Thursday, 31 July 2008

Siwezi kula mboga 1 kila siku!

Natambua kuwa sio mara yako ya kwanza kusikia hii sentensi "utakulaje mchicha kila siku, lazima ubadili mboga" kutoka kwa wanaume.

Huu msemo sasa umebadilika na kuwa imani kama sio kasumba,kwamba watu wanaamini kuwa hiyo ni kweli na wengine wanakbali kuwa kwa kufanya hivyo kunakufanya ujiongezee hamu yako ya kula.

Kwa bahati mbaya sehemu fulani ya jamii inalihusisha hili swala la "mboga moja kila siku" na mahusiano yako ya kimapenzi kitu ambacho wanajua kuwa i vitu viwili tofauti.

Ili kujiongezea hamu zaidi ya kufurahia au kufanya mapenzi huitaji kubadili mwili wa mwanamke bali wewe unaehisi kukifiwakinai unapaswa kuliweka wazi hilo na kutafuta mbinu za kuboresha (ongeza chachandu) ili hamu ya kufanya iongezeke.

Nikiliweka hili kwenye "mboga" Mf leo umekuwa na hamu ya kula samaki wa kuchemsha (chukuchuku) ukamla naukafurahia kabisa,kesho hutokuwa na hamu ya kumla samaki huyo kama alivyo huenda ukawa umekinai hivyo badala ya kumtupa utajitahidi kuongeza viungo na kumuunga vema hali itakayofanya mboga yako (samaki yuleyule) kukuongezea hamu ya kula au kunoga kama sio kuwa mtamu zaidi.

Wanaume wengi wenye kuamini msemo huu utakuta ni wavivu au mbumbu (hawajui kujituma/sio wabunifu) wanasubiri kufanyiwa kila kitu na wanawake.

Sasa kama mpenzi (mwanamke) yeye zake ni kujituma kila siku kukufurahisha na kukuridhisha na wakati huohuo ajifurahishe yeye......kuna wakati utafika mwanamke unachoka au kukatishwa tamaa na hivyo unaamua "kuegesha" kama sio kusubiri mpaka utakapokuwa na nyege asilia (sio zile za kunyegeshwa).

Napenda utambue kuwa utamu wa ngono (mboga) unatofautiana kutokana na mitindo, mikao, "mood", wakati, mahali, ufanyaji, kujituma kwenu, nia yenu kwa wati huo!

Vilevile utamu haulingani,kwamba utamu wa bao la kwanza sio kama la tatu, bao la subuhi ni tofauti kabisa na lile la usiku/jioni na mabao ya leo hayatolingana na ya kesho.

Ilikujua zaidi na jinsi ya kupata utamu wa mboga tofauti kwenye chungu kimoja, katiza hapa kesho tafadhali.

Mida-mida.

Thursday, 24 July 2008

Hata nikingonoka lazima nijichue-Ushauri!

"Dinah,Naisifu kazi yako. Na mie ninaomba ushauri:Mimi ni mama wa watoto wawili, na nimeolewa ninaishi na mume wangu. Nilianza tabia ya kujichua kabla hata sijabikiriwa - though wakati huo nilikua naishia juu juu tu. (bikra ilikutwa hah hh ahahaha)!

Sasa huwezi amini mpaka leo hii bado naendelea na katabia haka, saa nyingine nikitoka tu kungonoka na mume wangu naingia bafuni kumalizia. Nimejaribu kumweleza baba watoto kwa maneno, vitendo kwamba a-prolong kamchezo tuwe tunafika wote lakini wapi.Most of the time nikishakua peke yangu tu, shughuli inaanza na raha ninayoipata its beyond explanation though ninaenjoy kungonoka pia.Je kuna abnomarlity yeyote hapo"

*****Ili kuondoa utata kabla hujachangia msomaji wangu mpenzi, bikira ni kutokuguswa kabisa na mwanaume/mwanamke, sio wote wanaokuwa na kile "kijiutandu" siku ya kuingiziwa/ingiliwa kwa mara ya kwanza.

Asante!

