Monday, 19 January 2009

Mume ni VVU mimi sina, nataka mtoto-Ushauri

"Hi Dinah
Mimi naitwa Tenisha-(si jina langu halisi) nimekuwa nafuatilia blog yako kwa muda mrefu na nimeona jinsi unavyosaidia watu kwa ushauri wako ,na mimi pia nikaona niseme yaliyoko moyoni kwangu.


Kwa kuanzia mimi nina miaka 25, niliolewa miaka miaka 4 iliyopita na sina mtoto (bado tulikuwa hatujapanga kufanya hivyo kwa wakati huo),ndoa yenye furaha na amani tele, mpaka mwaka 2008 mwezi April mambo yalipobadilika.


Mume wangu alipata ugonjwa kama unaofanana kabisa na Herpeszoster japo Doctor alisema huo ni mbaya zaidi , mimi nilikuwepo na nilimuuguza mpaka alipopona. Baada ya hapo Doctor alisema ingekuwa vizuri kama tungepima HIV, lakini kabla ya ndoa tulikuwa tumepima na wote tulikuwa negative.Lakini mimi nilikuwa na utaratibu wangu wa kupima mara kwa mara ninapopata nafasi ya kufanya hivyo.


Majibu yalipotoka yalikuwa ya kusikitisha, mimi nilikuwa na negative na mume wangu mpendwa alikuwa positive, nilillia sana sana (namaanisha hivyo ) lakini pia sikuweza kubadilisha ukweli.

Ikabaki hivyo tukaenda tena kupima Angaza na hospital tofauti majibu yakabaki hivyo kuwa mimi ni negative na mume wangu ni positive . Tokea hapo mpaka leo nimeshapima sehemu nyingi tofauti na majibu ni hayajabadilika.


Mume wangu namjua tokea tuko wachumba tabia yake naijua sio mtu wa kuhangaika na wanawake, nimekuwa namfuatilia sana nikawa najichosha mwenyewe (lakini ukweli zaidi anao mwenyewe kama ana nyumba ndogo mimi sijui).


Alikoupata sijui hata yeye mwenyewe alikiri hafahamu, ikabidi tukubaliane na ukweli, Sikutaka kumuuuliza sana kama alikuwa na mwanamke mwingine au la ! kwa sababu pia sikutaka akose amani na hali aliyonayo.


Basi ikabadi aanze dawa za kurefusha maisha (sio ARV)ambazo tulipewa na Doctor wetu. Wakati amepata huo ugonjwa tayari CD4 zilikuwa 200. Tuliongea na Doctor sana kuhusu maisha yetu na tulipenda sana kuwa na mtoto mwaka huu 2009, japo haiwezekani, njia aliyotuambia ni fertilization (nadhani wengine wanaijua)ambayo pia sio 100% .


Niliongea nae sana kuhusu mtoto yeye akasema alivyofikiria yeye nizae na kaka yake damu isiende mbali ,nilikataa hapo hapo nikamuambia sitaweza (never happen). Pia tulishauriwa asifanye mapenzi sana kwa mwezi kama mara 2 hivi au 3 asizidishe kwa ajili ya kulinda afya yake na huwa tunatumia condom na tuko makini sana kwa hilo.


Jamani kama nilivyosema hapo juu nina miaka 25, ninapata majaribu sana (kwa muonekano naonekana kama mdogo zaidi ya hiyo miaka na ni mzuri hilo nalifahamu hata mimi mwenyewe-hehe he hehe .) Kufanya mapenzi mara 3 kwa mwezi hakunitoshelezi pia nilizoea sana kufanya romace na deep kiss ila sasa hatuwezi kufanya hivyo ili kunilinda mimi asiniambukize.


Nampenda kumuacha naona siwezi, pia naona anahitaji mtu wa kumfariji kwa sababu bado anaona kama ni ndoto kwake. Na hatujawahi kumuambia mtu yoyote zaidi ya madoctor wanaotupima.

Naomba ushauri .
1.Nitafanyaje kuhusu mtoto , namhitaji sana mpaka huwa nakosa usingizi nikifikiria juu ya kupata mtoto wa njia ambayo hata mume wangu ataridhika na yeye na huyo mtoto (hataki nizae na mtu mwingine )

Jawabu: Hili linawezekana kabisa ila itabidi mchukue tahadhali sana na ni "risk" kwa mtoto. Kama mnaishi nchi zilizoendelea Mf-UK au US mnaweza kuliweka wazi hili suala la kuwa na mtoto huku mmoja wenua na VVU na wao watawaweka kwenye uangalifu mkubwa na kukukufanyia wewe mama (ukishika mimba) vipimo vya mara kwa mara ili kuhakikisha mtoto anakua vema tumboni bila hatari yakupata VVU, Mara nyingi mwanamke hupewa "course" ya madawa fulani kabla hamjanzakujaribu ili "kumimbana".


Kwa "case" yako ni rahasi zaidi kwa vile wewe huna VVU (japokuwa utakwenda through vipimo vingi na vya mara kwa mara kuhakikisha hilo, kuwa kweli huna kabisa-kabisa VVU), mwanamke akiwa hana VVU anaweza kuzaa mtoto ambae hana VVU tena bila kutumia madawa yeyote ya kumzuia mtoto kulikwaa gonjwa hilo kwa vile inasemekana kuwa mbegu za kiume hazibebi vijidudu vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kuliko mwanamke mwenye VVU.....tafadhali bonyeza link hapo pembeni kulia mwa blog hii kwenye maandishi yakijanani chini ya Profile yangu kuna maelezo ya kutosha kutoka kwa madaktari na pia unapata nasafi yakuwauliza maswali moja kwa moja, tafadhali jiweke karibu nao kwa ushauri zaidi wa kitibabu.


Kitu kingine unapaswa kufahami ni kuwa HIV Virus ziko za aina 3 tofauti. Aina mbili ambazo ni hatari zadi zinanawiri nchi za joto hasa Afrika na aina ya nyingine inastawi zaidi nchi za Baridi. Inasemekana kuwa ukiwa na VVU aina ya tatu na unaishi nchi za joto kuonekana sio rahisi ukilinganisha na zile mbili za "kiafrika".


Ndio maana nikasema kabla ya kuambiewa wendelea na suala la kumimbwa huwa wanakupa vipimo vingine lukuki ili kuwa na uhakika....tafadhali soma Tovuti nyingine inayojihusisha na kuzuia VVU kwa watoto....bonyeza hapo kulia kwenye Logo ya mtoto kwa maelezo zaidi ya kitaalamu.


