Saturday, 11 July 2009

Maji meupe ukeni, natumia Condom kwa kila tendo-Ushauri

"Habari dada DINAH.
Mimi ni msichana wa miaka26, nilianza mapenzi nikiwa form 2 lakini sasa ndiyo najuta. Nikiwa form 2 nilipata mpenzi ambaye alikuwa mkubwa sana kangu kwa umri na ndiye aliyenitoa bikira yangu.

Baada ya miaka 2 nikaanza kutokwa na majimaji sehemu za siri nikaenda hospital wakaniambia nimeambukizwa ugonjwa wa zinaa wakanipa dawa lakini majimaji meupe yakawa bado yanaendelea kutoka kuanzia hapo sikuweza kufanya tendo la ndoa bila Condom niliogopa kumwambukiza huyo mtu niliyekuwa naye.


Lakini dada dinah huyo mtu aliyenitoa bikra tuliachana nikapata kaka mwingine ambaye analengo la kuniona sasa dada tatizo ni kwamba tangu nikiwa form 2 hayo majimaji meupe ndiyo yalianza kutoka hadi leo ni miaka kama 7 bado yanatoka.

Nikienda hospital Dokta akinipima sionekani tatizo ila yanakuwa yananiwasha sana na kuna wakati natoka vipele. Nimetumia dawa kuanzia nikiwa form 2 hadi leo hii ila hayajaacha kutoka. Huyu kaka anayetaka kunioa nampenda ila sipendi kumuambukiza ugonjwa niliyonao? Sasa nifanyaje naomba ushauri.

Na je uwezekano wa mimi kubeba mimba upo?nampenda kweli huyu mchumba wangu na napenda anioe ila sasa nitafanyaje?nisaidie nipo katika wakati mgumu"

Dinah anasema:Pamoja na kuwa uliambukizwa Gonjwa la zinaa ambalo hujasema jina lake nadhani pia hujui Utoko ni nini. Ikiwa Daktari aligundua kuwa unatatizo na anakupa dawa ni wazi tatizo hilo lilikwisha hivyo hakukuwa na sababu ya wewe kuendelea kutumia dawa zile miaka saba baadae.

Hebu niambie kwa uwazi, maji hayo meupe yakoje? Kama maziwa yenye uzito wa cream (Utoko) au meupe kama maji ya yaliooshewa mchele (ugonjwa), meupe kama maji ya kunywa na yanatereza (ute unaojitokeza ukiwa na nyege au ukikaribia hedhi/yayi likiwa linapevuka) au meupe na yakiwa chupini huwa ya njao au kuna ukahawia kwa mbali na uzito wake kama cream(Ugonjwa).......ukinipa jibu hapa itanisaidia kukupa maelezo ya kutosha.


Sasa, hiyo hali ya muwasho na kutokwa na vipele kwa haraka haraka nadhani huenda inasababishwa na matumizi ya Condom (inategemea unatumia aina gani). Ikiwa unatumia Condom zilizotengenezwa kwa mpira wa Latex (Condom nyingi Bongo miaka ya 90s zilikuwa zikitengenezwa kwa aina hiyo ya mpira na actualy unaweza kabisa kusikia harufu ya mpira unapozitumia) hizi sio nzuri kwa watu wenye allergy.


Pamoja na kusema hivyo zipo Condoms za latex lakini hazina allergy lakini ili kujua hilo unapaswa kuzinusa, na ikiwa hazina ile harufu ya mpira basi ujue hazitokupa tatizo. Vilevile kuna Condom ambazo ni non-latex na wengi wanazipenda kwani hata material yake ni laini lakini imara na hazina harufu yeyote.


Hizi zimetengenezwa kwa kutumia Polyurethane na zinapatikana kwenye maduka Makubwa ya Madawa kila kona Dar es Salaam,hakikisha unasoma maelezo kabla ya kununua....usitegemee maelezo ya Mhudumu wa Duka la madawa (wengine hawajui au hawajali).

