Monday, 27 April 2009

Wifi anachukua nafasi yangu, nifanyeje?-Ushauri

"Nimegundua kuwa watu wanafanikiwa kuokoa mahusiano na ndoa zao kupitia blogu hii na mimi leo nimeona nichangie tatizo langu ili kupata ushauri wa watu wengine na zaidi kutoka kwako Dada Dinah.

Mimi ni mdada mtu mzima tu nimeolewa miaka si chini ya mitano, nina watoto wawili. Nimekuwa nikishindana na wifi yangu ambae ni dada wa damu wa mume wangu, ushindani wetu ni kama mtu na mke mwenzie lakini si hivyo.

Kabla sijaolewa na huyu mwanaume tulikuwa kwenye uhusiano wa mbali kwani mimi nilikuwa nasoma Ireland na yeye alikuwa Tanzania. Kipindi chote hicho hakukuwa na matatizo yeyote kati yangu na dada yake.


Baada ya kumaliza masomo nilihamia England kufanya kazi ambako ndiko tunaishi mpaka sasa. Ndoa yetu ilifungiwa Tanzania na Mume wangu akanifuata huku na baada ya muda tukasaidiana na kumleta dada yake ambaye ndio wifi yangu huyu mwenye vituko kila kukicha ambavyo vinahatarisha ndoa yangu.


Imefikia hatua wifi yangu kuchagua nini kifanyike ndani ya nyumba yangu, aina gani ya vifaa vinunuliwe ikiwa tunafanya marekebisho hapa ndani, wapi tuende au tusiende, tukamtembele nani nalini na kinachonikasirisha zaidi ni kaka mtu kumsikiliza dadake na sio mimi mkewe.


Ikitokea mimi na mume wangu tumejadili jambo la kufanya kwa ajili ya familia yetu ndogo mume wangu anachukua simu na kumwambie kila kitu mdogo wake na kitakachosemwa na mdogo wake basi ndio kitakachofanywa na sio mimi hata kama sehemu ya jambo hilo pesa zangu zinahusika. Yaani imekuwa kama akili ya mume wangu haifanyi kazi basi anatumia ya dada yake kufanya maamuzi.


Kitu kingine kinachoniumiza roho na kunipa donge ni pale ninapotoka kazini jioni au siku za mwisho wa wiki wote tuko nyumbani, badala mume wangu atumie muda huo na mimi yeye atakuwa kwenye simu na dada yake wakiongea maongezi yasiyoisha tena kwa kilugha chao na kucheka.


Nimevumilia sana na nimefanya vikao na ndugu wa pande zote mbili na hata kuzungumza na mume wangu lakini hakuna mabadiliko yeyote, nimekuwa mkiwa ndani ya ndoa yangu na sijui nini cha kufanya, japokuwa nampenda mume wangu lakini kama suluhisho ni kutoka kwenye hii ndoa basi nitatoka ili kutafuta amani na furaha kwingine lakini sio ndani ya ndoa hii.


Wifi yangu huyu ni mkubwa zaidi ya mume wangu, ameolewa na anawatoto kadhaa wote wako Mkoani Kagera Tanzania.
Naombeni ushauri ndugu zangu"

Jawabu:Mmh Dada tatizo unalokabiliana nalo ni zito sana kwa mwanamke yeyote yule ndani ya ndoa. Kwanza kabisa nakupa pongezi kwa kuwa mvumilivu na kwa ushirikiano wa kuchangia tatizo lako mahali hapa.


Nisingependa kuingia ndani sana lakini nashindwa kujizuia kupata hisia kuwa Mumeo na Dada'ke hawajiamini kwa vile umewasaidia kwa namna fulani kujikomboa kimaisha......ndio Ulaya sio mwisho wa matatizo lakini ukweli utabaki pale pale kuwa, kama ukifanikiwa kupata kazi you better off huko kuliko Bongo. Sasa nahisi hawa wanafamilia hawaamini kuwa wewe mwaamke ndio sababu ya wao kuwa huko na hilo linafanya kupoteza ile hali ya kujiamini.


