Thursday, 1 January 2009

Nilihisi, nikahakiki na kupoteza mapenzi-Ushuhuda!


"Hi, dada Dinah, Mie ni yule msichana mwenye miaka 28 ambaye niliehisi nikahakiki na kupoteza mapenzi.


Kusema ukweli nashukuru sana kwa msaada wa wadau wote nimeweza kufata ushauri wenu na nikawa muwazi kuwa kama huwezi kuniheshimu mimi mkeo basi chukua pete zako na cheti chako cha ndoa peleka huko kuliko na umuhimu uniache mie na watoto wangu nitawatafutia baba atakaeniheshimu mie na watoto wangu, akaona sasa inaweza ikawa soo zaidi ikabidi awe mpole.

Naamini hata kama atafanya atafanya kwa adabu na heshima nisijue. Nashukuru ndoa yangu sasa inakuwa na amani tena kuliko ya zamani na inarudi kwa kasi ya ajabu na hata majibu yake ni mazuri kama akiona amejibu halafu nimebadili uso kidogo basi hapohapo naombwa msamaha na kuambiwa "Samahani mke wangu kama majibu yangu yalikuudhi maana sitaki kukuudhi kabisa" inabidi niwe mpole.

Sasa sijajua ni kwa ajili ya kuogopa kuachwa kwa ajili ya mwanume mwengine au ni kaamua tu kujirudi tu kwa kuona haya na aibu? yule malaya wake sijamsikia hata kunibipu kakaa kimya kabisa.


Kilichobaki ni mie sasa kurudisha mapenzi maana si unajua tena mwanamke akishapoteza mapenzi na kukinai, najitahidi sana kila nikiwaangalia wanangu najikuta sina jinsi inabidi tu niwahurumie na kupunguza ukali na hasira.

Nashukuru sana Dada Dinah na Wadau woote mlionisaidia kwa mawazo yenu mbalimbali."

No comments: