Nimetambulisha mchumba via simu, sasa hapatikani-Ushauri

"Nina msichana wangu nasoma naye chuo kimoja nje ya nchi na tumekuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi cha miaka miwili sasa. Nampenda na yeye anaonyesha dalili zote za kunipenda mimi. Kila kitu nikimwambia huwa ananielewa haraka kitu ambacho ni muhimu sana kwangu.

Mwezi huu wa Tisa amepata likizo ya kurudi Tanzania, ndipo nikachukuwa nafasi hiyo kutaka uchumba wangu ujulikane kwa wazazi hivyo nikamuelekeza kwetu na akafika. Mimi nikawatambulisha wazazi wangu kwa njia ya simu kuwa huyo ndie chaguo langu yaani ndie atakuwa mke wangu baadaye.

Wazazi waliniunga mkono!! ila kuna kitu nashindwa kukielewa naomba ushauri wenu, tangu mpenzi amefika kuna line ya simu anaitumia ambayo ina tatizo la kutopiga huku nilipo hata kutuma message. Yaani akitaka kupiga au kutuma message hadi atumie namba ya mama yake au ya dada yake sasa sometime ikitokea watu hao wanakuwa na shughuli zao au hawapo ndio hatuwasiliani kabisa hadi mimi nimpigie.

Nilimwambia mchumba abadilishe hiyo line akaniambia atabadilisha, sasa ni Mwezi umepita line bado anayo ileile na sidhani kwamba hana hela. Je hapa kulikoni? naomba ushauri wenu wadau."

Dinah anasema: Hongera sana kwa kuchumbia! Asante kwa mail na uvumilivu wako pia. Tatizo lako ni kutojiamini hali inayopelekea wewe kushindwa kumuamini mwenzio. Natambua ugumu wa kuwa na mpenzi mbali na wewe, lakini ukiwa na ukosefu wa kujiamini inakuwa even harder!

Ni kweli mawasiliano kwa baadhi Network Bongo huwa magumu kwani ni lazima vyombo hivyo vya mawasiliano kuwa na "ubia" na vyombo vya mawasiliano vya nchi husika ambayo wewe unaishi ili kufanikisha mawasiliano(nilipata usumbufu huo nilipokuwa nawasiliana na mtu aliyekuwa akitumia Zantel). Hivyo hili lisikupe hofu sana au hata kumfikiria mwenzio mabaya.


Huenda suala la yeye kubadilisha mtandao/line ni rahisi sana kulifikiria, lakini tambua kuwa huyu Binti kaenda nyumbani kuonda ndugu zake baada ya muda mrefu kuwa mbali nao, wewe ulikuwa nae kila siku na baada ya muda huo mfupi utaendelea kuwa nae.


Kibongo-bongo, unapokwenda nyumbani kila mtu anapenda ku-spend muda na wewe kwa vile hawajakuona kwa muda mrefu hivyo inatokea kuwa unakuwa busy sana na shughuli za kifamilia na suala la kubadili nambari ya simu ili kukuondoa hofu wewe mpenzi linakuwa la mwisho kwani anajua moyoni anakupenda na anawasiliana na wewe kupitia Mama na ndugu zake wengine, ktk hali halisi hii ingekufanya uwe na Amani myoni kuwa yupo na watu unaweza kuwaamini, imagine angekuwa anawasiliana na wewe Via rafiki au kibanda cha Simu?

Ni matumaini yangu ulifanyia kazi vema maelezo ya wasomaji wangu. Naamini Mpenzi sasa amerudi na kila kitu kiko sawa, nawatakia maisha mema yenye amani na furaha na Mungu awajaalie mfunge ndoa na kuishi maishamarefu ya ndoa.

