He's too busy kuwa na mimi, nampenda-anipenda-Ushauri

"Hi dinah,

Mimi ni msichana wa miaka 27, nina mpenzi ambaye tulianza mahusiano yetu tangu 2007. Tulipoanza mapenzi yetu yalikuwa motomoto, tulionana mara kwa mara na tulielewana vizuri tu. Ilifikia mahali na kunitamkia kwamba ifikapo October 2009 tutafunga ndoa.

Kwa kweli nilifurahi sana, kwasababu ni mtu ambaye ananijali sana. Chakushangaza kadri siku zinapozidi kwenda amekuwa bize sana na promises zimekuwa nyingi. Tunapopanga kuonana au kutoka out mara nyingi hatokei, nikimtumia sms anaweza asijibu kabisa, then baadaye anatoa sababu zisizokuwa za msingi na kusisitiza kwamba bado ananipenda sana.

Isitoshe sijamuuliza kuhusu ahadi aliyoitoa ya ndoa maana naona kama nitamforce. Kwa kweli naumia sana moyoni kwa sababu hana muda na mimi yuko bize kupita kiasi, lakini anadai ananipenda.

Sitaki kumjibu vibaya wala kumtamkia its over kwasababu nampenda nataka aje kuwa baba watoto wangu lakini ananiumiza kwa sababu ya the way he treats me. Naomba ushauri wako kwasababu kuna kitu kimenikaa moyoni nashindwa hata la kufanya.

Nimejitahidi kukaa kimya lakini wapi bado ananipigia simu na kunitumia sms bado kuwa bado
ananipenda. Sasa najiuliza mapenzi gani haya wakati mtu mwenyewe hana muda na mimi, muda wote ni wakazi ambayo anafanya hapahapa Dar.

Ni mimi mdau,
mery."

Dinah anasema: Hello Mery, asante kwa mail na ufafanuzi kuhusu umri wa mpenzi wako ambao hakika ni umri ambao vijana wehu huanza kutulia kiakili (anakaribia miaka 31). Nakubaliana na wewe kwenye swali la "mapenzi gani haya wakati yeye hana muda na mimi?".

Kutokana na tabia yake (kwa mujibu wa maelezo yako) kuna mawili-matatu yanawezekana:-
(1)-Inawezekana ni kweli anashughuli nyingi za kikazi zinazomzuia kukutana na wewe.

(2)-Vilevile kuna uwezekano mkubwa tu kuwa anaendesha maisha kivingine na anakuweka wewe kama spare tire incase huko aliko hakutokwenda atakavyo.

(3)-Hana mpango wa kuwa na wewe tena ila hajui namna gani ya kumaliza uhusiano hivyo anafanya hivyo ili wewe ukate tamaa na uchoke kumsubiri na hivyo u call it a day.

Kwanini basi nimedhania hivyo? Kwa sababu huyu bwana alikutamkia kuwa atakuoa au mtafunga ndoa mwezi wa Kumi mwaka huu lakini hakuchukua hatua zozote zinazoendana na matamshi yake Mf-Kujitambulisha kwenu na kupewa utaratiubu wa kufunga ndoa na wewe na hatimae kuanza maandalizi...mwezi Octoba sio mbali na nijuavyo mie maandalizi ya kufunga ndoa hasa kwa kufuata taratibu za kijamii Tanzania huchukua muda mrefu.

Kwenye uhusiano wenu kuna ukosefu wa mawasiliano, kwa maana kwamba hamzungumzii maisha yenu kama wapenzi kwa uwazi, wewe unadhani kuzungumzia ahadi yake ni kama kumlazimisha na yeye huenda anahisi kutokuzungumzia kwako suala la ndoa ni dalili kuwa huna mpango wa kuolewa nae au hauko tayari.

Unajua, kuna tofauti ya kati ya kukumbushia jambo ktk mtindo wa kuzungumza na kukumbushia jambo hilohilo ktk mtindo wa kudai/lazimisha (demand).....napata picha hapa kuwa hukujua tofauti hizo na wewe ukadhania kuwa kukumbushia ni ku demand yeye afunge ndoa nawe.

Nini cha kufanya: Kwa unampenda mpenzi wako na unaamini kuwa na yeye anakupenda lakini kwa bahati mbaya hatujui ni nini hasa kinasababisha yeye kuwa hivyo alivyo, fuata haya nitakayokueleza ili kupata ukweli utakao kusaidia kufanya uamuzi wa busara....

Naja midaz....

Comments

Anonymous said…
Pole sana mdogo wangu dear kwa nini una haraka mbona bado mdogo tu usiumie roho kuanzia sasa kwani bado kuna mengi pindi ukiolewa sikutishi lakini ndio kawaida na mimi nimetoka huko huko nilipendana sana na wapenzi wangu lakini baada ya ndoa lazima wanabadilika huo ndio uanaume!

Kitu cha kufanya ni kama vile wote tunavyopewa ushauri inabidi ujikaze ukae kimya na kutizama mambo mengine ya muhim pia jaribu kujikaza japo unampenda ujikaushe madam anasema anakupenda na mara nyingine na wewe ujifanye upo busy japo kwa mambo tu ya outing japo kwa shoga zako hapo ndio utaona kama kweli na yeye anakupenda kikweli au siyo.

