Thursday, 9 April 2009

Miaka 5 na Mume wa Mtu-Ushuhuda

MIAKA MITANO NA MUME WA MTU - USHUHUDAPole da dinah kwa kazi ngumu ya kuelimisha jamii. Nakumbuka mada hiyo hapo juu niliitoa mwaka jana ila nashukuru kuna walionipa ushauri mzuri nikaweza kufanikiwa japo kuna walioniponda.


Dada yangu nimeamua kusalimu amri nimeshaachana na mume wa watu na kuamua kukaa kutulia kuhangaika na maisha yangu huku nikimwomba Mungu anisamehe sana. Ila nahitaji ushauri nini cha kufanya kwa sababu jamaa kakataa kuwaweka wazi kwa ndugu zake na hata mkewe kuwa hayuko na mimi.


Tena anasema walivojua tunauhusiano ndo watakavojua tumeachana sasa kinanishinda kitu kimoja coz mkewe ananitumia sms za matusi kila kukicha, mara anapiga simu nashindwa la kufanya sipokei wala kujibu Je nifanyeje ili huyu mwanamke asiendelee kunisumbua na ajue its over me na husbad wake? Naomba ushauri wako dada pamoja na wachangiaji wote.
Niwatakie siku njema"

Jawabu:Asante sana kwa kurudi tena na kutuma "feedback". Miaka mitano sio "kitoto" yeye huyo mwanaume mwenye tabia chafu haamini kabisa kuwa wewe kama mwanamke unaejiamini umesimama na kumwambia sasa imetosha na kila mtu achukue ustaarabu wake.


Sio wanawake wengiwa Kibongo wenye kujiamini kama ulivyoamua kuwa wewe hasa ukizingatia mume huyo wa mtu alikuwa akikuangalia ktk hjaliz zote hasa kiuchumi. Hali ya yeye kukufanyia kila kitu ali-relax nakujua kuwa "imetoka" yaani huwezi kuacha maraha anayokupa na mapesa na ndio maana hataki kabisa kuliweka wazi hilo kwa ndugu na jamaa zake. Chukulia kuwa hilo ni tatizo lake na anapaswa kurekebisha mambo na mkewe ili apate kile alichokuwa akikifuata kwako.

Huyo mwanamke anahasira sana na wewe, kama ambavyo mwanamke yeyote angeweza kujisikia baada ya kuibiwa mumewe. Tofauti ni kuwa mwanamke huyu badala ya kufanyia kazi suala zima la kwanini hasa mumewe alitoka na wewe kwa kipindi kirefu hivyo na kujaribu kujirekebisha na kuimarisha ndoa yake anapoteza muda kukutukana wewe....again chukulia kuwa hilo ni tatizo lake kwani wewe umekwisha nawa mikono na huusiki na lolote linalotokea kwenye uhusiano wao hivi sasa.

Kutokupokea wala kujibu ni uamuzi mzuri sana, sasa ilikuondoa usumbufu wa huyo mwanamke badilisha nambari yako ya simu na hakikisha hakuna mtu kutoka pande hiyo anaijua nambari mpya hiyo.

Kuwa na siku nzuri.

7 comments:

Anonymous said...

nakumbuka wewe dada ulisema huyo mke mwenza umemficha hajui kama wewe ndo upo nae husband wake, sasa leo nashangaa wapokea mitusi toka kwa huyo mke mwenza, ts right ana hasira hata ungekuwa wewe ungefanya the same kuibiwa asikwambie mtu inauma sana tena saaaana,
Lkn pia nikupongeze kufikia huo uamuzi ambao wengi huwashinda, hasa wanawake to be more specific, sasa kama umeweza wastahili hongera, ila unatakiwa kuwa siriazi na unachosema hapa coz huyo jamaa anaweza akawa ana kuja siku moja moja ambavyo huwezi jua na mke wake kama ana mfatilia still so unaweza jikuta siku ya siku upo chini ya ulinzi wa mkewe atakufanya chochote including application ya hasira ya kuibiwa na kumpata live mwizi, hope unajua kinachofuata hapo....imagine ungekuwa wewe ndo unahangaika hivyo umemkuta mwizi wako ungemfanyaje, so jibu utakuwa nalo.
Uamzi mzuri big up!

