Saturday, 28 February 2009

Baada ya kutibu tatizo nimepoteza ute "terezi" -Ushauri

"Hi Dada Dinah, kwanza pole kwa majukumu makubwa ya kuelimisha jamii.
Mimi ni msichana wa miaka 26 nina tatizo la kukaukiwa majimaji yaani ile fluid mucus ndani ya uke ni nzito.

Nimeshaenda kwa madaktari mara 2, nimepimwa vipimo vyote, nilichukuliwa majimaji ukeni , vipimo vya mkojo,choo kikubwa, pamoja na kupigwa ultra sound ya tumbo ili kuangaliwa kama kuna tatizo.


Mara ya kwanza nikaambiwa nina maambukizo kwenye mirija ya uzazi pamoja na fungus ukeni kwa kuwa nilikuwa nahisi kuwashwa kila wakati. Nikatumia dawa za vidonge pamoja na kupaka kwa sababu ya zile fungus.


Nikakaa kama miezi miwili nikaenda tena kucheki na kufanyiwa vipimo kama vile vya mara ya kwanza, nikaambiwa sina tatizo lolote mirija imeshakuwa safi na fangasi pia zilikuwa zimeisha.
Nikapewa tena dawa za kutumia na mpaka sasa ni mwezi tena sijaona mabadiliko yoyote.


Dactari alisema nikimaliza dawa kila kitu kitakuwa safi, lakini naona Fluid bado ni kavu yaani nzito, haijalishi ni siku za hatari au za kawaida. Je nifanye nini angali natafuta mtoto? kwani inasemekana kuwa wenye ute mzito hawawezi kushika mimba.


Ufafanuzi; Naomba nieleze kwamba tatizo sio kujisafisha kwani ile makala ya kujisafisha ya kipindi cha nyuma niliisoma na ninaifanyia kazi kama kawaida. Tatizo linakuja kwamba ile fluid inayotoka the whole month ni ile nzito tu na sio ile fluid ya kuteleza au kuvutika kama elastic. Kwani ninavyojua kuna fluid za aina mbili, moja ni ule utoko mweupe na unakuwa mzito, mwingine ni ule wa kuteleza kwa ajili ya kusafirishia mbegu za kiume.


Mimi tatizo langu sana sana ni ule wa kuvutika au wa kuteleza yaani hata ukiingiza kidole wakati wa kijiswafi inakuwa rahisi. Mimi wakati wote unakuwa ni ule utoko tu, tena wakati mwingine kwa mfano nikishajisafisha ile jioni, asubuhi ninajikuta ni kukavu sana hata kidole tena hakiwezi kuingia. Nikijitahidi sana kidole kikiingia basi nakuta ute ule umeganga kwenye zile kuta na mzito kabisa.

Je niende tena kwa Wataalam wanisafishe mirija ya uzazi au nifanye nini?
Naombeni ushauri wenu wana blog pamoja na dada Dinah.
Happy"

Jawabu: Happy asante kwa mail na ufafanuzi wa kina kuhusiana na tatizo lako, kama ulivyolieleza tatizo lako ni la kitibabu zaidi na sio Kisaikolojia au Kihisia. Hivyo mimi kama Dinah itakuwa ngumu kukushauri lolote kwa vile sina utaalamu wa kitibabu (Daktari).


Mirija ya Uzazi kuziba ni tatizo "serious" na usipokuwa muangalifu linaweza kupelekea wewe kuwa Mgumba (kwamba hutoshika mimba kirahisi lakini kwa juhudi za madaktari, afya ya mbegu za mumeo na juhudi zako wewe mwenyewe unaweza ukashika mimba nakuzaa mtoto mwenye afya njema kabisa), kama umeolewa na uko tayari (zingatia tatizo lako) huu ndio wakati wako mzuri wa kuanza kujaribu kumimbika.


Kutokana na maelezo yako nafikiri upotevu wa ute "terezi" ambao mara nyingi hujitokeza unapokaribia kupevusha yai (siku hatari kama hutaki mimba na ziku za kumimbika kama wataka kuwa mama) na vilevile unaponyegeka/nyegeshwa inaweza kusababishwa na "side effects" za madawa uliyokuwa ukitumia kwa kifupi ni kuwa Dawa hizo zimekusababishia ukavu ukeni.


Matumizi ya madawa mbali mbali achilia tatizo ulilotibiwa, mara nyingi hukanganya/changanya mpangilio wa homono mwilini mwa mwanamke na mzunguuko wa hedhi kwa ujumla, hivyo ukirudi kwa daktari na kumueleza nini kinatokea hivi sasa atakupatia dawa zilizo-base kwenye homono ili "kuzichangamsha" ili zianze kufanya kazi ipasavyo au kuziongeza kama zilikuwa zimepungua.


Ikiwa unapata nyege kama kawaida na ute "terezi" basi hutakiwi kuwa na hofu lakini kama unakuwa na nyege lakini uke bado mkavu tafadhali rudi tena kwa Daktari na mueleze kwa uwazi kabisa, usione haya kuzungumzia nia yako ya kufurahia tendo la ngono na hatimae kushika mimba.

Muulize daktari maswali mengi kuhusiana na hofu yako ambayo inasababishwa na tatizo alilokutibu na yeye atakupatia msaada zaidi na hata madawa ya kuzifanya homono kujirudi kama sio kuziongeza (dawa hizo zipo na zinapatikana ikiwa Daktari kashauri uzitumie).


Nakutakia kila la kheri.

Friday, 27 February 2009

Hivi Bikira inatoka kwa nyeto?-Ushauri

"Mambo dada dinah na pole kwa kazi. Nilikuwa nauliza eti punyeto au masturbation ina ondoa bikira? Nauliza hivi kwa sababu rafiki yangu ana afanya punyeto kwa kutumia kanga anajiweka huko chini.Sasa kwa mfano mtu umejingiza kitu ndani ya uke na bikira ikatoka, ukienda hospital kucheck utajulikana kama imetoka kwa ajili ya kuingiliwa na mwanaume au umefanya punyeto au kama watu wengine wanavosema kama inatoka kwa ajili ya kuendesha baskeli, au itakuwa hospital wanajua imetoka kwa design ya hivyo labda ya kuendesha baskeli?


Najua nakusumbua samahani sana....Je, nakipindi chako kinaanza saa ngapi na kwahiyo hiyo jumapili ndio unatumia hiyo number tu ukimaliza hapo hutumii tena hiyo number, kwasababu mie nilikuwa sijui hii radio nimesearch kwenye internet ndio nikaona hii blog, naomba nijibu hili swali jengine nilokuuliza nakuomba msamaha tena kwa sababu najua nakusumbua.
Kazi njema."


Jawabu:Asante sana kwa mail yako. Kwa maana halisi ya Bikira ni ile hali ya mwanamke ambae hajawahi kabisa kuguswa na mwanaume kwa maana ya kuingiliwa kingono na hajui raha/utamu wa ngono. Mwanamke huyu huwa na kijiutandu mfano wa kingozi laini juu ya uke wake (pale uume unapoingia) yaani chini kidogo ya kikojoleo (kitundu cha mkojo).


Hivyo basi kwa jibu la haraka haraka hapa ni kuwa Nyeto inatoa Bikira, yaani kusikilizia ule utamu wa ngono ni wazi kuwa wewe sio bikira tena, kwa sababu mwili wako unaponyegeka hufanya misuli ya uke kutanuka na ute kujitokeza pale mahali ambapo ule "utandu" ndio ulipo((pale uume unapoingia).


Kule kuhangaika kwako kingono (inaweza kuwa juu-chini, huku na huku au kuzunguusha kiuno) na hatimae kubana na kubanua misuli yako ya uke kwa ndani na nje unapofika kileleni kwa kujipa mkono/nyeto ni wazi kuwa kutakuwa kunakamsuguano ambako kanaondoa "utandu" ambao kikwetu ndio Bikira yenyewe.


Pamoja nakusema hivyo kuna aina mbili za Bikira moja ni ile yenye "utandu" na huendelea kubaki pale hasa kama binti husika ni mtu wa kutofanya shughuli ngumu na nyingine ni ile ambayo haina "utandu" ambayo nadhani mabinti wengi miaka hii ndio wanayo kutokana na mitindo ya maisha tunayoishi siku hizi. Bila kujali utofauti wake, zote zinajulikana na kuhesabika kama Bikira kwa vile binti hajui Ngono ikoje na hujaguswa kabisa mwili wako na mwanaume.


Napenda utambue kuwa michezo kama kukimbia/kuruka kamba, mazoezi ya viungo, kuendesha baiskeli hakuondoi bikira kama inavyo ondolewa na tendo la ngono, kinachotoka pale ni ule utandu na ubikira (hujui utamu wa ngono na hujawhai kulifanya tendo hilo) unabaki palepale......tofauti ni kuwa wewe ambae huna utandu uume unaweza kuingia haraka kuliko yule mwenye utandu.

Kingine ni kuwa mwenye utandu hutokwa na damu nyingi zaidi kuliko yule ambae hana utandu. Lakini wote ni bikira kwa vile hajui utamu wake kwa Nyeto na hamjawahi kungonoka.


Ukifanya nyeto kwa kutumia kanga (kama ulivyosema) bila kuigusisha kwenye uke (unapoingia uume) na ukawa unaigusisha kwenye kisimi tu ni wazi kuwa Daktari hatoweza kugundua kuwa umeingiliwa na mwanaume, kwa maana kuwa hujaingiziwa uume ukeni.....lakini ktk hali halisi hautokuwa Bikira kwa vile unajua utamu wa ngono tayari.


Kama ukifanya hivyo (Nyeto) na ukajiingizia kidole au sanamu Daktari akikuangalia atajua kuwa umeingiliwa kingono, kwao haijalishi ulitumia nini, watakachokiona ni kuwa ukeni kuna kitu kiliingia....nini kiliingia ni juu yako wao wanajua kinachoingia pale ni uume hatakama ni wa plastic....hivyo hutohesabika kuwa ni bikira.


Upande wa kulia kuna Nembo ya Bongo radio, ukibonyeza hiyo itakupeleka kwenue ukurasa wa Radio hiyo. Fuata maelekezo ili kusikiliza. Kipindi ni kila J'2 saa tatu kamili Usiku Tanzania. Karibu sana.


Vumilia mpaka utakapo kuwa mkubwa, umekutana na mtu umpendae na uko tayari kwa ajili hiyo ili kufanya the moment kuwa extra special, kwani ni siku pekee utakayoikumbuka ktk maisha yako yote hivyo ni muhimu kuruhusu mtu umpendae na kumuamini ili akutambulishe ktk umlimwengu huu wa Ngono, ikiwezekana basi ndio awe mumeo.


Tafadhali usifanye Nyeto kama wewe bado ni bikira, subiri mpaka utakapoanza ngono na mpenzi/mume wako.

Kila la kheri.

Thursday, 26 February 2009

Pesa anazo lakini hanihusishi-Ushauri

"Mimi ni mwanamke wa 25 nimeolewa miaka 3 iliyopita kwasasa ni mjamzito hivyo niliacha kwenda kazini tangu mimba hii ilipoingia kutokana na matatito ya kiafya. Mume wangu ana nafasi nzuri kazini na kipato chake kinakidhi mahitaji ya familia yetu.


Baada ya matumizi muhimu kwa kawaida najua anabakisha kama laki 5 kila mwezi lakini hakuwahi kunijulisha kama ana pesa hizo au ana plan gani na mabaki hayo ya pesa, nikimuuliza anasema hana pesa.


Wakati huo mimi kuwa baada ya mahitaji muhimu najua pesa fulani hubaki na sasa amefikisha million 5 lakini hataki kusema ukweli, Pesa hizo zipo kwenye account nami najua password yake lakini yeye hatambui hilo.
Je mtu wa design hii nimchukulie kama alivyo au nimweleze ukweli"


Jawabu: Asante kwa ushirikiano wako, inaonyesha wewe ni mmoja kati ya wanawake wachache ambae ulikuwa ukijituma ili kuchangia kipato ndani ya nyumba na ninachokiona hapa ni ile hali ya "kujishitukia" kwa vile hufanyi kazi unafikiri mume wako atakunyanyasa na bila kujijua unaamua kuomba pesa ambazo pengine wala huzihitaji....kama ulivyosema mwenyewe kuwa anakamilisha mahitaji yote muhimu.


Kitu kingine ninachokionahapa ni kuwa na hofu kuwa anaweza kuwa anazitumia pesa zinazobaki kwa ajili ya mambo mengine kama vile "kuwekeza" kwenye Ulevi na wanawake nje ya ndoa yane kwa vile tu wewe ni mjamzito (kutokana na matatizo ya kiafya ni wazi kuwa tendo la ndoa halipo vile inavyotakiwa kitu ambacho kinaongeza hofu).


Lakini kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa pesa zote zinazobaki baada ya mahitaji muhimu anazitunza Benk, hazitumii kivingine. Kumbuka wewe ni mjamzito which means kuna "mtu" mwingine ataongezeka kwenye familia yenu ndogo na badala ya kuwa wawili mtakuwa watatu nahivyo basi majukumu yataongezeka na kwa mshahara wa mtu mmoja tu mtoto hatokuwa na maisha bore.


Sasa ili mtoto kuwa na maisha bora au angalau "comfortable" ni wazi kuwa kuna ulazima wa ninyi kama wazazi kujiandaa na jukumu hilo jipya. Si hivyo tu bali kuna matukio ambayo hujitokeza bila mipango kama sehemu ya maisha yetu yanaitwa "udhuru" ni wazi kwa akiba inahitajika incase kitu kama hicho kinaibuka.


