Wednesday, 18 March 2009

Penzi limepauka Baada ya Kutoka Ulaya-Ushauri!

"Dinah pamoja na wanablog hi(wenzangu) hope Mungu amewapendelea bado mpo wazima, nashukuru kwa hilo.Tatizo langu i wish to know what is going on!


Habari ipo hivi; ni ndefu najitahid kuifupisha and if theres any question I will be there plz, I have a boyfriend and I Love him so very much! Tatizo ni kuwa simwelewi siku hizi kwani hataki tuonane na nikimpigia simu hapokei, nikituma text anajibu siku anayojiskia. Nikimwuliza vp mbona hivi anauliza kwanini kwani yeye ni mzima wa afya wewe tu" ndo anavyojibu kwa msg mana sim hapig wala hapokei.


Huyu bwana miaka minne nyuma alikua anasoma UK kamaliza na mwaka jana karudi yupo TZ, nilimpigia kabla hajarudi nikamwuliza unakuja lini? akaniambia zilikua zimebaki siku chache.

Siku ya siku ikafika akawa amekuja na alipofika alinipigia kanifahamisha amefika na akanipa namba yake na kusema kuwa kuna kazi anafanya na atanicheki baadae, nikamwambia poa. Lakini ile baadae aliyoniambia haijafika hadi leo kuanzia mwaka jana mwezi wa tisa hadi leo tarehe 25 february!

Ndo hivyo, namwuliza kwanini unafanya hivi? anasema "kwani nimefanya nini?" Hasemi chochote na nikimwuliza is it over between us hasemi kitu, kanisumbua sana ukizingatia nilikuwa namsubiri tangu aende kusoma miaka minne anarudi leo ananifanyia mambo kama hayo,kweli is it fair?


I have been faithful for him since I knew him, sio hapo tu nimwaminifu hata kabla sasa kwanini anakua hivi? sijui anafanya nini? anawaza nini? or what is he passing through?Sasa ndio nawaza niachane nae na nimfute katika maisha yangu kwani naona anazidi kuniumiza tu. Pia najiuliza sijui ana matatizo gani what if naswitch my mind to another man and soon later he come back, how wil it be??

Ndugu zangu nasubiri mchango, mawazo,ushauri kutoka kwenu,nitakuwa najibu maswali yenu kama kuna mahali hamjanielewa.
thanx"

Jawabu:Hello, asante kwa kuwa na subira lakini hata hivyo maelezo ya wasomaji wangu kwa kiasi fulani yatakuwa yamekufungua macho nakuanza kuyafanyia kazi yale ambayo ulidhani kuwa yatakusaidia.


Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa kuna mambo mawili-matatu yanayomfanya bwana kukukwepa tangu arudi nyumbani. Kama sio kuwa alikuwa na wewe ktk mtindo wa kupoteza muda au kwa maana nyingine wanasema "4 fun" na hakuwa "serious" na uhusiano wenu basi yuko kwenye mshituko wa hali halisi ya maisha hapo nyumbani tofauti na alivyodhania wakati yuko Ulaya. Vilevile huenda kurudi kwake nyumbani hakukuwa kwa kujiandaa bali kushitukizwa (karudi bila kukamilisha mipango yake kimaisha) hali inayoweza kusababisha mshituko.


Kwa kawaida mwanaume anapokuwa hajakamilishamipango yake kimaisha suala la uhusiano wa kimapenzi huchukua nafasi ya tatu kama sio ya mwisho kabisa, yaani inakuwa sio muhimu sana na anaweza kuchukulia mapenzi au uhusiano ni kupotezeanaa mida kwani sote tunatambua kuwa anapokuwa na mpenzi ni kujiongezea jukumu maishani. Sasa kama majukumu uliyonayo yanakushinda au hujayamudu vya kutosha kwanini basi ujiongezee jukumu lingine.


Kukukwepa haina maana kuwa jamaa hakupendi la hasha! huenda anakupenda ila mpangilio wake kimaisha hauruhusu yeye kuwa na wewe na hapendi kukuumiza au anashindwa namna gani akuambie kuwa anakupenda sana tu lakini angependa uendelee na maisha yako.


Napenda ufahamu kuwa pamoja na kuwa wanaume wanahitaji mapenzi, kupendwa, kujaaliwa nakadhalika kama ilivyo kwetu sisi wanawake, wao wanalichukulia suala zima tofauti kabisa natunavyolichukulia sisi wanawake

Nakuja sasa hivi...

35 comments:

Anonymous said...

mpendwa,mbona anaonyesha kila kitu waziiii.The way it looks for me ,hana mpango na wewe .Move soon efore u go crazy

mbelembele2008@yahoo.com said...

mie nakushauri umpige chini kwani anayokufanyia ni dalili kwamba yeye hakupendi na wala hakumiss.ila uwe mwangalifu kwani magonjwa mengi.tafuta umpendae.huyo hakutaki.give it up babe!!!!!!!

Dada Kemmy said...

Pole sana mrembo!
Kwanza kabisa kwa jinsi nilivyomsoma huyo noyfriend wako atakuwa na msichana mwingine pengine ndo maana anakufanyia visa wewe may be ni trick ya kukuacha.
Nakushauri tafuta ukweli kwanza kwa maana ya kuchunguza kimya kimya ukipata ukweli pls take ur time jione na wewe wa thamani zaidi yake,maana sioni logic ya kukaa unabembeleza mtu asiyebembelezeka kama unapiga simu hapokei,na he dont want even to reply any text wanini sasa??inauma sana najua lakini anza kujiona wa thamani wewe kwanza kisha utaona ya nini kung'ang'ania expired love mimi naita!
Ukichunguza ukapata ukweli pls run away from his arm!
Mwisho muombe na mungu akupe jibu sahihi na mume sahihi pole sana!

Anonymous said...

Pole sana mpenzi. Huyo hakutaki anashindwa tu jinsi ya kukwambia. Imeshanitokea pia, nikaachana na huyo mtu. Anafeel guilty kwa kukuweka miaka minne. Achana nae, utapata mwingine, na usirudi nyuma tena, atakuharibia na hatakuoa

Anonymous said...

Ni miezi sita since arudi. Hakupigii simu, hapokei simu zako. Msg anajibu akijiskia na tena kifedhuli.

Wewe dada ni nini tena unataka? Hiyo ndio over. M telling u from expirience. Unajua not all men can say 'it's over', wengi wao wanakuwa cowards and wanakimbia. he is one of them. So u better read the signs and move on.

Huyo atakuwa kaona hufai kwake, ukute katafuta mwingine na anakuonea huruma kukwambia. Hivo anajaribu kukukera ili wewe umwache. Yani hataki hata kuonana na wewe. Dada be brave and smart.

Mwandikie msg kama hivi.. 'hi, miezi 6 imepita, sielewi kinachoendelea, kama wewe umechoka ila unaona huruma kuniambia basi naomba nikusaidie kusema kwamba mimi na wewe basi, nakutakia kila la heri, i wil move on wit my life, God stil loves me.'

Nikupe moyo dadangu? God loves u. N u have been faithful and good to urself and this man, basi mungu atakupa mwanaume mzuri sana atakeakupenda na kukuthamini.

Mimi niliwahi kufanyiwa kama wewe, niliumia kwa miaka miwili, i was stupid and young and naive.. but nimejifunza. Now nimepata a man ambae ananithamini siwezi kukueleza, i feel like a woman and he loves me dearly, yani i am alive again and i believe again. So usife moyo. U will get there. But this man, muache.

Au kama huwezi kumwacha basi mchunguze, for sure utakuta ana mtu. Na hata kama hana, wewe huoni kama hakutaki? Please please usipoteze muda wako.

Anonymous said...

Pole sana mdada,
hilo lililokupata wala usione la ajabu na wala lickuchanganye kichwa, waafrika wengi (especially watanzania)si wanawake or wanaume wakienda nchi za ulaya huwa wanazuzuka sana!, kama alikuwa na mpnz bongo basi atamletea mapozi ya ajabu ajabu sasa sijui ndo kumuonesha mtu kwamba yeye ametoka Ulaya me i dont know! u have to call your boyfriend na muongee kuhusu unavyojisika kutokana na mambo yake, na akueleze msimamo wake uko vp na we utoe msimamo wako ili msije mkalaumiana mbeleni, usiachane nae kwanza mpk umsikie anasemeaje kuhusu mustakabali wa mapenzi yenu, majibu atakayokupa they will show you what to follow kama kuachana naye au kuendelea naye.
Shushu "Hot"

Anonymous said...

Girl, he doesnt want u anymore. Not all men can say bye, most men are cowards. So honey move on wit ur life. God loves u and u wil get the man that was meant only for u. Do not give up on God coz he has not forgotten u. Leave that son of a gun. He probably met someone wen he was in UK. To him u r history. Stop wasting ur time.

Anonymous said...

Hapa ili upate uhakika wa mia kwa mia ni mpaka mkutane naye uso kwa uso, na umuulize kulikoni. Kwasababu wewe unampenda, na huenda na yeye ni vivyo hivyo, kwahiyo ukiamua vinginevyo, siku akikujia tena wakati umeshamnyaka mwingine utaumia sana, na huenda akakupa sababu za msingi kwanini alikuwa akikugandisha.
Katika maumbile na tabia za watu, wapo watu ambao hawapo wawazi moja kwa moja,wanataka jambo liende muda ukifika. Wapo watu wanamipangilio kichwani, lakini kimatendo huwezi kuwajua. Kwahiyo inabidi kusomana, inabidi kuulizana na la msingi ni kuwa na subira.
Hatuwezi kujua moja kwa moja kuwa jamaa yako yukoje, na usikimbilie kusema labda jamaa kampata mwingine, huenda, lakini usihakikishe kabla hamjakutana. Siunajua tena `mtu akipaa majuu hubadilika, lakini sio kwa wote.
Hayo ndio maoni yangu
emu-three

Anonymous said...

