumeo lishe bora).

Hivyo basi ili kufanikisha hili unapaswa kutegea siku ambazo wewe unajua yai lako limepevuka na linasubiri kurutubishwa na mbegu ya kiume. Ukingonoka kwenye siku hatari kuliko zote ni wazi kuwa zile mbegu za jinsia ya kiume zitakuwa za kwanza kurutubisha yai na kufanya mimba ambayo itakuwa ya mtoto wa kiume. Hii ni njia asilia.

Njia ya kisasa ni ile ya kitaalam kuchukua yai lako na kuchagua mbegu za kiume tu kutoka kwa mumeo nakurutubia manualy (nje ya mwili wako) kisha wanakupandikiza, yaani wanakuwekea mimba (yai na mbegu walizounganisha) kwenye Womb (mji wa mimba) na hapo kunakuwa na uhakika wa kuzaa sio tu mtoto wa kiume bali wanaweza kuwa mapacha 2-3 wa kiume.....inaghalimu mamilioni ya shilingi though.

Kidokezo; imni ya kujaribu mpaka upate mtoto wa kike au kiume bila kuzingatia kwenu mkoje intrms of jinsia sio njema kwani mtajikuta mnazaa watoto ambao hamtaeza kuwamudu.

Natumaini maelezo yangu na ya wachangiaji wengine yatakuwa yamekusaidia kwa namna moja au nyingine, kwa niamba yao basi twawatakia kila lililo jema na Mungu afanikishe matakwa yenu kwa mapenzi yake.

Midaz!

Thursday, 4 June 2009

Nilikuwa napita tu,sasa aning'ang'ania-Ushauri!

"Dinah Mpenzi,
first of all am in cross-roads, yaani ni balaa. Najua watu wengi wakishasoma hii e-mail watanipaka sana, lakini najua kuna wachache watanishauri how to over-come na hicho ndo kitu cha msingi sana kwa sasa. Hali hii inaweza ikamtokea mtu yoyote.

Mimi ni mdada mwenye miaka 23 ninaingiza 24 karibuni, nina kazi nzuri kiasi, nina masters ila bado sijaolewa na wala sina mtoto. Kisa cha kuwaandikia wewe pamoja na bloggers kinaanza kama hivi:

Nilikuwa na boyfriend mwenye miaka 26 sasa, nimekuwa nae toka A-level mpaka chuo nillivyomaliza under-graduate, we dated for six years, nilikuwa nampenda kuliko chochote sikudhani kama kuna maisha bila yeye. Kwao hawakuwa na uwezo sana, hivyo mara nyingi nilikuwa namsaidia kimahitaji coz kwetu kwa wakati ule kidogo mungu alituwekea mkono, lazima nishukuru.


Tulivyo maliza chuo , nikapata kazi lakini yeye alikuwa bado hajapata hivyo nikamtafutia kazi akakataa kufanya eti mshahara mdogo, nikamwambia tukazane na mambo yatakuwa sawa lakini akagoma, alafu kila siku akawa ananiomba hela nikiwa sina ananinunia, basi ikaenda mpaka nikamwambia nimechoka. Maana nilikuja kugundua he was only using me.


Basi nikachukia wanaume, and I stayed single for 9 months, then I met this guy, amenizidi Umri he is 44, at first nikamtolea nje then as time goes nikajikuta nampenda, mbaya zaidi ameoa, sikujali nikasema i'm having my time na huyu atleast katulia, he is matured, mizinga na ujinga wa kitoto hana, mpaka hapo ntakapopata wangu.


Now we have like 10 months, baba kanogewa, and more worse kaenda kumwambia mpaka mkewe kwamba nina mwanamke nataka kumuoa mke wa pili na ana mtoto wangu, mke kaja juu, ndoa yao imekuwa haina amani, mimi mwenyewe sina amani.


Nikamwambia kwanini umefanya hivyo anasema "mie nakupenda na siwezi kukuacha ukawa na mwanaume mwingine", nikamwambia we have to end this thing lakini hataki ananiambia eti basi mimi simpendi, nikamwambia "do u know that u'r married, na mimi i have to look for my own sio wewe na mbaya zaidi i can not be your second wife".


Ikawa ni zogo bin zogo, yaani tulipo hapa hatuna amani, nimechanganyikiwa. Familia yangu inataka kuni-dis-own na baadhi ya friends wanishauri nikubali kuwa nae b'coz ananipenda sana, sio mhuni and he is down to earth kwangu.


Lakini mimi naona that's not proper he belongs to someone else, mpaka mkewe nishaongea nae ananiomba nimwache. I feel guilty, sincerely speaking huyu mwanaume na mimi pia nampenda he is so loving, sijawahi ku-enjoy kama hivi. Ila sasa ni wa mtu mwingine sina budi kum-rejesha. please nishaurini jinsi ya kumuacha tafadhali. msinitukane hapa ndio nimeona ni kimbilio naweza kupata ushauri.
thank you."

