Thursday, 26 February 2009

Pesa anazo lakini hanihusishi-Ushauri

"Mimi ni mwanamke wa 25 nimeolewa miaka 3 iliyopita kwasasa ni mjamzito hivyo niliacha kwenda kazini tangu mimba hii ilipoingia kutokana na matatito ya kiafya. Mume wangu ana nafasi nzuri kazini na kipato chake kinakidhi mahitaji ya familia yetu.


Baada ya matumizi muhimu kwa kawaida najua anabakisha kama laki 5 kila mwezi lakini hakuwahi kunijulisha kama ana pesa hizo au ana plan gani na mabaki hayo ya pesa, nikimuuliza anasema hana pesa.


Wakati huo mimi kuwa baada ya mahitaji muhimu najua pesa fulani hubaki na sasa amefikisha million 5 lakini hataki kusema ukweli, Pesa hizo zipo kwenye account nami najua password yake lakini yeye hatambui hilo.
Je mtu wa design hii nimchukulie kama alivyo au nimweleze ukweli"


Jawabu: Asante kwa ushirikiano wako, inaonyesha wewe ni mmoja kati ya wanawake wachache ambae ulikuwa ukijituma ili kuchangia kipato ndani ya nyumba na ninachokiona hapa ni ile hali ya "kujishitukia" kwa vile hufanyi kazi unafikiri mume wako atakunyanyasa na bila kujijua unaamua kuomba pesa ambazo pengine wala huzihitaji....kama ulivyosema mwenyewe kuwa anakamilisha mahitaji yote muhimu.


Kitu kingine ninachokionahapa ni kuwa na hofu kuwa anaweza kuwa anazitumia pesa zinazobaki kwa ajili ya mambo mengine kama vile "kuwekeza" kwenye Ulevi na wanawake nje ya ndoa yane kwa vile tu wewe ni mjamzito (kutokana na matatizo ya kiafya ni wazi kuwa tendo la ndoa halipo vile inavyotakiwa kitu ambacho kinaongeza hofu).


Lakini kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa pesa zote zinazobaki baada ya mahitaji muhimu anazitunza Benk, hazitumii kivingine. Kumbuka wewe ni mjamzito which means kuna "mtu" mwingine ataongezeka kwenye familia yenu ndogo na badala ya kuwa wawili mtakuwa watatu nahivyo basi majukumu yataongezeka na kwa mshahara wa mtu mmoja tu mtoto hatokuwa na maisha bore.


Sasa ili mtoto kuwa na maisha bora au angalau "comfortable" ni wazi kuwa kuna ulazima wa ninyi kama wazazi kujiandaa na jukumu hilo jipya. Si hivyo tu bali kuna matukio ambayo hujitokeza bila mipango kama sehemu ya maisha yetu yanaitwa "udhuru" ni wazi kwa akiba inahitajika incase kitu kama hicho kinaibuka.


Sote tunapokuwa na mipango fulani na pesa tunazotunza ili kukamilisha jambo fulani alafu mtu akaibuka na kukuomba seti au kukuazima ni wazi kuwa utamwambia kuwa huna pesa....sio huna kabisaaa bali ulizonazo zinamipango yake muhimu na hutaki kuzigusa unless upate "udhuru" kama kuuguliwa, msiba n.k.


Umchukuliaje?-Since unalo neno/namba ya siri ya Benki Akaunti basi mchukulie kuwa ni mmoja kati ya mwanaume wachache wanaojua majukumu yao, anangalia mbele na sio pale mlipo (kuvaa miwani ya mbao) pia ni muaminifu na ndio maana akakupa neno/namba ya siri ya account (natumai hukuitafuta mwenyewe balia likupa baada ya kuomba).....vinginevyo mume wako anajaribu kufanya mambo yake kama mwanaume na wewe unapaswa kumuamini.


Nini cha kufanya-Hakuna ukweli wa kumuambia hapo kwasababu moja, Pesa ni zake, Pili hazitumii bali ziko pale zimetulia, tatu wewe unataka pesa za nini wakati kila kitu unatimiziwa ndani ya nyumba?


