Wednesday, 13 May 2009

Ndoa imenishinda, Mume anitaka tena-Ushauri!

"Dada dinah! Baada ya kusoma blogu yako na kuona unawasaidia wengi nami leo nimeamua kuandika mkasa wangu. Mimi nina umri wa miaka 28 nimeolewa miaka minne iliyopita na kwenye ndoa yetu tumebahatika kupata mtoto mmoja wa kike.


Dada dinah kabla ya kuoana na mume wangu tulikuwa wachumba kwa takriban miaka minne, kwenye kipindi cha uchumba ni mwaka mmoja tu ndo tuliishi kwa mapenzi ya kweli na raha za kila aina mwaka uliofuata akaanza visa, mara namfuma na msg za wanawake nikimuuliza anakuwa mkali, nikienda kwake nakutavipodozi au nguo za ndani nilizoacha zimefichwa.


Dada dinah mapenzi yakawa hayapo tena, naweza nikakaa wiki mbili sijaenda kwake na siku nikienda yeye amechoka na hataki tufanye chochote. Kuna siku nilienda akanikatalia tusifanye kitu, kesho yake asubuhi nikawa nafanya usafi wa nafagia nje nikakuta mfuko ndani kuna condom 3 zilizotumika.


Nilisikia kufa nikaziweka kitandani nikaacha kufanya usafi nikaondoka kwa hasira. Aliporudi alipozikuta akaanza kupiga simu na kuomba msamaha, kwa kuwa bado nilikuwa nampenda yakaisha. Lakini tabia hiyo iliendelea na nilipozidi kumbana akatamka kwamba hatujaoana kwahiyo bado anachagua yupi atakayemfaa kuwa mke kwa kweli niliumia sana na mapenzi yakaanza kupungua.


Ikafikia mahali nikawa nasikia tetesi kwa majirani anavyobadili wanawake kama haitoshi akatembea na rafiki yangu nilipojua hilo kwa kweli nikaamua kuachana nae. Alikiri na kuomba msamaha lakini ilikuwa nimeshachoshwa nae, akawa anaomba msamaha sana na kunibembeleza kwa bahati mbaya nikaja kushika ujauzito wake. Alipojua akaanza kuharakisha kufunga ndoa na kunisihi nisitoe.

Kama binadamu nikamuua kusamehe na tukafunga ndoa 2005, nikajua atabadilika ktk ndoa lakini wapi mambo yakawa yaleyale kufuma msg, akisafiri nakuta condom kwenye begi kasahau, mbaya zaidi akaanza manyanyaso na kashfa ndani ya nyumba na vipigo bila sababu za msingi.


Nikaamua kuvumilia nilee mtoto, Mungu amenisaidia mwanangu ana miaka mitatu sasa na nimebahatika kupata kazi kwenye Shirika moja nje ya Dar nikaamua kuondoka na nimeanza maisha mapya. Kwa kweli mapenzi naye yameisha kabisa hata yale ya kujilazimisha.

Sasa anaomba msamaha nirudi atajirekebisha na kwa mwezi anakuja mara 3. Jamani mie nimechoka kurudi siwezi na ninamuogopa saana kukutana nae kimwili kwa tabia zake tusijepeana maradhi huwa namsihi tutumie condom hataki.

Mie nimeamua kuachana nae kabisa na yeye nimemwambia lakini anazidi kuomba msamaha na kukiri makosa yake na anahidi kujirekebisha, kaahidi mpaka kuninunulia gari nimsamehe. Jamani hebu mnishauri mie nimechoka nae na sitaki kurudiana nae maisha nayoishi sasa ni ya amani sana."

Jawabu: Hongera sana kwa hatua uliyoichukua na msimamo unaoendelea nao. Inasikitisha kuona kwamba kile kipindi ambacho watu ndio hufurahia zaidi wewe ulikutana na vituko vingi kuliko umri uliokuwa nao kipindi hicho.

Nashindwa kujizuia kufikiria kuwa ulikubali kufunga ndoa kwa vile tu ulikuwa na Mimba, kama isingekuwa mimba labda usingeolewa nae.....kwa bahati mbaya hatuwezi kubadili yaliyokwisha tokea.

