Wednesday, 15 April 2009

Miezi 2 tayari ndoa imekuwa ndoano-Ushuhuda!

"Dada Dinah na kushukuru sana kwa kuweka hii blog kweli inatusaidia, ,mimi ni yule dada niliye omba ushauri hapa heading ikiwa miezi miwili tayari ndoa imekua ndoano. Jamani ninawashukuru wote mliochangia mada maana ushauri wenu niliuchukua nakuufanyia kazi kwa kweli nimeona mabandikiko makubwa sana.


Ninasema asante na ninaomba mzipokee shukrani zangu za dhati. Niliongea na mume wangu nikamueleza ukweli kua mwanae nilinaye tmboni ananisababisha nichoke sana na mwili muda wote umelegea legea nikamueleza kua hatamasharti anayonipa yananipa wakati mgumu najikuta nina waza muda wote kwa kweli nashukuru maana sikuamini kama ange-react namna ile kwanza alilia sana nakuomba msamaha kwangu lakini pia alimuomba mwanae pia kama vile anamsikia.


Sikuamini na kuanzia siku ile ananisaidia kupika kama napika ugali basi yeye anapika mboga wakati mwingine nikirudi nakuta kasha pika kipo mezani yani nafurahia kwakweli maana siku akiona sijakaa sawa basi hata kuogeshwa wakati mwingine nikirudi nakuta ameshafua nguo zote kazikunja vizuri.

Kwakweli sikujua kama angeweza kubadilika namna hii, kama siku za weekend yupo off basi saa kumi na moja anakuamsha mama twende tukafue mapema ili upatemda wakupumzika, akiona unafanya kazi sana bila kupumzika ,unashangaa anakuita njoo chumbani ukifika unaambiwa njoo mama nifundishe kuimba huu wimbo au hebu niangalie kuna kipele mgongoni basi tu ili akupe muda upumzike, kweli kilio changu kimegeuka kuwa furaha muda wote .

Dada Dinah ninakushukuru sana kwa ushauri wako na wachangiaji wote mungu awabariki . "

Dinah anasema: Hongera sana kwa kufanikiwa hilo. Tubarikiwe sote!

5 comments:

Anonymous said...

machozi yamenilenga lenga kwa shukrani zako, kweli kila kitu kinawezekana

Anonymous said...

Dah! How happy you are, coz it sounds sweet and smooth! Dada hongera sana,pamoja na mchango wa wanablog Mungu wetu ni wa huruma sana,yaani naona kama ni mimi vile am happy for u my dear. Nami nilileta mada yangu hapa nipokea maoni mbalimbali,kwahiyo nipo nyuma yako nikisubir mwuujiza wangu ili niweye kufurah na kutoa ushuhuda kama wewe. Dada Dinah be blessd" mama Juniour

Anonymous said...

Maisha ya ndoa yanahitaji subira,uaminifu na kuhurumiana. Wengi wanaovunja ndoa zao wanakuja kujuta baadaye, kwasababu walichukua hatua hizo bila kufikiria, au kupata muda wa kufikiri.
Tunashukuru kuwa wewe ulifuata mawazo mema na kuyafanyia kazi. Tunaomba usibweteke, kwani wapo ambao baada ya kumuona mume anafanya kazi zote akawa anakunja nne kwenye kochi huku anasoma gazeti au anasikiliza taarabu na kuagiza, `niletee hiki, nifanyie hiki, mbona siku hizi hufanyi hivi....Na baya zaidi mume akitaka kitu anaonyeshea kwa mguu `si-kile pale,siu-ende mwenyewe...
Mke akijibidisha katika majukumu yake ni starehe ya aina yake. Ukimuona mkeo anakutandikia kitanda, au anakutengea maji ya kuoga,kuna `upendo na kujali' kwa namna yake. Na mume akijituma kwa shughuli za namana fulani kuna `hali ya kuaminiana' au sio.
Kusaidiana kuwepo, hasa kipindi cha matatizo,kuchoka nk, lakini sifa ya mke kama mke na sifa ya mume kama mume, tusizisahau, kwani tukizisahau, basi hata ile hali ya `mume wangu au mke wangu' itapotea na matokeo yake mengine!
emu-three

So much said...

Am happy for u,Mungu atakujalia utajifungua salama usalimi na mtoto mwenye afya.

Anonymous said...

Dinah,,,u rock honey!! unachangia sana katika kuimarisha na kutunza mahusiano yetu,,ubarikiwe zaidi. Mdada nakupa hongera na uzidi kufanikiwa kwenye ndoa yako