Friday, 28 November 2008

Niache Mpenzi kwa ajili ya Ndugu?-Ushauri.


"Dada Dinah,ningeomba ushauri wako.
Nimekua na mpenzi wangu kwa zaidi ya miaka miwili ingawa alikua anaishi kwao lakini alikua akija kwangu na hata kushinda au kulala siku zingine. Sasa hivi majuzi mdogo wangu wa kiume alihamia kwangu baada ya chuo chao kufungwa ghafla na hivyo tukawa tukiishi nae.


Tatizo likaanzia hapo, siku moja nikarudi nakumpa mdogo wangu hela akanunue vitu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mpenzi wangu huyu akaanza kulalamika sana mpaka sasa bado hatujapata mwafaka.


Zaidi anadai kua kuwa atasitisha kuja kwangu kwani inaonekana amekua akikwaza ndugu zangu na pia anadai kua huyu mdogo wangu ham-respect na pia anaona kama yeye anamzibia uhuru wa kukaa nami kama ndugu yake.


Nilipokaa na mdogo wangu kumwuliza yeye alikana kabisa katu katu kwamba hana tatizo nae na pia anamheshimu sana kama shemeji yake. Niliporudi na kumueleza huyu mpenzi wangu akaruka akasema ni mnafiki na wala hamaanishi hivyo.


Cha ajabu nimemwambia niwakutanishe yeye na mdogo wangu amekataa akisema hawezi kukaa na kubisha na shemeji yake yeye atakachokifanya ni kutokuja kwangu. JE HAPO MIMI NIFANYEJE KWANI NIKO NJIA PANDA,nafikiria niachane nae au la kwani simwelewi anataka nini?

Jana nikawa nimempa hatima kua kama hawezi kuishi na ndugu zangu kwa upendo kama anaonipa mimi basi sioni sababu ya kuwa nae akanitumia msg kua NITAFUTE ATAKAE WEZA WAPENDA NDUGU ZANGU.Nimekua njia panda kwani kiukweli nilikua na malengo makubwa nae ila naona nashindwa. Je nifanyeje? Iteitei"

Jawabu: Pole kwa kuwekwa njia panda. Ningependa kufafanua kidogo tu hapa kabla sijaendelea. Hata siku moja Mpenzi wako hawezi kupenda ndugu zako kama anavyokupenda wewe! Husitegemee mpenzi wako kuwapenda ndugu zako, kwani halazimiki kufanya hivyo.


Yeye kukupenda wewe haina maana kuwa aipende familia yako nzima, ikitokea wanaelewana na wakampenda na yeye akawapenda kama ndugu zako (sio kama akupendavyo wewe) mshukuru Mungu, vinginevyo anapaswa kuwaheshimu (na wao wamheshimu pia) na sio kuwapenda. Kupenda ni hisia, hailazimishwi.


Ndugu wakati mwingine huwa wakorofi, baadhi huwa wanaamini kuwa unamaliza pesa kwa mwanamke na sio kwao kama ndugu zako. Wanasahau kuwa wewe sasa ni mtu mzima unastahili kuwa na maamuzi yako na kuendesha aina ya maisha utakayo au niseme kuwa na maisha yako.


Wewe umekuwa na mpenzi wako kwa muda wa miaka miwili na uhusiano wenu ni mzuri na wakaribu kiasi kwamba Binti huja kushinda na kulala kwako mara kwa mara. Katika hali halisi huyu binti alikwisha jiona yeye ndio mwanamke kwenye nyumba yako au hapo kwako, lazima alikuwa akijipa majukumu fulani kama "mwanamke" na jukumu moja wapo ni kufanya manunuzi kwa ajili ya matumizi hapo nyumbani.....huenda wewe ulikuwa hujui au hukutilia maanani kama mwanaume.


Sasa baada ya mdogo wako kuja hapo kwako, wewe ukahamisha jukumu moja la kufanya manunuzi kwa ajili ya matumizi hapo nyumbani ambalo labda kwake yeye mpenzi wako lilikuwa jukumu muhimu sana kama mwanamke wako au mwanamke ndani ya nyumba. Hakika hapo ndipo alipokwazika na kumempotezea kujiamini kwake.


Wewe kama mwanaume ulitakiwa kugundua hilo (alipokasirika) na kumrudishia jukumu hilo yeye, kwamba endelea kumpa pesa za manunuzi ya vitu yeye na sio Mgeni (mdogo wako). Huyu mpenzi wako aliposema kuwa anasitisha kuja hapo kwako kwa vile Mdogo wako hamheshimu na vilevile kuwapa uhuru ninyi kama ndugu, alitegemea wewe kuwa upande wake kama mpenzi wake.


Sio kwa kumuunga mkono na kwenda kumsakama mdogo wako bali kwa kumhakikishia kuwa unampenda na hakuna mtu atakaeingilia na kuharibu penzi lenu. Avumilie kwa sasa kwani mdogo wako yuko hapo kwa muda tu.


Kwasababu hukumuelewa (wanawake wengine husema hivi kumbe wanamaanisha vile), ndio maana amekataa kukutana na kupatanishwa, alichotaka huyu ni kuhakikishiwa nafasi yake kwako kama mpenzi na kurudishiwa jukumu ambalo labda alikuwa kalizoea kama mwanamke wako.

Uwepo wa mdogo wako hapo nyumbani inakuwa ni tishio kwake hasa kama hawakuwahi kukutana kabla, kwani baadhi ya wanawake hudhani kuwa ndugu wanaweza kuwa-feed wapenzi wao maneno ili watimuliwe.......sasa kwa vile Dogo ni mwanaume huenda hata muda mwingi unatumia nae kuliko kufanya hivyo na mpenzi wako hali inayoweza kumfanya ajishitukie....(asijiamini).


Nilichokiona hapa ni kuwa ninyi wawili mnapendana na wote hamjui mnataka nini kutoka kwenye uhusiano wenu na hivyo mnabaki kupigana mikwara, yeye hataki kuja kwako tena ili kukupa uhuru na ndugu yako.


Wewe unataka aishi na ndugu zako kwa upendo kama anaokupa wewe na akishindwa huoni sababu ya kuwa nae(sasa uko nae kwa ajili ya ndugu zako au kwa vile unampenda?)......kumbuka yeye hajatamka kuachana na wewe.....lakini kutokana na mkwara wako kakupa jibu zuri kabisa kuwa ukatafute mtu atakaependa ndugu zako kitu ambacho hakiwezekani!


Kuishi na ndugu na kuwapa upendo kama anaokupa wewe ni kitu ambacho hakiwezekani (rejea maelezo yangu ya awali), lakini kuishi nao kwa heshima ili kuboresha amani inawezekana.


