Monday, 12 January 2009

Ushuhuda! Katangaza ndoa lakini....Ushauri!

"Dada dinah pole sana kwa kazi za kuelimisha jamii. Mimi ni msichana wa miaka 24 ,nina tatizo ambalo naomba msaada wako pamoja na wadau wengine tena naomba kama inawezekana unipe favour unisaidie angalau ndani ya wiki hii ili nisije nikajiharibia.


Dada tatizo langu ni hili; mimi nina mchumba ambaye tunategemea kufunga ndoa mwezi wa tano mchumba wangu ambaye kwa kweli nampenda sana yeye anakipato kidogo ukilinganisha na mimi, lakini nimejitahidi kumuonesha kua fedha wala dhahabu haviwezi kuleta furaha ya moyo.

Sasa juzi alinifuata na kuniomba nimsaidie kulipa mahari jamani kweli nilisikitika alivyo kujana kuniambia ''dia kweli nakupenda toka moyoni na napenda ndoa yetu iwe hata kesho tatizo linakuja kua hela zina nipungukia na natakiwa mwezi wa pili nipeleke mahari nisaidie mpenzi nimekwama '' ukizingatia kua huo mwezi wa pili ndio anatakiwa aende ili akapewe tarehe ya ndoa.

Kusema kweli hela anayoipata ni ndogo ukilinganisha na kile anachodaiwa, sasa dada naogopa kumsaidia japo naumia sana, naogopa baadae kwenye ndoa asije akaniletea dharau kua hatamahari ulijilipia mwenyewe.


Nisaidieni kua nimsaidie au nizibe masikio japo ni mambo mengi tuna saidiana ila hili nimeliona ni kubwa. Nitashukuru kupata ushauri wenu ilinikaufanyie kazi .


USHUHUDA: Dada mimi nilisoma Makala yako inayo husu jinsi yakumfanya mwanaume atangaze ndoa, kweli nilifanya hivyo na nikashangaa siku tatu baada ya kumfanyia vibweka nikashangaa anakuja nakuomba tena kwa magoti ''Dia naommba unisikilize shida yangu '' nikamuinua eeeh sema shida gani ya kunipigia magoti ? nataka tufunge ndoa yani tena mwakani sitaki hata mwezi wa sita ufike .

Nikauliza kulikoni mpenzi, nikasikia ooh nimeamua tu. Nikahoji utaamuaje fasta hivyo ? nikasikia "duh hayo maswali mengi sana ina maanisha hutaki ?" nikasema kimoyomoyo mambo ya dada Dinah hayo , nikasikia dia nataka nifaidi kwa karibu sasa najua nikibung'aa nitakuta mwana siwangu.


Kuuanzia pale wivu ulizidi nikashangaa ananisindikiza kila mahali ukaribu ulizidi sana wakati mwingine naambiwa kabisa mama unanitia wivu. Samahani kwa mlolongo wa maneno. Nilikua najaribu kutoa ushuhuda ."

Jawabu-Hongera sana kwa kufanikiwa kumfanya atangaze ndoa, unajua kuna wanaume wengine wanakuwa na wewe kwenye uhusiano kwa muda mrefu bila kuonyesha nia ya kutaka kuwa na wewe daima (Ndoa), sio kuwa hataki bali anadhani bado anamuda wa kusubiri sasa hilo likitokea basi ndio wewe mwanamke unapaswa kumsaidia kwa kumfanyia mambo niliyoelezea ambayo wewe uliyafuata na yametimia.


Ushirikiano-Ni moja kati ya nguzo tano za kuboresha uhusiano wowote wa kimapenzi, tunapozungumzia kushirikiana na kufanya mambo pamoja kwa faina yenu nyote wawili hatuzungumzii kwenye kuwa pamoja katika kufanya maamuzi au kufanya mapenzi tu bali hata kwenye suala zima la kiuchumi.


