Monday, 13 July 2009

Boyfriend anataka ngono, lakini mie naogopa-Ushuari


Hi,
Dada Samahani mimi ni msichana wa miaka 23 Sijawahi kufanya mapenzi ila nikiwa na umri wa miaka kama 6 tulikuwa tunacheza mambo ya kitoto.

Kwa sasa nimepata Mpenzi ila kinachonisikitisha anataka tufanye mapenzi ila mimi siko tayari nifanyeje.

1. Naogopa kupata Mimba kwa sasa

Dinah anasema:Sio kitu kizuri kuzaa nje ya ndoa na labda baadae kuwa mama wa watoto wenye baba tofauti hasa kama huyo Bf hatofungandoa na wewe. Vilevile sio vema kuwa mama kabla wewe mwenyewe hujafahamu maisha yako yamesimama wapi, kwamba huja-settle au kukamilisha malengo yako kama mwanamke.

2. Naogopa kupata Ukimwi


Dinah anasema: Kweli hali sasa inatisha sana kwani sio tu kuwa maambukizo ni mengi zaidi kuliko miaka kumi iliyopita bali pia hivi sasa tuna kizazi kilichokwisha ambukizwa, kwa maana kuwa walizaliwa na VIRUS au waliambukizwa wakati wa ukuaji wao kutokana na ukosefu wa elimu juu ya kuishi na walioathirika na virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Hivyo basi ninyi mnaokua miaka hii ambao wengi mlizaliwa miaka ya mwishoni mwa miaka ya 80 mnakuwa kwenye hatari kubwa ya kuanza uhusiano na watu waliokwisha ambukizwa na wazazi wao kabla ua baada ya kuzaliwa, hivyo basi mnatakiwa kuchukua tahadhari kabla ya kujikita kwenye masuala ya mahusiano ya kimapenzi na hata ngono.

Hili tatizo ni kubwa na haijalishi wether uko nje ya ndoa au hujaanza kabisa ngono au umefunga ndoa, wote tunapaswa kuishi kwa taadhari na kujenga mzoea ya kuangalia afya kabla na baada ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na ngono.

3. Naogopa kama naweza kumpa na anaweza kuniacha na naogopa kutendwa kwa sababu naona marafiki zangu wanavyotendwa na wanavyoumia.

Dinah anasema: Sio mara zote mpenzi wa kwanza ndio anakuwa mume hasa kama wote wawili "hamjakuwa" kiakili au hamjakamilisha malengo yenu kimaisha kama individuals. Hivi kama uoga wako ni kuachwa mara tu baada kutoa mwili wako kwake basi ni vema ukaliweka wazi hilo kwa mpenzi wako huyo.

Umri ulionao ni mdogo sana kuanza kufikiria suala la kutendwa, kwani vijana wa umri huo wengi bado wanajaribu kupata uzoefu kwa kujihusisha na mahusiaono tofauti na baadhi hawapendi kuwabaki na mpenzi mmoja kwa muda mrefu kwa vile hawako tayari kufunga ndoa, wanachokifanya ni ku-have fun na kupata experience.

Mwambie kwa kujiamini kabisa kuwa, "nitakuwa tayari kutoa mwili wangu (kufanya ngono) kwa mume wangu" kwa maana kuwa utafanya ngono utakapofunga ndoa, sasa kama yeye ametualia/kua kiakili, yuko tayari kukufanya wewe mkewe na anakupenda kweli basi atavumilia na siku moja kufunga ndoa na wewe ili kufurahia "ua" lako.

Akitoka baruti au kubembeleza umpe sasa na atakuona ujue hayuko tayari kuwa na wewe kwa muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja na nusu. (hii itasaidia kuokoa muda wako na vilevile utakuwa umenusuru kuumia kwani hutokuwa umengonoka nae).



4. Nasumbuliwa na kutokwa na uchafu Mweupe kwenye sehemu zangu za siri mzito nifanyeje kwa sababu hii hali inanikera sana.