Pamoja na mambo mengine mengi Uamininifu ni nguzo muhimu ili kuwa na uhusiano bora wenye kuzaa ndoa thabiti.
Kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
Hapo naona ni wasiwasi wako tu.
Ukizingatia yuko likizo kwa muda mfupi baada ya hapo atarudi huko muwe pamoja. Tatizo la laini yake umesema ni kutopiga wala kupokea message huko ulipo tu. Ukimpigia na mawasiliano na watu wengine huko Tz haina tatizo lolote.
Mie naona anashindwa kuibadili kwa kuhofia usumbufu wa kuisambaza ile mpya kwani ukibadili laini inakubidi tena ufanye kazi ya kuisambaza ili watu wako wayajue mabadiliko hayo. Japo inawezekana kununua laini nyingine ambayo itakuwepo kwa ajili yako tu; Ni wazi kwamba ukimhitaji hutompata kwa muda mwafaka sababu itakuwa mara kaweka laini hii kwa ajili yako mara kaweka laini ile iliyozoeleka Tz. Hapo haitakuwepo tofuti na hiyo ya kutumia laini ya ndugu zake. Unaweza kuvumilia ktk kipindi hicho cha likizo muendelee kuwasiliana hivyo. Pia waweza kumuuliza kwa upole sababu ya kutobadili naamini atakupa sababu zitakazokuridhisha.
Ni hayo tu.
2mJ.
Anonymous said…
Mimi naungana na msemaji wa kwanza kuwa sioni tatizo kama unaweza kuwasiliana nae kupitia ndugu zake.Kuwa mvumilivu ndio mambo ya mahusiano na uchumba hayo acha kumhisi mwenzio vibaya.
Anonymous said…
Wewe jamaa yangu! pamoja na kwenda shule bado una utotoutoto tu?

Yaani simu tu ni tatizo wakati ukimtafuta unampata kirahisi.Unapotaka abadili laini huoni ni gharama na yeye yuko likizo kwa muda tu? mbona unashindwa kuwa mvumilivu na kuwa na busara?

Hebu vuta subira kwanza si atakuja huko hivi karibuni?halafu kama na yeye anatembelea hii blog akaona kuwa umejitundika humu kumtafutia ushushushu utaingia matatani akijua kuwa wewe si mtu mvumilivu umejaa mashaka ya kitoto tu.

Mambo ya mahusiano na uchumba yanahitaji uvumilivu mkubwa siyo kila wakati kufikiria kinyume tu.Aidha umeyaparamia ungali bado hujakomaa.Kaa fikiri kwanza acha kuweweseka juu ya mpenzio eti kisa laini ya simu du!!
Anonymous said…
Wewe hufai kuwa mchumba au mme. Yaani muda mfupi tu umeanza kusaka ushauri? Utahimili kweli mikiki ya kwenye ndoa! Kuwa mwanamme tafadhali.
Vumilia. Kama unaona hujiwezi bora umwache dada wa watu.
Anonymous said…
Ni sawa kabisa wayasemayo wadau,kwani hata mimi wangu yuko hivyo ila simdhanii chochote kwakuwa tunaaminiana.Kitu cha kwanza munatakiwa kuaminiana ili kubolesha mahusiano yenu.kama hamuaminiani mahusiano yenu yatakua ya wasiwasi.Kitu cha kwanza katika mapenzi ni UPENDO Cha Pili ni UAMINIFU na cha Tatu ni MAWASILIANO YA KARIBU Cha nne UVUMILIVU-ni hayo tu ndugu yungu
KWA USHAURI ZAIDI: dasseph@yahoo.com or 520-881-9019
chaoga said…
inategemea na mtandao gani yupo, upande wa sms mie namtetea lakini kwenye kupiga simu nakataa mitandao yetu upande wa kupiga simu hamna kikwazo kabisaa na kama ushamwambia abadilishe namba na mpaka leo hajabadilisha basi kuna tatizo huko aliko angalia bwana asije akawa kakutana na binamu zake....!!!! TAFUTA NDUGU YAKO YEYOTE AENDE AKAMTEMBELEE AKIWA NA LAINI MPYA AMKABIDHI TUONE
Bennet said…
Mimi namshauri awasiliane na kitengo cha huduma kwa wateja katika kampuni hiyo anayotumia line yao, na wao watamsaidia mara moja hilo walasioni kama tatizo la kukuweka roho juu
Anonymous said…
km ni voda aje tutamsaidia kwani hayo matatizo yapo sn tu