Ma dear yani mbona all the red signs zinajionyesha HE IS JUST NOT INTO YOU. futa vumbi anza mbele bado unachance ya kumpata ambaye HE IS INTO YOU!!!! all the best dear tafuta hicho kitabu isome kitakupa mwangaza wa mambo ya malavidavi

Anonymous said...

AChana nae huyo... tangu mwaka jana September arudi hajakutafuta? Na jinsi wanaume ninavyowajua wasivyoweza kustahimili.. anataka kutuambia hana hamu ya kungonoka? Kama anayo sasa ana ngonoka na nani na ww ndo gfriend wake? Dada fumbua macho... huyo ana mwingine FULL STOP. Miezi yote hiyo anamlala nani? wanaume huwa hawawezi kukaa muda mrefu bila kungonoka! angakutafuta tu kam hana mtu

Juliet said...

Mamie pole sana lakini usife moyo,mi naomba unijibie maswali yangu haya ili nijaribu kukushauri,mawasiliano kwa ujumla yalikua vipi wakati kaenda Uk? na je alishawahi kurudi likizo? na kama alirudi mlionana na mambo yalikuaje?hope umenielewa!

Anonymous said...

hapo juu napenda comment yako ya movie he is just not into you thats so true.achana nae .

SIMON KITURURU said...

Yote wameshaongea wengine.
Lakini, usishangae kuwa yeye ndio anakuchunguza wewe.

nakumbuka miezi michache niliyokuwa Bongo karibu kila mtu unayemfahamu kuna mtu atakuambia ana MDUDU.

Na nilikutana na raiki zangu wawili waliokuwa wanawaogopa ma girlfriends zao kutokana na kuambiwa kuwa kuna jamaa wenye mdudu vibosile walikuwa wanawatumbuiza kinamna.

Nakumbuka mpaka ugomvi mmoja uliozuka baada ya jamaa kushauri wakapime na mwanadada kuanza kulia kuwa: yani navyojitunza na yote tuliokuwa tunaongea kwa simu bado huniami na unasikiliza ya watu, Wakati mimi ulivyokuwa ulaya niliamini unajitunza kunisubiri.

Kwa kifupi nachotaka kusema ni; BONGO kunatisha toto wengi labda Bwana yako katishwa kuhusu wewe hata kama ni kwa uongo.

Wapiga tararila na watunzi wahadithi za watu wengi Bongo Nyoso.

Ongea naye kwanza kama bado chale la kuwa kakuacha halijatulia ingawa najua kwa kuuliza hapa unajua tayari UMEACHWA!:-(

Anonymous said...

Dada Mungu atakusaidia na atakureward kwa uaminifu wako na trust yako uliokua nayo kwa jamaa, lakini ukweli dalili zi wazi mapenzi ya kweli hayawezi kuwa hivi,miezi 6? bila kukuona? Mwambie black and white juu ya msimamo wako hata kwa simu/text sababu wakati mwingine ukimya unamanisha NO,
Mimi ni kijana wa kiume na kitu kinachokabiriana na hicho kimenitokea na sasa nina regreat kumuamini mtu ambae ameutenda moyo wangu nilikuja nyumbani kwenye graduation yake lakini hakuniruhu kwenda na mawasiliano yakawa shida watu walinishauri nimuache lakini sababu nilimpenda sana nna kumwamini sikujali lakini nasikitika sasa ameniacha wakati moyo wangu haukua umejiandaa kuachwa na mtu niliemuhesabu kama mke wangu mtarajiwa so kunusuru moyo wako tafadhali act now ili uwe na peace of mind,mueleze ukweli kuwa imetosha na kama kweli bado anakupenda na kukujali utamuona na kama ndo hivyo hivyo basi anza ukurasa mpya na usijali Mungu atakupa mtu atakae jali feelings zako.

mdada said...

mh dada mwenye tatizo pole sana naelewa unayopitia ila niko ktk upande mwingine wa shilingi nitakujibu ktk sehemu 2:
1)Inawezekana jamaa yako alipokuwa UK hakuna la maana alilofanya(hakusoma na kama alisoma hakuna alichofanya tunawaona wengi huku wanadai wanasoma miaka nenda rudi akiona kimeharibika anarudi tz ila ndio amekiharibu) yuko ktk shock ya kuona wenzie wako mbali kimaisha(kikazi na kijamii) ni tatizo kubwa hasa kwa wenzetu wanaume anashindwa kuadjust vipi ktk jamii manake watu wanategemea arudi na afanye mambo makubwa si alikuwa nje bwana....inawezekana ana msongo wa kimawazo na hana jinsi ya kuanza kukwambia ushauri wasiliana naye akuambie tatizo ni nini na ana mpango gani na wewe kama hakushirikishi akiwa na matatizo huyo hakufai so akili kichwani mama
2)ana mtu anamzingua huko na anakuona we wa nini so if thats the case leave the dude alone he is just not into u(as s1 said hapo juu) hujasema mawasiliano yalikuwaje alipokuwa UK wengi huwa na watu wa kupozea huku na hadi kuishi nao(kusave bills aka kumove in) na akipanga kurudi nyumbani anajua nani amtakaye kimaisha sasa huyo mwenzio miezi sita kimyaaaaaa dada bado wauliza ufanyeje?? mi ningeshaanza zangu zamani so move on na maisha yako na msahau kama he was meant to be urs ataruka weee lakini atarudi kwako when time is right ila kabla hujafanya uamuzi wowote ningekushauri ufanye mawasiliano naye for the last time akiuchuna endelea na maisha si mwisho mami(mi nilitoswa jamaa kaamua kurudi tz nikipiga simu naletewa visingizio kibaoo nikaachana naye kaiaina nimeenda likizo akanipigia simu eti niongee na gf wake mpya nimhakikishie kuwa mi na yeye hakuna lolote kati yetu imagine!!)

