Habari dada!
Hongera kwa kazi nzuri unayoifanya kwa kusaidia kwa ushauri kwa watu wanaohitaji msaada,
nikiwa mmoja wapo ya wanaperuzi wa blog mbalimbali nimeona niombe ushauri kwako.
Mwaka huu ulipoanza nilipata mchumba ambaye wakati tunakutana mimi nilikuwa nimeajiriwa na yeye akiwa bado so unakuta tulipokuwa tunatoka out I had to share cost with him ili asijione ni mzigo kwake.
Aunt huyu Mchumba kwangu namwona ni mtu wa ajabu maana anaweza akaniita sehemu na kuagiza vitu na bill inapokuja ananirushia mpira mwanzo nilidhani kwa sababu hana kazi but now amepata kazi lakini bado anafanya the same.
Kama juzi tulitoka na rafiki zake bill ilipokuja akalipa chakula na kunirushia mpira bill ya vinywaji, kisa alijua siku hiyo nimepata pesa Ofisini. Kwa shingo upande nikatoa na kulipia vinywaji. Aunt hii sio mara ya kwanza there are time nilifiwa na ilinibidi kusafiri kwenda nyumbani (Kijijini) wakati msiba umetokea ilikuwa kama 3 days before birthday yake.
Niliporudi kama 2 dayz baada ya siku yake huyu Mchumba akawa ananikumbushia zawadi yake bila hata huruma kwamba nilitumia pesa kusafiri kwenye msiba tena wala yeye hakunipa hata shilingi kwa ajili ya safari.
Jamani eti hii ni kawaida au huyu wangu kazidi?
MJ"
Dinah anasema:Habari ni njema tu MJ, asante kwa mail na kwa uvumilivu as nimechelewa kukujibu. Ni matumaini yangu wachangiaji walisaidia kwa kiasi kikubwa kupitia michango yao.
Mh huyu wako kweli kazidi, mwanaume gani anashupalia zawadi ya b'day? Kwanza wanaume muhangaikaji (au tumuite a real man) huwa hawajishughulishi sana na kumbu kumbu za kuzaliwa kwake kwa kupata zawadi au kufanya party bali kutafuta mikakati ya kijiweka sawa kimaisha kwa vile umri unakwenda mbele na majukumu yanakwenda kuongezeka.
Kwa kawaida wanawake tumezoea kuangaliwa na kujaaliwa kiuchumi na wanaume hata kama tunasenti zetu wenyewe kutokana na shughuli zetu, sio kwa sababu ya mfumo dume, la hasha! ni kutokana na matakwa yake Mwenyezi Mungu, kwamba mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakuwa mtafutaji. Tumekuwa tukiona hayo kwa macho, mama na baba wote wananya kazi lakini ni baba pekee ndiye anaefanya kila kitu kinachohusu manunuzi au pesa.
Kwa baadhi ya wanaume kumjali na kumtunza mwanamke kiuchumi ni sehemu ya UANAUME, kwamba asipofanya hivyo Ego yake inaumia na pengine kujiona useless. Lakini siku zinavyozidi kwenda mambo yanabadilika wenyewe tunaita maendeleo au usawa.
Nasikitika kusema sehemu kubwa ya jamii inalichukulia suala la Usawa tofauti kabisa na lengo au dhumuni la kuwa sawa, kwamba pamoja na kuwa tunatofautiana kijinsia sote tuna haki sawa ya kupata Elimu, Kulipwa mshahara kutokana na uwezo wa kikazi/cheo, kukataa/kukubali/kupinga au kufanya maamuzi, haki ya kuongoza kisiasa, kiuchumi au hata kingono, haki ya kutaliki n.k. Hii yote ni katika kuondoa mfumo dume ambao ulikuwa unakandamiza wanawake wengi Duniani.
Sasa baada ya wanawake kujua haki zao na kuwa na sauti baada ya ule mkutano wa Beijing, wakabadilika na kuwa sio sawa bali ni kujiamini kupita kiasi hali inayopelekea wao kuonekana au kuwa wajeuri. Hii imesababisha wanaume wengi hivi sasa kuwa wachunaji, ndio wapo wanaume wengi siku hizi wanatumia wanawake kiuchumi, wanafanya exactly what women used to do or are doing which katka hali halisi is wrong na haijalishi wewe ni mwanamke au mwanaume, huna hali ya kumtumia mwenzio kiuchumi na badala yake unatakiwa kushirikiana nae.
