Saturday, 3 October 2009

Namuonea huruma Soon to be Ex Wife-Ushauri

"Heloo dada Dinah, pole sana kwa kazi. Nimeona nikutumie hii mail kwa ajili ya ushauri.
Tatizo langu ni kwamba dada, mimi ni mdada wa miaka 24 nimeajiriwa. Huwa napenda sana kutembelea blogs mbali mbali na kuchat katika pita pita hizo nikakutana na mtu (Mwanaume) tukawa tunawasiliana aliniambia kuwa ana mtoto ila mama wa mtoto wametengena na yuko nje ya Tanzania kaolewa na Mwanaume mwingine na wamezaa.

Tuliendelea kuwasiliana kwa simu na kuchat kupitia internet hadi ilipofika siku tukaonana. Baada ya kuonana siku ya kwanza tuliendelea kuwasiliana kwa simu na pia kupanga miadi ya kuonana tena na tena hadi siku aliponitamkia kuwa anapenda niwe mpenzi wake.

Kiukweli nami pia nilimpenda ila kwa wakati huo nilikuwa kwenye matatizo na mpenzi wangu wa awali so nikaona haina haja ya kuendelea kuteseka wakati tayari kuna mtu anaonesha kunipenda kwa dhati.Basi tukawa wapenzi.


Tatizo lilianza pindi mpenzi wangu wa awali alivyogundua kuwa nina ukaribu na huyo mjamaa ambae kumbe anamfahamu. Siku moja akanipigia na kuniambia kuwa yule mtu ameoa tena kwa ndoa ya Kanisani na wanaishi wote na mkewe, nikamwambia mbona mimi ameniambia tofauti.

Basi ikabidi nimbane kweli huyu jamaa mpya nae akaniambia kuwa ameoa ila yeye na mkewe wana matatizo ya muda mrefu sana ambayo sio rahisi kusameheka na isitoshe huwa hawalali pamoja! na anachosubiri yeye ni ruhusa ya kupeana Talaka kwani swala lao limeshafika mbali.


Kwakuwa alikuwa ananionyesha mapenzi ya dhati, nikawa niko tayari kuendelea naye hapo nakiri kweli nilikuwa mdhaifu kwani nilistahili kuachana naye baada ya kugundua ukweli lakini tatizo ni kwamba tulishakula kiapo kuwa hatutaachana kwa namna yoyote ile.

Hadi sasa tuna muda wa miaka miwili. Ushauri niutakao ni je, niendelee na huyu mtu au niachane naye??? kwanini nataka ushauri wa hivyo ni kwa sababu nafsi inamuonea huruma sana mkewe ingawa kiukweli anaonekana wazi kuna kitu kikubwa alimkosea mumewe kwani mara nyingi huwa anamuomba msamaha naona hayo kwenye simu yake na pia huwa anapiga na huyu kaka huwa anaweka loudspeaker nami nasikia.


Ameahidi pindi atakapotengana na mkewe yuko radhi kunioa, hilo pia nahofia kwa kuwa sijui namna ya kuieleza familia yangu kwani itabidi niweke wazi kuwa alikuwa mume wa mtu kabla hawajasikia kwa watu.

Kwetu mimi ni mtoto wa pekee wa kike. Samahani kwa mail ndefu, na sijui kama nitakuwa nimejielezea vizuri ukanielewa ila kama utakuwa na maswali ya kuniuliza ili uweze kunisaidia sawa unaweza kuniuliza nitakuwa tayari kujibu ili nisiendelee kuteseka.

Asante sana, kazi njema.
Lizzy"

Dinah anasema: Mdogo wangu Lizy, mtu akishindwa kuwa mkweli mwanzoni kabisa mwa uhusiano ni wazi kuwa daima hatokuwa mkweli kwako. Kutokana na maelezo yako huyu Jamaa alikuwa anam-cheat mkewe via internet (wako wengi sana hawa viumbe wake kwa waume wanao abuse maendeleo ya mawasiliano).