Ninyi ni wapenzi na uhusiano wenu ni mzuri na baada ya muda mfupi mtakwenda kula kiapo cha kuishi maisha yenu yote kama mke na mume. Hili likitokea ni wazi kuwa kutakuwa na suala la kusaidiana ili kufanya maisha yenu ya ndoa yawe mazuri na kuishi vile mpendavyo na sio kwa shida kuu.


Kutokana na maelezo yako unaonyesha ni binti mwenye kuthamini mwanaume na haujaegemea sana kwenye suala la Usawa ambao mimi huwa naona ni ujeuri ambao wanawake wengi wanaubeba kwa kisingizio cha "Usawa" na ndio maana mpenzi wako akawa huru kuja moja moja kwako na kuomba msaada, katika hali halisi alipaswa kwenda kuomba/kopa rafiki zake au hata baba yake.


Mahari-Haya ni malipo yanayotolewa na mwanaume ili kuruhusiwa kuoa binti husika, matumizi na maana ya "malipo" haya ni tofauti na inategemea na Mila za wahusika. Mf-Ninakotoka mimi mahali sio ya wazazi, wajomba na shangazi bali ni yako wewe binti.


Ikipokelewa kama ni mifugo au pesa basi baada ya muda unakabidhiwa kwa maana kuwa unahitaji kitu cha kuanzia maishani wewe na mume wako. Mahari hiyo haiesabiki kuwa inatoka kwa kijana anaetaka kuoa bali inatokwa upande wa pili yaani familia ya mumeo, sasa binti hapa anaweza kupewa nafasi ya kutaja kiasi cha "malipo" anachotaka kutoka upande wa pili na mara nyingi Mahari hiyo hutumika kufanya maandalizi ya sherehe ya ndoa na sio kuanzishiwa biashara (hakuna kulipana ikiwa ndoa itaharibika).


Vilevile binti anaweza kuamua mahari ilipwe kwa mafungu (taratibu) au asipokee kabisa na hii inategemeana na uwezo wa familia ya mpenzi wake ambayo kwa wakati huu atakuwa anaijua vema.


Lakini Mila nyingi huwa na malipo ya awali ambayo ndio muhimu "kimila" ( na sio pesa nyingi, zaidi ni kununua vifaa/vitu fulani fulani kwa wanafamilia bibi, mkwe sijui mkaza mjomba n.k) kabla Mahari haijalipwa, hayo yakikamilishwa mipango ya ndoa inaanza mara moja na Mahari inaweza kulipwa baadae hata baada ya kufunga ndoa.


Kasumba-Suala la "ndio maana ukajilipoa mahali" lisikusumbue kichwa, ni kasumba tu ya wanawake wajinga wajinga ambao wanaamini kuwa ni lazima kuolewa na mwanaume mwenye "mahela" na wanaangalia zaidi kiasi gani cha pesa as for Mahari mwanamke mwenzao kalipiwa.......lakini katika hali halisi ulipiwe elfu 20 au milioni 50 bado utahitaji mapenzi na mambo mengine mengi ambayo hayahusishi pesa, ili kuifanya ndoa yako iwe nzuri, yenye afya, furaha na amani hapo baadae.


Nini cha kufanya-Mchumba wako kasema (kama ulivyoandika) "Dia kweli nakupenda toka moyoni napenda ndoa yetu iwe hata kesho tatizo linakuja kuwa hela zinanipungukia natakiwa mwezi wa pili nipeleke Mahari nisaidie mpenzi nimekwama".


Huyu bwana (kutokana na nukuu hiyo hapo juu) anaomba kuongezewa pesa ili a-top up kile kidogo alichonacho ndani ya muda aliopewa na sio kukuomba wewe mpenzi wake ujilipie Mahari yote, kwa maana nyingine, inawezekana kabisa ikawa sio msaada wa pesa anaotaka kutoka kwako bali ni wewe kuzungumza na familia yako kumpa muda zaidi wa kukusanya pesa ili kukamilisha mambo.


Kama kweli mnapenda na nia yenu ni kuishi kwa shida na raha maisha yenu yote yaliyobaki basi msaidie kwa kuongezea kile kidogo alichonacho. Huitaji kumwambia mtu yeyote kuwa umemuongezea mchumba senti ili akamilishe mahari on time. Chukulia kuwa mmeamua kuchanga kufanya jambo muhimu kwa ajili ya maisha yenu kama vile kununua kiwanja na kujenga nyumba pamoja.

