Sitaki kumpotezea muda na nimekuwa honest,lakini hanielewi-Ushauri

s"Dada Dinah, ni mara yangu ya kwanza kukuandikia lakini nimekuwa nafuatilia sasa blog yako hii na kwa kweli ni kitu ambacho tunakihitaji sana kwani inasaidia sana kufumbua matatizo mbalimbali ya kimapenzi.

Sasa mimi nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa mbali kwa muda wa miaka mitano hivi, kutokana na mimi kuwa nje ya nchi. Katika kipindi chote hiki tumekuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara ambayo kwa kweli yamesaidia kuweka live penzi letu.

Sasa kwa jinsi mambo yalivyo ukiwa nje ya nchi ni kwamba mambo yanaweza kuwa unpredictable sana, kwani kutokana na mambo yanavyokwenda sioni kama nitaweza kurudi nyumbani hivi karibuni, kwa kuzingatia hilo na pia kwa kuzingatia kwamba umri unakimbia sana mimi nina miaka 31 na mpenzi wangu ana miaka 30 nikaona kuwa itabidi kuchukua maamuzi mazito.

Kwahivyo nikamwambia mpenzi kuwa mimi naona kuwa ni vizuri kama kila mmoja wetu akaamua kumove on ikitokea kuwa atapata wa kumfaa ili isije ikafika kesho na kesho kutwa tukaza kupeana lawama kutokana na ukweli kuwa labda nikarudi nyumbani tukakuta kuwa hatuwezi kuishi pamoja sababu labda wote wawili tumebadilika sana kwani tumekuwa mbali mbali kwa muda wote huu kufikiria kuwa tungeishi pamoja.


Nilipomueleza hivyo mwenzangu aliumia sana na ikawa akinitupia lawama mimi kuwa eti labda nimepata mwingine na ndio maana naamua kumtosa, lakini kwa ukweli ni kuwa mimi nilikuwa naangalia picha nzima kwamba tusiwe tunapotezeana wakati kwani umri wetu ndio unakimbia.

Kwa jinsi mwenzangu alivyo react ni kwamba hakubaliani na hilo na kwakweli ameumia sana kitu kilichonifanya nijidoubt labda uaamuzi niliochukua si sahihi kwani imefikia mahali inaniumiza kichwa sana. Ukweli ni kuwa I do care for her lakini inabidi mara nyingine uangalie jinsi hali halisi inavyokwenda katika maisha.

Sijui wewe na wadau wengine mnaonaje kuhusu swala hili, naomba msaada na mawazo yenu wote. Ahsante sana na samahani kwa mail ndefu kama hii, tuendelee kuelimishana katika swala zima la mahusiano"

Dinah anasema:Asante kwa kuniandikia, nadhani kosa ulilofanya hapa ni kufanya uamuzi ulioegemea upande mmoja tu (upande wako peke yako) bila kumuhusisha yeye (mpenzi wako), umefanya uamuzi kisha ukampa matokea....yaani hamkuzungumza na wote wawili kukubaliana kumaliza uhusiano au kutafuta namna nyingine ili uhusiano wenu uendelee.

Mwanamke yeyote mwenye mwanaume Ulaya anatarajia Big, sasa unapomuibukia na kumaliza uhusiano ktk mtindo huu, kidogo inakuwa ngumu kuamini, kuelewa na kukubali.

Kumbuka mko kwenye uhusiano na kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji, inawezekana katolea nje wanaume wengine wengi tu kwa ajili yako kwa vile aliamini kuwa siku moja mtakuja kuishi pamoja.

Mimi nakushauri, uzungumze nae na umpe picha kamili ya maisha ya huko uliko. Kwasababu, watu wengi hapa nyumbani hawajui ni kiasi gani maisha yanaweza kuwa magumu huko Ughaibuni (ugumu interms of kutoruhusiwa kutoka nje mpaka wakurudishie kitabu chako, unaweza ukasubiri milele*).