Ni wazi kabisa wakati unakutana na huyu jamaa kwenye mtandao ulikuwa kwenye wakati mgumu kimapenzi hivyo kuwa Vanulable hali iliyopelekea huyo mpenzi mume wa mtu kuchukua advantage na kukulubuni. Ili aku-win akaamua kukupa mapenzi ya dhati ambayo alijua kabisa unayahitaji kwa vile ulikuwa huyapati kutoka kwa Mpenzi wako wa awali.

Kama walivyosema baadhi ya wachangiaji na pengine wewe pia unajua hasa kama ni Mkristo, kwamba Ndoa ya kikristo daima huwa haivunjiki unless mmoja wa wanandoa hao afariki. Hata kama wametengana bado hawatoruhusiwa kufungandoa tena unless mmoja wako kafa......vinginevyo labda Serikali iingilie na Talaka itolewe kwa amri ya Mahakama lakini hata hivyo mpaka Hakimu anakubali kuamrisha Talaka inatakiwa kuwe na vithibitisho kuwa wanandoa hao wametengena kwa muda gani na lini hasa ilikuwa mara ya mwisho kufanya ngono.

Kama bado wanaishi pamoja lakini "hawalali kitanda kimoja" bado haitoshi kumshawishi mtu yeyote kuwa wawili hao hawana ndoa. Ndio maana siku zote wanandoa wakitengana hushauriwa kuishi mbali-mbali kwa muda fulani (nadhani miaka miwili or something) ili Talaka yao Kisheria baade ije kuwa Valid.


Kama Jamaa hampi mapenzi, attention wala affection kutokana na kutumia muda mwingi kwenye Internet na pengine nje ya nyumbani pale anapokuwa na wewe ni wazi kuwa huyu mwanamke anahai ya kudai au hata ku-demand vitu hivyo na kila akifanya hivyo mumewe anakuwa mkali na kuzusha mabaya juu ya mkewe kwa vile tayari amejenga mapenzi na wewe hali inayomfanya mwanamama huyo kuomba msamaha kwa mumewe.


Mimi na wewe hatujui undani wa maisha yao ya kindoa as hayatuhusu, lakini kama kweli huyu Jamaa angekuwa hana nia na mkewe na anataka kweli kumtaliki basi angekuwa muwazi tangu mwanzo kuwa anafamilia lakini uhusiano wao sio mzuri na sio kukudanganya kuwa Mkewe kaolewa nje ya nchi.....hilo Mosi. Pili, angekuwa anaisha pake yake mahali, Tatu angekuambia tangu awali kosa alilofanyiwa na mkewe ambali anashindwa kumsamehe.

Mmekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa miaka miwili ikiwa na maana ulinza na huyu Baba ukiwa mtoto wa miaka 22. Ktk umri wa miaka 24, mimi binafsi nisingekushauri kujikita na kuendelea na uhusiano na mtu ambae tayari alioa/ameoa na watoto kwani haitokupa Amani kwenye maisha yako yote, hasa ukizingatia kuwa sasa umekwisha anza kuhisi guilt kila unaposikia sauti ya mke wa jamaa akiomba msamaha n.k.

Sio tu utakuwa unadhurumu ujana wako bali utakuwa umeumiza mwanamke mwenzio na watoto ambao walikuwa matunda ya ndoa yao. Si huyu jamaa wala yule wa zamani...wote hawakufai.

Nakushauri umalize uhusiano na huyo Mume wa mtu kisha anza maisha yako upya, kumbuka kuwa unahitaji mwanaume ili ku-share nae mapenzi na sio mwanamke mwingine wala watoto wao.

Kitu cha mwisho ningependa kukisema ni kuwa, huyo jamaa sio tu kuwa anaroho mbaya kiasi cha kushindwa kumsamehe mkewe kwa kosa analolijua yeye pia hana heshima kwa wanawake wote kwa ujumla kwa sababu zifuatazo:-

-Kukudanganya wewe mwanamke on your face.
-Kumuweka mkewe kwenye loudspeaker.
-Kukuonyesha sms za mkewe.

