Monday, 9 February 2009

Nilitoka na mume wake,nimesaidia wamerudiana lakini....

"Hey Dinah, natumai kuwa wewe ni mzima kabisa. Mie nina changamoto ambayo naamini kabisa wanablog wenzangu wanaweza kunisaidia kwa ushauri.

Nina BF ambaye nimekuwa naye kwa miaka mitatu sasa, kwa vigezo nilivyonavyo ni kwamba nampenda sasa kabla sijakutana naye sikuwahi kufikiri wala kutamani kuolewa. Isipokuwa niliwahi kuwa na BF ambaye tulikuwa marafiki wa kawaida kwa muda mrefu kabla ya kuamua kungonoana then we parted ways.

Mapenzi yetu yalikolea na kuwa matamu zaidi automatically tukajikuta tunakaa pamoja. Kwa kweli sikuwahi kusikia raha ya kuwepo dunia kama wakati huo. Lakini wakati sisi tukiendelea kufaidi maisha kwa kiwango hicho BF wangu alikuwa ametengana na mke wake kwa mifarakano ambayo wenyewe wanaijua na kwa muda mrefu wamekuwa wakikaa mikoa tofauti mpaka sasa.


Nadhani mke wake alikuwa akitufuatilia na kujua kuwa tupo pamoja. Asili ya kazi zangu ni safari, hivyo katika safari zangu nilikwenda Mkoa ambao mkewe anaishi. Nikakutana naye akanifanyia bifu baadae tukapata audience akaniuliza kama nipo na mumewe mie nikatoa nje kwani niliogopa mkono maana nilimwona mshari kama nini.


Kwa bahati mbaya au nzuri nikaenda tena katika Mkoa ule tukaonana akanihadithia mambo mengi kuhusu mume wake ambaye mimi ni BF wangu. Alinieleza walianzia mbali katika maisha na kwamba sasa wamefika pazuri mume wake ndio anamfanyia hivyo.


Nilimwuliza kama mumewe anatunza watoto wao 2 akasema ndiyo lakini anataka arudi kwake kwani anampenda sana. Nilimwonea huruma na ikanigusa sana kwa sababu mimi ndiye ninayesababisha hivyo.


Niliporudi home nilimketisha BF nikamwambia situation na kwamba uamuzi wangu ni kwamba kwa kuwa sina mpango wa kuolewa basi we could be together while she is with his wife and everything will be ok.


To my surprise alikataa katakata kwamba yeye hamtaki na wala hana mpango wa kumrudia. Mimi nilihisi kwamba inawezekana anahisi namtega but I was very sincere. Siku zikapita na mimi huruma ikaendelea kunishika lakini mume wa mtu nampenda.


Tukawa tunapanga mikakati mingi na mke wake ili nimsaidie mumewe arudi kwake kumbuka kwamba nimekataa katakata kwamba mimi sipo na mume wake. Kwa bahati mbaya sana alikuja mkoa tunaoishi kwa majukumu ya kifamilia (msiba).


Kama baba wa watoto iliwajibika kumfariji na nadhani hapo ndipo walipo ombana radhi na kusameheana , wakaanza upya. Mimi pia nipo pembeni nafurahia mafanikio yao. Mke wake akaendelea kunisisitiza nimsaidie ampate mwanamke aliyemkamata mume wake. Kwa mara ya kwanza niliona kuwa ananitega lakini moyoni nikasema mtego huo hauwezi kunikamata.


Naomba nikufahamishe kwamba aliponiuliza mara ya kwanza nilikataa kushirikiana na mumewe lakini nilikiri kumfahamu na kwamba huwa tunawasiliana isipokuwa ni nyanja za kazi tu. Nilipoona anazidi kusisitiza nimsaidie nikamua kufikia maamuzi magumu sana ya kumwacha mpenzi wangu huyo.


Ilikuwa ngumu sana kwani nampenda sana huyu mwanaume. Nilijaribu kumwambia kwa lugha ya taratibu na upole sana lakini hakuwa tayari kabisa. Nilimwambia nafanya hivyo kwa ajili yake na mke wake. Bado akakataa.


