Baba kanilea na kunisomesha, Mama anasema si baba yangu!!

"Hi Dada dinah nina matatzo sana hivyo I need your advice. Mimi ni kijana wa miaka 21, it is a long story but I wil make it short and clear. Ni kwamba, mimi nimezaliwa Kenya when my dady met with Mum there but walikuwa ni wapenzi yaani hawakufunga ndoa.


Nilipofikisha miaka 2, baba alinichukua nikaenda kuishi Moshi na bibi, anadai kuwa matunzo kwa mama hayakuwa mazuri. Tangu alivyonichukua hadi nafikisha miaka 17 Mama hakuwahi kuja kuniona wala hakutaka kujua habari zangu japokuwa hakuwa mbali sana yaani ni kiasi cha kutumia Tsh elfu3 kama nauli.


Nilipofikisha hiyo miaka kumi na saba ndio akaja kuniona. Kipindi chote nilikuwa naishi na baba tu kwani alirudi nyumbani. Sasa baada ya Mama kuja anadai eti yule niliyekuwa naishi nae na kuamini kuwa ni Baba yangu was not my father na kwamba my father is from Uganda but huyu Baba ndio ninayemfahamu, ndiye aliyenilea na kunisomesha mapka nilipofikia na hajajua hilo, kwamba mimi sio mtoto wake. Je nifanye nini?"

Dinah anasema:Pole kwa mawazo yanayosonga akili yako hivi sasa kuhusiana na ukweli juu ya nani ni baba yako wa damu. Ukweli utabaki kuwa mama siku zote ndio anajua baba wa mtoto ni nani?

Nasikitika kusema kuwa kuna akina baba wengi tu walilea na wanaendelea kulea watoto ambao Kibailojia au kidamu sio wa kwao lakini kwa vile wanashiriki tendo la ndoa na wake/wanawake zao basi hujenga ukukaribu na mimba ile na mtoto anapozaliwa huona kabisa kuwa ni wa kwake na hivyo kujenda bond kama baba hali ambayo humathiri Kisaikolojia huyu baba na hatimae kuona mtoto huyo anafanana na watu wa karibu na familia yake kama sio yeye mwenyewe.

Pamoja na kusema hivyo, sina maana kuwa huyo si baba yako na wala siwezi kukubaliana wala kukataa kuwa yule Mganda pia ndio baba yako wa damu. Kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji huenda hata huyo Mganda sio baba yako.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha wazi kuwa hauko interested na mwanamke huyo japokuwa ndio aliyekuzaa hivyo huna budi kumpa heshima kama mzazi wako wa kike kwani hajui kuwa mama ni nini hasa kwani sio yeye aliyekulea bali bibi yako.

Sitokulaumu kwa kupoteza interest au hata mapenzi juu ya mzazi wako huyo wa kike kwani hakutaka kujihusisha na wewe, sasa kwa vile umekuwa mkubwa na yeye anazeeka ndio kashituka na kuona hakutakuwa na mtu wa kumsaidia hapo ndio akakumbuka ala kumbe nina mtoto Tz!

Inawezekana kabisa hakujua ni namna gani atakujia na hakutaka kuomba msamaha kutokana na kujiweka mbali na maisha yako wakati ulipokuwa ukimuhitaji zaidi (ulipokuwa mtoto) na njia pekee ya kujiweka karibu na wewe ili kupata atakacho ni kupandikiza uongo bila kujali (Again) kuwa akuwa atakupa msongamano wa mawazo (stress), kuumiza hisia zako (emotional) na Kisaikolojia.

Mimi nakushauri kama ifuatavyo,
Mosi, Kamwe tena mwiko kabisa kumueleza baba yako Mtanzania kuhusu hili suala, kwani litamuumiza sana na hata kusababisha matatizo makubwa (inategemea na atakavyolipokea) sio yeye tu bali Bibi yako, ndugu jamaa na marafiki.