Kosa-Ulishindwa kung'amua kuwa umemnyang'anya mpenzi wako jukumu ambalo lilikuwa muhimu, pia ulishindwa ku-handle the issue kama mwanaume na badala yake ukatoa lawama huku na kuzipeleka kwa Mdogo wako alafu tena kwa mpenzi wako na mbaya zaidi ukaegemea upande wa mdogo wako badala ya mpenzi wako ambae pengine angekuwa mkeo (una mipango mingi nae).


Nini cha kufanya-Mtafute Mpenzi wako, Omba msamaha kutokana na uamuzi wako(kama mwelevu na yeye pia atakuomba msamaha kwani alikosa pia kwa kusema vitu indirect) na kaeni chini mzungumzie hili suala kwa uwazi zaidi.


Kama kutakuwa na tatizo lolote au mpenzi wako anahisi kutojiamini mbele ya ndugu zako basi mhakikishie mapenzi yako juu yake, ni kiasi gani umeji-commite kwake na ungependa penzi lenu liende wapi kama ni uchumba alafu ndoa.....kama hivyo ndivyo basi ungependa yeye na ndugu zako kuheshimiana (sio kupendana).


Siku nyingine maneno maneno yakitokea usiende kuuliza upande wapili kabla hujapata ushahidi, "handle" kiutu uzima kwa kufanya uchunguzi, pata ushahidi kisha zungumza nao kwa nyakati tofauti na kuwapa onyo.


Hakuna sababu ya kumuacha Mpenzi wako kwani inaonyesha kuwa anakupenda, ila hajiamini. Kama na wewe unampenda na unamtaka basi mtafute, muelezane, msameheane, muonyeshane mapenzi na mrudiane.


Kila la kheri.

Thursday, 27 November 2008

Nampenda rafiki wa X je nimkubali?-Ushauri.

"Hello Dinah kwanza pole na kazi,
Mimi ni msicha mwenye umri wa miaka 26, mwanafunzi wa moja kati ya vyuo hapa Tanzania. Shosti nahitaji sana ushauri maana maji yamenifika shingoni. Nilikuwa na Boyfriend kwa muda mrefu lakini kwa bahati mbaya mimi nikapata shule mbali kidogo na mkoa ninaoishi.Boyfriend wangu alifurahi lakini nahisi haikua furaha ya kweli kwani baada ya kuondoka na kukaa miezi sita hapo shuleni tabia yake ilibadilika nikimpigia simu anashindwa kuongea nikimwambia nimemiss ananijibu kana kwamba kuna mtu anamuogopa.


Baada ya mwezi mmoja baadae alinitumia message na kuniambia ana msichana mwingine kwasababu hajaweza kuvumilia, I was so frustrared baada ya kusikia hivyo kwani nilikua nampenda lakini baadae nilifikiria nakugundua hakuna umuhimu wa kuendelea nae nikamjibu kama ameamua hivyo ni sawa.


Tatizo linakuja huyo boyfriend wangu alieniacha ana rafiki yake ambaye nasoma nae chuo na anajua uhusiano tuliokua nao, ila baada ya kujua kuwa rafiki yake siko nae tena ameanza kunitaka na mimi nampenda sana na napenda awe boyfriend wangu kwani nae hana msichana kwa sasa je Dinah NIMKUBALI huyu mwanaume because I real need a boyfriend au itakua vibaya kwasabau ni rafiki wa my X boyfriend?"


Jawabu:Wanawake wa magharibi wanaamini kuwa sio vema kutoka na mwanaume kutoka kwenye mzunguuko wa rafiki zake na ni mwiko kabisa kutoka na Ex mpenzi wa rafiki yako wa kike, lakini ndio wanaongoza sio kutembea nao bali ni kuwaiba kabisa!. Sasa kuna faida gani kujiwekea miiko wakati wanashindwa kuitekeleza?Huyu bwana hana undugu na Rafiki yake, hivyo kama mnapendana kweli na mnania moja ya kuwa kwenye uhusiano go for it!


Lakini kama huna uhakika na hisia zako za kimapenzi lakini kwa vile unahitaji kuwa nae (kama ulivyosema) "I really need a boyfriend" basi ningekushauri usimkubali kwa sasa na badala yake usubiri kwanza mpaka utakapo kuwa "in love" ili uhusiano uwe extra special n avilevile usije ukaumizwa hisia tena.
Take it slow ili kujenga hisia halisi na za kweli za kimapenzi na kumbuka tu kuwa " You can never need a boyfriend, (they come and go)....you need Education (you will have it for the rest of your life).....we only want them.

Nakutakia kila lililojema.

Wednesday, 26 November 2008

Miaka 5 na mume wa mtu, Familia hamtaki-Ushauri.

"Habari yako da Dinah !!!!

Mi msichana mwenye umri wa miaka 29, sasa nimekuwa na uhusiano na mwanaume wa mtu takriban miaka mitano sasa na kipindi chote tulichowahi kukaa ananijali sana na kunitimizia mahitaji yote ninayohitaji ikiwa ni pamoja na mapenzi ya dhati mpaka ikafika kipindi mkewe akajua lakini baadae mwenyewe akasalimu amri na kutuacha tuendelee na penzi letu.


Sasa dada yangu kinachoniumiza kichwa familia yangu haitaki kumsikia kabisa huyu kaka na tumeshapanga mipango mingi ya kimaisha so niko kwenye "dilema" najiuliza nianzie wapi kwani nilishawahi kumgusia hiyo ishu tukagombana sana na akaishia kusema atakuwa mgeni wa nani kwa sababu mkewe ashamtenga hawajagongonoka miaka yote 5 wala kulala kitanda kimoja toka alipogungua mumewe ana uhusiano nje.


Na mimi pia kwa sasa naona ni mda wangu wa kumpata mume awe wangu peke yangu naomba ushauri wako dada nifanyeje na wadau wa blog hii nisaidieni kwasababu toka nimekuwa na huyu jamaa hajawahi kujitokeza mtu hata kusema nakupenda ya unafiki.


Kazi njema dada Dinah tunashukuru sana kutuelimisha kupita hii blog yako Mungu akubariki."

Jawabu: Aisee nimeshituka lakini nimefurahishwa na uwazi wako, ndio nia na madhumuni ya D'hicious watu kuwa wazi kwani sote tunajua haya mambo yapo na ya natokea, hapa tunasaidiana na kujifunza namna ya kukabiliana nayo kama sio kuyazuia yasitokee kabisa. Safi sana dada.

Unajua kuna mambo mengine unatakiwa kujigeuzia kibao kwanza upate picha ya itakavyokuwa kabla hujaamua kutenda......ingekuwa wewe ndio mkewe na akaamua kutoka na mwanamke mwingine ungefanya nini? ungejisikiaje?