Natambua sio vema kuzungumzia Makabila lakini ni wazi kuwa kuna Makabila mengine hapa Tanzania wanajali sana kuwa juu kwa kila kitu, sasa ikitokea wanakutana na mtu amabe yuko juu kabla yao inakuwa taabu. Ninaamini kabisa kuwa Mumeo hajiamini mbele yako kwa vile inaonyesha umesoma na una kazi nzuri kulingana na Elimu yako, hili ni gumu sana kwa mwanaume yeyote kuishi nalo achilia ukabila wake.


Hili linalotokea kwenye uhusiano wako huenda ni matokeo ya u-bully wa dada mtu kwa mdogo wake ambae ndio mume (lazima kutakuwa na walakini kwenye udada-kaka wao) pia inawezekana ni mambo ya "Ego" tu, Sasa kwa vile mumeo ni mdogo (kutoka na maelezo yako) inawezekana huwa anasikitika au kulalamika kwa dada yake kutokana na kutojiamini kwake, Mf-Unafanya vitu vikubwa ambavyo ktk hali halisi yeye kama mwanaume anadhani ni jukumu lake n.k


Umesema (kwenye maelezo yako) kuwa umezungumza na mumeo kuhusu tabia yake na ile ya dada yake lakini hakukuwa na mabadiliko, inawezekana kabisa namna unavyo wasiliana na mumeo ni tofauti na unavyopaswa kufanya.


Linapotoke tatizo kama lako ambalo linahusu ndugu wa mumeo unatakiwa kuongea na mumeo kwa upendo na mapenzi lakini wakati huohuo unakuwa "firm". Ukiwakilisha hoja zako kwa mumeo ktk mtindo wa kulalamika na kunung'unika mumeo hatochukulia umwambiayo "serious" na badala yake atadhania kuwa wewe unawalakini na dada'ke na unajaribu kuwatenganisha kama ndugu.


Nini cha kufanya: Jitahidi kujiweka kwenye "mood" nzuri yaani kuwa mwenye furaha (hii itakusaidia kumuonyesha mumeo kuwa huna chuki na dada'ke na wala huna hasira nae mumeo). Zungumza na mumeo kwa mapenzi na kwa uwazi kabisa bila kuficha kitu.........na anza kwa kuelezea hisia zako za kimapenzi juu yake, mueleze ni namna gani unafuraha kuwa mke wake na kuchangia kila kitu kwenye maisha yenu, mwambie ni namna gani wakati mwingine unajisikia mpwekwe pale anapojisahau na kutumia muda wake mwingi peke yake (usigusie kuhusu dada'ke).


Mkumbushie namna gani uhusiano wenu ulivyokuwa hapo awali (kabla Dada'ke hajaungana nanyi huko Ughaibuni lakini usimtaje wala kugusia ujio wake), onyesha ni namna gani mlikuwa mnatumia muda mwingi pamoja sio tu kama mke na mume bali wapenzi na marafiki. Muonyeshe ni namna gani ulikuwa unafurahia ukaribu wenu na unaweza kuongezea jinsi uhusiano wenu kingono ulivyokuwa then.


....wakati unaongea yote haya hakikisha hakuna umbali kati yenu na umuonyeshe mapenzi ya hisia ambayo hujawahi kumuonyesha kwa muda mrefu au hujawahi tangu mkutane, usisahau kutabasamu na ku-flirt kimtindo na mumeo huku unamuangalia moja kwa moja kwenye macho yake, mwambie hufikirii hata siku moja kuishi bila yeye na utafanya kila uwezalo kuhakikisha uhusiano wenu unakuwa bora, uliotawaliwa na mapenzi......(hapa atakuwa tayari kupokea "kibomu").

Malizia kwa kusema kuwa, ungetaka uhusiano wenu uwe kama ulivyokuwa mwanzo kwani hivi sasa hauna furaha, amani wala raha ndani ya ndoa yenu kama ilivyokuwa awali na ungependa mabadiliko.....ondoka na nenda kufanya hsughuli zako.