Ikiwezekana kaa mbali na huyo mama kwa kumwambia kuwa huitaji kuwa nae karibu kwa na asikutembelee wala kuzoea kuja hapo nyumbani na badala yake mwambie wewe utakuwa ukimtembelea huko Kenya kila unapohitaji kufanya hivyo kwani tayari wewe ni mtu mzima.

Pili, Ukisha muweka mbali tafuta wasaa na uzungumze nae hata kama ni kwa simu na umwambie yalioujaza moyo wako ikiwa ni pamoja na msimamo wako juu ya baba aliyekulea (hata iweje ndio unamtambua kama baba yako n.k) na juu yake(utampa heshima kama mzazi wa kike na hadithi za masiha yake ya ujana azi-keep mwenyewe).

Tatu, Kama unataka/ukipenda kuwa na amani moyoni juu ya Mzazi wako wa Damu basi utalazimika kum-bana mzazi huyo akupe ukweli halisi kama kweli anauhakika kuwa Mganda ndio Baba wa damu au anadhania tu lakini inawezeakana hata yeye sio baba na ukweli ni kuwa hajui baba ni nani na akaamua kusingizia wanaume wote aliotembea nao.

Usimuonee aibu wala usihisi Guilt kutokana na katabia kake kachafu ka kulala na wanaume ovyo tena bila kinga, hakikisha unam-bana akupe ukweli wote mpaka kwanini hasa akamsingizia huyu baba wa Tz na kitu gani kilimfanya asijihusishe na wewe na sasa nini kimemfanya akukumbuke (yote yalioujaza moyo wako yatoe) kwani unahaki zote za kujua kwa uhakika kama huyo Mganda ni baba wa damu au unaenda kubahatisha tu!

Akihakiki na kukupa maelezo ya kutosheleza na wewe kuhisi the argue ya kutaka kujua ukweli basi omba mawasiliano ya huyo Mganda ili ufanye nae mawasiliano na ikiwezekana kufanya vipimo vya DNA ili upate amani moyoni na sio kwenda kuanza kujipendekeza kwa mtu au hata familia ambayo huijuia achilia mbali Tamaduni zao za Kiganda.


Akisita nakuja na hadithi nyingine ambazo zinaashiria kuwa hana uhakika na Mganda, kwamba inawezekana pia sio baba wa damu basi achana na the issue na endelea na maisha yako na baba wa Tz. Wewe hautokuwa wa kwanza kulelewa na mzazi ambae sio wa damu kwani kuna watoto wengi tu wanalelewa na wazazi ambao sio wa damu lakini wanapendwa, kujaaliwa, kupewa msingi na mwanzo mzuri tu wa kimaisha kama ulioupata wewe.

Kuna watoto wanaishi na wazazi wao wa damu lakini hawapati ulichokipata wewe, kwa uzoefu wako umeona kabisa kuwa mama hakukutaka ulipokuwa mdogo na alikupa matunzo mabaya kiasi kwamba baba Mtz akahofia kuwa ungeendelea kuishi na mama huyo huenda usingefikisha miaka 21, ungejifia ktk umri mdogo sana.

Kumbuka kwenye suala la DNA, hakikisha humpi jukumu lakufuatilia kwani anaweza kuwa ana-demand pesa kwa kisingizo cha kufuatilia, hakikisha unalifanya mwenyewe na kama hakuna sababu ya wewe kufanya vipimo hivyo kwa vile una amani moyoni kuwa Baba Mtz ndio baba yako hakikisha unamuweka mama huyo mbali kabisa na familia yako ya Tz ili kuepusha matatizo ambayo yatakuathiri wewe na Baba mTz.

Kama nilivyosema awali kuwa kuna asilimia kubwa sana ya kina baba hapa Duniani wamelea na kusomesha watoto ambao sio wao wa damu, lakini kwa vile hawataki masumbuko ya akili, Saikolojia, hisia na hata kuharibu ukaribu wao wa kifamilia wanaamua kudharau maelezo ya watu wengine pia vipimo ya DNA na kuendelea na maisha yako kama kawaida.

Najipa matumaini kuwa umefanyia kazi maelezo na ushaurio kutoka kwa wachangiaji na utafanya uamuzi wa busara ili kuishi kwa amani na furaha.
Kila la kheri!