Dinah anasema: Huo uchafu unaitwa Utoko, ni asili kwa mwanamke yeyote anaekaribia na aliyevuja ungo (Balehe) kutokwa na ute huo mzito wenye rangi nyeupe. Kwa vile wewe bado hujajiingiza kwenye uhusiano wa kingono basi unatakiwa kuwa mvumilivu na kuwa msafi kwa kutawaza/dha kila unapokojoa, badilisha chupi mara tatu-nne kwa siku au mara tu unapoona Utoko huo kwenye chupi.

Utakapo anza kufanya ngono au utakapofungandoa na kuanz akungonoka basi utapaswa kuwa unajiswafi (Hapo juu kulia unaweza kutafuta topic inasema "jinsi ya kuswafi ume" au "Utoko" ili kufahamu vema zaidi).


5 Je nikiwa tayari kumpa huyu mpenzi wangu penzi mambo gani ambayo nitazingatia.

Dinah anasema: Utakapokuwa tayari kutoa mwiliwa kwa mpenzi wako huyu, njoo hapa nitakueleza kwa undani na kwa uwazi kabisa.



6. Je nitajitayarisha vipi naomba ushauri wako kwa sababu huyu jamaa tuko naye huu mwaka na nusu na nimemwomba anipe muda wa mwezi mmoja tena.
Nashukuru sana Dada yangu.

Dinah anasema: Mwezi mmoja hautoshi kwa wewe kufanya uamuzia mbao utabadilisha maisha yako milele, kitendo cha wewe kufanya ngono bila kuwa tayari (kufanya ili kumridhisha BF) kitakufanya ujute na hutoweza ku-undo kilichokwisha tokea. Pia napenda utambue kuwa mwaka mmoja na nusu sio muda mrefu sana kwenye uhusiano kupelekea ninyi wawili kufanya ngono.


Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa hauko tayari kufanya ngono kwa sasa na pengine unahitaji muda zaidi ya mwezi mmoja. Ikiwa kweli huyo Bf wako anakupenda basi hakika ataendelea kukusubiri hata kamani miaka 5 au hata mpaka mtakapofunga ndoa au utakapokuwa tayari kufanya hivyo.


Kumbuka ni wewe pekee mwenye mamlaka juu ya mwili wako, ni wewe pekee mwenye nafasi kuu ya kuchangua maisha yako ya kingono na sio mwanaume no matter how much u love him or he loves u.

Mara utakapokuwa tayari kuchukua uhusiano wenu kwenye hatua nyingine basi utahitaji kuwa na uhakika kuwa unachokwenda kufanya ndio kweli unakitaka na kamwe hutojutia, hakikisha unatoa mwili wako kwa mtu ambae mnapendana, mnaaminiana na mmepima afya kwa maana ya kuangaliwa kiuchunguzi kama hamna magonjwa yeyote ya zinaa ikiwa ni pamoja na kubwa lao UKIMWI.

Siku ya siku ikifika njoo nikupe maelezo zaidi ya nini ch akufanya, lakini kwa sasa zingatia na fanyia kazi ushauri uliopewa na wasomaji wa D'hicious.


Dinah anadokeza:Tafadhali usim-attack binti huyu mdogo, mpe ushauri utakao msaidia kama vile ambavyo utamfanyia mdogo wako ikiwa atakuja kwako kwa ushauri. Asante.

****Shukrani za dhati ziwafikie wachangiaji wote, tuendelee kushirikiana.
Binti muuliza maswali nakutakia kila la kheri ktk kufanyia kazi ushauri uliopewa na hatimae kufanya uamuzi wa busara.

17 Wamechangia Mada, bonyeza hapa kwa mchango wako.:

Anonymous said...

We binti usijaribu ngono kabla ya ndoa, kwanza ni dhambi kwa mujibu wa dini zetu (waislam na wakristo) na ni fahari sana siku ya ndoa ukikutwa bikra na Mumeo utapata heshima ya kipekee sana (haina maana ambao hawakukutwa bikra hawaheshimiki, ila si kiivyo).

Tatu, wasichana wengine wana wivu kwa wenye bikra hivyo watawashawishi waipoteze kwa namna yoyote ile hata kwa kuwanyanyapaa eti washamba, bado watoto, hawajui starehe, hawajui maisha,na mambo mengine mengi tu ili wajione hawafai, tafadhari sana usijaribu subiri mpaka ndoa maadam umeshaonyesha uwezo wa kujitunza mpaka hivi sasa.