2.Mimi jamani bado mdogo nina mihemuko ya ujana nahitaji kufanya mapenzi nifurahie pia sitaki kutoka nje ya ndoa.


Jawabu:Kutokana nakilichotokea kwenye ndoa yako na kama ulivyodai kuwa unampenda mume wako na nyote mnaonekana ni waelevu basi sio mbaya kama utashauriana na mume wako na kukubaliana kuwa wewe uwe ukitumia "sanamu" kujiridhsiha pale unapohitaji zaidi. Matumizi ya sanamu za ngono sio kitu ambacho mimi binafsi huwa nashauri wapenzi kutumia kwavile naamini katika uumbaji wake Mungu, lakini kama "issue" ndio hii ya VVU ninafuraha kabisa kusema....tafadhali kanunueni sanamu ili wewe uweze kukabiliana na mihamko yako.


Utakachotakiwa kufanya hapa ni kuwa "mbinafsi" kidogo ili kuzuia kumtamanisha mumeo ambae kutoka na ushauri wa Daktari hapaswi kufanya ngono mara nyingi kama ilivyokuwa hapo awali kabla hajajua kuwa anaishi na VVU.*****


Nitashukuru wa ushauri /maoni kutoka kwako Dinah na wengineo. Nimejieleza kwa kifupi ila nina imani nitakuwa nimeeleweka na nitapata ushauri mzuri.
Tenisha"

Jawabu:Tenisha, asante kwa kuwa mfuatiliaji wa mahali hapa, shukurani kwa mail yako na kwa uwazi wako.

Pamoja na kuwa nimekujibu moja kwa moja ningependa nitoe maelezo kwa ujumla ili kuweka sawa au kujazilizia mengi na mazuri yaliyosemwa na wachangiaji. Inasikitisha wengi wamekushauri uachane na mumeo (kitu ambacho mwanaume actually angekifanya kama wewe ungekuwa na VVU).


Kuna wachangiaji wamgehusia suala la "rushwa", ni kweli kabisa watu wengi wanatoa "kitu kidogo" kwa madaktari ili wapatie majibu ya uongo (hawana HIV) lakini ktk hali halisi wanakuwa navyo na wanajua kuwa alikwisha vikwaa miaka ya nyuma, lakini kwa vile CD4 ziko juu, wanaendelea na maisha kama kawaida na zitakapo pungua na kudaka maambukizo wakati tayari yuko kwenye ndoa unaweza kusukumiwa wewe lawama kuwa ulikuwa "kicheche" ndani ya ndoa.


Kama ulivyosema ulijitahidi kumchunguza na kuhakikisha kuwa hana tabia ya "kuchomoka" nje ya ndoa yenu, inawezekana ni kweli kabisa hajaupata baada ya kutoka nje ya ndoa, kuna uwezekano mkubwa aliupata kabla ya ndoa na akafanya "makaratee" na Dk ili kupata majibu kama yako.


Kuna njia nyingine za mtu kupata VVU ambavyo sio lazima iwe Ngono (inategemea na shughuli zake) kama Nesi au Daktari anaefanya kazi na waathirika wa VVU. Vilevile kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu namna ya kuishi na watu wenye VVU ambao tayari wanaugua....kutokana na utu au ukaribu wa wahusika au ukosefu wa vifaa hapo nyumbani mtu anaweza kujisikia vibaya kuosha kidonda/kinywa kwa kuvaa mpira na badala yake akatumia mikono mitupu ambayo huenda ilikuwa na mkato/mchubuko ndani ya ukucha n.k.


Pia wapo watu ambao wanaambukiza wenzao kwa makusudi kwa kujichoma sindano kisha kuwachoma wenzao na sindano za kushonea, pini, kitu chochote chenye ncha kali au hata kuweka vifaa vya kunyolea walivyovitumia karibu au hata kuvibadilisha(kuonda visafi na kuweka vyao walivyotumia).Njia nyingine ambayo mtu anaweza kupata VVU ni kunyoa, tengeneza nywele Salon, sio wahudumu wote wa sehemu hizo wanatumia bidhaa maalumu iliyothibitishwa kitaalamu ili kuuwa vijidudu vinavyosababisha UKIMWI na wanapofanyia kazi nywele zako sio wakati wote wanaikwepa ngozi, wakati mwingine inatokea bahati mbaya ngozi naguswa, sasa kama kifaa hicho kilimnyoa mtu mwenye VVU ni wazi unakuwa hatarini (Inashauriwa kwenda na mashine/vifaa vyako mwenyewe just incase)


Kutokana na maelezo yako nahisi mumeo alijua alichonacho mwilini mwake (VVU) na akawa muangalifu sana kila anapofanya mapenzi na wewe ili asije kukuambukiza, lazima alihakikisha unakuwa tayari kabla ya tendo na hakuwa akilazimisha ikiwa hauko kwenye "mood".


Ni vema jamii ikabadilika jinsi inavyolichukulia suala la VVU. UKIMWI ni gonjwa hatari kama yalivyo magonjwa mengine mengi ambayo hayana tiba bali dawa ya kupunguza makali yake Mf ni Pumu, Moyo, Kisukari, Saratani mbali mbali, Matatizo ya akili n.k tofauti yake ni kuwa UKIMWI unaambukiza wakati hayo mengine hayaambukizi lakini yote yanaua na ktk hali halisi baadhi yake yanakuondoa haraka kuliko yule mwenye VVU.


Tukumbuke kuwa hivi sasa tunamezunguukwa na jamii kubwa inayoishi na VVU, na kuwa na vijidudu hivyo haina maana kuwa wewe ni mgonjwa japokuwa unatakiwa kuwa muangalifu na kumuona Daktari wako mara tu unapojisikia tofauti (maumivu au kujisikia ovyo/vibaya), hii inasaidia wao kukufanyia vipimo na kujua tatizo ni nini....huenda umekumbana na maambukizo fulani na hivyo inakuwa vema kulitibu tatizo hilo kabla halijawa sugu kwani mwili wa mtu mwenye VVU hauna kinga za kutosha za kupigana na magonjwa/maambukizo mbali(sote tunalijua hili).


Elimu kuhusu UKIMWI in terms of kujilinda, unavyoambukiza na kujizuia imetosha lakini sasa inahitajika elimu kuhusu namna ya kuishi na VVU na kuishi na watu wenye VVU.


Kidokezo:Napenda kuwakumbusha rafiki zangu. Condom ni asilimia 100 lakini kutokanana sababu za kisheria hiyo asilimia moja ambayo inafanya bidhaa hii kuwa 99% inalinda Kampuni husika kwa utengenezaji wa bidhaa hiyo, ikiwa wewe utaitumia vibaya na kupata maambukizo ya VVU.

Unapoamua kutumia Condom, mnapaswa kuwa waangalifu kama sio kuziruka harakati nyingine za kuandaana kuelekea kwenye safari yenu kabla ya kuvalia vazi hilo maalumu. Kushikana nyeti, kugusisha nyeti zenu, kubusu, kunyonyana huko chini n.k....huwezi kufanya vyote hivyo kisha ukadai "nilivaa Condom au alivaa Condom hivyo sina HIV", kama ndio katabia kako ka kutumia condom baada ya kufanya yote hayo bila Condom......kapime!


Wapo wanandoa kama huyu Mdada (nawafahamu) ila wao walifunga ndoa wakijua kabisa mmoja wao ana VVU baada ya mkewe kufariki, pia ilithibitishwa baada ya Njemba kupima. Siku zote wanadai kutumia Condom na walipokuwa wanataka "mimba" ndio walikuwa wanakwenda nyama 2 nyama lakini kwa uangalifu na kwa kuzingatia lengo moja tu ambalo ni kusababisha mimba na sio mambo ya utamu au kwenda mwendo mrefu. Sasa wanawatoto wawili wenye afya na mkewe hana VVU huyo bwana yuko chini ya matumizi ya madawa.


Fafadhali mpenzi msomaji ukipata nafasi tembelea Tovuti husika kuhusu HIV ili kujifuza zaidi mabadiliko ya wadudu hao, kuishi navyo, kuishi na walionavyo, ngono na mpenzi mwenye VVU na mambo mengine mengi kwa faida yako, huenda sio wewe leo lakini kesho ikawa mdogo wako au hata rafiki yako kama sio mtoto wako.

Kila la kheri Tenisha, na hongera sana kwa kuwa na mapenzi ya dhati kwa mumeo. Mungu akubariki na nawatakia maisha marefu ya ndoa.


Friday, 16 January 2009

Ex anataka kuniharibia ndoa yangu-Ushauri

"Heri ya mwaka mpya dinah,
Mimi ni mwanamke wa miaka 30 nimeolewa na mume anaeni-treat vizuri sana. Hivi majuzi mume wangu alikua amesafiri nikapata namba ya mchumba wangu wa zamani ambaye ndio alikuwa bf wangu wa kwanza aliyenibikiri tukaanza kuongea kwenye simu tupo miji tofauti.


Nikawa so happy tukawa tunatombana kwenye simu nalegea kabisa lakini nikishamaliza kuongea nae najisikia vibaya sana kwanini namfanyia hivi mume wangu nikasema lazima ni-stop kuongea na huyu bf wa zamani.


Siku moja nikaamua kumwambia kuwa mimi nampenda mume wangu kwahiyo naomba tu-stop kuwasiliana. Alikasirika ile mbaya akasema atamwambia mume wangu kuwa nilikua nawasiliana nae sasa naogopa mume wangu ataniacha hata sijui nifanyaje dada dinah nampenda sana mume wangu naomba ushauri asante. "

Jawabu:Mwaka umechanganya kabla ya muda wake, heri ya mwaka mpya nawe pia. Asante sana kwa kuniandikia.


Sasa rafiki hata kama uliipata namba ya Ex kitu gani kilikufanya umsake na kuanzisha mawasiliano ukijuwa wazi kuwa penzi la kwanza huwa haliishi.....watapita wengi lakini wa kwanza daima atakuwa wa kwanza tu, ndio ulipojifunzia mambo, ndio ulipozijulia hisia za kupenda kiumbe wa jinsia tofauti na yako. Fanya yoote lakini stay away na 1st bf.


Kitendo ulichokifanya ni kibaya na kinahesabika kama "cheating" kwa vile ulipata hisia za kutamani, ulivuta hisia za alivyo huyo ex na ukajishikana na yeye akajipa mkono na hatimae wote mkafika mwisho wa safari......mkiwa simuni, mihemo, sauti za mahaba na kila kitu kilifanyika na kupenya kwenye akili zenu na mioyo yenu......shetani alikupitia eti??


Ofcoz mwanaume yeyote mjinga-mjinga lazima angekasirika, unalianzisha zali alafu sasa unamkatisha, kwani ulipoanza ulikuwa hujui kuwa unampenda mume wako?


Kama unaweza kufanya ngono via simu na Ex kwanini usingefanya hivyo na mume wako? Ni wazi kuwa unahisia fulani na Ex pia nahisi hiyo nambari yake ya simu ulikuwa nayo tangu zamani, ila ulikuwa unajaribu zali kuona itakuaje kukumbushiana enzi (hehehe just joking).....naelewa hilo na ndio maana huwa nashauri watu kukaa mbali na Ex hata kama waliachana kwa vita vya ghuba au kwa kuelewana.


Nini cha kufanya-Hakikisha huyo Ex hajui unapoishi na vilevile hajui mawasiliano mengine zaidi ya nambari yako ya simu. Kama nambari ya simu ya ndani (land line) basi waombe jamaa wa simu kublock nambari yake na ikiwa mlikuwa mnawasiliana via simu ya mkononi(mobile) unaweza kufanya hivyo mwenyewe (m-block) na kuanzia hapo cheza mbali (jitenge) naye au watu wengine walio karibu na ex wako huyo, ukifanikiwa hili utakuwa umeshinda na hakuta kuwa na sababu ya mume wako kujua nini kilitokea....hilo mosi.


Pili, ikiwa anajua mizunguuko ya mumeo na mawasiliano mengine kama emails basi hakikisha mume wako anajua nini kilitokea kutoka kwako moja kwa moja na sio kutoka sehemu ya tatu, kuwa wazi lakini usivuke mipaka ili kulinda hisia zake.