Ukiangalia points hizi kwa undani ni kuwa alikuwa anajionyesha kwako ni namna gani basi "anatakiwa na mkewe" hivyo ukileta ujinga wakati wowote atarudi kwa mkewe.

Kila la kheri ktk kufanyia kazi yote uliyoshauriwa na kwenye kufanya maamuzi ya busara.

18 comments:

Anonymous said...

Lizy achana na mume wa mtu, kwanza anaonekana hajui kusamehe huyo. Kama anashindwa kumsamehe mkewe, je nawewe siku ukimkosea si ndo atakubwaga hivyo hivyo???

Anonymous said...

Binti pole sana kwa njia ya panda inayokukabili!!

Napenda kuchangia mambo yafuatayo juu ya tatizo lako:

Kwanza nianze kwa kukwambia kwamba wewe ni msichana mbichi sana. Miaka 24 kufikia hatua hiyo ni hatari mno!!!

Kwa umri wako unahitaji kujituliza kwanza kabla hujaanzana na wanaume kwa sababu hapo unachotafuta si maisha yako ya baadaye bali unatafuta kujichafua na kumalizwa na wanaume hao.Sioni sababu za kimsingi za kukukimbiza na tufani zote hizo.

Jambo lingine elewa kwamba mahusiano yote uliyo nayo yana kasoro za wazi sana kiasi kwamba hakuna linalokupasa hata kubaki hapo zaidi ya kukimbia.

Kama mapenzi yako na yule boyfriend wako wa mwanzo hayako vizuri, na pia huyu mwingine ndo hivyo yuko kwenye ndoa, basi binti jiokoe haraka hakuna penye usalama hapo kwani utapoteza muda wako bure na kujichafua bure kabisa.

Hata kama huyo unayempenda sasa unaona labda atampa talaka huyo mkewe kwa mawazo yangu sioni kama hiyo itakuwa ndoa sahihi na yenye furaha maishani mwako wewe hasa ukizingatia kuwa hujawahi kuolewa zaidi ya kutombwa tu.Umri wako bado very young unahofu ya nini?una maana hakuna wanaokupenda ambao hawajajichanganya hivyo na wenye upendo wa kweli?Binti hilo ni giza totoro limekutanda hebu chukua tochi mulika uone ukweli kulikoni.Mume wa mtu ni mume tu usifurahie kuachana kwao ukaona nafuu ya mchukuzi!! huoni hayohayo yatakupata wewe kwa huyohuyo?Umesema huwa mke wa huyo jamaa anamuomba msamaha ili amsamehe kwa sababu inaonekana mkewe ndiye alimkosea, kama huyo jamaa hawezi kumsamehe huoni hata wewe hutakuja samehewa nawe kwani nawe kama binadamu utakosea jambo na likicharuka litakutimua tu?

Mimi nakushauri pamoja na kwamba kutombana kumenoga lakini chukua tahadhari mapema.Kosa ulilifanya lakini epuka kulirudia tena kama ni mapenzi ya kutombana yamewanogea basi weka stop sasa ili utunze heshima yako.Ni muhimu ujue kwamba msiba wa mapenzi unaompata mke wa jamaa yako utakugeukia wewe na kuwa mchungu sana kwako.

Mwisho niseme hebu tulia binti una umri mdogo ambao najua hutakosa kumpata mtu atakayekufaa kuwa mume wako.Sasa hivi unakimbizana na kutuliza minyege tu wala huna future life yoyote na mijaa hiyo sanasana itakumaliza na kukuchakaza na kukuacha soremba!!!