Nne, japokuwa kuna kondom haziaminiki 100% , zinaweza kupasuka, mimba, ukimwi,magonjwa ya zinaa nje nje na kama wewe ni muumini mzuri wa dini yako kondom hazikubaliki kidini.

Tano, kama kweli huyo jamaa anakupenda atakuelewa na atasubiri mpaka mfunge ndoa halali vinginevyo ataondoa thamani (bikra) yako na ataanza kukunyanyasa - yaani hivyo anavyombembeleza ni kwa sababu hajapata, akishapata tu tegemea mabadiliko makubwa sana (ndio ataonyesha rangi zake halisi amini nakwambia hatakuwa kama kabla hajapata.
Kama unadhani unamfahamu M'ume kabla hajakutia unajidanganya!!

Narudia tena, kama kweli anakupenda ataheshimu uamuzi wako wa kusubiri mpaka ndoa halali vinginevyo "itakula kwako".

Sita, Wewe ni kati ya wasichana wachache sana ambao wameweza kujitunza mpaka umri huo, tafadhari endelea kujitunza. Kumbuka katika maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa, riziki yako ni yako tu hakuna wa kuichukua.

Saba, elewa ngono ni kama ulevi fulani hivi ukionja tu kosa, huachi ndio maana ni rahisi sana kugombana na yeyote awe mzazi,ndugu,rafiki, n.k kwa sababu ya ngono (ingawa wengine wanachanganya na neno mapenzi, ngono na mapenzi/tendo la ndoa ni vitu tofauti kabisa).

Nane, ni rahisi sana kupanga mipango yako ya kimaisha/kielimu na kuifanikisha kirahisi kabla hujaanza mahusiano ya ki ngono, elewa ukisha anza tu, huna maamuzi ya pekee yako tena. Mbali na mzazi/mlezi ambae unapaswa kumshirikisha hivi sasa itabidi na huyo jamaa nae umhusishe kwa kuwa uamuzi mwingine unaweza kuathiri mahusiano kwa kiasi kikubwa.

Tisa, kuna mambo ya kujifunza kuhusu hili tendo kabla hujajihusisha nalo, kama ujiandaeje,ufanyeje na mwenzio nini afanyeje kabla ya kutiana,hayo Dinnah ameyaeleza vizuri tu unaweza kuyapitia katika makala zake.

Elewa Dinnah anachofanya ni kuelewesha jamii "in a constructive manner" (yaani kwa nia njema au mtazamo chanya)na wala si kufundisha UZINZI.

Mafundisho ya Dinnah hata tulio kwenye ndoa yanatusaidia sana kuboresha ndoa zetu kama mtu akitumia kwa UZINZI hiyo ni yeye na shetani wake hakuna aliye mlazimisha.

Jambo la LAZIMA KUFANYWA KWA WOTE NI KWENDA KUPIMA AFYA ZENU kabla ya kufunga ndoa angalau mara tatu kila baada ya miezi mitatu na wakati huo huo mkiendelea kujitunza kama awali.

Huo mwezi mmoja uliompa mmeshapima afya mara ngapi?? kama bado usivue chupi kabisaa ni hatari iliyojificha huwezi kuiona kwa macho tu mpaka vipimo vya kisayansi.

Lugha za nakupenda sana,ananipenda sana, ninamuamini,ananiamini, ninamuonea huruma hapo si mahala pake, elewa watu wengi sana wameambukizwa Ukimwi na magonjwa ya zinaa na waliokuwa wanawaamini sana, wanawapenda sana, wanawaogopa sana, n.k

Kumi, sisi wote tunakupa ushauri tu lakini maamuzi ni yako mwenyewe na kumbuka uamuzi utakao ufanya kuhusu jambo hili hivi sasa ndio utakao amua Mustakabari (future) ya maisha yako ya baadae.

Ukifanya maamuzi sahihi ni faida kwako na ukifanya maamuzi mabovu ni hasara/majuto kwako kwa siku zijazo.

