Thursday, 1 January 2009

Ushuhuda wa aliyehisi, akahakiki na kupoteza mapenzi!


"Hi, dada Dinah,Mie ni yule msichana mwenye miaka 28 ambaye niliehisi nikahakiki na kupoteza mapenzi. Kusema ukweli nashukuru sana kwa msaada wa wadau wote nimeweza kufata ushauri wenu na nikawa muwazi kuwa kama huwezi kuniheshimu mimi mkeo basi chukua pete zako na cheti chako cha ndoa peleka huko kuliko na umuhimu uniache mie na watoto wangu nitawatafutia baba atakaeniheshimu mie na watoto wangu, akaona sasa inaweza ikawa soo zaidi ikabidi awe mpole.
Naamini hata kama atafanya atafanya kwa adabu na heshima nisijue. Nashukuru ndoa yangu sasa inakuwa na amani tena kuliko ya zamani na inarudi kwa kasi ya ajabu na hata majibu yake ni mazuri kama akiona amejibu halafu nimebadili uso kidogo basi hapohapo naombwa msamaha na kuambiwa "Samahani mke wangu kama majibu yangu yalikuudhi maana sitaki kukuudhi kabisa" inabidi niwe mpole. Sasa sijajua ni kwa ajili ya kuogopa kuachwa kwa ajili ya mwanume mwengine au ni kaamua tu kujirudi tu kwa kuona haya na aibu?
Na yule malaya wake sijamsikia hata kunibipu kakaa kimya kabisa. Kilichobaki ni mie sasa kurudisha mapenzi maana si unajua tena mwanamke akishapoteza mapenzi na kukinai, najitahidi sana kila nikiwaangalia wanangu najikuta sina jinsi inabidi tu niwahurumie na kupunguza ukali na hasira. Nashukuru sana Dada Dina na Wadau woote mlionisaidia kwa mawazo yenu mbalimbali."

4 comments:

Anonymous said...

Hongera sana mama kwa kurudisha upendo kwa mumeo.Umefanya kazi nzuri ya kuzungumza na mwenzi wako hadi sasa mnaendelea kujenga uhusiano wenu.
Bila shaka utaendelea kumtunza mumeo na watoto wako.Jambo moja muhimu katika hilo SAME NA SAHAU yote yalijiri hapo nyumma ili muangalie yaliyo mbele yenu.Usilogwe ukakumbushia kidonda kitakuwa kikubwa,jenga imani kwa mumeo naye atajifunza kujenga imani kwako.Pamoja na kwamba hajakuambia inawezekana hata wewe una jambo linalomkwaza,lakini kalifumbia macho.

Zaidi ya yote asnate sana kwa kurejea kutupa feed back.You are really a good mom.Please keep connected with your husband.Good luck in your future life.

Anonymous said...

HONGERA SANA KWA HILO DADA, KILALA KHERI,ENDELEA KUMUOMBA NA MUNGU MAMBO YATAKUWA MAZURIZAIDI.

LAJK

Anonymous said...

Mama wawili nimefurahi sana kusikia maelewano na mumeo yamerudi vizuri. Mimi ni mwanaume nilipoisoma habari yako mwanzoni nilisikitika na kuhuzunika sana, kwani yaliyokupata ni mazito mno. Kama alivyosema anony wa kwanza samehe japokuwa najua kusahau ni ngumu. Jitahidi kuwa nae karibu na kujiangalia ww mwenyewe ili mumeo ajue ni jinsi gani alitaka kupoteza tunu njema ambaye ni wewe mkewe. Kila la heri.

Anonymous said...

Dada Dinnah hongera haya ndio mambo jamii inapaswa kusisitizia. Kwamba kuwe na msamaha katika ndoa, kusahau yaliyopita na kusonga mbele. Sio kukomaa na devorce.

Dada nakupongeza jenga familia ulikuwa kwenye bonde la maisha sasa panda kileleni kwa furaha na amani.

Happy New Year 2009
..