Wednesday, 23 July 2008

Anazuia nisicheze na "vipele" vya raha-Ushauri!

Habari yako Dinah? Mimi nina tatizo nataka kushare nawe pamoja na watu wote wanaotembelea dinahicious. Nina gf(she have 23yr) ambaye nakili nampenda sana na naamini naye ananpenda pia.

Tatizo linakuja tukiwa kwenye tendo letu tukufu huwa hataki nim-busu (kunyonya,kulamba nk) ktk sehemu zile ambazo nahisi atanyegeka(masikioni,shingoni kwenye 'k'nk),sehem ambayo naweza fanya nitakacho ni kwenye matiti lakini kwingine kote anasema ninamtekenya.

Hii inanipaga wakati mgumu kwani inasababisha most of time yeye kuskia maumivu kutokana na kutonyevuka vizuri. Jana (14jul) ilibidi nifanye kazi ya ziada hadi kuifikia 'k'yake na kumbusu vya kutosha alifurahi sana na to be honest ndio ilkuwa siku ya kwanza kumsikia akiimba mziki wa mapenzi tukiwa kitandani.

Nilienjoy sana kuona amekuasatisfied(na aliniambia kuwa nimempa raha kuliko siku zote),nilpotaka kurudia tena baada ya break alikataa kabisa nakudai eti amechafuka.

Nataka awe anajisikia hivyo kila tunapo-make love,naomba ushauri wako nifanye nini ili niweze kumpa raha?.NB:Hanionei aibu kwani huwa namnyoa na yeye pia ananinyoa.

Apendaye kwa dhati.

Monday, 21 July 2008

Guna,piga kelele,hangaika,lia, tomasa,,zungumza wakati wa kungonoka!

Natambua kuwa sote huwa tunatoa sauti fulani wakati wa kufanya mapenzi/ngono japokuwa inategemea zaidi na raha uipatayo mpaka kufikia utamu wenyewe. Sauti, kelele, miguno, mihemo (kuhema), kuhangaika (yaweza kuwa ni kukata kiuno au huku na huku), kutomasa huwa kunatofautiana kufuatia hatua mnayoifikia na kiwango cha raha kuelekea utamu wa kungonoana.

Hayo yote kwa ujumla huwa naita kupeana matumaini/moyo ili kila mmoja wenu atamue kuwa anachokifanya ni sahihi na hivyo kuongeza juhudi kukupa utamu "tu ze makisimamu".

Ukifanya mapenzi (ngonoana) na mtu ambae anatulia tu na kusikilizia hakika inaudhi/katisha tamaa na wakati mwingine hukupotezea ule mshawasha wa kuendelea kufanya mambo yako kwani mwenzio yeye anakuwa "kaegesha tu" alafu wewe ndio wajituma kuliko kiwango lakini Jitu wala halionyeshi lina-furahia au kuumia basi ili ujue umekosea......hehehehehe

Nakuja.......

Saturday, 19 July 2008

Tangu nimeachana na wangu, sitaki Demu-Ushauri!

"Eti dinah wewe ni profesheno kwenye mambo ya LOVE???mi namatatizo kichizi ya kisaikolojia ,Tangu niachane na chick wangu feb 2007 mpaka leo sitaki demu na wala sijisikii kabisa kuwa na uhusiano vipi ninamatatizo gani???

Aalafu kwa nini simpati demu mwenye sifa ninazotaka?? best wishes"

Jawabu:Shukurani kwa kukubali ku-share tatizo lako hapa kwa faida ya watu wengine wenye tatizo kama lako au ambao watakumbana nalo hapo baadae.

Sidhani kama unatatizo, hiyo ni hali ya kwaida inatupata watu wote tunapoachana na wapenzi wetu ambao tulikuwa tukiwapenda sana au tumekuwa nao kwa muda mrefu. Inakuchukua muda mrefu kabla hujaondokana na hilo yaani kwa kifupi ni kuwa alikuumiza sana au uliumia sana kumaliza/ua uhusiano hali inayokufanya upoteze imani na wanawake kwa ujumla ukihofia wao kuwa kama yeye at the end. Japo kuwa sio kweli kwani wanawake tunatofautiana. Hivyo all u need is time to heal jeraha lako.