Kila la kheri ktk kukamilisha shughuli za ndoa. Mungu akujaalie.

12 comments:

Anonymous said...

Dada kama unampenda huyo kaka then ni bora umsaidie ili muanze maisha. Kwani Mahari ni nini? si utamaduni tuu uliwekwa na baadhi ya watu. Sasa kama unataka kumsaidia ni bora ukamsaida.. Lakini kabla hujaamua kufanya hivyo, kwanza fikilia mambo machache, jambo la kwanza ni hli: Jee ni kweli kabisa ndani ya moyo wako upo tayari kuolewa na mtu aliye na kipato chini yako? Kama jibu ni YES then go ahead with 100% determination kwamba utafanya kila liwezekanalo kuongeza kipato chake, na kwamwe katika maisha yenu pesa haitokuwa kikwazo cha penzi lenu.

Na kama jibu ni sijui, basi ni bora ukaomba ndoa ihairishwe mpaka utakapo jua nini unataka.

Make sure maamuzi yako sio emotion zaidi, bali umefikiria. Kumbuka ya kwamba ndoa ni ndoano. na safari ya ndoa inaanzia unapopajua kwenda usipopajua, so who knows how the ride is going to be? Kwa hiyo kama you real ready, then funga mkanda and enjoy the ride.

Mwisho, ukiamua kumsaidia mahari, then MAKE SURE HATA SIKU MMOJA HUTOFUNGUA MDOMO WAKO NA KUMWAMBIA KWAMBA "MAHARI YENYEWE NILIKUSAIDIA"

www.jamii1.blogspot.com

Anonymous said...

Dada uliyeuliza hili swali,mimi sijaolewa ila nitakujibu kama ifuatavyo
1 ukimsadia kulipa mahari si mila kwanza za makabila mengi ya tz
2 ukimsaidia kulipa baada ya miaka 10 mna watoto 3, mauudhi yameanza atakwambia hata mahari ulijilipa mwenywe sasa mwanamke gani?una kiherehere cha kuolewa.
3 pia anapoteza uanamme wake kihalisi.

Anonymous said...

Dada kuwa muwazi tu mtazamo wa haraka unaonyesha ur after money not love,kipato cha huyo jamaa si basic point hapa.ww kama na mawe sababisha mkaishi wote mtapata zaidi kwani na imani usharidhika naye, so kipato chake au kuomba kusaidiwa kulipa mahali kisiwe kigezo cha ww kuona kama utachekwa..hakuna kitu cha ajabu hapo hiyo ipo sana japo ni kimyakimya watu hawasemi! pia labda kama umeona mpita njia au ww ulikuwa mpita njia, ts u!!

Kuhusu ww kuchangia kwenye mahali eti atakucheka baadae its illogical aidha useme hamjuani vizuri lkn kuna incedence kama hizo hakukuwa na tatizo mpaka now ingawa inaweza kuwa ni bahati nasibu. Lkn kama mpo siriaz na relation yenu sioni logic questioning income ambayo bila shaka uliijua b4 n u took tht 4granted.ss hapa ungesema kuwa ulikuwa unamtumia tu hata kama alikuwa na kipato kidogo ila kama umeridhika naye sioni sababu ya kusita.......unaweza kuona sio ishu lkn with time unaweza regret unless kama unaye mwingine ambaye yupo better economically ndio ana kuzingua! watch out kuna mmoja alikuja kuomba ushauri hapa kaolewa na kibabu cha kizungu kisa hela lkn kwenye sita kwa sita ni 0+0=.........,minyege tu imembaki na kuanza kutoka nje ya ndoa na vijana wengine of which ni risk kuachwa akikutwa/kugundulika kama ana cheat.

