Monday, 14 December 2009

Binti kaniacha...je nichukue gari langu n.k?-Ushauri

"Habrai yako Dinah,
Hebu tusaidiane hapa, nilikuwa na mpenzi wangu kwa miaka 4 hivi, na nia yetu ilikuwa tufunge ndoa mwaka huu. Baadaye binti alihama mji na kuishi mji mwingine kikazi, hivyo nikawa namtembelea mara mbili kwa mwezi, na nikafanya hivyo kwa takriban miaka miwili.

Kidogokidogo nikaanza kuona tofauti za mawasiliano na sikusita kumwambia, japo sikuona mabadiliko tofauti na hali kuzidi kuwa mbaya, nami nikaendelea kumueleza na kujaribu kuongeza mapenzi kwake ili nisimpoteze.

Baada ya kuona haitoshi nikaamua kumshawishi tufunge ndoa ili awe wangu kabisa na ikiwezekana nimrudishe mji ninaoishi mimi. Kwa kuwa dini zetu ni tofauti tukakubaliana kila mmoja akaongee na familia yake ili tuoane kila mtu na dini yake.

Mimi nikafanikiwa ila yeye akasema kwao hawataki kusikia eti mototo wao anaolewa na Muislam. Basi nikamshauri tuendelee tu kuwa wapenzi kwa muda zaidi kama hawataki tuoane kwa sasa.

Yeye akasema hana jibu maana anahisi anachanganyikiwa tu. Kuanzia hapo hali ikazidi kuwa mbaya mawasiliano ni tabu, sms nikituma asubuhi atajibu jioni, simu mpaka nipige mara 10 ndio ipokelewe nk. Hata nikisafiri kumfuata huko aliko ngono sipewi kwa kisingizio kuwa matatizo tuliyonayo yanamkosesha hamu ya ngono.

Hivyo nikakaa zaidi ya miezi 8 bila ngono japo tunaonana na kulala pamoja mara mbili kwa kila mwezi.Ghafla siku moja baada ya kutopokea simu zangu nyingi sana ndio akanambia alikuwa ananifanyia hivyo visa makusudi ili nimchukie alafu nimuache, maana anaona uhusiano wetu hauto work out as wazazi wake hawanitaki.

Katika kipindi chote hiki cha mapenzi kulikuwa na kusaidiana kwa hapa na pale na niliwahi kumuachia gari atumie. Jee ni haki niendelee kumuachia gari yangu atumie hata baada ya kuniacha?

Jee jamii itaniona nina roho mbaya, na nitajisikiaje siku nikikuta mwanaume mwingine anaye mtomba anatumia jasho langu? Nisaidieni mawazo yenu, kumbukeni kuna vingi nilivyomfanyia kama furnitures, Ada ya Pango etc.

Kindiki"

Dinah anasema:Kindiki asante sana kwa ushirikiano, Hakika kuna wanaume wenye mapenzi ya kweli na wavumilivu sana hapa Duniani. Nimesoma comments na nikagundua kina kaka wamekupa ushauri mzuri ambao natumanini umesaidia wewe kufanya uamuzi mzuri.

Hili liwe fundisho kwa kaka zangu, acheni tabia ya kuwafanyia kila kitu wanawake. Kwani nyie ni baba zao? Kama ni mapenzi mnapendana wote wawili, kama ni ngono mnaifanya wote wawili na kama ni utamu wote mnaupata, sasa inakuaje wewe umfanyie kila kitu yeye na yeye hakufanyii lolote zaidi ya kukuchanganya na Midume mingine?

Sisemi kuwa usimsaide au kumnunulia zawadi mpenzi wako au usimjali kiuchumi kama anahitaji msaada huo, la hasha! Linapokuja suala la kufanyiana mambo makubwa kama kununua Kiwanja, nyumba, gari n.k mnatakiwa kufanya hayo mkiwa na uhakika na uhusiano wenu, kwamba ni wa kudumu/wachumba mnaelekea kufunga ndoa hivyo sio tu unamsaidia yeye bali wewe pia kwani mtakuwa mnaishi pamoja au kwenda kuishi pamoja.

Mf. kwa kulipa pango la nyumba na kununua vitu muhimu kama fenicha, gari n.k itakuwa kwa ajili yenu wote wawili na sio yeye peke yake....sijui mnanielewa? Kuna wanawake ukiwa nao basi utasomesha wadogo zake wote na kujengea wazazi wake nyumba na ukikamilisha yote hayo anakutema vilevile. Wapo wanawake siku hizi wanachukulia wanaume kama ajira, yaani akiwa kwenye uhusiano ndio kapata ajira.

Mimi binafsi nakushauri uchukue Gari lako na uliuze ili kuondoa mikosi na kumbukumbu za huyo mdada. Vingine ambavyo havishikiki achana navyo. Next time unajiingiza kwenye uhusiano hakuna kununulia mtu gari, mtafutie Dereva.

Mungu atajaalia mwaka huu mpya utaanza maishamapya na mpenzi mpya atakae kupenda kwa dhati, kukuthamini na kukuheshimu. Hakikisha hurudii makosa.

Kila la kheri!

20 comments:

vivica said...

pole sn ndugu yangu inauma ukifikiria kuwa ulikuwa unapoteza bmda kwa mtu asyekupenda na naweza kusema hana huruma coz yy kashakuwa mtu mzima wazazi hawawezi kumzuia kuolewa na ampendae namwenye future.kiukweli nikiangalia hapo huyo dada kapata bwana mwingine huko alipohamia maana mabadiliko yalianza yy alipohamia mji mwingine.cha kufanya kachukue gari lako na vitu vyako vingine maana ukimuachia atakuja tumia mwanaume mwenzako,wakati umelitolea jasho ww.sisi wanawake jamani wakati mwingine tunazidi tukipendwa tunaleta nyodo lol!!pole kaka angu,u jus focus na maisha yako usimfikirie yy tena ipo cku utampata atakayekufaa huwezi jua mungu kakupangia nn na anakuepusha nn hapo?

Amos Bwire said...

Brother Kindiki. Kwanza Hongera kwa kuwa bonge la gentleman kwa kumnunulia mrembo wako gari, kumlipia rent and so and so wakati nawe you still hustle. That's real getlemanly. Salute! Pili nakupa pole kwa mkasa uliokupata. Najua inauma. Ok, historia inajieleza wazi hapo kwamba shemeji keshapata mtu mwingine wa kumkuna, hivyo nadhani unahitaji straight answer to your question. Well, napenda kukwambia kwamba ni aibu kwa mwanaume kumpora mali mwanamke anapoachana naye. Why? Listen mdogo wangu, hawa warembo ni mapambo yetu, na moja ya jukumu tulilonalo sie kama wanaume ni kuwarembesha...kuwapodoa... kuwaburudisha...kuwadekeza... kuwabembeleza... aka KUWALEA!Chochote wanachohitaji ambacho kiko ndani ya uwezo wetu TUNAPASWA kuwatimizia... achana na kile wanachotupa in return, that's their friggin' business! Sasa pale itokeapo tunaachana nao, ili society iendelee kututambua na kutuheshimu kama gentlemen basi ni shurti tuwaachie KILA KITU tulichowanunulia... hata kama mnaishi kwenye nyumba moja na wewe ndie mlipa kodi, mkikorofishana basi ni bora wewe mwanaume ndio uhame nyumba na kumuachia huyo mrembo hiyo muishiyo. Yes,I know it's hell, but that's the fact of life. Ukigombana na mwanamke na kumpora vitu hutaongeza chochote zaidi ya kujiona mchemfu na big loser tu... Kwanini usimwachie yeye hilo deni moyoni? Who knows...maybe baada ya kuzuga na huyo mpita njia wake(Alieviparamia baada ya kuviona vyaelea...) atakuja realiaze her fooshness na kuja kukupigia magoti? Na hapo ndipo mapenzi halisi yatapoanza... This shit happens more than often bro. But hey, this is my take on this stuff. Chill bro...you're not the first and won't you be the last.

Anonymous said...

Mdogo wangu, kwanza pole sana kwa ndinga hiyo.Kweli inaumiza sana,lakini usighadhibike inawezekana ni nafuu ya mchukuzi kwani hujui nini kingetokea huko mbeleni.Mambo mengine yanapitia sababu fulani lakini kumbe ni njia ya kuepukana na mambo mengine.

Kwa kuwa wewe ni mwanaume mimi naona hilo ni jambo jepesi kwani walimbwende walioiva kishenzi wapo tosha na kumwaga utaibua mwingine hivi punde.