Sote tunapokuwa na mipango fulani na pesa tunazotunza ili kukamilisha jambo fulani alafu mtu akaibuka na kukuomba seti au kukuazima ni wazi kuwa utamwambia kuwa huna pesa....sio huna kabisaaa bali ulizonazo zinamipango yake muhimu na hutaki kuzigusa unless upate "udhuru" kama kuuguliwa, msiba n.k.


Umchukuliaje?-Since unalo neno/namba ya siri ya Benki Akaunti basi mchukulie kuwa ni mmoja kati ya mwanaume wachache wanaojua majukumu yao, anangalia mbele na sio pale mlipo (kuvaa miwani ya mbao) pia ni muaminifu na ndio maana akakupa neno/namba ya siri ya account (natumai hukuitafuta mwenyewe balia likupa baada ya kuomba).....vinginevyo mume wako anajaribu kufanya mambo yake kama mwanaume na wewe unapaswa kumuamini.


Nini cha kufanya-Hakuna ukweli wa kumuambia hapo kwasababu moja, Pesa ni zake, Pili hazitumii bali ziko pale zimetulia, tatu wewe unataka pesa za nini wakati kila kitu unatimiziwa ndani ya nyumba?


Kama unawasiwasi sana na wewe ni mwanamke kamilifu na mke hivi sasa ni lazima ulifunzwa namna ya kupata unachotaka kutoka kwa mume wako kwa kutumia lugha ya kimapenzi (siwezi kusema hapa kwani kaka zangu wakijua hatutopata kitu), sasa tumia mbinu hiyo kwa mume wako na hakika atakueleza mipango yake kuhusu pesa hizo (akiba) na hapo utapata amani moyoni mwako.

Acha kujishitukia kwa vile umeacha kazi, jiamini hali itakayokusaidia kumuamini mume wako.
Kila la kheri.

Wednesday, 25 February 2009

Nikifanya mapenzi nawaza Mwanamke, ni Ulesbo?-Ushauri

"Mpendwa Dinah, Kwanza napenda kusema hongera sana kwa kazi hii nzuri.
Pili ningependa kusema kuwa niko desparate sana kupata msaada wako maana nina tatizo ambalo mimi binafsi naliconsider kuwa ni serious sana. Nina imani na wewe kuwa utanipatia japo uwezo tu wa kulitafakari vizuri maana linanichangana akili!!


Basi kwa kifupi mimi ni mwanamke wa miaka 32 na nimeolewa miaka 7 sasa na tumezaa watoto wawili na mume wangu. Naweza kusema mpaka sasa Mungu anaendelea kunibariki na sote tunaifurahia ndoa sina tatizo kwa hilo.


Ila tu naona tatizo labda linaanza sasa kwasababu zifuatazo:-
Zamani nilipokuwa college na umri wa kama miaka 18-20, nilipata feelings za kufanya mapenzi na mwanamke mwenzangu, feelings hizi zilikuwa kali sana kiasi kwamba nilianzisha urafiki na msichana mmoja ambae tulikuwa karibu sana lakini hatuku have sex ila tulikiss tu.


Baadae nilipomaliza college nikasahau kabisa na feelings hizo zikapotea kabisa. Sasa kuanzia kama miaka miwili iliopita zile feelings zimerudi tena, nimeanza kuwa na fikra sana za kukutana kimwili na mwanamke(fantasies), siku za mwanzo sikuichukulia serious kwasababu nilidhani ni kitu cha kuja na kupita tu, lakini siku zinavozidi kwenda naona feelings hizi zinazidi kupita kiasi, ninakuwa nafantasise sana kuwa na mwanamke mwenzangu.


Imefikia hatua nimeaanza kumuwaza sana dada mmoja ambae ni rafiki tu na ananipenda sana(kiurafiki lakini), nimeanza kuwaza kumkiss na kulala nae. Imefikia hatua nataka kuact on these feelings kabisa.


Sasa the worse ni kwamba nikifanya mapenzi na mume wangu naanza kufantasise kuhusu wanawake na hii inanisumbua sana.The worst to this ni kuwa dada mmoja ameshahisi kuhusu feelings zangu na sasa anataka urafiki nami wa kimapenzi, nilimuambia hii issue kupata ushauri tu kama rafiki, (ni lesbian) na sasa naogopa nisije nikacheat nae. Siko tayari kuharibu this marriage kwasabu nampenda bado mume wangu ndio maana naomba msaada wako.


Swali: Je hii ni normal kwa wanawake wa umri kama wangu? na kama si normal je mimi ni lesbian? nimeshaolewa na nina watoto na feelings za kuwa na mwanamke ndio zinanimaliza nguvu, Please help?

Nitashukuru kama utapost hili tatizo langu ili nisikie watu wengine wanasemaje pia.Kazi njema.
Justice!"

Jawabu:Asante sana kwa kuipenda kazi yangu na ninafurahi kukukaribisha mahali hapa. Nilipo ona mail yako nusura niifutilie mbali lakini baadae nikakumbuka kufuata taaluma, kwamba unafanya kazi bila kujali Ujinsia, Urafiki wala Ukabila.....haya tunaenda hivi;


Inasemekena kuwa kuna wanawake ambao tangu wamezaliwa wanakuwa na homono za kiume na hata miili yao inakuwa kama wanaume napengine hata miondoko yao inakuwa ya kiume japokuwa wanakuwa na viungo vya kike kama matiti, uke, hips n.k


Alafu kuna wale ambao wanaamua kuwa hivyo kutoakana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuathirika kisaikolojia...mfano; kuumizwa na wanaume kwenye mahusiano ya mwanzo, kutokufurahia ngono na mwanaume kwa vile walibakwa/abused huko mwanzo, kujiendekeza, kukata tamaa kwa vile hawapati wanaume kama wapenzi.


Vilevile kutokuwa na mama/baba kwenye maisha yake, kulelewa na mama(single mom) ambae anahasira na wanaume na kuku-feed ubaya wa wanaume hali itakayo kuathiri kisaikolojia, Mazoea, Usawa (mwanamke kuwa powerful kipesa), Uchumi (mabinti kukubali kusagwa na wadada powerful kifedha), Uoga wa kupata Mimba n.k.


Kunauwezekano mkubwa kuwa wewe ulisoma Shule ya wasichana watupu na haikuwa yakwenda nakurudi (day), Wasichana wengi waliopitia shule hizi mara nyingi huathirika Kisaikolojia na kujikuta wanaibua "hisia" dhidi ya wanawake wenzao pale wanapokuwa kwenye harakati za ukuaji (mabadiliko ya kimwili).


Sote tunajua kuwa kipindi cha ukuaji kwa wanawake ni kigumu kuliko, kuna hisia za ngono zinaibuka na hakika unahisi kabisa kushikwa-shikwa sehemu fulani za mwili wako...Mf-Kiuno, matiti n.k......sasa kwa vile wanawake tunatabia ya kuaminiana na kulala kitanda kimoja, kuoga pamoja, kushikana mikono, mabega, viuno n.k. (sio miaka hii though...damn I dont trust women anymore hihihihi ni noma!) kwa vile hatuna mboo hivyo baadhi uruhusu wanawake wenzao kufanya hivyo bila matata kabisa ili kuua ile hali ya mahitaji ya miili yao ambayo ktk hali halisi (kidini na kitamaduni) ni mwanaume tu ndio anapaswa kuiondoa......hali ambayo hujenga mazoea kwa baadhi ya wasichana na siku moja utakuta wanaamua kufanya ngono.


Kwa kawaida wanadamu huwa hatusahau wapenzi wetu wa mwanzao waliotutambulisha kwenye ulimwengu wa Ngono, sio kwa vile walikuwa "wazuri kitandani" la hasha! bali walikusababishia ile raha/utamu kwa mara ya kwanza na ndio maana kuna watu wanaamini kuwa Penzi la mwanzo huwa haliishi lakini uweli ni kuwa zile hisia ulizonazo then huwezi kuzisahau.


Sasa, kama wewe binti ambae sasa ni mwanamke ulianza kamchezo hako kachafu na mwanamke mwenzio ni wazi kuwa mara kwa mara utakuwa unakumbukia ilivyokuwa, ulivyojisikia.....ni uzoefu wako pekee na wa mwanzo kabisa hivyo lazima utakuwa unakumbukia au hata kutamani kurudia lakini that doesnt make you lesbo but a young woman (18-20 then ni mtoto tu) who didn't know what she was doing.


Kosa-Ulilofanya ni kwenda kumuuliza Lesbo kuhusiana na hisia zako, hata kama angekuwa mwanaume ukamuibukia na swali la hisia zako Mf za 3some na yeye anapenda the idea hakika atakufuatilia ili mkafanye. Ulitakiwa kuzungumza na mumeo au hata Daktari ambae angekupeleka kwa Mtaalam wa Ngono na Saikolojia na wangekusaidia.


Fantasies-Wapenzi wengi mara chache hufikiria watu wengine wakiwa wanafanya mapenzi hasa kama wanafanya tendo hilo na wanahsindwa kufikia mshindo.....Mfano; mume wako anaweza kabisa akawa anamfikiria anafira a.k.a ana-TIGO-a wakati anafanya mapenzi na wewe, hiyo haitamfanya akuombe mlango wa nyuma ili afanye kweli au kumfanya yeye Shoga/Basha.....(kumbuka mikundu inafanana hakuna wa kiume wala wa kike).

Ukweli atakuwa anajaribu kufikiria kitu tofauti na anachokifanya kila siku ili ufurahishe zaidi hiyo haitomfanya yeye kuwa shoga au kukuomba TIGO ili afanye kweli.....unless u r up 4 it?


Sio lazima u-fulfill kila fantancy.....some fantansies zinapaswa kuachwa huko huko they are belong,they are just ndoto za mchana. Huwezi kuziendekeza na kuharibu uhusiano wako na mume wako na vilevile kuharibu maisha ya watoto ambayo yatakuwa bora kama wote mtakuwa pale kwa ajili ya watoto wenu.


Is it Normal?-Kufikiria, kumbuka na hatimae kuvuta hisia kuhusu mpenzi wako wa zamani ambae labda ndio alikutambulisha kwenye ulimwengu wa ngono kwa kujua utamu wake ni kawaida (normal) sasa kwavile wewe wako alikuwa mwanamke mwenzio ndio hivyo tena lakini huko sio kuwa "jinsia hiyo ya kishoga".


Nini cha kufanya-Kwa mujibu wa maelezo yako ni wazi kuwa unampenda mume wako na anakuvutia, kama unaweza kuvutiwa na mume wako amabe ni jinsia tofauti na wewe ni basi wewe sio Msagaji hivyo basi nakushauri uende kuonana na mwanaSaikolojia na mueleze tatizo lako kwa uwazi kabisa na yeye atakupa therapy ambayo itakusaidia kuondokana na mawazo hayo machafu.


Wekeza hisia zako zaidi kwa mume wako, kuwa mbunifu zaidi.....wanaume watamu na wana mengi yakufanya juu ya mwili wa mwanaume kwa vile Mungu aliwaumba hivyo. Mwanamke hakuumbwa hivyo kwa hiyo hata siku moja mwanamke mwenzio hawezi kabisa kufanya lolote kama mwanaume kwa vile hakuumbwa kuujua na kuufanyia kazi mwili wa mwanamke.

Natumai majibu yangu na maelezo mazuri ya wasomaji wangu takakuwa yamekusaidia kwa kiasi fulani.

Kila la kheri.

Hanifikishi Kileleni....

"Dada Dinah, Mimi ni mwanamke wa miaka 26 nina mpenzi ambaye tumependana sana na mungu akijaalia ndoa yetu itakuwa june mwaka huu.

Tatizo langu ni kwamba yaani ule muda wa majambozi sifiki kileleni kabisa yaani yeye style yake ya kunitomba ni ile ya up and down (simple harmonic motion) tena kwa nguvu toka mwanzo mbaka yeye anapokojoa sasa mimi sisikii raha yoyote ile.

Before yeye niliwahi kuwa na mpenzi ambaye alikuwa ananitomba kwa kukatika kiuno na nilikuwa nakojoa sana tu kila mara, sasa naomba wadau mnisaidie jamani jinsi ya kumwambia namna ya kunitomba . asante mdada"

Jawabu: Asante kwa mail yako(nakujibu moja kwa moja kwa vile nimeshawahi kujibu/elezea hili suala few times). Tatizo lako sio kubwa kwani unauzoefu na unajua kabisa ufanyaji gani ambao huwa au ulikuwa unakusababishia kilele. Suala muhimu hapo ni kuwa wazi nakumuambia mpenzi wako namna gani unataka akufanye na wewe kujituma.

Vilevile pitia Makala za nyuma na utakutana na maelezo mengi tu ambayo yatakusaidia ktk ufurahiaji wa maisha yako ya kingono....mfano ni somo la "uwazi katika mapenzi/ngono", "mwanamke na kilele", "mapenzi ni sanaa", "namna ya kuita kilele".

Shukrani.

Tuesday, 24 February 2009

Ushuhuda wa Mama Johnson wa Mza!

Hi My Dear Dinah.
Its me again Mama Johnson From Mza.

How is Valentine 2 all Tanzanian?
Napenda kuwashukuru watanzaia na Non-tanzanian wote ambao mmenishauri hapo chini. Mimi ni Ma Johnson ambae nilituma mada yangu kwa da Dinah ikisomeka NAHISI MUME WANGU ANAJISAHAU. Especcialy my special thankfull to you Dear Dinah.

Let me tell u maana ilikuwa as a story what happened to me.
Baada ya kuwasilisha mada yangu hapa mezani sikuwa na jinsi ilinibidi ningoje matokeo kwa kujua kuwa ntapata challenges lakini na jibu litapatikana.


Nilivumilia na nikasitisha mawasiliano. Sikuwasiliana nae kwa njia yoyote ile. I was do as he do to me. Akinitumia sms nikawa simjibu. Akinipigia napokea namjibu in short kama niko kazini namwambia niko bussy kidogo ngoja ntakupigia. Na kama ni mida ya jioni namwambia ngoja ntakupigia mtoto ananisumbua mwisho wa yote sipigi wala sijibu sms zake.


