Wednesday, 6 May 2009

Kanitambulisha kwao, anamtu yaani sielewi-Ushauri

"Jamani me dada Dinah nina jambo ila sifahamu tu wapi ni kutumie kwa mail gani lakini hii issue imekaa hivi: Mimi nina mpenzi ambae tunapenda sana sana na siku ya kwanza alivyoniona tu akawaambia ndugu zake kuwa ameshapata mke yule ambae anamuhitaji na kumuelezea mama yake mzazi. Mimi nimekuja kuambiwa na Binamu yake kuwa najulikana kabisa home cha kushangaza hajaniambia chochote hiyo moja.

Pili huyu anamtu amezaa nae na uzuri ameshaniambia kama anamtoto kinachoniuma mpaka leo wanaendelea kula bata mimi roho inaniuma sana sana sio siri, mtihani ulionipata ni kwamba nilimpigia simu kama mara 4 hivi hajapokea imepita masaa kadhaa anipigia na kunifokea "we si unajua kama niko na huyu mwanamke kinachokufanya upige non stop nini? sipendi mgambane ndio mana nimeamua kutopokea simu yako"


Kwa kweli imeniuma sana huwa hasemi lakini siku hiyo alinidhihirishia kabisa kwamba asipo pokea simu yangu nielewa tu yuko na huyo mwanamke. Niligomba sana pasipo kujibu neno lolote haikutosha nilituma msg za kumkashifu mwanamke pamoja na yeye yote ni hasira tu, nikawa kimya na yeye kimya.


Nikajirudi kwa kuona kimya kimezidi, na chat nae tuna story kama kawaida lakini hana mapenzi tena na mimi yaani inaniuma sana sana kumkosa. Alikua akinipa gudtime sana sikua nikipiga simu kwake yeye ndio alikua akipiga lakini sasa mimi ndio napiga na nisipopiga yeye hapigi. Nikituma msg za malalamiko kwanini anafanya hivyo? yeye hanijibu.

Sasa hapa sielewi kanimwaga au vipi ni bora anitamkie tu kama hataki kuendelea na mimi lakini si kukaa kimyaa jamani inauma sio siri kukaa kimyaa ina maanisha nini jamani mbona mwenzenu niko njia panda?

Naombeni ushauri nifanye nini?"

Dinah anasema;Pale ulipolitumia ndio mwake kabisa, shukrani kwa ushirikiano wako.
Kutokana na maelezo yako inaelekea sehemu ya familia ya jamaa yako hasa Mama yake kama ulivyogusia hawampendi huyo mwanamke aliyezaa nae sasa ktk kuwazuga ikabidi atafute mwanamke mwingine ambae ndio wewe na kumtambulisha kwa Mama yake huenda ni kwa jina, picha, au kwa mbali yaani unakatiza kwa mbali mtu anaonyeshwa "yule dada ndio mpenzi wangu nataka kuoa".

Kuna uwezekano mkubwa kabisa kafanya hivyo ili asipate "radhi" ya mama'ke au anataka tu kumfanya mama yake apunguze kidomodomo ili yeye na mama watoto wake waendelee kuishi vema. Kinachosikitisha ni kuwa wewe umezama kwenye mapenzi na mwanaume wa mwanamke mwenzio kwa maana nyingine inakuwa kama vile umeingilia mapenzi yao (well hii ndio itawajia kichwani wanawake wengi) lakini ktk hali halisi haikuwa hivyo, wewe ulipendwa na kijana huyo kisha ukampenda alafu ndio ukajatambulishwa kuwa kuna mwenzio ambae amezaa nae.


Ulichokosea hapo ni kuendelea na uhusiano na huyo Njemba huku ukijua kabisa kuwa unachangia na mwenye mali (aliyezaa nae) na mara kwa mara anakuwa huko na anathubutu kukufokea kabisa kuwa "unajua niko na yule mwanamke, kinakufanya unipigie non stop nini ?"hapo ni wazi kuwa hajali hisia zako na hakuthamini wewe kama mpenzi wake. Siku hiyo ungenawa mikono kutoka kwenye uhusiano huo.


Sio lazima mtu akutamkie kuwa hakutaki au hataki kuwa na wewe, wakati mwingine unasaoma vitendo vyake (Mf, kutokupokea au kukupigia simu), namna anavyoku-treat(Mf,anakufokea) na kadhalika. Huyu Jamaa hakuhitaji tena, kwani alichokitaka tayari kimepatikana nacho ni kufunika ukweli kwa Mama yake kuwa yeye bado anaendeleza uhusiano na mzazi mwenzie.


Natambua unavyojisikia, nafahamu maumivu ya kimapenzi unayokabiliana nayo lakini ni vema kuumia sasa na kujitahidi kumsahau huyo jamaa, kuyasahau yote mliyokuwa mkiyafanya pamoja kama wapenzi.

Njia nzuri ya kumsahau ni kumchukulia kuwa ni "kicheche", kumbuka kuna UKIMWI, fikiria.....kama ingekuwa wewe ndio umezaa na huyo jamaa alafu kijimwanamke kingine kinamsumbua bwana wako kwa simu ungejisikiaje?

Mungu atakusaidia na utasahau kila kitu na utakutana na Kijana mwingine asiye na mtu.
Kila la kheri.

10 comments:

Anonymous said...

Loh dada mwanamke mwenzangu pole sana lakini ndugu yangu huko si ndio kukataliwa unataka nini tena?

Amekaa kimya umeshachanganyikiwa je akikwambia sikutaki si utajichukia nafsi yako?

Na kama alikupa good time ndio hivyo mwenzio anapewa sasa na
kwa vile alishaonja asali na hadi
wamechonga mzinga yaani ana mtoto
si uwaache tu na wewe utafute mwingine? jipambe kwani hakuna mwanamke mbaya na nenda sehem ambazo utapata wanaohitaji na utathaminiwa au unataka kubanana na uteseke kwa mapenzi!

Mimi najua kama yeye anasema wa nini kwani hakuna wanaosema watakupata lini si ujaribu kwani
wanaume ndio hao hao wewe jaribu bahati yako na utapata tu atakaekupnda kwa dhati na kukuthamini kuliko kuchangia na kila siku utaumia inaonyesha mwenzio yaani mpenzi wako ameshanogewa kwa mzazi mwenzie na wewe hakujali tena ndio maana hajibu au kukupigia. sasa ukipata boma yaani kukeambia sikutaki si utakufa kwa kihoro bora umia hapo ulipofika na tafuta wa peke yako
pole sana jikaze na cool down. Good lucky

Anonymous said...

Jamani nimecheka sana baada ya kusoma hii msg, mie sio kawaida yangu kuandika comments katika blog hii mie huwa msomaji tu. ila leo imenibidi niandike. unajua nini Dears wakati nasoma hii msg nikawa nashituka kuwa wewe dada umejuaje mambo ambayo yananisibu na wewe umekuja kuyatundika hapa. inshort yaani na mie nina tatizo hilihili kama lako eti. ila mie tofauti ni hivi, kuna kaka yuko ugaibuni tuna kama miaka 4 sasa tunawasiliana tu ila hatujawahi kuonana, sasa hivi tulikuwa kwenye malove na mawasiliano ya nguvu na alihaadi atakuja june/july this year tufenge ndoa and then tuondoke. kipindicha nyuma nilikuwa nimekata tamaa maake alikuwa anakuja kwa mawasiliano juuu and then anakaa kimya this time akawa hata mwenyewe kakiri kuwa hataki kunipoteza tena, kama miezi 3 hivi iliyopita tumekuwa kwenye serious mawasiliano. cha ajab last wk jumamosi nikawa nimembeep, nawe akawa kabeep ila nikawahi kupokea nikasikiakama mazungumzo yaani yeye na sauti ya mwanamke tena wanaongea sauti za kimahaba. gafula akakata cm nikabeep tena akanitumia msg kuwa bado kalala atanipigia badae. na mimi nikawa mpole kweli badae akapiga sikutaka kumwambia what happened, yeye akaniambia kuwa week inayafuata anasafri kikazi mda wa wk moja kwa hiyo hatapata mda wa kunipigia cm ila msg na online tutachat sana. nikasema sawa kkila ck nikawa nambeep anaingia online tunachat, sasa siku moja nikambeep kama mara 4 hivi hakuingia online, kesho yake nikambeep tena kama mara 4 napo hakuingia online, cha ajabu kesho yake nikakuta kaacha offline msg, yaani ananifokea tena kuwa usitegemea kuchat au kuongea na mimi kila siku hilo sahahu nina vitu vingi sana vya kufanya katika maisha yangu. kwa kweli the way msg ilivyokuwa dry iliniuma sana tangu siku hiyo na mimi sijambeep tena wala kutuma msg na yeye kakaa kimya. siku mbili za mwazo zilikuwa zinaniuma sana ila kwa sasa nimeshanza kuloose interest naye ila roho nyingine inasema subiri tu. na mie nasubiri akinipigia tu cm namporomoshea hisia zangu. to summarize wewe dada na wewe kaaa kimya tu wala usihagaike kutuma msg wala nini, kama ni wako atakuja tu maake siku hizi prayers ni wengi sana kila la heri liliojema