Sio rahisi kupata mwanamke mwenye sifa zote uzitakazo kwani huyo atakuwa "perfect" na "there is no such thing" hapa duniani, kwani hata Malaika hawako hivyo. Ukiwa tayari kupenda tena au kuwa kwenye uhusiano basi fuata moyo wako lakini suisahau akili yako.

Jiwekee sifa utakazo kwa mwanamke lakini ikiwa utamdondokea mmoja ambae ana-tick box 5 muhimu out of 10 mchukue nyingine utarekebisha ukiwa ndani ya uhisiano. Kitu muhimu cha kuzingatia sio sifa alizonazo bali hisia zako za kimapenzi juu yake na je utakuwa mtu mwenye furaha ukiwa nae karibu?

Sasa take your time to get over kilichotokea alafu ukiwa sawa/tayari mambo yatakuwa bomba kuliko ilivyo kuwa na EX, kumbuka kwenda taratibu, kuwa wazi na boresha mawasiliano ili ikusaidie kumfahamu mwenzio zaidi.

I hope nimekujibu vema na umenielewa.

Nitumie nini kuondoa michirizi ya Uzazi?

"Dinah dada nakukubali! Mimi nina shida naomba ushauri ikibidi kutatua tatizo langu. Mimi nina tatizo la michirizi iliyotokana na uzazi nina kitoto kimoja ila mwili wangu matakoni na hipsi kama kenge.

Sasa nilikuwa nauliza je hii michirizi itatoka? na ninunue kitu gani itoke maana nimeshakwenda maduka mbali mbali (jina kapuni) hamna kitu.Naomba ushauri wako/wenu nifanyeje ndoa yangu ipo mashakani? Nisaidie naomba saaaaana?"

Jawabu: Asante sana kwa kunikubali na pia kwa kuchangia swali lako mahali hapa. Nasikitika kusema kuwa michirizi (stretch marks) haitoki bali inapungua tu kwa kutumia bidhaa zilizotengenezwa maalumu kabisa kwa ajili hiyo.

Pamoja na kusema hivyo inasemekana kuwa kuna dawa za kuzuia na kuondioa kabisa alama hizo juu ya ngozi ambazo baadhi ya wanaume huziita "mistari ya utamu" lakini dawa hizo hazijathibitishwa kisayansi kitu kitakachonifanya niseme kuwa hakuna dawa ya uhakika ya kuzuia na kuondoa kabisha michirizi.

Michirizi hiyo hujitokeza kwa mwanamke yeyote (wengi wetu tunayo) sehemu mbali mbali za miili yetu kama vile kwenye matiti, matakoni, sehemu ya kwapa/chini ya mkono, mapajani, sehemu ya nyumba ya miguu na kinachosababisha hili kutokea na kutanuka kwa ngozi yako sehemu husika (mahali ilipo).

Michirizi hii pia huwapata zaidi mama wajawazito au wazazi na hilo hutokana na kutanuka kwa ngozi yako sehemu hiyo ya tumbo na meneo ya karibu kama vile kiunoni, n.k.

Natambua hofu ya ndoa yako kuwa hatarini kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wako baada ya kujifungua kwa vile mistari hiyo (mabadiliko ya mwili wako) inaweza au inakusababishia ujisikie huvutii tena kama zamani au "ukajishitukia" kuwa mumeo havutiwi na wewe tena hali itakayokufanya umkimbie au uanze "vijitabia vya ajabu" kamavile kufanya mapenzi gizani, kwenda kubadilishai nguo mahali ambapo yeye hayupo, kulala na nguo zako, kufanya mapenzi ukiwa "full dressed" nakadhalika yaani kwa kifupi inakupunguzia ile hali ya kujiamini ukiwa mtupu(uchi) mbele ya mpenzi wako.