Nini cha kufanya: Unahitaji mawasiliano ya haraka sana ikiwa unampenda na unataka kuendelea na uchumba wenu ili baade mkafunge ndoa na kuishi pamoja kama mtu mmoja, usipojitahidi na kuweka mambo wazi sasa ni wazi kuwa ndoa yenu haitodumu au haitokuwepo kabisa kwani huyo sio mwanaume ambae mwanamke yeyote angependa kuolewa nae unless unataka kuolewa ili kuondoa "mkosi".
Tafuta siku nzuri na andaa mazingira mema ili uweze kuzungumza nae, hakikisha huna hasira na wala suiongee ktk mtindo wa ku-demand mabadiliko. Mwambie mpenzi mchumba wako kuwa unampenda na ungependa siku moja muishi kama mke na mume ( kwavile tayari mmechumbiana tayari), lakini kuna vitu vichache vinavyoweza kufanya hilo lisitokee.
Sema kwa uwazi, kuwa sio kwamba ulisahau kumnunulia zawadi bali mambo yaliingilia hapo kati na ikabidi usafiri kwa ajili ya shughuli za kifamilia hali iliyopelekea wewe kutokuwa na senti. Mueleze, kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi watu wanashirikiana kwa kila jambo na kila hali hivyo hukutegemea yeye ku-demand zawadi ya b'day bila hata kujali hisia zako baada ya kufiwa.
Orodhesha kuwa (kama nilivyo panga ili uweze kutoa your point mwisho), ili uhusiano wenu uwe bora unahitaji viungo vitano muhimu:-
(1)-Kusikilizana/kuelewana.
(2)-Kuheshimiana/thaminiana.
(3)-Kusaidiana.
(4)-Kuaminiana
(5)-Kushirikiana, "tunatakiwa kuonyesha ushirikiano huo kimapenzi, kimwili na kiuchumi".
Endelea kwa kusema kwa upole na upendo ukimuangalia machoni, kuwa unaamini ktk ushirikiano na kusaidiana kiuchumi na sio kushindana au kuwa tegemezi. Malizia kwa kusema sisi ni wachumba hivi sasa, tunatakiwa kuanza kujiandaa na maisha yetu ya baade kwa kuanza kushirikiana. Ongeza, ungependa kuanzia sasa tushirikiane na kukubaliana nini tunakwenda kufanya kabla ya kukifanya.
Mf: Kabla hatujatoka out ni vema mkapanga mnaenda wapi? mtakaa kwa muda gani? watu mtakao kutana nao huko walialikwa na ninyi au wakwenda wenyewe? na mtatumia kiasi gani?
Akikubaliana na wewe basi hakikisha unaangalia mabadiliko na wewe kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ushirikiano huo unakuwepo (inaelekea yeye hajui ) so wewe sasa unajua hakikisha unakuwa a leader lakini sio in a kijeuri way bali loving way.
Akibisha ua kuwa mkali na hataki kukusikiliza ua hata kukuelewa basi tambua njemba hiyo inakutumia kiuchumi ili kuonekana ina hela Mpe buti la meno kisha anza upya na utakutana na mtu mwenye kujali na kukupenda kwa dhati.......si unajua mtu akiwa limbukeni wa kulipwa mshahara, anataka Dunia nzima wajue anajua kuzitumia (kumbuka hakuwa na kazi b4).
Nakutakia kila la kheri.
Tuesday, 1 September 2009
Je ni kawaida au huyu wangu kazidi?-Ushauri
Labels:
Ananichuna,
demand,
kazidi,
mchunaji
| Unaifikiriaje hii? |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



13 Wamechangia Mada, bonyeza hapa kwa mchango wako.:
Wewe dada kimbia, tena kimbia sana, huyo ni tapeli, tapeli mkubwa. Kama unataka kujua hebu acha kumlipa bill wakati wa kujivinjari au kama birthday uone jinsi mambo yatakavyojeuka. Nilimpata wa namna hiyo, yaani hata petrol alitaka nimnunulie, ule upya wa mapenzi ulipoisha, nikawa ninampa excuse za kutokua na pesa wakati anataka nimfanyie kitu, basi akawa anapandisha hasira na mimi I stood my grounds - basi hata sijui penzi liliishia wapi kwa sababu alikuwa anafwata ATM dada, ATM narudia, and funny enough mimi ninaumri mdogo zaidi yake- yaani kimbia hapo hapendwi mtu...... ni pochi tu
Unajua dada yetu, hiyo kwa wanawake wengi watasema sio kawaida, kwasababu tumezoea kuwa mume ndiye `mfadhili', lakini maisha sasa yamebadilika, akina mama wengi sasa wanaweza, na sio ajabu kwa wao kuwafadhili wanaume. Mkifika sehemu ya kustarehe basi mfadhili anakuwa mke. Na tunadhani kuwa masugar-mami ndio wenye tabia hiyo , hapana, hii yote inategemea na kipato.