Ukiweka wazi ni nini hasa kinakuzuia wewe kusafiri au hata kurudi nyumbani kwa sasa na hujui lini utaweza kufanya hivyo, akikuelewa ndio uanze kuzungumzia suala la uhusiano wenu. Hakikisha unampa nafasi yeye kukuambia msimamo wake na nini hasa anataka out of uhusiano wenu....msikilize kwa makini. Kisha mpe maelezo kutokana na matarajio yake au atakayo out of uhusiano huo.

Weka kila kitu wazi, kama kuna uwezekano wa yeye kukufuata uko nini afanye na kama hakuna mwambie kwa uwazi kabisa kwanini haiwezekani, kwa sababu kibongobongo wapenzi hutegemea sana kupandishwa majuu lakini hawajui urahisi na ugumu wake.....sasa mpe hali halisi.

Hakuna uwezekano wa kukufuata na huna mpango wa kurudi Bongo sasa:
Mwambie hali halisi kuwa, umri aliofikia wanawake wengi hupenda kuanza kujiandaa na ndoa, kuanza familia n.k. na wewe ungependa kufanya hivyo lakini unasikitika kuwa hutoweza kutimizia hayo kutokana na umbali na mambo yanavyokuendea huko uliko. Muombe radhi kwa kumpotezea muda kwani mipango haikuwa kama ulivyotarajia.

Akikubaliana na wewe, ahidi kuendeleza urafiki na wasiliana nae kila upatapo muda. Akiendelea kutokukuelewa na kukutupia lawama then punguza mawasiliano kama sio kuyakata kabisa.

Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
Mmmmmmmmm pole sana dada.Lakini nakupongeza kwa uwazi wako licha ya kumuumiza jamaa yako.

Kwa kweli mimi naona kuwa muwazi ni jambo muhimu licha ya kwakmba labda katika kumwambia mwenzio hukuchukua tahadhari namna ya kuwasilisha hoja yako.Mimi naona hoja yako ni yamsingi,ila ulihitaji umakini wa namna fulani kuwasilisha.Kama anakupenda lazima aumie tena uko nje basi anaona wewe unamzingua tu ulipata mtu ingawa sivyo.

Nadhani kwa msingi wa wewe kutorudi Bongo ndiyo kunakupa mstakabali wa kuachana na jamaa kwa kweli sababu si nzito sana kama ungekuwa na namna nyingine ya kumfikisha jamaa hapo ulipo au wewe kwenda huko mkamalize mambo,lakini najua bila shaka wewe unasita kutumbukiza mguu huko kwa sababu ya the so called makalatasi!! Dada mfanyie mpango mwenzio huyo aje kusoma huko uliko kama uko vizuri ili muweze kumaliza mambo yenu.Au mpe mwaliko wa aina fulani aje kama kweli wewe unampenda jamaa yako.Kama umeona mwezi na wewe labda ndiyo sababu unamtema jamaa bila kuangalia upande wa pili wa shilingi.

Dada unajua unaweza kumuua mtu hivihivi kwani amekusubuli miaka yote hiyo na bado umwambie no way out take your charge? Je kuna juhudi zozote umewahi/mumwewahi kuzifanya ili kufanikisha azima yenu?

