Friday, 10 April 2009

Kijana utaoa lini?-Ushauri

Ni swali aliloulizwa mfanyakazi mwenzetu
"Sina mpango wa harusi na wala sitaki kusikia Habari hiyo tena?" bwana harusi mtarajiwa aling’aka na kuinuka kutoka nje.

Kila mmoja wetu pale ndani aliduwaa, kwani katika harusi tuliyokuwa tukiisubiria kwa hamu ilikuwa hii, je kulikoni, michango kadi kila kitu kilishaanza! Ushauri wa haraka unahitajika ili kama inawezekana tuiokoe harusi hii au la jamaa ajiandae kivingine.


Jamaa huyu alikuwa akiishi na mdogo wake ambaye alimchukua nyumbani kwao alipomaliza kidato cha nne, na kuamua kumuendeleza. Ilibidi ajinyime, na kujinyima huko ndiko kuliko changia hata achelewe kuoa. Ilibidi akope kazini, kuhakikisha mdogo wake naye anasoma hadi akafikia chuo kikuu, huu ni mwaka wake wa mwisho.


Jamaa akaona sasa naye atafute jiko, kwani umri umekwenda na alichofanya ni kuenda kijijini akampate `kuku wa kienyeji’ ambaye kamaliza kidato cha nne, mrembo kweliweli. Alipomfikisha hapa Dar na kumtambulisha kwa mdogo wake, kuwa huyo ndiye shemeji yake na kwamba watafunga ndoa lakini ameonelea asubiri mdogo mtu amalize chuo ili isimkwaze katika mipangilio yake.


Siku zikaenda na jamaa akawa anasafiri safari za kikazi kwahiyo nyumba inakuwa chini ya mdogo wake ambaye mara kwa mara alikuwa akija kulala hapo kama yupo safari vinginevyo alikuwa akikaa chuoni, sasa inabidi akae na shemejiye.


Siku moja jamaa, akarudi bila taarifa,ndipo yalipompata ambayo hatayasahau maishani, na kuapa kuwa yeye hana mpango wa kuoa tena. Kwani hilo sio tukio la kwanza, alishasalitiwa kabla na rafiki yake mpenzi na hii ya sasa imekuwa kali zaidi kwani aliyemsaliti ni mdogo wake toka nitoke. Aliwakuta `live’


Kumbe huyu binti na mdogo wake walikuwa wapenzi huko kijijini wakiwa shule, yeye yupo vidato binti alikuwa msingi. Na katika ahadi zao ni kuwa jamaa akimaliza shule walianzishe. Siku zilivyokwenda binti akawa anasakamwa na wazazi wake kwani wachumba wengi walishaposa bila mafanikio, ndipo alipokuja huyu jamaa ikawa ni hitimisho.


Uolewe na huyu! lasivyo atakuoa mzee Kijashimo kama mke wa pili. Binti akawa hana jinsi, `hata hivyo jamaa huyu mpya anafaa sana, nimempenda...' binti alisema.
Kwahiyo binti alipoletwa Dar, hakuamini kukutana ma mpenzi wake wa udogoni/utotoni na kisiri wakawa wanajirusha.


Za mwizi arubaini wamefumwa na kubainisha ukweli. Jamaa alishindwa la kufanya kwani kijijini alishakabidhiwa binti wa watu kwa heshima na kiapo na binti alikubali kuwa huyu sasa anafaa(kwa kweli alivutika naye alikiri binti) na alishaamua huyu anafaa kumuoa, hakujua kuwa atakutana na mpenzi wake wa kijijini tena.


Tukirudi kwa mdogo wake ndiye kipenzi cha wazazi wake, kumtelekeza hawezi. Alipoliona tukio hili alizimia kwa muda.

Ujumbe ndio huo tunaomba sana ushauri wenu.

emu-three na wadau wengine hapa kazini.

Jawabu: Hiki kisa kinasikitisha sana lakini sioni sababu ya kumfanyaKijana kususa kufunga ndoa kwa vile tu matukio mawili yaliyotokea. Natambua wazi kuwa atahitaji muda ili kuondokana na kilichojijenga Kisaikolojia na pengine akahitaji wataalamu ili kumsaidia ku-over come hilo.


