Friday, 26 June 2009

Nilipinduliwa nikaolewa tena ila mume2 simuelewi-Ushauri

"Dear Dinah
Mimi ni mdada wa miaka 28 niliolewa na mume wa kwanza na nilijaliwa kupata nae watoto
wawili.Mume alikua hodari sana kwa kila kitu katika mambo ya ndoa na tulipendana
sana hadi nilipopinduliwa na mwanamke mwenzangu bahati yake sasa ndio anakula raha
zote.

Nilivumilia saana baada ya kupinduliwa kwa vile mwanamme tulipendana saana
na hasa nilizingatia kuhusu watoto kwani alionyesha mapenzi saana pia kwa watoto wetu wa
kinyume na sasa nilivyoachika.

Kama unavyojua ndoa za waislam ni mwaname ndio
anapoama kumuacha mwanamke huwa na haki japo wewe bado unampenda akiamua
kukuacha huwa halazimishwi kuwa na wewe ila mwanamke ni hadi uwe na sababu
ya kimsingi kama vile ametaka tigo au analewa na hakutimizii mahitaji, lakini mambo mengine
huwa huwezi kuachika!

Dinah anasema: Hii wala sio haki, mwanamke unakandamizwa kwa kenda mbele kha! Eti mpaka uwe na sababu. Pole kwa kuachwa ukiwa bado unampenda mumeo wa kwanza.

Anyway hayo yamepita! Nilikaa nimeumia kwa muda wa miaka sita sikutamani tena
mwaname yoyote kwani pale nilipoishi sikupata mwaname aliemfikia ex wangu hata robo
yake kwa hiyo nikaendesha tu maisha yangu mwenyewe na watoto wangu.

Kama unavyojua jinsia hasa mwanamke ukishaolewa na kuonja utamu wa ngono,
nilifanikiwa kumpata mwaname mwingine nchi nyingine lakini alikua na asili ya nchi
yangu lakini tu alizaliwa kule. Sasa tulikubaliana kuowana na tukajaliwa kuishi
nchi ambayo niliishi mimi. Na huyu pia tulipendana sana ila kwa bahati mbaya
hakuweza kupata kazi kwani nchi hiyo ilikua na ubaguzi sana wa wageni!


Nilibahatika kushika mimba na nilitabiriwa kuwa nitazaa mtoto wa kiume
kitu ambacho kilinifanya niende ughaibuni mwa Ulaya kwani ningezaa mtoto
wa kiume nchini mwangu baada ya muda mtoto huyo angelazimika arudi
kwao kwani watoto hawafati mama! Tulikubaliana vizuri na mume wangu
na tulikua tunawasiliana kama kawaida na mapenzi yalikua mazuri tu.

Kitu cha kushangaza niliposettle huko ulaya ughaibuni mwenzangu
kanibadilikia kabisa! Namfahamisha njia za wenzie wanavyofanya
ili tuweze kuishi pamoja lakini haonyeshi interest kabisa kuja kuishi
na mimi na kisingizio eti wenzake wamemwambia maneno mengi kuhusu
mimi eti namsema na kusema namsimanga!

Na kibaya kabisa hata mtoto wake ambae toka azaliwe hajamuona, hamjali kabisa
na sasa ndio hana hata mawasiliano na nikimpigia simu anaongea
kama kalazimishwa! Nikimuandikia email hajibu!

Nimejitahidi kufuata mafunzo yangu niliyofundishwa, kwani na mie pia kabla ya hii blong
yako nilialikwa na hadi nilikua nyakanga nimejitahidi kumfanyiakila aina ya mapenzi ili kuboresha ndoa yetu, ikiweno kumsemesha maneno mazuri vitendo na hata kumvumilia na wakati mwingine hata kujifanya mtumwa kwake pia huchangia mafunzo yote
ninayoyapata kumtumia na yeye pia kama general kwani nahofia yeye ni negative thinking na hapendi kuambiwa.

Eti unamfundisha lakini mwaname habadilika kabisa! Najua ananipenda lakini anapenda kunitesa kwani nimeshadai talaka hadi nimechoka haniachi na huniignore tu pindi nikiomba talaka!