NDIMI mimi mpweke

Anonymous said...

sorry lakini mdau,sijakupata kabisaa stori yako sijaelewa.Napenda sana kuchangia lakini please clarify.Kama umetambulishwa kwao ,je iweje tena binamu yake ndo akwambie home wanakufahamu .Kwa kweli upande wangu hueleweke.In Umesema hana mapenzi na wewe tena,sasa ingekuwa mimi ningeliona wazi kwamba hanipendi na afterall unajua kabisa yuko na mwanamke mwingine.Na amekwambia.Please mdada usijiumize roho mwakwetu move on ,anza upya Acha mambo ya kukashifu watu na matusi kwenye simu haisaidii.Si umeona makshafsa and all bado yuko na huyo mwanamke sasa ujue kweli hakupendi.Pole endelea na maisha yako.Move on

Anonymous said...

my dear hayo yamenikuta mm ni kitu ambacho nakijua ni hivi ukiweza ukae kimya hata ukipata mwingine kuwa nae utashangaa kuna siku atakutafuta yaani utashangaa wanawake tumekuwa na tabia za kishirikina sana huwezijua ila kuna siku utasimama tu ndg yangu hana mapenzi tena raha ya mapenzi kutafutana yaani siku ukiwa busy na mwingine utamwona anaanza ooohhh sijui nini wanaume hawa aaaaahhh

Anonymous said...

Huyo amekuonyesha wazi kuwa bado anampenda mzazi mwenzie, ni bora umwage manyanga, usubiri wako mwingine. Najua ni ngumu kwa mtu uliyeshampenda, lakini waweza kusonga mbele kuliko kuendelea kujidanganya. Kwa jinsi ninavyoona, huyu hata mkioana, mzazi mwenzie ataendelea kuwa kisingizio cha kukutana wao. Wanaume wengi wagumu kukutamkia kuwa wamekumwaga, ishara tu ndio zitakupa majibu. Kua

Anonymous said...

Kitu cha muhimu ni kumpa muda,kwani huenda yupo katika wakati mgumu kuhusiana na huyo wa mwanzoni, kiasi kwamba ameshindwa kumuacha yeye moja kwa moja. Cha kufanya, na baada yakumpa muda muendee na mueleze kinaga-ubaga, nini nia yako na mueleze ukweli kwanini ilitokea ilivyotokea. Kama kweli anakupenda atajua kuwa hilo limetokea kwasababu ya wivu.
Katika mapenzi ambapo kuna mtoto kunakuwa na kigugumizi kwa mwanaume, na ikiwa huyo mke aliye na mtoto bado anampenda mwanaume. Kwa vile anamtoto atamtumia kama ngao yake,na kila kitu atakitaka kwa kutumia mtoto.
Sasa wewe unachotakiwa ni kuwa na subira, na kujifanya kuwa unawapenda , unamjali huyo mwenzako na unampenda mtoto. Kwa njia hiyo huyo jamaa ataona wewe hutakuwa kikwazo kwake na `mtoto’ wake’ Kumbuka mwanzako anapendwa kwasababu ya ngao ya mtoto, kwahiyo wewe kuilegeza hiyo ngao ni kumuonyesha kuwa unaweza ukaishi vyema na familia hiyo iliyotangulia!
Hayo ndio maoni yangu
emu-three

Anonymous said...