Ila kuhusu ndoa ni bora usipush sana kwani mara nyingi mapenzi ya uchumba huwa matamu sana kuliko ya ndoa believe! na pia elewa kuwa ndoa imeandikwa kwa Mungu kwa hiyo siku ikifika imefika na kama Mungu kakuandikia awe baba wa watoto wako atakua tu usiwe na wasi wasi na kama Mungu hakuandika utapata baba bora aliekuwa siyo busy atakae kuwa sana na wewe na kuwashughulikia watoto wake pia.

Sasa kama kuanzia sasa yupo busy na mkiowana mambo yatazidi ya nyumba na watoto itakuwaje! Fikiria mdogo wangu na usijiumize na mapenzi kuanzia sasa kwani Kilichoandikwa na Mungu hakiweza kufutika so wewe subiri na kubaliana nae pindi akikwambia anakupenda kwani mapenzi ni pande zote mbili siyo upande mmoja.

Nakutakia kila la kheir na good lucky kwa huyo au mwingine alie bora zaidi wa kukujali wewe na watoto wenu hopeful.
Anonymous said…
Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapo, je huyu rafikiyo anafanya kazi gani, kwasababu kuna aina za kazi ambazo zinaweza zikamkwaza mtu kiasi kwamba kwa vile hamjaoana akazipa kipaumbele kwanza.
Lakini pia kuna watu wanaimani zao kuwa kuzoeana sana kabla ya ndoa kunaondoa hamu mapema, hizo ni imani za baadhi ya watu, na zinaenda zaidi ya kusema, `ukimzoesha mwenzako hivi na hivi na vile mapema, siku mkioana utapata shida kwani atavidai na wewe ukasindwa kuvitimiza'. Hizo ni hisia na zipo kwa baadhi yetu.
Mimi kwa ushauri wangu, ni wewe kutokata tamaa, na hilo la yeye kuwa busy isiwe kigezo cha kukukatisha tamaa, kama kweli unampenda. Muda mchache utakaokuwa naye utumie vyema kuweka malengo yake na yeye. Anza kumuonyesha kuwa unajali anachokifanya huku na wewe unatoa mapendekezo yako, hasa la ndoa, kwasababu hujui kwanini yupo busy kiasi hicho.
Lingine ni kuwa na subira, subira katika kila kitu ni muhimu,pupa inapupisha na kuharibu kile kilichochema. Jiwekee malengo yako,kamilisha malengo yako ambayo yanaweza kukusaidia baadaye kabla hamjaingia kwenye ndoa, hii itakusaidia kupunguza mawazo.
Nakutakia kila-laheri na mungu atakusaidia, kwani ukimuombaa hakunyimi ila inakupa apendavyo na sisi mara nyingi hatujui hekima yake!
emu-three
Anonymous said…
VUMILIA BINTI MIHARAKA YA NINI?KAMA JAMAA YAKO ANAKUAMBIA ANAKUPENDA SASA YA NINI MIKELELE TENA?JE UNAWEZA KUTUAMBIA KAZI YAKE ILI TUJUE NATURE YA KAZI YAKE TUONE KAMA INAMKEEP BUSY JAMAA?

HUYO MPENZIO NI MUUNGWANA USIWE NA KIWEWE CHA KUONANA NAYE KILA WAKATI KWANI SASA NI WAKATI WA KUSAKA MAISHA YENU.INAWEZEKANA TATIZO LAKO NI KULE KUTOMBWA KWAMBA HUIPATI MBOO YA JAMAA KARIBUKARIBU HIVYO UNAONA SHIDA.

MAMBO YA NDOA NI TARATIBU USIWE NA HARAKA YASIJEKUKUTOKEA PUANI.NAKUSIHI UWE MVUMILIVU HADI JAMAA TAKAPOKUJA RASMI MAMBO YATAJIPA.MUHIMU NI MAWASILIANO TU KAMA YAPO NA JAMAA ANAKUPA UKWELI WA JINSI ANAVYOKUPENDA ACHANA NA KELELE USIJE UKAMWANGA UNGA PENYE KUKU WENGI.AKIJUA UNALALAMA ATAKUTEMA MAANA HIYO ITAMTHIBITISHIA KUWA WEWE NI MPIGA KELELE TU HUFAI KUWA MKE.
Anonymous said…
Daer pole sana kwa yaliyokukuta.
kama yupo bz jua kuna kimada ambacho yupo nacho bz haiwezekani mwanzo mapenzi ya noge alafu ghafla ubiz uanze ina maana bado hauja shtuka kwamba kuna mwenzako ambaye tayari anakurithi taratibu kama bado haujaona endelea kwa muda kidogo alafu unanipa matokeo ananza kidogo kidogo mwishoe hatokuwa na mawasiliano nawe tena.

Chamsingi wewe msikilizie tuu jinsi anavyoendelea na tabia yake na jaribu sana kumchunguza kwamba dear mbona mapenzi yetu yalikuwa mazuri iweje sasa umebadilika kiasi kwamba sikuelewi ukiona anajibu mbovu jua mapenzi kayaelekeza kwingine alafu achana naye kabisa asije kukusababishia magonjwa ya ajabu.
Anonymous said…
pole sana dear usiwe na wasiwasi inawezekana huyo mpenzi wako anakupena sana ila kutokana na kazi anayoifanya labda anakua busy kiasi kwamba mnashindwa kuwa pamoja mara kwa mara kinachotakiwa hapo ni kuwa na uvumilivu na kumuonyesha upendo kuna kipindi atapunguza majukumu na mtakua mnadumisha uhusiano wenu