Kibaya zaidi pindi nikimwambia mapenzi au kufanya mambo mazuri huwa
haonyeshi kufurahia kabisa lakini nastahimili na kushindwa, nikilalamika
hapo ndio hujibu Bomu yaani utajuta kuzaliwa na pia mara nyingi hupenda
kujibu urgument than mapenzi.

Imefikia hata hapo nchini kwangu hataki niende na hunipa sababu zake ambazo haziniingii akilini na nikilazimisha kwenda basi atanikimbia akae mbali eti kikazi hadi siku zangu ziishe nisafiri
na nikimpigia simu au kumtext hapokei au harudishi text au kupiga simu.


Alitokea kwenda kwao hata bila ya kuniambia na mimi kwa mapenzi yangu
nilifurahi na kutaka kumfuata lakini alivyojua nataka kwenda kwanza alinambia hakai
sana amekwenda tu kibisahara kidogo, nilivyosema nitakwenda na tutarudi nchi yangu
pamoja alinikatia hata simu akawa hapokei na matokeao nikaambiwa eti
simu niliyokua nampigia imeibiwa nikaona sasa huko ndio kukataliwa.


Nikawa najaribu hadi nikafanikiwa kumpata nchini mwangu nikawa naongea
nae lakini hana mood na hata nikimwambia naumwa au mtoto anaumwa
haonyeshi kutujali kabisa!

Email anasoma lakini hajibu kwani nikimpigia
huzungumzia salam alizozipata lakini hajibu na kila mara mie tu ndio
nimpigie na mara nyingi nikimpigia anakua hana mood ya kuongea na mimi!


Nampenda saana lakini naumia nimejitahidi sasa mwaka wa tatu lakini mwaname
haonyeshi hata dalili ya kubadilika!na anadharau sijapata kuona au kusikia!
naomba ushauri ndugu yenu nifanyaje kwani sipendi kuachika
na hata nikiachika sitamani tena mwanamme kwani wanaume
unakaa nao vizuri baada ya muda wanabadilika kitu kinakufanya
unachukia maisha yako na maisha ya ndoa na mapenzi kwa ujumla!.


Nimekaa kusoma tu za wenzangu huona mengine yanazidiana na yangu
lakini mimi sina raha ya maisha na hata mtoto wangu, na kila kitu kwangu
naona hakina faida ila nasoma dini yangu lakini mara nyingi huwa katika majonzi
na kuona kama mimi sina bahati duniani na leo nimeona na mimi nipate
ushauri kutoka kwako Dinah na wengine.
Ni mimi Salha"

Dinah anasema:Salha mpendwa asante kwa kunivumilia (nimekuwa busy kimtindo).
Ni mwanamke mvumilivu sana na sina budi kukupa hongera kwa hilo. Inasikitisha huyu mume wako wa sasa anasikiliza zaidi marafiki badala ya kujali maisha yake yeye kama yeye na familia yake ambayo ni wewe na mtoto aliyezaliwa.

Kama ulivyosema ndoa ya mwanzo ilikuwa ya kiislamu, sina shaka hata hii ya sasa ni ya kiislamu. Kwa mujibu wa Imani hii ya Dini inasemekana* (usininukuhu) kuwa mwanamke ni mtu wa kukaa ndani tu na mwanaume ndio mtu wa kujishughulisha na kuhakikisha anamtimizia mkewe mahitaji yake yote.

Apart from Imani hiyo ya Dini, utafutaji, uwindaji na kumuangalia mwanamke na kumpa mahitaji yake yote au kujitahidi angalau kidogo sio lazima yawe yote, wanaume wanaamini kuwa ni jukumu lao na hii ni kutokana na EGO zao as men.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa hajisikii vema au niseme hatuko comfortable wewe kumfanyia kila kitu na yeye anakaa tu akisubiri kupewa au kuambiwa nini cha kufanya (ulipokuwa unampa mbinu za kujiunga nawe huko Ulaya) na "mwanamke" si unajua wanaume wengine na dharau zao, wanadhani wanawake zetu ni ku gossip tu na hatuna uwezo wa kujituma na kufanya mambo makubwa kimaisha na kijamii.