Mwisho, nakuona kama msichana mmoja hivi kwenye tamthilia ya "EDGE OF PARADISE" (anaitwa Shola kama sijakosea) inayorushwa Channel 5 (EATV) Kila J'pili, J'nne na J'mosi. Lakini kaka yake anaitwa "DOSSIE" tafadhari itazame naamini utajifunza kitu.

Kwa kipande kilichorushwa jana J'pili yuko katika mazingila kama yako kabisaaa (anataka/anashawishiwa kutoa bikra yake).

Anonymous said...

Kwanza kabisa nakupa hongera kama uliyosema ni sawa, kuwa hujawahi kufanya mapenzi hadi sasa, na bahati nzuri umempata mchumba.
Katika kufuatilia kwangu nimegundua kuwa wengi wanaoshauri kuwa ni vyema `kupimana' kwanza kabla ya ndoa wanataka kupata `wanachama' lakini kiundani kabisa `wanajuta'
Ni bora ilioje kama mumepata bahati ya kukutana kwa mara kwanza mkiwa mumeshafunga ndoa! Unampa umpendaye zawadi asilia toka kwa Muumba, zawadi ya `ubikira wako'. Na itokee bahati kuwa na mchumba wako sio kicheche, kwakweli mimi nawaonea wivu.
Na bora ilioje kama wote mumepima afya zenu, na kujikuta mpo safi kwani humuwezi mkajua afya zenu vyema mpaka mpimwe.
Baada ya kusema hayo ushauri wangu ni kuwa kazi uzi huohuo, kuwa kama unanipenda kweli `tufunge ndoa kwanza,na kabla ya kufunga ndoa twende hospitali tukapimwe afya zetu' hapo utakuwa umetatua tatizo no 1 hadi tatu.Tatizo no 4 hadi kuendelea yatakuwa rahisi kwani mtashirikiana na mwenzako, kwani mengi ya hayo yanahitaji ushirikiano,na ushirikiano wa yule ambaye mumeshawekeana ahadi mbele za Mungu. Nafikiri yeye pamoja na wewe mkifuata ushauri wa Dinah wa mara kwa mara(pitia pia mapitio yake ya awali)mtajenga familia njema na wala hamtakuwa na wasiwasi. Nakutakia kila-lakheri
emu-three

Anonymous said...

Binti,wanikumbusha enzi yangu.kwa upande wangu mimi nilimjua mwanaume nikiwa na miaka 25.Urafiki wetu ulianza nikiwa na miaka 20.Nilikua muoga kama wewe,lakini alinipa muda bila kuchoka.Nilitumia miaka yote mitano kumpenda yeye jinsi alivyo,nilikua mawazi kwake na yeye akajifunza kuwa muwazi kama mimi.
Nilipofurahi ama kuchukia nililhakikisha kuwa anajua,ikitokea tukagombana tulisuluhisha,kusamehana na kusahau yaliyopita.Mpaka nilipomjua kimwili hapo penzi lilikua tamu haswa na mpaka leo nipo naye.
Nakushauri wote mkapime ili mjue afya zenu.
Ninayo imani kuwa,hapa utapata ushauri mzuri na wa kufaa kutoka kwa dada Dina na wachangiaji wengine.
Kila lakheri mdogo wangu.

Regina Paul said...

Kwanza hongera kwakuwa mvumilivu,

Ushauri,
Kwanza kama wewe unahitaji kufanya mapenzi then unaogopa kuambukizwa virusi mwambie boyfriend wako mkapime na vilevile kama unaogopa kupata mimba basi mwambie atumie kondom.

Pili kuhusu kuhusu kuachwa hilo lipo kwasababu wanaume wengi hupenda kukujua jinsi ulivyo alabu baada yakukujua tu anakuacha hawana mapenzi ya kweli ila wanatamani.

Pia anaweza akakupenda zaidi ya anavyokupenda sasa kwasababu umejitunza mpaka ulipofikia (unabikira) hivyo inategemea na mapenzi ya mwanaume kama kweli kayaelekeza kwako.
Asante.

ignorant said...

Kwanza nakupa hongera sana kwa kufikia umri huo bila kufanya mapenzi au kungonoka. Hata hivyo maelezo yako kuhusu uchafu unaotoka katika kuma na pia tendo ulilofanya ukiwa mtoto, unaweza ukawa umepata uoga kufanya kukutana kimwili na mwanaume ambao umekusaidia kuhimili maombi ya kufanya mapenzi hadi kufikia umri huo.