Kwa kawaida wanandoa huwa wanashauriwa kuto kuachana au kuvunja ndoa, hata mimi sipendi kabisa kuharibu ndoa au uhusiano lakini ikiwa mhusika anahatarisha maisha yako basi inabidi ndoa ivunjike tu ili kuokoa maisha yako.

Kuachana nae kienyeji tu haitomfanya aache kukusumbua. Suala muhimu ni kutafuta Wanasheria wanajihusiaha na masuala ya Ndoa na Talaka kwa msaada zaidi ili umtaliki mumeo kisheria kitu kitakachomuondolea "mamlaka" anayodhani anayo juu yako kwa vile tu mlifunga ndoa.

Kama unapata taabu kuwapata Wanasheria (najua Wakibongo wanamaringo sana, watakuzunguusha weee), unaweza kutembelea Mahakama yeyote iliyokaribu na wewe na kuomba kuonana na Jaji na kumueleza nia yako ya kumtaliki mumeo na sababu ya kutaka kufanya hivyo.


Yeye atakuuliza maswali machache kama vile, mara ya mwisho kufanya mapenzi ilikuwa lini? Sasa anaishi wapi? na wewe unaishi wapi? Mmetengena kwa muda gani? pia unaweza kuulizwa kama unaweza kumudu mahitaji ya mtoto n.k. kisha utapatiwa barua ya kumulika mumeo hapo Mahakamani ili wasikilize upande wake wa "hadithi".....haijalishi hata kama atatoa machozi ya damu na kuomba misamaha yote hakikisha unabaki na msimamo wako, kuwa ndoa imekushinda kutokana na tabia yake chafu.


Pamoja na kuwa wewe na soon Ex mume wako mnatofauti na hutaki kubaki kwenye ndoa, hakikisha mtoto anakuwa na uhusiano mzuri na baba yake. Kamwe usim-feed mtoto wako na uchafu aliokuwa anaufanya baba'ke, kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha Binti yako kujenga chuki na baba yake kitu ambacho nisingeshauri.

Kila la kheri!

11 comments:

Anonymous said...

Hadithi yako dada ni kama ya kwangu. Kweli huyu nimjuae anashinda akiinsist mambo ya ndoa na kuomba msamaha. Mimi nishamsamehe kwa kauli niwezavyo, na ilibidi nimwombe Mungu anisaidie kumsamehe maana nilikuwa naumwa sana. Sasa hivi huwa ninasali kila siku na kuomba iliuhusiano uvunjike kabisa. Ninamaana nikiamka na kurudi kulala kila kitu kinachonikumbusha yeye kiwekimeangamizwa kabisa. Nasema na akili yangu yote, pamoja na roho yangu, na moyo wangu, na utu wangu wote, sitaki uhusiano tena tena tena. Kwa vile tabia yake ilikuwa pamoja na uwongo mwingi, sina uhakika kama kuna wakati anajipooza moyo kwa maana watu kama hawa huwa wanafarijika wakisha succeed kwa vitendo vyao na kusema nilijua ninaweza, ukweli ni sina nia naye. Kwa kweli ikiwa anaumia ya kweli, yangu ni kumwonea huruma, maana sina njia ya kumsaidia hata chembe. Najua nilikuwa hivyo hivyo bila wa kunipa pole. Sasa kwa sababu yeye bado ana wengi wa kuchagua, hatapata shida mbeleni. Nikiamua kuolewa na kuanza familia, itabidi aseme acha basi nimchukue nani angalau nami pia nianze familia. Kwa hivyo sio kama hana kabisa. UKweli wote, na ushahidi wangu ni mmoja, siwezi kurudiana nae na sitaki. Ingekuwa vyema ikiwa angeendelea na maisha yake, amchague yule ambae anaempenda kama almasi. Mimi na huyu tupendanao kama udongo tujifariji na kidogo tulichonacho. The little I have now is more precious than the tones I was promised in deception.
Kwa hivyo mama nani. Asikutishe na hao wanawake wasikutishe. Acha waendelee kuchezeana na kupulekana out.Atajificha na kufanya ngono na kurudi kulia mlangoni nisamehe. Wewe mwambie nimekusamehe lakini sikutaki tena. Kama ni ngono utapata kule nje, kama unataka mwanamke wa kuoa wanakutafuta wengi, wewe chagua tu! Ukweli ndio huu, there is no Hope for the Wicked and no peace for the wicked. ukimwona anacheka ni vicheko vya uwongo, ndani kunawaka moto na amani hana. Hayo ndio aliyopanda sasa anavuna. Mungu hadanganyi, amani anayokupea ndiyo ya kipekee. "Didn't i tell you never to call me again, Move on, I've Moved on...now you agree that you're not ok! you need help" Ok! bro I got that help, thanks for showing me the way. Don't worry, someday you'll settle down with one, and I ain't gonna have any hard feelings. If you will ever be favoured, then I too can be favoured with someone. So it goes both ways. YAWN!!!!!!!