Alafu mwenyewe hapo mwisho umesema kuwa unadhani kuwa sasa ni muda wako wa kuwa na mume wako peke yako, kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa unaamini kuwa kila mke anapaswa kuwa na mume wake peke yake.


Lakini umesahau kuwa huyo mpenzi wako sio wako peke yako na hata akikuoa hatokuwa wako peke yako, hajawahi kuwa wako peke yako na basi hivyo hatokuwa wako peke yako.


Kutembea na Mume wa mtu ni kosa, hata siku moja usijaribu kulala na mume wa mwenzio ukijua kuwa ana mke wake nyumbani. Kumuiba mume wa mtu sio tu kwamba ulimuumiza mwanamke mwenzio na watoto ambao wamezaliwa ndani ndoa yake bali unachangia kwa kiasi kikubwa kufanya watu wasiheshimu ndoa tena.


Familia yako haitaki kumsikia kabisa Mpenzi wako kwa vile wanajua kuwa ni mume wa mtu mwingine, wanakupenda na wasingependa na wewe kwenda kupata matatizo ambayo mke wa huyo jamaa anayapata kwa sababu yako. Yaani wanahofia kuwa Jamaa akikuoa atakuacha na kwenda kutafuta mwanamke mwingine kama alivyokuja kwako.


Huyu bwana ni mnafiki na muongo, kama mkewe kamtenga kwa miaka yote Mitano jiulize kwa nini basi hakumpa Talaka? Hiyo pekee inakuambia kuwa jamaa anampenda mke wake na hayuko tayari kumuacha kwa ajili yako. Hilo moja.


Kitu kingine cha wewe kuzingatia ili kugundua kuwa huyu bwana hana mpango na wewe kama mkewe ni kuwa, kwa kawaida mwanaume aliyetulia kiakili, kimaisha (sio mwanafunzi) hawezi kukaa na wewe kwa muda wa miaka mitano bila kutangaza ndoa.....mwisho ni mwaka mmoja tu....anataliki na kukuoa wewe(kama anamke) na ikiwa hakuwahi kuoa basi inakuwa kama vile kutereza mahali pakavu....pili.


Tatu, inakuwaje awe ametengwa na wanalale vitanda tofauti lakini kila siku anakwenda kulala kwa mkewe? Oh well, anaweza kuzuga tu ili jamii isigundue uchafu wake au wasihisi kuwa yeye na mkwewe wanauhusiano wa ajabu (huenda wameelewana hivyo kwa vile mkewe hawezi kumpa ngono ya kutosha mumewe).


Kama nilivyogusia hapo juu, kuna uwezekano mkubwa kabisa wameelewana kuwa Mume akutumie wewe tu(asibadili wanawake kila leo) kwa ngono kwa vile yeye mkewe hawezi kumpa ngono mumewe kama ambavyo anahitaji.


Sasa ili kukufanya usimuache na kuwa na mwanaume mwingine (kutokana na maelewano na mkewe) hali inayoweza kuwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa VVU......anajitahidi kukupa huduma zote unazohitaji.......usijiamini nakusema alisalim amri kumbe wawili hao wanajua walifanyalo.


Usikute wanapendana sana na wanafanya mapenzi kila wanapohitajiana lakini kwa vile anajua wazi kabisa akikuambia wewe hivyo hutofurahi hivyo ni heri kukuambia kile unachotaka kusikia.....(wanaume wengi husema kile wanawake wanapenda kusikia ili kuepuka mizozo au kuachwa).


Hakuna wakati wa kuwa na mume wala muda wa kuolewa unless unataka kufunda ndoa kwa sababu nyingine na sio mapenzi. Umri wako ni mdogo sana kuhofia muda wa kuolewa (hiyo kuolewa b4 hujafikisha miaka 30 waachieni wenye kuamini kuolewa ni bahati).


Lakini wewe Olewa unapokuwa na mpenzi mmoja (sio mpenzi wa mtu) mnapendana kwa dhati,wote mnania moja ya kuishi maisha yenu yote pamoja na mko tayari kwa wakati huo. Vinginevyo furahia maisha yako kama yanavyokuja.


Nini cha kufanya-Maliza uhusiano na mume huyo wa mwenzio, kufanya hivyo sio mwisho wa maisha yako bali ni mwanzo mpya wa maisha yako. Bado kijana na ninauhakika kabisa utapata mpenzi mpya ambae atakuwa mume wako peke yako.


Tangu umekuwa na uhusiano na mume wa mtu umedai kuwa hakutokea hata mwanaume mmoja aliyekutamkia kuwa anakupenda hata kwa kinafiki, ni kwa vile walikuwa wanakuiba hivyo hakukuwa na sababu ya wao kuji-commite kwako wakati wanajua kwamwe huwezi kuwa wao peke yako........wanaume hawapendi kuchangia, wanapenda kumiliki mwanamke wake peke yake.


Hivyo ukiachana na huyo Mume wa watu, utaona watakavyo miminika. Jitahidi tu kubadilisha mtindo wa maisha yako (soma makala hapo chini).

Kila la kheri.

Tuesday, 25 November 2008

Nimejikuta nampenda, kumbe anawake 2!-Ushauri

"Hi, Dada dinah hujambo mpenzi wangu?
Mie naomba nitafute ushauri kupitia kwa watuma comments nisikie watu na we Dinah unaishaurije hii Kesi?


Nina miaka 38, sina Mume kwa sasa(nimeachika). Kuna mwanamme amenichanganya sana.Tulipokuwawadogo tuliwahi kusoma pamoja na ilitokea tukapendana sana, lakini sikutaka kuwa na mahusiano ya ngono na shukuru hilo lilifanikwa kwani hatuwahi kutombana.


Mwenzangu huyo alibahatika kwenda Masomoni na mimi huku nikaolewa kwani kwa kipindi hicho kwa mila zetu huku hatukuwa tukichaguwa waume bali wazazi ndio waliokuwa wakipanga. Niliishi na Mume wangu vizuri na nilibahatika kupata kazi ya kuajiriwa. Kwa kuwa nilikua mtu wake wa karibu(huyo mwanaume)aliheshimu ndoa yangu.


Kwa bahati mbaya baada ya kurudi kutoka masomoni hakupata Kibarua kwa ulaini hivyo maisha yalimuwia magumu. Mie nikaamua kumsaidia kwakumpatia pesa mpaka pale alipopata kazi.