Pili, naungana na wewe kwa sababu zako zote, kasoro ya 3. Mie nitazungumzia kwanini natofautiana kidogo kimawazo kuhusu sababu yako ya 3 na wengine watakupa ushauri kwa sababu zingine.

Kumekua na imani potofu (kwa maoni yangu) baina ya wanawake na pengine wanaume pia kwamba tendo la kujamiiana kati ya mwanamke na mwanaume humfanya mwanamke atumike. Hakuna anaefikiri au kuamini kwama mwanaume nae anatumika. Kwa upande fulani, imani hii ndo inawafanya wanawake wengi wasifurahie kujamiiana kwani wanadhani wanatumikia wanaume.

Dada ondoa shaka kwamba mwanaume ukimpa mikasi basi anaweza kukuacha. Hakuna mwanaume anaeoa kwa ajili aje kukutomba tu, lazima kuna sababu zingine zinazomfanya akuoe. Hivyo kama hizo sababu au vigezo vingine havipo, hata kama utaweza kumlaghai kwa kumnyima hiyo ili akuoe, nahukakikishia kua atakuacha mara tu baada ya kuionja.

Cha msingi ni kujua ni kwanini anakupenda, hivyo vigezo ndiyo vinapaswa kumshawishi kupanga kuishi nawe maisha yenu yote na wala sio kuma. Jua kila mwanamke anayo kuma.

Kwa kumalizia, kuna wanaume wengi tu wanaoweza kukubali kumuoa mwanamke asiye bikira lakini ana tabia nzuri kuliko kuoa bikira mwenye tabia mbaya.

Ignorant

Anonymous said...

Mmmhhh!! wewe binti wa maana sana!!!

Kwanza nakupongeza sana kwa utulivu wako na pia kwa kujiheshimu na kuwa katika maadili mema bila kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Jambo la pili nakupongeza sana kwa kuja hapa kuweka jambo lako wazi ili upate msaada wa maana namna ya kulikabili hilo jinamizi la kufanya ngono lisije kukunyemelea pasipo ridhaa yako na dhamiri yako hasa.Ni wachache wasichana wa jinsi yako.

Kwanza nianze kwa kusema kwamba suala la kufanya mapenzi na mtu ambaye si mume wako linahitaji tahadhari kubwa sana;Kama wewe ni mkristo au mwislamu tendo hilo linakuingiza kwenye dosari kubwa ya kutenda dhambi mbele za Mungu wako.Hilo ndilo liwe la kwanza kulifikiria mara mpenzi wako anapokutaka mapenzi kabla hamjaoana.

jambo lingine ambalo umeligusia mwenyewe ni kwamba usijaribu kabisa kumruhusu mtu kufanya naye ngono bila maamuzi ya busara sana.Suala la ngono linahitahitaji kuwa na muda mrefu sana kutafakari kama hilo ni jambo linalotoka ndani ya uhuru,utayari na uamuzi wa kweli kutoka katika dhamiri yako kwani ukifanya hivyo kwa kurubuniwa au kushauriwa na mtu ile dhamiri itauawa sana kama halijatokea kwenye maamuzi yako sahihi na maelekevu kwa sababu umejitunza hadi hapo basi asubili muoane.

Jambo lingine umelisemea mimi nikiwa mwanaume nataka nikueleze ukweli binti kwamba vija wa siku hizi ni wasanii kwelikweli.Unaweza kuamini kwamba jamaa yako anakupenda na akakuambia kuwa tutaoana na zile zawadi na ofa za hapa na pale na manjo njo mengi ya kukuvutia nia kubwa ni ili akupate umpe kuma yako.Ole wako ukimsogeza umekula mwande binti.Akisha kula taratibu anajongea.Usimsogeze mwanaume afike hadi huko chini; Ni HATARI!!!
Kama mpenzio ana nia nzuri nawe basi akuheshimu kwa sababu umejitunza sana si kwamba hakuna waliokutaka kabla.Majuto ya wadada yamekuwa kero kubwa katika jamii kama ulivyosema wasichana wanalia na kulaani.Mwambie subira yavuta heri kama si wanafunzi basi fungeni ndoa mambo yaishe ili muweze kumegeana ngono halali kabisa.

