Tuesday, 20 October 2009

SMS kwa jina la kike mhusika Dume-Ushauri!

"DEAR,
MImi ni kijana mwenye umri wa miaka 24, nina mpenzi ambaye hadi sasa nimekuwa nae kwa mda wa mwaka mmoja. Mpenzi wangu huyu ni msiri sana linapokuja suala la matumizi ya simu. Kwenye simu yake inaonyesha anamtu mwingine ambae anaishi Mtwara na huwa wanawasiliiana mara kwa mara, lakini kila nikimuuliza ni nani huyo? yeye anasema kuwa ni rafiki yake na ni mwanamke.

Lakini katika uchunguzi nilioufanya nimegundu mtu huyu ambaye ni rafiki yake ni Mwanaume kwani amekuwa wanawasiliana kwa sms, akitumiwa tu sms husoma na kuzifuta haraka sana. Sasa tarehe 16/9/2009, Tulitoka na kwenda Biashara Club kwa ajili ya msosi, Mpenzi akatoka kidogo na kwa bahati mbaya akawa ameissahau simu yake mezani.


Mara sms ikaingia, kwa sababu nilikuwa na wasiwasi na mawasiliano yake ya mara kwa mara nikaamua kuisoma ile sms ikisema wakutane mda wa saa mbili usiku, wakati ujumbe umeingia ilikuwa ni saa mmoja usiku.


Namba ya huyo mtuma ujumbe imetunzwa kwenye simu kwa jina la MASA, kutokana na sms niliyo soma na kupata uhakika zaidi ambao nilikuwa nautafuta niliamua kumwambia mpenzi kuwa na hitajika nyumbani kwani kuna tatizo, sikuweza kuendelea kuwepo pale, sasa ili nijue ukweli wake nifanye nini?
Naomba ushauri wako dada.
it's me Hassan"

Dinah anasema: Hassan, pole kwa mkasa huo. Hiyo ni tabia ya watu wengi ambao sio waaminifu, wanakuwa na wapenzi nje ya mahusiano yao na kutunza mawasiliano ya simu kwa majina ya ambayo sio halisi. Mf- Kamani mwanamke watatunza kwa jina la kiume na kama ni wa Kiume basi jina litakuwa la kike.

Jambo muhimu ni kwenda kufanya vipimo ili kujua kama uko huru kutoka HIV! Kwani hali ni mbaya sana na inatisha.

Katika hali halisi unapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi huitaji kuwa na siri, kila kitu unachodhani ni muhimu mwenzako kujua basi utaweka wazi jambo husika, hata kama mtu huyo anampenzi mwingine kwa sababu nyingine labda za kimapenzi au kiuchumi (wapo watu wanakuwa na wapenzi 2, mmoja wa kimapenzi na mwingine kwa ajili ya pesa) pia unatakiwa kuweka wazi hilo ili huyo anaetaka uhusiano na wewe aweze kufanya uamuzi wa busara.

Nasikitika kusema kuwa mpenzi wako sio mwaminifu na kuna uwezekano mkubwa anakuchanganya wewe na mwanaume mwingine. Ni vema kama utamueleza mpenzi wako ukweli wa nini kilichokufanya uondoke usiku ule mlipokuwa nje kwa ajili ya chakula, muulize kuhusu huyo Jamaa anaewasiliana nae na kama wanangonoana n.k.

Kisha msikilize anasemaje na umwambie uwazi kuhusu msimamo wako Mf- hutaki kum-share yeye na mwanume mwingine, hupendezwi na tabia yake ya usiri. Sasa kama hakuna kinachoendelea na huyo jamaa wa SMS (mana'ke inawezekana njemba inamtaka tu lakini hajafanya nayo ngono)....mwambie Demu abadilishe tabia yake ili uweze kumuamini.

Kama walikwisha ngonoka, ni wazi kuwa mdada huyo hakufai hivyo basi achana nae na subiri kupata binti mwingine atakaejiheshimu nakuheshimu uhusiano wenu na kukuthamini wewe kama mwanadamu.

Kila la kheri!

4 comments:

Anonymous said...

Mkabili na ukweli huo na umweleze msimamo wako; ikiwa huna mpango naye basi achana nae ; lakini ikiwa unaona anafaa kuwa mwenzi wa maisha yako muweke bayana kumweleza thamani unayompa na mipango yako na kumwomba ajirekebishe kwa faida yenu wote na pia umpe nafasi ya kujieleza ni kwa nini hilo limetokea! Nakutakia kila la kheri

Anonymous said...

Huna haja ya kumfuatilia sana huyo mrembo wako.Huyo si mke wako hata kidogo anao uamuzi wa kujikita kwa mtu atakayempendezesha zaidi.

La muhimu wewe chukua hatua nyingine ya kukimbia kama unajua hilo linakuumiza.Nadhani kama na wewe huna jambo jema kwake unalolipanga kwa maisha ya baadaye mimi naona wote pamoja naye mko gizani sana.Vijana wengi wametanguliza mapenzi kuliko maisha yao ya kujiandaa na kupangilia mambo ya kuoa.Wanaume wamekuwa kama bubu hawataki kuwaambia wasichana wao ukweli juu ya nini wanakitafuta.Huwatamani wadada kuwakamua tu.Kwa hiyo kama huyo dada naona wewe huna kauli ya maana hana sababu ya kukuzingatia wewe.

Ukweli ni kwamba wadada wengi wanahitaji maisha na wala si kukamuliwa tu hivihivi.Ukiona mdada umemkamua usifikiri amependa sana ila anajaribu tu kukuridhisha ili yamkini uwe na uamuzi wa dhati kupanga naye maisha ya baadayelakini vijana mnazidi tu kuwarubuni mabinti za watu.

Wewe mwanaume mwenzangu huyo dada achaneni naye kama hujamwambia jambo lolote la maana.Tafuta mwingine ambaye hana mipango yoyote kama utampata.

nakutakia kila la heri na epuka kugombana na binti huyu.

Nobody said...

huyo si mwaminifu kabisa na kuna sababu nyingi tu zewazavyo kupelekea mtu kutokuwa mwaminifu.
utoto,tamaa ya fedha,uhuni ,nk fuata ushauri wa anon wa juu hapo.ukiona hakuna mabadiliko basi usisite kusonga mbele ndugu.siku hizi kuna magonjwa mengi asije akakuangamiza

Anonymous said...

Yaani haina aja ya ushauri kaka!Umeshasema jina la kike mhusika ni dume......Kama unabusara za kutosha utakuwa ushajua unapigwa dude...Kama hamna kitu kwani aweke jina la uongo?Ni hayo tu....Fanya uamuzi ulio sahihi kulingana na moyo wako na akili yako!