Akaamua kutafuta mke kitu ambacho aliniarifu na nikampongeza kwa hilo. Akabahatika kwenda masomoni tena kwa muda usiopungua miaka mitano. Akiwa masomoni huku nyuma ndoa yangu ikapata mtihani na kuharibika hivyo nikaachika. Huyu jamaa aliposikia nimeachika , akaanza kurejesha zile za nyuma (uhusiano wa kimapenzi) ingawa bado yuko masomoni.


Kwa kua tulipendana miaka hio na Dini ya kiisilamu inaruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja haikua shida kwangu kumrudisha moyoni kwangu. Sikumpa jibu la moja kwa moja ,lakini, nikajikuta nimerudisha penzi na nimempenda sana, mawasiliano yalikuwa mzuri na hazikupita siku mbili bila Simu, Email, Chat za maneno matamu, I love you N.K ndio usiseme Dada Dinah.


Kwa hivyo nimeingia kikweli kweli na nilikua nasubiri arudi tu nimpe jibu la ndio. Kilichotokea dinah mpenzi, juzi nilikua naongea na rafiki yake wa karibu, natulikuwa tukiongea mambo ya kawaida tu. Yule rafiki yake ndio kuniambia kuwa jamaa (yule mwanaume nimpendae yuko masomoni) ana wake wawili tayari na kila mwanamke anamtoto mmoja.


Nikauliza kaoa lini? Nikaambiwa alienda conference nchi jirani ndio akakutana na huyo mke wa pili na kuoa. Kumpenda nampenda lakini ninamasuala mengi kichwani kuhusu huyu mtu kiasi cha kunichangaya na naomba wanablog wenzangu mnishauri nawe da Dinah.


Kwa nini mwazo wa mazungumzo yetu hakuniambia ana wake wawili? Kama ana moyo wa kuoa wake watau anatamaa huyu, ataongeza na 4 na 5 na hatimae atatupa ukimwi wote.


Nilimuomba dada yangu amuulize jamaa kijanja kama kweli ana wake wawili lakini hakumpa jibu na tokea siku hiyo kakata mawasiliano nami, hapigi simu, wala hachat tena. Mimi nimeamua nisiwasiliane nae, nijitahidi ili niweze kumtoa mawazoni mwangu.


Kwa kweli kipindi hiki nina hali ngumu kimawazo, naomba ushauri kwa yeyote, pale ambapo nimefanya sivyo pia mnikosowe ili nisirudie tena kosa.
Nashukuru sana"

Jawabu: Pole sana rafiki kwa kuumizwa hisia zako, hivi kuna nini kati ya uwazi na wanaume? Hali hii inatisha sana jamani. Wachangiaji wangu wengi hawakuelewa unataka ushauri juu ya nini? Kutokana na majibu yao nimegundua kuwa hawakukuelewa nilivyokuelewa mimi. Sasa nitaweka sawa hapa kidogo ili tuwe kwenye mstari alafu nitakupa ushauri wangu.

Huyu mdada sio kwamba anataka ushauri wa nini cha kufanya baada ya kugundua mpenzi wake alieyempenda kuwa ana mke zaidi ya moja tayari(Hawasiliani nae na anajitahidi kumuondoa moyoni mwake ili amsahau).


Yeye anaomba ushauri kwa kile alichokikosea (wapi kakosea), kama basi alikosea mkosoe na umwambie nini cha kufanya ili asirudie kosa (kama kuna mahali amekosea)......nadhani tuko kwenye mstari mmoja sasa.

Dada yangu mpendwa, kutokana na maelezo yako nimegundua kitu kimoja ambacho kwa mpenzi wako hakikuwa mapenzi bali huruma na "guilt" kutokana na msaada mkubwa uliompatia alipokuwa hana kazi.


Wapi ulikosea-Baada ya ndoa yako kuharibika yeye kama rafiki yako wa karibu alihisi kuwa anajukumu kubwa kukusaidia kwa namna yeyote ile kama ambavyo wewe ulifanya hapo awali.


Baada ya kuachana na mumeo ni wazi kuwa ulifanya uamuzi wa haraka kujiingiza kwenye ushusiano mpya (ni kosa kubwa hilo) kwa vile unapotoka kwenye uhusiano "serious" na wa muda mrefu mara zote unakuwa "Emotionaly vanurable" hivyo mtu akijitokeza na kuonyesha kukutaka/tamani au kukupa "attention" unaanza kujisikia poa na kuanza kujiamini tena kama mwanamke hali inayoweza kusababisha kuanzisha uhusiano na anae kutaka/kupa-attention na kuamini kuwa anakupenda, lakini katika hali halisi sio hivyo.


Sasa kutokana na historia yenu kama wapenzi mlipokuwa wadogo na kubaki marafiki wazuri kwa muda mrefu, ilikuwa rahisi kwako wewe kushawishika na kuamini kuwa kweli unapendwa......ulipaswa kujiuliza hili swali, "nimetoka kwenye ndoa na nilikuwa peke yangu (bila mke mwenza), je ilikuwa sahihi kuingia kwenye ndoa nyingine na kuwa mke wa pili? Kilichosababisha ndoa yangu kufa je hakitokea tena ikiwa nitafunga ndoa tena? Ni muda gani nahitaji kuwa tayari kuingia kwenye uhusiano mpya"?.......bikakabla hujauachia moyo na hisia zako juu ya huyu bwana.


Unapotoka kwenye ndoa au siku zote haishauriwi kuingilia ndoa ya mtu mwingine hata kama unampenda huyo mume au Imani ya Dini yako inaruhusu, hakikisha unajiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi ambao auhusishi mwanamke mwingine.


Kuna vijana wengi tu ambao hawana wapenzi, kuna wanaume wengi ambao wameachwa au kufiwa na wake zao na huwa wanatafuta kupenda tena na kufunga ndoa kwa mara ya pili. Hata kama walizaa na wake zao bado utakuwa hujaingilia uhusiano wa mwanamke mwenzio kwa vile mwanamke huyo hayupo kwenye maisha ya mwanaume husika.


Sio vema kumhukumu kuwa huyu jamaa ni Malaya kwani hatuna uhakika kama analala ovyo na wanawake tofauti kila kukicha na badala yake akipenda anafuata sheria ya Dini yake na kuoa. Ila kwako wewe dada yetu hakuwa na nia hiyo, alikuwa anajaribu kukuliwaza ki-emotionaly kupitia mawasiliano yenu ya Simu, Chat na Emails mara kwa mara na kama nilivyosema alikuwa akihisi "guilt" kutokana na msaada uliompa.


Hakutaka kuliweka wazi kwako kuwa tayari anawake wawili kwa vile hakutaka kukuumiza zaidi hisia zako za kimapenzi juu yake ambazo alikuwa na uhakika kuwa zimejengeka, kutokana na unavyozungumza nae mara kwa mara. Hilo ndio limemfanya aamue kuuchuna kwa vile hana mpango na wewe kama mke wake wa tatu au hata Kimada.