Kwanza labda niulize kwa nini unajiona kama umelose kiungo chako cha mwili? Hebu fikiria kama haya yangetokea wakati mmeshaowana na mna watoto, jee ungeweza kufanya maamuzi ya busara? Huu ni ushauri wangu, Kwanza kabisa nakuwekea bayana "ACHANA NAE AND MOVE ON" ukweli ni kwamba mwanaume ambae anacheza na wewe wakati hamjaowana ni most like atacheza na wewe mkishaowana, hakuna mjadala.

Kama unaona ni lazima uwe nae au dunia itaacha kuzunguka, basi fanya haya yafuatayo.
Kwanza muombe uonane nae sura kwa sura, kisha akikubali jiandae kuwa mwana mke wa shughuli siku hiyo.

Mkikutana mwambia moja kwa moja kwamba kilicho kufanya uitishe mkutaano huo ni kujua hatima ya penzi lenu, mwambie unaona kwamba mpenzi lina yumba na ni dhahiri kabisa kinacho changia ni mahusiano baina yake na mama mtoto wake. Weka bayana kwamba huna wivu na mama mtoto kwani yule ni mzazi mwenzie lakini unacho jali ni Afya yako na maisha yako, kwamba hauko tayari kushare maradhi na mapenzi. Sasa mpe kamba ajinyonge mwenyewe, Mwambie CHAGUA MOJA MIMI AU MAMA MTOTO? Jiandae na majibu yote mawili akisema wewe, then weka sheria mahususi kwamba: Maongezi yote baina ya wawili hao ni lazima yawe juu ya mtoto na si kingine, na wewe ungependa kushiriki kwa kujua kila anapokwenda kwa huyo mzazi mwenzie.

Akisema anataka mzazi mwenzie, mwambie shukurani, GoodLuck na wewe ondoka zako.....

Ed

sam said...

mmh hii ni jambo kubwa haswa kama umewahi kuwa katika hali hii.lakini mm naomba kutoa maoni yangu kama mwanaume,kuna wakati wanawake huwa mnashindwa kutuelewa haswa inapofikia kwenye mambo haya ya malove davi,unajua huyo tayari ni mzazi mwenzie,na pia wana mtt tayari,sasa kile kitendo cha yeye kukwambia wazi kuwa nina mtt na nimezaa na fulani ni jambo ambalo unapaswa kuliangalia kwa mtazamo chanya(+ve i mean)kuwa ni kweli anamapenzi nawe,na yeye kuendelea kuwasiliana na huyo dada ni pengine ni kwa sababu ya mtoto,na nataka hapa kusisitiza na wanawake mnielewe hata mkinihukumu sawa,hakuna mwanaume anaweza kukubali mtoto wake ateseke kwa sababu ya mwanamke regadless ya mapenzi unayompa au aliyo nayo kwako kama yupo katika normal common sense maana kuna mambo ya nguvu za giza.sasa kwa kuwa ameshakuambia na ukambeep hakupiga kama ndio ameshakuzoesha beep nitakupigia sawa,lakini yakubidi ulewe kama hakupiga tulia,na mkikutana muulize kiungwana atakwambia,na hata akikuambia kuwa alikuwa na mzazi mwenzie,na usifurahiswe na hilo pengine kutokana na hisia za kike za wivu ,ndio si unamapenzi nae lazima utapata wivu mm nashauri usioneshe hasira zako hapo,tulia na onesha kukubaliana na hali halisi,na jaribu kujifunza kumpenda huyo mtoto,na ikiwezekana muombe akuoneshe huyo mtoto,na anza kumfanya kama ni mtoto wako,mwanaume akiuliza vipi mwambie umenipenda na unataka kunioa na huyu ni mtoto wako na mimi ni wangu moja kwa moja,na hata ukishaingia kwenye ndoa chukua mtoto huyo kama wako,faida ya hili ni kuwa kwanza utajenga imani kwa mwanaume kuwa hutamtesea mtoto wake hata akikuoa,pili utasaidia kupunguza sababu ya yeye kukutana na huyo mzazi mwenzie,tatu utajenga mapenzi na imani kubwa kwa mwanaume kuwa kweli wewe ni mwanamke muolewaje kwani kwa sasa sio siri kina dada wengi wanpoteza sifa za kuolewa bila wao kujijua na kuanza kutafuta mchawi pasi na kumpata.Nikirudi nyuma nini sababu ya mwanaume kufoka ulipobeep mfululizo,kwanza ni lazima tukumbuke,kuwa kuwa kwenye mahusiano sio jela,kwani hata wanawake mtakubaliana na mm pale mwanaume napokubana hata kutoka nje inakuwa kosa jinsi ndoa na mahusiano yapokuwa mtihani kama si ndoano,sasa na kwa wanaume ni hivyo hivyo,kuna uhuru fulani,mwamini utajenga mahusianao yako yawe bora zaidi(hapa naomba nieleweke si kwa wale wanaume wanaotaka kucheat kwa kivuli cha mzazi mwenzangu),na hakuna mwanaume anaweza kukusaliti huku hakijua unajua.na hata hata kama unakata kuiba au kupora huyo mzazi mwezake mume yaaani mnamgombe huyo mshikaji nakwambia utashinda ukifuata haya.samahani kwa kuandika kirefu kidogo kwani nimguswa,am man who understand,sir2510@yahoo.com,for personal ushauri tu.your welcome