Mimi nauhakika kabisa kuwa mumeo hatosumbuliwa au kuwa "put off" na hizo alama ikiwa wewe bado ni yuleyule na unafanya mambo yako fulani kama awalia au ukaongeza ujuzi kidogo ili kufurahia zaidi.

Unachotakiwa kufanya ni kujirudishia tena ile hali ya kujiamini kwa kufanya mazoezi ili ku-shape up, kula na kunywa vizuri ili ngozi inawiri, badili mtindo wa mavazi......kwamba, kama ulikuwa mtu wa khanga mbili sasa pia moja, kama ulikuwa mtu wa khanga moja sasa piga gauni bila khanga au sketi na blauzi nakama ulikuwa mtu wa magauni basi sasa wewe anza kupiga suruali na kaptura, hali kadhalika unaweza kupia mini.


Yaani badili muonekano wako kwa ujumla na usijisahau ukawa mama nanihii, bali kuwa wewe na wakati huohuo mama wa mtoto wako sio MAMA FULANI( hili linaathiri wanawake kisaikolojia na kimwili pia).

Ikiwa unashindwa kuwa huru mbele ya mume wako hata baada ya kufanya nilivyokuambia basi ni wakati wa kuifanyia kazi Nguzo ya tano ya uhusiano bora ambayo ni mawasiliano, weka wazi hofu yako. Muulize mabadiliko gani anayaona juu ya ngozi yako tangu umejifungua? Akisema machirizi muulize je michirizi yako inamkera?

Asipo gusia michirizi kama sehemu ya mabadiliko juu ya ngozi yako basi ujue jamaa hana habari na anakupenda pia anafurahia kama ilivyokuwa awali.

Kila la kheri mdada!

Wednesday, 16 July 2008

Namna 5 za kumshukia Mwanaume!

Habari za wakati kama huu, ninafuraha sana kurudi hapa baada ya kuwa likizo ndefu kuliko zote nilizowahi kuwa nazo ktk maisha yangu. Nilikuwa na wakati mzuri sana na nilifurahia kila sekunde ya kuwepo kwangu kule nilikokwenda na shukurani zimuendee mwenyeji wangu......I know Too Much Info, najaribu kuboresha mawasiliano na wewe msomaji wangu. Au?

Unakumbuka ktk Makala zilizopita niliwahi kuzungumzia namna ya "kumshukia" mwanamke hali kadhalika nilitoa maelezo ya "kumshukia" mwanaume. Tofauti ni kwamba kwa upande wa wanawake niliweka mitindo tofauti ya unyonyaji, sasa leo nitakupa namana tano za unyonyaji wa uume ili kumpa mpenzi wako raha ambayo hujawahi kumpatia.

Anza kuushughulikia uume kama nilivyokufundisha (rejea topic ya "jinsi ya kunyonya uume") au vile ujuavyo wewe ila leo mpe ile mimi huwa naita "60minutes suck" ambayo inajumuisha aina tano za unyonyaji na unazifanya zote kwa wakati mmoja bila yeye mpenzi wako kulijua hilo.

Inaweza kukuchukua kati ya dakika 10-45 au saa nzima inategemea na wewe kama unachoka haraka au yeye mwanaume kwani kuna wanaume wengine hawa "cheki" mapema na kuna wengine ndio vile tena, ukiweka mdomo tu meno nje(kamwaga).

1-Mpatie ile ya taratibu ambayo unanyonya mwanzo mpaka mwisho (kichwani mpaka mwisho au karibu na mwisho manake wengine wamezidishiwa) usije ukajijeruhi bure.

2-Bila kutoka/pumzika unganisha ile ya muda mrefu ambapo uume unakaa ndani ya mdomo kwa muda zaidi, kwamba unaenda juu-chini haraka na kwa kukaza misuli ya mdomo kama mara tatu hivi alafu unabaki huko chini (uume ukiwa full mdomoni) kabla hujarudi juu nakuanza kucheza na kichwa kwa kutimia ulimi na midomo yako ya nje(lips).