Anonymous said...

`Akaahidi mpaka kuninunulia gari’ hii ni special message kwa ndugu zangu, manake wangekuambia,` sasa unataka nini tena, mwambia akununulie na nyumba’! Huo ni mtego wa panya, ila..
Mara nyingi tunapenda kujifunza kutokana na makosa, wengi wanajuta baada ya kuachana na wapenzi wao na kupambana na kile walichozani ni dhahabu. Mara nyingi mimi nashauri kuwa katika hii hali ya maisha ya namna hii,ni vyema tukapeana muda wa kutafakari,tukapeana muda wa kutathimini, lakini subira hiyo hatuna, kwasababu haya ni mapenzi,na mapenzi ni baina ya mke na mume, kwa wakati unasema ngoja nimpe muda, ndio wakati mwenzako unavutia kwake.
Kuna baadhi ya mambo umeyaeleza,kuwa `mlishafunga ndoa’ je hiyo ndoa mlisha-ivunja au mliamua tu kutengana kihasira? Kwasababu kama ndoa bado ipo, inabidi utafakari mawili, kuwa je kuja kuja kwake kuna muelekeo wa mabadiliko, au ndio kwasababu amegonga mwamba huko alkokwenda? Na je utajuaje kuwa kabadilika?
Unasema anakuja mara tatu kwako,je akija kama hamjavunja ndoa, inakuwaje, analala guest na wewe kwako au bado mnangonoka kama kawaida. Hapa nawashauri sana hasa nyie wanawake mliokumbwa na matatizo kama haya kuwa waangalifu na HIV. Mtu kama huyu akija kwako baada ya kugundua kuwa anaruka huku na huku na wanawake mbalimbali, usiogope kumwambia `kapime kwanza, kabla ya yote’ Jamani dunia ya sasa imebadilika, ili tuweze kuudhibiti huu ugonjwa inabidi tuwe makini na tusicheze na afya zetu.
Kwa ushauri wangu, huyo bado ni mumeo, kama hamjavunja ndoa, mpe masharti ya kumpima kama kweli kabadilika,likiwemo hili la kupima, na akuthibitishie kuwa kweli hana mwingine, na hapo inabidi ufanye uchunguzi wa ziada, ili kumpima ukweli wake. Lakini la muhimu ni je kweli `unampenda’ ingawaje unasema mapenzi yameisha, lakini nafikiri yameisha kwa sababu ya hasira, inabidi utulize moyo na ujiulize kweli `bado nampenda mwenzangu’ kama-atajirekebisha.
Maisha ya ndoa ni mchakato wenye matamu na machungu, kama umeonja tamu pekee huwezi jua uchungu wake,na ukionja chungu yake, huwezi jua kuwa yanaweza kuwa matamu tena,lakini utamu na uchungu vyote vimo humo humo.
emu-three

Anonymous said...

habari yako dada yangu kwa miee kama mie siwezi kuingilia mapenzi yako sijuwi unampenda vipi ex huband wako,lakini kwa mkasa huo uliotowa namie yalinikuta hayohayo tena sio wewe umeona condom,miee nishawafuma ndani kitandani wamelala,tukaachana mwezi tukarejeana kwa jinsi nilivyokua nampendaa,maji yakanifika shingoni nikapata nafasi ya kazi nje ya nchi basii toka hapo yule bwana simtaki hata kumsikiaa maana na maradhi haya tungeumizana,sasa ndio narudi kwako mpenzi nakushaurii angalia maisha yako na mtoto wako usimsisikilize huyo mwanaume alikuona hufai sasa iweje unafaa achana naeee angalia maisha yako.