Kama ni hela u still can find while mpo wote coz mta enjoy kama kawa.ila uamuzi ni wako hapa ushauri tu coz ww unamjua zaidi huyo man wako ingawa hujasema 4how long umekuwa naye na kwakuwa umesema pesa si furaha ya moyo, kipato chake shouldnt be a poit of discussion,kwanza ni muwazi kwako coz angekuwa mwingine ange bit around the bush for so long na ww unaweza mdis kumbe yupo siriaz, so if ur siriaz utaamua vizuri.
hongera 4tht stage,
all the best

lajk@ymail.com

Anonymous said...

I don't know kama hizi ni mada mbili tofauti au ni moja,but anyway kwa muomba ushauri wa kwanza about kumlipia boyfriend wako Mahari ,Don't even try kumsaidia mpenzi wako katika suala la mahari ever ,unless umeona kashindwa kabisa na hana jinsi na may be huyo mwanaume wako awe so nice,hana Gubu and u r sure that he real loves only u, but otherwise kila mkigombana hilo litakua ndo tusi kwako kwamba ulijitolea mahari(ulijioa)
Kunawanaume wako so nice i witnessed one of the couples boyfriend wake hakua na kipato kizuri mwanamke akaamua kulipa mahari na wanaishi vizuri with no quarels but hiyo inategemeana na mwanaume wako yukoje ,so kama unajua haitakuletea matatizo do it but kama unajua itakuletea matatizo u better not do it.

Goodlucky
Baby!!!!!!!!

Anonymous said...

Hey mwana,
Una mawazo mazuri ambayo ningekusihi uyaendeleze.Bila shaka kufuatia maelezo yako unamfahamu vizuri huyo mpenzi wako na hali yake ya kiuchumi.Pia umemshiba sana ndiyo maana umekata shauri kuoana naye.

ushauri wangu ni kwamba tafadhali sana msaidie hiyo shida yake maandamu kwa malelezo yako mlikuwa mnasaidiana longi.Usihofu kwamba baadaye ataanza kukusuta kwa hilo jema utakalofanya.ujinga na upumbavu utakuwa juu yake.hakuna jamii itakayovumilia ujinga wwake kama kweli itatokea,bali wewe utabaki muungwana kabisa mwenye staha ya hali ya juu.

Mimi ninayeandika hapa nimeoa.Wakati nimechumbia nilipangiwa vitu mbalimbali kupeleka ukweni.kwa bahati nzuti nilikuwa na kazi nzuri na mchmba wangu alikuwa na kazi pia ya kufaa.Yeye bila kumuomba mimi aliamua mwenyewe kuvipunguza kwa kutoa pesa zake mwenyewe kama sehemu ya kusaidiana maana ssi yeye aliyevihitaji vikolombwezo vyote vilivyohitajika.Kwa hiyo alinisaidia nusu nami nikatoa nusu.La msingi hapo alijua kuwa pesa ninazohitajika kutumia ni pesa yetu wote maana ndo tulikuwa tunajiandaa kufunga ndoa baada ya muda si mrefu.

kwa msingi huo wewe dada msaidie kwani huyo kijana mumeshibana na kuridhiana,na kama tangu mwanzo mumekuwa mkisaidiana kwa nini hili liwe gumu ambalo tena ndilo la kuwafanikisha katika ndoa yenu ili ifungwe?Mimi mke wangu alinisaidia na tunaishai kwa kuheshimiana,hasa mimi namheshimu sana na kujivunia kwa sababu najua ana utu na kunijali.Kama ulivyosema mwenyewe kwamba mara zote umemwambia kuwa pesa siyo kiegezo cha ndoa japo wewe unamzidi mashpidi ya uchumi,hilo ni jambo muhimu basi kuona umuhimu wa kuchukua jukumu hapo.

Ungekuwa ughaibuni hakuna mahari ya kutoa kuoa.tena nguvu kubwa huwa kwa mwanamke katika masuala mazima kuoana.hata harusi inafungiwa kwenye kanisa la mwanamkau nyumbani kwao au mjini kwako mwanamke.kwa hiyo jivunie sana kwamba unachangia kumwezesha mpenzio kuondoa aibu kwamba ameshindwa kufanya/kutimiza mahitaji hayo.