Suala sio Mdogo mtu kuwa kipenzi cha wazazi basi asitelekezwe kama alifanya kosa la kumsaliti kaka yake hakika alikuwa akistahili adhabu kubwa zaidi ya kuterekezwa lakini Mdogo mtu hajafanya kosa na kama ilivyo kwa kaka yake na mpenzi “wao” yeye pia ni “Victim” wa utaratibu wa maisha ktk jamii yetu ya kibongo.


Hakuna mwenye kosa kati yao hao wanandugu wawili na huyo binti, nafikiri jamii iliyokuwa ikiwazunguuka ndio inapaswa kulaumiwa kwani kama kungekuwa na “uhuru” wa jina kutambulishana kwa wazazi kama “marafiki wa karibu” ambao huenda pengine wana hisia za kimapenzi lakini hawako tayari kujihusisha na mwanya gono(inawezekana kabisa).


Hivyo basi kama jamii ya Kibongo ingeachia kidogo ili vijana waweze kurafikiana na badala ya kuwatisha unawaeleza ukweli wa mambo hali ambayo ingesaidia kwa kiasi kikubwa kwa familia ya binti na Mdogo wake kijana muathirika kufahamu ukaribu wa wawili hao na hivyo wasingeruhusu kaka mtu kuchukua jumla.


Kaka mtu anachopaswa kufanya ni kuwaacha wapendanao hao waendelee namapenzi yao kwa ni wao ndio walioanza kupendana na penzi lao lilikuwa asilia ulikinganisha na yeye, pengine huyo mwanamke hana mapenzi na huyo aliyemleta mjini (kaka mtu) lakini alikubali tu kwa vile hakutaka kuolewa kama mke wa pili na Mzee Kijashimo kama alivyotishiwa na Familia yake.


Kwa kifupi basi napenda kusema kuwa haya ndio matokeo ya kuficha ficha pale tunapokuwa na mafariki wa jinsia tofauti ktk umri wa ukuaji. Unajua kile kipindi cha ukuaji kila mmoja wetu huwa na hisia za kuwa na mtu wa karibu ambae mara nyingi huwa tunarafikiana kwa muda mrefu na kupendana bila kujihusisha na ngono.


Lakini tatizo linakuja kwa wazazi, ndugu na jamii kuhisi kuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya “matusi”. Badala ya kuwasaidia na kuwalezea nini cha kufanya kukabiliana na masumbufu ya ukuaji na kuwa huru kumuona rafiki yako wa jinsia nyingine unapigwa marufuku kama sio kuhamishwa na shule kabisa.


Naelewa kuwa jamii, wazazi na ndugu wanajaribu kulinda binti/kijana wao na kuzuia wasiharibu maisha yao ya badae kwa kutiana mimba ktk umri mdogo lakini hapo hapo itambulike kuwa kuna umuhimu wa kujua nani anarafikiana na mtoto wako na urafiki wao ni namna gani hasa.


Ushauri wangu ni kwa Kaka kujipa muda na kufurahia maisha yake badala ya kuhofia lini atapata “jiko” na wapi hasa linapatikana. Akumbuke kuwa Mapenzi hayalazimishwi na vilevile kila linachotokea ktk maisha yetu huwa kuna sababu kwanini hasa kimetokea.


Huyo binti hata kama ungefunga nae ndoa asingekuwa akikupenda kama alivyokuwa akimpenda Yule aliyeujaza moyo wake na kwa vyovyote vila lazima angenda tafuta mapenzi ambayo yasingekuwepo hapo ndani na hivyo ndoa yenu ingeharibika.


Napenda kuwashauri ninyi marafiki zake kumuacha jamaa aishi vile apendavyo kwani kutokana na maisha ya sasa kufunga ndoa ni uamuzi wa mtu pale anapokutana na Yule atakae ujaza moyo wake kwa mapenzi, ila kasumba ya kukimbilia kijijini unapohisi umri wa kuoa umefika sio haki kwako wewe muaji na Yule muolewaji kwani ndoa yenu ita-base kwenye “wajibu” na kila kitu maishani mwenu kitakuwa wajibu na sio mapenzi.