Anonymous said...

Wapendwa Nawashukurv sana sana sana! Kwa mchango ulonipatia,nitamwomba Mungu aniongoza namna ntakavyofanyia kaz michango mlionipa. Aksanteni sana,ila niwaulize nyie wanaume mnaotoka ulaya na kuwatenda mambo ya hiyana walo mlowaconsider wapenz before u left mnawaza nini!! Mschana akiwa kicheche tabu akitulia tabu,mnataka nini nyie? Jamani moyo hauna spare' kwanin hamna huruma! Wapendwa mlochangia nawashukuru oo kwa Juliet uliyeuliza swali,huwa anarud kila novemba,sasa hapo pia pana habar pana ila labda uelewe tu kama nilivyokwishaeleza. Asante pia kwa dada Dina nakuombea baraka endelea na moyo huo huo,kaz njema dada.

Anonymous said...

Dear huyu mwanaume ni wazi kabisa hakutaki, sasa hapo kuna mawili, (1) yawezekana kaambiwa kitu kuhusu wewe wakati akiwa nje maye be kuwa umekuwa na mahusiano na mtu mwingine.

(2) Atakuwa ana mtu mwingine, ongea naye na akwambie ukweli kuhusu mahusiano yenu, maana waweza kuamua kuachana naye na ukapata mtu mwingine cha kushangaza naye akaanza kukufuata ndivyo wanaume walio wengi walivyo, be very care full hakikisha unapata uhakika kutoka kwake, na kingine usisononeke sana huwezi jua m/mungu anakuepusha nini kwa huyo jamaa, utapata mwingine anayekupenda zaidi na yeye na utajutia muda uliopotezea kwa.

nakutakia kila la heri dear,

Mary

Anonymous said...

mmhh.. dada wala ucijilazimishe kwake, mwache kabisaa wala ucimtafute tena na wewe mkatie mawasiliano kabisa,huwezi jua labda anaugojwa katoka nao huko majuu, anaogopa kukuambukiza na kukueleza ukweli pia hawezi labda hakuwa mwaminifu kwako,yameshatokea haya ninayoyasema kwa watu wangu wa karibu so just let it go..usiharakishe mahusiano mapya just to hurt him..im sure God has sumthing better for you!

Anonymous said...

Mi nakushauri tofauti,fanya juu chini ukutane nae ana kwa ana kabla hujaamua kitu,kuna girlfriend wangu hivo hivo alipotoka nje ya nchi akakata mawasiliano nami hataki tukutane wale hapokei simu na nilimpenda sana.Kumbe alipata ajali na kuumia mkono vibaya sasa akadhani sitamtaka tena.Tumeoana na tuna watoto 2 sasa.

Anonymous said...

Dada mwenye tatizo.. sasa mbona unaleta habari/feedback nusunusu.. inakuwa ngumu kukushauri vizuri sometimes. Umedokeza kuwa alikuwa anarudi kila November halafu ukasema hiyo nayo habari yake pana!!! so kuna mengi yamejificha. sio lazima useme kila kitu lakini angalau utufungue macho sisi tunaokushauri ili tusikushauri vinginevyo. be blessed!

Anonymous said...

hi dada nina swali kwake feel free kunijibu ,As sijaelewa kabisa how comes mpo mji mmoja na hamwezi kuonana kwa miezi 6,yaani mnaishi wote dar au mpo mikoa tofauti maana nimechanganyikiwa.Lakini hata kama sina jibu kwanza ushauri wangi nii huu,mpendwa move on nawasihi wanawake wenzangu tufike mahala tuone nyeupe na nyeusi,na baada ya kuona tujue its about time to move on,sasa unataka kumchunguza kwa how long ,kuchunguza nini tena mpendwa,yaani unapoteza mwaka wako mzima kwa ajili ya nini?Please mpendwa move on.Mweleze tu uamuzi wako .Je waamini kwa _Mungu anaplan nzuri na wewe then mshukuru Mungu na endelea mbele.Mara wa kadhaa wadada tunasali Mungu atuonyeshe wenzi wetu.Sasa akijibu kwa kutuonyesha hao tuliokuwa nao sio bado tunaquestion.Ehe jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu.huyu jamaa angekuwa ni mpango wa Mungu mambo yangekuwa tofauti believe mi naongea na experience.Mungu akusimamae!