Anonymous said...

Pole sana lakini we dada mi nakushangaa! na nasikitika kusema kuwa hiyo huwa ndio tabia ya wanawake wengi ya kutaka kusamehe na wakati si tu unaona indicators isipokuwa umejithibitishia mwenyewe kuwa huyo mwanaume hakufai...! hata nashangaa kwanini uliruhusu ukapata mimba wakati kabla ulishamfuma na vitu vya wanawake wengine ndani, msg na hata condoms tena zilizotumika... Na alivyokuwa mzuri mwanaume huyo akawa anakiri na kukuomba msamaha... Jamani.. wakati mwingine na sisi wanawake tuwe na maamuzi yetu. Inakuwaje unamng'ang'ania mwanaume kama luba wakati hata anadiriki kukuambia kuwa anatafuta mke wa kuoa! that meant kuwa wewe hakuwa ameridhika na wewe in the first place na ndio maana he went around kissing other frogs... Na kwa huruma yetu wanawake ambayo mi huwa naiona ni ya kijinga, ukawa unamsamehe on several occassions na ukakubali kuolewa. OK yalishapita. Sasa rafiki yangu you don't need to go back. Kuwa independent fanya kile unachoona kinafaa. Huyo jamaa hakufai japo ni baba wa mtoto wako. Utakuja dhurika bure kwa vile hata condoms hataki utumie wakati tayari unajua behaviour yake. Forget about the car! kwani hilo gari ni nini? na kwani huwezi kuja linunua mwenyewe hadi hiyo promise ikufanye ufikirie kurudi kwake? mi nadhani kwanza hakupendi na kukuingia kwa gear ya kukununulia gari ni upuuzi! kifupi my friend achana nae... hakufai kabisa. Soma alama za nyakati. Ulipata indicators nyingi kabla kuwa hakufai, ukatoa benefit of doubt kuwa atabadilika akikuoa na umethibitisha kuwa hajabadilika. Je ni nini kinakupa hope kuwa ukirudi this time atakuwa tofauti na tabia yake uliyokwisha iona? kwanza mshamba ni mwanaume gani wa karne hii anampiga mwanamke? MWACHEEE! lea mwanao hata kama hatakupa msaaada jitahidi utamlea. achana na ndoa hiyo!

Anonymous said...

jamaa ni wale tunasikiaga chupi mkononi. huyo atakusumbua sana. yeye anatakiwa apate chupi mkononi mwenzake ndio anaweza kuishi nae. achana nae wala usimpe nafasi!


jaba

Anonymous said...

Maskini dada angu,pole sana,mie sijaolewa bado ila i can feel ur pain my dear,ningependa kukushauri kwamba usikubali kabisa kurudiana nae,maelezo yako yanaeleweka kabisa,umekuwa mvumilivu sana maskini ukiwa una matumaini kwamba atabadilika lakini hajaonyesha ushirikiano katika hilo,na Mungu amekujalia una kazi so kama unaeza kumlea mtoto kwa kipato unachokipata basi haina haja dada angu kuanza kuumizwa moyo wako,,,sawa mamy! move on my dear,asije kukuletea magonjwa bure,,,yani kimbia kabisa usimpe chance,kama ulikua unamsamehe lakini bado anarudia tht means hiyo ipo kwenye damu yake na haezi kuacha,itafika siku atarudia tu! pole sana ila be strong

Anonymous said...