Wakati huo nilikuwa nafatilia mawazo ya wanablog wenzanu ya kuwa nimfate dar bila taarifa yoyote wakati huo ndo tulikuwa tunaelekea kwenye Valentine Day. Nilifatilia maombi ya ruhusa ofisini angalau kwa siku tano ili nije dar boss wangu hakuniruhusu kwa sababu Mi ni Accounts Administrator na huwa tunafunga hesabu za mwezi tar ambazo nilikuwa nimeomba. So it was difficult to move.


Basi Mpaka ikafika tar 14 no call from me to him and no call from him to me. Roho iliniuma sana ukizingatia mi ndo nilianza kuuchuna. Siku hiyo ya tar 14 nikatoka kazini mchana as u know it was week-end. Nilipitiliza hadi home nikaandaa chakula mapema nikaoga na kujipumzisha.
Ikafika saa mbili yausiku sm yangu ikaita. Kupokea ni yeye akaniuliza uko wapi nikamwambia niko hm akaniambia toka unifungulie geti. It was supries. I felt like iwant to fall down.


Nikatoka nikamfungulia. Akaniambia samahani sana nimekuja bila taarifa. nikamwambia no worries its your home and am your married wife. Akasema nimeitahidi sana nije maana siku hiyo yaani tar 14 mwezi huu wa pili ndo tulifunga ndoa AICT na tulikuwa tunatimiza miaka 5 ya ndoa mwezi huu.


Baada ya yote akanilaumu nimebadilika nimekuwa mjeuri akinipigia sizunumzi nae akinitumia sms simjibu. Na mi nikamwambia na mi nilikuwa naumia hivyo wakati ule najitahidi kuwa karibu nae ye anakuwa mbali. Akanisihi nisifanye hivyo maana yuko mbali nipunguze mawazo he loves me sour much, hayuko radhi kunisaliti ila ni majukumu tena ya mda mchache tu.


Alikaa tarehe 16 alfajiri akaondoka. Sikumwamini hata kidogo nilijua ananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Yaani da Dinah ye aliondoka kwa flight ya saa mbili pass through Nairobi. Mi nikaondoka na Flight ya saa sita mchana.


Nilichukua chumba jirani na hotel anayoishi na kwa mda mfupi nikagundua kuwa chakula hula pale kila siku jioni. nilijenga mazoea na yule dada muudumu nikampatia cash kidogo. Akawa karibu na mimi mno. So kila nilichomdadisi alinipa ushirikiano wa kutosha bila chochote.


Pale pale kwa maelezo ya yule dada nikajua no one alse ila baadae niligundua yule dada alijua habari za pale wa kuwa house boy wa mr wangu ni jamaa bf wake. Nikamuuliza kwani huyo kaka yupo akasema alikwenda mza kuiona familia yake amerudi leo amefika tu nakuondoka ameenda kazini. Ilipofika saa mbili ya usiku alikuja pale hotelini akapata dinner akaenda nyumbani kulala. Saa tano ya usiku nikamtuma yule dada aniitie yule bf wake alishagaa sana nikamwambia aende.


Alipomwita nilimuuliza unanifahamu mimi akasema nahisi nilikuona seemu ila sikumbuki ni wapi. Nikamwambia kumbuka vizuri hapo hapo nikamwuliza na uyo mtoto je? Akamtazama kwa makini akasema huyu mtoto anafanana na bossi wangu theni akasema nimekutambua ni wewe ndopicha zako na mtoto zimetapakaa mle ndani. nikamuulizabosi wako yupo akasema yuko anaangalia tv.


Nikamwambia beba huyo mtoto twende hakuna kumshitua. Akaniongoza hadi ndani Da dinah, hakuwa na taarifa kama tuko pale lakini nilimkuta ameshika picha yangu niliopiga sku ya wapendanao akiitazama kwa hisia wakati huo alikuwa ametoka kunipigia sm nikamwambia niko home najiandaa kulala.


Alipata mshituko usiosemekana. Na mi nilipofika nilidhibiti sm yake vilivyo sikuona sms ambayo itanipa hofu ya kusalitiwa. & now i have find out the true. Kwa mda wa siku mbili nilikuwa pale kweli da dinna Mr wangu yuko bussy mpaka nilimwonea huruma. Napenda kuwashauri wanawake wenzangu tusiwalaumu wala kuwalaumu wapenzi wetu.

Tuwapende tuwe karibu nao, Na watuambiapo jambo lolote tusiwablame inatakiwa uvumilivu na maelewano.Thanks all for your information. And many thankis to You Dinah.
Samahani nimeandika marefu kama gazeti.

Regards.
Mama Johnson.
Mza.

Friday, 20 February 2009

Viagra!


Mambo vipi wewe!

Kwenye Topic ya 12 Feb 2009.
Naona watu wanashauriana vitu ambavyo inaonyesha kuwa vinafanywa na wengi kwenye mahisano ya kimapenzi bilakujua kwanini hasa Viagra ipo na inafanya kazi gani? Kama ilivyo kwenye matumizi ya karanga na korosho....wengi wanadhani inaongeza nyege lakini ktk hali halisi "nuts" zinaongeza uzalishaji mzuri na wenye afya wa Shahawa/Manii na sio nyege.Kuna msemaji mmoja katoa actually "somo" (hehehehe nimecheka mpaka nimeanguka alafu ndio nikaanza kusikitika) kuwa unaisaga Viagra kisha unaichanganya na Juice na kumpa mumeo....sasa huoni kuwa huko ni kumbaka? Unamlisha dawa ya kusimamisha uume bila yeye kuandaa mwili na akili yake tayari kwa tendo hilo takatifu?Come on wanadada, kama yeye akifanya hivyo wakati wewe huna hamu ya ngono kwa vile uwezo wako mdogo utajisikiaje? Hakika utaenda kumshitaki kuwa kakubaka kwa wakuu wa mtaa.Itambulike kuwa Viagra haimpi mwanaume nyege bali inasababisha mapigo ya moyo kwenda kasi na hivyo kusukuma damu kwenye mishipa ya uume wake na kusababisha uume kusimama. Nyege inategemea zaidi akili/Saikolojia na kuachiwa kwa "homono" (wacha nitafute jina lake kwa kiswahili hapa) na sio mapigo ya moyo na msukumo wa damu.Mwanaume kama anauwezo mdogo wa kungonoka hata ufanye nini hawezi kuwa na nyege unless zije zenywe pale mwili wake unapokuwa tayari....japo kuwa kuna dawa za kumfaya anyegeke lakini haiwi kama vile kunyegeka kiasilia.Vilevile kutokuwa au kupungukiwa na nguvu za kiume kwamba mwanaume hawezi kusimamisha lakini anakuwa na nyege kama kawaida ila Mboo haidisi (hawa ndio wanahitaji Viagra) ni tofauti na mwanaume mwenye uwezo mdogo wa kungonoka a.k.a low sex drive.

Ukweli sasa.
Inasemekana kuwa Viagra ilibuniwa au tengenezwa maalumu kabisa kama dawa ya kutibu Ugonjwa wa moyo, sasa kusimamisha uume ilikuwa moja ya "side effect" ya dawa hiyo (kabla hawajaibadilisha jina na matumizi yake).


Sasa mwanaume yeyote mwenye tatizo la kusimamisha a.k.a ED iwe haisimami kabisa ua ule ugumu wake unakuw ahautoshi kuingia ukeni ndio huwa wanashauri wa Daktari husika kutumia "buluu" na hiyo hufanyika mara baada ya kuangaliwa afya yake nahivyo kupimiwa kiwango gani atumie.


Wanaume walio wahi kuzitumia au wale wanaozitumia wanaweza kueleza kwa kirefu zaidi.

Jaribu kufahamu mwili wa mumeo wako na namna gani unafanya kazi badala ya kuchanganya mambo kwa mfano wengi wanafikiri kusimamisha ndio nyege na nyege ndio kusimamisha.


Ili mwanaume asimamishe ofcoz anahitaji kusisimuliwa ili kunyegeka, mnyegeko ukitokea ndio anasimamisha....lakini kama anatatizo ED basi atasisimka (nyege kibao) lakini misuli ya uume itagoma kusimama na hapo ndio atahitaji msaada wa Daktari na hatimae kupatiwa kidonge buluu.


Tafadhali ongezea kutokana na uzoefu wako.

Ty.

Thursday, 19 February 2009

M3 anaomba tufichue yale yanayoweza kuharibu ndoa!

"Moja ya dhumuni la kuanzisha blog hii (dada Dinah,kama nimekosea unisahihishe), ni kujaribu kufichua yale yanaharibu mahusiano na kuboresha yale yalipo, kwa kuyaweka wazi kwa kila mmoja, ili kama wewe hukuwa nalo utajifunza au utaliacha ili uende sambamba na mwenzako.


Kwahili la kutokujaliana, ni vyema sisi kama wanaume au wewe kama mwanamke ukasema nini hasa kinachokufanya usifanye hivi au ukafanya vile, kwani kusema ukweli huo, ndiko kunakoweza kutusaidia.


Mimi ningependa kufichua yale ambayo wanaume tunayo, na kawanini tunafanya hivyo. Kwa upande huo wa kutokuwasiliana, ipo dhana tumejijengea kuwa si vyema kumzoesha mkeo kila kitu, kwamba mimi nafanya hivi au nataka kufanya vile kwa mfano kukupigia simu mara kwa mara inaleta mazoea ambayo ukikosa kupigiwa utaleta dhana potofu, hii ni moja ya sababu.


Lakini ipo sababu kubwa ambayo hata nyie wanawake mnayo, ni ile ya kujisahau. Kwamba sinimeshaoa, sinimesha-olewa, kuna sababu gani ya kuhangaika mara simu mara nifanye hiki na kadhalika.


Wengi wanasema eti mkishaoana, mnazoeana kama dada na kaka. Wewe dada ni dada na mke au mume ni hivyo hivyo, havina mbadala. Jiulize kama ni dada yako unaweza ukaoga nae? Kwahiyo kila siku inapokwenda hakikisha unajiweka kama vile `unatafuta’.


Kila siku inapokwenda hakikisha hufanyi makosa ya kumfanya mwenzako ahamanike ni `vipita njia’ kwani jamani kila kukicha vinazaliwa vyombo…. Kwahiyo hasa kwa hawa wanaosafiri hukutana ni vishawishi hivyo ambavyo vinawaweka njia panda.


Jingine la muhimi ni mawasiliano. Hili ni tatizo, sugu,sisemi mawasiliano ya simu,nasema mawasiliana kama mke na mume. Sisi wanaume mara nyingi hatupendi kujadilia, hasa katika maswala ya ndani, ya kimahusiano, tunataka kufanya.


Mnapokuwa ndani mjaribi kujadili, kuelezena na kupeana ushauri kuhusu hili au lile. Nashangaa wengine wanasema maswala ya mapenzi hayahitajiki majadiliano mkiwa mumeshaoana,kwanii mnatafute nini zaidi! Inabidi tujadili, tuelekezaneni ka kuwekana sawa.

Unaacha bwana au bibi keshasafiri unaanza kulalamika huku nyuma. Pale mkiwa uso kwa uso ndipo pa kujadili. Mhh, yapo mengi ngoja niwaachie wenzangu, wenye nia ya kufichua uzaifu huu, ili tujenge mahusiano mema.
emu-three"

Nafichua, machache ya wanawake ambayo yanaweza kuharibu ndoa;
(1)-Kufunga ndoa bila kuwa tayari (kufuata mkumbo, kuamini ni baraka, kufuata pesa).

(2)-Wanawake tukipenda na kupendwa huwa na tabia ya kujisahau pale tunapojuwa tumeolewa, u dont put an effort anymore kwa kuamini kuwa amekuoa so hawezi kwenda popote.

(3)-Kutokujua tofauti kati ya Mpenzi na uhusiano......wengi hutegemea "hisia" kuboresha penzi hawajui kuwa unatakiwa kufanya kazi ya ziada kuwa na uhusiano udumu.

(4)-Kukimbilia kuzaa (kwa imani kuwa ni kukoleza mapenzi) bila kuwa tayari/kujua utajigawa vipi kati ya mapenzi, uhusiano na majukumu kama mama.

(5)-Kumtegemea mwanaume kwa kila kitu yaani kumfanya "ajira".

(6)-Kujiachia kwa maana ya kutojipenda tena na una"tilia" vivazi vizuri ikiwa tu unakwenda kwenye sherehe au unakoga na kujifukiza manukato siku ukiwa unataka tendo.

(7)-Kuchukulia Ngono kama wajibu.......uvivu wa kujifunza kupenda tendo hilo takatifu.

(8)-Kuamini ktk msaidizi (houseBoy/Girl)......kumpikia mwanaume ni alama ya upendo (kule nitokako mimi) hivyo Vigoli huwa hatupikii wanaume ovyo-ovyo unless njemba kama imekuja kuchumbia.

(9)-Heshima ya uoga....huna mpango wa kumheshimu mume wako lakini unamuogopa au unaogopa kuachwa.

(10)-Kutokuwa na tabia ya kum-challenge mumeo, kila asemacho wewe ni "ndio bwana"...challenge him, onyesha kuwa u r smart woman!

(11)-Kutokumpa mume wako muda wa kutosha....unakuwa busy na marafiki/shoga au familia yako kila wiki.

(12)-Kujihusisha sana kwenye familia yake hasa kama kuna migogoro kati ya ndugu na ndugu. Unatakiwa kuwa upande wa mume wako lakini jua ur limit, kamwe usiponde ndugu zake hata kama yeye anawaponda.