Uwe huru kabisa katika hilo na litakupa chati kubwa sana katika mapenzi yenu maandamu wewe umekiri kabisa kuwa si pesa zitakazowapelekea kupendana katika ndoa.Holla mwana maliza mambo mkafaidiane huko.

Anonymous said...

Mapenzi ya kweli ni ya kusaidiana, na hii inaweza ikaanzia hata mkiwa bado wachumba. Ndio hiyo ni dhana kuwa mwanaume ndiye anayetakiwa awe anamsaidia mwanamke, lakini hii inategemea na uwezo, kwani tukiamua kuifuatilia hii dhana ina maana kuwa mwanamke tajiri hatakiwi kuolewa na mwanaume masikini.
Upendo haujali umri, hali za kipato au maumbile, upendo mara nyingi hujengwa na hisia za ndani. Wangapi, wangapi wameoana na utakuta hawaendani kabisa na sura zao, umri wao, au kipato chao au hata maumbile yao. Huu ni ushahidi tosha kuwa upendo hujengwa na hisia zitokazo ndani, nje ni vikorombwenzo tu.
Ndugu yetu, mahari unaweza ukachangia bila wasiwasi, na hata ukiweza unaweza ukajitolea ukayatoa yote. Kwasababu mahari ni mali yako wewe, na wewe ndiwe ulitakiwa utaje kiasi gani kutegemea na umuonavyo mwenzako. Sasa wewe kama uliamua uolewe kwa dau kubwa na mume hana uwezo huo,inabidi umpe tafu kama wanavyosema wanamitaa. Hii haina shaka kabisa.
Na ni kwa maoni tu. Tunapotaja kiwango cha mahari tusitaje kiasi kikubwa, tutawafanya waoaji wakate tamaa. Kiwango kikubwa hakimaanishi kuwa wewe una thamani. Muangalie na mwenzako uwezo wake ili muanze maisha vizuri.
Hayo ndiyo maoni yangu
emu-three

tutahny said...

ndugu hongera sana. mm ni msichana ninao ushuhuda wa dada mmoja ilikuwa km ww jamaa anatangaza ndoa hila hela hazitoshi kutoa mahali,aliamua kumuomba mpz wake yule dada aliamua kumsaidia mpz wake kutoa mahali ktk hali ya mapenzi kwavile wote wanapnda kilichokuja kutokea later wapo ndani ya ndoa jamaa mshiko ulikuja kukubali akaanza kufanya dharau kwa mke wake kurudi usiku hiyo haikutosha ilifikia hatua anakuja na wanawake zake ndani usiku chi=umba wanacholala na mke wake wanavunja amri ya sita mkeo yupo. mke akalalamika jamaa alikuja sema ww mwenyewe si ulijitolea mahali kwan mm nilitoa. yule dada alikiangalia kweli alimsaidia mpz wake kuongezea mahali ktk hali ya mapenzi kweli alikuwa anampenda, kilichotokea yule mama aliachana na mume wake, jamaa aliendelea na maisha yake hadi sasa hapo pamoja. ushauri wangu kwako, bora hasimalize hiyo mahali then atamalizia later kuliko umsaidie coz later atakuja sema kama ulivyosema unaogopa au kukufanyia km huyu anti niliyekuambia. nikweli ilitokea miaka ya 80's so be carefull even if u luv him dnt du that ma frnd utajajuta later. ni hayo tu

Anonymous said...

Huyo jamaa ni bwege wa kutupwa na anapenda mteremko japo kipato chake ni kidogo.
Mahali ni jambo muhimu sana, inafaa liwe jasho lako ili uonyeshe upo serious...basi angeenda kukopa au angekwambia ana shida nyingine harafu ungempa hy hela angeenda kulipia mahali.
Dunia ya saa imebadilika sana, kwa sie waislam swala la mahali anatakiwa aseme mwanamke...kwahiyo anapata fursa ya kujadili na mume mtarajiwa, kwahiyo unaweza hata kuoa kwa mahali ya tende, kusoma kurani hata shilingi mia maadam umetoa kitu kidogo tu lkn siku hizi mahali mamilioni, jamani unaniuzia??