Anonymous said...

Pole sana.but wanaume sio wote wabaya wala wanawake sio wote wabaya coz ubaya hauna jinsia.mie pia niko kwenye njia panda.nina msichana kwa muda wa miaka 3.tumependana sana mpaka hivi juzi juzi mambo yameanza kubadilika.nikitaka simu yake anakataa na akinipa huwa anakuwa na wasiwasi.yani nimeona kila dalili kuwa ana mtu mwengine ila hajui aanze vp kuniambia siwajuwa mwenye macho aambiwi tazama.hakuna hivi wala vile.mapenzi ya siku hizi yamekuwa kama ubuyu mara yakimumunywa yanaisha tamu.pole dada.mpende akupendae asio kupenda achana nae.wako utaonaraha@yahoo.com

Anonymous said...

naona yote wameshaongelewa ha muhim mwambie naoamba tuonane kabla ya kuamua chochote then mtakachokiongelea mda huo ndio mtaamua cha kufanya lakni more of it expect the worse, lakni prepare your self, na kuwa strong hata kama unaumia usimuoneshe weknes yako,kawani itakuuma zaid na utashindwa kumove on.

na ikiwa haikuwa wewe na yeye please jitahidi kutake time kutafuta umpendae usivamie tu kwa sababu eti na wewe uwe na bwana ili kumuoneshea kama na wewe ndie hii itakuathiri isitoshe wewe ni mwanamke isijekupoa jina baya, kwani utakuwa na mwengine lakni mawazo yako yote ya kwa huyo jamaa alierudi ulaya,kuna kila aina ya maradhi yanamsubiri binadam ayapokee, nakama haitokuwa hata namba ya sim pia kama utaweza basi change move kwa kila kitu ondoa memory yake yote and start again

good dada

Anonymous said...

You laidy, listen from a men point of view. Leo nitawapeni lecture inayoitwa men 101. The guy doesn't want you. I don't care nini wanachosema wanablog wengine.

Ingekuwa ni few days ningekwambua labda mambo mengi yanamgubika, but it is almost 6 month since he came back. So, clear talk baby let the sucker go. Go get your self a real MAN. not some sorry ass like him.

Anonymous said...

Mtafute uongee nae sio wote wanao toka ulaya wanakuwa hivyo wapo wenye commitment zao msije kutupotezea wachumba wetu hapa..aidha go back to mwenendo wako kama ulitoka na mtu jamaa kazipta ndio nitolee hiyo, lkn pia kuna mtu kaongea point hapo juu pengine ameshindwa ku meet expectations zake so yupo undecided kwenye swala lako ikiwa mliahidiana kuona mara akirudi''chunguza''.

Wewe mtafute mkae muongee ujue mipangalio kiujumla na kuhusu wewe kwani kama mipango ipo ujue usisubiri hewa, to me its very unusualkama mpenzi wake kukuchunia kiasi hicho tafuta ufumbuzi wa hili kwa upole kabisa huenda akawa ana problems yupo comfused na so yupo undecide nini afanye...kuna comment eti wote wanaotoka ulaya wanaona kama wapo tofauti....acha kudanganya watu there is no difference kinacho matter ni commitment tu, kwani hata kutulia nako kuna mtu na mtu mimi toka nipo ulaya sijawahi tongoza walakungonoka 4quite some time now na siku nikirudi inabidi yeye ndo anipokee, na mpnz simu anapigiwa mya be 5 times a week japo ana lalamika kwamba haitoshi coz nikiwa tz ni almost every hour anapigiwa.

So dada japo ha2jui mwenendo wa mapnz yenu cha msingi hapa nikumtafuta ongea nae wats up then decide from there.pia hujasema toka ametoka ulaya hamjakaa hata 1day?, kama mlikaa mlizungumza nini kuhusu mahusino yenu?? Na usilalamike sana coz hata some of you mwatudanganya pia, mimi binafsi nimedanywa na two GFs i call em fools coz hawakujua nn wanafanya walipo achwa ndo walijua thamani yangu na kuhangaika huku na kule kurudisha penzi nili discard..pia usiwe sexist ktk hili wote tuna mapungufu tukubali ukweli usipo danganya wewe usifikiri wote hawadanganyi wapo ambao sijui niwape jina gani... mtafute ongea nae ila kuna kitu trust me si bure!!

pole sana sister

lajk!

Anonymous said...