(13)-Ile kaingia tu unamuwahi na nini kilitokea b4 hata hajanywa chai/kaa chini nakutuliza akili...hujui siku yake ilivyokuwa mama, ongea nae lugha ya mapenzi kumlainisha, mkande ili awe relax kabla hujamshitaki mwanao kuwa aligoma kwenda shule au kafeli jaribio la hisabati.

Yapo mengi ila kwa sasa wacha nitunze ndoa yangu.
Midas.

Wednesday, 18 February 2009

Tatizo ni mimi au yeye? Kufika kunako ni mbinde-Ushauri!

"Habari.
Kwanza napenda kutoa hongera kwa blog hii kwani kwa kiasi fulani naona kuwa inawasaidia watu kujifunza mambo mengi kuhusu maisha ya mapenzi na mambo kama hayo.

Sasa basi nianze kwa suala langu la msingi ambalo nalileta hapa kwa ajili ya kuomba msaada wa ushauri. Mimi ni kijana wa miaka takribani 30 hivi na niko katika ndoa na mke wangu mwenye miaka 27 kwa mwaka wa pili sasa, ni miezi michache ilopita tumejaaliwa mtoto.


Sie hua na tabia ya kukutana kimwili kadri mmoja wetu anavyojiskia. Yaani namaanisha hatuna ratiba ya kua ni mara ngapi kwa wiki lazima tukitane, hivyo basi yaweza kutokea tukakutana mara 3 kwa wiki ama pia ipite mwezi hatujakutana.


Kitu ambacho nimekihisi pengine ni cha kinyume kwa mke wangu ni kua wakati tukitiana ni ngumu sana kumfikisha kileleni yeye kwa njia ya kawaida. Hapa namaanisha naweza kwenda mimi yeye akawa bado. Pia nikipumzika na kwenda mara ya pili naweza fika yeye akawa bado.


Mimi nimejaaliwa kuchelewa kufika kiasi kua kama sina usongo sana naweza tumia dakika 10 kufika kwa bao la kwanza, la pili linachukua muda zaidi hinyo nnaamini namsugua vilivyo mke wangu na kwa kawaida pia hua namtaarisha /tunataarishana kwa muda kabla hatujaanza majamboz.


Nimejaribu hata kua namchezea kisimi chake kabla mimi sijapanda ili arizike lakini hua pia inamchukua muda mrefu sana kwa yeye kupiz kwa kuchezewa tu. Huwezi amani mpaka kidole/mkono unachoka kwa shuhuli hiyo. Kwa muda sasa niliamua kufanya ivyo ili nihakikishe yeye kapizi na mimi ndo napanda napiga yangu.


Hili linanisumbua kidogo as sielewi kua atakuwa anamatatizo au ni ipi suluhu ya swala hili. Naomba ushauri wa kina ili tuweze kufurahia ndoa yetu."

Jawabu:Asante kwa Mail yako. Hebu soma Makala hii kwa kubofya hapa ili upate mwanga kabla sijakupa maelezo ambayo yatasaidia ili kufanikisha matokea mazuri ya tendo hili tamu kuliko yote Duniani alafu takatifu.


Kuchelewa kwa dk10 haitoshi kumfanya mwanamke afike kileleni hata kilele via Kisimi inaweza kuchukua dk15 kwa baadhi ya wanawake, ningekubali kuwa umajaaliwa kuchelewa kama ungekuwa unakwenda kwa angalu dk45 baada ya lile bao la kwanza ambalo mara nyingi huwa linawahi sana.


Pamoja na kuwa mwanamke anamchango mkubwa zaidi ili kufika kileleni wewe mwanaume unapaswa kujua mbinu nyingine za kumfikisha Mf-kumchezea kisimi mpaka anafika lafu ndio na wewe unaingia na kumaliza ng'we yako vilevile ujifunze mbinu za kujizuia ili yeye mkeo afikie kule kunako utamu zaidi ya mara moja kwa mpigo.


Ili kufika kileleni baada ya kujifungua mwanamke anahitaji ushirikiano wako hasa linapokuja suala la kukabiliana na majukumu kama mzazi/mama(anahitaji muda mwingi wa kupumzika) pamoja na kusema hivyo pia anapaswa kujifunza upya namna ya kufurahia na kulipenda tendo hilo, kuwa tayari kiakili na kimwili na kujituma wakati mchezo unaendelea.

Natumai wachangiaji na maelezo yangu yatakuwa yamekusaidia kwa kiasi fulani.
Kila la kheri.

Tuesday, 17 February 2009

Hivi ni kweli kuwa akitereza basi hatoacha?-Mchango

"Dinah na wadau wengine hii imekaaje. Naona kama ina ukweli mkubwa sana kwani mimi mme wangu amewahi kucheat na nikamkamata lakini alitubu. Sasa naona tena dalili. Na katika kusomasome nimekutana na hii. Dinah na Wadau mna maoni gani katika habari ifuatayo.


If a guy cheats on you, He'll do it again. If you stay, he'll cheat even more No woman can make aguy stop cheating, not even his mother. Cheaters are like a small kid, oncethey tasted sweets, no matter what you do or say, they'll find a way to gethold of them. Stop looking for water in a desert, because you'll find none.


Advice: Leave the looser and find a real man who'll give you his all OR staywith the cheat and be a subscriber of Kleenex Tissues, cos you will beweeping till you get to your grave. He might even find a girl to replaceyou, cos he doesn't really need you, or he'll keep you to cook for him and do his laundry, while he gets his groove on.

YAANI, HAPA NAHISI KAMA MIMI VILE!"

Jawabu:Sehemu pekee yenye ukweli ni "no woman can make a guy stop cheating" hata kwa upande wa pili hakuna mwanaume anaeweza kumfanya mwanamke aache kutereza. Whoever wrote this ni feminist na anahasira, machungu na chuki dhidi ya wanaume kitu ambacho wanaume pia wanaandika kuhusu wanawake.


Watu wa namna hii huwa rahisi sana ku-turn kuwa players 4 life au watu wa ngono bila uhusiano hawajiiti machangudoa lakini wako radhi kufanya ngono bila kuhusisha hisia, labda kw avile hawalipwi ndio maana hawataki kuitwa CDs.

Hii ni kwa vile wanakuwa wamekata tamaa kama sio kuogopa kuumizwa tena na jinsia hiyo kwani wanachukulia kila mwanamke/mwanaume anatabia hiyo hivyo ni bora kuwa na mtu kama yeye.

Kama mwanaume hajakuoa au hamko kwenye uhusianoa mbao ni commited hata mimi nitakushauri uanze mbele ikiwa mpenzi wako atatereza, lakini hadidhi iko tofauti kwa wachumba, mume/mke kwani mpaka mtu anatereza lazima kuna walakini kwenye uhusiano hivyo badala ya kumuacha mwenza wako ni bora kutafuta ukweli wa nini hasa kimepungua/kosekana kwenye uhusiano wenu mpaka achomoke??!!


Kufanya mikakati kw akushirikiana na yeye kukubali kosa na wewe kuwa tayari kumsamehe na kusahau (japo inachukua muda mrefu), mwenza wako kugundua nini alikuwa anakunyima na yeye kurekebisha ni wazi kuwa itafanya uhusiano wenu kuwa mzuri, Imara na wenye afya kuliko hapo awali.


Sikutumi utereze ili kuboresha uhusiano, la hasha!
Ninachojaribu kusema ahapa ni kuwa mwenza wako akifanya kosa la kusaliti ndoa/penzi haina maana kuwa ndio basi tena.....siku zote kuna njia ya kufikia muafaka.


Kama wapenzi mkachukua tahadhali mapema, mkajuana vema, mkaafikiana kushurikiana kwenye kila kona na mkawa wazi na kufanyia kazi uhusiano wenu badala ya kuachia "tunapendana" peke yake.


Unajua uhusiano ni kama ajira yenu ya pili, usipokuwa na bidii au kutokuwa makini ni wazi kuwa kibarua kitaota majani na mmoja wenu kutoka kwenye uhusiano 4 good au kutereza. Hivyo basi mimi sikubalini kabisa kuwa mwanaume au hata mwanamke akitereza basi ndio anakuwa wa kutereza unless kama ni hulka yake.


Vinginevyo ikitokea hiyo na mnapendana basi pigania penzi lenu na kulifanya liwe lenye afya na bora zaidi ya mwanzo.....kuweka "rules" kwenye uhusiano pale mmoja anapokuwa mtivu wa nidhamu ni muhimu.......wakati mwingine watu wanakuwa kama watoto, wanahitaji muongozo kutoka kwa mama.

Usiamini ktk ufeminist tafadhali, ni hatari kwa afya yako ya kimapenzi na Ngono.
Kila lililojema.

Monday, 16 February 2009

Wakikutana nami tu basi ni kwaheri!-Kulikoni?

"Hello Dinah.
Mimi ni mwanamke in my mid 30s na nipo single wala sijawahi kuolewa na sina mpango huo nina tatizo naomba nisaidiwe. Nikiongea na mwanaume thru phone wanakuwa na hamu sana ya kuniona hawawezi hata kutulia. Wanakuwa wananisumbua kwa simu nyingi wakitaka miadi na mimi. Hii hutokea kwa watu wasionijua lakini hata wachache ambao tumewahi kukutana tukiwa watoto halafu tukapotezana.


Tatizo lipo hivi; baada ya jitihada zao kubwa za kutaka tukutane inapokuwa tumekutana sijui kunatokea nini maana hupotea na wala hawanipigii tena na namna mimi nipo huwa sihangaiki tena kuwatafuta. Huwa najisikia vibaya sana naona labda sura yangu huwa ina shida au wakiniona sijajua wanafikiria nini. Suala hili linaniumiza roho sana.


Sio kwamba ninawataka la hasha ila sijui ni nini kinafanya ile kasi wanayokuja nayo iishe mara wanaponiona. Bahati mbaya nimekutana na wanaume kama wa nne hivi ambapo watatu nilikutana nao usiku. Ifahamike kwamba wengi wa hao wanaume kwa sababu ya hamu yao ya kukutana nao huingilia ratiba zangu kwa hiyo nakutana nao bila kupanga.


Hivi nitakuwa na matatizo gani? Ninaye mpenzi wangu na ananipenda dearly na kuna wanaume wengine ambao tunaonana mara nyingi tu na wananifukuzia kama nini. Hivi Dinah tatizo linaweza kuwa nini mungu wangu.


Unajua imefika mahali sitaki tena kukutana na watu wanaopata hamu ya kukutana na mimi baada ya mawasiliano ya simu. Rafiki zangu wengi wameniambia ninaongea vizuri katika simu sasa hata hao watu si waendelee kusiliza sauti yangu kwenye simu hata kama hawataki kuniona tena.


Mimi tayari nina matatizo hayo msiniongezee matatizo kwa comment zenu ndugu zangu msije mkanifanya nijitundike kitanzi bure kwani mimi ni mhehe. Nikisema swela tegemeeni kupokea maiti yangu. Please comfort me ninaonekana kama nyani nini.Yaani kinachonishangaza ni hiyo kasi yao ya kutaka kuniona na wakiniona kunikacha.
Asante"

Jawabu:Hey Mnyalu, Nimependa mkwara wako hehehehe! Sasa wewe unampenzi inakuwaje unawasiliana na wanaume wengina na hata kuonana nao? Unatoa wapi huo muda mdada ei?!!

Uenikumbusha kisa kimoja kilimpata rafiki yangu Chuoni, kwa mujibu wa maelezo yake ni kuwa yeye alijiingiza kwenye "uwanja" wa kutafuta wapenzi kwa njia ya net kwa maana ya kwenda kujiandikisha kwenye Dating/find love sites kwa ajili ya kupata mpenzi.

Alijenga uhusiano na kijana mmoja bila kuonana nae kwa muda mrefu tu mpaka wakaanza kuitana mpenzi n.k na siku moja wakaamua kukutana ana kwa ana ili kuzungumza na kufahamiana ktk hali halisi.


Yule Binti (rafiki yangu) alijiandaa na kwenda huko walikoaagana kukutana na alipofika jamaa hakuwepo so ikabidi binti amsubiri, jamaa akapiga simu kuwa yuko njiani anakenda mahali pale. Baada ya muda, jamaa akafika mahali pale wakaongea kidogo mara jamaa akadai kuwa anakiu, kwa bahati mbaya hakukuwa na duka karibu la vinywaji so ikabidi binti aingie garini na jamaa wakaenda mpaka dukani.Jamaa akampa yule binti 50p (nusu£1) akamuomba aende kumchukulia maji dukani........binti aliporudi gari na ile njemba haikuwepo. Ikabidi Binti arudi nyumbani. Kesho yake alipokuja Chuoni ndio akaanza kunisimulia akiwa analia na kulalamika kuwa kwanini Njemba ile imemkimbia, kama haikutaka kuwa nae si ingemwambia tu moja kwa moja, inamana yeye ni mbaya na anatisha bla-bla-blaaa!


Mimi nikamwambia kuwa amshukuru Mungu kuwa huyo Njemba kajiondokea bila kwaheri, huenda ni muuaji au mbakaji kwani humjui kihalisi bali kimtandao, nikamwambia huenda mlivyoongea aliona hauko "interested" na ngono, au ni mzuri sana na hawezi kuwa na wewe kwani anahofia kuibiwa siku moja nakadhalika.


Sasa hata wewe nitakuambia hivyo-hivyo kuwa inawezekana kabisa unapoongea nao wanahisi kuwa wataweza kukushawishi ufanye kile ambacho wanakitaka ambacho ni ngono kwa wanaume karibu wote....mwanaume akionyesha "interest" na wewe kinachopita akilini mwake ni Ngono kwanza alafu mengine yanafuatia.