Hapa atakuita/kufuata akitaka kujua nini hasa unamaanisha au atabaki kimya akitafakari uliyomueleza.....usitegemee jibu au mabadiliko siku hiyo hiyo hivyo basi mpe muda na endelea kumuonyesha "mood" nzuri na kama vipi muda wa kitandani ukifika mpe mambo matamu bila kinyongo.

Wakati unaendelea kusubiri mabadiliko ya tabia ya mumeo, mtafute wifi yako na ongea nae ana kwa ana (no sms wala simu) na yeye mpe kitu cheupe kwa kifupi bila hasira wala chuki lakini cheza na Saikolojia yake.

Mwambie kuanzia muda leo aache tabia yake ya kuingilia maamuzi ndani ya ndoa yako, mwambie ulivyoolewa hukuolewa na watu wawili bali mume wako pekee ambae unampenda kwa moyo wako wote na hauko tayari kuumiza hisia za mume wako kwa kufanya mambo machafu ambayo kwa kiasi kikubwa yatakuwa yamesababishwa na tabia yake chafu (hii kisaikolojia itamfanya ahofie kaka yake kuumizwa na wewe na bila shaka atakimbia kwenda kumuambia).

Sasa kwa vile ulimpa mumeo mambo hadimu usiku uliopita alafu leo dada mtu anakuja na issue ya wewe kutopenda kumuumiza hisia hakika itafanya kazi vema kabisa.

Endelea kusubiri mabadiliko ambayo yatajitokeza ndani ya wiki chache hasa kama mumeo anakupenda lakini ikitokea vinginevyo na wanaendelea na tabia yao mbaya basi siombaya kama utatafuta ustaarabu mwingine......lakini nakuhakikishia kabisa kuwa mbinu hizi zitafanya maajabu kwenye uhusiano wako.

Kila lililo jema Mdada.

15 comments:

Anonymous said...

Pole sana, jambo kama hilo ni adimu sana kutokea huku nje tunakoishi. Lakini since wote ni Watanzania then kuna posibilities za kuleta ushenzi wetu hata nchi hizi za watu.

Dada yangu ukweli ni kwamba huyo mumeo ana lake jambo ambalo anakutaka na tatizo sio huyo wifi yako, bali anatumia mgongo wa huyu wifi kukukinaisha ili useme la moyoni na yeye aseme kama ndivyo ulivyo amua basi sawa.

Ushauri wangu ni huu mpenzi. Kwanza kabisa muombe mtu mzima mwenzio wasaa kidogo mzungumze. Siku hiyo jiambie kwamba "Ni lazima uzungumze bila pressure, yaani kuwa katika state of calm". Mwambia yote uliyo nayo moyoni ukimuomba ukisikilize kisha ukimaliza ataruhusiwa kutoa comment au kuchangia hoja. Usiruhusu mabishano yatokee katika maongezi hayo kwani yanaweza kupelekea cheche baina yenu. Vile vile angalia kauli yako usitumie maneno kama " wewe na dada yako wapenzi" au " dada yako anakutafutia mahawara", use respected words.

Mueleze kwamba unaona uhusiano wenu umebadilika sana tangu dada yake aje. Mweleze bayana kwamba humchukii dada yake, bali unataka kuzungumzia haki yako ya msingi ambayo ni "MKE". Mwambie kwamba umejitahidi kuvumilia lakini umeshindwa na sasa unaitaji kupatia jawabu tatizo hili sugu. Muwekee wazi kwamba tabia hii inaweza kutia doa kwenye uhusiano, na kwamba hauko radhi kuendelea na mahusiano yasio na HESHIMA. Again make it straight forward kwamba you will not continue to a victim on one way relationship. Then he have to make a choice au wewe or dada yake.

Dada Kemmy said...

Pole sana dada kwa kuishi bila amani ndani ya ndoa yako!
Kwanza nataka nikwambie kitu kama sikosei mumeo na huyo wifi yako ni watu wa kagera, kwanza kabisa tabia zao wengi ni F, msinishambulie jamani mie mwenyewe ndo kabila langu kwahiyo am talking through experience nawajua hawa watu vizuri sana!na story yako na mie ilitaka kuanza kujitokeza ndani mwangu kwakweli niliikemea vilivyo, haya sas huyo wifi yako hata kama ni mkubwa unatakiwa umweleze ukweli bwana kwako hapo sio kwake sawa?mambo ya uswahili wake akaufanye akiwa ndani ya nyumba yake sio hapo kwako yaani unatakiwa umweleze ukweli kama unashindwa basi umtafutie watu wazima wampashe haswaa, jamani mawifi KERO ASIKWAMBIE MTU, pole sana mpenzi lakini hujashindwa bado wewe ni mwanamke hebu amka jisimamie mwenyewe na mumeo nae anakosea kabisa uanze na mumeo kumweleza wewe ndo mama mwenye nyumba hapo anayofanya dadake sio sahihi kabisa na inabidi uwe na sauti sio wifi sasa wewe anza hv hapo si kwako? sasa ukiamka unapanga ratiba za home wewe kama atazipangua atajijua lakini wewe ujiwekee ratiba zako kama leo tutakula wali maharage au pilau basi hakuna wa kupinga hapo, akipinga sasa anataka maneno mbofumbofu...kingine basi huyo wifi nadhani anaona wivu tu unaomsumbua ndo maana anataka kushindana na wewe!mie kwangu basi kulikuwa na kiumbe wa dizaini hiyo dada basi bwana yeye tatizo lake alikuwa hafanyi kazi akiamka anakaa kwenye tv na kukunja 4 jingine ananivalia kanga ya kifua na kujitingisha ndani ya nyumba yangu, mama nilivumilia mpaka nikachoka siku nilipovimba nikampasulia jipu weee mbona alitimka bila kuaga kwakweli ni bora ukaishi kwa amani ndani ya nyumba yako kuliko kuishi na hilo kabila lol!!!!!!!dada kuna sehemu kuna wadau wengi sana wanapita nadhani nikuelekeze pia ukatoe tatizo lako utaweza kushauriwa pia,www.harusiyangu.com kuna forum za topic utaona, dada Dinah pia mshauri huyu mwanamke mwenzetu kwakweli!

Anonymous said...

hi Dinah, pole na majukumu. mimi ni mpenzi mkubwa wa Blog yako, nina matatizo ila sijui ni wapi naweza kuandika hayo yanayonisumbua ili nipate msaada wako.
please tell me what to do.
waiting for ur reply
thank you!

Anonymous said...

Hivi kuna nini kati ya mawifi:- mke hapatani na wifi yake, kulikoni?
Kutokana na uzoefu wangu, zipo sababu zisizo na msingi kwa watu hawa wawili. Mke kwa upande wake na dada mtu kwa upande mwingine.
Dada mtu anachukulia kuwa mke amekuja kufilisi mali yao, akimaanisha kuwa kaka yao ni mtu wa familia yao, kwahiyo anachokichuma ni mali ya familia yao, kutoka juu. Hapa anashindwa kujua kuwa hii ni familia nyingine kutoka kwenye familia kuu, na kwahiyo inajenga utegemezi wa kwake, na familia hii imeundwa na mke na mume,kama ilivyokuwa imeundwa famila mama, ya baba na mama yao.
Mke kwa upande wake anaona wifi yake ni kikwazo, yeye anataka siasa yake anayoipenda yeye na mume wake.Anataka uamuzi na Uhuru kama familia tegemezi. Kwahapa wengine wanajisahau kabisa kuwa familia hii ni chimbuko la familia juu, yaani familia kuu, na ya kuwa matunda aliyoyakuta huenda yametokana na jasho la familia kuu na wanafamilia akiwemo huyo wifi yake.
Hatuwezi kukataa kuwa wapo wadada zetu wakorofi ambao wanapenda kaka yao awe kama awali,kabla hajaja wifi yao na pia inabidi tukubali kuwa wapo wake zetu wasiopenda familia kuu na wanatokana nayo zaidi ya mume wake.
Chamuhimu hapa, `wewe kama mume unatakiwa uwe kati na kati, kwani mke ni mwenzako mnatakiwa mshirikiane kwa kila kitu,lakini ndugu zako ni nduguzo, hawana mbadili,unatakiwa uwe nao pamoja kwa yale yanayostahili udugu. Na wewe kama mke ujue hapo ulipofika kumetokana na uliowakuta, waheshimu na washirikishe kama ndugu zako, usiweke vikwazo!
Mambo yakizidi, kaeni kikao,ongeeni na shaurianeni, ili kila mmoja ajue mipaka yake na wajibu wake. Mke awe mke na sio dada, na dada awe ndugu na sio mke,ila wote muwe kitu kimoja.
emu-three

Anonymous said...