Tatu, Mueleze mumeo kuwa alipokuwa safarini, ex alianza kuwasiliana na wewe lakini hukuwa "comfortable" ukaamua kukatisha mawasiliano hayo kwa kumpiga marufuku huyo bwana (ex), na ulipofanya hivyo huyo bwana (ex) akakasirika na kusema kuwa atahakikisha ndoa yetu inavunjika.....alafu omba ushauri kwa mumeo kwa kusema mfanye nini?


Mumeo anaweza kukuhoji maswali ambayo baadhi ya wachangiaji au hata mimi mwenyewe nimekuhoji, hivyo hakikisha umejiandaa kutoa majibu ya kuridhisha vinginevyo anaweza kukushitukia kuwa wewe ndio ulianzisha zali.

Ndoa haiwezi kuvunjia kwa ku-cheat kwa simu japokuwa inaweza kusababisha mabishano makubwa, hasira baina yenu na hali ya kutokuaminiana ktk uhusiano wenu kwa kipindi fulani, lakini yote yatapita na hali itakuwa ya amani na furaha.......yote hayo yanategemeana wewe mwanamke utakavyojitahidi kurudisha Uaminifu ndani ya ndoa yenu.

Tafadhali jaribu kuheshimu ndoa yako ili kusaidia kurudisha thamani ya ndoa katka jamii.

Kila la kheri.

Monday, 12 January 2009

Ushuhuda! Katangaza ndoa lakini....Ushauri!

"Dada dinah pole sana kwa kazi za kuelimisha jamii. Mimi ni msichana wa miaka 24 ,nina tatizo ambalo naomba msaada wako pamoja na wadau wengine tena naomba kama inawezekana unipe favour unisaidie angalau ndani ya wiki hii ili nisije nikajiharibia.


Dada tatizo langu ni hili; mimi nina mchumba ambaye tunategemea kufunga ndoa mwezi wa tano mchumba wangu ambaye kwa kweli nampenda sana yeye anakipato kidogo ukilinganisha na mimi, lakini nimejitahidi kumuonesha kua fedha wala dhahabu haviwezi kuleta furaha ya moyo.

Sasa juzi alinifuata na kuniomba nimsaidie kulipa mahari jamani kweli nilisikitika alivyo kujana kuniambia ''dia kweli nakupenda toka moyoni na napenda ndoa yetu iwe hata kesho tatizo linakuja kua hela zina nipungukia na natakiwa mwezi wa pili nipeleke mahari nisaidie mpenzi nimekwama '' ukizingatia kua huo mwezi wa pili ndio anatakiwa aende ili akapewe tarehe ya ndoa.

Kusema kweli hela anayoipata ni ndogo ukilinganisha na kile anachodaiwa, sasa dada naogopa kumsaidia japo naumia sana, naogopa baadae kwenye ndoa asije akaniletea dharau kua hatamahari ulijilipia mwenyewe.


Nisaidieni kua nimsaidie au nizibe masikio japo ni mambo mengi tuna saidiana ila hili nimeliona ni kubwa. Nitashukuru kupata ushauri wenu ilinikaufanyie kazi .


USHUHUDA: Dada mimi nilisoma Makala yako inayo husu jinsi yakumfanya mwanaume atangaze ndoa, kweli nilifanya hivyo na nikashangaa siku tatu baada ya kumfanyia vibweka nikashangaa anakuja nakuomba tena kwa magoti ''Dia naommba unisikilize shida yangu '' nikamuinua eeeh sema shida gani ya kunipigia magoti ? nataka tufunge ndoa yani tena mwakani sitaki hata mwezi wa sita ufike .

Nikauliza kulikoni mpenzi, nikasikia ooh nimeamua tu. Nikahoji utaamuaje fasta hivyo ? nikasikia "duh hayo maswali mengi sana ina maanisha hutaki ?" nikasema kimoyomoyo mambo ya dada Dinah hayo , nikasikia dia nataka nifaidi kwa karibu sasa najua nikibung'aa nitakuta mwana siwangu.


Kuuanzia pale wivu ulizidi nikashangaa ananisindikiza kila mahali ukaribu ulizidi sana wakati mwingine naambiwa kabisa mama unanitia wivu. Samahani kwa mlolongo wa maneno. Nilikua najaribu kutoa ushuhuda ."

Jawabu-Hongera sana kwa kufanikiwa kumfanya atangaze ndoa, unajua kuna wanaume wengine wanakuwa na wewe kwenye uhusiano kwa muda mrefu bila kuonyesha nia ya kutaka kuwa na wewe daima (Ndoa), sio kuwa hataki bali anadhani bado anamuda wa kusubiri sasa hilo likitokea basi ndio wewe mwanamke unapaswa kumsaidia kwa kumfanyia mambo niliyoelezea ambayo wewe uliyafuata na yametimia.


Ushirikiano-Ni moja kati ya nguzo tano za kuboresha uhusiano wowote wa kimapenzi, tunapozungumzia kushirikiana na kufanya mambo pamoja kwa faina yenu nyote wawili hatuzungumzii kwenye kuwa pamoja katika kufanya maamuzi au kufanya mapenzi tu bali hata kwenye suala zima la kiuchumi.


Ninyi ni wapenzi na uhusiano wenu ni mzuri na baada ya muda mfupi mtakwenda kula kiapo cha kuishi maisha yenu yote kama mke na mume. Hili likitokea ni wazi kuwa kutakuwa na suala la kusaidiana ili kufanya maisha yenu ya ndoa yawe mazuri na kuishi vile mpendavyo na sio kwa shida kuu.


Kutokana na maelezo yako unaonyesha ni binti mwenye kuthamini mwanaume na haujaegemea sana kwenye suala la Usawa ambao mimi huwa naona ni ujeuri ambao wanawake wengi wanaubeba kwa kisingizio cha "Usawa" na ndio maana mpenzi wako akawa huru kuja moja moja kwako na kuomba msaada, katika hali halisi alipaswa kwenda kuomba/kopa rafiki zake au hata baba yake.


Mahari-Haya ni malipo yanayotolewa na mwanaume ili kuruhusiwa kuoa binti husika, matumizi na maana ya "malipo" haya ni tofauti na inategemea na Mila za wahusika. Mf-Ninakotoka mimi mahali sio ya wazazi, wajomba na shangazi bali ni yako wewe binti.