Nini cha kufanya-Chukulia yote yaliyotokea ni ya kawaida na ni mwanzo mzuri wa maisha yako mapya kama mwanamke. Ulikuwa binti wa Baba yako, ukawa mke wa mume wako huu ni wakati wa kuwa wewe kama wewe hivyo basi badili yote uliyokuwa ukiyafanya ulipokuwa mke wa.....na sasa ibua mikakati mipya ya maisha yako.


Kama unaweza basi, hama mahali ulipokuwa ukiishi au badilisha mpangilio wa vitu ndani ya nyumba yako, badili mtindo wa maisha yako kwa kuanza kufanya mazoezi.....hii itakusaidia sana kuondokana na mawazo na wakati huohuo kukufanya uwe "fit".


Badilisha mtindo wa mavazi yako uliyokuwa ukiyavaa ulipokuwa mke wa.....na sasa vaa kama mwanamke yeyote ambae ni kijana, "single", anajua anataka nini maishani na anaejiamini (kama unataka msaada kwenye hili nitafute).


Ibua "hobbie", anza kujichanganya na rafiki zako, ndugu na jamaa kila mwisho wa wiki. Epuka marafiki au ndugu ambao watakuwa na waume/wapenzi wao, hakikisha unasisitiza kuwa unataka mfurahie mwisho wa wiki mkiwa wanawake tu.


Kwa kufanya hayo machache niliyokueleza yatakusaidia sana kuvuka siku hadi siku na hatimae utajikuta mwaka umepita, huna mawazo tena na Ex mume wako wala rafiki, hutojilaumu tena kwa kosa ulilofanya na kubwa kabisa ni kuwa tayari kwa uhusiano mpya.

Kila la kheri.

Monday, 17 November 2008

Hakukua na m'naume maishani mwake, kajenga chuki!-Ushauri
" Kwangu mimi dinah na wadau wote ni kua mimi ni Mwanaume nilikutana na Mwanamke na tukatokea kupendana sana, shida kwake yeye ni kwamba alikwisha athirika Kisaikolojia kutokana na wanaume.


Kwa maelezo yake kwangu ni kua, aliwahi kuwa na Mwanaume hapo awali na alimpenda sana, baadae alikuja kuachwa na huyo Mwanaume kwa ajili ya Mwanamke mwingine ambae alikuwa ni rafiki yake.


Kitu ambacho kilimuumiza sana mpaka kufikia kuwachukia wanamme wote kuwa si watu wa kuwaamini au kuwa nao kwenye mahusiano. Japokuwa hivi sasa tuko pamoja nilipata taabu kubwa ya kumshawishi mpaka akakubali.


Vilevile huyu mpenzi wangu alishuhudia uhusiano mbaya kati ya Mama na Baba yake baada ya baba'ke kumuacha mama'ke alipokuwa mdogo akisoma hivyo amelelewa na mama peke yake mpaka sasa anafanya kazi akiwa bado chini ya mama yake.


Mambo kama hayo anayajumuisha katika kuwachukia wanamme kitu ambacho simlaumu kwani kwa namna moja au nyingine naona yuko sawa. Sasa je? Mtu kama huyu ni kitu gani hasa naweza kufanya kwenye uhusiano wetu ili ile hali ya kisilani na hasira kwa wanamme iweze kumtoka au kupungua?


Kwasababu mim ini binaadamu kama wengine kwamba naweza kukosea, na huwa nakosea wakati mwingine nakua na shughuli nyingi na ninahindwa hata kupata nafasi ya kumpigia Simu au kwenda kwao.


Hayo na mengine yamekua ni makosa yanayonijumuisha kule alikotoka wakati mimi siko hivyo. Matarajio yetu ni kuoana as soon as mungu atapenda kwa vile mimi mambo yangu bado hayajawa sawa sana ndiyo maana sijamuweka tayari na wala sijamwambia ni lini tutaoana.


Hatua za mwanzo tulikwisha pima ukimwi na kuwa tuko safi kwa kua mume na mke lakini kuhusu wazazi bado hatujaliweka jambo hili wazi. Hapo ndipo nauliza ni vipi niwe mwanaume bora/mwema kwa mtu kama huyu ili ajue nampenda na kwamba si lazima samaki mmoja akioza lazima waoze wote!

Nasubiri ushauri wako,wenu washika dau".Jawabu: Hongera sana kwa kuwa na mpenzi muwazi (kukueleza past yake) na vilevile nafurahishwa na nia yako ya kutaka kumuonyesha kuwa wewe ni mwanaume bora na sio kama hao waliopita maishani mwake.Napenda utambue tu kuwa kupima afya zenu ni wajibu (kila mtu anapaswa kupima kabla hajangonoka na mpenzi mpya) na sio hatua za mwanzo ya kwenda kufunga ndoa. Hatua ya mwanzo ya kutaka kufunga ndoa ni kuchumbia (kujitambulisha na kumaliza mambo ya Desturi na Mila kama yapo).


Mpenzi wako (kutokana na maelezo yako) hana kisirani na wanaume na ndio maana yuko na wewe hivi sasa, lakini inaweza ikawa binde litakapokuja suala la kufunga ndoa kwa vile hana imani tena na wanaume hivyo anaweza kuhofia kutokewa na kile kilichomtokea mama yake na kudhani ni heri kuwa na uhusiano ambao unampa uhuru kwa kuondoka atakapoona mambo yanakuwa sio mambo!1-Kitu ambacho unatakiwa kukifanya kwa mtu kama huyo mpenzi wako ni kumuonyesha mapenzi ya kweli na yaliyo wazi, kuwa kwenye mawasiliano muda wote hata kama unashughuli nyingi (busy) haikufanyi ushindwe kumpigia simu au kumtumia ujumbe mfupi (text).

Hakikisha unakuwa wazi na shughuli zako, Mf:-Unapotoka asubuhi kwenda kazini hakikisha unazungumza nae kwanza kabla hujatoka, ikiwezekana utakapofika mahali pa kazi pia sema umefika salama. Kuwa na maongezi ya kutosha kuhusu uhusiano wenu kabla hujaenda kulala hali itakayofanya ubaki kichwani mwake mpaka atakapopitiwa na usingizi.


Unapokuwa na nafasi katikati ya siku m-check anaendeleaje na umueleze hali yako kwa nusu siku hiyo. Kabla hujatoka pia wasiliana nae kuwa unatoka na ukifika nyumbani pia muambie kuwa umefika salama......hii ikiwa tabia yako itamfanya Kisaikolojia akuamini nakuhisi kuwa wewe uko tofauti, unamjali na kumpenda na baada ya muda atakuwa akifanya hivyo kwako.


