Thursday, 21 May 2009

It's Two!!


Leo ni Siku na Mwezi ambapo D'hicious inasheherekea Miaka miwili tangu ianzishwe. Siku hii ni maalumu (Special) sana kwangu, sio kwavile ni muanzilishi wa Dinahicious Blog/Live na labda mwanamke wa kwanza kuzungumzia "Unyago" kwa uwazi na kwa faida ya kila mtu (wake kwa waume) bali pia tarehe kama hii kuna tukio muhimu sana lililo badilisha maisha yangu lilitokea hivyo basi ninafuraha sana.....miaka 2! Huh!
Kabla sijasema mengi napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukurani zangu za dhati kwako wewe Msomaji, Mchangiaji, Msikilizaji wa Bongo Radio na Muuliza maswali, wote kwa pamoja ndio mnaifanya D'hicious Blog/live kuendelea kuwepo. Pia shukrani kwako wewe uliyoiweka D'hicious kwenye blogs/tovuti yako.

D'hicious imefanikiwa kwa kiasi kikubwa tangu ianzishwe miaka miwili iliyopita. Dinahicious imerudisha mahusiano mengi ambayo yalivunjika au yalikuwa yakielekea kuvunjika. Dinahicious imefanikisha baadhi ya wasomaji wake kufanikiwa kushika Mimba na kuzaa kwa kutumia njia asilia kabisa.

Dinahicious imerudisha ndoa na kuboresha ndoa nyingi, Dinahicious "imesababisha" watu kupata wapenzi na hatimae kufunga ndoa kwa kutumia mbinu zilizoelezwa mahali hapa, vilevile D'hicious imefanikisha wake kwa waume kubadili mienendo yao na kufurahia maisha na mafanikio makubwa kupita yote ni kwa Jamii ya Kibongo taratibu sasa inakubali kuzungumzia Ngono, Mahusiano na Mapenzi kwa uwazi bila uoga wala aibu.

Dinahicious ilivyoanza hakukuwa na blog au tovuti ya Kiswahili yenye kuzungumzia Ngono kwa uwazi katika mtindo wa kufundisha na kukumbusha. Lakini hivi sasa hali ni tofauti kwani wengi wameibuka na kujisikia huru kuizungumzia ngono bila aibu.....ni mafanikio makubwa kwa upande wangu na ninahisi faraja sana kuona kuwa, kwa kufanya kitu kidogo tu nimeweza kusababisha mabadiliko kwenye sehemu fulani ya Jamii yangu ya Kibongo.

Kama ambavyo mmeshuhudia tangu kuanza kwa mwaka huu kumekuwa na mabadiliko kwa maana kuwa, nimekuwa nikijibu maswali zaidi kuliko kutoa mafunzo kama ilivyokuwa hapo awali. Hii yote sio tu kutokana na uwingi wa maswali ninayopokea bali pia ni kwasababu matumizi mabaya ya kazi zangu.

Baadhi ya Magazeti ya Udaku na Blogs wamekuwa wakitumia kazi zangu bila kuweka vielelezo kuwa wametoa kwangu au kuweka anuani ya D'hicious, sasa ili kupunguza matumizi mabaya ya kazi zangu nimeamua kufanya mafunzo kwa njia ya sauti (radio) na sio maandishi (blog).

Kwa maana hiyo basi D'hicous itaendela ku-publish maswali yote ninayopokea na nitakuwa nayajibu kwa uwazi kabisa kama kawaida yangu na mafunzo yataendela kupatikana Radioni.

Juma Pili hii kutakuwa na kipindi maalum radioni kwa ajili ya kuadhimisha Miaka miwili ya blog na kipindi chenyewe, unakaribishwa sana ili kutoa mchango wako kwa njia ya simu.

Mungu aendelee kukupa uzima na endelea kujikumbusha/kujifunza mambo muhimu ili kuboresha uhusiano wako wa kimapenzi kupitia D'hicious blog/live.

**GQ, Dj Dennis, Mpenzi Mume wangu na SamChom bila ninyi heri nitoweke Duniani.

Mwisho mzuri wa wiki,
Asante sana.

21 comments:

Anonymous said...

ni radio gani hiyo jumapili dada dina

Anonymous said...

Hongera sana dada miaka miwili sio kitoto.

JayJay said...

Miaka miwili na bado uko juu Dinah. Big up dada

Mimi said...

Dinah hongera sana bidada

Naila said...

Siamini ni miaka miwili sasa mwee sku zakimbia namengi umetufanyia dada.

Anonymous said...

Happy birthday Dinahicious.
Well done Dinah.

Anonymous said...

Dinah hongera sana mpenzi. Jamani Dinah hivi umeolewa lini? Mimi ni mmoja wa wadau wako wakubwa! Nakupenda sana na Mungu akujalie na akuzidishie nguvu na uwezo wa kutusaidia sie katika kubadilishana ujuzi.