Anonymous said...

dada,umri wako bado mdogo,jamani mbon wasichana siku hizi mko desparate hivyo,embu tulia upate mwanaume mwingine asiye na matatizo akuoe,wewe ndio utakuwa rensiposible na yote hayo,kwakifupi,sikushauri kabisa huko,

Anonymous said...

mhh dada,kuwa makini,kwanini hawezi kusamehe,embu mchunguze kwamakini,huyo hapana,muulize je nawewe ukimkosea atakuacha aoe mke mwingine?na wewe unafurahia upuuzi wa kukuwekea kwenye loudspeaker,to me HANAHESHIMA,MWAMBIE KWANZA AMSAMEHE MKE WAKE,NAKUHAKIKISHIA HATA MKIKAA PAMOJA HAKUTAKUWA NA RAHA.NA AMUHESHIMU MKEWE,YEYE PIA NI BINADAMU HATUKO PERFECT.

Anonymous said...

sijui nikwambiaje dadayangu, if the guy is in such a serious misunderstanding as he tries to potray to you he would have left his wife along time ago, with or without your presence in his life. what he is trying to do is just get even with his wife while at the same time getting some free pussy and pitty from you. wakaka single wako kibao even better than that guy who is cheating on his wife.get your own life and some good guys will be flowing your way. wala usiumize kichwa.na wanaume kama hao wanaocheat kisa wamekosewa na wake zao ujue hata akikuoa wewe mkigombana atatafuta pa kwenda.

Anonymous said...

Pole sana dada, lakini ukweli ni kwamba huyo kaka anakudanganya, ni mchafuzi tu kwa wasichana kwani ni wanawake wengi sana amewaambia kuwa ameachana na mke wake na yuko nje ya nchi mara yupo tz ila hamtaki tena, ukweli ni kwamba ni muongo sana huyo jamaa, na kaongopea wengi tu, kama sikosei huyo Kijana anamiliki blog. na ni mwajiriwa serikalini, so akili kichwani mwako. ukitaka hata jina nitakutajia ha ha ha ha

Anonymous said...

MMH WE MAMII MWACHE MUME WA MTU HUYO SHOSTI !! MAAN KAMA UNAONA HUNA AMANI BASI UJUE NAYE PIA HANA AMANI HIZO NITAMAA ZA MUDA TAFUTA WAKO AMBAYE HANA MKE NA WALA HAJAOA KWANI NDOA ZA KANISANI NI SUMU NI KIFO TU HUTENGANISHA LKN KTK HALI YA KAWAIDA HUWA HAWAACHANI KABISAAAAAAAAA!! SO UTAUMIA BURE NA PINDI UKIINGIA NDANI SASA UTAKUWA NA NA WASIWASI WA BURE NA WIVU UTAKUWA MKUBWA SANA!! MUINGU AKUSAIDIE TU KWANI HUYO EX BOYFRIEND AMEKUPENDA NA BADO ANAKUPENDA NDIO MAANA HAJATAKA UJE KUUMIA BURE !! KUNA USEMI KUWA UKIRUKA MKOJO UTAKANYAGA...!! POLE SANA

Anonymous said...

dada jionee huruma mwenyewe kwanza,kuingia kwenye relationship yenye misukusuko,mshirikishe Mungu ,atakupa jibu.

Anonymous said...

Dada pole sana maana ni kweli upo njiapanda. Kikistu, ukishafunga ndoa, ni milele hakuna kuachana. Hivyo, kama alishafunga ndoa kanisani hakuna talaka, watatengana tu lakini ni lazima (I insist , ni lazima) watarudiana. Kilichounganishwa na Mungu mwnanadamu asikitenganishe, hilo hutamkwa na mchungaji/padri wakati wa kufunga ndoa. Hivyo watarudiana tu na utaaibika. Kukoseana katika ndoa ni kawaida, kama hawezi kumsamehe huyo, wewe je? au wewe ni malaika?Achana nae, tafuta wako na ufunge ndoa yenye baraka za Mungu.I wish u all the best hun.

miram3 said...