Dada Dina na Wapendwa wengine,
Kuna kitu kimoja ambacho wapenzi wengi wanashindwa kukifanya inapotokea wanataka kuachana na wapenzi wao,na sababu ya msingi siijui, labda mtanisaidia.
Nacho ni kushindwa 'to get the message delivered' kwa mpenzi wako kwamba mapenzi yenu yamefikia mwisho,ni wachache sana wanaweza kuwa na ujasiri wa namna hii.
Madhara ya kufanya hivyo ni mengi ikiwa na ya kisaikolojia, lakini kitu kizuri muhusika atakuwa anafahamu kuwa mapenzi yamekwisha.
Sasa katika hali aliyo nayo huyu dada hapa yuko njia panda,hajui kama mapenzi yamekwisha au imekuwaje,kwa kifupi HAELEWI.
Dada jaribu kutafuta rafiki au ndugu zake wa karibu sana ambao ni waelewa na mtaongea ili wapange kuwe na kikao cha wote, kama atakataa basi watume waende wakamuulize wakuletee jibu kama mapenzi basi au mnaendelea kama yanaendelea basi mambo yawe kama zamani.
Mtakapokuwa katika hicho kikao jaribu kuuliza sababu zinazomfanya yeye afanye anavyofanya. Jaribu kutumia lugha nzuri na upendo.
Endelea kujitunza dada kwa wakati huu, kama MUNGU amepanga awe wako basi atakuwa wako tu,kama MUNGU ameona hakufahi basi ujue ANAKUPENDA NA AMEKUOKOA KUTOKA KATIKA MAMBO YA HATARI SANA KWAKO.
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com

Anonymous said...

wewe huyo kijana namjua ameacha wangapi wewe pia unajua. ila London alikuwa na msichana wake ambaye nimesikia wanatarajia kufunga Arusi mwezi wa sita. pole sana Wema we tafuta tu mwingine.

Anonymous said...

Ndugu zangu ulaya hakuna kitu hivyo acaha kabisa kudhani kuwa watu wakitoka ULAYA hubadilika na kukacha maboy/magirl friends wao.Hiyo inakuwa tabia ya mtu tu wala haishonani na hilo.Sijitetei kwa vile niko huku majuu.

Wewe dada tulia acha kuhangaika, sana,mambo yatajionyesha yenyewe muda si mrefu.Tulia kama ulivyosema umejiheshimu kwa muda mrefu.Fanya hivyo wala usimbughudhi huyo jamaa, hiyo itakusaidia sana kumpa mtihani hata yeye.Kama umejitunza humkumtunzia yeye bali ulijitunzia wewe na hicho ndicho kitakupa heshima ya kupata mtu wa uhakika zaidi.Watu wanaona usifikiri hakuna wanaokukodolea macho wapo!!

Kwa sasa usiseme kitu wala kumtafuta, kwani amekulia nini cha kwako?Je, yeye anaishi wapi na wewe unaishi wapi?Ninakupongeza kwa uaminifu wako hasa kwa ajili yako mwenyewe.Mambo yakigoma kabisa hadi muda mwingi baadaye naomba nitafute inagwa una kidonda cha mtu aliyetoka Ulaya, lakini mimi sitakuwa hivyo.Uaminifu wako umekupa soko kubwa kwani ni wachache wanaoweza kufanya hivyo.Good luck sister.

Anonymous said...

mmmh pole dear ila kama hapo juu mdau alivyochangia nami pia napenda kukuuliza mlikuwa mnawasiliana wakati akiwa UK,maana aliporudi kakutaarifu na namba ya ke kakupa sasa tatizo amekaa kimya na hafanyi yale ambayo angetakiw akuyafanya kama bf wako,mi naona kwakuwa nawe unampenda na ulimngoja sana kabla hujaamua kutafuta mwingine mwombe nafasi walau dk chache na umwambie jinsi unavyojisikia vibaya kutokana na yeye kutokuwa na muda na wewe na hivyobasi upo tayari kutafuta mwingine,yani cha msingi ajue kabisa kwamba wewe unaelekea kufanya nini maana anaweza akajidai umemwacha na mengine mengi tu,yani yote haya ni katika kuhakikisha mnaachana kwa amani,utamuona tu anaweza akakubaliana na wewe kabisa na hapo utakuwa umepata ukweli kwamba si wako na hakupendi hivyo huna budi kutafuta mwingine,hata akijidai ooh kazi nyingi mbane na maswali,japokuwa hukueleza mawasiliano yalikuwaje kabla hajaondoka kama alikuwa mtu wa kukutafuta sana na saivi ndo analeta nyodo basi kashaanza na mwingine anaona haya kukwambia ukweli,yani anasubirie umwache wewe ,ila cha msingi mwambie ukweli umechoka kwani unahisi hana feelings zozote na wewe,mwanume gani ambaye hataki hata sikia sauti ya demu wake,mshenzi sana,ni vema kama mtu humtaki mwambie tu,ili asipoteze muda,pole sana ila yapo hayo wengi yameshawakuta,wala usijione huna bahati utapata mwingine mtayependana mwache akae na mapozi yake.bye

Anonymous said...