Kama unawasiwasi sana na wewe ni mwanamke kamilifu na mke hivi sasa ni lazima ulifunzwa namna ya kupata unachotaka kutoka kwa mume wako kwa kutumia lugha ya kimapenzi (siwezi kusema hapa kwani kaka zangu wakijua hatutopata kitu), sasa tumia mbinu hiyo kwa mume wako na hakika atakueleza mipango yake kuhusu pesa hizo (akiba) na hapo utapata amani moyoni mwako.

Acha kujishitukia kwa vile umeacha kazi, jiamini hali itakayokusaidia kumuamini mume wako.
Kila la kheri.

13 comments:

Anonymous said...

ukiona mwanamume anayemwambia kila kitu mke wake ,huyo anakuwa na kasolo kubwa sana.wanaume huwa wana mipango mingi sana kwa familia na kwa faida ya familia. ni vizuri na busara usimchefue kwa kutaka kujua anataka kufanya nini, wakati ikifika atakwambia. ukitaka kuharibu ndoa yako, mchokonoe sana mumeo, angekuwa na nia mbaya asingeweka kiasi hicho,atakuwa anajinyima pia.
mpende mumeo,huyo ni wako.kwa nia nzuri kabisa.

Anonymous said...

ukiona mwanamume anayemwambia kila kitu mke wake ,huyo anakuwa na kasolo kubwa sana.wanaume huwa wana mipango mingi sana kwa familia na kwa faida ya familia. ni vizuri na busara usimchefue kwa kutaka kujua anataka kufanya nini, wakati ikifika atakwambia. ukitaka kuharibu ndoa yako, mchokonoe sana mumeo, angekuwa na nia mbaya asingeweka kiasi hicho,atakuwa anajinyima pia.
mpende mumeo,huyo ni wako.kwa nia nzuri kabisa.

Anonymous said...

Wewe dada "usimwage unga penye kuku wengi"Hata kama hakwambii hizo ni pesa zenu wote, tena una bahati kwamba unajua hata p/word ya account yake, wwewe tulia tu maadamu matumizi yanawekwa wazi na hushindishwi na njaa.

Wewe umesema pia ni mfanya kazi, ingawa hujatueleza unafanya kazi gani sijui ya kuajiliwa au yako binafsi.Kama umeajiliwa Je, wewe hicho kipato mchako mnakifanyia nini?Au Je, wewe anajua umeweka kiasi gani benki?

Jambo la muhimu uwe mvumilivu sana katika suala kama hilo vinginevyo watu hapa watachangia mawazo ambayo yatakuchanganya na kukuharibia ndoa yako.

Inawezekana kabisa kwamba mumeo ana mipango madhubuti kwa ajili ya maisha yenu, hivyo anaona akikueleza mabaki ya mapesa yenu unaweza kuyahitaji mtumie vinginevyo, hapa nina maana labda ameona matumizi yako hayana uangalifu.Lakini hilo sina uhakika nalo ila la muhimu tulia nenda taratibu utaona tu kitu mumeo atakachokushirikisha baadaye.

Kumbuka wanawake wengine kwa kuwahusisha wameweza kuharibu mipango.Nakumbuka hata watu wengine walipoarifiwa kuwa watapandishwa vyeo makazini mwao,wakawashirikisha wanawake wao, na wanawake wakatoa siri kwa wengine mitaani kiasi cha kuvuja siri na kusitisha kupewa nafasi hizo.be careful kulalamika juu ya jambo kama hilo.Tulia na lichukulie kwa hekima zote kwani hayo ni maisha yenu ya ndani yanaweza kuwaua bure hata ushangae kwa nini ulikwenda nje kutafuta msaada wa mawazo.Tulia na mimba yako hadi uzae na matumizi yahitaji kwa mumeo uone kama yanaleta shida.

Anonymous said...

Katika maswala ya `ndani’ na yenye `utata’ mojawapo ni tatizo la`kuaminiana’. Tatizo hili ndilo linatupelekea mpaka watu wanaogopa kuandikina urithi. Kuaminiana huanzia kwenye uchumba,jinsi gani unavyomuona mwenzako, lakini pia hujengwa na tamaduni za kuwa mwanaume hastahili kumueleza kila kitu mkewe, na hii ni kwasababu ya `historia ya kusalitiana’ baadaye.
Tukubali kuwa kuna matukio mengi yametokea sababu ya `pesa’ na mali, wanawake kuwaua wanaume zao kwasababu ya pesa, na nyingine kwasababu mume kaandika urithi kwa mkewe,na mke kampata mwingine, kwahiyo anaamua kuondoa kiwingu.
Hii ipo, lakini ipo sababu ya uduni wa elimu na kufikiri asilimia kubwa (hapa Tanzania) ya wanawake hawakusoma, ni wake za nyumbani(mambo ya sheria hawajui), ni rahisi kurubuniwa na tamaa za nje bila kujua athari zake baadaye, kwahiyo wanaume wengi hawana uaminifu na wake zao kwa hilo. Hili ni swala nyeti, kwasababu hata wake wanaofanya kazi ni wachache sana wanaowaeleza waume zao kipato chao.
Kwa maoni yangu, huyo mume wako huenda ni wale wanaoamini kuwa mke hastahili kuambiwa kila kitu hasa katika maswala ya kipato, au jinsi gani anavyokuamini wewe, au jinsi gani mnavyoshirikiana katika swala zima za kipato chenu. Hili mngelianza mapema, huenda isingekuwa shida. Mfano, jinsi gani ulivyoamua kuitafuta password kwa siri bila hata yeye kujua. Hii ni ishara kuwa kuna `walakini katika kushirikiana kwenu’
Nini kifanyike ni kuambizana ukweli, na pia wewe uwe wa kwanza kuiweka hali halisi ya kipato chako kwa mumeo,ili ajenge uaminifu nawe. Uwe mara kwa mara unamuambia ukweli mumeo, nini unataka kununua,na kipi kifanyike ili kuweka bajeti yenu sawa, jaribu kukwepa `umimi’ . Nataka hiki,au kile, sema tufanye hili, tununue hiki…
Mara nyingi nyie wanawake mnachangia hili, mfano ukiambiwa kuna kiasi Fulani cha hela, utakimbilia mambo yako mengi, sherehe, kujipamba, na hata kununua vile visivyo muhimu, hili tunaliona hasa kwa wake wa nyumbani.
emu-three

Anonymous said...

Emu three Big-up.

Huo ndio ukweli, na kama sababu ni msingi wa kutokuaminiana katika pesa usitegemee akuonyeshe. Kama hali hiyo inakusumbua ni vyema uanze wewe kumshirikisha kipato chako bila ya kuficha, na bado hata ukimwambia angalia jinsi unavyoomba kwa matumizi kama si ya lazima itakuwa sumu ya kumfanya aone akikuambia utamissuse na kuendelea kuwa msiri

Anonymous said...

nashukuru kwa mawazo yenu yananipa moyo,mchangia wa 9.27am umusema ukweli kuhusu kutokuaminiana mimi simuamini 100%mumewangu kwani pesa yangu kipindi hicho yeye ndio alikuwa mpanga bajeti hata nikitaka kusuka yeye hunipa akiwa anatoka naweza kumpa kama ninazo ndio maana naona kama ananidhurum

Anonymous said...

Dada yangu pole sana na wasiwasi mkubwa ulionao kuhusu pesa za familia yenu.

Mimi nashauri uzungumze na mumeo na mshirikishane katika mipango yenu kwani wewe unaona hiyo milioni 5 ni pesa nyingi sana. Hiyo pesa ni ndogo sana hasa ukichukulia kushuka kwa thamani ya pesa ya Tanzania hivyo kama mume wako ni mtu wa mawazo ya mbele anajua kwa hakika hana pesa. Utakapo jifungua matumizi ya pesa yataongezeka na hata hivyo mnatakiwa kujiandaa na kuwa na kitegauchumi cha baadae kwani mshahara wa kazi hautoshi kabisa kwa maisha ya sasa. Sijui kama mmeshajenga, kama bado basi ni hakika hana pesa, pia kumbuka kuna emergency inaweza kutokea wakati wotote ambayo inaweza kuwa inahitaji pesa nyingi zaidi ya hiyo aliyonayo na mambo kama hayo.

Hivyo mwanadada usiwe na wasiwasi unachotakiwa ni kuongea na mume wako kuhusi maisha ya baadae na jaribu kumshauri tufanye hili au lile kwa maendeleo ya familia yenu. Ukija na mipango atakusikiliza na sio kusema una hela unanificha.

Hope uko hapo.

Mwanablog FL.

Anonymous said...

Sasa dada wewe unataka kujua nini wakati hata p.word unaijua, ths means mmeo anakushirikisha mkewe, amini usiamini kuna wake ambao hawajui hata brief case p.word ya husband. however huwezi a-z ya husband hiyo never on earth! hata yeye hajui a-z kuhusu wewe??!!!!, so far mm naona husband wako yupo poa hata amekupa p.word, na inaonyesha ana malengo madhubuti na familia yenu, ukitaka afungue account nyingine kimya kimya mtibue uone,jaribu kumshauri mambo ya msingi ktk maisha yenu as long as hela ipo tatizo nini?.

Aidha hujasema kama wewe mshahara wako ulitumiaje lkn all in all usijaribu kumtibua huyo mmeo, jaribu kujua malengo yake ya badae, thts it, angekuwa anatumia ovyo labda, lkn anabana matumizi na ku save...he is good, mshauri kufungua miradi, kuna wafanya kazi wengine siku hizi wanwapa hela hizo wafanya biashara wanapata interest rates mtakayo kubaliana kila mwezi, hela bank tu uzushi miaka hii bank zenye za tz wizi mtupu, they make so much money lkn nyie kama wateja hampati faida ya hela zenu ipasavyo kama interest rate!
all the best

lajk!

Anonymous said...

mpenz wala ucmchokoze huyo mumeo, tena mshukuru mungu kwa kumpata mwanaume kama huyo, coz inaonyesha mumeo ana mipango endelevu kwa maisha yenu, ukiona mwanaume anakumbuka kuweka akiba na wala hatapanyi pesa zake kwa starehe ni jambo la kupendeza.Ninachokushauri kama huwa anakuomba ushauri kwa mipango yake uwe unamshauri kufanya vitu vizuri kwa faida yenu na watoto be proud kwa kumpata mume kama huyo na wala usisikitike hicho ni kitu cha kawaida kwa wanaume.'Enjoy ya life'.
Shushu "hot"

Anonymous said...

Jamani mdogo wangu,mi naona labda na umri pia unachangia wewe kupanic,your still young my dear.Anyway sio mdogo kihivyo,ila nataka nikuambie hivi mume wako ana akili zake maana asipoweka akiba siku itatokea issue ya maana sana halafu hana hata cent unajua utamlaumu sana kama sio kumdharau.Lets say kaja mtu mnaemfahamu,anashida sana na hela ila anakiwanja ambacho bei yake halisi ni mil 10,anamwambia mume wako nipe mil 3 tu nakuachia kiwanja ili tu mimi nitatue matatizo yangu,then wew na mume wako mnakuwa hamna hata hiyo mil 1,unajua itawauma sana!we mwache tu asave pesa,na mwanaume lazima ajitahidi kusave maana anaogopa kuja kudhalilika siku ambayo kunatokea dharura na yeye kama baba kila mtu anamwangalia atasolve vipi hili tatizo.Dogo kama walivyokushauri waliotangulia,usitake kumtibua shemeji halafu akafungua account nyingine ambayo hutaijua na huko akawa anabakisha vijisenti vya wewe kuwa unaangalia ili akikuambia hana hela uridhike!mwache kabisa mdogo wangu,maadamu anakulea vizuri,na hapo ukijifungua maisha yanakuwa so expensive,na unaweza ukute mkaka wa watu kaweka kwa ajili yako ukijifungua akupe full macare!tena mpende sana mumeo,anaakili sana.

Anonymous said...

Tangu lini mwanamke akaambiwa dili za pesa ww?? kuna dili nyingine mkiambiwa hamchewi kuzitoa kwa mashoga wenu saloon ndo mana huwa hampaswi kuambiwa. we hujui mwanake ni dhaifu siku zote??Mkibanwa kidogo na TAKUKURU uchwara au viaskari upelelezi mtatoa siri tu.

Ingwe.

Anonymous said...

Big up anony 9.06.00AM,yani hilo ni jibu zuri sana,mimi ni mwanamke pia lakini nakubaliana na wewe kabisa,wanawake si ni wambea sana,tukikutana tu saloon au huku maofisini ooh mume wangu ananini sijui,yani sipendi hii tabia,wakina baba kazaneni kufisha vipato vyenu maana sisi midomo sijui huwa inawaasha au!

Anonymous said...

POLE SANA DADA KWA YANAYOKUSIBU. PAMOJA NA KWAMBA NAHESHIMU OPINION ZOTE ZA WATOA USHAURI HAPA, LEO NAOMBA NIPINGANE NA BAADHI YA HAO WANAOSEMA ETI MWANAUME ANAYEMWAMBIA KILA KITU MKEWE ANA KASORO, HIVI MKO SERIOUS AU MNATANIA. NADHANI MOJAWAPO YA VITU VINAVYOVUNJA NDOA AU UHUSIANO NI KUTOKUAMINIANA(PESA NA SEX VIKIWA NAMBA MOJA), SISEMI KUWA HUYO MWANAUME ETI ASEME KILA MARA ANAPOSPEND HELA, AMA HATA VITU VIDOGODOGO VINAVYOHITAJI HELA ASEME, YEYE NDIO KICHWA CHA FAMILIA HIVYO ANA HAKI ZOTE ZA KUFANYA HIVYO, ILA ANABIDI AMSHIRIKISHE MKEWE KATIKA ISSUE ZOTE ZA FEDHA, NARUDIA TENA AMSHIRIKISHE MKEWE. NDIO! MKE ANA HAKI YA KUJUA ACCOUNTS ZOTE ALIZONAZO MUMEWE NA PENGINE HATA KUWA NA JOINT ACCOUNT MOJA PAMOJA, HII NDIO MAANA YA NDOA. ITAEPUSHA MENGI, ITAJENGA UAMINIFU NA URAFIKI KATIKA NDOA. KUMBUKA IKITOKEA BAHATI MBAYA MMOJA WENU AKITANGULIA(KUFA), BASI ALIYEBAKIA ESPECIALLY M/KE ANA UHAKIKA NA SECURITY YAKE KIFEDHA, SIYO MARA AANZE KUHISI OOH LABDA ALIKUWA NA HELA HIZI, MARA HIZI SIJUI ALIZIFANYIA NINI, HAYO YALIKUWA MAMBO YA KIZAMANI AMBAPO WANAUME NDIO WALOIKUWA WANAHANDLE KILA KITU FINANCIALLY.
PILI, MUMEO AKIKUSHIRIKISHA KATIKA HAYA ITAKUJENGEA WEWE KAMA MKE WAKE CONFIDENSE KATIKA MAISHA, UTAKUWA UNAJIAMINI NA KUFANYA MAMBO MENGINE MAKUBWA TU AMBAYO HATA YAKAMSHANGAZA MUMEO, NDIO MUME IS THE HEAD LAKINI MKE NI NECK, BILA HIYO SHINGO HICHO KICHWA HAKITASIMAMA, INAONEKANA HUYU M/MME PAMOJA NA BAADHI YENU HUMU BADO MNA ILE MITAZAMO YA KIZAMANI ETI MZEE NDIO ANASHIKA PESA, UPUMBAVU MTUPU. DADA YANGU TAFUTA KAULI YA UPOLE, KAA NA MUMEO NA UMUELEZE UNAVYOJISIKIA, NINAUHAKIKA MUMEO ATAPENDA KUKUSHIRIKISHA PIA. IKIBIDI FUNGUENI JOINT ACCOUNT NYINGINE AMBAYO WOTE MNA PASSWORD MOJA NA MUWE MNASHIRIKISHANA INAPOHITAJIKA KUTUMIA PESA HIZO, OFCOURSE KILA MMOJA AWE NA POCKET MONEY YA MAMBO YA BINAFSI. BY THE WAY MIMI NI M'KE NIMOLEWE MIAKA 9 SASA NA WATOTO WAWILI, KIPINDI NILIVYOKUWA MJAMZITO NA MIMBA YA PILI SIKUFANYA KAZI, LAKINI NILIKUWA NAWEZA KWENDA KWENYE ACCOUNT YA MUME WANGU(namfahamisha lakini)NATOA HELA NA NAENDA KUNUNUA KINACHOHITAJIKA, AU NAMPELEKA MTOTO MOVIE, HII ILINIJENGEA CONFINDENCE SANA YA MAISHA MPAKA NILIPORUDI KAZINI, KAMA MUMEO ANAKUAMINI NA UNAMPA FEEDBACK HAITALETA SHIDA!!
-MAGE!!