Comments

Egubo.G.M said…
Japokuwa Siri ya Baba wa Mtoto anaijua Mama, But si busara hata kidogo kwa huyo mama kukujulisha habari za Baba yako Mzazi katika umri huo ulio nao. Alikuwa wapi siku zote hizo kukujulisha ungali mdogo huenda ungejipanga vema kuliko hivi sasa kukabiliana na jambo hilo. You need another many year kuyazoea na kuyaanza maisha mapya na huyo Baba wa Kiganda. Swali ni kwamba ni kweli hata huyo baba wa kiganda ni Baba yako Mzazi au Mama yako alikuwa hajatulia vizuri anabahatisha Mzazi mwenza? anyway natania tu Mjomba siku hizi kuna vipimo vya DNA ikibidi utafanya hivyo lakini itakugharimu kukubali matokeo.
Anonymous said…
...mueleze wazi hata kama si biological father, anastahili heshima zote za baba. Kwa historia hiyo, huhitaji hata kuomba ushauri,anastahili kuwa baba kwako. Mama yako mbona alikutelekeza kwa miaka yote hiyo? na huyo mganda alikuwa wapi? sasa anachotaka nini?
lucie said…
huyo mamako hajatulia, siku zote alikuwa wapi. achana nae mweshimu baba yako aliekulea. huyo ndo babako. ye kama alijua huyo sio babako kwa nini alikuacha nae?achana na mawazo hayo soma uje uwasaidie wazazi wako. tena mpe ukweli mama yako.
Anonymous said…
Pole sana kaka, unajua ukweli siku zote unauma sana, na ni kweli kwamba ajuaye baba wa mtoto ni mama siku zote. Unachopaswa kufanya ni kuchunguza kwanza ni kwanini mama yako akuambie jambo hilo sasa hivi, inawezekana labda kuna mgogoro baina yake na huyo baba mlezi. All in all you need to do the DNA test bro, though inaumiza but you need to know the truth.
Anonymous said…
oh! yah! ni kweli itabidi ucheki DNA na hao mababa, eventhough ikagundulika huyu baba mtz si baba yako, nakushauri uendelee kumtreat kama baba yako mzazi, coz ndo kakufikisha hapo,na huyo mchukulie tu ndo baba yako wa ukweli.i mean umejua ukweli ila ukweli usikubadilishe the way you used to be with your dad.
Anonymous said…
sikiliza wewe, biology doesnt make one a father. watu wangapi wanasingiziwa mimba na wanalea wototo wasiokuwa wao mpaka mama anakufa kabla hajatoboa siri? watu wangapi wana-adopt watoto na wanakuwa na uhusiano mzuri na watoto hao kuliko hata ambavyo wangekuwa na baba zao halisi? kimsingi, inawezekana kabisa huyo aliyekulea ndio baba ako wa ukweli kwani mama yako asingeweza kumsingizia mtu ambaye hajawahi hata kutembea nae. mazingira mimba ya wewe ilivyoshika ndio yaliyomfanya huyo baba mlezi aamini wewe ni mtoto wake, kwa hiyo inawezekana kabisa ndie babako halisi, kwani mimba huingia siku moja kwa tendo moja na mbegu moja. it doesnt take 2 or a million sperms to create a pregnancy. usianze kutaka kutafuta baba wakati wa utu uzima hainogi hata kidogo. hata baba mzazi hauishi nae milele, ukioa au ukiolewa tu anakuwa mbali kidogo. dont mind. mimi nimelelewa na mama wa kambo na what i feel about her is more than what I could have felt for mama mzazi. keep cool n take care. tchao!
Anonymous said…
pole sana ndugu yangu
ma naamini umri ulionao na mzazi uliyemzoea inatosha kabisa kwani itakuchukua miaka kwa wewe kumkubali huyo baba mpya na kuyasahau maisha yako ya zamani na kuanza maisha mapya na babampya
je huyo baba wa kiganda atakukubali kama mwanae?
je wewe upo tayari kumkubali huyo baba mpya?