Kwahiyo kama wewe unapokutana nao na kuzungumza mnayozungumza huenda labda wakakutongoza n.k lakini wewe ukaweka vigingi na kuonyesha msimamo wako kama mwanamke mwenye mpenzi ambae hunampango wa kuolewa n.k inawa-put off kwa vile wanaume wengi hawapendi ku-share mwanake, wanaume wengi waliotulia wanapenda kuwa na mwanamke wao peke yao (losers ndio wana-share hihihihi).


Ikiwa nia yao ilikuwa ni kurafikiana ili siku moja mngonoke na wewe ukawaonyesha no interest ni wazi kuwa hawatakuwa na mpango na wewe kwa vile hakuna nafasi ya wao kupata wanachokitaka au walichodhania kuwa watakipata kutoka kwako.


Wao kukata mawasiliano na wewe haina maana kuwa wewe ni waajabu, unatisha au vyovyote unavyojihisi ambavyo ni hasi a.k.a "negative" bali ni kutotaka kukupotezea wewe na kujipotezea wao muda, hasa ukizingatia hawataki urafiki wa kawaida bali mambo fulani.


Nini cha kufanya-Acha kabisa kuwasiliana na watu ambao huwajui na hawakujui na kamwe suipange mihadi ya kukutana na mwanaume ukijua wazi kuwa unampenzi wako. Ingekuwa mpenzi wako anawasiliana na wanawake simuni na hatime kukutana nao ana kwa ana ungejisikiaje?


Sasa unaweza kudhani ni sawa tu kwa vile yeye mpenzi wako hajui nini unakifanya akiwa hayupo karibu, lakini ni wazi kuwa hatofurahia tabia hiyo na inaweza kuua kabisa hali ya kukuamini au yeye kujiamini ndani ya uhusiano wenu na kusababisha matatizo mengine ambayo yanaweza kuharibu uhusiano wenu mzuri.

Natumai wachangiaji na mimi hatutosababisha ujitundike.....kila la kheri.

Friday, 13 February 2009

Nahisi mume wangu anajisahau-Ushauri!

"Dear Dinah, Habari ya kwako? Pole na shughuli za hapa na pale.
Mi ni mdada ambae nimeolewa na nimebahatika kupata mtoto na ni mwajiriwa. Katika kipindi chote cha maisha yetu ya ndoa tulichelewa kupata mtoto lakini mwenzangu hakujali hilo alinisihi niache mawazo na zaidi tumuombe mungu maana hashindwi na jambo.


Wakati huo mme wangu alikuwa mwajiriwa katika kampuni moja hapa Mza. Mara kwa mara alikuwa akisafiri lakini tulikuwa tuko pamoja mara nyingi. Na mapenzi yetu yalizidi kushamiri siku hadi siku. Nilipopata ujauzito tulifurahi sana tatizo nilitokea kumchukia sana mme wangu, hakujari hilo aliona ni hali ya mimba tu.


Tatizo mwenzangu kwa sasa amehama kimakazi amepata ajira nyingine huko Dar na mi niko Mza yapata sasa miezi 6. Huwa anakuja mza endapo ikitokea. Tatizo ni kwamba hadumishi mawasiliano baina yetu. Mara zote mi ndo huwa nampigia cm yeye hanipigii na ikitokea akapiga zaidi anaulizia habari za mtoto tu, na nikimtumia sms hajibu.


Mi binafsi huwa napenda sana kutumiana sms za malavidavi as u know yuko far away from me so we get connected through mobile. Lakini ye haonyeshi kujali. Jana usiku nilimmisi sana nikaona nimpigie angalau tutakiane uciku mwema lakini nilipompigia alipokea vizuri nikamuuliza uko wapi maana kulikuwa na kelele kama za redio na nafikiri alikuwa akisikiliza taarifa ya habari akanijibu kwa mkato.


Niliko we haikuhusu ongea shida yako.' Sio sii dada niliumia sana ukizingatia nampenda. Na wazo la kumsaliti sina. Nikimpigia sm nikambana sana anaishia kunisisitiza kuwa nimsamehe yuko bize sana na kazi anaandaa mazingira ya baadae tusijeteseka. Lakini dada ni kweli mtu unaweza ukawa bize kiasi cha kusahau familia yako hususan mkeo? Naomba unishauri nijue nini cha kufanya au katika maelezo hayo kuna kitu gani umeona kinaendelea hapo?
Thanks Ma love, Its Me Ma Johnson.Mza."

Jawabu:Habari ya mimi ni njema kabisa namshukuru Mungu, Shukrani za dhati kwa ushirikiano wako.

Ni rahisi kwa mwanamke yeyote kuhisi kuwa mume akiwa bize kila wakati, anakujibu kwa mkato au kutoonyesha furaha kila anapoongea na wewe acha tu kuwa hakutafuti ni wazi kuwa anamwanamke mwingine lakini ktk hali halisi sio lazima iwe hivyo hasa kama unawaelewa vema hawa viumbe.


Ukiangalia kwa undani uhusiano wako ulikuwa mzuri na ni wazi kabisa kuwa mume wako anakupenda na ndio maana alivulimia na kuendelea kuwa na wewe kipindi kile ambacho hukushika mimba na hatimae ukaipata na kumchukia yeye kama matokea ya mabadiliko ya Homono mwilini mwako.


Huyu mume inawezekana kabisa ameathrika Kisaikolojia baada ya kuchukiwa na wewe kipindi chote cha miezi tisa ya uja uzito wako lakini hakutaka na hataki kuliweka hilo wazi kama unavyowajua wanaume na UANAMUME wao a.k.a Ego.


Vilevile inategemea na wewe ulivyokuwa unalichukulia suala zima la yeye kuhamishwa kikazi, je uliomba au kuonyesha hali ya kutaka kuambatana nae na mhamie huko ilimuwe wote au uliona poa tu yeye akiwa huko na kuja kuwatembelea pale anapoweza......uliwahi kujiuliza je, asipoweza kuja kuwatembelea itakuwaje?......kama ulikataa au kuchukulia kawaida kukaa mbali nae inaweza kumsumbua akili yake.


Ninachokiona hapa ni hofu juu ya familia yake changa ambayo iko mbali, mawazo juu ya shughuli za kikazi (inategemea anafanya nini), mawazo juu ya kuhama Mkoa peke yake au aichukue familia yake, na je akifanya hivyo mtaishi wapi? Je kazini kwako watakubali kukupa uamisho na ukihama utafanya kazi wapi?


Gharama za kimaisha mahali ambapo hamjawahi kuishi (mf Dar maisha ni ghali sana kama hujawahi kuishi mahali hapo)....haya akifanya uamuzi huo na mkaahamia Dar alafu mara akapoteza kazi itakuwaje?


Unajua wanaume wanafikiria au kuchukulia mambo tofauti sana na sisi wanawake, kuna mambo mengi ambayo yanamsumbua kichwani kiasi kwamba anasahau mapenzi ya kihisia na kiromantiki na badala yake anajali zaidi uhai na usalama wenu wewe na mtoto hali inayoweza kupelekea yeye kuwa "dry" anapoongea na wewe na kuuliza unataka nini na je mtoto anaendeleaje......uhai na usalama wenu ndio muhimu na hayo nimapenzi.


Sasa kwa vile yuko mbali huenda alihitaji zaidi kupewa moyo na wewe kuonyesha kuwa uko tayari kuhamia huko kama vipi. Yeye kukuenga kimaongezi hasa unapoanzisha mambo ya kulomantika wakati yeye akilini anawaza maisha yenu ya baade kama "baba" kwa kweli itakuwa ni usumbufu.....hiyo haina maana kuwa hakupendi la hasha! Anakupenda sana lakini wakati huohuo anajua bila ku-provide vitu muhimu kwa familia yake ni wazi kuwa atajihisi kuwa hana umuhimu kama mwanaume.


Pamoja nakusema yote niliyoyasema haina maana kuwa hawezi kuwa na "kimwana" mpya huko aliko, inawezekana kabisa na vitendo vyake vinaweza kumfanya mwanamke yeyote kuhisi kuwa Jamaa ana mtu huko.


Mwanadamu yeyote kamili (mume/mke) anaweza kushawishika kufanya maovu au kusaliti ndoa yake kutokana na sababu mbalimbali lakini wengi huwa wanajizuia kutokana na mapenzi yao kwa wenza wao kwa vile wasingependa wapenzi wako kufanya kile ambacho wao wanaenda/taka kukifanya.


Nini chakufanya-Acha kuwa "romantic" kila wakati unapowasiliana nae na badala yake jaribu kumuonyesha kuwa unamjali, unaelewa na unajali yanayosumbua akili yake kwa sasa (kwa kufuatilia niliyogusia hapo juu) lakini wakilisha kwa namna yako kwa vile wewe ndio unamjua namna ya kuzungumza na mumeo.


Muonyeshe mume wako (kwa kuzungumza kwa upendo na kwa mapenzi) kuwa ungependa kujiunga nae huko aliko (msikilize anasemaje), mpe mawazo/maoni yako juu ya nini kifanyike ili kurahisisha hilo, mpe mipango ya kimaisha ikiwa atapoteza ajira au ikiwa utajiunga nae huko Dar....onyesha kuwa wewe ni mwanamke mpenda maendeleo na unambinu na mipango kibao ya kusababisha mabadiliko kwenye familia yenu (hata kama hapo mwanzo huku wa hivyo).....hii itafungua njia akilini mwake na kumpunguzia mawazo.


Alafu kila mnapokaribia mwisho wa maongezi ndio "romantika" sasa hapo ili akipitiwa na usingizi ubaki akilini mwake na ninakuhakikishia kuwa mambo yatabadilika kitu kitakacho saidia sana kuboresha uhusiano wenu wa mbali kwa sasa.


Ikiwa anaendelea kuwa "dry" nakuonyesha kutokukujali kama ulivyosema baada ya kujitahidi na kufanya nilivyo kueleza na mengine buni mwenyewe na hakikisha unayafanyia kazi (sio waishia kuongea kwenye simu tu) basi fanya kama alivyosema Mchangiaji mmoja kuwa funga safari bila kumtaarifu na Pay a sapuraizi viziti......

Kila la kheri!

Thursday, 12 February 2009

Miaka 10 sijaridhika kingono-Nisaidieni!

"Dada Dinah na Wadau wengine naombeni msaada jamani.
Mimi nina mme wangu na tunapendana lakini shida iko kwenye sijui niite kuridhishana!? Mtanisaidia baada ya kueleza tatizo.


Ndoa yetu in miaka 10 sasa. Tatizo langu lina historia ndefu lakini naomba mawazo yenu ili tuboreshe au inisaidie. Maana niko njia panda ya kucheat japo sijawahi tangu nikiwa msichana na sasa nina miaka 30+.


Mimi nimejaaliwa kuwa na nyege za kutosha tu na hivyo mme wangu huniona nina tatizo. Sijui kwa kuwa sikufanya wakati nikiwa msichana!. Mpaka nimeanza kujuta kwa nini sikufanya hivyo labda ningekuwa sina shida hii, maana sasa naona nataka kurudia matapishi.


ILA NINA MSIMAMO SANA NA HILI HATA KAZINI KWANGU WANANIJUA. Sasa tatizo langu, natamani tufanye kwa wiki hata mara 2 ila mme wangu anataka mara moja kila baaada ya wiki 2.


Yeye ni mtu wa mazoezi hata mimi kanifundisha. Lakini shida ni kwamba hawezi kabisa kudindisha hata nikimchezea vipi kama siku hiyo hataki. Ninaumia sana wakati mwingine, maana ninajieleza kuwa ningependa tu anifanyie hata romance.


Anasema nimechoka na sina nguvu kabisa Darl mpenzi. Nimejitahidi kumlisha vizuri vyakula vifaavyo, kama vile kumnunulia korosho, kumkaangia karanga, na vinginevyo. Lakini akijitutumua mara moja basi.


Hata wakati mwingi bao moja tu anakuwa hoi!! Dinah na wasomaji wengine nahitaji msaada wenu mapema, maana nimechanganyikiwa mwenzenu. Kumbuka: Mimi ni mfanyakazi na siyo mama wa nyumbani hivyo najitahidi hata vi-surprise ili kumweka sawa lakini akifika kitandani analalamika kweli. Nimechoka, najisikia nguvu sina. Nimejitahidi hata kumjengea imani kwamba anaweza kwa kumsifia na kumshangilia anapoweza lakini hali ndio hiyo.
Nini jamani kinamsimu Mume wangu????
Mwanablog."

Jawabu:Asante Mwanablog kwa ushirikiano wako vilevile kwa nyongeza ya maelezo ambayo baadhi ya wasomaji waliomba uwaeleze ili wajue nini cha kukushauri.

Kuna sababu nyingii ambazo zinaweza kumfanya mume kushindwa kufanya mapenzi na mkewe na moja ni usafi, kutovutiwa, masumbuko ya akili yanayosababishwa na shughuli na ugumu wa kimaisha(stress),matatizo ya kiafya, kuwa na -affair/cheating (japokuwa kwa baadhi ngono huongezeka kwa wake zao ikiwa wanapata nje)n.k.


Napenda utambue kuwa Karanga na Korosho haziongezi nyege bali zinaongeza uwingi wa Shahawa zenye ubora, safi na zenye afya hasa kama wewe ni mpenzi wa kucheza nazo na vilevile kama unataka ushike mimba haraka.


Mumeo hana tatizo la kushindwa kusimamisha tatizo ambalo kwa wanawake linajulikana kama kukosa/kuishiwa nyege ambalo nimelielezea siku chache zilizopita bali anauwezo mdogo wa kungonoka(low sex drive) ukilinganisha na uwezo wako(high sex drive).


