Ushuhuda wa Mama Johnson wa Mza!

Hi My Dear Dinah.
Its me again Mama Johnson From Mza.

How is Valentine 2 all Tanzanian?
Napenda kuwashukuru watanzaia na Non-tanzanian wote ambao mmenishauri hapo chini. Mimi ni Ma Johnson ambae nilituma mada yangu kwa da Dinah ikisomeka NAHISI MUME WANGU ANAJISAHAU. Especcialy my special thankfull to you Dear Dinah.

Let me tell u maana ilikuwa as a story what happened to me.
Baada ya kuwasilisha mada yangu hapa mezani sikuwa na jinsi ilinibidi ningoje matokeo kwa kujua kuwa ntapata challenges lakini na jibu litapatikana.


Nilivumilia na nikasitisha mawasiliano. Sikuwasiliana nae kwa njia yoyote ile. I was do as he do to me. Akinitumia sms nikawa simjibu. Akinipigia napokea namjibu in short kama niko kazini namwambia niko bussy kidogo ngoja ntakupigia. Na kama ni mida ya jioni namwambia ngoja ntakupigia mtoto ananisumbua mwisho wa yote sipigi wala sijibu sms zake.


Wakati huo nilikuwa nafatilia mawazo ya wanablog wenzanu ya kuwa nimfate dar bila taarifa yoyote wakati huo ndo tulikuwa tunaelekea kwenye Valentine Day. Nilifatilia maombi ya ruhusa ofisini angalau kwa siku tano ili nije dar boss wangu hakuniruhusu kwa sababu Mi ni Accounts Administrator na huwa tunafunga hesabu za mwezi tar ambazo nilikuwa nimeomba. So it was difficult to move.


Basi Mpaka ikafika tar 14 no call from me to him and no call from him to me. Roho iliniuma sana ukizingatia mi ndo nilianza kuuchuna. Siku hiyo ya tar 14 nikatoka kazini mchana as u know it was week-end. Nilipitiliza hadi home nikaandaa chakula mapema nikaoga na kujipumzisha.
Ikafika saa mbili yausiku sm yangu ikaita. Kupokea ni yeye akaniuliza uko wapi nikamwambia niko hm akaniambia toka unifungulie geti. It was supries. I felt like iwant to fall down.


Nikatoka nikamfungulia. Akaniambia samahani sana nimekuja bila taarifa. nikamwambia no worries its your home and am your married wife. Akasema nimeitahidi sana nije maana siku hiyo yaani tar 14 mwezi huu wa pili ndo tulifunga ndoa AICT na tulikuwa tunatimiza miaka 5 ya ndoa mwezi huu.


Baada ya yote akanilaumu nimebadilika nimekuwa mjeuri akinipigia sizunumzi nae akinitumia sms simjibu. Na mi nikamwambia na mi nilikuwa naumia hivyo wakati ule najitahidi kuwa karibu nae ye anakuwa mbali. Akanisihi nisifanye hivyo maana yuko mbali nipunguze mawazo he loves me sour much, hayuko radhi kunisaliti ila ni majukumu tena ya mda mchache tu.


Alikaa tarehe 16 alfajiri akaondoka. Sikumwamini hata kidogo nilijua ananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Yaani da Dinah ye aliondoka kwa flight ya saa mbili pass through Nairobi. Mi nikaondoka na Flight ya saa sita mchana.


Nilichukua chumba jirani na hotel anayoishi na kwa mda mfupi nikagundua kuwa chakula hula pale kila siku jioni. nilijenga mazoea na yule dada muudumu nikampatia cash kidogo. Akawa karibu na mimi mno. So kila nilichomdadisi alinipa ushirikiano wa kutosha bila chochote.


Pale pale kwa maelezo ya yule dada nikajua no one alse ila baadae niligundua yule dada alijua habari za pale wa kuwa house boy wa mr wangu ni jamaa bf wake. Nikamuuliza kwani huyo kaka yupo akasema alikwenda mza kuiona familia yake amerudi leo amefika tu nakuondoka ameenda kazini. Ilipofika saa mbili ya usiku alikuja pale hotelini akapata dinner akaenda nyumbani kulala. Saa tano ya usiku nikamtuma yule dada aniitie yule bf wake alishagaa sana nikamwambia aende.