Kuhusu gari nadhani ulichukue ili usiendelee kuumia rohoni mwako hasa ukijua kuwa huyo mdada ni lazima atachukuliwa na mwingine.Wewe usijali kwani ulimpa si kwa mkataba bali ulitaka tu atumie kwa wakati huo mnavinjaliana. Vitu vingine achana navyo lakini gari beba dogo hakuna usalama hapo.Sioni kama hata yeye ataona furaha kulitumia hilo gari kama si kuliuza.

narudia tena kusema pole dogo.Ningekufahamu ningeku-direct kwa dada mmoja ambaye kweli ungemhusudu sana na kuona ulichelewa wapi kumpata mapema.Ila yeye kungonolewa before marriage sahau hadi kieleweke cha kutundika shela ndipo utauona uchi wake. Huyo Kajitunza hasa.

Nakutakia kila la heri katika mawindo mapya.

Anonymous said...

Pole kwa yaliyokusibu ndugu yangu. Mie naona huyo mwanamke hafai kwa sababu kama alikuwa anaona relationship yenu haitawork kwa nini alikuwa anakuzungusha? Au alikuwa anaogopa kukwambia coz umemsaidia mambo mengi?
Anyway, mie ninachokushauri ni kwamba chukua vinavyochukulika na uachane nae. There is nothing more u can do. Wish u all the best in ur life.

Anonymous said...

pole sana mkubwa!ila ndo hali ya dunia kaka,mi naona haina haja ya kumwachia gari lako na vitu vyako!chukua malizi zako zote hata vijiko maana inaonyesha huyo demu alikua hana nia na wewe wala alikua hakupendi wala nn!kuna usemi unasema;ukimwaka ugali mi namwaga mboga'hivyo amekutosa hivyo na wewe chukua vi2 vyako coz haina maana bora umpe mdogo wako apigie bakola kuliko kumwachia huyo demu.kesho na kesho kutwa utanikuta namtomba mimi huyo demu wako na gari lako natembelea roho itauma mwishoe utajiua bure au kumuua mwanamke kwa hasira.poa bro jipe moyo!

Anonymous said...

pole sana mkubwa!ila ndo hali ya dunia kaka,mi naona haina haja ya kumwachia gari lako na vitu vyako!chukua malizi zako zote hata vijiko maana inaonyesha huyo demu alikua hana nia na wewe wala alikua hakupendi wala nn!kuna usemi unasema;ukimwaka ugali mi namwaga mboga'hivyo amekutosa hivyo na wewe chukua vi2 vyako coz haina maana bora umpe mdogo wako apigie bakola kuliko kumwachia huyo demu.kesho na kesho kutwa utanikuta namtomba mimi huyo demu wako na gari lako natembelea roho itauma mwishoe utajiua bure au kumuua mwanamke kwa hasira.poa bro jipe moyo!

Anonymous said...

Pole sana kaka. Mungu atakupa mwingine utakae mpenda kama huyo, kuhusu mali, ulivyimnunulia inategemea wewe mwenyewe na roho yako unaweza ukasamehe kama unavingine na la kama unaona huna gari lingine ni hilo tu lichukue maana usiumie mara 2, yaani umpendae kakutema na unataabika na usafiri, jamaa yake pamoja na yeye watakucheka. Ila pole sana kaka.

Anonymous said...

Chukua kila kilicho chako hata kama ni mkufu ama Hereni

Bro wewe hapo ulikuwa unainvest in your future vitu vyote hivyo ulimpa ukiwa na lengo la kuinvest for your wife to be! Sasas kama anaona wewe hufai basi anza na kila kilicho chako labda pango lakini furnitures and everything! Unajua huo umekua ni mchezo wa baadhi ya wanawake wasio waaminifu kutugeuza wanaume kuwa daraja fulani! Sasa kama yeye amempata aliye zaidi yako; huna budi wewe kuondoka na vilivyo vyako; mimi hata chupi nilivyonunua nitabeba! To teach her a good lesson!

Wewe ulijituma kwa moyo mmoja kumpendezesha ili nyote mfurahi

Pole sana!

Anonymous said...

Kindiki we wa ajabu kweli!!! Dunia ya leo hii bado unababaishwa na mwanamke???,kwa taarifa yako hana chochote cha maana ambacho huwezi kukipata kwa mabinti wengine wengi tu wa Kiislam. Labda kama unataka haramu!!

