Friday, 19 June 2009

Ushuhuda kutoka kwa Asif King!

Habari za saa hizi dada Dinah na wachangiaji wote. Mimi ni Asif King sijui unanikumbuka? nilikuja hapa kuomba msaada wa mawazo na ushauri kuhusu mke wangu ambae anaishi Ughaibuni na watoto wetu wawili. Napenda kusema Mungu awabariki sana kwa kuweza kuokoa ndoa yangu. Kama isingekuwa Blog hii na wachangiaji wake hasa kiongozi wao Dinah basi ndoa yangu ingekuwa historia.

Ni karibu miezi miwili tangu nilipopata ushauri wenu na kuufanyia kazi na ninamshukuru Mungu mke wangu alinisikiliza na kuonyesha kunielewa na kuahidi kurudi nyumbani mara moja ili tuongee vizuri. Kama kawaida nilimtumia tiketi na akaja na sasa ninavyoongea yuko hapa Tanzania na watoto watafuata baada ya kufunga shule kwa ajili ya mapumziko ya summer, hivi sasa wanaangaliwa na Ndugu huko huko Ughaibuni.

Leo hii nimeamua kuja hapa kusema yaliyotokea kwani sasa nina uhakika na maamuzi ya mke wangu kuwa kweli atabaki hapa nyumbani kama mlivyonishauri nimshawishi.

Kwakweli sina jinsi ya kuwashukuru Ndugu zangu kwa wema wenu na muda wenu mliotumia kunishauri kupitia Blog hii, nilikuwa nimekata tamaa kabisa na nikawa tayari kupoteza ndoa yangu lakini Dinah akaniambia kwanini nikimbilie kuoa mwanamke mwingine wakati sijajaribu kuiokoa ndoa yangu? Dada kwa kweli kama ni kipaji basi ni cha pekee, hakuna mtu alinishauri yote niyoyapata hapa kwa Dinah, naahidi kuja tena hapa kama tutatetereka tena kwenye ndoa yetu.

Mungu awabariki sana tena sana wote mliochangia, wote mlionipa ushauri mzuri na kunitaka nisioe, wote mlionipa moyo na matumaini ya kuwa mvumilivu. Nimeamini ukichangia tatizo unapata suluhisho haraka kuliko kukaa nalo moyoni. Ule ukurasa na maoni yake yote nime print na nimeyatuza kwenye faili langu kwa kumbu kumbu.

Nisiwachoshe sana jamani, mke ananisubiri. Kwaherini na endeleeni kuokoa ndoa za wengine kama mlivyo okoa yangu.

Dinah anasema: Habari ni njema tu.
Shukrani kwa kurudi tena mahali hapa, nimesoma wakala wako nikahisi machozi yananilengalenga kwa furaha, D'hicious imeokoa Ndoa nyingine tena!

Hongera sana Asif kwa kufanikiwa kuokoa ndoa yako na hatimae kuvinjari na mkeo. Kusoma Mkasa wa huyu bwana unaweza kubonyeza hapa

2 comments:

Anonymous said...

Ahmdulillah rabbil-allameen. Mshukuru sana Muumba wa Mbingu na Ardhi kwa kusali!!
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru dad Dinah mwenye kuanzisha na kui controll hii blog, kwa hakika c blogu ya wamalaya, si blogu ya wahuni bali ni blogu ya watu wema, tena wanaoshauriana ktk mema. Siku nikijaliwa kupata mchumba[mke] nitampa zawadi nzuri nayo ni kumuondoa ktk giza na kumpeleka ktk Nu'ru kwa kumuonesha blog hiii!!!!!!!!
Mwatima

jj said...

Kweli kabisa Mwatima mtu ukiwa na mwenzi hata rafiki jaribu kumuonyesha blog hii, kwa kipindi chote nilichosoma hii blog nimefaidika mengi sana ikiwa ni pamoja na kutokuwa kubali tena kuwa mtumwa wa mapenzi.

Hongera Asif na mungu aitangulie ndoa yako ambayo ilitaka kuingiliwa na mdudu wa siku hizi, yaani si ajabu watu kufunga ndoa after one year unasikia wametengana. Keep in praying