Pia suala la magonjwa umelisema mwenyewe ni muhimu kujipa tahadhari hata kama kuna kupima.Unajua ukionja hutaacha ukikose utakuwa mtumwa kabisa wa hicho kitu.Na hapo ujue kama jamaa atakutelekeza utahitaji kukutana namwingine atakayehitaji ngono mwendo huo utakuwa aluta continua.

Narudia tena kusema umejipa heshima kubwa kwa kutoruhusu mtu kunusa na liboo lake huko chini.Tena zaidi umempendeza sana Mungu muumba wako.Amini usiamini hata watu wengi wanajua kuwa wewe ni bikira maana waliokutongoza ukawakataa wanasimuliana.Basi usitake uharibu heshima hiyo kwa tendo kama hilo ambalo ni mchezo tu wa kujifurahisha na hatimaye unabaki na kumbukumbu za kukuumiza dhamirini kwako.

Mwisho nasema KATAAAAAAAAA kabisa kumvulia nguo huyo jamaa na hata yeyote yule ambaye si mume wako.

Kila la heri na baraka kutoka kwa Mungu wako.

Anonymous said...

HONGERA BINTI KWA KUTUNZA UBIKIRA WAKO HADI MIAKA HIYO.kATAA KUMPA HUYO JAMAA INAWEZEKANA AMEDUMU KATIKA URAFIKI NAWE ILI TU AKUPATE AKUDUNDE HALAFU AKUAGE HATA BILA NENO.

hIYO NI MEDHARI TUNZA SANA HADI UOLEWE WENGI WANALIA KWA KUWAAMINI WANAUME LAKINI BAADAYE WAMEWACHIA MSIBA MKUBWA WA MAPENZI.cHONDECHONDE USIKUBALI BINTI WEWE!!

Anonymous said...

Ahsante sana mdogo wangu kwa kutanguliza kutafuta ushauri kabla ya kutoa ruhusa jamaa ale tunda.Sitaki kuingia sana kidini lakini kwa ushauri mwepesi tu kama waumini wa dini fulani mnge-refer vitabu vinasemaje juu ya ngono nje ya ndoa, Kuna vitu viwili yaani kupenda na kutamani, sasa jiulize mdogo wangu je anakupenda au anakutamani?, nowadays maradhi ni mengi na huwezi kumjua huko alikokuwa kabla ya kukutana na wewe alikuwa na nani. Kama ana nia nzuri na wewe mwambie avumilie mpaka hapo mtakapofunganishwa mkataba wa kuishi kama mke na mume.
Juu ya kutokwa uchafu nakushauri uwaone wataalamu wa magonjwa ya kike watakusaidia.
Ahsante

Anonymous said...

Binti una bahati maana wote waliotoa ushauri wamekupenda na kukupa ushauri wa maana sana.Nimesoma karibu wote wameongea mambo yanayofanana kama vile walikuwa pamoja kuandika.Basi zingatia walilokushauri.

Jinamizi la ngono limekithiri na kuleta misiba katika jamii.Chunga sana.Mmoja wa washauri amekuambia kuna kutamani na kupenda.Anayekupenda anakujali na kukutunza pia.Kwa hiyo hawezi kukuvunjia heshima.Anayekutamani huyo ni hatari aipata anachokihitaji tamaa inaishia hapohapo na wala hatakuwa na hamu tena nawe.Kwa hiyo kama jamaa yako anakupenda basi akuheshimu asikutake ngono kabla ya kuoana.mwambie wewe ni bikira na umejitunza hivyo kwa ajili ya mtu mmoja tu mwenye mapenzi mema na mimi atakayekuwa tayari kunivumilia hadi vigeregere na vifijo visikike kanisa au msikitini.

Nakutakia kila lililo jema binti tena umewafundisha na wengine watunze ubikira.

Anonymous said...