Fanya chini juu kumleta jamaa huko uliko kama hujajichanganya huko ukawa umeishapata jamaa mwingine kwani kila jambo lina jambo lingine nyuma yake.Kamaulivyosema umri unakwenda hivyo mfanyie jamaa mpango.Hivi wewe ni lazima tu uishi huko ughaibuni?Utakuja kumkumbuka jamaa huyo ukimpoteza.Najua hata mimi niko ughaibuni kwa hiyo story za watu wa ughaibuni nazijua kwa marefu na mapana.Kila la heri dada.
Anonymous said…
naomba nikuulize swali we kaka ungekuwa ww umemsubiri mtu kwa mda wote huo halafu akwambie hayo maneno karahisirahisi tu ungekubali?ukweli usingekubali wala kumuelewa huyo mtu na ndivyo ivyo ivyo ilivyotokea kwa huyo dada na hata ingekuwa mm nisingekuelewa,hayo maswala ilibidi umweleze mwanzoni kabisa wakati unaondoka bongo na sio ss.kiukweli umeshampotezea muda na inaonyesha huna mapenzi ya dhati kwake na ni muharibifu tu,
hivi ww unajua uchungu wa mapenzi,umeshawahi kutendwa au kuachwa ww?tena bila kosa wa sababu za msingi?huyo dada anakupenda sn ndo mana kaweza kuvumilia mda wote huo halafu leo umwambie habari zisizieleweka kwa kweli utapata laana(what goes around come around)usichezee moyo wa mtu kaka hajaumbwa kwa chuma huyo wa plastik ni binadam km ww.chunga sn na fanya maamuzi ya busara zaidi
Anonymous said…
Pole sana bro.sometimes mambo yanatokea.but swali lakujiuliza kwanini tuwatese wanaotupenda?maumivu ya mapenzi yanauma sana.je utajisikia vp uje upate habari kuwa mpenzi wako amejitoa uhai sababu ya uamuzi wako.kama kweli unampenda mfanyie safari aje kuishi nawewe huko uliko coz uko kwenye sayari hii hii.plz tengeza mambo kabla ujakuja kujuta.from ur bro mustayoo@yahoo.com
Anonymous said…
Wewe kaka mimi sikubaliani na wewe katika swala hilo,si uamuzi sahihi kwa mtu unayempenda labda kama mapenzi kwake yameisha ila kama mnapendana kweli hautadiriki kuchukua uamuzi huo.mwenzio amekuvumilia for five yrs leo eti unasema atafute mtu atakaye pendana nae awe nae.yeye anakupenda wewe labda umwambie humpendi tena lakini km mtu unampenda hata iweje utarudi ili uwe nae.
Anonymous said…
Kwa kweli sidhani kama uamuzi ulioufanya ni sahihi given that hakuna ambapo mlikosana... kwa kweli jaribu kuvaa viatu vya mwenzako, unamsubiri mpenzio kwa miaka mitano na uko tayari kufanya chochote kwa ili mradi mapenzi yenu yaendelee then anakuja kukudiappoint... Mabaya sana..
Ninachokiona mm hakina tofauti na cha huyo mpenzio, lazima umepata mtu wala tusidanganyane hapa wewe kubali makosa na umueleze unamuacha for another lover.. lakini fahamu what goes arround comes arround so get prepared.
Unknown said…
Mapenzi ya kweli hayana muda wala umbali keep it going brother!

Deo, DSM
Nuru said…
Lakini mi sioni kama huo umri umeenda sana kwamba ndio kigezo cha kumuacha mwenzio ukizingatia amekusubiria kwa muda mrefu we unafikiri kawakataa wangapi leo ndio uchukue huo uamuzi embu assume ungekuwa wewe ungejisikiaje kwani usipende kutenda jambo kwa mwenzio pasipokuliangalia je ungetendwa wewe hivyo ungeafiki mi nafikiri kama kweli unampenda we jitahidi tu urudi huku mtimize mipango yenu yote mliyoahidiana.
Anonymous said…
Napenda kuchangaia hii mada kama ifuatavyo, kwanza ningependa kujua ni kitu gani kinakufanya ushindwe kurudi nyumbani hivi karibuni. Umeishi ughaibuni sasa kwa miaka 5 ni dhahiri kuwa unafanya kazi na unakipato cha kukuwezesha kuishi huko ughaibuni. Kama kweli unampenda mwenzio na hutaki kumpotezea muda kwa nini basi usiombe likizo ukarudi nyumbani ukamuoa mkeo halafu ukafanya mipango ya kakaa naye huko ughaibuni, yote hayo yanawezekana labda tu uwe unaishi huko ughaibuni kwa magendo. Ni vema hapa ukawa muwazi sema umeshampata bibi wa kizungu huko anakuweka ndani maana watu wengi wanaokuja huku ughaibuni wakiona hawataki kurudi nyumbani na deal zote zimeshindikana anamtafuta bibi wa kizungu anamuoa. kwa kweli hapa unampotezea mwenzako muda tumeweza sisi wanafunzi kuwaleta wake zetu huku ughaibuni wewe unashindwa nini?????????
Anonymous said…
Hapa wadada najua hamtachangia chochote lakini angekuwa mwanaume ndiye anasema hivyo tungeona cha MOTO.