Pole sana dada. Mtazamo wangu 'KAMA KUSOMA HUJUI' HATA PICHA HUTIZAMI?' BInti anza maisha mapya na msahau huyo kiumbe. WAjua ktk mapenzi ni timing kuachwa ama kuacha. Sasa huyo mpenzio wa zamani anaona ugumu kukuambia kuwa hakutaki tena. Mara nyingi binadamu tukiwa na wapenzi wa kisomo cha kawaida then mmoja akabahatika kupata elimu zaidi ya mwenzie uwezekano wa penzi kudumu ni mdogo mno.
SWALI. 1. Ni kwanini asikueleze tarehe anayokuja ili ukampokee Airport? Nijuavyo mimi wewe kama mpenzi wake ulitakiwa uwepo Airport.
2. Alikutambulisha kwa baadhi ya marafiki wa karibu au ndugu angalau mmoja wawili?
3. Unajua anapoishi? au ndugu/marafiki zake wanapoishi?

USHAURI:
Yanekana bado upo njia panda na huamini kinachoendelea. Miezi 6 ni mingi mno kutokuonana na mawasiliano ni ya kusua sua. Sikushauri uonane naye kwani wanawake sisi ni wepesi wa kudanganyika. Mtakuwa wanawake 2 kwa mwanaume 1. Kaza moyo uma meno AHANA NAYE! mkionana utampa faida bure! KUwa kiburi japo unaumia kindanindani. Pili sali/swali sana.

sis H. said...

pole dada na msichana mwenzangu. huyo achana nae hana future kabisa na wewe. jamani miaka minne ni mingi sana kwa wale wenye upendo wa kweli kuwa mbalimbali, angekuwa bado ankupenda nadhani angepata hamu ya kuwa na wewe muda wote baada ya kurudi kutoka huko UK. kaza moyo dada nashauri uachane nae kabisa na usihangaike kumpigia simu au kumtumia msg ulizotuma zinatosha kabisa,nadhani unaweza ukasonga mbele bila yeye. mbona umekaa 4yrs bila kuwa nae pembeni na maisha yameenda iweje sasa akusumbue kichwa je is he the only man for u in this world?the answer is no, sasa hupaswi kupoteza muda wa kumfikiria yeye, mtoe kabisa moyoni mwako kwa kushiriki sana ibada na kuomba mungu akupe mwanga wa kuwa na mtu mwenye upendo wa dhati. usikurupuke dia ukimwi nao uko nje nje hakikisha unakuwa makini.penda pale ambapo unapendwa.
usiwaze kwamba eti nikiwa na mwingine anaweza kurudi baadaye, ni kweli kuna uwezekazo akarudi na kujifanya ana upendo wa dhati ila nakuhakikishia utakapojaribu kumkabidhi moyo wako lzm atakuja kukusumbua tu naongea hivi kwa sababu ilikwishanitokea.sisemi kwamba incidence zitafanana hapana ila ndugu yangu huwa mimi naamini usemi mmoja kwamba ALL MEN ARE EQUAL EXCEPT THEIR NAMES AND FACES. nakushauri uchukue uamuzi wa kuachana na kumuazia huyo asiyekupenda leo hii,weka moyo wako free kwa ajili ya kukaribisha upendo wa dhati kutoka kwa ambaye naamini Mungu atakupatia.natamani niendelee kuandika ila nadhani kwa hayo machae utakuwa umenipata.nakutakia kila la kheri kwa matumaini kwamba mazuri yanakuja. nothing is impossible under the sun.muombe Mungu

Anonymous said...

Du!!(huku nikiwa nimetoa mijicho) pole sana dada yangu.

Kwa kifupi huyo jamaa hakupendi na pengine ameshapata mwingine. Mimi kama mwanaume najua hizo nazo ni miongoni mwa mbinu z kumtosa mwanamke.

Kuna mshikaji niliyekuwa nikisomanae alimfanyiaga msichana wake kama hivo. Msichana alivyolazimisha kuonana nae kama wewe unavyotaka kufanya, jamaa alimkubalia na akamwalika hosteli wkend moja.
Ili kumwonyesha demu kuwa alikuwa hapendwi na jamaa alikua na demu mwingine,siku ya siku jamaa akamwalika na demu wake mpya ili waje wamtambulishe rasmi.
Kilichonisikitisha ni pale alipowakuta jamaa na demu wake wakiwa wanaangaliea CD ya x na huku demu mpya amevaa chupi tu.

Tafadhali usije lazimisha kuonana na huyo mshikaji,na kwasababu hajatoa mahari,huna haja ya kuofia atakapokukuta na uhusiono mpya itakuaje.
Actualy huwa naomba nije nipate msichana mwaminifu kama ww na huyo jamaa atakuja ku-regret for the rest of his life kukutosa, na hawezi kuishi maisha ya furaha katika huo uhusiano wake mpya.

Tulia na utampata Mungu aliyekuchagulia muda muafaka ukifika.

Ingwe.

events said...

