Viagra!


Mambo vipi wewe!

Kwenye Topic ya 12 Feb 2009.
Naona watu wanashauriana vitu ambavyo inaonyesha kuwa vinafanywa na wengi kwenye mahisano ya kimapenzi bilakujua kwanini hasa Viagra ipo na inafanya kazi gani? Kama ilivyo kwenye matumizi ya karanga na korosho....wengi wanadhani inaongeza nyege lakini ktk hali halisi "nuts" zinaongeza uzalishaji mzuri na wenye afya wa Shahawa/Manii na sio nyege.



Kuna msemaji mmoja katoa actually "somo" (hehehehe nimecheka mpaka nimeanguka alafu ndio nikaanza kusikitika) kuwa unaisaga Viagra kisha unaichanganya na Juice na kumpa mumeo....sasa huoni kuwa huko ni kumbaka? Unamlisha dawa ya kusimamisha uume bila yeye kuandaa mwili na akili yake tayari kwa tendo hilo takatifu?



Come on wanadada, kama yeye akifanya hivyo wakati wewe huna hamu ya ngono kwa vile uwezo wako mdogo utajisikiaje? Hakika utaenda kumshitaki kuwa kakubaka kwa wakuu wa mtaa.



Itambulike kuwa Viagra haimpi mwanaume nyege bali inasababisha mapigo ya moyo kwenda kasi na hivyo kusukuma damu kwenye mishipa ya uume wake na kusababisha uume kusimama. Nyege inategemea zaidi akili/Saikolojia na kuachiwa kwa "homono" (wacha nitafute jina lake kwa kiswahili hapa) na sio mapigo ya moyo na msukumo wa damu.



Mwanaume kama anauwezo mdogo wa kungonoka hata ufanye nini hawezi kuwa na nyege unless zije zenywe pale mwili wake unapokuwa tayari....japo kuwa kuna dawa za kumfaya anyegeke lakini haiwi kama vile kunyegeka kiasilia.



Vilevile kutokuwa au kupungukiwa na nguvu za kiume kwamba mwanaume hawezi kusimamisha lakini anakuwa na nyege kama kawaida ila Mboo haidisi (hawa ndio wanahitaji Viagra) ni tofauti na mwanaume mwenye uwezo mdogo wa kungonoka a.k.a low sex drive.

Ukweli sasa.
Inasemekana kuwa Viagra ilibuniwa au tengenezwa maalumu kabisa kama dawa ya kutibu Ugonjwa wa moyo, sasa kusimamisha uume ilikuwa moja ya "side effect" ya dawa hiyo (kabla hawajaibadilisha jina na matumizi yake).


Sasa mwanaume yeyote mwenye tatizo la kusimamisha a.k.a ED iwe haisimami kabisa ua ule ugumu wake unakuw ahautoshi kuingia ukeni ndio huwa wanashauri wa Daktari husika kutumia "buluu" na hiyo hufanyika mara baada ya kuangaliwa afya yake nahivyo kupimiwa kiwango gani atumie.


Wanaume walio wahi kuzitumia au wale wanaozitumia wanaweza kueleza kwa kirefu zaidi.

Jaribu kufahamu mwili wa mumeo wako na namna gani unafanya kazi badala ya kuchanganya mambo kwa mfano wengi wanafikiri kusimamisha ndio nyege na nyege ndio kusimamisha.


Ili mwanaume asimamishe ofcoz anahitaji kusisimuliwa ili kunyegeka, mnyegeko ukitokea ndio anasimamisha....lakini kama anatatizo ED basi atasisimka (nyege kibao) lakini misuli ya uume itagoma kusimama na hapo ndio atahitaji msaada wa Daktari na hatimae kupatiwa kidonge buluu.


Tafadhali ongezea kutokana na uzoefu wako.

Ty.