Ikipokelewa kama ni mifugo au pesa basi baada ya muda unakabidhiwa kwa maana kuwa unahitaji kitu cha kuanzia maishani wewe na mume wako. Mahari hiyo haiesabiki kuwa inatoka kwa kijana anaetaka kuoa bali inatokwa upande wa pili yaani familia ya mumeo, sasa binti hapa anaweza kupewa nafasi ya kutaja kiasi cha "malipo" anachotaka kutoka upande wa pili na mara nyingi Mahari hiyo hutumika kufanya maandalizi ya sherehe ya ndoa na sio kuanzishiwa biashara (hakuna kulipana ikiwa ndoa itaharibika).


Vilevile binti anaweza kuamua mahari ilipwe kwa mafungu (taratibu) au asipokee kabisa na hii inategemeana na uwezo wa familia ya mpenzi wake ambayo kwa wakati huu atakuwa anaijua vema.


Lakini Mila nyingi huwa na malipo ya awali ambayo ndio muhimu "kimila" ( na sio pesa nyingi, zaidi ni kununua vifaa/vitu fulani fulani kwa wanafamilia bibi, mkwe sijui mkaza mjomba n.k) kabla Mahari haijalipwa, hayo yakikamilishwa mipango ya ndoa inaanza mara moja na Mahari inaweza kulipwa baadae hata baada ya kufunga ndoa.


Kasumba-Suala la "ndio maana ukajilipoa mahali" lisikusumbue kichwa, ni kasumba tu ya wanawake wajinga wajinga ambao wanaamini kuwa ni lazima kuolewa na mwanaume mwenye "mahela" na wanaangalia zaidi kiasi gani cha pesa as for Mahari mwanamke mwenzao kalipiwa.......lakini katika hali halisi ulipiwe elfu 20 au milioni 50 bado utahitaji mapenzi na mambo mengine mengi ambayo hayahusishi pesa, ili kuifanya ndoa yako iwe nzuri, yenye afya, furaha na amani hapo baadae.


Nini cha kufanya-Mchumba wako kasema (kama ulivyoandika) "Dia kweli nakupenda toka moyoni napenda ndoa yetu iwe hata kesho tatizo linakuja kuwa hela zinanipungukia natakiwa mwezi wa pili nipeleke Mahari nisaidie mpenzi nimekwama".


Huyu bwana (kutokana na nukuu hiyo hapo juu) anaomba kuongezewa pesa ili a-top up kile kidogo alichonacho ndani ya muda aliopewa na sio kukuomba wewe mpenzi wake ujilipie Mahari yote, kwa maana nyingine, inawezekana kabisa ikawa sio msaada wa pesa anaotaka kutoka kwako bali ni wewe kuzungumza na familia yako kumpa muda zaidi wa kukusanya pesa ili kukamilisha mambo.


Kama kweli mnapenda na nia yenu ni kuishi kwa shida na raha maisha yenu yote yaliyobaki basi msaidie kwa kuongezea kile kidogo alichonacho. Huitaji kumwambia mtu yeyote kuwa umemuongezea mchumba senti ili akamilishe mahari on time. Chukulia kuwa mmeamua kuchanga kufanya jambo muhimu kwa ajili ya maisha yenu kama vile kununua kiwanja na kujenga nyumba pamoja.

Kila la kheri ktk kukamilisha shughuli za ndoa. Mungu akujaalie.

Wednesday, 7 January 2009

Alini-treat kama taka, sasa yu mahututi...nijimuvuzishe?

"Dada Dinah,Mimi ni mdada wa miaka 38, ninaishi ughaibuni. Ninaelimu, kazi na ya kunipa kipato cha kunitosha. Miaka miwili iliyopita nikiwa 36 nilikutana na kijana wa kitanzania ambae alikuwa 29 wakati huo.

Alihamia kwangu na tuliishi vizuri tu, hakutaka rafiki yake hata mmoja ajue anaishi wapi. Katika kipindi tunaisha wote nilipata mimba, alipogundua nina mimba alitaka nikaitoe lakini nilikataa akaanza kunitomba kama ugomvi na alihakikisha kila siku tunatombana tena dog style!


Siku moja nikiwa kazini nikaona damu imeanza kutoka, niliomba Mungu isiendelee lakini jioni ya siku ile nilijua tu mimba haipo tena ilekuwa kama ya wiki 5-6. Baada ya kuishi kwangu kwa miezi kama 4-5 siku moja aliniambia amepata apartment yake na kwamba yeye na mimi tutakuwa tunatembeleana.


Alipohama alibaki na funguo za nyumba akawa anakuja mara nyingi mwisho wa wiki, lakini hataki rafiki zake wajue kama anakuja kwangu. Kwakuwa ninataka sana mtoto basi niliamua kutombana nae ili nipate mimba lakini kila tukitombana anamwaga shahawa nje.


Mwezi wa tisa mwaka huu kulitokea tatizo ambalo lilitufanya tukutane mahali ambapo alikuja na rafiki zake, pale alijifanya kunisalimia kama tu mtu anaemfahamu na akawa yuko karibu na wasichana wengine, nishindwa kuvumilia nikamwambia mimi na yeye iwe mwisho ana funguo zangu anirudishie.

Alikuwa akibembeleza sana na nilimrudisha mwezi wa kumi na moja mwanzoni, ila funguo sikumpa.Kuna siku aliniambia anakuja, lakini hakutokea, kesho yake nilimpigia simu na simu yake ilikuwa imefungwa, sikuwa na mtu wa kumuuliza kwani rafiki zake siko karibu nao. Baada ya mwezi ndiyo nikagundua kuwa alipata ajali ya gari na sasa hivi ni mgonjwa mahututi hospitali.
Dinah ninaomba ushauri."

Jawabu-Pole sana kwa kupoteza mimba, sasa dada yangu ilikuwaje mpaka ukawa unaruhusu akungonoe kwa nguvu na kwa mtindo ambao ulijua wazi kuwa unaweza kusababisha mimba kutoka? au ndio mapenzi ya dhati?


Natumaini ulienda kwa Daktari wakakuchunguza na kukusafisha, kwasbabu usipofanya hivyo unaweza usishike mimba tena au ukawa na matatizo mengine ya viungo vya uzazi hapo baadae. Ikiwa hukwenda basi hima, fanya haraka na weka mihadi na Daktari kwa uchunguzi na umueleze ilivyokuwa kwa uwazi.....namna ulivyokuwa ukifanywa kwa fujo ili mimba iharibike.


Huyu bwana huenda anaendesha maisha mengine bila wewe kujua, usikute Bongo ameacha familia na anahofia kuharibu uhusiano wake na watu wake na ndio maana alikuwa naficha uhusiano wane kwa watu wengine ambao wako karibu sana na yeye. Kutokana na maelezo yako huyu bwana alikuwa anakutumia.

Uamuzi uliouchukua wa kumaliza uhusiano ulikuwa wa busara kwani huyo sio mtu mwenye kujali na wala hana huruma, kama hakutaka kuzaa na wewe kwanini basi asingekuwa akimwaga nje tango mwanzo? Na hata kama hakuwa tayari au hakutaka kuzaa na wewe, kitendo cha kukufanya kwa fujo ili kuharibu mimba ni cha kinyama na hapaswi kusamehewa. Hicho kitendo alichokifanya kinaweza kabisa kukusababishia matatizo makubwa hapo baade, wakati huo utakuwa umeshasahau.


Lakini kwa vile mlikuwa mmerudiana mwenzi wa kumi na moja lakini kwa bahati mbaya hakutokea kwako baada ya kupeana mihadi na wewe baadae ukagundua kuwa amepata ajali na yuko mahututi, kama mpenzi wake na unampenda ni vema basi ukaenda kumjulia hali huko Hospitali.


Mungu akimjaalia na akapona basi mpe kitu cheupe a.k.a live, kuhusiana na kuficha uhusiano wenu na matokea yako ndio kama ilivyokuwa. Kisha mpe msimamo wako kuhusiana na aina gani ya uhusiano unataka, nini unategemea kutoka kwenye uhusiano huo na nia yako ya kuwa mama.......kuwa muangalifu hapa ktk maamuzi. Ikiwa kapata ulemavu basi tambua kuwa atakubali haraka haraka so u can look after him......


Katika hali halisi, huyu kijana hajakomaa/kua kiakili na hajui majukumu yake kama mwanaume, najua unajua kuwa hakufai........hivyo sioni sababu ya wewe kupoteza muda wako na mtu kama huyo mwenye akili ya ki-teenager.

Zingatia furaha yako kwenye uhusiano wa kimapenzi uutakao, hata kama unataka sana mtoto hakikisha unazaa na mwanaume ambae anania kama yako ya kuwa na mtoto, kumpenda, kumjali, kumtimizia mahitaji na kuwa pale kwa ajili yake.


Angalia hamu yako ya kuwa na mtoto isikufanye ujiingize kwenye uhusiano "abusive" kama wa huyu kaka aliepata ajali. Chukulia kila siku kama inavyokuja na hakika siku moja utakutana na Mkaka mwenye nia nzuri tu yakutaka kuwa "baba".


Usikimbilie Vijana "single" ambao wanadai hawajawahi kuoa kabisa, nenda kwa wanaume "single" ambao ni wajane (kuwa makini na hoji nini kilimuua mke wake) au "single" waliotalikiwa (kuwa muangalifu na dadisi nini hasa kilisababisha mwanamke mwenzio kutoa/kupewa talaka). Hii jamii akilini huwa wametulia na hawana haraka/mapepe vilevile wanauzoefu mzuri sana wa kimaisha tofauti na wale "BNNK" a.k.a bado nipo nipo kwanza.

Kila la kheri.

Friday, 2 January 2009

Mume wangu namtaka na Bf namtaka-Ushauri

"Habari dada Dinah,
Mimi ni dada wa miaka 29, ambaye niliolewa miaka 7 iliyopita pia kwa kipindi chote niliwahi kushika ujauzito wa miezi 7 kisha mimba ilitoka. Hadi hivi leo yapata miaka mitano sijawahi tena kupata ujauzito.

Mume wangu ni Mzungu na ni mtu wa makamo ambaye kanipita zaidi ya miaka 29. Dada na wadau wengine nakiri nilijiwahisha kuolewa kwa tamaa ya pesa na maisha bora kutoka kwa Mzungu huyo.


Ni kweli vipesa vya kubadilishia nguo, mboga hazinipigi chenga. Miaka yote sita tuliishi Tz lakini sasa tumeamua kuwa huku ughaibuni. Dada tatizo langu la kutoshika mimba lilinichanganya mpaka nikaunda urafiki wa chinichini(siri) na kijana mwenzangu Mtanzania ambaye yupo bongo, niliona ngoja nijaribu huku nione kama mimi ndio ninatatizio au mume wangu.


Dada tumetombana wee siku za hatari najiachi sijaona dalili yeyote ya mimba. Pamoja na kujaribu urafiki na kijana mwenzangu tumechonga mzinga kwani urafiki wetu ni wa miaka 3 sasa, mwenzangu yeye yupo single.

Sasa dada si unajua mapenzi ya kijana kwa kijana ni raha tupu ukimpata awezae? dada sio siri huyu boyfriend ananifikisha kunako halafu ni very hadsome......mwangu ana V shape,ananipeti vilivyo, ingawa kipato chake si kama changu.

So ndugu zanguni juzi juzi nimeenda Bongo mwenyewe bila ma husband, basi boyfriend akaja nipokea tulieenda kulala hotelini siku hiyo sikutaka kwenda kwangu mbezi, tulikuwa tumemisiana kichizi.


Ila kufika usiku mpenzi wangu huyo alinieleza kuwa eti anataka kuoa, ametafutiwa mke Mombasa na bibi yake, pia ndugu wanamkera kuwa lazima aoe. Sio siri mimi nina moyo mwepezi ikaniuma basi nililia ingawa nimeolewa.


Akasema sasa kama wewe upo Ulaya unakaa miezi 3 ndio unakuja Bongo, tena unarudi Ulaya lipi bora mim ikuoa au kukaa na kufuta machangudoa? Pia nilisha mwahidi kuwa ningemsaidia juu chini naye awe huku Ughaibuni?


Hivi ndugu tarehe 24 Januari ndio Ndoa. mimi nampenda, pia nina wivu nae sana, Pia ameniomba pesa ya mchango wa harusi, nikimuliza anadai ooh hata kama naoa fanya juu chini unilete Ulaya na huyu mke ataenda kukaa kwao Mombasa.


Anaendelea ooh yote umeyataka wewe kwani siku zote hizo ningekuwa nawe Ulaya mke ningepewa saa ngapi. Na yeye pia anaonekana upendo nami bado. Jamani namzimia, anasifa nizihitajizo za kuitwa mwanume, anajua jinsi ya kuniandaa kuliko mume wangu.