Kama ulivyosema tatizo hili unalokabiliana nalo lina historia ndefu, inaelekea ni hali ambayo mume wako alikuwa nayo tangu zamani ama kabla hamjafunga ndoa. Huenda kabla wakati yupo kwenye ile "fooolis age" , huenda hamkuwa pamoja then alikuwa anakwenda hata mara tano kwa siku lakini baada ya kukua na hatimae kufunga ndoa hali ikabadilika.


Ninachokiona hapa (kutokana na maelezo yako) ni kuwa mumeo hajui anauwezo mdogo wa kungonoka na vilevile hajui kuwa hata wanawake huwa tunaumbwa na uwezo mkubwa wa kungonoka na unaridhika ikiwa angalau unapata mara 3 kwa siku....kila siku na sio mara moja kila baada ya siku saba(unless kama yuko mbali utaweza kuvumilia).


Natambua unavyojisikia kwa kutokupata ngono ya kutosha kutoka kwa mume wako kutokana na matakwa ya mwili wako lakini nasikitika kusema hakuna kitu kitakachofanyika ili mume wako awe "compartible" na wewe kwenye "sekta" ya Ngono kwani hivyo ndivyo alivyoumbwa.


Nini cha kufanya-Unatakiwa wewe kuliweka wazi hili kwa mpenzi wako na mlizungumzie, kamamumeo ni muelevu atatafuta mbinu nyingine za kukuridhisha kama vile kucheza na mwili wako kw amuda mrefu na kutumia zaidi ulimi na vidole ikiwa yeye hajisikii kukuingilia (hawezi kusimamisha)....kisaikolojia atakuwa anafurahia kwa vile wewe mkewe anaekupenda unafurahia anachokufanyia na unaridhika.


Kama wewe mwenyewe unashindwa kumuambia mume moja kwa moja kwa kuhofia kumuumiza hisia zake (anaweza kutafasiri unamwambia hawezi mambo na hilo linaweza kumuuma sana) basi unaweza kutumia Wataalamu, Mfano maeleo ya wewe kuwa na "high sex drive" yakitoka kwa Daktari na yeye kuwashauri mfanye mambo mengine zaidi ya kutumia viungo vya siri(uke na uume) itasaidia kwani haitokuwa inatoka kwako...si unajua baadhi ya wanaume wetu wa kiafrika??!!.


Kitu kingine unachopaswa kufanya ni kujisaidia mwenyewe pale unapozidiwa, kwa mfano anaporudi na anadai kachoka jaribu kupata "romance" kutoka kwake na zungumza nae kwa mapenzi na hapo unaweza kutumia vidole vyake au vyakwako kujifikisha kunako utamu. Akigundua kuwa hata vidole vyake vinakutosha basi anaweza kuwa akifanya hivyo kila mara unapohitaji na yeye hajisikii au hana nyege/hasimamishi.

Mshukuru Mungu amekuumba hivyo ulivyo kwani wanawake wengine hata nyege hawajui ilivyo, Kila la kheri.

Wednesday, 11 February 2009

Miaka 16 ya ndoa lakini twaoneana aibu-Help!

"Halo dinah mimi ni mwanamke nimeolewa mie na mume wangu tunapendana sana tupo pamoja miaka 16 tatizo ni kwamba nadhani tunaoneana aibu wakati wa kufanya mapenzi huwa tunanyamaza kimya hatuongei hata kama tunasikia raha au kama mume wangu au mimi akimuuliza mwenzie unasikia raha au tuongee chochote cha mapenzi tunacheka sana tunaona kama joke sijui kwanini? Je hii ni kawaida mume na mke kuoneana aibu naomba unisaidie."


Jawabu:Hello, ni kawaida kabisa kwa baadhi ya "pea". Sidhani kama mnaoneana aibu kwa vile tu hamuongei wakakati mnafanya mapenzi na mkiongea basi ni kicheko. Ingekuwa rahisi mimi kukubali kuwa mnaoneana aibu kama ungesema kuwa kabla hajavua nguo mnazibana macho, au akitaka kunyonya matiti wewe unajibana-bana nakufunika usoo wako au yeye kuweka mkono kwenye uume kama sio kufanya mapenzi gizani.Nafikiri ninyi wote wawili sio watu wa kuongea au kutoa sauti za utamu/raha wakati mnafanya mapenzi na mmezoea hivyo kama ulivyosema ni miaka 16 sasa tangu mmefunga ndoa na ndio maana mmoja wenu akiibuka na swali linakuwa kichekesho kwa vile sio kitu ambacho mmekuwa mkikifanya kabla ya hapo.Kama mnadhani mnapenda au wewe unapenda kumsikia mumeo akiongea au kutoa kijisauti basi mnaweza kuanza taratibu na kufanya hivyo mara kwa mara na baada ya kuda mtakuwa mmezoea.

Kila la kheri.

Tuesday, 10 February 2009

Hivi mke anaweza kupoteza "nyege" ikiwa mume yuko mbali?

"Dada Dinah, katika kuongezea hoja hii, nimekutana na watu walioathirika na mambo kama hayo. Kwasababu ya hisia, au kwasababu ya uoaga au kwasababu ambayo siijui, ndio maana inamenibidi niiongezee hoja hapa ili utusaidie kwa hili.


Likizo yangu hii nilipandisha milimani kidogo, kule nimewakuta akina mama ambao wameolewa lakini kukutana kwao na waume zao ni baada ya miezi mitatu,sita wengine hata mwaka, hawamjui mume.


Na unajua tena akina mama wa kijijini ni watu wanaoheshimu ndoa zao, hawawezi kuteleza nje, kujichua au kutenda tendo lolote ambalo litakuwa kinyume na imani zao za ndoa. Sasa tatizo imezua tatizo, kwani kuna akina mama ambao wanadai hisia zao za kimapenzi, hisia za tendo la ndoa zimekwisha kabisa.


Kuna dada mmoja ambaye tulisoma naye, aliniambia kuwa mume wake akija, anajiandaa kama kawaida, anampa maromance ya kila namna, lakini hisia hiyo haipo kabisa, yeye anasema huwa hatimaye anajidai kuwa anasikia utamu ili tu kumliwaza mume wake amalize aondoke zake.


Hii hali mimi naiona kama ni mateso, sijui kwa wenzangu, lakini hawa akina mama wanateseka, Je swali langu ni hili,ina maana wanawake wakikaa sana hamu yao hupotea kabisa? au kuna sababau zinazofanya hali hii itokee?


Na je inawezekana hali hiyo ikarejeshwa na kwa namna gani, kwasababu wengi nilioongea nao, walijaribu hata kwenda kwa wataalam (hosp na dawa za kienyeji)lakini haikusaidia kitu, wanabakia,ukimaliza funika. Tusaidiana kwa hili.

mimiemu-three"

Jawabu:Shukrani M3, ni kweli mwanamke anaweza kupoteza hamu ya kutaka kufanya mapenzi na hii inasababishwa na mambo mengi tofauti kama vile kutopenda tendo lenyewe kwa maana kwamba unalifanya kama wajibu na njia ya kuleta watoto duniani(kuzaa), uchovu wa mara kwa mara, kuugua kwa muda mrefu, kutokujua raha/utamu wa tendo na umuhimu wake (kasumba kuwa ngono ni kwa wanaume tu na ndio wao pekee wanasikia utamu), Mahangaiko ya kiakili a.k.a "stress", kukaribia au kuwa kwenye kipindi cha kikomo cha hedhi, matumizi ya madawa ili kutibu matatizo ya kiafya, n.k.


Pamoja na sababu nilizozitaja pia matatizo ya mahusiano yanaweza kuwa sababu kuu ya mwanamke kupoteza hamu ya kungonoka na mumewe, vilevile bila kusahau utendaji mbovu wa mume wakati wa kufanya mapenzi (inaweza kum-putt off mwanamke 4 good), kutokuwa na mapenzi na mume (ngumu kufanya mapenzi na mtu ambe humpendi),baada ya kujifungua mototo.


Hili ni tatizo kubwa tu miongoni mwa wanawake ambalo linajulikana pia kimatibabu (Medicaly) japokuwa matibabu yake sio lazima yake yale ya kutumia dawa(kitibabu) kama matatizo mengine ya kiafya.Kama nilivyosema awali kuwa tatizo hili linaweza kuwa limesababushwa na matukio fulani Kimwili (Diets,kuzaa,matatizo ya kiafya, umri kunenepa/konda ghafla,matumizi ya madawa yakuzuia mimba n.k.) au Kiakili (stress, Depression, Kisaikolojia n.k) na hakuna uhusiano wowote na “Ukabila” kwamba kabila fulani tu ndio hawana au wanapoteza/ishiwa hamu ya kutaka kungonoka bali ni tatizo ambalo linaweza kumpa mtu yeyote kama ilivyo kwa matatizo mengine tofauti-tofauti.


Sasa kwa vile tatizo hili linasababishwa na matatizo ya Kimwili na Kiakili, ni vema mwanamke huyu akaenda kupata msaada wa Kitaalamu na huko akaelezea kwa uwazi (well watamtaka kueleza kwa uwazi lolote atakalo ulizwa) kuhusu historia ya maisha yake tangu alipokuwa mdogo.


Vilevile uhusiano wake wa kimapenzi na mume wake ulivyoaanza, ulivyokuwa na sasa ulivyo ili “Psychologist”, ajue namna gani ya kumsaidia “Kiaikolojia” alafu ndio suala la tiba ya mwili litafuata ambapo litahusisha Daktari Bingwa wa Magonjwa na Kike, Mtaalamu wa mahusiano na Mapenzi na yule wa Ngono....kuna “Sextherapist” siku hizi.

Tafadhali kama unasumbuliwa na tatizo hili nenda haraka kumuona Daktari ili ufurahie utukufu wa uumbaji wake Mungu.

Asante M3 kwa kuleta hili suala hapa, natambua utakuwa umewakilisha wanawake wengi ambao wanaona haya kuuliza wazi au hawajui nini cha kufanya na mtaalamu gani hasa anaweza kuwasaidia.

Ukiniluzia kitu gani nahofia maishani mwangu! Nitakuambia kupoteza uwezo wa kungonoka, niko radhi nilale njaa aisee!

Siku njema.

Monday, 9 February 2009

Nilitoka na mume wake,nimesaidia wamerudiana lakini....

"Hey Dinah, natumai kuwa wewe ni mzima kabisa. Mie nina changamoto ambayo naamini kabisa wanablog wenzangu wanaweza kunisaidia kwa ushauri.

Nina BF ambaye nimekuwa naye kwa miaka mitatu sasa, kwa vigezo nilivyonavyo ni kwamba nampenda sasa kabla sijakutana naye sikuwahi kufikiri wala kutamani kuolewa. Isipokuwa niliwahi kuwa na BF ambaye tulikuwa marafiki wa kawaida kwa muda mrefu kabla ya kuamua kungonoana then we parted ways.

Mapenzi yetu yalikolea na kuwa matamu zaidi automatically tukajikuta tunakaa pamoja. Kwa kweli sikuwahi kusikia raha ya kuwepo dunia kama wakati huo. Lakini wakati sisi tukiendelea kufaidi maisha kwa kiwango hicho BF wangu alikuwa ametengana na mke wake kwa mifarakano ambayo wenyewe wanaijua na kwa muda mrefu wamekuwa wakikaa mikoa tofauti mpaka sasa.


Nadhani mke wake alikuwa akitufuatilia na kujua kuwa tupo pamoja. Asili ya kazi zangu ni safari, hivyo katika safari zangu nilikwenda Mkoa ambao mkewe anaishi. Nikakutana naye akanifanyia bifu baadae tukapata audience akaniuliza kama nipo na mumewe mie nikatoa nje kwani niliogopa mkono maana nilimwona mshari kama nini.


Kwa bahati mbaya au nzuri nikaenda tena katika Mkoa ule tukaonana akanihadithia mambo mengi kuhusu mume wake ambaye mimi ni BF wangu. Alinieleza walianzia mbali katika maisha na kwamba sasa wamefika pazuri mume wake ndio anamfanyia hivyo.


Nilimwuliza kama mumewe anatunza watoto wao 2 akasema ndiyo lakini anataka arudi kwake kwani anampenda sana. Nilimwonea huruma na ikanigusa sana kwa sababu mimi ndiye ninayesababisha hivyo.


Niliporudi home nilimketisha BF nikamwambia situation na kwamba uamuzi wangu ni kwamba kwa kuwa sina mpango wa kuolewa basi we could be together while she is with his wife and everything will be ok.


To my surprise alikataa katakata kwamba yeye hamtaki na wala hana mpango wa kumrudia. Mimi nilihisi kwamba inawezekana anahisi namtega but I was very sincere. Siku zikapita na mimi huruma ikaendelea kunishika lakini mume wa mtu nampenda.


Tukawa tunapanga mikakati mingi na mke wake ili nimsaidie mumewe arudi kwake kumbuka kwamba nimekataa katakata kwamba mimi sipo na mume wake. Kwa bahati mbaya sana alikuja mkoa tunaoishi kwa majukumu ya kifamilia (msiba).


Kama baba wa watoto iliwajibika kumfariji na nadhani hapo ndipo walipo ombana radhi na kusameheana , wakaanza upya. Mimi pia nipo pembeni nafurahia mafanikio yao. Mke wake akaendelea kunisisitiza nimsaidie ampate mwanamke aliyemkamata mume wake. Kwa mara ya kwanza niliona kuwa ananitega lakini moyoni nikasema mtego huo hauwezi kunikamata.


Naomba nikufahamishe kwamba aliponiuliza mara ya kwanza nilikataa kushirikiana na mumewe lakini nilikiri kumfahamu na kwamba huwa tunawasiliana isipokuwa ni nyanja za kazi tu. Nilipoona anazidi kusisitiza nimsaidie nikamua kufikia maamuzi magumu sana ya kumwacha mpenzi wangu huyo.