Hivi watu wengine mkoje, unahofia "eti watu watanionaje badala ya Allah atakuonaje". We ni Muislam kuzini ni dhambi kubwa sana na kuishi na binti asiye muislam kindoa ni madhambi makubwa vilevile.

Kibinti chenyewe kinakufanyia usanii bado unaking'ang'ania tu hali hiyo umekahonga mpaka gari je ukiwa huna kitu?? - Hebu kuwa Mwanaume kweli na mwenye akili timamu ujiongeze mwenyewe.

Tafuta binti wa Kiislam kama wewe umuoe kwa taratibu za dini yako na umtangulize Allah mbele - OGOPA ALLAH ATAKUONAJE NA SIYO WATU WATAKUONAJE. Acha Madhambi hasa ZINAA.

Anonymous said...

Mlipue tu, malaya huyo...hana mpango wala nini. tena komba vyoote ulivomnunulia, hata chupi!

Anonymous said...

aah mdau chukua chako,kama gari lipo katika himaya yako(vibali na registraa kwa jina lako),basi rudisha mchuma getini huo,utamuachiaje mtu kitu ka hiyo wakati ulikua unamuazima tu,na isitoshe ana mtu huyo,na huyo mtu kwa taarifa yako atakua na uwezo ka wako,wa kumnunulia gari au hata nyumba,si unajua hawa watu huwa wanachagua SUB ambae atalingana na wewe KI UWEZO au hata kukuzidi,mi naamini hio,So RUDISHA MCHUMA GETINI haraka.

Anonymous said...

acha ufala wewe kitu kiko wazi, piga chini huyo demu chukua na gari lako.
umuachie gari lako kwani dada yako huyo?
acha ubwege, nyie ndo mnatufanya madume tuitwe mabwege.

Anonymous said...

Pole sana ndugu! Kwakuwa alishakufanyia na visa mbalimbali, ni vema ukichukua gari na vingine mwachie ili vije kumkumbusha yale aliyokutendea kwani inaonyesha hakuwa na mpango wa kuolewa na wewe ndo maana alianza kukuletea zengwe toka mapema.
Ww chukua gari lako na sahau yaliyopita, wala ucje thubutu kwenda kujibembeleza kwakuwa huyo hana hekima, na ni nyoka huyo.

Anonymous said...

Pole sana ndugu yangu,it seems hata kabla ya kuhama alikuwa na hako katabia,kama aliwahi kukufanyia fadhila zinazolingana na hilo gari achana nae mwachie hilo gari lakini kama hajawahi,mwambie akupatie funguo za gari uanze mbele yeye atanunuliwa jingine na huyo mmewe mpya si kipya kinyemi!

Anonymous said...

hiyo Gari mwachie tu...walahi atajutia baadae tu...

MasterP said...

pole sana ila kuwa soldier mwana.
madem wako wengi wewe mpotezee tu.
sasa hiyo gari ulimpa na kadi yake au ?

kama vipi mwana usione makunyanzi kachukue mchuma huyo hana mapenzi na wewe tena there is no reason ya wewe kumuachia gari yako.kwani uliinunua kwa maboksi ?

nurdin said...

Dah bro k,ckia huyu demu asikuzingue kama vp chukua ndnga lako jkatae hzo huduma ulizo mpa kausha tu cio ishu,kwan huyu demu anaonekana kuna njemba anshtua kijot kiaina,kama ana tru love acngeleta miznguo dni ktu gani,au wazazi ndo wanamchagulia mtu mchumba kwa sas akuna mmependana bac mnatulia pamoja lkn huyo ana mpango m2wangu k,

Anonymous said...

bwire i real contribute man, nakuadmire u sound mtu mwenye uelewa mkubwa, keep it up,

clara said...

mie namhunga mkono kaka bwire kwakweli nimependa comment yako big up

Kindiki said...

Hello!! Nawashukuru sana kwa michango yenu, maana ... Hello!!
Nawashukuru sana kwa michango yenu, maana imenipa faraja, kweli ukiwa na jambo linakusumbua usikae nalo moyoni, liweke wazi ili waungwana watoe ushauri.

Nimependa michango yenu wote kuanzi Vivica, Bwire hadi anony wa mwisho. Naamini nikifanyia mawazo yenu nitapata jawabu.

regards,
Kindiki@gmail.com