Kwa ujumla wewe dada huna huruma kabisa.Yaani mpenzio kakungoja kwa miaka mitano yote leo unakuja kusema eti hutaki kwenda Bongo hivyo kila mtu ajue ustaarabu wake? Tuambie tu kwamba tangu umekuwa huko ughaibuni ulishaibua dume lingine. Unashindwaje kufanya chini juu umsaidie huyo mpenzio aje huko kaama wewe hutaki kwenda bongo?

Yaani hata ningekuwa mimi ningeudhika na kuchanganyikiwa sana kwa sababu subira yake yote kimwana unaolewa naye ,punde tu unageuka eti nisimpotezee muda,mbona tayari umempotezea muda?

Mimi nakushauri fikiri na tafakari kama hakuna jamaa limekugiribu huko ughaibuni rejea kwa mpenzio tafuta njia ya kukutana na mpenzio huyo ili uepuke kumuumiza sana na yamkini umwepusha na gadhabu na maamuzi anayoweza kuchukua ambayo si sahihi.

Mara nyingi imeonekana wanaume ni wasanii sana na kukacha wadada.Lakini leo ukurasa umefunguliwa mwingine kabisa.Najua utamu wa maisha ya ughaibuni ingawa ni karaha tupu.Tafuta mbinu ya kumleta mpenzio huku ughaibuni acha kutupa porojo zako kama siyo ulishadakwa na jamaa lingine.
Anonymous said…
Kaka huo umauzi uliouchukua wa kumwambia mwenzako kuwa kila mtu ashike ustaarabu wake sio mzuri na lazima aone kuwa umepata mwanamke mwingine thats why unamwambia kila mtu ashike ustaarabu wake. Kiukweli kama ulikuwa unajua kuwa hautorudi tena Tz ni bora ungemwambia mapema ili ajue ustaarabu wake, sasa miaka mitano imeshapita na age yake imeshakwenda sasa ana miaka 30 na inawezekana alikuwa anakataa wachumba wanaojitokeza kwake kwa ajili yako. Na sasa umri wa kupata mchumba kwa haraka umeshapita na kwake kupata mtu wa kumwambia atamuoa ni ngumu sana kutokana na umri wenyewe. Kiukweli umempotezea muda wa kutosha halafu unakuja mumcheat. Sio fresh hivyo ulivyomfanyia.
Anonymous said…
ulikuwa wapi kumwambia miaka yote hiyo? tuwe na heshima ya mapenzi kwa kweli inasikitisha sana mtakuja kusababisha watoto wa watu wanywe sumu
Anonymous said…
Pole sana ndugu yangu kwa matatizo uliyonayo au kwa maamuzi mazito uliyoyafanya. Kuna utofauti wa maumivu kwenye break-up kati ya anayeanzisha na yule anayeambiwa kuhusu break-up. Hata ingekuwa msichana ndo ameanza kukwambia wewe, nawe pia ungeumia kama yeye alivyoumia. Ila bado hujaweka wazi tatizo ni nini, umri unaenda? Mbona mna miaka 5 pamoja na hukuliona hilo, dada wa watu anaumia kwa kuwa tayari umeshampotezea muda. Kwa kuwa wewe ndio muamuzi, basi chochote ulichokiamua kitakuwa ni kwa manufaa yako na sidhani kama unamfavour mwenzio! Labda useme sababu nyingine ya kutengana ndio unaweza kupata ushauri wa maana!
Gulam said…