Binti wewe kama mdogo wangu nakupa hongera sana. Swali ulilouliza ni la msingi na litakusaidia wewe maishani kwako. Mengi umeelezewa kwenye hizo comments ila nimeipenda na nimemuunga mkono mtoaji comment wa kwanza. Huyu mtu hakujui wala humjui ila ametumia muda wake kukuelewesha wewe ili akusaidie na kukuokoa katika hili janga la ngono bila mpangilio. Tafadhali nakusihi fuata ushauri wako. Achana na mambo ya ngono sasa hivi na huyo kijana kama anakupenda kwa dhati basi atasubiri nawe fanya hicho ndio kipimo cha mapenzi yake kwako. Kwani nani kasema na kahalalisha huyo ndio atakae kua mume wako. Anaweza kulala nawew mwisho akakuacha ukabaki namaumivu. Akupenadaye kwa dhati atakuvumilia mpaka hapo wote mtakua tayari bila shinikizi na tayari kwa ndoa.

Mungu akulinde na akutie nguvu ya kuweza kupambana na vishawishi vya kidunia yasio na mbele wala nyuma.

PM said...

Mdogo wangu, kwanza hongera saaana, mko wachache sana, hivo inabidi ujisifu mwenyewe.
Mimi nimeona mwaka jana, nilijuana na binti kwa miezi kadhaa, na hata siku moja sikuwahi kumgusia kuhusu ngono, tuliamua kufunga ndoa, na huwezi kuamini usiku wa ndoa, mke wangu alikuwa ni bikra!
Heshima niliyonayo kwa mke wangu ni ya kipekee, na imani niliyonayo kwake haina kipimo.
Hivi sasa naishi nje ya nchi, na yeye yuko home tz, ila nina imani nae 100%!
Jitunze mdogo wangu, sisi wanaume ni waongo sana, anataka kukuonja tu, maana kama kweli anataka kukuoa, apeleke posa, mfunge ndoa ili apate zawadi ambayo wanaume wengi wanaililia - BIKIRA!

Anonymous said...

Fuata ushauri wa mtu wa kwanza, wa pili na wote waliokuhusia kufanya ngono ndani ya ndoa tena ukiwa na mumeo halali tu!!

Mwenyezi Mungu akuepushe na mtihani huo unaokukabili inshaallah
Mwatima

Anonymous said...

Pamoja na pongezi ulizopewa na wadau hapa chini nami pia nakupongeza kwa kujiheshimu kwa kutunza usichana wako kwa kipindi chote hicho.

kwa miaka ya sasa kumkuta msichana mwenye umri kama wako ana bikira ni kitu adimu sana

ila nataka dina an wadau wa hapa watuambie faida za kungonoka ukiwa na umri mdogo....naimani kuna faida na hasara zake.

Anonymous said...

Hongera kujitunza hata sasa. Muda mliovumiliana ni marefu. Sasa mkapime afya zenu, aje kwa wazazi, mfunge ndoa, umpe anachotaka. Kabla ya yote muone daktari wa akina mama akupime huo uchafu unaotaka ukeni, upate matibabu. Yaweza kuwa fangasi. Ila ni ugonjwa wa kawaida unaowatokea akina mama wengi, hivyo usiogope na utapona kabisa.

mbilinyi said...

hongera sana dada na nakupa hongera kwa kuwa wengi hawakuweza kuvumilia hadi hapo ulipofikia kwa kuwa kuna vishawishi vingi.

hadi hapo mwombe Mungu akuongoze ili uweze kufanikisha yale yanayompendeza,

nakuomba kwa wakati mwingine usitumie tena picha ya mtu mwingine kuombea mawazo, hii ni picha ya Lauren Nicole London (born December 4, 1984 California Los Angeles)

lucie said...

soma mama achana na hayo mambo ya ngono. siku hizi bila elimu ni kazi bure. hakuna watu waongo kama wanaume. anakudanganya kwa sababu anaona maziwa yamesimama, ngoja akupe la kukupa kama utamuona. soma mdogo wangu. soma. hakuna kilicho mkombozi kama elimu. achana na huyo mtu/watu. kama anakupenda akusubiri.

Dinah said...

Asante Mbilinyi.
Hiyo Picha hajaiweka muombaushauri bali nimeweka mimi Kupitia (picasa) ili kujaza nafasi kwani maelezo yake yalikuwa mafupi mno. Asante.