Kuhusu suala la wewe kupata mtoto hapo baadae nadhani lipo ikiwa Mungu atapenda iwe hivyo kwani tatizo ambalo labda ungehofia limetibiwa miaka saba iliyopita.

Nakutakia kila la kheri na Hongera sana kwa kuzingatia matumiz ya Condoms.

**Oh hey....Nipe maelezo kuhusu rangi na texture ya maji maji meupe yakutokayo ukeni ili niweze kukupa jawabu la uhakika ili uchukue hatua za haraka kwenda kuonana na Daktari bingwa wa Magonjwa ya wanawake.

7 comments:

Anonymous said...

mpendwa pole kwa yaliyokukuta, i can imagine how stresfully u r ila usikate tamaa.je hao madaktari unaowaona ni bingwa wa magonjwa ya kina mama?
ila all in all, mi nakushauri tafuta pia tiba za asili,sio WAGANGA,la hasha hizi traditional herbs.
hapa moshi kuna pahali mjini panaitwa mombasa store jaman wanasaidia sana kwa dawa za miti shamba. ni wahindi.
ila hata dar es salaam mbona kuna herbalists wengi tu, unajua miti shamba sio uchawi,ila sio unaenda kwa mtu anaetibu uchawi na miti shamba pia, muhimbili kuna kitengo cha miti shamba,
pia kuna hospitali inaitwa HOLISTIC, iko makumbusho.wanatibu sana coz nina ushahidi thabiti.wako makini sana so go and try mpenzi.incase of any help rudi tena kwa dina nitakupa my contacts naitwa mama na.

Anonymous said...

Maji meupe,

dada kama hayana harufu basi wewe unafika kileleni, huo ni utoko tu!!! niliwai pata mrembo zaman kidogo halipata hali hiyo, si ugonjwa bali ni pale m'ke anapopata raha--utoko wake na wa'me basi unatengeneza hiyo kitu.

Anonymous said...

acha utoto, hujamwona daktari. huo si ugonjwa wa zinaa kama unavyotaka kuamini. sawa ni ugonjwa lakini wa kawaida kwa wanawake. unaitwa vaginal candidiasis, umehamasishwa pia na wadudu wasababishao vaginosis[bcterial]. matibabu yake ni.
1.usafi wa kumani, kila umalizapo kutiwa, kunawa, na uchambapo kama unatumia maji,flash kinyuma nyuma.
2. tumia dawa iitwayo fluconzole moja kwa siku kwa siku 14 mfululizo.
3. tia dawa iitwayo gynazole au cotrimazole vaginal peseries kwa muda wa siku saba usiku tu.
4. tumia dawa iitwayo norfloxacin kwa siku 7 mara mbili kutwa.
dawa zole zimaenda pamoja.
kama maji hayo yatakuwa yanatoa harufu ya samaki aliyeoza, waweza kulazimika kuongeza dawa nyingine iitwayo secnidazole 2gm start.

Kuma zilizo na maji hayo huwa ni tamu sana kutomaba peku, kwani uterezi wake huwa safi sana na mnato fulani. pole lakini.

Anonymous said...