Nilimtoa nyumbani kwa nguvu na kwa ugomvi mkubwa sana. Ilikuwa vibaya kwa sababu tulikuwa tukiishi nyumbani kwangu. Aliona kama nimemnyanyapaa. Baadaye alifanikiwa kuondoka na kurudi kwake. Hata hivyo alikuwa anakuja nyumbani kwangu mara nyingi tu.


Baada ya muda mrefu wa mawasiliano ya mbali hivyo akaanza kukata mawasiliano kwa muda mrefu kama wiki mbili tatu hivi simsikii. Akiibuka anasema atakuja nyumbani anataka kungonoka. Tukingonoka anapotoea tena kwa muda wa mwezi or so na akirudi anataka kungonoka.


Hiyo tabia ikanichosha nikaamua kumwambia kwamba ilipofika panatosha kwa sababu naona kama ananifanyia mzaha na kutaka kuniumiza roho. Yeye akasema kwamba nilimuumiza sana kwa kumfukuza nyumbani kwangu na kwamba jeraha nililosababisha litachukua muda kupona.

Mimi nimechoshwa na hiyo tabia na kila ninapojaribu kumwacha nashindwa kwani akitokea nasahau kwamba nilitaka kumwacha tunaendekeza libeneke.

Wanawake wenzangu nisaidieni lakini pia wanaume naomba ushauri kwani tabia zenu zinafanana.
Kim from Atown"

Jawabu:Hi Kim, hapa kila kitu kiko sawia kabisa. Kwanza napenda kukupa pongezi kwa kutokuwa mbinafsi na kumsaidia mwanamke mwenzio kurudiana na mume wake. Hongera sana kwa hilo.


Ni kawaida kwa wake na waume ktk umri fulani kutojiona au kufikiria kama sio kutamani kuolewa au hata kuzaa (muda ukifika utalifikiria hilo na kutenda kama ifuatavyo), natambua uamuzi wako wa "kutojikita" kwenye ndoa ulikufanya uone kawaida kutoka na mwanaume yeyote utakae mpenda bila kujali kaoa na familia au la, nafahamu uamuzi wako ulikupa hali ya kujiamini sana kama mwanamke kitu ambacho ni kizuri...i mean kujiamini.


Lakini katika hali halisi no matter how unajiamini na kujitegemea usithubutu kutoka na mume wa mtu kwa kudhania kuwa hutoruhusu akuoe au kumuacha mkewe kwa ajili yako......kwani kwa kufanya hivyo sio tu utakuwa unaumiza mwanamke mwenzio bali pia utakuwa unaharibu mpangilio mzima wa maisha ya mtoto au watoto waliozaliwa kwenye ndoa hiyo na vilevile kufanya watu ktk jamii kutothamini ndoa(kitendo chako kinatoa ujumbe kuwa huthamini ndoa za watu).


Kutokana na sehemu ya maelezo yako inaelekea huyu bwana pamoja na matatizo mengine ya kindoa kama vile kuzozana mara kwa mara kitu kinachoweza kusababisha asipate ngono na mapenzi ya kutosha kutoka kwa mkewe.


Huyu bwana sio tu alikuwa akihitaji hifadhi kutoka kwako ili apumzike kiakili (kutokana na matatizo ya kindoa) bali na ngono pia. Unajua, linapokuja suala la ngono, akili kutulia na kuwa "comfy", hakuna maswali ya kipuuzi-puuzi, lawama za kizembe na malalamiko ya ajabu-ajabu kama sio kusingiziwa, mwanaume wanaweza kuhamia na kusahau familia yake kama unavyo "blink" vifuniko vya macho yako......bila shaka umeshuhudia hilo na unauzoefu mzuri tu.


Kuachana na mtu unaempenda ni ngumu sana na ndio maana huwa nawashauri "wateja wangu" kama kweli wanania ya kufanya hivyo lakini upande wa pili bado unasumbua kama huyo Ex bf wako ni kukata mawasiliano kwa kubadilisha nambari za simu na anuani ya makazi. Vinginevyo kila mkionana utahisi kutaka kuwa karibu nae na kufanya chochote na hivyo uhusiano wenu utakuwa ule wa on and off kwa vile wewe bado unampenda na yeye bado anapata ngono tamu na ya bure kutoka kwako.


Lakini kwa vile mkewe anamtafuta "mwizi wake" ambae ndio wewe lakini yeye hajui kuwa wewe uliyesababisha mumewe arudi nyumbani ndio "adui" ni vema kuachana kabisa na huyo bwana kwani huwezi kujua huyo Mdada anataka kumfanya nini huyo aliyemlia mumewe.....well huenda anataka tu kujua nini ulikuwa ukimfanyia mumewe ili na yeye afanye (fanya utafiti ujue anataka nini hasa kutoka kwa mwizi wake kwanza hehehehe unaweza kutolewa macho kama sio roho.......mtu chake atii).

Sasa mimi nakushauri utumie nguvu (kibali cha Polisi) ili kuzua huyo bwana asije tena kwako, kwa kufanya hivyo itasaidia wewe na yeye kuepuka "ngono chafu" na mume wa mtu. Natambua kuwa unampenda huyo mume wa mtu lakini kumbuka sio wako na kamwe hawezi kuwa wako.

Pamoja na uamuzi wako wa kuwa mwenyewe for life haina maana basi utembee na mwanaume hata kama ni mume wa mtu, jaribu kuwa mchunguzi unapotaka kuanzisha uhusiano ili usirudie kosa. Hakikisha unamfahamu mhusika kabla hujaji-comminte kwake kama mpenzi, hakikisha unakujua kwake, anaishi na nani n.k.

Wapo wanaume wengi tu ambao hawana wake kwa vile hawako tayari kuoa kuoa kwa mara ya pili baada ya Talaka au wake zao wamefariki dunia, nadhani wanaume wa namna hiyo wanakufaa zaidi na mtakuwa compartible in a way.

Kila la kheri.

11 comments:

Anonymous said...

Sasa dada- huyo bwana umeshamzoea hivyo- je hutampa tena?

Kama wote ni waislam basi uwe mke mwenza!

Anonymous said...

we dada, jitaidi kutafuta mpenzi wako mpya bwana. Mara nyingi mnawatega wanaume wenye ndoa wkt mnaona kabisa mnachofanya sio kizuri. sikatai kuwa wapo wanaume marijali ambao hawatosheki ndani. We tafuta tu mwanaume mwingine saiz yako mtapendana tu na utamsahau huyu bingwa na umintroduce kwa huyo jamaa bila shaka ataacha kukufuata. hlf akikufuata, sio lazima umpe game na wewe. Mnyime mwambie uko period hawezi kulazimisha unless unatoa tako.

jaba

Carol said...

Achana na mume wa mwenzio, tafuta wako, unataka ushauri wa nini? unafikiri kuna yoyote anafurahia unachofanya, kwa nini usitafute wa kwako? stay away from that man. Unaitesa familia yake bure including watoto.Ur so selfish girl!

Anonymous said...

Kusema ukweli kabisa dada mie nimeumia sana kwa jinsi ulivyomuumiza mwenzio maana hata mie ilishawahi kunitokea , jamani mume anauma jamani waume wa wenzenu hata kama akisema atajiua juu yaki please jiepushe nae jamani tunaumia sana tunaochukuliwa waume maana unaangalia ushajitolea kuwa na mume wako kwa maisha yako yote, ikitokea kitu tofauti inauma jamani. pili nakupa hongera sana kwa kuwasaidia wakarudiana kweli katika jambo la thawabu ulilolifanya toka umezaliwa ni hilo na Mungu atakuzidishia na atakusaidia sana na wewe utapata wako peke yako japo hutaki kuolewa, tatu mi nakuomba achana na huyo jamaa kabisa maana anaweza akawa anakuja kwako kwa ajili ya ngono tuu ila ana mwengine pembeni ambaye anamkeep busy ila akiona mambo yamemchunia ndio anapikutafut , wee kaa naye chini mwambie nilikuwa nataka ukae na mkeo kwa amani sasa msharudiana nao mba ukae nae usimcheat tena na wewe uachane nae kabisa. mie nakutakia kila la kheri.
Key

Anonymous said...