je upo tayari toka moyoni mwako kukubal chalenges ambazo zinakujia katika kuanza maisha hayo mapya?
nadhani hayo ni maswali ya wewe kujiuliza ndio ufanye maamuzi.
me nadhani uendelee na maisha yako na huyo baba unayeamini ndio baba yako.
me naamini anakupenda kama mwanae na amekukubali katika maisha yake
pia jaribu kukaa na mama yako muulize kwa nini anakuambia wakati huu?
alikuwa wapi kipindi chote hicho?
mbona alikuwa haji kukutembelea waati wote huo?
je huyo baba yako anakutambua?
alikuwa wapi wakati wote kukutafuta?
Mungu akutangulie kwenye kufanya maamuzi hasa wakati huu mgumu ulionao mpendwa
mama sarah said…
Mdogo wangu Pole, Huyo mama yako hana busara na hana mapendo nawe yaonekana yuko after something, eigher kumkomoa huyo baba uliyenae au anaona sasa ushakua wa manufaa anataka kukuhasimisha na huyo baba yako, kwa mawazo yangu, hata kama kuna mababa wengine saba, mama yako atakuambia, basi uamue huyu alie kupenda na kukulea tangia udogo hadi leo na anakuthamini kuliko huyo mama. ndie baba yako.Huna haja ya kufanya DNA, unless baba yako ahitaji. kuna watu wengi wametunzwa na kulelewa na watu ambao sio biological father. Kwa mfano huyo mama yako ni biological lakini hana mapendo. kwa hivyo ni heri ungekua na mama hata wa kulea angekuthamini na kukujali. Usiumize kichwa chako kwa hilo, mwambie mama yako, so longer tangia ulipofungua macho umeambiwa huyo ndie baba yako atabaki kua baba yako hadi utakufa. mwambie na baba yako aliekulea ingawa mama ameleta hio hadithi, lakini wewe hauwezi kubadiri msimamowako na yeye ndio baba yako
Anonymous said…
MDOgo wangu usisikilize wanawake wa kikenya ni waongo sana. huyo mama sasa hivi anakuhitaji ndio maana anaona njia ya kukupata ni kukudanganya. mimi nakaa nao na jinsiwanavyowatreat waume zao hutapenda. ni waongo hao sana and they know how to manipulate. be becaful
Anonymous said…
wewe endelea na huyu baba ukiona mama anaendela kusemesha kuhusu baba mwingine just tell her very short and clear unitoke na umalaya wako , huyu ndiyo baba ninayemfahamu otherwise utapata shida
Anonymous said…
dah,ila mdogo wangu usikate tamaa huyo alokulea ndo baba yako hata kama kuna mwingine n ur mama simz hajapenda unavyolelewa vizuri,pliz kama kweli huyo wa uganda ni dady wako respec him bt ol in ol wa moshi ndo dady mwenye uchungu
Anonymous said…
Kwanza mshukuru mungu kwa kuonyesha tabia halisi ya huyo mama yako! Naungana nao wote wanaosema mama amejua sasa wewe ni wa kutegemewa na ndio maana anakuja na manipulative schemes! Endelea kumheshimu kama mama lakini katu usiruhusu akusababishie matatizo kwa kuharibu uhusiano na HUYO BABA YAKO! ALIYEKULEA NA KUKLINDA NA KUJITOLEA KWA MAISHA YAKE YOTE! Wala katu usijisumbue na jitu lilongonoka samahani kwa neo hili kali lakini ndo ukweli! usijisumbue kabisa na huyo baba wa uganda wala mama wa kikenya; kifupi hao sio watu ni viumbe walio na sura ya binadamu! Mshukuru Mungu na umuombe amlinde mzazi wako huyu wa Moshi ili aje afaidi matunda ya juhudi zake! na alaaniwe huyo mama yako kwa kutoja li hata hisia zako mpaka akadiriki kuja kukusimulia huo upuuzi! Forget about biology theories even Man Jesus was not raised by his biological father!