JPhamber said...

hongera sana cousin....you are the only one ambaye unaweza kuelezea majambos bila aibu

EDWIN NDAKI said...

najua mpambnano jinsi ulivyo mgumu wa kublog.

nakutakia kila la kheri katika majukumu yako na afya njema

tutafika tu

Anonymous said...

hongera mi dear!!!!iko wapi keki tuikate????????

ROGERSBIZ said...

blog nzuri.

Anonymous said...

Hongera sana dada Dinah, kazi kubwa uliyoifanya ni zaidi ya miaka miwili, kumbuka kuna watu waliishi na waume zao na wake zao zaidi ya miaka kumi bila raha, bila kuelewana, lakini kwa darasa lako wameiona raha ya ndoa.
Kwa niaba ya familia yangu na kwa niaba ya wadau wenzangu ambao wanashirikiana nawe kwa kupitia mgongo wangu tunakutakia kila laheri na mafanikio mema, na uzidi kuliendeleza gurudumu hili la kuziokoa ndoa za waja wa mwenyezimungu.
emu-three

Anonymous said...

Nami nitakuwa sinashukurani kukupa zangu hongera, hongera sanaaaa dada Dihan, unatuelimisha vya kutosha. ongeza mada mama tupo wote lete maada sister. Nakuzimia kichizi.

Anonymous said...

Hongera Dinahicious kwa kutimiza miaka 2, ama kweli si kazi ndogo, mungu atakulipa kwa kila unachofanya, msaada wako ni mkubwa sana kwa jamii yetu.

maombi yangu ni kwamba kuna wengine ambao kusikiliza radio ni tatizo au muda hauruhusu na vitu kama hivyo na ni wapenzi wazuri wa blog yako (wachangiaji na waulizaji) je, itakuwaje kama majibu yatatoka radio tu??

ahsante nadhani utalifikiria hilo pia.

Anonymous said...

Dahaaaaa! Dada dinah hii glob imetusaidia sana, mm binafsi imenifundisha mengi kupitia michango ya watu.

Ila dada naomba nisaidie kitu ukitaka kutuma ishu yako unafanyaje? nisaidie plse coz na mimi nina ishu yangu nataka unisaidie.

happy bday dinahicious. big up sana

Anonymous said...

Hongera Dina kwa kazi nzuri, nakukubali saaaaaaana. Bt naamini bila Mungu ni bora ufe na si wanadamu, maana nao watakufa watakuacha.

Anonymous said...

honger sana dada dinah!
mie pia nina swalilangu,last week nilikutumia kwa ile mail ya radio lakini naona hadi leo huja li-publish.please naomba unisaidie uliweke ili watu wanisaidie au ht kama wewe unaweza pekeyako nitashukuru sana.plz inusuru ndoa yangu da dinah.

Dinah said...

Anny hapo juu, maswali yote yanayonifikia hutokea hapa "ubaoni". Ila hayatoki mara tu baada ya wewe kutuma kwani kunawengine hutumakabla yako hivyo basi unahitaji kuwa mvumilivu nakuendelea kupitia hapa ili kuona swali lako na ushauri kutoka kwa wasomaji wa blog hii.

Huwa nayahariri na kuyaweka yajitoe yenyewe kulingana na lini yamepokelewa.

Mfano ukituma swali leo ni wazi kuwa litatoka wiki ijayo na sio on the same day u sent it.

Asante kwa suhirikiano wako.

Anonymous said...

Hongera sana da Dinah!
nitakuwa mkosefu wa fadhila kama nitashindwa kukupa hongera kwa kutimiza miaka miwili na kukushukuru kwa mchango wako. tangu niijue blog yako miezi sita iliyopita nimefanikiwa sana katika mahusiano yangu ya kimapenzi. May our mighty God bless you and your family, uendelee kutupa mambo mazuri zaidi.
Shuhu 'hot'

shamim a.k.a Zeze said...

hongera shostitooo...endeleza libeneke miaka kumi ijayo watu woote tujue kungonoka KIUKWELIIII

jeromy E said...

sister Dinna inelekea mimi ni mgeni zaidi kuliko wengine.. sijaelewa unamanisha nini kusema miaka miwili ya blog yako kwani nimeanza kperuzi blog yako long back early 2008, na pia zaidi ya hapo nilikuta post za 2007,, sasa mbona ni zaidi ya miaka miwili...?? ila tisa kumi nakupa hongera sana kwa kazi nzuri unazofanya sijawahi kukumbana na matatizo magumu katk mahusianao ila kutoka blog yako nimejifunza mengi sana sana na hakika mimi na mwandan wangu tunaenjoy to the maximum ever since kwa kila jambo uvumilivu, uaminifu, kungonoka sana na maisha kwa ujumla. HONGERA SANA DADA,,,,KEEP IT UP TO THE SKY