Mambo vipi ndugu na jamaa,yaani we dada mimi ni mwanaume lakini umenitia kizunguzungu na story yako,toka lini ukaona mwizi anashangiliwa?? wewe umeiba mme wa mtu ambye ana watoto kwa kipindi kirefu, tena unafanya hivyo kwa kufurahia alafu tena unataka watu wakushauri ! wakushauri nini??.Sizani kama una huruma kwa mkewe kama unavyodai,ila unataka watu tukupungunzie`guilty` unayohisi.Ni kweli binadamu wote tuko dhaifu hayuko kamili.we achanaq na huyo jamaa,akikataa mwambie mkewe kuwa humtaki yeye anakusumbua halafu tulia tafuta wako.sio wanaume wote tuko hivyo ni huyo mpumbavu tu

Anonymous said...

Matatizo ya ndoa ni nyeti, na hasa yakichanganyikana na maridhishano ya kimwili. Wengi wanapogombana wanakimbilia kususiana hata tendo la ndoa, nahii ni hatari. Kwani wanaume mara nyingi wanapenda kuchukua mwanya huu kufanya ufusuka wao, panapotokea migongano, tofauti na wanawake. Hii ni tabia ya baadhi ya wanaume. Sababu kubwa, wengi wa wanaume wanachukulia kigezo cha kutuliza akili! Ni kweli mke ni kitulizo chema cha roho,hasa ukimpata anayejua hiyo kazi na mbaya zaidi umpate ambaye atakupa ambacho hukuwahi kukipata kwa mkeo

Magomvi ya ndoa yanapotokea wengi wanachukua nafasi hiyo kuwadhulumu wanandoa, hii naiita dhuluma, kwasababu hawa watu walishaoana, mtu mwingine anapochukua nafasi hiyo kabla ya kuachana au kuoana wanakuwa wanaiba. Hii inaweza ikawa kosa la mwanaume kwa kutokuwa muwazi kwa nyumba ndogo hiyo.
Nakubali kuwa wanaume wengine ni wajanja wa kutongoza, na akitongoza hakosi, lakini kwanini wanawake musiwe na subira kwa kudadisi undani wa huyu mtu,na ukigundua kuwa ni mume wa mtu achana naye, kwasababu fikiria kama wewe ungefanyiwa hivyo ingekuwaje? Huenda unaweza ukasema `si-alinitaka yeye mwenyewe’, ni rahisi kutamka hivyo kama hujaolewa au hujaoa, lakini ukiingia ndani ya ndoa, utagundua uchungu wake. Akija mtu wa namna hiyo mwambie kama unanitaka ngoja kwanza nimuulize mke wako kama ataridhia!
Kwa ushauri wangu, wewe umeshafanya kosa, na moyo umeshakusuta, na huruma imekuingia, basi achana kabisa na huyu mume wa mtu. Muelimishe na msusie kungonoka kabisa,kama ni urafiki uwe wa kawaida, lakini usingie maungoni, kwasababu unachofanya leo kwa mwenzako na kesho utafanyiwa wewe, je utafurahi ukifanyiwa hivyo.
Emu-three

Anonymous said...

hi Kim,

Pole kwanza kwa mkasa huu...niseme kuwa unavuta hisia za wengi,

Sasa basi, piga moyo konde, uachane na huyo bwana. Madamu uliweza kumtoa nyumbani kwako hutashindwa kummtoa mawazoni mwako. Ikibidi kata mawasiliano kabisa japokuwa najua ni vigumu

Ulijitahidi kumshauri arudiane na mkewa na kweli walifanikiwa lakini sasa kwa kufanya hivyo, inabidi wewe uachane naye. Mungu atakupa thawabu kwa hilo.

Jikaze tu, sijui una umri gani lakini nadhani bado una nafasi ya kupata mwingine mtakayeendana pia! usikate tamaa...haya mambo ni magumu lakini yanawezekana

Kila la heri

PapaaK

Anonymous said...

Kwanza nikupongeze kwa uamuzi uliofikia wa kumrejeshea mwanamke mwenzio kiburudisho, ila hilo swala la kuendelea kung'onoka nahuyo jamaa fanya life kabisa, sio fair, try to imagine kama wewe husband wako ndo anafnaya hivyo, you will obviously feel bad jaribu kuwa mstaarabu, natambua swala la mautamuz lkn sishauri kushare love, huyo mwanaume ni limbukeni hata wewe anaweza kuja kukufanyia hivyo ikiwa mtarudisha relationship seriously.

Lkn pia mimi huwa nashindwa kushangaa hawa wanawake wa aina yako wanatoka nje ya ndoa yao na wewe unataka akuoe sasa ww ukiwa kam mkewe akiwa na mwanamke mwingine utaridhika??

Think of you and the other woman too, hapo mnacheza na risk hadi ya magonjwa huyo jamaa ni limbukeni hana lolote, nishaona wanawake wa hivyo wengi sana wakizipata wanajifanya mke wazamani sio dili kachoka/ used wanataka new products, by the way wewe huna watoto so bado huja chuja kivile with tym ukiwa na watoto u'll be kama huyo aliye kimbiwa.

However, umeonyesha sense ya humanity na huruma japo haipo complete, try to make it complete. mbona vidume wengi tu na wataalamu kama kawa jamani,tena rijali utakimbia mwenyewe hizo raha tulia tu utapata wako ambaye atakuwa husband wako unajinafasi naye bila woga hao waume za watu ni sawa na nguo ya kuazima haisitiri mat***!!!!

Ni hayo tu sister, take kea

by Barakam@ymail

Anonymous said...

me ningependa kukushauri tu mpnz achana na huyo mume wa mtu tafuta mwanaume wa kwako, kwanza hata cdhani kama unaenjoy mapenzi kwa hali hy, mapenzi co kutiana tu kuna kutoka pamoja na kufanya vitu mbalimbali pamoja, sasa hapo naona hauko free na huyo m2 na mapnz ackwambie mtu yanauma, ujue kuna cku tu huyo mwenye mali atakufanyizia lazima. ulifanya uamuzi mzuri kuwapatanisha na nakuomba ufanye uamuzi mzuri pia kwa kuachana na huyo m2, napenda kukwambia pia kwamba kwa jinc ulivyoelezea inaonekana huyo jamaa pia anampenda mkewe.najua utaumia coz ulimpenda sana jamaa lkn jiachie kuwa huru wape nafac wanaume wngine wakupende i hop utapata atakae kuridhisha pia. Ciao!!

Kim from A- Town said...

Hey there,
Dinnah, mie ni Kim from Arusha. Am very greatful for this blog kwa sababu mara nyingi watu tumekuwa katika dillema na hatujui nini tufanye. Lakini kwa kuwa na hii blog kunatusaidia kupata ufumbuzi wa changamoto zetu.
Binafsi nimefarijika sana na contributions from you guys na naahidi kuzifanyia kazi. Najua imewagusa wengi hasa waume za watu na wengine wamekuwa wakali sana. Lakini all in all it shows how bad this is and I hope there are other people out there whether a man of a woman who are in the same situation, hii itatusaidia kuona ni kwa jinsi gani watu wanaumia juu ya waume zao.
It has so hard for me to make this decision but I promise I will the best I can kumuacha huyu kaka aendelee na mkewe and I will be very happy to see them as a happy family.
Nawashukuru sana walionishauri constructively. Nimefurahia ushauri wa Papaak, Em - three, Key. Em - three you are doing great mara zote nimesoma comments zako unashauri watu vizuri. Carol stop blaming the victim because we are here to help each other and I think that was what Dinnah had in mind when constructing this blog.
Thank you so much guys and God bless you. Dinnah hongera sana.

Anonymous said...

KWANZA NAPENDA KUKUPONGEZA KWA UAMUZI WA KUACHANA NA MUME WA WATU JAPO ULIKUWA MGUMU.
PILI NAPENDA TU KUKUPA FACT KUWA AHA UNAZOZISIKIA UNAPOKUWA NAE MKEWE ALISHAZISIKIA PIA WALIPOKUWA WANAANZA UHUSIANO WAO, ALL WOMEN ARE THE SAME! NIKIWA NA MAANA KUWA HATA WEWE UTAKUWA NA MATATIZO NAE SIKU ZA USONI UTAKAPOKUWA NAE, KUMBUKA KUWA KUNA KIPINI CHA HONEMOON KWENE KILA NA UHUSIANO NA KUNA KIPINI CHA KUTOELEWANA PIA, MWENZIO ALIKUWA KWENE STAGE NGUMU KATIA NDOA NDIO MAANA KAKIMBILIA KWAKO, THINK ABOUT THAT, KAMA ANAWEZA KUKUMBIA MKE WAKATI UKIWA MGUMU NA WEWE SI EXCEPTIONAL!