Sasa tatizo la huyu mume wako wala sio kubwa sana japokuwa litachukua muda mrefu kidogo kwa yeye kubadilika, tatizo lake ni kutojiamini kama mwanaume na kujishitukia kuwa anapoteza uanamme wake kwa vile wewe ni mwanamke unaejituma na kumuangalia yeye na watoto wako.

Kuna uwezekano mkubwa akawa anadhani kuwa, mumeo wa zamani ambae ni baba wa watoto wawili wa mwanzo ndio anaerekebisha mambo hapo nyumbani na yeye kama mumeo wa sasa anahisi kuwa ni useless na njia pekee ya kuonyesha uanaume wake kwako ni kwa kuwa na kiburi, m-bishi au mkorofi ndani ya uhusiano wenu.

Mwenyewe umekili kuwa anakupenda na wewe unampenda hivyo basi sio mbaya kama mtajitahidi na kuifanya ndoa hiyo kuendelea na pia kuwa bora kwakurekebisha maeneo machache ambayo mimi nadhani ndio chanzo cha yeye ku-withdraw kama mpenzi.


Kitu muhimu hapa ni ninyi wawili kushirikiana na kuwa kitu kimoja kama mke na mume na wakati huohuo wapenzi, na ili kufanikisha hili mumeo anapaswa kuacha tabia ya kusikiliza zaidi watu wengine na kujitahidi kuwaridhisha ili asionekane "anatawaliwa na mkewe".

Wanaume wengine ni wajinga wajinga, wakiona mwanaume mwenzao kapata mwanamke muhangaikaji na anajituma huwa wanapatwa na wivu na kuanza kum-feed mamneno ya uongo ili tu asifanikiwe kimaisha. Nasema hivyo kwa vile umegusia suala ya rafiki zake kusema wewe unamnyanyasa yeye. Hawa marafiki lengo lao ni kuharibu ndoa yenu na kwa vile mumeoo ana-give in upuuzi wao wewe unataeseka ndani ya ndoa yako.

Nini cha kufanya: Kwa vile umefanya yote ( kwa mujibu wa maelezo yako) nakujitahidi kumuonyesha mapenzi nakuongea nae vizuri kwa mapenzi lakini yeye haonyeshi kubadilika. Kuna uwezekano namna unavyowakilisha hoja zako sivyo ambavyo inatakiwa kwa mwanaume wa namna hiyo (asie jiamini,mwenye kiburi na dharau).

Mwanaume kama huyu ukimuibukia na issue inayokutatiza ktk mtindo wa mawasiliano na kumuonyesha mapenzi mara zote anakuona kuwa unajipendekeza kwake na kuwa uko-needy (kumbuka ni ndoa yako ya pili hivyo anadhani kuwa hutokwenda popote na utaendelea kuwa nae milele na kuvumilia upuuzi wake).

Sasa kama inawezekana wee mfuate huko kwenye nchi yake (huko anako ishi), kisha fanya nae mazungumzo kuhusu issues zote zinazokutatiza na zimekuwa zikikunyima raha kwa muda wa miaka mitatu sasa. Wakati unawakilisha hoja zako hakikisha hubembelezi na wakati huohuo humfokei (usiwe na hasira) na badala yake kuwa firm.

PSSST**Kwa vile hamjaonana kwa muda mrefu anaweza kutanga Ngono, hakikisha ukimpa usimfanyie mautundu yako yote au hata kama unavipya na badala yake kuwa mvivu-mvivu hivi, sio sana ila hakikisha unajifikiria wewe zaidi na sio yeye linapokuja suala la kupata utamu/kilele.**

Sasa kuna sheria za kuwakilisha hoja au issues zinazokutatiza kwenye ndoa au uhusiano wa kimapenzi kwa mujibu wa aliyenifunza nayo ni (1)-Vizia siku ambayo mumeo hayuko moody na tengeneza mazingira mazuri (badilisha mpangilio wa vitundani, ongeza/punguza mapembo.