Tuelewe kuwa urafiki wa kweli ni ule `wakusaidiana kwenye dhiki na faraja' na sio ule wa mwisho wa mwezi. Lakini ulilolisema lina-walakini, kwani hatujui upande mwingine wa shilingi, je anafanya hivyo kwa sababu gani, ana majukumu mengi, au kunani?
Lamuhimu kwa vile mumeshakuwa wachumba ni heri uanze kujenga tabia ya kuelezana ukweli. Anzeni tabia ya kupanga mambo kimpango(bajeti)
`mwenzanguee, mwezi huu kipato changu ni kadhaa, na wewe je, je tufanyeje, na je nani atafadhili hiki au kile...' hii kwanini inakuwa ngumu. Na kama hamuaminiani, huo uchumba una dosari.
Ushauri wangu usikate tamaa, hiyo ni kawaida,na inaweza ikawa kawaida kwa baadhi ya watu, ila kuibadili inategemea na wewe `ucheshi wako' jinsi gani mlivyoivana,na unaweza mkaivana kwa kuelezana ukweli, ili ajue majukumu yake. Huenda bado anaile hisia ya kuwa tegemezi'ipo siku atabadilika na wewe unaweza ukawa chachu ya kumbadili.
Mungu atawajalia mkienda kwa `heri'
emu-three
NB. Tunaomba darasa la simu za mikononi nafikiri ulishaligusia nyuma,ulielezee KIUNDANI ZAIDI,yaani zipo ndoa nyingi zinavunjika kwasababu ya simu za mikononi. Je kwanini kitu kidogo kama hiki kivunje ndoa? je ni haki mume kutokutumia simu ya mke au mke kutumia simu ya mume, na hata kusomeana meseji? kama watu hawaaminiani kwa hili basi kuna kinachoendelea ndani yake, na kwangu mimi nitaiita ndoa hiyo ya `kutegeana' Je dada Dinah,utazisaidiaje ndoa hizi za kutegeana. (unaweza kuifuta sehemu hii ya NB)
Pole sana D; huyo kazidi ila siku hz wanaume wamejenga kitabia hicho sana hasa akijua mchumba/gf au mke wake ana kipato kizuri. Cha muhimu, Mueleze kuwa ulimsaidia mwanzo bse hakuwa na kazi lakini from now asimame kama mwanaume, na ikibidi hata mdanganye kuna matatizo kazini so unalipwa half ya salary yako ili ajue huna hela aanze kujituma mwenyewe, pia angalia yawezekana hana mapenzi anachotaka ni hela yako tu.
Dada kwanza pole msiba pili pole na uyu mchumba ambaye anaonekana rugumya kwa kiswahili ni baili halafu anapenda kulalia upande mmoja watu kama hawa wapo lakini kaa naye chini muelezee kipi kinakuudhi ndani ya moyo wako lakini kwa upole fulani hivi usiposema dada mume kama huyu katu hawezi kubadilika kwasababu amezoea vya kunyonga vya kuchinja hawezi,lakini ukimeleza huyu ataelewa japo taratibu lakini sms imfikie mlengwa atabadilika pole pole ni hayo tu dada pole kwa mkasa huu,wanaume tuone aibu kidogo jamani
Pole sana dada kwa yanayo kukuta.............huyo mtu wako hiyo ndio tabia yake na usitegemeekuwa atakuja kubadilika ........msingi uliomjengea mwanzo kwa kumchukulia kuwa yeye hana kazi tayari anaona kuwa wewe kufanya pia ni wajibu wako...........japo kuwa pia kumbuka maisha ni kusaidiana hicyo kama uko na nafasi unaweza kumsaidia mwezni wako
Duh mwenzangu kwanza inabidi nikupe pole sana, hii sio kawaida kabisa. Mimi navyofahamu outing yoyote ambayo yeye ndo atakwambia mtoke kila kitu ni juu yake usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na kila kitu mnapokuwa somewhere. Ila kama wewe utakuwa umeamua kumtoa au mtoke basi ujue utagharamia wewe lakini kwa mwanaume perfect lazima awe na shy kidogo so hatayeye atachangia gharama. Ila kwa mtizamo tu huyo jamaa yuko kukutumia zaidi (kimaslahi)na c kimapenzi. Ushauri wangu mweleze ukweli then uone atakujibu nini ndo uamue what next.