Dinah anasema:Mpendwa bi mdogo nashukuru kwa mail yako, uwazi na uvumilivu wako. Kutoka na mwanamume wa mwenzio ni kosa kubwa sana na haijalishi kisingizio gani utatumia bado kitendo chako kitabaki kuwa ni kosa.

Hii ni mara ya nne ndani ya mwaka mmoja natoa maelezo juu ya mwanamke kutoka na mume wa mwanamke mwenzie, japokuwa tendo ni moja bado sababu na kwanini ilitokea na kitugani kifanyike inatofautina kutokana na maelezo ya mhusika.


Uamuzi wako wa kusitisha uhusiano huo ni wa busara na kutokana na umri wako sina budi kukupongeza. Mpaka imefikia mkewe anakuomba wewe umuachie mume wake ni wazi anamuhitaji na kumpenda huyo mumewe kuliko wewe unavyomhitaji napengine kumpenda.


Kuna sababu nyingi zinazomfanya mkewe aendelee kumhitaji mumewe na kubwa kuliko zote ni watoto, hasa kama bado ni wadogo (miaka 44 bado atakuwa na watoto wako shule) huyo mwanamke mwenzio ambae ni mke wa huyo soon to be ex hawara yako anapigania sio mapenzi yake juu ya mumewe bali mapenzi ya mumewe kwa watoto ambao hawana hatia yeyote na wahastahili kusumbuliwa kiakili, kimwili na kihisia.

Kumuacha mwanaume ni rahisi sana, haijalishi unapenda kiasi gani kama kuna sabau za msingi huwezi kuendelea kuwa nae unampa kitu cheupe na kikavu....hakuna kuweka "unajua nakupenda au nilikupenda", usimwambie "unajua wewe umeoa na unawatoto" mwanaume yeyote Fala kwake hilo sio tatizo kwani anajua atakulala wewe na bado mkewe na watoto watabaki kuwa wake.

Unapaswa kumwambia kitu kibaya na nitakachomuumiza na kitakachomfanya ashukuru Mungu kuwa na mkewe nyumbani....hata kama ni uongo utumie ili kuua uhusiano huo ambao unaumiza hisia sio tu za mkewe bali zake huyo mwanaume na watoto.


Kama mwanamke mdoo na wa kisasa unaejua maisha yalivyo na jinsi gani watoto walioko ndani ya ndoa huteseka baada ya wazazi wao kuachana, usingethubutu kabisa kukubali kutoka nahuyo m-baba kwa kipindi chote hicho.......well yametokea na hatuwezi kuyabadili bali ni kutafuta namna gani basi ya kuwezesha wewe kutengana na hatimae kuachana kabisa na mume huyo wa mwenzio.


Basi kwa kuzingatia yaliyosemwa na wasemaji hapo chini unaweza pia kutekeleza haya yafuatayo:-

1-Badilisha mawasiliano yako.
2-Kama inawezekana badilisha makazi.
3-Badilisha mtindo wako wa maisha.
4-Unaweza kutambua mipaka kati yako na hao unawaita marafiki kwani kutokanana ushauri wao sio wazuri na hawakutakii mema.
5-Zingatia kazi zako zaidi kuliko kitu kingine
6-Tambua kuwa wanaume wako tofauti, kama yule alikuumiza na kukufanya uchukie wote basi jifunze na utambue kuwa kila mwanadamu anaumbwa na tabia zake kama an individual.
7-Jiamini ili kupata mpenzi wa umri wako na ambae hana mzigo.

Tambua kuwa wewe ni mrembo, umesoma, unajitegemea na bado kijana, sasa kitu gani kinakufanya utoke na mwanaume mtu mzima aliechovya-chovya maisha yake yote kabla hujazaliwa?

Kila la kheri!

Tuesday, 2 June 2009

Nifanyeje kumridhisha Demu wangu-Ushauri

"Nifanyeje, Mimi ni kijana wa miaka 29 sasa. Niko kwenye mahusiano na msichana ninayempenda sana. Nimepata kuwa na mahusiano na wasichana wengine huko nyuma, ukweli ni kwamba katika mahusiano yangu ya awali,wasichana wote walikuwa wakiridhika sana na Ngono kwani nilikuwa nikiwafikisha(Orgasm) mara kwa mara na ilikuwa rahisi kujua japokuwa walikuwa wakiniambia.


Wengi wao waliipenda saizi ya uume wangu(Mkubwa kiasi).Najua kabisa kwamba size si kitu ila kusema ukweli nilikuwa nikijitahidi sana kuwaridhisha. Kwani kwangu mimi bila kumridhisha mwanamke mwenyewe siridhiki.