Hello Dina, ulikuwa wapi wewe? Hope everything is ok.Kwanza nikwambie nilikuwa mapumzikoni nikapata muda wa kufungua makala za nyuma, u know waht? Nimejifunza mengi sana lakini zaidi hii kitu yako unaiita endiketa ni koboko Dinah. Unajua the man was on topo and he was like "Are you YOU?" U know what I mean? I think I was new and badala ya kupiga mabao machache kama tulivyozoea tulipiga double. Nilijihisi kama nimechelewa lakini nikagundua kuwa kila jambo hutokea for a purpose n' this is the right moment for me 2 know this. Dinah, upo juu!!! Heri tumbo lililokuzaa na matiti uliyonyonya. Your mother must be very proud of you.
Leo naandika nikiwa nimeguswa sana na habari ya huyu dada ambaye amemsubiri mpenzi wake aliyekuwa majuu kwa muda wa miaka minne n' when he is back this is what she gets.
Ladies, let's talk about this a bit. Unajua mwanamke akimpenda mwanaume mapenzi ya dhati basi anampenda kweli na anasacrifice mambo mengi sana in order to maintain the relationship. Like the lady am talking about, am conviinced that she was faithful to his man for four solid years hoping that he will someday come back and start a family. This man is bastard!, son of a bitch!Whatever the reasons he has, he was supposed to tell the lady the truth. Does he really know what it takes to sacrifice so much. Does he know how many men have approached the lady and she refused b'se she believes he loves her? I mean, how can he do that to her.
I know that he might have reasons to do that why can't he spell them out. Hata kama itamuumiza this lady lakini itakuwa rahisi kwake to get used to the idea and start moving on.
Nimeguswa sana kwa sababu katika watu waliochangia baadhi yao wamesema kitu kama hicho kiliwapata na hao ni wachache kati ya wengi ambao yamewapata na wamebaki na majeraha wala hawatamani tena kujiingiza katika mahusiano mengine ambayo wanaamini kuwa yataumiza kama mwanzio au zaidi. Why is this happening to us. I believe the world is the better place for all sexes to live in and loving one another is the best feeling of all.
Hii inatokea mara nyingi mpaka inakuwa kama ugonjwa wa kuambukiza ambao dawa yake haijapatikana na tunahangaika kuitafuta kama ambayo dawa ya ukimwi inavyotafutwa.
Kibaya zaidi n ugumu tunaoupata katika kuwaondoa hao wanaume katika akili na mioyo yetu. It so hard because in our minds and hearts we believe that they are the only men for our lives. We are not sure if there are other men out there who will be like them forgeting how bad they treat us.
Wakati mwingine dalili zote zinajionyesha kwamba mwanaume doesn't love you any more kama ilivyotokea kwa our beloved lady but it's hard to embrace the idea and we go on and on kuwabembembeleza.
Men should know that we women are precious thing the world have ever had since creation. They must figure out the world without women.
Men stop kututesa jamani. Moyo hauna mfupa kama ungekuwa nayo basi mabaki yake yangeonekana kwa jinsi ambavyo mara nyingi inatendwa, inaumizwa na inakuwa, maana feelings zikifa ndio moyo umekufa.
Inawezekana kuna mada zilitolewa huko nyuma lakini nafikiri itkluwa vzurikama watu watatupa first hand inforamtion and what they did to overcome the problem. Ni muhimu Dinah, wanaoteseka ni wengi.
Lakini pia tutafurahi kupata namna ya kuendelea kubaki nao hawa wapenzi wetu. Ni kazi ngumu kuanzish mahusiano mapya mara kwa mara.
Thank you

Anonymous said...

mi naona ufate ushauri wa dinah na pia mtu kuwa ukaya sio kubadilika ni tabia ya mtu, mimi nimeondoka TZ nikiwa single.. nimekaa mtoni mwaka wa tatu wa masomo ya udaktari nikiwa single sababu sijaona mwanamke huku wa kuwa na future naye zaidi ya bibie ameena ambaye alikuwa rafiki wa kawaida since 2003 baadaye nimeamuwa ku book anisubiri nikirudi nioe..
so kubadilika kwa mtu inategemea na wewe mwenyewe...
dr.ngenya@gmail.com
asanteni sana...
u can move on he`z such a jerk!

Anonymous said...

mimi nashukuru mungu ameumba wanaume kwa sababu bila ya wao maisha ya mwanamke hayakamiliki,ila nimeamini hakuna viumbe ambao wana roho mbaya , wabinafsi kama wanaume, sio wote lakini wachache walio hivo ukikutana nao run a mile, and this one my sister is one of them , hanan kuzongwa na maisha wala nini, hakutaki lakini hataki kukwambia, believe me inauma kama nini, mimi uchungu naujua , boyfriend wangu nilimfuata ulaya nikawa nasoma anakaa kwake na mimi nakaa kwangu , baada ya kuwa pamoja miaka 3 , alikimbia bila kunijulisha akarudi bongo kuoa, na simu akabadilisha aliporudi, did he even bother to tell me its over b4 he got marriage NO, so mimi naona miaka ulimsubirir ni mingi,ila kama ana nia na wewe angekutafuta as soon as he legs touched bongo, so move on my dear, i have lived the experience wanaume ni waongo na wabinafsi wanajipendelea wao hawajali feelings za wengine move on he's a looser and a jerck he does not know what he 's missing.by the way huyo jerck wangu mimi my Ex aliponiacha nililia nikamove on na nikasoma sheria, degree na masters he never destroy my life.am living proof stay away from jerks !!live your life.