(2)-Anza kwa kuelezea hisia zako juu yake, umuhimu wenu kwa watoto na namna gani basi watoto wote wanavyo muhitaji kama baba (hii itamfanya asihisi kuwa anatengwa na watoto wa ex mumeo)

(3)-Kumbushia maisha yenu ya kimapenzi mlivyokuwa mkianzana na jinsi gani ulikuwa unafurahia na kiasii gani basi unakosa hayo yote. Mueleze namna gani unajisikia kila unapozungumza nae na hisia hizo zinavyozidi kila mnapokuwa pamoja.

Mwambie kuhusu hisia zako dhidi ya marafiki zake, sio kwamba unawachukia lakini unahisi kuwa wanachukua nafasi yako...kwamba mumeo anafanya maamuzi kwa kufuata marafiki zake na sio wewe mkewe.

(4)-Muulize ni kitu gani hasa kinamuudhi kuhusu wewe? na ni kitu gani hakipendi kuhusu uhusiano wenu pia angependa kubadilisha nini ikiwa atapewa nafansi ya kubadili kitu kuhusu uhusiano wenu na ndoa kwa ujumla......mara nyingi hii itamfaya na yeye akuulize maswali hayo hayo kitu ambacho ndio unakihitaji.

(5)-Kumbuka kumpa nafasi ya kujieleza ikiwa anataka kufanya hivyo, usilazimishe aseme kitu kama haonyeshio kufanya hivyo (hapa inamaa unayosema yanamuingia taratibu).

(6)-Fikiri huku unaasikiliza maelezo yake na wakati huo huo kuelewa. Kwamwe usiongee wakati yeye anajieleza na ikiwa yeye ataingilia wakati unajieleza kaa kimya na umsikilize lakini kumbuka kufikiri huku unaongea/sikiliza hii itasaidia kuepusha mabishao.

(7)-Kamwe usionyeshe Kiburi wala usimuonyeshe kuwa unamuhitaji sana hata kama ni kweli unamuhitaji, mdhihilishie kuwa wewe ni mwanamke unaejiamini na unaweza kuendesha maisha bila mwanaume lakini huwezi kuzuia moyo wako kupenda, na mtu pekee unampenda ni yeye mumeo. Hivyo humuhitaji (as in need) bali unataka awepo kwenye maisha yako na watoto wako.

(8)-Sasa mueleze yote yalioujaza moyo wako, kumbuka kutokulalamika, kubembeleza, kulaumu, wala ku-demand na kubwa kabisa hakuna kuonyesha mapenzi.....mpe straight face na tazama macho yake....this is your moment inaweza kubadilisha mwenendo mzika wa ndoa yako.

(9)-Mara tu baada ya maongezi kuisha usionyeshe ile "straight face" na badala yake kuwa more loving na ikitokea anataka mambo fulani huu ndio wakati wa kumuonyesha zile vitu adimu, ambavyo hawezi kuvipata ovyo-ovyo.

(10)-Badilisha mtindo wa maisha yako, you are only 28 hivyo bado mdogo na unaweza kuwa bonge la sista duu kwa maana ya mavazi na kujipenda (sio lazima uvae nguo za ajabu ajabu unawez akuvaa kufuatana na Imani yako ya Dini lakini ukavutia nakupendeza). Hakikisha unavutia kuliko ilivyo sasa.

Ibua interest mpya, mfano kufanya mazoezi ili kuweka mwili wako vema zaidi na utavutia zaidi ukiwa mtupu, valia nguzo za ndani zenye mvuto, ongeza ubunifu kwenye mapishi yako n.k

Endelea namtindo huu mpya wa kimaisha na baada ya wiki chache utaona mabadiliko......lakini kama haitatokea ndani ya wiki chache (nazungumiza kati ya wiki 2-miezi 3) basi itakuwa ni wakati muafaka kupata msaada kutoka kwa wale waliowafungisha ndoa.

Kila la kheri!

