Wednesday, 4 February 2009

Tuliachana, sasa nusu anitaka nusu hanitaki-Ushauri!

"Mambo vipi Dinah,
Mimi ni kijana wa miaka 29. Nimekuwa na mahusiano na msichana mmoja wa miaka 25. Kwa sasa tumeachana kwa takribani miezi sita. Tatizo nililonalo ni kuwa tangu tuachane baadae niliona kuwa bado namfeel na yeye alionyesha kuwa bado ananifeel hivyo niliamua kumueleza dukuduku langu.


Yeye akaniambaia kuwa niendelee na maisha yangu, ghafla baada ya wiki mbili akanitumia msg kuwa anani-miss sana kuwa nae na kuwa bado ananipenda na ataendelea kunipenda daima. Mimi nikaamua kumuuliza kuwa yeye hisia zake kwangu zikoje? Jibu alilonipa ni kuwa nusu anataka kuwa nami na nusu hataki kuwa nami.


Pia ameniambia kuwa bado ananipenda sana na hajapenda mwanaume yeyote so far. Pia hajatembea na mwanaume yeyote tangu tuachane.Sasa wandugu hapa huyu mrembo anania gani na mimi? Kama still ananipenda and half anawish niwe nae then kwa nini hataki au kusita niwe nae?


Maana hata nikimwita tu anagoma kuja. Yaani kwa kifupi haeleweki msimamo wake kuwa nini hasa anataka. Mawasiliano yetu sio mabaya. Tunasalimiana kama kawaida.

Dada Dinah na wanablog naombeni ushauri."

Jawabu:Mambo ni mazuri kabisa Kaka, nafurahia likizo baada ya kuwa kule "busy" kwa taribani mwezi na nusu.


Sasa rafiki hujaeleza sababu ilisababisha wewe na binti huyo kuachana kitu kitakachofanya watu, well labda mimi tu kushindwa kukupa maelezo ya kutosheleza na yenye uhakika. Unajua, unapotoka kwneyeuhusiano kutokana na tofauti fulani fulani haina maana kuwa na mapenzi yamekwisha juu ya yule mpenzi wako.


Huenda kilichotokea au kusababisha muachane au namna ulivyomuacha au alivyokuacha ilimuuma sana na kumfanya apunguze hali ya kukuamini tena au kujiamini mwenyewe kwenye suala zima la mahusinao ya kimapenzi na hilo likitokea ni wazi kuwa atahitaji muda ku-sort out kichwa chake na hisia zake kabla hajawa na uhakika wa nini anakitaka ktk maisha yake ya kimapenzi na ngono ofcoz.Sheria moja kuu ya kurudiana baada ya kuachana (well sio sheria inayojuliakana bali huwa naitumia mimi kwa wateja wangu kama wewe leo hapa) ni kuwa unapoachana na mpenzi wako kisha ukagundua kuwa bado unahisi nae za kimapenzi ni kupigania penzi hilo kwa kuonyesha mapenzi ya kihisia ya hali ya juu kuliko mwanzo.........
badala ya kucheza ule mchezo wa "kutegeana".


You just go for it full speed, viginevyo wajanja watakuwahi na watapenda binti kuliko ulivyokuwa unapenda na hilo likitokea ujue wazi kuwa binti hatokuwa na mapenzi na wewe tena kwani mapenzi ya mpenzi mpya yatafunika penzi lako la kusua-sua.


Fafanua akisemacho-Wanawake wengi huwa hawako wazi kusema ukweli, wanakuachia wewe ung'amue anachomaanisha hasa kama anataka wewe umuonyeshe kuwa "unamuhitaji". Sijui nini kilitokea na kuwafanya ninyi wawili kutengana lakini ninachokiona hapa kutokana na maelezo yako ni kupimana misimamo au hisia.


Huyu binti alipokuambia uendelee na maisha yako ni wazi kuwa alikuwa anataka kusikia ukisema "siwezi kuendelea kuishi bila wewe, maisha yangu hayatokuwa kama yalivyokuwa bila wewe mpenzi".....sasa baada ya wewe kuuchuna na kuendelea na maisha yako kiukweli (ulidhani ndivyo alivyomaanisha).

Si umeona mwenyewe akaona hujapata "meseji" akaamua kukumbusha kwa SMS na kusema kuwa anaku-miss, anakupenda na atakupenda daima.....hapo alikuwa anasema ukweli ulio wazi kwa vile wewe hukupata ujumbe wa "endelea na maisha yako".

Kosa kubwa ulilifanya-Alipokuwambia kuwa ameku-miss, bado anakupenda na atafanya hivyo daima, hukupaswa kumuuliza hisia zake juu yako!! Ulitakiwa kumkumbatia na kumwambia kuwa unapenda pia na ungependa mrudiane au kujaribu tena uhusiano wenu.


Mwanamke anapokuwa wazi hivyo ujue kazidiwa na mapenzi(katumia mbinu zote umeshindwa kuelewa), binti anakuhakikishia kabisa kuwa uko peke yako moyoni mwake pale aliposema kuwa hajapenda wala kutoka na mwanaume mwingine (kumbuka ni miezi sita imepita), mwanamke akikaa miezi sita bila kuingia kwenye uhusiano mpya hata kama sio wa kimwili na bado anarudi kwako na kudai anakupenda ujue huyo ni 4 the keep hehehehe sio lazima iwe hivyo, usiogope my broda!.


Nia yake ni kutaka kurudiana na wewe lakini kwa bahati mbaya wewe huonyeshi kutaka kurudiana nae sina hakika ni kwavile huelewi anachokisema kwako au na wewe huna uhakika na hisia zako za kimapenzi juu yake??!!. Ile nusu anakutaka (ni hisia zake juu yako) na nusuhatakikuwa na wewe (ni kwavile hujamuonyesha kuwa unamtaka back).


Sasa skia, inakwenda hivi, sawa!......Muombe msamaha kwa kutokuwa nae kwa muda wa miezi sita (kwamwe usigusie nini kiliwaachanisha), mwambia hisia zako bila kumuuliza yeye anajisikiaje juu yako. Mwambie kuwa unampenda sana na ungependa kuishi maisha yako ukijuwa kuwa yeye ni mwanamke wako peke yako, mueleze kuwa utafanya kile uwezacho ili kufanya uhusiano wenu uwe mzuri, wenye mapenzi ya dhani na wenye afya.


Mwambie tangu mmekuwa mbali-mbali maisha yako yamekuwa sio kama vile yalivyokuwa mlipokuwa wote, mhakikishie kuwa utamuonyesha mapenzi motomoto ambayo hujawahi kumuonyesha hapo awali (hakikisha unafanya hivyo.....hata kama ni kumshukia chini au kumla denda kwa mtindo tofauti).....ongeza na mwengine ujuayo wewe kama mwanaume.


Usitegemee jibu la papo kwa hapo (hii inategemea na ufundi wako wa kubebembeleza, ikiwezekana toa chozi mshikaji...it'll work).....asipokubali on spot mpe muda na wewe kuwa kwenye mawasiliano mara nyingi kuliko kawaida.


Unapowasiliana hakikisha unamsalimia kikawaida nakuonyesha kuwa unajali, lakini kama vipi fanya mawasiliano ile mida ya "chombeza" hakikisha una-flirt(hata kama ni kwa SMS), unamkumbusha mlipokuna (ruka matatizo mliyokutana nayo au mlivyoachana), zungumzia maisha yako ya baade na yeye...Mf-Kama tungekuwa wote sasa hivi tungefanya hivi-vile nakadhalika.

Kila la kheri!

4 comments:

Anonymous said...

kaka achana na wasichana wa namna hiyo wengi wao ukikubali kurudiana nao ana kaa akiona men ingine ya muhimu kuliko ww anaingia mitini.usiumize moyo wako mwambie nenda tuu tusiwe mguu ndani mguu nje haiwasaidii wote

Anonymous said...

kaka usilazimishe penzi,jaribu tena mueleze kama haelewi tulia utapata mwingine anaye kupenda, pia hujaeleaz sababu iliyo wafanya muachane mwanzo,pengine hana imani nawewe kutokana na mazingira kumuacha mwanzo, so ulicheza na mind yake in a way anajishauri endapo ataumizwa tena.Fikiri kilicho kufanya umuache sitaki nataka pengine ni kutokana na wasi huo, pia kusema kwamba toka aachane na wewe haja fanya na men mwingine hapo hakuna proof, ukweli unaujua mwenyewe si kila tunavyo ambiwa tuamini, wengine huwa wana foji hata bikra sembuse kutembea na mtu mwingine, hiyo ni ktk kukujengea imani wewe kuwa yy ni mwaminifu.
ni hAYO TU.

lajk@ymail.com

Anonymous said...

Mapenzi ni kitu pekee na mitego au mitihani yake ni mingi. Kuna vitabu vingi-`novels', vinaelezea kuhusu wapenzi ambao walikutana na mara wakaachana kwa sababu fulani, hawa wapenzi wakakutana na wapenzi wengine, lakini kila wafanyalo wanakumbuka wapenzi wao wa mwanzo.
Hii ina maana kuwa kupenda au mapenzi hayataki kulazimishana.
Wapo waliolazimishana wakamudu mpaka wanazeeka kama mke na mume- haya ni nadra katika karne hizi. Watu hawa wa karne hizo, ukiingia undani wao watakuelezea mitihani na maumivu fulani ya moyoni.
Karine hii sio kama ile ya kulazimishana,watu wanakutana na kuhakiki upendo wao kuwa ni wa kweli au ni bora liende. Moyo unaweza ukapenda lakini matendo yakaamua vinginevyo, au matendo yanaweza yakawa ya kweli lakini hakuna upendo, yote hii ni mitihani ya mapenzi. Ukibahatika utavuna chema, na ukikosea, utasema aheri ningelijua!
Sasa nini la kufanya. Chakufanya ni wewe mwenyewe kuangalia upendo gani unao-utaka, ili kufikia kilele cha raha na maisha yako ya baadaye.
Wewe mlikutana mwanzoni, mkatekwa na penzi la pupa, mkaachana kwa sababu unazozijua wewe,lakini huenda kila ukikaa ulikuwa unamuwaza yeye na huenda na yeye alikuwa hivyohivyo. Cha muhimu hapa ni kuangalia nini kilichofanya mkosane, na je kikitokea hakitaathiri mapenzi yenu mapya,lakini yote haya hayahitaji pupa muda ukifika, lazima ukweli utasema.
Unachotakiwa, nikukutana naye na ku-ongea naye, elezaneni ukweli, nini unataka, naye umsikilize nini anataka, ili muone kuwa mnaivana, siku ya siku ukweli utagundulika, kwani, mapenzi ni kikohozi.
emu-three

Anonymous said...

Kuwa muwazi huyu dada ulimuumiza sana moyo ndio maana anataka/hataki tuambie ukweli mligombana kwa kosa gani? hapa unatupa upande 1 tena nusu umeacha details nyingi ambazo singesaidia kukushauri.