Aah!
Pole sana dada, I feel ur pain!! Usifikirie sana na kujilaumu mambo ya form 2, Balehe ndiyo iliyokuponza dada!!
Ushauri wangu kwako ni kwamba, Kwanza acha tabia yako ya kutombana nje ya ndoa, Mungu hapendi tabia hiyo. Maana ya kufunga ndoa ni maidhinisho ya kuwa ni halali kwenu kutombana kuanzia siku hiyo, Sasa ww mwenyewe fikiria mnaenda kuidhinisha nini na hali tayari mshavuana chupi? Hv mnafikiri mnamdanganya nani? Kwa taarifa tu mnajidanganya wenyewe kwakuwa Mwenyez Mungu anafahamu yote mliyofanya na uongo wenu pia anaujua. Si lengo langu ku preach ila tu ni ujumbe kwa wale wamwogopao na wamchao Mungu ambao wanaunganishwa na blog hii.
Enyi watu, mwogopeni mwenyezi Mungu na mcheni yeye peke yake na ishini ndani ya mipaka yake aliyokuamrisheni.
Pili, ni kuwa kuhusu tatizo lako, nakushauri uende kwa daktari umwele historia ya tatizo na chanzo chake [zinaa] na muda ambao unalo tatizo, na madawa uliyotumia. Umweleze bayyana kuhusu dalili unazoziona, tena ikiwezekana andika ktk kijkaratasi mambo unayopaswa kumweleza dokta ili usije sahau. Tazama nilivyokubainishia, ni kazi yako sasa kuyabainisha kwa daktari.
Eleza kwa uwazi wala usione aibu kwani hiyo ndiyo kazi ya daktari, usiposema kama chanzo ni ngono unafili atajuaje!? Kwani yeye ni Malaika! Pia kumweleza muda ambao umedumu na tatizo kutamsaidia daktari kwenye kukupa dawa kwani dozi hutegemea usugu wa tatizo.
Mwisho, nakuhusia kuwa, wewe na mumeo mkiwa ni wacha Mungu hamtakuwa na hofu ya kusalitiana wala hamtakuwa na hofu ya kuambukizana UKIMWI, NA wala hamtasalitiana kamwe. Ikutosheni ucha Mungu kuwa ndiyo Silaha tosha ktk maisha yako.
Sasa ww umekutana na mchumba wako disko, hv unategemea hatakusaliti cku zote za maisha yako?, maana mahali penyewe mlipokutana, mara nyingi wahuni ndio hukutana hukn. Just use ur common sense.
Mwatima

Anonymous said...

Akh dear mbona una hatari wewe ulikua bado mwanafunzi hata hukuogopa kutombwa na mwanamme tu siyo mume wako bila condom sasa dear ona umeenda kuokota ugonjwa huo na umeshakua sugu umebaki kujuta! Sasa je ungeokota HIV si ndio ungelia kilio cha mbwa mdomo juu wewe na wazee wako! Je umepimwa pia HIV.Mwambie doctor akupe dawa za gonolia pole sana na usiende tena bila condom na jitibishe kwanza kabla huaoana na mwenzio usije kumuambukiza maana inaonyesha kama ni gonolia imeshakua sugu! Sasa kweli unaenjoy hata hiyo sex mimaji na mipele au ndio kukunwa tu utoe muwasho mimi nakushauri jitibishe kwanza achana kwanza na mambo ya kutombwa kwani magonjwa mengi ya zina ukitombwa ndio yanazidi!

Pole na ogopea maisha yako na siku ingine usiende bila condom na pia hakisha hata kama huyo mnatka kuowana mnapimwa kwanza hospital tofauti na jaribu kumstukiza mwenzio wapi unataka mkapimwe maana bongo bwana nasikia mtu anaweza kumuhonga Dr na akamfichia hata kama ana HIV watu wanauza maisha ya watu kwa ajili ya pesa!
maisha yanatisha saana siku hizi.

Bye and take care and sorry for hilo gonjwa!

Anonymous said...

Umemuona dakitari bingwa wa mambo hayo au dakitari tu wakawaida? Kama ulimuoana dakitari wa kawaida miminingekushauri umuone dakiri bingwa, huenda kuna tatizo jingine.
emu-three

Anonymous said...

Mpendwa,
Pole na hali uliyonayo. Mtafute Dk mtaalam wa magonjwa ya kina Mama umuelezee bila ya kumficha ili ajue ukubwa wa tatizo halafu atakusaidia.
Kutokana na kukaa na tatizo hilo kwa muda mrefu uko katika hatari ya kutoshika mimba.
Nakusahuri umfahamishe huyo mumeo mtarajiwa ili nae akusaidie na ajue jinsi atakavyojikinga na atarajie nini kama hautashika mimba huko baadae.
Jitahidi kujitunza kwa kutakufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa,ili ni tendo la watu walio katika ndoa.
tmajaliwa@yahoo.com