Rudia kitendo hiki mara tano na hakikisha uume hauna mate kwamba usiachie mate mwengi yatapakae kwenye uume na kwenye pumbu au maeneoya karibu, inakuwa tamu zaidi kwake kwa sasa kama itakuwa kavu. Ofcoz unyevu utakuwepo kwa vile unatumia mdomo lakini hakikisha unameza kimiminika chako.

3-Hupaswi kutoka na sasa mpe nyevu (achia mate/kimiminika chako), lakini hapa unatakiwa kuitoa ngazi kwa ngazi au hatua kwa hatua kwamba baada ya hatua ya pili jirudishe juu(kichwani) kisha toka kabisa na sasa anza kulamba na kuuma shina la uume kwa kutumia midomo yako ya nje, zunguuka na kuhakikisha kila sehemu ya shina umeigusa.

Sasa ingiza kichwa na baki kichwani hapo na kuchezesha ulimi wako, shuka kidogo chini zaidi ya kichwa na shingo ya uume nabaki hapo kwa sekunda fulani, alafu enelea kushuka na kutulia kwa muda mpaka unafika mwisho wa uume au karibu na mwisho (inategemea na urefu) utahisi kichwa kimefika kwenye Koromeo hilo likitokea wewe rudi juu mpaka kichwani bila kupumzika mahali alafu anza tena.

Rudia hii kama mara tatu mpaka tano.....kabla hujaunganisha aina ya nne ambayo nitakuambia baadae.

Ikiwa unachoka mara kwa mara wakati wa safari hii ndefu (ofcoz midomo na ulimi huwa vinachoka) unaweza ukawa unaumzika kwa kubaki kichwani au kulamba-lamba lile shina na kumshika maeneo mengine ya mwili wake kama juu ya uume pale kwenye nywele, kwapani, shingoni, chuchu zake n.k (inategemea na vipele vya mume/mpenzio vilipo).

Kamwe usijitoe kabisa kwani utampoteza raha ya maisha uliomuanzishia.

Nakuja........endelea kuwepo!

Saturday, 12 July 2008

Huku ndio Kufika kileleni?-Ushauri!

"DINAH,nimetafuta sana email yako nimekosa,sijui umeiweka kwa wapi hapa, Naomba wadau WA BLOG HII MNISAIDIE. MIE NI MKUBWA BINTI WA MIAKA 27, LAKINI TOKA NIANZE KUFANYA MAPENZI SIJAWAHI KUPIZI.

NIMEPATA MPENZI MPYA YEYE UWA ANANICHEZEA SANA CHINI YAANI KUNIBUSU HADI NASIKIA KUTETEMEKA KWA RAHA, SASA UWA NAFIKIRI NATAKA KUPIZI LAKINI NASHINDWA KUJIZUIA NAMWAMBIA ANIACHE MAANA HATA NGUVU UWA ZINANIISHIA.

JE HUKO NDIO KUPIZI AU NIMWACHIE AENDEE MPAKA MWISHO? WAKATI MWINGINE HUWA NADHANI LABDA NIMEUBWA HIVI KWAMBA SIWEZI KUPIZI, NISAIDIENI NIFANYEJE NA MIMI NIIPATE RAHA HII AMBAYO WENZANGU WANAIPATA,PLEAZE HELP"

Thursday, 10 July 2008

Uke kukauka wakati wa kungonoka-Ushauri!

"Dada Dinah mbona hii blog yako haina sehemu ya kukucontact wewe, sijui e-mail yako ndio maana naandika swali langu hapa.Mimi jana nilifanya sex na binti fulani wa kizungu. It was first time to have sex na white woman, As usual nilitumia condom.

Nilifanya naye romance kama 2 hours kabla ya kumwingizia mboo. Alinyevuka sana kwenye K hadi vidole vyangu vililowana. She really enjoyed mambos yangu. Kama kawaida bao la kwanza lilikuja in few minutes. Nikachange condom faster, mboo ilikuwa bado iko high, nikaivaa condom ya pili ili nitafute bao la pili.

