Thursday, 19 February 2009

M3 anaomba tufichue yale yanayoweza kuharibu ndoa!

"Moja ya dhumuni la kuanzisha blog hii (dada Dinah,kama nimekosea unisahihishe), ni kujaribu kufichua yale yanaharibu mahusiano na kuboresha yale yalipo, kwa kuyaweka wazi kwa kila mmoja, ili kama wewe hukuwa nalo utajifunza au utaliacha ili uende sambamba na mwenzako.


Kwahili la kutokujaliana, ni vyema sisi kama wanaume au wewe kama mwanamke ukasema nini hasa kinachokufanya usifanye hivi au ukafanya vile, kwani kusema ukweli huo, ndiko kunakoweza kutusaidia.


Mimi ningependa kufichua yale ambayo wanaume tunayo, na kawanini tunafanya hivyo. Kwa upande huo wa kutokuwasiliana, ipo dhana tumejijengea kuwa si vyema kumzoesha mkeo kila kitu, kwamba mimi nafanya hivi au nataka kufanya vile kwa mfano kukupigia simu mara kwa mara inaleta mazoea ambayo ukikosa kupigiwa utaleta dhana potofu, hii ni moja ya sababu.


Lakini ipo sababu kubwa ambayo hata nyie wanawake mnayo, ni ile ya kujisahau. Kwamba sinimeshaoa, sinimesha-olewa, kuna sababu gani ya kuhangaika mara simu mara nifanye hiki na kadhalika.


Wengi wanasema eti mkishaoana, mnazoeana kama dada na kaka. Wewe dada ni dada na mke au mume ni hivyo hivyo, havina mbadala. Jiulize kama ni dada yako unaweza ukaoga nae? Kwahiyo kila siku inapokwenda hakikisha unajiweka kama vile `unatafuta’.


Kila siku inapokwenda hakikisha hufanyi makosa ya kumfanya mwenzako ahamanike ni `vipita njia’ kwani jamani kila kukicha vinazaliwa vyombo…. Kwahiyo hasa kwa hawa wanaosafiri hukutana ni vishawishi hivyo ambavyo vinawaweka njia panda.


Jingine la muhimi ni mawasiliano. Hili ni tatizo, sugu,sisemi mawasiliano ya simu,nasema mawasiliana kama mke na mume. Sisi wanaume mara nyingi hatupendi kujadilia, hasa katika maswala ya ndani, ya kimahusiano, tunataka kufanya.


Mnapokuwa ndani mjaribi kujadili, kuelezena na kupeana ushauri kuhusu hili au lile. Nashangaa wengine wanasema maswala ya mapenzi hayahitajiki majadiliano mkiwa mumeshaoana,kwanii mnatafute nini zaidi! Inabidi tujadili, tuelekezaneni ka kuwekana sawa.

Unaacha bwana au bibi keshasafiri unaanza kulalamika huku nyuma. Pale mkiwa uso kwa uso ndipo pa kujadili. Mhh, yapo mengi ngoja niwaachie wenzangu, wenye nia ya kufichua uzaifu huu, ili tujenge mahusiano mema.
emu-three"

Nafichua, machache ya wanawake ambayo yanaweza kuharibu ndoa;
(1)-Kufunga ndoa bila kuwa tayari (kufuata mkumbo, kuamini ni baraka, kufuata pesa).

(2)-Wanawake tukipenda na kupendwa huwa na tabia ya kujisahau pale tunapojuwa tumeolewa, u dont put an effort anymore kwa kuamini kuwa amekuoa so hawezi kwenda popote.

(3)-Kutokujua tofauti kati ya Mpenzi na uhusiano......wengi hutegemea "hisia" kuboresha penzi hawajui kuwa unatakiwa kufanya kazi ya ziada kuwa na uhusiano udumu.

(4)-Kukimbilia kuzaa (kwa imani kuwa ni kukoleza mapenzi) bila kuwa tayari/kujua utajigawa vipi kati ya mapenzi, uhusiano na majukumu kama mama.

(5)-Kumtegemea mwanaume kwa kila kitu yaani kumfanya "ajira".

(6)-Kujiachia kwa maana ya kutojipenda tena na una"tilia" vivazi vizuri ikiwa tu unakwenda kwenye sherehe au unakoga na kujifukiza manukato siku ukiwa unataka tendo.