Ni yaleyale! Mimi kabla sijasema lolote naomba ujiulize swali moja , kama wewe ni mke wa huyo jamaa, naumesikia hili unalolifanya sasa hivi ungesikiaje?
Ni kweli kupenda kupo lakini kila jambotunalolifanya tujaribu kufikiri mara mbili je ingekuwa mimi nafanyiwa hivi ningejisikiaje?
Nitaongea vizuri baadaye bado mfungo unaendelea
emu-three

Anonymous said...

Gal kumbuka kam alicheat na wewe jua akikuweka ndani itakula kwako.What Comes Around Goes Around,Na ndoa ya kanisani haivunjiki utafunga Bomani?

Anonymous said...

dada hujaweka wazi mambo yote, ungejua kwanza huyo mwanamke alimkosea nini jamaa and then judge that reason of their trouble if its strong or nonsense. Usichezee penzi lako kuna makosa huwa hayana excuse husan ktk maisha ya wanandoa.

andika upya mada yako ueleze wazi chanzo cha matatizo yao,sisi hatujui lolote na hatuwezi kutoa ushauri kwa habari nusu nusu ktk maamuzi mazito kama haya

Mama Gs said...

Nafa,
Lizy mbona wewe msichana mdogo sana kubeba mzigo huo! Hapa naona kinachokusumbua ni uchanga wa akili. Ungekuwa mkubwa akili ingekuwa imeiva kuchanganua mambo.
1. Huyo mwanaume piga ua ni mme wa mtu. Wewe unamsaidia kutatua frustrations tu za kwenye marriage.
2. Mrudie Mungu akusamehe kwa yote uliyotenda kwa kujua au kwa kutokujua ili akupatie wako wa maisha na mwenye mapenzi ya kweli.
3. Kwa kuwa huyo baba anakupenda, mshauri na mtake amsamehe mkewe warudiane. Sidhani kama amemkosea kiasi hicho. Ni kwa vile tu unamtimizia haja zake ndio maana hataki kumsamehe. Angekuwa na ukame angekuwa amemsamehe. Kwa maana nyingine, wewe pia unachangia kubomoa zaidi. Acha au saidia kujenga tena kwa kumshurutisha amrudie mkewe. Akikataa ujue hakupendi pia, ila anakutamani tu.
Pole mdogo wangu na Mungu akusaidie kutambua dhambi na kuungama.
Mungu anakupenda sana hata mpaka sasa hivi.
Mama Gs.

Anonymous said...

wewe achana na huyo mume wa mtu,anakudanganya tu.

Anonymous said...

Mimi nakushauri kimbia kabisa na upige goti Mungu akusamehe umpate wako,yalishawah kunikuta makubwa kijana kanitongoza akaniambia hana mke ila ana watoto 2,cku nilipopigiwa cmu na mkewe niliomba ardh ipasuke niingie

Anonymous said...

jamani lizzy!! ujue wewe utakuwa ni sawa na muuaji kwani siku yule mwanamke mwenzio atakapokutwa na maafayoyote yanayosababishwa na msongo wa mawazo nafsi yko haitakuwa na milele usijione we mjanja kusikia mwenzio anavyobembeleza penzi lake !! analo jambo bibie we achana nae kwanza huyo ex bf wako anakupenda ndio maana akakueleza ukweli !! yaani wewe ni sawa na tangazo la radio one la mzui wa pilipilimwache mwenzio akatunze mji wake sio kurandaranda naye!! ktk maneno yote uliyoambiwa kama bado unaendelea sasa unatafutwa kupigwa mawe hadharani!!

Anonymous said...

pole sana natumia nafasi kukushauri
uachane na huyo kaka kwanza ni mume na ni baba wa mtu kumbuka itakuwa ngumu kwako na kama ni ndoa ya kanisani itakuwa vigumu kuoa tena

Anonymous said...

Lizy usifikiri kuna kitu kikubwa huyo mwanaume ameuziwa na mke wake hizo ni trick wanazitumia wanaume anafanya kosa yeye basi mwanamke usionekane mpumbavu inabidi uombe msamaha tu wakati huna kosa lolote. Kulinda neno la biblia linalosema MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE.