Wednesday, 18 March 2009

Penzi limepauka Baada ya Kutoka Ulaya-Ushauri!

"Dinah pamoja na wanablog hi(wenzangu) hope Mungu amewapendelea bado mpo wazima, nashukuru kwa hilo.Tatizo langu i wish to know what is going on!


Habari ipo hivi; ni ndefu najitahid kuifupisha and if theres any question I will be there plz, I have a boyfriend and I Love him so very much! Tatizo ni kuwa simwelewi siku hizi kwani hataki tuonane na nikimpigia simu hapokei, nikituma text anajibu siku anayojiskia. Nikimwuliza vp mbona hivi anauliza kwanini kwani yeye ni mzima wa afya wewe tu" ndo anavyojibu kwa msg mana sim hapig wala hapokei.


Huyu bwana miaka minne nyuma alikua anasoma UK kamaliza na mwaka jana karudi yupo TZ, nilimpigia kabla hajarudi nikamwuliza unakuja lini? akaniambia zilikua zimebaki siku chache.

Siku ya siku ikafika akawa amekuja na alipofika alinipigia kanifahamisha amefika na akanipa namba yake na kusema kuwa kuna kazi anafanya na atanicheki baadae, nikamwambia poa. Lakini ile baadae aliyoniambia haijafika hadi leo kuanzia mwaka jana mwezi wa tisa hadi leo tarehe 25 february!

Ndo hivyo, namwuliza kwanini unafanya hivi? anasema "kwani nimefanya nini?" Hasemi chochote na nikimwuliza is it over between us hasemi kitu, kanisumbua sana ukizingatia nilikuwa namsubiri tangu aende kusoma miaka minne anarudi leo ananifanyia mambo kama hayo,kweli is it fair?


I have been faithful for him since I knew him, sio hapo tu nimwaminifu hata kabla sasa kwanini anakua hivi? sijui anafanya nini? anawaza nini? or what is he passing through?Sasa ndio nawaza niachane nae na nimfute katika maisha yangu kwani naona anazidi kuniumiza tu. Pia najiuliza sijui ana matatizo gani what if naswitch my mind to another man and soon later he come back, how wil it be??

Ndugu zangu nasubiri mchango, mawazo,ushauri kutoka kwenu,nitakuwa najibu maswali yenu kama kuna mahali hamjanielewa.
thanx"

Jawabu:Hello, asante kwa kuwa na subira lakini hata hivyo maelezo ya wasomaji wangu kwa kiasi fulani yatakuwa yamekufungua macho nakuanza kuyafanyia kazi yale ambayo ulidhani kuwa yatakusaidia.


Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa kuna mambo mawili-matatu yanayomfanya bwana kukukwepa tangu arudi nyumbani. Kama sio kuwa alikuwa na wewe ktk mtindo wa kupoteza muda au kwa maana nyingine wanasema "4 fun" na hakuwa "serious" na uhusiano wenu basi yuko kwenye mshituko wa hali halisi ya maisha hapo nyumbani tofauti na alivyodhania wakati yuko Ulaya. Vilevile huenda kurudi kwake nyumbani hakukuwa kwa kujiandaa bali kushitukizwa (karudi bila kukamilisha mipango yake kimaisha) hali inayoweza kusababisha mshituko.


Kwa kawaida mwanaume anapokuwa hajakamilishamipango yake kimaisha suala la uhusiano wa kimapenzi huchukua nafasi ya tatu kama sio ya mwisho kabisa, yaani inakuwa sio muhimu sana na anaweza kuchukulia mapenzi au uhusiano ni kupotezeanaa mida kwani sote tunatambua kuwa anapokuwa na mpenzi ni kujiongezea jukumu maishani. Sasa kama majukumu uliyonayo yanakushinda au hujayamudu vya kutosha kwanini basi ujiongezee jukumu lingine.


Kukukwepa haina maana kuwa jamaa hakupendi la hasha! huenda anakupenda ila mpangilio wake kimaisha hauruhusu yeye kuwa na wewe na hapendi kukuumiza au anashindwa namna gani akuambie kuwa anakupenda sana tu lakini angependa uendelee na maisha yako.


Napenda ufahamu kuwa pamoja na kuwa wanaume wanahitaji mapenzi, kupendwa, kujaaliwa nakadhalika kama ilivyo kwetu sisi wanawake, wao wanalichukulia suala zima tofauti kabisa natunavyolichukulia sisi wanawake

Nakuja sasa hivi...