Ilikuwa ngumu sana kwani nampenda sana huyu mwanaume. Nilijaribu kumwambia kwa lugha ya taratibu na upole sana lakini hakuwa tayari kabisa. Nilimwambia nafanya hivyo kwa ajili yake na mke wake. Bado akakataa.


Nilimtoa nyumbani kwa nguvu na kwa ugomvi mkubwa sana. Ilikuwa vibaya kwa sababu tulikuwa tukiishi nyumbani kwangu. Aliona kama nimemnyanyapaa. Baadaye alifanikiwa kuondoka na kurudi kwake. Hata hivyo alikuwa anakuja nyumbani kwangu mara nyingi tu.


Baada ya muda mrefu wa mawasiliano ya mbali hivyo akaanza kukata mawasiliano kwa muda mrefu kama wiki mbili tatu hivi simsikii. Akiibuka anasema atakuja nyumbani anataka kungonoka. Tukingonoka anapotoea tena kwa muda wa mwezi or so na akirudi anataka kungonoka.


Hiyo tabia ikanichosha nikaamua kumwambia kwamba ilipofika panatosha kwa sababu naona kama ananifanyia mzaha na kutaka kuniumiza roho. Yeye akasema kwamba nilimuumiza sana kwa kumfukuza nyumbani kwangu na kwamba jeraha nililosababisha litachukua muda kupona.

Mimi nimechoshwa na hiyo tabia na kila ninapojaribu kumwacha nashindwa kwani akitokea nasahau kwamba nilitaka kumwacha tunaendekeza libeneke.

Wanawake wenzangu nisaidieni lakini pia wanaume naomba ushauri kwani tabia zenu zinafanana.
Kim from Atown"

Jawabu:Hi Kim, hapa kila kitu kiko sawia kabisa. Kwanza napenda kukupa pongezi kwa kutokuwa mbinafsi na kumsaidia mwanamke mwenzio kurudiana na mume wake. Hongera sana kwa hilo.


Ni kawaida kwa wake na waume ktk umri fulani kutojiona au kufikiria kama sio kutamani kuolewa au hata kuzaa (muda ukifika utalifikiria hilo na kutenda kama ifuatavyo), natambua uamuzi wako wa "kutojikita" kwenye ndoa ulikufanya uone kawaida kutoka na mwanaume yeyote utakae mpenda bila kujali kaoa na familia au la, nafahamu uamuzi wako ulikupa hali ya kujiamini sana kama mwanamke kitu ambacho ni kizuri...i mean kujiamini.


Lakini katika hali halisi no matter how unajiamini na kujitegemea usithubutu kutoka na mume wa mtu kwa kudhania kuwa hutoruhusu akuoe au kumuacha mkewe kwa ajili yako......kwani kwa kufanya hivyo sio tu utakuwa unaumiza mwanamke mwenzio bali pia utakuwa unaharibu mpangilio mzima wa maisha ya mtoto au watoto waliozaliwa kwenye ndoa hiyo na vilevile kufanya watu ktk jamii kutothamini ndoa(kitendo chako kinatoa ujumbe kuwa huthamini ndoa za watu).


Kutokana na sehemu ya maelezo yako inaelekea huyu bwana pamoja na matatizo mengine ya kindoa kama vile kuzozana mara kwa mara kitu kinachoweza kusababisha asipate ngono na mapenzi ya kutosha kutoka kwa mkewe.


Huyu bwana sio tu alikuwa akihitaji hifadhi kutoka kwako ili apumzike kiakili (kutokana na matatizo ya kindoa) bali na ngono pia. Unajua, linapokuja suala la ngono, akili kutulia na kuwa "comfy", hakuna maswali ya kipuuzi-puuzi, lawama za kizembe na malalamiko ya ajabu-ajabu kama sio kusingiziwa, mwanaume wanaweza kuhamia na kusahau familia yake kama unavyo "blink" vifuniko vya macho yako......bila shaka umeshuhudia hilo na unauzoefu mzuri tu.


Kuachana na mtu unaempenda ni ngumu sana na ndio maana huwa nawashauri "wateja wangu" kama kweli wanania ya kufanya hivyo lakini upande wa pili bado unasumbua kama huyo Ex bf wako ni kukata mawasiliano kwa kubadilisha nambari za simu na anuani ya makazi. Vinginevyo kila mkionana utahisi kutaka kuwa karibu nae na kufanya chochote na hivyo uhusiano wenu utakuwa ule wa on and off kwa vile wewe bado unampenda na yeye bado anapata ngono tamu na ya bure kutoka kwako.


Lakini kwa vile mkewe anamtafuta "mwizi wake" ambae ndio wewe lakini yeye hajui kuwa wewe uliyesababisha mumewe arudi nyumbani ndio "adui" ni vema kuachana kabisa na huyo bwana kwani huwezi kujua huyo Mdada anataka kumfanya nini huyo aliyemlia mumewe.....well huenda anataka tu kujua nini ulikuwa ukimfanyia mumewe ili na yeye afanye (fanya utafiti ujue anataka nini hasa kutoka kwa mwizi wake kwanza hehehehe unaweza kutolewa macho kama sio roho.......mtu chake atii).

Sasa mimi nakushauri utumie nguvu (kibali cha Polisi) ili kuzua huyo bwana asije tena kwako, kwa kufanya hivyo itasaidia wewe na yeye kuepuka "ngono chafu" na mume wa mtu. Natambua kuwa unampenda huyo mume wa mtu lakini kumbuka sio wako na kamwe hawezi kuwa wako.

Pamoja na uamuzi wako wa kuwa mwenyewe for life haina maana basi utembee na mwanaume hata kama ni mume wa mtu, jaribu kuwa mchunguzi unapotaka kuanzisha uhusiano ili usirudie kosa. Hakikisha unamfahamu mhusika kabla hujaji-comminte kwake kama mpenzi, hakikisha unakujua kwake, anaishi na nani n.k.

Wapo wanaume wengi tu ambao hawana wake kwa vile hawako tayari kuoa kuoa kwa mara ya pili baada ya Talaka au wake zao wamefariki dunia, nadhani wanaume wa namna hiyo wanakufaa zaidi na mtakuwa compartible in a way.

Kila la kheri.

Friday, 6 February 2009

Hivi huyu ananipenda au Mchunaji?-Ushauri!

"Hi Dinah mdogowangu hujambo?
Naomba msaada wa ushauri kwa wanablog wenzangu. Mie ni mama mkubwa kiasi kwa umri, Nilikua na mwanaume tuliokua dini tofauti na tumeachana kwa miaka miwili sasa.


Kuna kijana ambae nimemzidi kwa takriban miaka miwili alivyosikia kama niaeachiaka tu, hapo hapo akaniambia yeye ananitaka na dakika hiyohiyo akaniambia kama niko tayari basi anaweza kufunga ndoa hata kesho, nilibaki nashangaa kwa nini haraka?


Mie sikumpa jibu la ndio wala hapana lakini nikabaki kumuambia labda ananijoke asingeweza kunioa kwa kua mie mkubwa kwake. Hali yangu kiuchumi na hata assets sio mbaya sana, Yule kijana ana kazi , ila kiuchumi nimemzidi ana mke na watoto watatu, ni muislam ndoa ya pili inaruhusiwa.


Alikua anamwamko sana wa kwenda kuongeza shule (degree ya pili) lakini hakua na sponsor na mwajiri alimkatalia ruhusa na akataka kuacha kazi, nilimshauri asiache ambembeleze mwajiri ruhusa. Sasa nikajiuliza ana mapenzi huyu au anataka kunituma nimsomeshe?


Baada ya mawasiliano, tukapoteana kwa kipindi kirefu kidogo kwa kuwa nilikua nje ya nchi. Tumeonana mwezi wa kwanza ki-accidental, ile mada imeanza tena, Na sasa ameshapata admission IFM hana sponsor, mimi niko nje ya nchi tena ila yeye anasisitiza anataka kuowa hata kwa remote, (kwa waislamu inaruhusika).


Najaribu kumsihi kwamba sasa hivituwasiliane tu na tuchunguzane, lakini yeye ameng'ang'ania antaka jawabu la kukubaliwa tuoane au laa ajikate. Hakuwa moyoni mwangu sana lakini nilikua nahisi with time hasa ukizingatia umri wangu naweza kumpenda.


Lakini ameng'angania ananipenda na anataka jawabu. Kwa tabia kama mme ndani simjui vizuri, nilijaribu kumuuliza kijana anaefanya nae kazi akaniambia kazini hayuko-organized na yuko hash, kwa nyumbani sijuiiii.

Wana blog naomba mnisaidie mawazo huyu kijana ananipenda kweli, au anataka kunitumia? lugha zake za kusisitiza hilo suala sikuzipenda sana kwani kunasiku ashaniambia ukinikataa mimi hutapata tena mtu kama mimi au hutapata mtu atakae kupenda kama mimi, au kwanini hujiulizi ni nini nilikupendea nisipende wanawake wenzio.nk.

Naomba ushauri jamani, ananipenda huyu? nimkubali? nimemwambia tusubiri kwa kua sipo nchini hadi november tuyazungumze yeye kagoma. Ushauri jamani hili jamaa linataka nini?"

Jawabu:Mimi sijambo Dada'ngu, habari za wakti kama huu mpendwa!
Huyo isije kuwa ni mmoja kati ya wale "wezi watupu", dada unajua siku hizi hata wanaume tena walio na familia zao(wake na watoto) wanachuna wanawake ambao mambo yao ni safi kiuchumi?.

Tena siku hizi nasikia wanawake walio nje ya Bongo au wenye kujiweza ndio wanaoibiwa kweli kweli, unaweza teremka pale Yapoti (airport) ukapokelwa na vijana/babaz watanashati wakitoa "offers" tofauti tofauti za ndoa hihihihihi.....turudi kwenye somo.


Kwenye maelezo yako tangu mwanzo mpaka mwisho hakuna mahali umeelezea hisia zako juu ya huyo kijana. Huyu kijana ni kweli anataka mdhamini kwa ajili ya masomo yake ya juu na ndio maana akakurukia mara tu alipogundua kuwa wewe na mumeo/mpenzi mmeachana.


Inawezekana kabisa kutokana na "kasumba" alidhani wewe utakuwa "desparate" kuwa na mwanaume au kuolewa kama inavyoaminika kwa wanaume wengi kuwa unapokuwa mdada mkubwa na kisha kuachika basi unakuwa huna "bahati", hivyo pamoja na kuwa ni mdogo kwako aliona utamkubali tu bila mizengwe.


Kwa upande wa pili huenda kijana kweli anakupenda, lakini je wewe unampenda? Tangu umetoka kwenye uhusiano mwingine ambao naamini ulikuwa wa muda mrefu na "serious" ni wazi unahitaji muda kuchuja hisia zako ili kuwa na uhakika vilevile kuwa tayari kujiingiza kwenye uhusiano mpya wa kawaida wa kimapenzi acha ndoa.


Kutokana na maisha ya sasa hakuna kitu kinaitwa kuchunguzana ili kufunga ndoa(ilikuwa miaka hiyo), siku hizi kupendana kwanza, ndio majuana taratibu na kuchunguzana na kuerekebisha kama inawezekana alafu unamalizai nakufanya maamuzi ya busara baada ya kugundua kasoro zake na yeye kugundua zako na kisha kujitoa mhanga na kukubali kuishi maisha yako yote (kufunga ndoa) bila kuzijali kasoro zake na utakachokifanya ni kumpenda mwenzio kila siku kama ndio mmeonana wiki iliyopita.....vinginevyo ndoa itakuwa ndoano.


Sasa, suala hapa sio kama yeye ni mchunaji au lah, kitu muhimu hapa ni wewe na hisia zako juu yake. Je unahisi kumpenda? kama sio je unadhani unaweza kurafikiana nae kikawaida tu? Vilevile unadhani siku moja unaweza kupendana nae na kuwa zaidi yamarafiki wa kawaida?

Nakuja....

Wednesday, 4 February 2009

Tuliachana, sasa nusu anitaka nusu hanitaki-Ushauri!

"Mambo vipi Dinah,
Mimi ni kijana wa miaka 29. Nimekuwa na mahusiano na msichana mmoja wa miaka 25. Kwa sasa tumeachana kwa takribani miezi sita. Tatizo nililonalo ni kuwa tangu tuachane baadae niliona kuwa bado namfeel na yeye alionyesha kuwa bado ananifeel hivyo niliamua kumueleza dukuduku langu.


Yeye akaniambaia kuwa niendelee na maisha yangu, ghafla baada ya wiki mbili akanitumia msg kuwa anani-miss sana kuwa nae na kuwa bado ananipenda na ataendelea kunipenda daima. Mimi nikaamua kumuuliza kuwa yeye hisia zake kwangu zikoje? Jibu alilonipa ni kuwa nusu anataka kuwa nami na nusu hataki kuwa nami.


Pia ameniambia kuwa bado ananipenda sana na hajapenda mwanaume yeyote so far. Pia hajatembea na mwanaume yeyote tangu tuachane.Sasa wandugu hapa huyu mrembo anania gani na mimi? Kama still ananipenda and half anawish niwe nae then kwa nini hataki au kusita niwe nae?


Maana hata nikimwita tu anagoma kuja. Yaani kwa kifupi haeleweki msimamo wake kuwa nini hasa anataka. Mawasiliano yetu sio mabaya. Tunasalimiana kama kawaida.

Dada Dinah na wanablog naombeni ushauri."

Jawabu:Mambo ni mazuri kabisa Kaka, nafurahia likizo baada ya kuwa kule "busy" kwa taribani mwezi na nusu.


Sasa rafiki hujaeleza sababu ilisababisha wewe na binti huyo kuachana kitu kitakachofanya watu, well labda mimi tu kushindwa kukupa maelezo ya kutosheleza na yenye uhakika. Unajua, unapotoka kwneyeuhusiano kutokana na tofauti fulani fulani haina maana kuwa na mapenzi yamekwisha juu ya yule mpenzi wako.