Kila la kheri.

7 comments:

Anonymous said...

kama naangalia movie vile tena ya kinigeria. duh ntarudi baadaye kwa ushauri

Anonymous said...

Mimi naona bora awaachie hawa ndege wawili waendelee na maisha yao. Mambo ya mapenzi hayo, pole kaka

So much said...

I dont ever want see you again Mshawahi kuiskia hii nyimbo wadau ya Uncle Sam.emu-three na wadau wenzako hii kali,sijawahi isikia ila sishangai sana vitu kama hivi hutokea.Kwanza naomba unisaidie kumpa pole huyo jamaa manake hili suala si dogo.Binafsi ningekuwa huyo jamaa nisingeoa tena coz picha unayoipata ni kuwa litanitokea tena.Mimi ningeendelea na maisha yangu kufanya kazi sana kutumia kwenda mbele coz haina maana ya kuwa na mwanamke ambaye anakusaliti.Kama alikuwa hamtaki si angekubali kuolewa tu na huyo mzee nani sijui.Na huyu mdogo wa mtu(ashakum si matusi) ni msenge aliyekubuhu how come unakuja msaliti aliyekutengenezea maisha mpaka hapo ulipofika kwa ajili ya uchi tu.Huyo ndio anayekufanya mjini ung'ae,uvutie na uwe na nyodo mbele za watu then leo unamsaliti!,ulikuja toka kijijini hata kuchomekea hujui na posta ulikuwa unakuskia leo yule mtu aliyejikalaisha maishani mwake kwa ajili yako,anasumbuka kwa ajili yako wewe mjaa laan leo unamgeuzia kibao.Jamani hii aibu gani hii?!uchi kitu gani wa kukufanya utoe utu wako kwa ndugu yako anayekusaidia kwa kila kitu na anayekuheshim na kukupenda.Huyo dogo undugu ungeisha kabisaa,kila kitu nasitisha kwangu simtaki yani hata maishani mwangu sitaki kumuona tena manake mtu kama huyu hatashindwa hata kuniwekea sumu.emu-three mwambie huyo kaka awatimue wote huyo anayejifanya kidume fukuza na huyo changu papa fukuza,tena kazi hiyo angeifanya siku hiyo aliyowafumania,kibaya zaidi nyumbani kwangu?!eeeh mola,malipo hapa hapa duniani ahera hesabu Mungu yupo na atamlipia tu.Hawa watu wawili wamekosa haya kabisa,yani hii kitu imenigusa sana utadhani nimefanyiwa mimi.Jamani samahani sana yani nina maswali mengi ya kujiuliza manake nimechanganyikiwa hivi wewe mdogo wa mtu uliyefanya hivi hukujua huyo ni shemeji yako?!mke mtarajiwa wa kaka yako?!kama mlikuwa wapenzi hiyo ishakuwa history ulitakiwa umpe heshima inayostahili.Halafu wewe hata sijui ni msomi gani usiyeweza kupembua manake unaweza ukasema kusoma hujui lakini hata picha uoni?!hujui kwamba this is unfair?.Na wewe demu kwani hukuona mtu mwingine wa kucheat nae hadi shemeji yako?mdogo wa bwanako?!jamani hizi tamaa hizi zitatuua.Anyways naona nikiendelea sitamaliza me namshauri huyo jamaa akae na atulie siku hizi haina haja ya kumfuata mchumba kijijini wengine ni magubegube yaliyoshindikana yeye atafute msichana tu mzuri ambaye ametulia hapo mjini wafahamiane vizuri then aoe ila biashara ya undugu nyumbani hakuna,udugu mnakutania kijijini mkija DAR kila mtu na 50 zake.Amuombe sana mungu kila siku kama mwislam aende msikitini na kama haleluya aende kanisani na akashtakie Mungu.
Samahani Dinah kwa maelezo marefu ila imeniuma na kunigusa
So much

Anonymous said...