Alipomwita nilimuuliza unanifahamu mimi akasema nahisi nilikuona seemu ila sikumbuki ni wapi. Nikamwambia kumbuka vizuri hapo hapo nikamwuliza na uyo mtoto je? Akamtazama kwa makini akasema huyu mtoto anafanana na bossi wangu theni akasema nimekutambua ni wewe ndopicha zako na mtoto zimetapakaa mle ndani. nikamuulizabosi wako yupo akasema yuko anaangalia tv.


Nikamwambia beba huyo mtoto twende hakuna kumshitua. Akaniongoza hadi ndani Da dinah, hakuwa na taarifa kama tuko pale lakini nilimkuta ameshika picha yangu niliopiga sku ya wapendanao akiitazama kwa hisia wakati huo alikuwa ametoka kunipigia sm nikamwambia niko home najiandaa kulala.


Alipata mshituko usiosemekana. Na mi nilipofika nilidhibiti sm yake vilivyo sikuona sms ambayo itanipa hofu ya kusalitiwa. & now i have find out the true. Kwa mda wa siku mbili nilikuwa pale kweli da dinna Mr wangu yuko bussy mpaka nilimwonea huruma. Napenda kuwashauri wanawake wenzangu tusiwalaumu wala kuwalaumu wapenzi wetu.

Tuwapende tuwe karibu nao, Na watuambiapo jambo lolote tusiwablame inatakiwa uvumilivu na maelewano.Thanks all for your information. And many thankis to You Dinah.
Samahani nimeandika marefu kama gazeti.

Regards.
Mama Johnson.
Mza.

Comments

Anonymous said…
hongera sana mama Johnson,
ni wanaume wachache sana wanaokuwa wakweli kama huyo wa kwako. wengine wanachukulia kazi kuwa kisingizio cha kufanya mambo yao mengine. mpende mumeo na msaidie katika shida zake, zidisha pendo kwani surprise aliyokupa ni uthibitisho tosha kwamba bado anakupenda sana.

Julie
Anonymous said…
Mama Johnson, jina la Bwana libarikiwe! Yaani nimefarijika sana kusoma ushuhuda wako huu. Jitahidi kuendelea kumwombea mumeo ili asije patwa na vishawishi na uendelee kumpenda/muendelee kupendana zaidi na zaidi!
Anonymous said…
Woooh!! what interesting story!!
kwa kweli story yako inavutia na haichoshi, me ni mmojawapo kati ya waliokushauri uje dar ufumanie (kwa mawazo yetu)u know wanawake ni watu wa kufikiria kusalitiwa na waume zetu espicially akiwa mbali nawe, ile kumchunia kimtindo naye akafeel the same ndo maana akaja kuhakikisha, kuja kwake mza ilitosha kabisa kukuhakikisha u'r the only one.Congrats kwa kupata mume mwaminifu nawe kuwa mvumilivu.
Gdday.
Shushu "hot"
Anonymous said…
Tunashukuru kwamba umegundua hali halisi, manake tunapowaambia mnakuwa hamtuelewi. Mara nyingi kutegemea na kazi unakuwa umebanwa kiasi kwamba unataka kuandika meseji kwa mpenzio,lakini kabla hujaimaliza, bosi huyu,au wateja hawa, utafikiri wanajua unataka kuandika hiyo meseji na wao wanataka kukuzuia.
Kitu chema katika ndoa nikuvumiliana,na kuaminiana. Ukiwa unamwamini mwenzako, nayeye atakuamini, lakini kama unamjengea shaka, basi naye itakuwa hivyohivyo. Mkumbuke kuwa nyie ni kitu kimoja, kwahiyo nyanja zenu za hisia zinatakiwa zishabihiane.
Swali kubwa lakujiuliza, je kama mwanao umempa shibe ya kutosha, anaweza kwenda kudoea kwa jirani?
emu-three
maujanja said…
That good thing dada pamoja na kutuomba radhi kwa maelezo yako mengi for sure wewe ni mwandishi mzuri sana.Pia nimejifunza panapo matatizo ndipo penzi hunoga hope unampenda mumeo more than it was b4.
Pia ushauri ulioutoa real ni mzuri mno yaani nimependa sana.
God bless U n ur family mama Jonhson
Anonymous said…
Thats great testmony. Hii itawafundisha wale wanawake ambao wana kawaida ya kuwa na negative perception kuhusu wanaume wao. Kuweni wavumilivu jamani. Wakati mwingine mnaweza kupoteza wapenzi wenu kwa sababu ya hisia potofu tu. Na wanaume wenye negative perception wapate fundisho pia. Nimefurahishwa na uamuzi wa huyu mama kwa kuamua kusoma maoni ya watu kwa makini then akaamua kuchagua njia muafaka wa kushughulikia tatizo lake. Hongera sana.
Anonymous said…
yaani mama Johnson sijui hata niseme nini... yaani unaonekana ni mwanamke mmoja mwenye busara sana!!! Yaani jinsi ulivyolihandle hili swala yaani mie mwenyewe nimeblow... Yaani wanawake wote tungekuwa na maamuzi ya busara kama ww walah tungokoa sana mahusiano yetu! Kiukweli kabisa mie nisingeweza ulivyofanya.. lazima tu ningeharibu pahala.. Manake busara NO! Yaani nimepungukiwa kabisa hiyo busara!!!
Anonymous said…
Hongera Mama Johnson kwa hilo, ila kusema ukweli ni wanaume wachache sana wa design ya mumeo, hasa ukizingatia mke yupo mbali, wapo wanopanga hata safari za uwongo kumbe hawaja safiri wapo na vimada mahotelini, zidisha tu heshima,muombe mungu mtakuwa na maisha mazuri ya furaha na yenye upendo.kitu ninacho kukumbusha ni kusema dukuduku lako sio ipo siku utanuna wakatu yeye kategwa sawasawa ataenda kutolea hasira zake huko, kununiana ni ni dangerous game kwa wapenda nao, ni ndio mianya ya kutoka nje ya mahusiano,

Hongera sana

Lajk
Anonymous said…
Mhh yani naikia raha saana yani hingera sana natamani ningekuwa mie Duuh yani sijui unafuraha gani yani hongera sana
mie nisingeweza ila ningeumia kupita kiasi maana na mie mume wanngu ni mtu wa kusafirisafiri na huwa anajisahau au sijui kwahkuwa anajua lazima mie ntaanza kumpigia hapigi. lakini Hongera sana
ila duh unamoyo a ujasiri na mie umenipa fundisho ntajaribu ila nilivyo na jazba sidhani kama ntakuwa na uvumilivu. hongera sana tena sana yani nakuonea raha mnoo
Anonymous said…
Mama Johnson thats awsome!
Mimi ni mwanaume ambaye nipo mbali na mke wangu na bahati nzuri wote huwa na kawaida ya kutembelea blog hii ya Dina. Tuliposoma matatizo yako wakati ule tulikuonea huruma sana pia yalituchochea kuwasiliana zaidi na zaidi. Leo tumefarijika kusikia habari njema hizo. Mungu awabariki na baba Johnson.
Anonymous said…
Sooo sweet, kama hadithi maskini. Tunakutakia kila la heri mpendwa, endelea kumombea Mungu nawe ujiombee muwe wenza wema.

Kina baba msitulaumu, sometimes matendo yenu yanatukwaza. Mume wangu mie yupo mjini hapa hapa, lakini wakati mwingine sms niliyomtumia leo nikiwa ofisini anasoma ana-respond kesho yake. Ukijitahidi sana kuuliza ukiwa home, atakuambia wallahi sikumbuki kuiona! Jamani, sawa nakubali yuko busy, hasa hizo sms ambazo hazikuonekana ni zangu tu au zote zilizoingia kwenye simuye.
Anyways, tuyaache hayo, ila mpendwa hii yako nimeipenda, endelea kuijenga ndoa yako iimarike zaidi...
Anonymous said…
i like that hongera mwaya umebarikiwa mume muaminifu.