Comments

Anonymous said…
ASANTE SANA MTOA HOJA. UNAJUA HATA MIMI NILIONA HIO COMMENT LAKINI NILIKUWA NAITAFUTIA WAKATI WAKE WA KURESPOND, NADHANI WAKATI NDIO HUU!
UNAJUA MTU AKIWA DESPARATE ANAWEZA KUTENDA MAMBO UKAJA UKAREGRET BAADAE. SASA WATU KATIKA KUMSAIDIA MUULIZA SWALI WENGINE WAKAANZA KUMSHAURI ETI MUWEKEE MUMEO VIAGRA KWENE CHAKULA, NILICHEKA KUFA. OK WAKATI WA KUWA SERIOUS SASA, VIAGRA INA SIDE EFFECTS KUBWA SANA MTU AKIITUMIA BILA VIPIMO MAALUM.
INABIDI KUZINGATIA WEIGHT NA UMRI UNAPOTUMIA VIAGRA. KWANZA MWANZONI ILITENGENEZWA KWA KUSAIDIA WALIO NA TATIZO LA ED (ERECTILE DISFUNCTION)NIKIWA NA MAANA KUWA WANAUME AMBAO HAWADINDISHI KABISA!!NA SIO KWA KILA ANAEJISIKIA ATUMIE.PILI KUNA VIPIMO VAKE SI KUTUMIA TU. WANAUME WANAO KARIBIA MIAKA 65 WANATAKIWA 50mg MARA MOJA KWA SIKU, WANAUME WA UMRI UNAOZIDI MIAKA 65 25mg MARA MOJA KWA SIKU PIA. SASA ULE MCHANGIAJI ALIESEMA ETI MUWEKEE MUMEO 100mg KWENE JUICE SIJUI KAPATA WAPI DATA ZAKE, PLIZ BE CAREFUL. PIA KUNA WATU HAWASHAURIWI KABISA KUTUMIA VIAGRA KUTOKANA NA UGONJWA WALIO NAO, MFANO HIGH BLOOD PRESSURE, DIABETES,UGONJWA WA FIGO NA MAINI PIA, MAANA ATHARI ZAKE NI BALAA NA MTU UNAWEZA KUPOTEZA MAISHA KABISA. NA PENGINE MUMEWE ANAZO HIZI CONDITIONS BILA KUJIJUA. USHAURI WANGU NAOMBA WATU WARESEARCH KWANZA KABLA KUTOA USHAURI, UNAWEZA KUDHANI UNAMSAIDIA MTU KUMBE UNASAIDIA KUUA. PIA NI VIZURI KUPATA USHAURI WA DAKTARI KABLA HUJATUMIA VIAGRA!
ALL THE BEST1
Mchangiaji Canada!
Anonymous said…
Vipi Dinah? Natumaini hujambo kabisa. Leo nawasiliana kutoka Udzungwa National Park nimekuja kupumzika na kujiliwaza baada ya wanablog kunishauri nijitahidi kumwacha mume wa mtu. Napenda tu niwajulishe kwamba nimeshachukua hatua za makusudi ingawa inauma kunyang'anywa tonge mdomoni isipokuwa kama halikuwa lako hauna budi kuachia. Nawashukuru papaak, baraka, em 3 na key kwa ushauri.Hivi mpaka mfikirie viagra njia nyingine zote zimeshindikana? Mimi nafikiri huyo mwanaume apate muda wa kupumzika vizuri kabisa kabla ya shughuli ya (mchokodozi) kungonoka kuanza. Pia suala la proper diet is vital ili kumtayarisha vizuri. I remember having almost da same problem but we came 2 realize kwamba yeye anachoka sana and he was frastrated wid family matters. We sat down and solved matatizo na everythin' ikawa fit. Ikiwa lazima atumie viagra basi apate ushauri wa dk.
Anonymous said…
Nafikiri si vyema kukimbilia kutumia madawa, hasa yanayoathiri mapigo ya moyo bila ushauri wa dakitari kwani huenda sio tatizo linalohitaji viagra.. Viagra nasikia ni moja ya madawa yanayoongeza mapigo ya moyo, ili dawa imsisimue mtu.
Kuna kisa cha jamaa aliamua kutumia viagra akiwa anamsubiri mpenzi wake, na bahati mbaya huyu mpenzi wake hakutokea kwa sababu fulani. Jamaa yaliyompata hatasahau.
Hili na mengine ni athari za kutokupendelea ushauri wa dakitari tunapoathirika kiafya. Tungeweza kusema ni umasikini, lakini kama mtu anauwezo wa kununua viagra, basi hali kidogo inamruhusu, sijui bei yake kiasi gani? Sasa kwanini asingemuona dakitari kwanza?