Dada Dinah nafikiri kuna wakati itabidi uwe unapit... Dada Dinah nafikiri kuna wakati itabidi uwe unapitia kila ujumbe unaotumwa na wadau wa blog hii kabla ya kuirusha hewan,kwan si malengo ya blog hii kuvunja ndoa za watu au kuwashawishi wazisaliti kama Aisha alivyopendekeza kwa eti kuwa bwana alomlalamikia mkewe kumkuta na sms ya kuomba shs 5,000 alishindwa kumtimizia matakwa yake,kama ndo hivyo sisi fukara tusingeoa,naamini Aisha kama ameolewa siku mumewe akiishiwa atamletea ndan mabwana wenye pesa,namhurumia sana aisha kwa kujifanya hafahamu maana ya maisha wewe uishie kuvaa tu na kwenda viwanja bila kujali watoto wanakula,kuvaa nini,kumbuka wanao wakijashindwa pata matunzo sitahili watakuja kuwashitaki lakin wewe huwezi kumshitaki mumeo eti kashindwa kukutoa out.usishawishi kuendeleza mabaya.
LUTUTU DAR.

Dinah said...

Anony@ 1:51pm, unaweza kutumia email bongo.radio@yahoo.com

au unaweza kunitumia via hapa kama ulivyofanya uliponitumia hiyo comment yako.

Asante kwa ushirikiano.

Anonymous said...

Pole mwanamke mwenzangu. naomba ku uliza huyo wifi yako hana bf au mume???? kama hana hebu jaribu kumshauri atafute maisha yake, mtu mzima huyo aliyekosa haya kwann anaingialia ndoa ya watu kiasi hicho??? hebu weka no yake ya cm hapa tumtumie msg za kumpasha coz i real feel you. pole sana

Anonymous said...

Naomba niulize una uhakika kama huyo dada ni dada yake maana watu wana mambo wanaweza wakawa ni mtu na gf wake ila wewe wanakuongopea ni ndugu, usimuamini mtu dunia hii yaani hebu fatilia uone kama ni tumbo moja, na kama wanatoka kagera huwa wanachukuana hata ndugu wa baba mmoja so kuwa makini. pili huyu wifi yako hana life yeye? i mean hana mume au bf wa kuconcentrate? coz ni mambo ya ajabu yeye kuwa incharge wa nyumba ya mwanamke mwenzie. i will b back

Anonymous said...

Wewe Lututu Dar, yaelekea ukweli umekugusa, unajua ni bora kukubali ukweli na kuupokea ili kujifunza kuliko kukasirika na kuendelea kubomoa. Kama wewe ni fukara haiwahusu wengine, point hapa ni jinsi ya kuangalia upande wako kama mume na kuplay part yako kama mume, mke naye nk. sasa ufukara sio hoja, wapo mafukara wengi tu kwenye ndoa lakini si wanafanya kazi bwana, kwa hiyo elfu tano utashindwa kumpa mkeo akikuomba? labda uniambie wewe ni fukara na mbahili pia which makes it even worse! Point hapa ni kujisahau sana kwa wanaume wengi mara wafungapo ndoa, na kuona sasa jukumu la kumfurahisha mwenzi wake sasa limekwisha, simaanishi hii sasa impe mke tiketi ya kuanza mapenzi na majirani no, ila tukubali kuwa hali hii inaweza kutokea sana tu iwapo mume atachangia, msistaajabu ikitokea!
Msitumie gia ya umasikini kwani mapenzi mara nyingi kwenye ndoa kama hamjui yahana gharama yoyote kwa sababu wote wawili mnajua hali halisi yenu financially, wanawake wengi wenye busara huridhika na kidogo mumewe anachopata lakini kama hagawiwi hata kidogo shida huanzia hapo. Oh BTW mimi nieolewa na ninaenjoy ndoa yangu ya miaka 9 sasa, mume wangu hana kipato kikubwa lakini nikichacha hua hasiti kunisaidia, na mimi kipato nipatacho kwenye kazi yangu natumia kwa mahitaji ya watoto wangu hasa ya shule na chakula. FYI mume wangu pia anachacha hata yeye sometimes, nampatia senti kidogo na life goes on, so Lututu your assumptions are very wrong my friend.
Aisha.

Anonymous said...

dada mwenye tatizo nakuombea Mungu akusaidie,mimi ni mkirsto na ninaamini kitabu changu kitakatifu biblia, mwanaume ataacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe na hao si wawili tena bali watakuwa mwili mmoja, mwanzo 2:24, kwaiyo mke mume na mke ndo wamehalalishwa na MUNGU KUAMBATANA NA SIO SHANGAZI, WIFI ,WALA MJOMBA, INA MAANA NDUGU WA PANDE ZOTE 2 ZA WANANDOA HAWANA MAAMUZI YEYOTE KUHUSU NDOA YA WATU 2. YANI MKE NA MUME, SIO KWAMBA WANDG WASISAIDIWE ILA HAWANA MAMLAKA KUINGILIA NDOA YA NDG YAO.

DADA HUYO MUMEO HAJUI MAANA HALISI YA NDOA, MI SIJUI WE DINI GANI ILA NAPENDA KUKUSHAURI OMBA SANA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA KWA KUOMBA MUNGU NA HUKU UKIWA WAZI WAZI KUZUNGUMZA NA MUMEO NA WIFI YAKO. NAAMINI MUNGU ATAKUTETEA TU.

MI ZAMANI NILIKUWA NAONA WAZUNGU NI WATU WA AJABU, LKN NIKAGUNDUA WAKO SAHIHI KABISA,NDOA YA WATU 2 WIFI,SHEMEJI MAMA MKWE HANA SAUTI. MIMI NINA MUME WANGU NA WANANGU 2 PACHA NA NILISHASEMA HAMNA WIFI WALA SHEMEJI KUHAMIA KWETU NA AKAWA NA MAAMUZI ANAKUJA KAMA MGENI ANASAIDIWA WAKAT WAKE UKIFIKA ANAONDOKA.

MS GBENNETT

Anonymous said...

Pole dada kwa maswahiba yanayokukuta. Naungana na dada kemmy, watu wengi wa kagera tabia zao ndo zilivyo. (Sorry kwa wa kagera watakaopitia. tho si wote but majority. Nimeshakuwa na uhusiano na mtu wa kagera, alikua ni mkatili kama shetani, na madada na ndugu ni maneno, umbea kila siku. So usishangae ndo walivyo. Ila ongea nae kama wadau walivyokushauri, na wewe usimame kama mke, usiwe unakubali kila kitu anachotaka wifi.

Anonymous said...

Dinah nakupa hongera kwa kazi yako nzuri.keep it up.

Anonymous said...

Kwa uoni wangu tusiguse kabila moja kwa moja kuwa,`kabila hili,lina tabia hiyo', ndio kuna tabia zimejijenga ndani ya makabila, lakini sio `mila' ila ni watu wenyewe wamejisheheni hivyo. Tujenge hoja tu kuwa mtu huyo asaidiweje.
Nasemahivyo kwasababu kuna watu hawataki kabisa kuoa kabila fulani kwasababu kama hizo zilizopandikizwa. Mimi naomba tusizidi kumwagia mafuta kwenye moto unaowaka, au nimekosea dada Dinah?
emu-three

Anonymous said...

Wajameni, sina mbavu na anonymous wa saa 10:42:00 AM.
Kha!

Anonymous said...

Dada Dinah nimependa utundu wako wa kuwakilisha tatizo kwa mpenzi. Mwenye tatizo ukifanikia njoo utuambie.