Huenda kilichotokea au kusababisha muachane au namna ulivyomuacha au alivyokuacha ilimuuma sana na kumfanya apunguze hali ya kukuamini tena au kujiamini mwenyewe kwenye suala zima la mahusinao ya kimapenzi na hilo likitokea ni wazi kuwa atahitaji muda ku-sort out kichwa chake na hisia zake kabla hajawa na uhakika wa nini anakitaka ktk maisha yake ya kimapenzi na ngono ofcoz.Sheria moja kuu ya kurudiana baada ya kuachana (well sio sheria inayojuliakana bali huwa naitumia mimi kwa wateja wangu kama wewe leo hapa) ni kuwa unapoachana na mpenzi wako kisha ukagundua kuwa bado unahisi nae za kimapenzi ni kupigania penzi hilo kwa kuonyesha mapenzi ya kihisia ya hali ya juu kuliko mwanzo.........
badala ya kucheza ule mchezo wa "kutegeana".


You just go for it full speed, viginevyo wajanja watakuwahi na watapenda binti kuliko ulivyokuwa unapenda na hilo likitokea ujue wazi kuwa binti hatokuwa na mapenzi na wewe tena kwani mapenzi ya mpenzi mpya yatafunika penzi lako la kusua-sua.


Fafanua akisemacho-Wanawake wengi huwa hawako wazi kusema ukweli, wanakuachia wewe ung'amue anachomaanisha hasa kama anataka wewe umuonyeshe kuwa "unamuhitaji". Sijui nini kilitokea na kuwafanya ninyi wawili kutengana lakini ninachokiona hapa kutokana na maelezo yako ni kupimana misimamo au hisia.


Huyu binti alipokuambia uendelee na maisha yako ni wazi kuwa alikuwa anataka kusikia ukisema "siwezi kuendelea kuishi bila wewe, maisha yangu hayatokuwa kama yalivyokuwa bila wewe mpenzi".....sasa baada ya wewe kuuchuna na kuendelea na maisha yako kiukweli (ulidhani ndivyo alivyomaanisha).

Si umeona mwenyewe akaona hujapata "meseji" akaamua kukumbusha kwa SMS na kusema kuwa anaku-miss, anakupenda na atakupenda daima.....hapo alikuwa anasema ukweli ulio wazi kwa vile wewe hukupata ujumbe wa "endelea na maisha yako".

Kosa kubwa ulilifanya-Alipokuwambia kuwa ameku-miss, bado anakupenda na atafanya hivyo daima, hukupaswa kumuuliza hisia zake juu yako!! Ulitakiwa kumkumbatia na kumwambia kuwa unapenda pia na ungependa mrudiane au kujaribu tena uhusiano wenu.


Mwanamke anapokuwa wazi hivyo ujue kazidiwa na mapenzi(katumia mbinu zote umeshindwa kuelewa), binti anakuhakikishia kabisa kuwa uko peke yako moyoni mwake pale aliposema kuwa hajapenda wala kutoka na mwanaume mwingine (kumbuka ni miezi sita imepita), mwanamke akikaa miezi sita bila kuingia kwenye uhusiano mpya hata kama sio wa kimwili na bado anarudi kwako na kudai anakupenda ujue huyo ni 4 the keep hehehehe sio lazima iwe hivyo, usiogope my broda!.


Nia yake ni kutaka kurudiana na wewe lakini kwa bahati mbaya wewe huonyeshi kutaka kurudiana nae sina hakika ni kwavile huelewi anachokisema kwako au na wewe huna uhakika na hisia zako za kimapenzi juu yake??!!. Ile nusu anakutaka (ni hisia zake juu yako) na nusuhatakikuwa na wewe (ni kwavile hujamuonyesha kuwa unamtaka back).


Sasa skia, inakwenda hivi, sawa!......Muombe msamaha kwa kutokuwa nae kwa muda wa miezi sita (kwamwe usigusie nini kiliwaachanisha), mwambia hisia zako bila kumuuliza yeye anajisikiaje juu yako. Mwambie kuwa unampenda sana na ungependa kuishi maisha yako ukijuwa kuwa yeye ni mwanamke wako peke yako, mueleze kuwa utafanya kile uwezacho ili kufanya uhusiano wenu uwe mzuri, wenye mapenzi ya dhani na wenye afya.


Mwambie tangu mmekuwa mbali-mbali maisha yako yamekuwa sio kama vile yalivyokuwa mlipokuwa wote, mhakikishie kuwa utamuonyesha mapenzi motomoto ambayo hujawahi kumuonyesha hapo awali (hakikisha unafanya hivyo.....hata kama ni kumshukia chini au kumla denda kwa mtindo tofauti).....ongeza na mwengine ujuayo wewe kama mwanaume.


Usitegemee jibu la papo kwa hapo (hii inategemea na ufundi wako wa kubebembeleza, ikiwezekana toa chozi mshikaji...it'll work).....asipokubali on spot mpe muda na wewe kuwa kwenye mawasiliano mara nyingi kuliko kawaida.


Unapowasiliana hakikisha unamsalimia kikawaida nakuonyesha kuwa unajali, lakini kama vipi fanya mawasiliano ile mida ya "chombeza" hakikisha una-flirt(hata kama ni kwa SMS), unamkumbusha mlipokuna (ruka matatizo mliyokutana nayo au mlivyoachana), zungumzia maisha yako ya baade na yeye...Mf-Kama tungekuwa wote sasa hivi tungefanya hivi-vile nakadhalika.

Kila la kheri!

Tuesday, 3 February 2009

Umewahi kuhisi ukamilifu kama mwanamke?

Mambo vipi wewe?

Ni muda mrefu umepita bila kukupa somo, natambua kuwa ulikuwa una-miss mambo fulani, sasa leo rafiki napenda ku-share hisia ambazo sina uhakika kama ni mimi tu ndio huwa nazipata au vinginevyo. Kama hujawahi kuzipata basi endelea kusoma ili ujue kwa undani.


Nafahamu kuwa unafahamu kwamba mwanamke siku zote anachelewa kufika kileleni hali inayofanya waume/wapenzi wetu kufanya wawezalo ili mwanamke uanze kisha yeye amalizie....awe wa mwisho.


Hali hii ikizoeleka inakuwa "boring", yaani kila siku wewe unakuwa wa kwanza! Inakuwa routine kitu ambacho mimi binafsi nakipiga vita kutokea kwenye mahusiano ya kimapenzi kwani kinaweza kufanya ule msisimko wa uhusiano wenu kuwa "butu" yaani uhusiano hauna masham-sham a.k.a hauna "makali"Licha ya hivyo, kuna wakati wewe mwanamke unatakakuhisi "uanamke wako" yaani kama ni mwanaume basi atasema mwanaume aliyekamilika. Ukamilifu wa mwanamke sio tu kujua aina za mapishi, kutoa penzi, kuwa mwepesi wakati wa kungonoana, mwenye kulipenda umbile lake zuri alilojaaliwa na M' Mungu, usafi na mwenye kuvutia bali pia uwezo wa kujua kumuwahisha mpenzi hasa kama mpenzi wako ni mmoja kati ya wale waliojaaliwa kwenda "mwendo mrefu" au kazoea kujizua na hivyo anashindwa kujiachia ili awahi....


Au inawezekana kabisa bao la kwanza kutoka kwake mpenzi wako linakuja haraka (kwaida kwa wanaume wengi hasa kama ananyege sana)lakini yatakayofuatia yanachukua "mwaka" hali inayoweza kukufanya utake kumuona mpenzi wako anakuja tena na tena....si wajua kale kasura ka “nakojoa” au “nakuja”...aah mimi huwa nakazimia sana na kaniniamshia hisia....wanasema “turn on”.


Unaweza kujitahidi kumfanyia manjonjo na masham-sham ili ashindwe kujizuia na kumaliza mapema lakini njema haifiki walanini.....hii ikitokea usikate tamaa na kujishtukia kuwa huwezi "game"...."game" unaiweza ila hujampatia tu......sasa nitakupa kambinu ambayo mwanaume yeyote hawezi kujizuia ikiwa utakapatia kambinu haka.


Kumbuka unapofanya hii mbinu lengo ni wewe na yeye kufurahia hivyo haijalishi ikiwa mtafika wote au yeye kuanza.........utahisi mchanganyiko wa hisia za raha, furaha, ukamili kama mwanamke na mapenzi ya dhati kwa mpenzi wako......inategemea zaidi na unavyolichukulia tendo hili takatifu, kama ni mpenzi wa tendo hili kama mimi basi utakuwa umenielewa vema.

Mkao-Kama kawaida mkao ni kifo cha mende na mtindo ni mwanamke chini.....kifo chamende ni mkao wenye mitindo mingi ambayo haichoshi na inakuwezesha wewe mwanamke kuwa incontrol na kuwa huru kumfanyia mume/mpenzi wako mambo mengi kwa kutumia uke wako kuliko mikao migine.


Si kwa vile nimesema kifo cha mende basi wewe unakimbilia kitandani na kujilaza chali na kujipanua.....hapana! cheza-cheza nae mpe ile inaitwa "stata", au "hapitaita" kabla ya mlo kamili(hajalishi ni mzunguuko wa ngapi)....si unajua kuwa kila bao linautamu tofauti??


Ili asijue nia yako ni nini basi unapaswa "kuzuga" na kumlaza yeye pale kitandani na kuanza kumfanyia "uchunguzi wa kina" kwa kutumia mikono/vidole, matiti, midomo, ulimi, mashavu ya uke.....na hakikisha unagusa kila kona ya mwili wake ambayo wewe unajua anapenda kuguswa.....


Baada ya hapo, jilaze pembeni yake na kumvuta ili aje juu yako au njia rahisi ni kukalia uume wake na kuhakikisha umeingia vya kutosha ndani yako alafu jilaze (full) juu yake bila uume kuchomoka kisha mkumbatie alafu jibilingishe nae.....hapo atakuwa juu yako moja kwa moja.....panua miguu yako vya kutosha ili kukuwezeza kuzunguusha kiuno cha ngono (sio kile cha ndombolo....bali kile nilichokizungumzia ktk Makala za nyuma).


Akisha kuwa juu yako muachie apige "tako" zake mbili/tatu yaani aende juu-chini au nje-ndani mara chache huku wewe ukizunguusha kiuno taratibu kutafuta kona nzuri ya kukibana kichwa......kisha mwambie atulize “ball” yaani hakuna ku-move.....no more takoz!


Alafu sasa, shikilia makalio yake na jaribu kuyakandamiza dhidi ya sehemu ya juu ya uke wako ili kumfanya asi-move(akitaka anaweza) lakini hiyo itakusaidia kumkumbusha kwa kumrudisha ndani kila akitaka kutoka kutokana na utamu.....na vilevile kukupa balance ya kufanya ukifanyacho.

Sasa anza kuzunuusha kiuno chako cha ngono ambacho kitakufanya uhisi kichwa cha uume kinasugua kona ya uke wako pale ulipoubana ktk mtido wa kuzunguuka, kubana na kuachia......endelea kuzunguusha kiuno chako cha ngono ktk nusu mzunguuko/duara yaani degree 180.....yaani huendi mzunguuko mzima unaenda nusu kisha unarudi ulikotoka nusu nyingine....kulia na kushoto.....


Uhatahisi jamaa anataka ku-move au atakushikilia kimtindo kama sio kutoa mihemo na miguno Fulani ya raha.......hatua hiyo ikifika ndio wakati wa kwenda mzunguuko mzima kwa kuongeza speed na kuipunguza.....Mf kukata kiuno cha ngono kutoka kulia kwenda kushoto ni rahisi na unakwenda haraka kuliko kile cha kutoka kushoto kwenda kulia. (inategemea kama wewe ni left heanded au vinginevyo)


Sasa unapobadilisha "rythim" kutoka haraka kwenda taratibu hakikisha unafanya kwa mpangilio huo, kwamba kutoka kulia kwenda kushoto haraka na kutoka kushoto kwenda kulia taratibu.....Hakika ile hali atakayokuwa akionyesha kuwa anafurahia itakufanya wewe ufurahie zaidi na utahisi utamu unakaribia.....

Hapa njemba itapagawa na kupiga "tako" mfurulizo ktk harakati za kufika kileleni.....wakati anafanya hivyo "relax" kiakili lakini kimwili endelea kufanya mambo uliyoanzisha ili mfike wote.

Kunauwezekano mkubwa kabisa akakuacha njia panda....hey ndio nia na madhumuni kumuwahisha......hii yote inachukua dakika dk 10 mpaka 20 ukiunganisha na romance (kuandaana) lakini kwa tendo peke yake ni dk 8-10 tu kitu na box......

Jaribu leo, ili kumpa mpenzi wako mwanzo mzuri wa mwezi.....kila la kheri.

Monday, 2 February 2009

Sitaki kuharibu Urafiki, napiga nyeto. Kuna madhara?

"Mimi ni kijana mwenye Umri wa Miaka 33 naishi nchi yaTanzania, na rafiki yangu wa kike yupo Tanzania kwa muda wamiaka 2 sasa. Kwa muda wote nimekuwa nimeshinda sana nasitaki kuvunja uhusiano wangu na huyo rafiki yangu, sasahivi karibuni baada ya kuona hali ngumu nikaamua kuanzakujichua au kupiga punyeto, naomba ushauri wenu je tendo hili lina hathari gani baadae nitakapo kutanana na rafikiyangu. Natanguliza shukrani zangu kwa majibu mtakayo nipa"

Jawabu: Nakushauri usome Makala za nyuma utakuna na maelezo ya kutosha kuhusiana na kujipa mkono. Asante kwa ushirikiano wako.