Tatizo huyu niliye naye sasa ambaye nampenda hata kuliko hao wa awali, namtimizia kila kitu, namwandaa vizuri ikiwa ni pamoja na kwenda chumvini, nampa maneno matamu na namtia kwa ufundi wote pia na kuchukua muda kupizi lakini cha kunishangaza katika kipindi cha miaka 2 tuliyokaa naye amewahi kufika kileleni mara moja tu.


Hiyo inaniuma sana maana naona kama simridhishi. Mapigo yangu ni yale yale kama ya zamani kwani ktk kujaribu nilikutana na mmoja wa wapenzi wangu wa zamani, akafika kileleni mara 2 ndani ya nngwe moja. Na akanihakikishia kwamba ktk wanaume mimi niko safi na ndio maana hata alikuwa tayari kufanya sex na mimi wakati tulishaachana na anauhusiano mwingine.

Mimi napenda kumridhisha mpenzi wangu wa sasa...nifanyeje Dinah????am serious"

Dinah anasema: Ngoja kwanza nicheke (hihihihihihihi) kwani nimeshindwa kujizuia....unajua unakosea wapi? kwenye mapigo yako yaleyale ya zamani...hebu up2date mapigo yako bana alah!

Asante sana kwa mail yako na kwa uwazi wako japokuwa umenisikitisha baada ya kwenda ku-cheat na mpenzi wa zamani ili kupima mapigo yako, unajua huyo ex ameshakutana na wanaume wangapi tangu mmeachana? Ngoma is real, kuishi na HIV Virus is dead expensive Dolla 60 kwa dozi moja kwa mwezi sio kitoto.....nilikuwa nawakumbusha tu, haya tuendelee sasa.

Binti huyo alifika mara moja tu ktk miaka miwili, hiyo inaonyesha wazi kuwa anauwezo wa kufika kileleni kama ifuatavyo bali wewe na yeye mnashindwa kuwasiliana vema na kwa uwazi. Kuna uwezekano mkubwa alifika kileleni kwa vile alikuwa nanyege nyingi hivyo basi huenda haukuwa ujuzi wako siku hiyo kama unavyodhania.

Kuna vijimakosa nimevigundua hapa, (1)- Ufanyaji wako ni uleule ambao kwa namna moja au nyingine sio cup of tea kwa mpenzi wako huyu wa sasa bali wale wa zamani hivyo basi unapaswa kubadilisha ufanyaji/mapigo yako kuanzia hivi sasa. Jaribu kuwa mbunifu zaidi.

(2)-Unatumia "kanuni" iliyokuwa ikiwafikisha wa zamani nahivyo basi unashupalia kumridhisha mpenzi wako bila kujua ni wapi hasa pakiguswa au fanyiwa kazi vilivyo anaridhika kama an individual.

Ni wazi kuwa hujui au umeshau kuwa wanawake tumetofautiana sana japokuwa wote tuna viungo vilevile, kila mwanamke anamatakwa yake linapokuja suala la kufanya mapenzi au kungonoka.

(3)-Mawasiliano yenu kwenye ngono sio mazuri. Mueleze mpenzi wako ni jinsi gani unaumia ikiwa mnafanya mapnezi lakini yey hafiki kileleni, muombe akuambie wazi ni kitu gani anapenda wewe ukifanye au umngonoe ktk mwendo gani ili afike kileleni....kuweni willing kujifunza na kujaribu vitu tofauti.

Hebu bonyeza hapa ili ufahamu mwanamke na kufika kileleni, Makala hii itajibu sehemu ya swali lako.

Hisia za mwanamke zinabadilika badilika kutokana na homono mwili mwake, hali inayoweza kusababisha kusua sua kwa mahitaji yake ya kingono (anakuwa na hamu lakini anashindwa kuzingatia tendo na kufikia mwisho/mshindo)......kabla sijaenda kwa undani kuhusu sababu za Kibailojia na Kisaikolojia, wewe kama mpenzi wake wa muda mrefu, unadhani yapi kati ya haya yafuatayo yanamhusu mpenzi wako nje na ndani?

(1)-Amewahi kutoa mimba au kuzaa?
(2)-Amewahi kuugua gonjwa lolote na kutumia dawa kutibu tatizo?
(3)-Mnatumia kinga? Hofu ya kushika mimba iau Ngojwa la zinaa inaweza kumfanya ashindwe kufika.
(4)-Uhusiano wenu ni rasmi au bado anaishi na wazazi wake? Hofu yakuwahi nyumbani inaweza kumfanya ashindwe kuzingatia tendo n.k.
(5)-Je anakuamini kwa asilimia zote (tangu useme ulitoka na ex wako ili kupima mapigo hata mimi napata shida kukuamini).

Kila la kheri.