'So much' amesema yote, mimi ushauri wangu, binti arudishwe kwao, kama anataka kurudi mjini basi akaanze safari yake upya, in short jamaa aachane naye kwa kuwa ameshaonyeshwa!

Pili, asiache kumsaidia dogo, kwa sababu experience inaonyesha siku zote mindugu yetu wenyewe ikibaunsi maisha inarudi upya na mzigo unakuwa wetu tena. Kwa hiyo yeye aendelee tu kumsaidia kwa huo mwaka wa mwisho, ila, arudi nyumbani na safari zake zikaanzie huko. Anatokea nyumbani (kijijini au kokote kule alikokuwa mwanzo), na kwenda chuo, likizo arudi huko huko nyumbani. In short asaidiwe kwa umbali, huku wazazi wake wakielezwa tabia fisadi za mwana wao...keleb...

Upendo said...

Dina, kwanza nampa pole huyo kaka kwa yote yaliyompata, namshauri atulize akili na kumwomba Mungu azidishie hekima pia ajue " nyumba, mali ni urithi apatao mtu kwa babaye, bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana.

Pole sana kaka yangu.


Lady P - Atown

Anonymous said...

Dada Dinah, nashukuru kwa ushauri wako, na ushauri kwa jamii, kwamba ni vyema mahusiano yakawekwa wazi, kama binti yako ana boy friend anatakiwa ajitambulishe.
Swali kwako dada Dinah na wadau wengine, je unaye mtoto wa kike, je upo radhi, bintiyo anarudi shuleni na mvulana na baada ya salamu,
`Mama huyu ndiye boy-friend wangu'?
Kwa mzazi nafikiri itakuwa vigumu sana kulikubali hili, sijui wenzangu, lakini upo umri ambao tunaweza tukakubaliana na hili.
Tatizo kubwa ni kuwa kijijini binti akimaliza la saba tu jamaa wengi wanamuwahi,kiasi kwamba yule binti hapati muda wa kutafakari, kumchunguza na kuwa na uamuzi wa haraka. Kwahiyo rafiki wa karibu na atakayemuona anampenda ni yule waliyezoeana naye wakiwa shule, na huenda sio `penzi halisi' kwasababu hakupata mwanya wa kukutana na wengine. Sasa je kwanini tuwape nafasi mapema hawa watoto wetu kushiriki katika mahusiano? Hili ni changamoto kwa wazazi, hasa karine hii mpya
Ni hayo tu katika kuchangia
emu-three

Dinah said...

Asante M3,
Sidhani kamani rahisi kwa kijana au binti kuja nyumbani kwa wazazi nakumtambulisha mtu kama bf wake kibongo inahesabika kuwa ni mpenzi.

Binti yangu akiwa na rafiki wa kiume nitajitahidi kumfahamu huyo kijana na sitomfikiria vibaya kuwa anakwenda kumtia mwanangu.

Nitajitahidi kuwa mzazi kwao wote wawili na kuwapa mafunzo ya kimaisha ambayo nitadhani ni muhimu kutegemeana na umri wao.

Nitatumia mbunu ili kuwa karibu nao kama marafiki (pea)kimasomo, kimaisha, kimichezo n.k ili kuwafanya wajisikie huru kuniomba ushauri.

Nitaweka ratiba ya wao kuwa pamoja na sio kila siku na kila wakati.

Ninachozungumzia hapa ni ile kurafikiana na jinsia tofauti ambayo inatokea kwa sababu ni nature sasa hilo likitokea sioni sababu ya wazazi kuwadhania kuwa wataenda kufanyamatusi na au kujaribu kuwatenganisha kama sio kumpiga mikwara nakumtisha kijana wa jinsia nyingine.

Malezi bora ya mtoto ni mipangilio na uelewa wa wazazi na sio kuwatishiwa kwani hiyo itafanya wafanye uchafu zaidi tena kwa siri.

Kila la kheri M3 na shukrani sana kwa Ushirikiano wako.