10 comments:

Anonymous said...

Pole sana Salha, na sote tunaosoma blogi hii tumuombee huyu mwanamama,kwani ni baadhi ya akina mama wachache wenye upendo wa dhati,lakini wanapenda kusipopendeka,mungu akujalie uyashinde hayo majaribu, na pendo lako lizae upendowa dhati.
Kuna usemi unaosema `kila jambo hutokea kwaminajili’ huu usemi tunausikia lakini una maana kubwa sana. Usemi huu hutufundisha subira, unatufundisha kuwa kila tukio hutokea, sio tu limetokea,lakini mwenyezi amelitoa, likatokea kwako kwasababu maalumu, unachotakiwa ni kumuomba na kuvuta subira.Hujui kwanini kafanya hivyo!
Katika historia ya mapenzi, kama utakaa usikilize watu zaidi ya kumi utapata picha ya ajabu, kuwa `yule ambaye ulidhani, kumbe siye’ na niwachache walioangukia kule walikokutaka. Hii ina maana kwamba ukifikiria hivi, kumbe mwenyezi sivyo alivyokupangia, yeye anakujua na anajua zaidi unachokitaka kuliko wewe.
Siri ya mapenzi ni kupenda na wewe upendwe, ikiwa kinyume chake ni machungu. Je kama umependa na hujapendwa ufanyeje?Na je hujui kuwa wapo wanaokupenda lakini huwapendi? Hili swali ni tete, na kila mmoja anajibu lake kutegemeana na mazoea au anavyotaka yeye. Je umuache, ukimuacha roho inaumia! Swali hapa je ni nani alisema huyo ndiye peke yake hapa duniani, je unauhakika gani kama akikupenda mtadumu naye milele? Jibu ni hisia zetu tu.
Mwanamama kwa ushauri wangu mdogo,ningekushauri , uvute subira, ukae bila mawasiliano naye kwa muda, huku ukufanya ibada, huku ukimjali mwanao , na huku ukikusanya nguvu na kujiweka katika hali nzuri. Nasema hali nzuri nikiwa na maana,jiweke `kiusichana’, usijiachie mwili ukazidi uzuri.
Baada ya muda kidogo, kama huyu jamaa anakupenda ataanza kuingiwa na wivu, atakutafuta, na akianza kukutafuta jifanye hamnazo, baadaye mualike muonane. Hamadi, akikuona ulivyopendeza, ulivyobadilika, atahisi `laaah nimeibiwa’, ataanza mapenzi ya kuhamaki, nawe iwe ndio umeanza, jikwatue jirembe na muweke sawa,lakini kwa safari hii,uwe kama unauma na kupuliza, yaani unajifanya kama vile hutaki.
Vinginevyo, vuta subira na muachie muweza, asikuambie mtu kuwa huyo unayempenda yupo peke yake, wapo wanapendeka na watakaokupenda zaidi ya huyo,na huenda ndio maana Mwenyezi anakukwepesha na hao ili umpate yule aliyekukadiria, na siku ukimpata utsema, `oh, ningelijua mapema kuwa wewe ndiye mahububu wangu, ningekutafua duniani kote…
emu-three

Anonymous said...

Emu three umeniliza sio siri yani maneno yako yamenitoa machozi kivipi basi, tatizo la salha ni sawa sawa na mm isipokua mwenzangu yy ana ndoa mm sina na pia nilishawahi kutoka hapa kwenye blog ya dada dina, jamani mapenzi yanauwa yanasononesha yanataabisha tena hasa kwa mtu uliyempenda eeh mungu mapenzi umeyaleta lakini yanatutaabisha wengine wallah. sio siri mm nimejaaliwa mapenzi mengi kwa ninae mpenda lakini ninae mpenda ndie sie laiti angejua jinsi gani ninavyotaabika juu yake wacha tu, well mm niliacha nikawa simpigii simu mana nalia peke yangu mpaka nimekua sugu. sasa basi yeye huyo bwana akanipigia simu siku hiyo anasema mbona uko kimyaa umpendae hajambo??unanipenda kweli si nikajiachia hapo nikamuuleza jinsi ninavyotabika kwake nikajua at least atabadilika. ndio kachochea sasa siku iliyofuata nikampigia simu hakupokea kabisaaaa usiku nikamtumia msg kimyaaa sasa hapa me mwenzenu sielewi kabisa amepanga kuni enjoy?amepanga kuniadhibu?amepanga kunidhalilisha na kwann ana umia nisimpompigia??na kwann nikimpigia ana crush simu eeeh mungu haya ni mapnz au ni adhabu??nimechoka mimi na sio kama sitongozwi ni nyuki wanaume wanao ni approach lakini moyo wangu nimemtundikia yeye huyu mwenye kunitesa nampenda sanaa jamani