2-Muambie mara kwa mara ni jinsi gani unampenda au unadhani yeye ni muhimu kiasi gani kwenye maisha yako....pamoja na kusemahivyo epuka kujifananisha na wanaume wengine wenye tabia mbaya ili uonekane wewe bora. Zingatia kuonyesha kwa vitendo wewe ni bora kisai gani na sio kwa kujifananisha na watu wengine kwa maneno tu.


3-Jitahidi kuwa nae kila mnapopata nafasi nakufanya hivyo, zungumza nae kuhusu mambo mengi tofauti hasa mipango yako ya baadae na unapofanya hivyo hakikisha unatumia uwingi kwa maana ya kuwa; badala ya kusema napenda baada ya miaka 3 nijenge nyumba, unasema napenda baada ya miaka mitatu tujenge nyumba n.k.


4-Mhusishe kwenye maamuzi yako, hofu yeyote kuhusu kazi, maisha n.k. hatakama unauhakika kabisa hawezi kukusaidia kimawazo (kutokana na upeo wake mdogo labda) lakini mhusishe hivyo-hivyo na wewe utakuwa na uamuzi wa kuyafanyia kazi maoni yake au kuyaacha palepale.


5-Kama mmejiingiza kwenye kufanya ngono/mapenzi, basi mnapofanya hakikisha wewe unafanya kwa mapenzi yako yote, onyesha jinsi gani una-admire umbo lake, ngozi yake, uzuri wake. Onyesha jinsi gani unashukuru kuwa yeye ni mpenzi wako mama wa watoto wako hapo baadae na kusahau mahitaji yako mpaka utakapokuwa na uhakika kuwa yeye ameridhika ndio sasa uhamishie hisia kwako. Au kwa kawaida anaweza kurudisha yote uliyomfanyia.6-Ikitokea anatatizo/huzuni basi kuwa wa kwanza kuwepo au kuonyesha hali yakutaka kusaidia, hataka kama uwezo wako mdogo wa kusaidia lakini uwepo wako pale ni muhimu zaidi kuliko kuwa na uwezo wa kutatua jambo fulani. Unajua kumjali mtu sio kumpa vitu ambavyo ni "material", uwezo wako wa kumpa matumaini, kuwa ple kuzungumza nae, kumpa ushauri wa nini cha kufanya inatosha kabisa.


Nadhani haya na mengine ya wasomaji wangu yatakusaidia kuwa mwanaume bora kwa mpenzi wako.


Kila la kheri.

Friday, 14 November 2008

Kumbe mpenzi ni Kaka...nimerudi tena-Ushauri!


"Habari dada dinah mimi niyule dada ambaye sikujua kuwa mpenzi wangu ni kaka tatizo lingine limejitokeza, nilikuwa naenda kuoga na simu yangu niliiacha kitandani mara baada ya kutoka kuoga nikakuta dada yangu ameshikilia simu yangu.Dada akaniambia/uliza "yaani we unatembea na Kaka" (tumuite Beka) akaanza kunitukana kwa kuniita "malaya mkubwa wewe hata baba yako mzazi utatembea nae na kuanzia sasa hivi nitakuwa na mchunga hata mume wangu".
Dada dinah nifanyaje? naumia kwa kutukanwa na dada yangu hasa kuniita hivyo, nisaidieni jamani? je nimuache huyo mtoto wa binamu wa mama yangu ambae ni mpenzi wanfu au nifanyaje? "


Jawabu: Pole sana kwa tatizo lingine lililojotokeza hivi sasa, Kuitwa Malaya mbona ni kawaida tu, wala huna haja ya kumia au kuwa na huzuni kutokana na kitu kidogo namna hiyo.Lakini jamani, inakuwaje mtu mwingine achukue simu yako ya mkononi na kusoma msg au hata kupokea simu bila ruhusa yako? Hicho ni kitu binfasi na kinaweza kuwa na mambo mengi binafsi ambayo hayapaswi kuonwa, sikiwa, somwa na mtu mwingine unless ni mpenzi wako.Baada ya ushauri uliotolewa hapa umeufanyia kazi au unaendelea kuufanyia kazi? Kama ungeufanyia kazi mapema hili suala la dada'ko kukutukana lisingekuwepo au lisingejitokeza. Mpenzi "Kaka" anasema nini kuhusu uhusiano wenu?Wakati mwingine mwanadamu unapaswa kuwa a little bit selfish na kutojali kwa sana hawa ndugu ambao hivi sasa kila mtu anaendesha maisha yake kivyake. Dada yako anamaisha yake na mume wake na anapaswa ku-focus huko, Mama yako anamaisha yake na mume wake ambae ni baba'ko na anapaswa ku-focus huko na wewe una maisha yako kama binti mdogo lakini unataka kuwa na maisha yako kama wao kwa kuungana na mtu mwingine ambae mnapendana na atakuwa baba wa watoto wako na unapaswa ku-focus huko.Pamoja na kusema hivyo sina maana kuwa uwadharau, hapana. Endelea kuwaheshimu, sikiliza ushauri wao na fanya maamuzi ya kuyafanyia kazi au kuyaacha pale pale kama yalivyowakilishwa kwako.Ulisema kuwa wewe na mpenzi wako mnakwenda kufunga ndoa(Ikiwa nakumbuka vema, nitaangalia). Kama kweli mnapendana na mnania moja na huyo Ndugu yako wa jina (sio wa damu) basi kuweni "serious" na fungeni ndoa (sio lazima iwe kubwa na kushirikisha kila mtu, mnaweza kufanya ya kiserikali ili wewe na yeye kuishi pamoja na kihalali kama mke na mume) ili kumaliza kesi.
Fanya uamuzi wa busara kwa kuzingatia nani ni muhimu kwenye maisha yako kama mwanamke, mama ambae anamaisha yake? dada ambae anamaisha yake? au Mume wako ambae mnapendana na mnakwenda kuwa na maisha yenu pamoja?Vinginevyo matatizo yatazidi kujitokeza juu ya matatizo mengine ambayo ukiyafuatilia kwa karibu utagundua ni kupotezeana mida tu.


Kila lililo jema!

Tuesday, 11 November 2008

Kubemenda mtoto ni Imani tu au kuna Ukweli?

Ni matumaini yangu kuwa unakumbuka ile somo kuhusu kufanya ngono baada ya kuzaa/jifungua kiasili, nilipokea maswali mengi kuhusu Kubemenda mtoto ambayo niliayajibu kwa kirefu kupitia Kipindi changu Radioni. Lakini kwa faida ya wale ambao hawakubahatik akunisikia basi karibus ana.

Unaweza kunipa maana ghalisi ya neno Kubemenda?

Nijuavyo mimi au nisema kama nilivyokuwa nikisikia, kubembenda mtoto ni kitendo cha baba na mama wa mtoto huyo kufanya mapenzi/ngono na watu tofauti kabla mtoto hajakua vya kutosha au hajatoka Arobaini. Inasemekama ktk kipindi hicho mama akifanya mapenzi basi mtoto anapata matatizo kiafya.

Matatizo yenyewe hujitokeza mtoto anapofikia umri wa kuanz akuropoka maneno, kutembea, kujaribu kusimama n.k. kwa kawaida ni kati ya miezi 6 na nane kwa watoto wengi lakini wengine huwahi au kuchelewa zaidi.

Matatizo hayo ambayo kama vile kuchelewa kufanya/anza hatu ahizo za mwanzo za ukuaji wake, mtoto anakuwa kama vile anautindio wa akili, anatokwa na udenda ovyo....yaani anakuwa mlemavu.

Endelea kuwepo basi........pia nitakupa maelezo muhimu yahusuyo ngono ya mdomo. Una nyege mpaka kwenye kope na mume anataka mpaka anatetemeka kama sio kulia lakini uke ndio uko"sore" unaamu kumpa mdomo na yeye akupe mdomo......si ndio? Nini kinafuata baada ya hapo basi?

Naja.....

Monday, 10 November 2008

Kuzuia mimba kiasili-Ushauri

"Samahani dinah mie kidogo niko nje ya mada ningeomba sana unifahamishe jinsi ya kuzuia mimba kwa njia ya kalenda kwani nimechoka kutumia midonge jamani tafadhali nifahamishe mpenzi ndugu yangu.
Yaani huwezi amini kitendo cha kuwa na mpenzi wangu kinanifanya niumwe kwa kufikiria mimba tu. Nimekua muoga mchezo nautaka ila tatizo kuingia kwa mimba hivyo basi nakuomba chonde chonde unifafanulie jinsi ya kuzuia kwa kutumia tarehe tafadhali naomba."


Jawabu: Asante kwa uvumilivu wako pia kwa ushirikiano wa kuuliza swali lako mahali hapa. Njia ya asili ya kuzuia mimba ni mbinu pekee ambayo wanamama wa miaka ile kabla ya madawa ya kisasa(kizungu) kugunduliwa. Njia hii inauhakika wa asilimia 96-mpaka 98 kama zilivyo njia nyingine za kuzuia mimba kama vile vidonge, sindano, patch, Coil. Njia nyingine asilia ni kumwaga nje (withdrawn), lakini hii unahitaji zaidi ushirikaino wa mpenzi wako, mawasiliano wakati wa tendo kwani akijisahau au kuchelewa ujue kitu na box.


Mipira (Condoms) ndio kinga pekee inayozuia mimba na magonjwa yote ya ngono kwa asilimia 99 na ile moja iliyobaki ni kwa ajili ya sababu za kisheria kulinda Makampuni incase mtu akatumia vibaya na kushika mimba au gonjwa la zinaa. Vilevile Kinga hii (Condom) ndio pekee ambayo ham-badilishi mwanamke kihomono au kimaumbile.Njia ya asili ya kuzuia mimba hutumiwa na wanawake ambao kwa namna moja au nyingine hawataki kutumia madawa ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya miili yao kama vile kunenepa, kutokwa na majimaji ukeni na pia kuna tetesi kuwa yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata Saratani ya Kizazi na Matiti.


Kuzuia mimba kwa kutumia tarehe inauhakika ikiwa mzunguuko wako ni uleule na sio mrefu (siku 32-35) wala mfupi (siku 18-24) bali ni ule wa kawaida ambao ni siku 28. Ili kutumia mtindo/mbinu hii ya kuzuia mimba unapaswa kuanza kuhesabu siku zako sasa na fuatilia kwa karibu mzunguuko wako na kuhakikisha kuwa una siku 28 sio chini wala juu ya hapo, kwa kawaida unaaza akufuatilia kwa miezi mitatu hadi sita (kama umewahi kutumia madawa ya kuzuia mimba) kabla hujaanza kuitumia njia hii.


Namna ya kuhesabu nitumiayo mimi-Ili kuwa na uhakika na urefu au ufupi wa mzunguuko wako unapaswa kuhesabu siku ya kwanza utakayo ona damu mpaka utakapo ona damu ya mwezi utakao fuata.

Mfn; leo tarehe 12 mwezi wa kumi na moja ndio umeanza hedhi basi hedhi ya mwezi ujao itakuwa tarehe 10 mwezi wa kumi na mbili.....hii ni kama mzunguuko wako usiobadilika (sio mrefu au mfupi) ambao ni siku ishirini na nane tu.Siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya tisa ni salama na huwezi kushika mimba, baada ya hapo mpaka siku ya kumi na nne (yai linapevuka) unakuwa hatarini, siku ya kumi na saba mpaka siku ya ishirini na mbili unakuwa salama tena mpaka siku ya ishirini na tatu mpaka ishirini na saba (yai pevu linashuka) hatarini lakini ile ya ishirini na nane siku ya hedhi nyingine unakuwa salama tena......comfusing ei?
Ili kuwa na uhakika kuwa uko kwenye mstari kuliko kuegemea kwenye tarehe tu unatakiwa kujua mabadiliko ya mwili wako. Unapokuwa hatarini kushika mimba mara nyingi utahisi nyege zaidi n avilevile utoko wako utabadilika na kuwa mlaini zaidi (kama lotion) na wakati mwingine utahisi ute unatoka (ule kama udenda/mlenda)....ukiona hivyo hakikisha unatumia Condom vinginevyo utashika mimba.
Unapokuwa salama mara nyingi hamu ya kungonoka inakuwa haipo sana unless "uchokozwe", vilevile utoko wako unakuwa mzito (kama cream/mafuta mazito)na mweupe sana yaani hata wakati wa kujiswafi inakuwa taabu na inaweza kukuchukua muda mrefu zaidi. Hali ikiwa hivi ujue uko salama kungonoka bila kinga ya kuzuia mimba.

Kila la kheri!

Friday, 7 November 2008

Unataka kuolewa in 2 yrs time? Hii ndio nafasi yako.


Kwa kawaida D'hicious huwa sifanyi haya mambo ya kutangaza lakini kutokana na maelezo ya huyu bwana kuna mawili matatu ambayo tutajifunza (ndio lengo la D'hicious) na ningependa kuyazungumzia siku zijazo, kwa sasa msome na kamilisha ndoto yake kwa kuwasiliana nae.
Tangazo hili litakuwa hapa kwa masaa machache tu kisha nitalipeleka kwa Mwakilanga ambae ana-deal na matangazo ya uchumba zaidi. Asante kwa ushirikiano.