Jamani pia nawahasa watu wasomao haya umri katika mapenzi ni kitu kizuri. Wazee bwana akifanya ni kimoja kwa week, au mbili, sometime ukimkalia utafikiri atakufia, akitomba kimoja atahema kama anakata roho.


Ndugu naombeni ushauri wenu, pia nimekiri kusaliti ndoa yangu najua ni dhambi, mume wangu namtaka handsomeboy namtaka niko njia panda dada yenu.

asanteni nawatakia HAPPY NEW YEAR:"

Jawabu: Habari ni njema tu Mdada, shukrani kwa kuniandikia, nitarudi baada ya muda mfupi kutoa maelezo yangu ambayo kwa namna moja au nyingine yatakusaidia ukiongezea na yale yaliyokwisha elezwa na wasomaji wangu.

Ni kweli kabisa watu wengi tu wanafunga ndoa kwa sababu fulani na sio mapenzi kama ambavyo baadhi yetu tunaamini, ni sehemu ndogo sana ya watu ambao wanafunga ndoa kwa sababu ya kupendana na kutaka kuishi kwa shinda na raha maisha yao yote. Umenifurahisha kwa kuwa muwazi kuelezea hali halisi na kwanini ulifunga ndoa na Mumeo huyo.

Ndoa bila mapenzi-Uamuzi wa kuolewa ili kuishi maisha fulani au kupata kitu fulani(makaratasi) sio wa ajabu kwa wanawake na wanaume wengi wa Kiafrika, lakini tofauti ni kuwa wengi wao hujitoa mapema mara tu baada ya ile "plan" kukamilika na kuachana Wazungu wa kisha kwenda kuendeleza mapenzi ya kweli huko waendako.....kila mtu nahitaji kupenda nakupendwa, maisha yangekuwa jehanam kama kusingekuwa kuna mapenzi baina ya watu wawili.


Kitendo unachokifanya nje ya ndoa yako sio kizuri na ni ukatili wa hali ya juu kwa mume wako. Ikiwa uliolewa kwa ajili ya kuishi maisha ya hali ya juu (ilikuwa mission) sasa ulitakiwa kuwa mbunifu na kufanya miradi ili kuchuma vya kutosha kisha ujitoe kwenye ndoa ambayo haina mapenzi ya dhati na imejaa uongo kitu kinachokufanya usiwe na raha wala amani.


Baada ya kujitoa (kuachana) ndio ungeenda kutafuta mapenzi na mtu mwanaume mwingine ukiwa huru na usingeumiza hisia za mumeo ambae mpaka sasa hajui kuwa anachangia mwili wako na mwanaume mwingine!......jaribu kujigeuzia angekuwa yeye mumeo anafanya hivyo na mwanamke mwingine ungejisikiaje?


Nilichogundua hapa ni kuwa ulikuwa na hisia za kimapenzi na mumeo na ndio maana mpaka leo bado uko nae, ila tatizo ni wewe na mumeo, hamlizungumzii hili suala la kujaribu njia tofauti ili mfanikiwe kupata mtoto.

Kutokana na tofauti kubwa kiumri huyo bwana (mumeo) anaweza akawa na huruma sana kwako na kuku-treat kama mtoto wake zaidi kuliko mpenzi, hali inayoweza kusababisha ashindwe kukumbushia suala hilo la kujaribu uzazi tena akijua ile mimba iliyoharibika imekuathiri Kisaikolojia (which ni kweli na nina amini kabisa kuwa kichwani hakuko sawa) na asingependa kukuumiza.

Mimba-Ikiwa ulishika mimba na ikatoka baada ya miezi saba (alikuwa mtoto mkubwa kabisa, tunasema "mtoto alifia tumboni") ni wazi kuwa mumeo hana matatizo yeyote, inawezekana wewe ndio unamatatizo yanayohusiana na viungo vyako vya uzazi kwa ndani.


Badala ya kwenda kutembea ovyo na mtu mwingine ulipaswa kutulia na kutafakari maisha yako ya nyuma na kutafuta nini hasa kinaweza kuwa sababu ya mimba (mtoto) kuharibika ndani ya miezi saba, sio hivyo tu bali ulitakiwa kuwa karibu na Madaktari wa magonjwa na kike na wale wanaojihusisha na masuala ya mimba na uzazi ili wakuchunguze na kuona kama kuna tatizo lolote lilijitokeza baada ya "mimba" kutoka, huenda ulihitaji kusafishwa mara kwa mara kwa mara...tafadhali fanya mpango ukamuone Daktari wako haraka iwezekanavyo.


Mapenzi na kjn-Linapokuja suala la mapenzi hakuna umri ni utundu, ujanja, kujali na kujituma kwa mtu umpendae. Kwa vile wewe upo kwenye ndoa bila kuwa na mapenzi na mumeo ndio maana ukahisi hivyo ulivyohisi. Kutokana na sifa ulizomiminia ni wazi kuwa unapenda huyo kijana na uko comfy kuwa nae karibu.

Nyumba ndogo kuoa-Kutokana na "hadithi" yote huyu kijana anachotaka kutoka kwako ni pesa au kurushwa/vutwa Ughaibuni na ile kujituma kwake ktk kufanya mapenzi ni moja ya mbinu zake ili avutwe na wewe haraka, lakini wewe ulichelewa kufanikisha hilo akabidi aje na "plan B" .

Baada ya kugundua hakuna juhudi zozote za kuharakisha na kumrekebishia mamabo ya kusafiri, ndio kakujia na "plan B" ambayo alijua wazi kuwa inakuumiza na itakufanya ufanye haraka kuweka mambo sawa ili aje kuishi huko uliko wewe.

Ktk hali halisi na maisha tunayoishi hivi sasa kijana kutafutiwa mke na bibi yake au hata baba yake haipo sana, japokuwa kuna ndugu na jamaa kutaka sana mtu afunge ndoa lakini bado unapewa nafasi ya kuchagua.....huwezi ukaenda kufunga ndoa na mtu kwa vile Bibi kamleta! Anachotaka hapa ni wewe kuwahisha mipango aondoke Bongo.

Huyu kijana angekuwa na mapenzi ya kweli kwako na sio mapenzi ya Ughaibuni angekushauri tangu mwanzo kuwa uachane na huyo Mzee (since u r not in love) ili yeye afunge ndoa na wewe na muende kuishi wote huko majuu.....hapa utaona wazi nini anachokitaka "out of relationship".