Anonymous said...

Dada kwani uko wapi?una jinsi tukawasiliana nje ya hapa?

Anonymous said...

Dear Emu three mbona umemjibu mwenzio vizuri namna hii yaani unajua kujibu sana! Je umesomea wapi au dada Dinah amekupa kozi! kwani kuna wengine huwa hawajui vipi mume anauma na hujijibia tu kumbe mwenzetu anapoamua kuingia katika uwanja huu huwa amefikwa kooni sasa sisi wajibu wetu ni kumliwaza kama ulivyojibu Um three hongera ngoja tuone na profesor Dinah atajibu nini na wengine.Kitu ninachowaomba ndugu zangu tumpe dua na moyo huyu dada ili aweze kuupita huu mtihani na Mnyezi Mungu atamvusha inshallah na kupata furaha kama mwanzo maana hana raha ya mtoto wake na hata maisha! Jamani wengine wanatamani wapate wanawake kama hawa na wengine hawajali.Pole dada Salha na mimi pia nakuombea dua ila si mjuzi saana wa kutoa ushauri ila subiri na fata ushauri wa Um three na pia nategemea Dinah atakupa tu ushauri mzuri utahisi tu furaha ya maisha japo umeumia sana. Pole dada Salha na Goodlucky.

Anonymous said...

Hey mdada,

Kusema ukweli mimi umenichanganyas mno, kwa kisa cvhako na huyo jamaa yako.

Kwanza umetueleza na kukusisitiza sana kwamba jamaa lina kiburi na dharau ambavyo hujapata kuona.hapohapo unasema jamaa unalipenda na kulihusudu sana.Huo upendo nashindwa kuubaini unajikita katika nini hasa?kwa umbile lake au kipato chake au kwa sababu anatoka nchi unayoijua mwenyeewe?Unawezaje uendelee kumvumilia na kumpenda mtu mwenye jeuri, dharau, na kiburi?Je, kwa sifa yake hiyo atafaa kweli kukujali na kukuthamini poor mama?

Kwa nini mnataabika na wanaume wajeuri na kuendelea kuteseka kwa sababu ya mwanadamu mwenzio aliyeamua kukufanyia ufidhuri wote huo?hao wanaume kweli wameisha , na hivi ni lazima kwa mama kama wewe umeonja ndoa mara mbili tena uendelee kuteswa katika ndoa badala ya kuachana endelea kusaka maisha yako yasiyokutesa akilini?

Uking'ang'ana na kitu mapenzi,kitakuua kabisa kifikra na kijinsia.Msiba wa mapenzi usiusogeze karibu nawe.Kwepa sana mtu anayekufanyia jeuri, na dharau.Huko ughaibuni uliko bado hujajifunza jambo unazidi kuteswa na jamaa lako hilo?Mimi niko ughaibuni nakushangaa unazidi kukonda na jamaa asiye na hata element moja ya kukujali na kumjali mtoto wake mwenyewe aliyemzaa.

Jamani dada zangu ndoa ni nzuri unapokuwa na mtu mnayeweza kuelewana, kuzungumza, kuwasiliana n.k sasa jamaa linakutosa hivyo bado upo beneti kulisaka,la nini mama?kama ni kutaka kutombwa basi tafuta njia mbadala isiyotesa na kukuangamizia maisha yako.Hujui hata liko pekee linakula wapi labda lina mke mwingine?nini unategemea dada yangu.Wewe kimbia mdada si salama hapo!!!!

Anonymous said...

Dear ma sister
kwakweli kisa chako kimenigusa sana tena mno. Ushauri wangu ni kwamba naomba ushikamane na ushauri wa emu3.
Kumbuka kwa uwezo wa Jalali mtihani huo utakuwa mwepes, kwani heri na shari vyote vyatoka kwake, na kupata na kukosa vyote ni mtihani. Muombe Mola kwani amesitiza sana kuwa yupo na wenye kusubiri basi nawe usihuzunike bali ushukuru na wala usikufuru kwa maana furaha ipo jirani nayo inakuja Inshaallah.
Mwatima

Anonymous said...

dear Salha, pole dear na mtihani uliokukuta.Kazana kufata ushauri mzuri na mbaya waachie wenyewe kwani kwenye ndoa ni kupigania mapenzi na maisha hasa ya watoto kuwa pamoja na wazazi wao na wewe kama ulivyosema kuwa umeomba talaka sana lakini mume hakuachi hii inaonyesha kuwa na yeye anakupenda ila tu kiburi kimemshika. Na wengi hufikiria unyumba ni kutombana tu siyo hivyo halafu wewe ni bado mke wa mtu na isitoshe dini ya kiislam inakataza sana mambo ya zina hasa mke wa mtu adhabu yake ni kubwa siyo kama ya mjane so dear vumilia tu.

mie pia yalinikuta kama wewe na najua ukiwa umempenda mtu na anakufanyia visa au ujeuri unakua hata hiyo feelings ya kutombwa unakua huna.

Jamani tumpe moyo huyo dada kwani sidhani kama ana hata hizo nyege kwa sasa maana amesema hata mtoto wake mwenyewe hana raha nae na maisha pia sasa hizo nyege jamani zitoke wapi. Dada Salha wewe cool to down na mumeo atarudi kama mke wa mwenzetu asif Goodlucky Mungu yupo na wewe just sali saana na ondoa mawazo fata tu ibada yako na mashauri wazuri ndio uyaweke akilini hopeful utasahau na kufanikiwa tu

jj said...

Pole sana dada kwa yaliyokukuta na bado yanaendelea kukuta. Sio siri hilo si lako peke yako mpenzi hata mimi yamenikuta, mimi bado ni binti yaani sijaolewa lakini yamenikuta si chini ya mara tatu. yaani naweza nikaa na kusema sipendi tena lakini kila nikitoa chance kwa mtu nakuta ni long person.

Nimeamua kumkabidhi kila kitu mwenyezi mungu maana yeye ndo ananijua vizuri na ninajua atanipa aliye wangu siku moja.
Dada yangu mtangulize mungu katika hilo jaribu lako maana hilo ndo jaribu alilokupa, dada kama huyo ni wako atajirekebisha tu na kurudi na kama si wako basi atakuonyesha aliye wako na kukuepusha na hao matapeli wa mapenzi. Natumai mungu anaona mateso yako ya kupenda asiyekupenda na very soon atakupa chaguo lako

Anonymous said...

Mama pole sana, naomba Mungu wangu akusaidie,akupiganie akushike na mkono wa kuume wa haki yake akuongoze katka njia ikupasayo kuiendea kwani furaha yakwel ipo kwake tu. Napenda kukushaur,wewe ni mama mwenye watoto naona ni bora utulie utafute namna yakulea watoto wako,ondoa wazo la mapenz kwasasa,try to relax, mimi nimetendwa like that na mtu niliyempenda,sijaacha kumpenda lakini so long hanithamini nakunitenda jeur,nimeamua kurelax na nipo cool ajabu nimejiona name wathamani sistahi5 ukatil wako,kwahyo mama tulia walee watoto Mungu atakuonyesha njia aliahid atatufanyia mlango wakutokea katka hayo matatzo mwombe.
Asante, Mungu akusaidie.

Anonymous said...