(7)-Kuchukulia Ngono kama wajibu.......uvivu wa kujifunza kupenda tendo hilo takatifu.

(8)-Kuamini ktk msaidizi (houseBoy/Girl)......kumpikia mwanaume ni alama ya upendo (kule nitokako mimi) hivyo Vigoli huwa hatupikii wanaume ovyo-ovyo unless njemba kama imekuja kuchumbia.

(9)-Heshima ya uoga....huna mpango wa kumheshimu mume wako lakini unamuogopa au unaogopa kuachwa.

(10)-Kutokuwa na tabia ya kum-challenge mumeo, kila asemacho wewe ni "ndio bwana"...challenge him, onyesha kuwa u r smart woman!

(11)-Kutokumpa mume wako muda wa kutosha....unakuwa busy na marafiki/shoga au familia yako kila wiki.

(12)-Kujihusisha sana kwenye familia yake hasa kama kuna migogoro kati ya ndugu na ndugu. Unatakiwa kuwa upande wa mume wako lakini jua ur limit, kamwe usiponde ndugu zake hata kama yeye anawaponda.

(13)-Ile kaingia tu unamuwahi na nini kilitokea b4 hata hajanywa chai/kaa chini nakutuliza akili...hujui siku yake ilivyokuwa mama, ongea nae lugha ya mapenzi kumlainisha, mkande ili awe relax kabla hujamshitaki mwanao kuwa aligoma kwenda shule au kafeli jaribio la hisabati.

Yapo mengi ila kwa sasa wacha nitunze ndoa yangu.
Midas.

11 comments:

Anonymous said...

Mawasiliano ni ufunguo wa kudumisha na kuendeleza ndoa ya furaha na matumaini. Communication is the key to a successful marriage. M3 nakubaliana na wewe. Shukran hii kweli inafundisha

Mdau said...

Hallo Da Dinnah

Nakushukuru kwa kazi nzuri unayofanya ya kufanya mahusiano yadumu.

Mimi nina dukuduku moja na ningependa kufahamu zaidi. Kuna hizi style za wanawake kuingiliwa uani yaani kuliwa tigo naona inakuwa popular siku zinavyozidi. Dukuduku langu ni kuwa hicho kitendo kinaongeza nini kwenye swala la mahusiano, kiimani Uwe mkristo kwa mwislam hakikubaliki je kisayansi kinakubalika? Nini madhara yake au faida zake?

Mdau wako.

Anonymous said...

ubinafsi ukitawala ndoa itavunjika. Kwa mfano mwananmmme anapotarajia kufaidi tu vya mkewe wakati yeye hatoi matumizi na support asitegemee kupendwa.

Nimeshuhudia jamaa mmoja kaoa mwanamke msomi mwenye hela kibao na ambaye yupo simple sana nusura nimuoe jamaa kamwahi sasa alipomuoa mke kamwekea tiles kwenye nyumba, kamsaidia kwenye arusi, kampa hela za kumsogeza na support kibao na pia kwa upendo mke kampa msaada jamaa alipokuwa anakwenda nje kusoma lakini cha ajabu mume huyo hamjali kabisa mke wake na anatangazia watu kupitia kwa ndugu kwamba mke wake hafai. Hii ni wakati jamaa hatumi hata sentyi tano ya matumizi, hajali watoto wake wa kuzaa, hatimizi wajibu wake kama mwanamme na bado anamkata mke wake ndo ampigie yeye hela zake anazifanyia nini huyu jamaa? jamani mtu kama huyu anataka nini? Ubinafsi haufai.

Anonymous said...

ubinafsi ukitawala ndoa itavunjika. Kwa mfano mwananmmme anapotarajia kufaidi tu vya mkewe wakati yeye hatoi matumizi na support asitegemee kupendwa.

