Friday, 24 April 2009

Anataka kuacha wake kuja kwangu-Ushauri

"Mambo vipi.
Mimi nilikuwa na mpenzi ambaye tumekuwa pamoja kwenye mahusiano kwa
miaka minne. Mwaka jana tuliachana kwa sababu kadhaa, na moja wapo ni kuwa eti
alikuwa anahisi ninamchezea hivyo sitamuoa. Pia alitaka nibadili dhehebu kutoka
Lutheran na kuwa Roman Catholic.Kwa kweli tuligombana sana kwa sababu sikuona haja ya kubadili Dini wakati Dini ni kati yangu na mungu. Sasa wakati tunagombana alikuwa akiniambia maneno kuwa sitapata msichana
atakayenipenda kama yeye.


Tumeachana kama miezi sita hivi. Mimi niliendelea kivyangu nikachukua mwanamke
mwingine na yeye pia akapata bwana wake. Sasa cha ajabu amekuja kwangu na
kuniomba turudiane. Eti huko alikoenda hakupenda kama anavyonipenda mimi.
Eti anajuta kwa makosa aliyofanya na kudhani she can replace me.


Pia anasema amegundua kuwa jamaa ni player tu. Ingawa alimuahidi kumuoa. Sasa ameniambia
kuwa ameamua kumuacha hata kama mimi sitakubali kurudiana nae. Sasa wadau
nishaurini.Hivi kweli huyu amedhamiria kujirekebisha na kuwa nami tu au ndio
anaona noma mambo yamwekwenda vibaya kwake? Nimchukue tena?


Halafu kitu kingine ameniambia kuwa yuko radhi kufanya mapenzi na mimi kama nitakubali coz the way I do it makes her feel good. Hata alipokuwa nae jamaa alimueleza kuwa bado nipo
kichwani kwake ingawa tumeachana."

Jawabu: Mambo poua kabisa hapa, vipi wewe? Miezi sita ni michache sana kwa yeye kukufuta kichwani kwake sio hivyo tu bali hata kuanzisha uhusiano mpya hasa kama mlipendana kwa hati na uhusiano wenu ulikuwa wa muda mrefu kama ulivyokuwa wenu. Hilo mosi.

Pili, inaelekea ninyi wawili mlikuwa mnataka vitu tofauti kwenye maisha yenu ya kimapenzi ukiachilia suala la kubadili Dini (Dini ni imani na sio muhimu sana kama mapenzi), mpenzi wako anataa sana kuolewa lakini wewe ukawa unachelewesha mambo labda hukuwa tayari au vinginevyo.

Inaelekea huyo Ex Mpenzi wako hajui kuwa unampenzi mpya na ndioa maana ameku-offer ngono akidhani kuwa una minyege mpaka kwenye kope, kama angejua sidhani kama angeshupaa kutaka kurudiana na wewe.

Mwanamke yeyote anaefananisha au kumponda mwanaume aliyekwisha kuwa nae sio wa kumuamini kwani yote anayoyasema kwako kuhusu mwanaume mwenzio ndio aliyokuwa akiyasema au atayasema kwa mwanaume wengine atakae kuwa nae kwamba yule jamaa hivi na vile na hajawahi nifikisha kabisa....kwanza ana kibamia n.k

Kutokana na maelezo yako hapa inaonyesha wazi kabisa kuwa unayo nia ya kurudiana nae ikiwa amedhamiria kujirekebisha.....lakini vipi kuhusu mpenzi ulienae hivi sasa?

Angalia wapi moyo wako unaridhia kwa ex mpenzi au kwa huyu wa sasa? Wapi unahisi unafuraha zaidi? Jiulize nini unataka kutoka kwenye uhusiano wako na je unakipata au kuna uwezekano wa kukipata? Lini ulihisi amani zaidi sasa au miezi sita iliyopita? Je uko tayari kufunga ndoa?

Kumbuka kuwa kama ulikuwa na mpenzi kwa miaka kadhaa kisha mkaachana na akaenda kulalwa na mtu mwingine kisha ukarudiana nae ilemiaka mliokuwa pamoja inafutika na mnaaza upya.....sasa je uko tayari kuanza upya na mtu aliyekuacha kwa ajili yamtu mwingine? Kama jibu ni ndio.....vipi kuhusu huyu mpenzi wako wa sasa? Kama yeye angefanya hivyo ungejisikiaje?