Dear Dina nimefurahi sana kwa kunijibu vizuri na umegusia vitu vingi vya kweli.Lakini kuhusu mambo ya talaka kwa wanaume watu wa dini ya kiislam madamu mwaname ameshakuacha wao hawawezi kulazimisha kwani Mungu mwenyewe halazimishi kitu na kuhusu mwanamke haachishwi kwa sababu wanataka kuinusuru ndoa isitoshe mwanamke siyo anaeacha hivyo akiwaendea watu wa dini hutaka kujua sababu kabla hawajaamua kumuachisha kwani talaka ni halali iliyochukiliwa na Mungu hadi ikiwa na sababu yake.

Watu wa kupatanisha ni familiya zote mbili lakini ikiwa moja imekubaliana na mfano mtoto au ndugu yao kwa hiyo hasa ya kike haiwezi kulazimisha kwanza ni kama kitu cha aibu mtoto wenu hatakiwi nyinyi mnataka tu je akimtese mtafanyaje?!

Tuyaache kama ulivyosema yamepita si ndwele ila nilitaka tu kukufahamisha kuwa wao wanafata sheria za dini ilivyoamrisha.

Kuhusu huyu mume2 yeye wala hahisi kabisa kuwa wa kwanza ananihudumia kwani tumekaa muda na pia alinijua mwenyewe nilikua na uwezo mzuri tu wa kurekebisha mambo. Pia wanaume mara nyingi hata kama mlipendana lakini hasa akikuacha yeye isitoshe kwa ajili ya mwingine hawezi tena kukujali ila watoto wake na mimi sipo na hao watoto wetu so hanihudumii kabisa na mume wangu ana uhakika kuwa hanihudumii na nilipo anajua tu mambo yangu safi kabisa namshukuru Mungu.

Sasa nashukuru kwa kunipa moyo na pia kuniambia kuwa siyo jambo kubwa na kuwa atarudi lakini dear mbona hujanipa ushari kitu gani cha kufanya mimi nakutegemea wewe si unajua tena msusi hajisuki sikuombei hata wewe na usomo wako lakini yakikufika hasa ya mapenzi nadhani utapagawa tu na kutafuta ushauri so na mie naomba unifahamishe kipi cha kufanya!

Believe me japo strong na sala zote lakin bilisi pia yupo karibu naumia na kukata tamaa na pia nahofia afya yangu si unajua tena kitu kupenda! Halafu alivyo mjeuri sidhani kama ataanza kuwasiliana na mimi hata baada ya miaka kumi! Yeye ni mtu asiye na haraka ya maisha pia alipata kunambia Mungu apishe mbali kitu chochote kikitokea means talaka baina yetu yeye atajitahidi na maisha baadae aangalie mtoto wake tu. Kwa kifupi alishaacha mke na hakuwa na tamaa tena ya kuoa kwa yaliotokea!tulipokutana tulidhani tabia zimemech ndio tukaowana kweli zilimech lakini maisha siyo yeye hasa ya mtoto!

Namuamini hanicheat na wala hana mwanamke mwingine na anaishi kwao hilo sina shaka nalo.Pia nadeal vizuri tu na wazee na ndugu zake ila siwezi kuwazungumzia kuhusu yaliotokea sasa hawatoamini pia kwani tukiwa pamoja kabla ya kunikimbia mara ya mwisho tulikua kama ndio kwanza tunaowana na hata watu kusema sisi always tupo honeymoon!

Sipendi family wajue kwani tutawapa shock na mara nyingine ndio inakua mwanzo wa matatizo!

Nasema hivi kwani ilinitokea ndoa yangu ya mwanzo na alipotaka kuoa mwingine wazee wake walifurahia kwa kujua tulikua na matatizo hawakushtuka. Dina si unajua kila mtu anakua kwa mtoto wake na mnapokua mnafuraha ndio wanawafurahia wote au siyo? So dear naomba ushauri means cha kufanya I am already crazy!! Sijui kuhusu yeye kwani sina mawasiliano muda hivi lakini nahisi wote ni kisebu sebu na kiroho.....! Wee acha tu kitu mapenzi!