Anonymous said...

Dada angu pole sana.
Kwa hilo dada usithubutu kumsaidia mahali au posa.
Wanawake wengi iwa wanafanya sana ujinga huu wa kumpa fedha mwanaume ili amwoe unajua nini kitakuja kukutokea.??
Kutokana na yeye kuwa na kipato chini ndoa yenu hapo baadae itakuja kupata misukosuko...ni dhahili jamaa anaweza akawa anajisikia inferior kwa vile wewe upo juu.
Na vilevile siku zote mwanaume iwa anataka awe juu sasa hapo wewe mshiko unao yeye hana mtaendana kweli.
Naona huyo sio kiwango chako dada.
jito.
jitonyile@yahoo.com

Anonymous said...

Dada Dina na wachangiaji,
Hii mada muhimu sana kwa wazazi wote wanaosoma blog hii. Mahari hisiwe kikwazo kwa watu kufunga ndoa,wazazi mtaje mahari kulingana na uweze wa muoaji.
Miaka ya nyuma sana ilitokea baba mtu akataja mahari ndogo sana,kama kwa sasa hivi mtu ataje mahari kuwa Sh.500/= halafu mzee akaiweka kwenye fremu na kuitundika ukutani sebuleni,dhumuni la huyu mzee lilikuwa tofauti na mada hii. Yeye alifanya mahari kuwa ndogo akiogopa binti yake kwenda kuteswa kwa kutaja mahari kubwa na pili aliamua kuiweka katika fremu ili siku ikaja ikatokea ugomvi,basi mume hasimtese mke amrudishe kwao na kuchukua Sh.500/= yake TENA ILE ILE ALIYOTOA mahari!!! Ndoa hii ilikuwa ya Kiislamu.
Dada uliye na tatizo hili nakushauri mambo yafuatayo:
1.Omba nafuu ya mahari kutoka kwa wazazi wako,yaani jaribu kuongea nao kwa upendo wapunguze mahari ili mumeo mtarajiwa aweza kulipa kiasi kidogo na kingine amalizie siku za baadae.
2.Kama kuomba nafuu itashindikana basi omba hasilipe yote,alipe kidogo ili nyingine aje kumaliza siku za mbeleni.
3.Kumsaidia sikushauri kwa sababu maisha ya ndoa huwa yanakumbwa na misukosuko mingi sana,inawezekana ikaja tokea kamzozo kadogo sana,wewe ukaja muambia 'wewe si mwanaume hara mahari nimekutolea mimi'jambo ambalo litamuumiza,au kama alivyosema mchangiaji mmoja inawaza kuja kutokea mgogoro akakuambia 'kwani mimi ndio nilikutolea mahari,si ulinitolea wewe mwenyewe'mimi sikuwa na mpango na wewe', ikaja ikakuumiza.
Kikawaida na nafikiri hata kidini kulingana na historia na hadithi za katika dini,ingawa sikumbuki sawasawa,mahari inashauriwa iwe ni jasho la mwanaume mwenyewe,ingawa pia kuna baadhi ya jamii mahari mwanaume anatolewa na baba yake kwa sababu kwao jukumu la kutoa mahari ni la baba kwa sababu inafahamika kuwa baba anamuolea mtoto wake.
Kwa mfano mimi tulipanga na mchumba wangu mahari ambayo ataenda kuwashawishi wazazi wake ili nilipe,wazazi walisema kwao wao binti hana wajibu wa kuwashawishi mahari,nilipangiwa kubwa ingawa ilikuwa ndani ya uwezo,lakini iliharibu mipangilio mingine kwa sababu kipindi cha harusi pesa zinatumika sana.Nilipokwenda kulipa nikatoa kidogo nyingine iliyobaki nikatakiwa kutaja tarehe ambayo nitaimalizia,nikataja na ilipofika nikaenda kumalizia na mimi na mchumba wangu tukarudishiwa thamani ya ng'ombe mmoja ili atuwezesha kuanzia maisha. Sisi ni wakristo.
Kwa hiyo kiujumla mahari inategemea na jamii ambapo ndoa inafungwa, kwa mfano nasikia India wazazi wa msichana ndio wanatoa mahari.
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com.