Anonymous said...

Wewe dada umesema umetambulisha nyumbani kwao, Je, umewahi kwenda pamoja naye akakutambulisha au umebaki na hadithi za binamu mtu?

Hata kama wanajua huko kwao hilo lisiwe kiegezo cha kukutia kiwewe chochote wewe.Yaani hata engagement bado hata kule kuchumbiana bado unahangaika nini mrembo wangu?

Unafikiri huyo mwanaume atasema sikupendi?haitatokea hivyo yeye atakula kotekote si vyote vitamu? jukumu liko kwako dada ndiye unahitaji kuuona mwelekeo wako.Utazidi kuchakazwa na huyo jamaa hata kiasi cha kukuzibia mianya yako ya kupata mtu wako.

Nyie kina dada zangu, mbona mnazenguliwa hivyo kisengesenge tu,hamjui kwamba mna thamani sana? mwanaume asikuzengue na kukula kuma tu kaeni mkao wa kujilinda daima usimpe kuma mwanaume mpaka kielewekeeeeeeee!!! tatizo lenu mnakubali kutombana hata hujui hulka ya mtu huyo na vitabia vingi.jaribu kujilinda na kujitunza.Wanaume wako kutafuta kula tu mambo ya kuoa au uaminifu ni nadra sana.Tena kina dada msiwe na wasiwasi juu ya kuolewa Mungu anao watu wenu bado wako njiani, la muhimu ni kuwa na subira na kujenga uaminifu katika maisha yenu.Kila nikisoma hapa blogini naona vilio vingi vya kudanganywa na kugiribiwa.Na ninaamini kabisa kina dada wengi ni waaminifu sana wanapopta mtu anayejiita anakupenda,huwa mnajaribu kutunza sana ulichokipata,lakini sisi wanaume uaminifu wetu mdogo kwani kila tako unaloliona unataka kulipapasa.

Wito wangu kina dada achaneni na kihelehele cha kutaka kuolewa au kutafuta boyfriend kwa pupa.Uwe mahiri sana katika kujihurumia mwenyewe kuwa ni lazima kuwa makini katika mambo hayo la sivyo mtaendelea kupoteza uthamani wenu amabo Mungu amewapa japokuwa ninyi wenyewe hamuuoni.Endelea kujitunza dada kabla wengi hawajakuona maana usije ukaachwa kwenye mataa daima.

Nakutakia kila la heri dada yangu.Amua jambo jema sasa achana na ubabaishaji huo kwani usipokuwa na mwanaume utaoza huko chini?mbona utajitunzia heshima yako vema kabisa.

Anonymous said...

Jamani! Achana naye huyo. Ndio unampenda lakini hakufai. Huyo hatakaa abadilike, sana sana akikuoa utakuwa hulali usiku unasubiri atoke kwa baby mama wake! Be strong and move on girl!