Duh mwenzangu kwanza inabidi nikupe pole sana, hii sio kawaida kabisa. Mimi navyofahamu outing yoyote ambayo yeye ndo atakwambia mtoke kila kitu ni juu yake usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na kila kitu mnapokuwa somewhere. Ila kama wewe utakuwa umeamua kumtoa au mtoke basi ujue utagharamia wewe lakini kwa mwanaume perfect lazima awe na shy kidogo so hatayeye atachangia gharama. Ila kwa mtizamo tu huyo jamaa yuko kukutumia zaidi (kimaslahi)na c kimapenzi. Ushauri wangu mweleze ukweli then uone atakujibu nini ndo uamue what next.
Dada wewe pole sana!!!
Mimi nikiwa mwanaume naona huyo jamaa haufai kabisa!!
Kwanza kwa kawaida wanaume tunaona aibu sana ujiweka chini ya mwanamke.Hata ama hatunazo tunajitutumua tu ili mradi tumaintain status zetu.
Pili wanaume tunapenda kutoa kwa kimada wangu zaidi ya jinsi tunavyoweza kusaidiwa na wapenzi wanawake.
Pia kwa msiba ulioupata kwa kawaida mwanaume angeweza hata kukugharimia nauli yako au angalau kuhusika na kitu fulani kwa msiba huo kama kweli ni jamaa ambaye ana upendo wa dhati kwako kama mchumba.Lakini badala yake anajipenda mwenyewe.
Kukudai zawadi ya b/day yake ungali na majinzi ya kufiwa na kutumia gharama, si hulka ya mwanaume ambaye kweli anakujali.Hiyo inaonyesha anajipenda yeye na hana huruma nawe hata kidogo.
Kukusukumizia bills za vinywaji na malaji wakati ana hela pia tena on the sport ni kukufedhehesha maana kama huna unaweza kuaibika.Ilibidi akuarifu mapema kama ana upungufu wa pesa ili mgawane hayo majukumu.
Kwa ujumla si hulka ya mwanaume ambaye kweli anajiamini ku parasite kwako wewe mpenzie ambaye mwanzo ulimhudumia kwa nia na upendo mzuri.Sina maana kwamba kwa sasa huwezi kuendelea kumsaidia, ila nina maana lazima aonyeshe kukujali na kuonyesha uanaume pia kuwa mwanaume ndiye mwenye jukumu zito zaidi kuliko wewe.Vinginevyo iwe kwa namna nyingine,lakini hadi umelalamika kuja kutaka ushauri humu, bila shaka jamaa huyo amezidi.
Je kama hiyo ndiyo hali ya sasa na bado hamjawekeana ahadi za kuishi pamoja mambo yatakuweje huko mbeleni?Chukua tahadhari kabla ya hatari.Kama kweli mko wachumba kihalali chukua hatua mapema ya kuzungumzia suala hilo aelewe kitu anachofanya si kizuri lazima kushare mambo.Utakuja shangaa hata mkioana pesa yako ndiyo itanunua kila kitu nyumbani mwenu yeye atakuwa anakubania na kufanyia mambo yake tu au kusaidia ndugu zake tu .
Kila la heri dada
mpenzi huyo wala hakujali, sio kwamba napenda kubomoa but naelewa coz nilishapitia hiyo hali. nilikua na mwanaume alikua tegemezi hadi nahisi kuchoka.hadi vocha ya kuwasiliana na mimi namnunulia na lilikua linakunywa basi balaa tu. unaeza kuta anakutumia na sababu anajua unajitolea basi anakugeuza NGO. BE AWARE , anakutumia
pole sana dada yangu, mimi nadhani inawezekana huyu mchumba amezoea hivyo baada ya kukuona kuwa una uwezo, ila hata hivyo amezidi kwa vile kama hana uwezo wa kulipia chochote au kabla hamjatoka nyumbani ni lazima mzungumze na mpange mtatumia kiasi gani, mimi nilianza kazi kabla ya mume na nilikuwa sina tatizo kumpatia hela za matumizi na wakati huo tuna mtoto mdogo,nina furaha kuwa mume wangu alikuja kupata kazi yenye kipato kikubwa kuliko changu na ili kunilipa fadhila za kumsaidia kwa miaka 2 bila kunung'unika aliniengage upya ( hapo tayari tushaoana ! ) na kunipatia vito vya tanzanite ninavyovipenda sana, hivyo nahisi amejilegeza, naomba kabla ya kutoka mjue mnaenda wapi mnatumia kiasi gani na ni nani mlipaji wa bili, sisi hata sasa kwenye ndoa moto ni uleule, kama hatuna hela hatutoki, kama mimi ninazo yeye hana tunatoka sehemu ya uwezo wa hicho kilichopo, mara nyingi sisi hubaki home na kuangalia movies, so many nights, lakini huyo bado hajakuoa atakumalizia hata hela ambayo ungeweza kuisave ikakusaidia.. Mungu akubariki sana..
pole dada, tatizo ni kwamba kujitolea mara nyingine huonekana ni wajibu. Kitendo cha kushare gharama na mpenzio ni jambo zuri kama litafanywa kwa utaratibu mzuri. Wa kwako kalemaa sana, mpaka anadai birthday penye majonzi? hakumbuki hata nauli hakukuchangia. Hakumbuki ulivyojitoa kabla hajapata kazi? Kama umempenda kwa dhati basi manapotoka muwe mnajadiliana gharama na atalipa. Ila huyo akikuoa atakuumiza, hutapata raha ya kuitwa mke.
mh,dada pole,tena pole sana.
mimi pia ilinitokea karibia kama wewe,mwanaume alikuwa na kazi na mimi nina kazi ila since yeye ana makato mengi akawa anaona mimi ndie wa kutoa kila kitu kuanzia chakula,vinywaji and almost everything,nikiendesha gari lake ujue linawaka taa nyekundu na hapo ujue natakiwa kuweka mafuta,yeye haweki,tukitoka hachangii hata senti,bado mipombe anakunywa, hela yake ni ya pombe tu na gym,,,daa nilitoka hapo nikaona hapa sio penyewe.
kwa hiyo pole dear, i understand how it feels. you can stand on your own, wekeni mikakati,kama hamuelewani toka kungali mapema...
jamani, dada bora we mchumba mi mume, mwali kuamzia uchumba, nilianza kwa kuamini kuwa it was my obligation as a patner,and later on as a wife kusaidia hata kutoa chochote nilichokuwa nacho kwa ajili ya maendelaeo ya familia ndogo tulioplan kuitengeneza, kwa bahati nzuri nina kipato kikubwa kuliko yeye basiikawa sababu, hatoi kitu bali demand ikawa kubwa kwa upand e wake,
Kiukweli, nikajisahau mimi nikawa nampa yeye tuuu, kwa bahati njema tena nikabahtika kupata mtoto wa kiume, mwali ilikuwa more responsibility kwa upande wangu, imagine hata nepi moja!!!!! ila sikuwa na jinsi kwa sababu nilikuwa kwaenye ndoa ya kikristo...
to cut the story short, ikafikia kipindi nilijenga kabanda kangu, nikasafiri kwenda kusoma kurudi kauza kibanda changu kwa kigezo kuwa alikuwa ametikisika kiuchumi katika muda wa miezi 16 niliokuwa nje,,,, kiukweli maji yalifika shingoni, nikaona isiwe tabu coz i was not going anywhere with him... we are now separated
Tangu akae mbali nami, niendelea vizuri, mwanangu yuko darasa la kwanza kweney shule nzuri, kanyumba kangu kiujumla naisha si haba na ni mtu mwenye furaha tele.
MWALI KUKWAMBIA YOTE HAYO NATAKA UWE MAKINI NA CHOICES ZA PATNERS WA SIKU HIZI... UKIMAKE WRONG CHOICE THEN YOU WILL RUIN YOUR OWN LIFE...NAJUA UNAMPENDA KAA NAE,UMWELEZE ABADILIKE, UKIONA HAVIBADILIKI.... KIMBIAAAAAA
Post a Comment