Nawaomba akina dada, ambao wanamtindo wakuwawekea waume zao madawa bila wao kujua waache kwani mtaua bila kukusudia,mtawathiri waume wenu kiakili na punde wakigundua `sijui mutasemaje?' Wapo ambao wanawawekea waume zao `limbwata' Hili jinamizi la limbwata limegundulika kuwa ni sawa na madawa ya kulevya, linamuathiri mtu kiakili na uwezo wake wa kufikiri hupungua.
Jamani mtapata dhambi nyie! Mtu alikuwa na akili zake, mchapa kazi ,mara anabadilika, hajui cha kazi ila kumfikiria mkewe...jamani tunaenda wapi? Hayo sio mapenzi,ila ni ulimbukeni.
emu-three
Anonymous said…
Habari ndugu,hii mada nimeipenda sana sababu kubwa ni kwamba mimi sio mtumuiaji wa hayo madawa ya kuongeza nguvu za kiume lakini rafiki yangu anatumia.Dina na wachangiaji huyu rafiki yangu ana miaka 22 hebu niambieni yatakayompata baadae.Me sikufahamu kama anatumia manake alipozinunua na kutumwa yeye hakuwepo alikuwa amesafiri mimi nikapokea nikaona huyu ni swahiba wangu nikafungua nikaona vibox vya dawa.Nikampigia na kumwambia kuna mzigo wako umekuja na nimeufungua ila naona kama dawa ila sizielewi akasema aaahah hizo ni za project katika Chemistry.Mimi sikubisha coz major yangu ni Business yeye ni Engineer ila alarm zikawa zinalia sababu hachukui chemistry tena na hajawahi kuzungumzia kama anachukua chemistry hata siku moja najua anachukua Phyiscs,maths na maajabu mengine ya field yake.Kuna siku akanambia nitoe nini sijui katika bag lake la shule ndio nikaona vile vidonge vimeshaanza kutumia na ile pakiti niliyoiyona inakaribia kuisha.Sasa najiuliza katika umri wa miaka 22 unatumia dawa hizi hivi ukifika miaka 30 itakuwaje?na jinsi nilivyozisoma zinasema unywe dakika 45 kabla ya kutombana na tumbo liwe tupu,sasa utaweza hata kusimamisha mboo kweli manake utakuwa usharegea.Yeye hajui kama mimi najua anajua kwamba mimi hata sijui.Namuonea huruma rafiki yangu naona ujana huu na kutaka kuonekana ana nguvu nyingi utaishia pabaya na utamfanya vibaya.
Anonymous said…
Athari za haya madawa ni kwamba ukiyazoea, inakuwa kama mlevi wa madawa ya kulevya, yaani asipoyatumia nguvu inakuwa haipo(mjamaa amelala mpaka apate mshituko). Nashangaa kwanini kijana mdogo kama huyo anaamua kutumia hayo madawa,wakati wengi wanaoshauriwa kutumia ni wale waliopevuka kiumri? Sijui, nafikiri kuna walakini.
Mshauri sana,kabla haijajijenga mwilini. Mwambie wewe upo tayari hata kwa bao moja, sio lazima msuguane mpaka kutoke moshi...hahahah, just a jokey.
Lakini vyovyote iwavyo, sio vizuri kuyatumia hayo madawa kama huna matatizo,na kujijua vyema ni bora kuwaona wataalamu. Ujana una raha zake na karaha zake,usipokuwa mwerevu utaiga kila kitu, na matokeo yake utayaona uzeeni.
emu-three
Anonymous said…
Diabetes sio 1 ya magonjwa unayokatazwa kutumia viagra mi ni 1 wapo natumia kwa ushauri wa daktari.Lakini watu wawe waangalifu na viagra tulishawani kumpoteza makamu wa rais ambaye hakujua ana matatizo ya moyo alipita pharmacy akanunua na kufa usiku huo huo.
Unknown said…
Mtu akishupaza shingo atavujika gafla nawala hatapata dawa!