Lajk!

Anonymous said...

kweli mwanamke mwenzagu ukathubutu kukaa na mume wa mtu 5yrs!!!!!!!!!!!! hivi nawe unategemea kuolewa au????? jamani inabidi mtuonee huruma tulioko kwenye ndoa tunateseka jamani!
mrs,farry

Anonymous said...

DADA NAKUPONGEZA KWA UAMUZI ULIOUFANYA JAPO SINA BUDI KUAMINI KUWA HAUKUWA MRAHISI.
KWANZA, MIMI NAONA KAZI KUBWA ILIYOBAKIA NI KWA HUYO MNAMUME.WEWE YAKO UMESHAMALIZA. MKEWE KUKUPIGIA SIMU NA KUKUSUMBUA NI WAZI KUWA MUME WAKE HAJAFANYA ALICHOTAKIWA KUFANYA NACHO NI KUMUELEZEA MKEWE WAZI KUWA UHUSIANO WENU SASA UMESHAKUFA.
PILI, HUYO MKEWE KUKUSUMBUA NA SIMU ZA MATUSI NI KUWA HAYO NDIO MATOKEO YA CHOICES TUNAZOZIFANYA MAISHANI. UNAJUA KILA TENDO TUTENDALO HAPA DUNIANI LINA MATOKEO YAKE(CONSEQUENCES), ZAWEZA KUWA POSITIVE AU NEGATIVE, BAHATI MBAYA ZAKO NI NEGATIVE, KWA HIYO KWA UPANDE MWINGINE IS LIKE YOU ARE PAYING BACK KWA ULIYOMFANYIA MWANAMKE MWENZIO. USHAURI WANGU MIMI SIKU ZOTE KWA WANAWAKE WENZANGU NI KUWA JITAHIDI SANA USIWE WEWE NDIO WA KULETA HUZUNI KWENYE NDOA YA WATU HATA KAMA WANA MATATIZO YAO, MAANA NA WEWE SIKU MOJA UTAKUWA NA WAKO UKIFANYIWA HIVYO UTAJISIKIAJE? SINA HAJA YA KUPREACH, ILA YOU NEED TO DEAL WITH THE REALITY. POLE SANA DADA NA TIME WILL HEAL YOU WOUNDS!

Anonymous said...

lol da dina bbwana mbona sijakubaliana na wewe kwenye jibu lako,hivi ni kweli kila mwanaume anayetoka nje basi mkewe anachemsha,please!!!.sikiza dada mi nimetongozwa na married men na woote walikuwa na rings zao vidoleni.so mimi ndo nilikuwa na power ya decision.Namshukuru Mungu kwa kunipa moyo huu sababu wasichana kama mimi tunajiingiza humo sababu ya mapene hamna lolote no love no nothing. sorry dinah lakini hii isuue lol anywho katika hii feedback Dada jambo la msingi na heri badili no yako ya simu kwishney.Lol asikudanganye mtu shogaangu alikuwa na bifu na ex girl wajamaa yake hata mimi nilimjibia sms.sababu kwa hali ya ubinadamu ni ngumu kusoma majitusi na kashfa na kunyamaza kimya.soln alipata no mpya ya simu sasa anasihi kwa amaniiiii.Goodluck

Anonymous said...

Natamani sana kukupongeza kwa uamuzi uliofanya wa kumuacha mume wa mtu lakini nashindwa, unisamehe kwa hilo kidogo nina hasira na wewe. Wewe ni mwanamke na utaolewa siku moja Mungu akipenda, haya ukajaibiwa mumeo kwa miaka mitano si utapelekwa mirembe? Jamani women think b4 you make some stupid decisions, ukiiba boyfriend wa mtu mkiwa shuleni bora mara mia lakini mume wa mtu kisa anakutimizia mahitaji yako, this is very selfish, nina maana kuwa wewe ni katika wale wanawake selfish tunaowaona kila siku, ndio ana issue na mkewe sasa wewe ndio suluhisho bibi?? bila kujijua wewe ndio umezidisha matatizo kwenye ndoa ya watu, kumbe labda usingejitokeza kwake huyo bwana sasa hivi angekuwa anaenjoy ndoa yake na mkewe, ndoa zote zina matatizo shoga asikudanganye mtu lakini mara nyingi waachie wenye ndoa watibuane wenyewe watapatana, na kama wataachana wewe usiwe ndio uliowatenganisha. Anways hongera kwa kuchukua uamuzi huo ila shosti wacha na wewe uone cha moto kama alivyojisikia huyo mkewe. Kila la heri!!
Shamsa.