"Hi dada Dinah! Kwanza kabisa nakusalimu sana na pole kwa kazi yako ngumu na yenye msaada mkubwa kwa jamii.Dada mimi nina ombi kwako. Naomba niitumie site/blog yako kuweka tangazo langu ambalo nadhani labda litakuwa tofauti na matakwa ya wengi kama ilivyokawaida yake.

Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 34 na niko Marekani kwa miaka 7 nikifakamia elimu na kuandaa maisha yangu vilivyo. Natafuta rafiki msichana ambaye natarajia kuweka uchumba baada ya kufahamiana na kuelewana vizuri na kuoana ndani ya miaka si zaidi ya miwili ijayo.

Nimekaa hapa US muda wote nikila shule na nimekutana na wasichana wengi wa kibongo,lakini bahati mbaya sijaridhika na yeyote kutokana na sababu mbalimbali. Na ieleweke hapa kwamba sijafanya urafiki na yeyote kwa kuogopa mambo kadhaa ambayo sitayataja hapa, yaani sijaona mwenye sifa ya kuwa mke wangu.

Hivyo nimeamua kurudi nyumbani.Mambo yafuatayo ni muhimu kuyazingatia kwa yeyote atakayekuwa tayari kuanza mawasiliano nami:a. Awe mkristo mwaminifu ambaye nafasi yake ya kwanza amempa Mungu katika yote mema ayafanyayo.

a)-Haidhuru ni dini gani ya kikristo anatoka, bali awe tayari kubadili dini yake mara tutakapoivana kuwa Mlutheri kwani mimi ni muumini wa Lutheran.

b)- Awe na Elimu kuanzia kidato cha nne hadi juu na mwenye nia ya kuendelezwa ili afikie kiwango kizuri cha elimu inayokubalika kitaifa na kimataifa(Digrri ya kwanza) na mimi niko tayari kumgharimia.

c)-Awe tayari kwenda nami shambani kwani nina shamba kule Chanika ambalo nataka kuwekeza mifugo mara nitakaporudi huko baada ya miaka mitatu ijayo.Hivyo nikimleta US asipende kubaki hapa, kwani mimi nategemea kufundisha pale mlimani au Mzumbe ili kuijenga nchi yangu.

d)-Awe na heshima, na mwenye kusikiliza memngi lakini yeye aseme machache yenye maana.Sijali kabila, mimi natokea Mbeya.

e)-Awe mtu wa mawasiliano sana na muwazi katika mambo mengi.

f)-Asiwe na umri zaidi ya miaka 34. Pia awe hajawahi kuolewa au kuzaa kabla ya ndoa.

Dada Dinah hayo ndiyo yenye umuhimu kwangu. Naomba kwa yeyote atakayekuwa tayri kuwasiliana nami atume barua pepe kwa anwani hii : abosili@yahoo.com.

Nitashukuru sana iwapo utanikubalia kuniwekea ombi langu kwenye blog yako hii muhimu.Unisamehe kama nitakuwa kwa aina yeyote nime-abuse the proper use of your blog.

Please bear in your mind that I am serious with this issue, so take care of me!! Mungu akubariki sana kuendelea kutoa ushauri wako nasaha kwa jamii yenye dharura na nyufa nyingi za kimaisha."

Tafadhali kuwa mstaarabu kwa kaka Abosili. Asante.

Monday, 3 November 2008

Aruka hedhi, nikioa tutapata mtoto?-Ushauri

"Dada Dinah ur a great hero in all about sex education and health in general, Kwa kweli mimi nataka kukuuliza hili kuhusiana na huyu girlfriend wangu niliye naye. Ni kweli nampenda na nilianza naye akiwa bikira kiasi nimeamua kama mungu akipenda tuoane naye na nimeanza kumtambulisha kwa baadhi ya ndugu zangu.

Dada dinah nisaidie mwenzio cz huyu girlfriend wangu ana tatizo la kuruka hedhi zake ila ya mwisho imeniacha na mawazo mengi mpaka sasa maana siku ya mwisho amepata period ni mwezi wa saba mwaka huu mpaka sasa tumesubiria lakini hatujaona dalili zozote naogapa mpaka nikampeleka mwenyewe kupima mimba lakini hamna maana nilihofu ana mimba lakini wapi.

Sasa nikamshauri aende kwa Daktari anasema amemuulizia rafiki yake amemwambia huwa inatokea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa stress na n.k lakini naona imezidi na ananipa wakati mgumu kwani sijui ni kwa nini iwe ivyo maana nataka kumuoa ila kama ndo ivi tutaweza kupata mtoto kama mungu atatusaidia kuoana naye? Naomba msaada wako wa kina dada pls tusaidie wana jamii.
Mdau, Kahama. "

Jawabu: Kukosa hedhi kunaweza kusababishwa na vitu mbalimbali pamoja na hali ya hewa ambayo inaweza kuhoroganya/kanganya Homono, mahangaiko ya akili yanayosababishwa na maisha(stress) pia inaweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi.

Ni kweli kabisa kuwa "stress" na hali ya hewa inaweza kuwa sababu. Kama mpenzi wako amehamia huko mliko hivi sasa for the past 12months basi mmpe muda ili mwili wake uzoee.

Ikiwa mpenzi wako anatumia madawa ya kuzuia mimba hakika anaweza kuwa anaruka sana siku zake, kuna baadhi hupata Hedhi mara tatu kwa mwaka, wengine mara nne nakadhalika inategemea aina gani ya kinga ya mimba unatumia.


Kwa vile mpenzi wako anapata damu yake mara fulani fulani sio kwamba anakosa kabisa ana kwa mwaka anakwenda mara tatu basi sidhani kama anaweza kupata matatizo ya kushikamimba ya hatimae kujifungua.


Suala muhimu kwake na kwako wewe ni kufuatilia terehe zake kila mwenzi hasa miezi ile ambayo anaona damu yake(hedhi). Mtakapo funga ndoa na mkaamua kuwa ni wakati muafaka wa kujaribu kwa ajili ya mtoto (kushika mimba) basi mfanye hivyo kwenye zile siku ambazo yai liko tayari kurutubishwa yaani limepevuka na linasubiri kushuka.


Ili kujua siku hizo mpenzi wako anaweza akatumia kalenda(tarehe) na vilevile anaweza kutumia njia za kiasili kama vile kuangalia na kufuatilia mabadiliko ya mwili wake.

Nitakueleza mabadiliko hayo ya mwili mara baada ya masaa machache.....

Bofya hapa kusoma maelezo ambayo ni majibu ya swali kuhusu kuruka hedhi