Tafakari majibu ya maswali nilikuuliza kisha fanya uamuzi wa busara ambao hutojutia hapo badae. Kila lililo jema!

6 comments:

Anonymous said...

Wewe jee miezi hiyo sita ulikuwa na mpenzi? Na kama unae jee unampango nae gani? Tuangalie ngoma jamani.

Mimi nadhani kama mnapendane then endeleeni, lakini kwa condition kwamba kila mmoja ameshapima ngoma, na mkapima tena baada ya miezi mitatu.

Kumbuka alikuacha sababu ya jambo ambalo halijabadilika mpaka leo. so kuwa muangalifu.

Anonymous said...

Huyo mwanamke anaugonjwa wa wivu.
Alijiona yeye mali na angekuendesha atakavyo, sasa anaona umepata mnayesikilizana eti anasema anataka awe na wewe.

Ushauri achana naye kwani hata akija tena kwako ataanza mengine yakukuendesha atakavyo.

Ushauri wa mwisho mwambie asikilize ule wimbo wa Ali Kiba Cinderella

Anonymous said...

Hi Brother,

Huyo dada anahangaika tu na maisha, hana maamuzi juu ya anataka mpenzi wa namna gani katika maisha yake. Kilichobaki anajaribu kutest huku na huko. Kama alikoenda angeridhishwa sidhani kama angerudi. Hivyo wewe angaalia kama huyu mwanamke uliyenaye unampenda huyu achana naye ni tapeli wa mapenzi anataka kukuvurugia.

Anonymous said...

Kwanza hata wewe inaonyesha hujatulia! We si umesema ulipata mchumba? Sasa umemuweka wapi? Hebu acha tamaa! Umezungumzia mahusiano yako na Dini(MUNGU) Ni Mungu gani anaruhusu zinaa? We unataka watu wakushauri kuzini na huyo dada, Mungu wako anakushauri nini ktk vitab vyake vitukufu kuhusu zinaa?. Dont be ignorant, inaonyesha una tabia ya umalaya, na huyo demu wako pia ni malaya!
Ushauri wangu ni kuwa fikir upya kuhusu maisha yako, na tafakari je huyo mwanamke unampenda kwa dhati? Na kama unampenda je na yeye anakupenda? Then make decision, aidha umuoe au utafute mke bora mwingine na sio kuendekeza zinaa tu!
But all in all, the woman doesnt love u with all of heart, coz ya mambo aliyofanya.
By Mwatima

Anonymous said...

Wewe umesema ulipata mwingine na yeye akapata mwingine, yeye huko kachemsha,ligwaride limemshinda anakuja kwako, je wewe na mwenzako mnaendaje?
Kwasababu wewe hupo peke yako tena una mwenzako, au sio? Na uamuzi utakaochukua utakufurahisha wewe kama `bado unampenda zilipendwa' na kumuumiza `aliyekusitiri wakati wa shida'
Kitu kikubwa cha kujiuliza, je unayempenda ni yupi kati yao, na je unamfikiriaje huyu uliye naye sasa. Kumbuka kwa hali uliyo nayo `hujiamini' wewe mwenyewe. Kaa chini ufikirie unalolifanya na ujiulize kama wewe ungefanyiwa hivyo ingekuwaje! Isije ikawa kesho na keshokutwa unajutia uamuzi uliochukua.
Kwa msaada zaidi, wewe umekaa na wote na unawafahamu vilivyo, angalia nini unachokitaka katika maisha yako, sidhani wote wako sawa,kitabia, kisura na nk.
Ila ni vyema uhakikishe usalama wako,kwani kwa namna hiyo umeshatembea na watu zaidi ya watatu. Upime kabla hujaamua kutulia.
emu-three

Anonymous said...

Asanteni wote kwa ushauri wenu. Mimi mpaka sasa sijampa jibu huyu dada kuhusu kurudiana nae. Pia naomba nimjibu dada dinah kuwa nilishamueleza kuwa nina mwanamke mwingine. Na yeye akaniambia yuko radhi kumake love na mimi ingawa nina mwanamke mwingine. Anasema kuwa amechoka kuumia na anataka atulie. Na ananitaka mimi. Halafu kitu kingine ameniambia kuwa anataka nimpe mimba coz ana hamu na mtoto halafu ana miaka 28. So anaona miaka ya kuzaa inayoyoma.

Thanks all.