Anonymous said...

Sijawahi kusoma mkasa huo, Ila leo nimeamin kuwa kweli a woman is different! & she is dangerous!!! Yaani kweli unadiriki kuwa na mume wa mwanamke mwenzako miaka 5!? Aiseee, kweli leo nimekubali kuwa wanawake wao kwa wao hawapendani na wanafanyiana unyama! Hiv we dada unategemea kuolewa kweli? Kosa ulilofanya halina tofauti na mtu anayekuua huku anakuhurumia! Soma mkasa ktk gazeti la UWAZI unaosema NILIMUUA MUME WANGU ILI NIOLEWE NA TAJIRI. Yaani huna tofauti na mwanamke huyo japokuwa we umemfanyia mwanamke mwenzio. Use common sense vp ingekuwa niwewe. Na kama ungekuwa na moto ndo ungekuwa ushamuua mwanamke mwenzio. Ok huu si wakati wa kujiuliza ni jinsi gan ya kumuatak mwanamke mwenzi ni wakati wa kufanya tawba [toba] ya kweli kwa mola wako. Na ili kuepuka usumbufu wa mwanamke uliye muumiza ni kubadili laini. Mshahara wa ufisadi ulioufanya ni kuwa utaolewa na mwanaume kicheche! Ili nawe uonje uchungu wa mume. Imeandikwa 'maana mzinzi atamuoa mzinzi mwenzake' So, if happen dont wonder!! U wil be responsible for that.
Sikuhukumu ila natoa fundisho kwa wengine maana blog hii wanasoma wengi hivyo nili ni fundisho kwa wengine wenye tabia mbaya kama yako.
By mw.
Enjoy ur day

Anonymous said...

Naomba dada Dinah usitupilie mbali hii maaana leo ninataka kukucritisize kwa wema lakini na si kwa ubaya, again this is just my opinion na nadhani utaipokea in a more positive way.
Binafsi nadhani umekosea unaposema "Huyo mwanamke anatakiwa alifanyie kazi suala zima la kwanini mumewe alitoka nje na wewe na ajaribu kujirekebisha badala yake anatumia muda mwingi kukutukana wewe...again chukulia kuwa hilo ni tatizo lake". really, mi nadhani si wanaume wote watokao nje ya ndoa wana issue na wake zao, japokuwa huyo dada alisema ndivyo alivyoambiwa na hilo buzi, what if the guy is lying just to get into her underwear? what if ame mbrainwash huyo muuliza swali ili aamini hivyo na kumbe sivyo? nadhani umekuwa too judgemental kwenye hii issue! ndoa zina matatizo karibu zote, lakini haimaanishi ndio gia ya kutoka nje, ukisema kama ulivyosema basi ina maana unaipa goahead hiyo concept nzima ya wanaume kucheat. Nadhani ushauri mzuri ungekuwa ayafanyayo huyo dada ni outcome ya hasira alizonazo juu ya uhusiano wa mumewe na huyo dada period. Just because ameacha kutembea na huyo mume wa mtu, haimaanishi hataadhibiwa, lazima avune matunda ya alichokipanda kwa miaka mitano, damn that's a long time lol, hata ingekuwa mimi ni huyo mke ninayeibiwa nisingetuma matusi tu kwenye simu, ningefanya yasiyofikirika, i swear pamoja na kwamba nina issue na mume wangu haimuhusu mtu mwingine kuja kujenga kambi kwenye ndoa yetu!
Again that's just my opinion, nadhani anahitaji hongera kwa kuacha alichokuwa anafanya, lakini mkewe jamaa pia anahitaji hongera zaidi kwa kumvumilia mumewe mzinzi kwa miaka mitano. Again si wanaume wote watokao nje ya ndoa wana issue na wake zao, infact wengi wako bored na wanataka kutest sehemu nyingine, ndio maana wengi wakishikwa wanajuta na kutubu mbele za wake zao!! Pasaka njema Dinah!!