Wee dada pole sana kwa mikikimikiki hiyo ya urafiki hadi ndoa.Kwa kweli moshi ulifuka kitambo kiasi kwamba ungebaini kuwa palkuwa na moto mkal hata usingethubutu kufunga ndoa naye.Hata hivyo mimi binafsi nakushauri sana usifanye haraka kuamua kurudiana naye,chukua muda mrefu kulitafakari jambo hilo.

Taba yake uloielezea hapa ni ya hatari sana.Tafuta nmana nyingine ya kupata kukaa naye kwa mashauri na wadhamini wenu wa ndoa,hata hivyo hilo lwwe baadaye sana,kwa sasa hebu kwanza msahau huyo jamaa.Kukununulia gari si hoja,kwani kuwa na gari ndyo maisha?Au unataka ununuliwe gari na ukimwi juu yake au ukose amani moyoni na umepaki gari hapo nje itakusaidia nini dada yangu?Kwani muda wote huo unatembelea nini?

Dada yangu pamoja na kufunga ndoa lakini jiangalie sasa kama jamaa hana uamnifu basi chukua njia yako askubembeleze kwani amezoea kula kuma nyng kwa mtndo mmoja wala hatatosheka akaacha usijedanganywa,kama utaamua kumsamehe n kwamba umeamua tu kuchukuliana naye kwa tabia hiyo li mradi uite mume wangu.Na kama mke wake hata ukimwambia tutumie condom ipo siku atakwambia nataka kuzaa mtoto wa pil utasemaje mama?kimbia hiyo hatari kabsa.

Inawezekana jamaa huyo pesa anazo sana na labda ndiyo kitu kinawazingua hapo, na kwamba jamaa ndo maana anatomba hata nla kias.Tafadhal dada jihadhari kabla ya hatari.

Anonymous said...

Heee Dada! pole sana na yaliyokusibu. Ila uzuri ni kwamba wewe mwenyewe ushasema hutaki kurudiana nae kutokana na tabia zake. Mimi nakushauri fuata moyo wako utajiepusha na mengi, kutokuwa na amani, kuhisi anafanya nini na nani. Nadhani wewe upeshapita hizo enzi, Kama uliamua kuondoka kwa vile ulishindwa kuvumilia inamaanisha uliyofanyiwa yalikuwa makubwa na ya kuuma. Maisha yako ni bora kuliko hata gari alilokuahidi. Nakushauri ufanye kazi kwa bidii ili usimame imara. Hii sio karne ya kuchezea maisha! magonjwa yako mengi, sana na una mtoto wa kulea, Take care

Anonymous said...

ahsanteni sn kwa ushauri wenu kwani mmenipa moyo wa kusonga mbele zaidi na maisha yangu,wala sitarudi tena nyuma,kwani sioni cha zaidi kwenye hy ndoa ht kupeana majambozz kwake ni tabu cjui kwakuwa huwa anachovya sana nje?kuhusu ndoa bado hatujaachana najua hilo litatake time lakini atakuja toa tu kwn ndoa yetu ni ya kiislam,hvy at the end atachoka 2 kukaa mwyw.nashukuru mungu yng yananinyookea na sitashindwa kumlea mwanangu.

Anonymous said...

Mhh.

Pole sana dada yangu. Ukishaona hali kama hiyo huna budi kung'atuka lakiini hii ni kwa mawazo yangu mie. Haujui na anajifanya hauoni uthamani wako ukiwa nae. Atakumaliz huyo na hali hii ni mbaya maradhi mama. Pigania maisha ya mwanao, Msijekufa mkamwacha mtoto mdogo. Mwache yeye aendelee na maisha yake. Ni bora yeye asiejali akaangamia pekee kuliko kwenda wote mkamwacha mtoto wenu akiwa mdogo. Dont rush take it slowly but sure. Uamuzi ni wako it depend on how much u care for ur live and ur child life.

Its Ma Johnson.
Mza.

Anonymous said...

nashukuru sn kwa ushauri wenu mlonipa kwani mmenipa moyo,na nina imani nitasonga mbele zaidi katika maisha yangu,yote mlonambia nimeyafanyia kazi ni yana ukweli asilimia 100.mpk najiuliza siku zote nilikuwa wapi nisifungue macho????.mbarikiwe nyote .