Nimeshuhudia jamaa mmoja kaoa mwanamke msomi mwenye hela kibao na ambaye yupo simple sana nusura nimuoe jamaa kamwahi sasa alipomuoa mke kamwekea tiles kwenye nyumba, kamsaidia kwenye arusi, kampa hela za kumsogeza na support kibao na pia kwa upendo mke kampa msaada jamaa alipokuwa anakwenda nje kusoma lakini cha ajabu mume huyo hamjali kabisa mke wake na anatangazia watu kupitia kwa ndugu kwamba mke wake hafai. Hii ni wakati jamaa hatumi hata sentyi tano ya matumizi, hajali watoto wake wa kuzaa, hatimizi wajibu wake kama mwanamme na bado anamkata mke wake ndo ampigie yeye hela zake anazifanyia nini huyu jamaa? jamani mtu kama huyu anataka nini? Ubinafsi haufai.

Anonymous said...

Wanaume ndio waanzilishi wa kuvunja ndoa. Tabia zote mbaya wanazo wao matokea yake mke akiwa mjeuri anaonekana yy ndo mwenye makosa! Jamani WANAUME MUWE KIINI CHA MABADILIKO!!!!!

mimi said...

this z very impotanti topic ile mimi nataka kumuuliza kaka M3 ivi kwanii nyie mnacheat kwenye mahusiano yeni ya kimapenzi..labda wewe hauna tabia iyo lakini in general u mite hv an idea sasa tel me wats da reason..
Mimi

kijogoo said...

mimi sasa hii ndio lugha gani nimeisoma zaid ya mara 10 sijaifahamu unakusudia nini.
kijogoo

Anonymous said...

Kwanini wanaume `tunacheat’ (tunakwenda nje ya ndoa)? Hili ni swali gumu kwa mtu mmoja kulijibu peke yake, kwani ni swala la uzoefu zaidi, ni swali la kila mtu imemsibu nini mpaka akaamua kurukia dirishani, lakini yapo mambo muhimu ambayo yanafaa kila mmoja ayajue kabla ya kumnyoshea mwenzake kidole.
Kwanza tujue kuwa mtu na akili yake `timamu’ hawezi akaamua tu ngoja niisaliti ndoa, labda kama ana ugonjwa wa ngono. Wengi walioamua kufanya hivi wanasababu `maalumu’ amabazo tunatakiwa tuwe wawazi kuzieleza ili tuweze kusaidiana, sababu zinaweza zikazidiana kutegemeana na uvumilivu wa mtu, tabia na upendo uliopo. Mficha maradhi hukomoka mwenyewe. Hili ni muhimu kulielewa.
Pili, nini msingi mkuu wa kuoana, (tunaoana ili kuulinda utu wetu, vinginevyo tungekuwa kama visivyo binadamu, mnakutana mnamaliza hamu zenu …) .Hii ni ajenda kubwa, na mara nyingi wanaume wanakuwa na sababu zao tofauti na wanawake,lakini msingi mkuu kuliko yote umelalia upande wa kiimani zaidi. Ndio maana ndoa nyingi zinafungiwa seheme za imani, na kama ni bomani bado kunakuwa na kiapo cha imani, ambacho kinalindwana katiba husika.
Tatu, ni mtu na hulka yake, licha ya sababu ya kukufanya ufanye hilo, lakini mara nyingi ubinafsi unakuwa ndio chanzo, kwani kama kila mtu angekuwa anajiuliza hivi mimi ningefanyiwa hivi ingekuwaje,nitajisikiaje,nahisi hali yoyote yakuumizana isingetokea. Kila mtu anajifikiria mwenyewe, ndio maana hata hii mijadala `ya kwanini hivi’ , kila mtu anamnyoshea mwenzake kidole kuwa nyie ndio sababu, hatujui vidole vitatu vinatunyoshea wenyewe, ikiwa na maana wewe una makosa matatu lakini huyaoni unaliona laa mwenzako. Subira haipo na ndoa inahitaji subira.
Nafikiri tukianzia na vigezo hivyo vitatu tutaweza kujijibu wenyewe kwanini sisi, wanaume,sisi wanawake ,huyu au yule ameamua kuisaliti ndoa yake,au amelisaliti pendo(Mziki wa Mwasiti unaweza ukausindkiza huu mjadala).
Huu ni utangulizi wangu, je wewe unasemaje?
emu-three

Anonymous said...

Kijogoo lugha ipi unayoiulizia, kwasababu wote hapo juu wametumia kiswahili?

kjogoo said...

lugha aliyotumia MIMI

Anonymous said...

KiswaEnglish, siunajua tena...