Anonymous said...

Holla wee binti!
Mimi nakushauri msaidie huyo mchumba wako.Usijali hayo maneno mengi yasiyo na uhakika.hata kama huyo mpenzi wako atakuja kukutukana baadaye hiyo si hoja maana wewe utakuwa ulitenda wema.Mbona hata wengine wengi wanatendewa wema na baadaye huwa wanageuka kuwa watu wasiyo na shukrani? Kuna mambo kadhaa ambayo naomba uyaangalie hapa chini:

Kwanza kabisa sisi watoa maoni ni watu wa jinsi tofauti, rika tofauti, kabila tofauti, mila tofauti tabia tofauti na mengineyo.Mambo hayo niliyoyataja yaweza kuwa sababu kubwa ya mtu kukwambia usimsaidie au umsaidie kulinga na hayo yaliyomjenga mtu.

Pia jambo la tabia ya ubahili,kuna watu wengine ni bahili sana hawana tabia ya kusaidia wengine, na tabia hiyohiyo mtu anaweza kuileta au kuipandikiza kwa wengine na kukushauri wewe usimsaidie huyo mpenzi wako.Kumbuka wewe ndiye unayemjua na kumwelewa huyo jamaa yako,hasa kulingana na jinsi mwenyewe ulivyosema.Bila shaka jibu unalo moyoni ila uko kwenye dilema,na hapa umekuja ili uonyeshwe njia halali.Basi mimi nakushauri kata shauri la kumsaidia kwa sababu kama mimi ninavyoelewa msaada hauna majuto hasa kama ulitolewa kwa moyo wote.Tena la kwako ni jema zaidi maana unamsaidia mtu unayejenga naye familia.

Jambo lingine ni muhimu uelewe kwamba hapa wengine wanatoa maoni kwa kejeli na matusi juu,kwa hiyo usitegemee sana kwamba patakupa jibu murua zaidi ya yale unayoweza kuyatafakari mwenyewe kwa jinsi unavyoyajua mazingira yanayokuzunguka, ukweli wa mambo na hisia za moyo wako wewe.Kwa hiyo chambua zaidi ili upate ushauri wa busara kutoka michango hii.Lakini jambo lako liko mikonoi mwako zaidi,na hii ni muhimu ujue kabisaaaaa.Wachangiaji hapa hawatakuja kukutafutia mchumba wala kukujengea familia.

Mwisho niseme hivi kwamba ni bora zaidi kutukanwa kwa kutenda mazuri kuliko kutukanwa kwa kutenda mabaya.Pia mtenda mazuri akitukanwa, yale matusi humrudia atukanaye wewe wasafishwa na ukweli wa huruma yako na upendo mwingi uliokukirimia fikra sahihi za kufanya mema.Ukitukanwa hutapungukiwa akili na utu bali utaendelea kuhekimika zaidi.

nakutakia kila la heri katika maamuzi yako.

Anonymous said...

Muuliza swali, pole sana kwa tatizo linalokukabidhi.
Mimi nimeolewa miaka 8 sasa na mimi ninatoka familia ilio na uwezo kinume na mume wangu lakini ilipofikia suala la mahari kama mwanaume alitafuta mbinu kadhaa za kumsaidia. Ninachojaribu kukuambia ni kuwa, kamwe usije ukamsaidia mwanaume kulipa mahari. Wewe pride ako kama mwanamke iko wapi, najua ni vigumu sana kwasababu unampenda mno, lakini kumbuka siku zote mwanamke anataka kuona mwanaume wake akionesha ujasiri for the sake of their love, mwanamke anapenda kuwa rescued na kupata securiti toka kwa mwanaume, sasa kama hata mahari tu shida, itakuwaje katika kukabiliana na challenge za hio ndoa?? hapo ndio kipimo!!