Kwa mwanaume, ngono haina maana sana kwao kama sisi wanawake, anaweza kuwa na uhusiano na wewe wa kingono na kuifanya vema kabisa lakini hisia zake za kimapenzi hazipo kwako. Atafanya kila awezalo ili kupata akitakacho.....in ur case ni kubebwa nje ya nchi.

Nini cha kufanya-Achana nae, yaani uhusiano wenu uwe umekufa kuanzia hivi sasa na mchango wa harusi yake usitoe. Najua itakuwa ngumu sana kwavile kijana anakaa Bongo na wewe unaishi huko uishiko. Kata mawasiliano (block mail Add na namba yake). Kuachana na mtu uliejenga hisia za kimapenzi juu yake sio rahisi lakini inafikia wakati inabidi tu uachane nae na kuendelea na maisha yako.

Umekaa kwenye ndoa bila mapenzi kwa muda mrefu sana, karibu miaka nane! Hiyo ni adhabu tayari kwenu nyote, kama nilivyosema hapo awali. Ikiwa umechuma vya kutosha, unamakaratasi ya nchi husika na bado unahisi kutompenda huyo "babu" basi anza mbele kwa faida yake na yako.

Tafuta Wanasheria wanaojihusisha na Talaka na watakupa ushauri mzuri na kutaliki mumeo usiempenda kama ifuatavyo.....lakini hakikisha unabakiza urafiki kwa maana kuwa usioachane na kibabu cha watu kwa fujo na vita na kuua urafiki, keep the friendship na kuwa pake kwa ajili yake akihitaji msaada ili kuonyesha shukrani kwa ulichovuna kutokana na yeye kukuoa wewe miaka nane iliyopita.


Bada ya hapo utakuwa huru ku-date mwanaume kijana yeyote utakaemdondokea na yeye kukufia. Maish aya kimapenzi sio rahisi na mara zote huwa tunafanya makosa ambayo tuki-share kwa uwazi na watu wengine kwa namna moja au nyingine tunasaidia watu wengine wasifanye makosa kama yale tuliyofanya sisi.

Psst-Siku hizi hata wanaume wamekuwa "wachunaji" a.k.a wizi, inaweza ikawa sio kujihusisha kimapenzi na wewe mwanamke bali hata kutaka mfanye biashara ambayo haipo.

Natumai maelezo yangu ukichanganya na ya wachangiaji utakuwa umepata mwanga wa nini cha kufanya. Nakutakia kila la kheri kwenye uamuzi utakao uchukua.

Thursday, 1 January 2009

Ushuhuda wa aliyehisi, akahakiki na kupoteza mapenzi!


"Hi, dada Dinah,Mie ni yule msichana mwenye miaka 28 ambaye niliehisi nikahakiki na kupoteza mapenzi. Kusema ukweli nashukuru sana kwa msaada wa wadau wote nimeweza kufata ushauri wenu na nikawa muwazi kuwa kama huwezi kuniheshimu mimi mkeo basi chukua pete zako na cheti chako cha ndoa peleka huko kuliko na umuhimu uniache mie na watoto wangu nitawatafutia baba atakaeniheshimu mie na watoto wangu, akaona sasa inaweza ikawa soo zaidi ikabidi awe mpole.
Naamini hata kama atafanya atafanya kwa adabu na heshima nisijue. Nashukuru ndoa yangu sasa inakuwa na amani tena kuliko ya zamani na inarudi kwa kasi ya ajabu na hata majibu yake ni mazuri kama akiona amejibu halafu nimebadili uso kidogo basi hapohapo naombwa msamaha na kuambiwa "Samahani mke wangu kama majibu yangu yalikuudhi maana sitaki kukuudhi kabisa" inabidi niwe mpole. Sasa sijajua ni kwa ajili ya kuogopa kuachwa kwa ajili ya mwanume mwengine au ni kaamua tu kujirudi tu kwa kuona haya na aibu?
Na yule malaya wake sijamsikia hata kunibipu kakaa kimya kabisa. Kilichobaki ni mie sasa kurudisha mapenzi maana si unajua tena mwanamke akishapoteza mapenzi na kukinai, najitahidi sana kila nikiwaangalia wanangu najikuta sina jinsi inabidi tu niwahurumie na kupunguza ukali na hasira. Nashukuru sana Dada Dina na Wadau woote mlionisaidia kwa mawazo yenu mbalimbali."

Nilihisi, nikahakiki na kupoteza mapenzi-Ushuhuda!


"Hi, dada Dinah, Mie ni yule msichana mwenye miaka 28 ambaye niliehisi nikahakiki na kupoteza mapenzi.


Kusema ukweli nashukuru sana kwa msaada wa wadau wote nimeweza kufata ushauri wenu na nikawa muwazi kuwa kama huwezi kuniheshimu mimi mkeo basi chukua pete zako na cheti chako cha ndoa peleka huko kuliko na umuhimu uniache mie na watoto wangu nitawatafutia baba atakaeniheshimu mie na watoto wangu, akaona sasa inaweza ikawa soo zaidi ikabidi awe mpole.

Naamini hata kama atafanya atafanya kwa adabu na heshima nisijue. Nashukuru ndoa yangu sasa inakuwa na amani tena kuliko ya zamani na inarudi kwa kasi ya ajabu na hata majibu yake ni mazuri kama akiona amejibu halafu nimebadili uso kidogo basi hapohapo naombwa msamaha na kuambiwa "Samahani mke wangu kama majibu yangu yalikuudhi maana sitaki kukuudhi kabisa" inabidi niwe mpole.

Sasa sijajua ni kwa ajili ya kuogopa kuachwa kwa ajili ya mwanume mwengine au ni kaamua tu kujirudi tu kwa kuona haya na aibu? yule malaya wake sijamsikia hata kunibipu kakaa kimya kabisa.


Kilichobaki ni mie sasa kurudisha mapenzi maana si unajua tena mwanamke akishapoteza mapenzi na kukinai, najitahidi sana kila nikiwaangalia wanangu najikuta sina jinsi inabidi tu niwahurumie na kupunguza ukali na hasira.

Nashukuru sana Dada Dinah na Wadau woote mlionisaidia kwa mawazo yenu mbalimbali."