Kumbuka penzi la kweli huwa halifi hata likifa hal... Kumbuka penzi la kweli huwa halifi hata likifa haliozi na likioza harufu yake huwa nzuri ya kuvutiaaa!!!!!! kaka unamnyanyasa mwenzio kisa uko ughaibuni? huyo dada ana penzi la dhati kwako ndio maana anakuvumilia muda wote huo! please huyo ndio mwanamke wa maisha yako!
Anonymous said…
ndugu ingawa umekuwa wazi lakini kama ni maisha unatafuta kipi kikuzuiacho kuja mfunge ndoa kam mke na mume na mapendana na ikibidi mkaishi wote nje...miaka mitano kwenye relation ni kama ndugu,kwani kitu gani kinachowazuia kufunga ndoa??? mimi sikushauri muachane tambulishaneni kwa wazazi wenu mmalize mambo ,ndugu huyu unayetaka kuachana unamfahamu udhaifu wake,in and out na yeye anakujua in and out kwwa nini kwenda kustruggle kuanza new relation kuanza kumsoma mtu mwingine huoni unapoteza muda mara mbili zaidi, unaweza ukaanza maisha na mwingine ukakutana na bomu ukatamani urudi kwa huyu uliyemuacha na tayari ni too late...fikiria mara mbili ndugu
fatma said…
umeshampotezea muda na tayari umeshamuathiri mwenzio kisaikolojia.usicheze na mioyo ya watu hasa ktk mapenzi,u can kill somebody.
sometimes waweza fanya uamuzi fulani kukuhusu,but take time and look if ungekuwa wewe,hw iz it burns inside your heart.hapo unapigia mstari ule usemi usemwao na wengi kwamba mtu akienda nje ya nchi basi yule mpenzi wake wa bongo ndio basi tena anakuwa ameshamwagwa.
But ukweli sio hivyo,kinachohitajika ni mapenz ya kweli na future ipo popote,jaribu kuwa mstaarab ndugu.
mimi nahisi hujakurupuka kufanya hayo maamuzi,but i can thnk that ushapata kijimwanamke kingine kinakupeleka puta ukamsahau yule wako wa ukweli uliyemuacha bongo.
I conclude;
HUNA MAPENZI YA DHATI,SIO MUAMINIFU,MDANGANYIFU,HUNA MOYO WA HURUMA NA PIA NI MSALITI MKUBWA WA MAPENZI.
Anonymous said…
Ndugu yangu kuwa wazi mambo yako ya karatasi yako vp?tuelezane ukweli tu tukupe ushauri zaidi wa kukusaidia,mwenzako pengine humwelezi situation yako,
Unknown said…
Jamani kaka hebu jiweke kwenye nafasi ya huyo dada ungekuwa wewe ingekuwaje? ni maamuzi magumu sana mkiwa kwenye mahusiano na hasa ukizingatia mmekaa 5years. Fikiri tena halafu ndo uamue umri si hoja ya msingi hata umbali pia. umeshampotezea mwenzio muda. nakushauri kaa chini then ndo u make proper decision
Anonymous said…
Inawezekana unafikiria alikuwa anakusubiri ila yeye hata! Usidhani kila mwanamke anauvumilivu wa mwanamme. Mchunguze huyo mwanamke utampata anajaribu juu chini aachane na mambo ya kale na huyu mwanamme. Kuna watu huwa ni kama nyasi iliyokauka wanafaa watupwe motoni. The only pain affecting that woman is that she is feeling a negative power pulling her back. Trust me she wants with all her heart to fall in love again, with ANOTHER MAN. I wishh her all the very best in finding her new love. I really do!