Tuliendelea, yeye akacum, mimi nikawa bado. Nikaandelea kumpa vitu. Mimi asili yangu huwa bao la pili linachukua zaidi ya nusu saa kutoka. Hivyo basi nilimsugua sana hadi nadhani fluid kwenye K ikakauka. Akaanza kusikia maumivu. Ikabidi niache bila kucum.

Nataka kujua tatizo la kukauka Fluid kwenye uke linasabishwa na nini? This is my 4th experince katika wasichana ambao niliweza kufanya nao sex. Huwa walikuwa na tatizo la fluid kukauka na kuanza kusikia maumivu, na inabidi niache in-out movement. Japo nakuwa bado sijafika kilele. Mimi naona wasichana kama hawa wananikatizia utamu.

Lakini kuna msichana mmoja ambaye nilifanya naye sex bila condom( tulikuwa tumepima ngoma) yeye fluid yake ili kauka kiasi ila hakulalamika kuhusu maumivu. Je tuseme kuwa condoms zinakausha fluid ya uke?? Pia kondom zinawaumiza kwenye uke?
Ni mimi kijana mtundu."

Jawabu:Shukurani zikufiie kwa kunitumia swali lako mahali hapa, anuani yangu inapatikana kwenye profile lakini pia unaweza kuuliza kupitia hapa (Kama ulivyo fanya ktk hili).

Swala la kukauka kwa K mara baada ya mwanake kufika kileleni ni la kwaida kwa wanawake wengi na huwa na sababu mbali mbali ambazo mimi nitakutajia kwa kifupi tu kamaifuatavyo:-

1-Mwanamke huitaji kunyegeshwa tena baada ya bao la lake la kwanza, inategemea lilipopatikana kama kwenye Kipele G, Kwenye Kisimi, Mwisho wa Uke au kuta za uke. Ikiwa amepata bao "via" kisimi hapo lazima atahiji muda kidogo wa kupumzika (rejea Topic isemayo Maeneo matano ya utamu wa ngono kwa mwanamke) kama dakika kumi 5+ kisha wewe mpenzi wake ni wajibu wako kumnyegesha tena kwa kucheza na sehemu nyngine za mwili wake mbali na Kisimi. Inaweza kuwa kum-busu, kumla denda huku unamshika-mshika na kadhalika.

2-Mwanamke kuwa na uwezo mdogo wa kungonoana (low sex drive/libido) kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa hamjuani hivyo yawezekana yeye yuko hivyo na mara baada ya wewe kupiga bao la kwanza ksiha kurudi na "kumpigisha" yeye bao lake ndio ilikuwa mwisho wa "game" mpaka kesho au labda wiki ijayo kama sio mwezi mwezi ujao. Kama ulihitaji tena kwenda basi ulitakiwa kumfaya aendelee kuwa "interested" kiakili nakimazingira zaidi ya kimwili na pia ungepaswa kutumia kilainisho kwa ajili ya Condom au hata K-Y Jel.

3-Mwanamke kutokuvutiwa na ufanyaji wako, kama ulivyosema kuwa ilikubidi uache nje-ndani, swala l a kungonoana ni pana na sio kusimamisha kisha kupiga nje-ndani mwanzo mpaka mwisho (msome Simon Kitururu kwenye Comment yake kwani kamaliza yote niliyotakakusema).


4-Mwanamke kutokuwa na mapenzi pia inaweza kuwa sababu ya Uke wake kuwa mkavu mara baada ya zile nyege mshindo kumalizika/kumtoka (baada ya yeye kufikia Mshindo), mwanamke kama hana mapenzi huishiwa hamu ya kuendelea kungonoka haraka sana mara tu baada ya bao lake la kwanza.

5-Kuchoka au Uvivu, mwanamke kama kachoka au mvivu hali hiyo ya ukavu ukeni hujitokeza kwa vile akili yake inakuwa haipo/haizingatii kilekinachofanyika bali saa ngapi atapata nafasi ya kwenda kulala/pumzika.

Condom huwa hazisababishi Uke kukauka tena japokuwa inashauriwa kubadili au kutumia kilainisho kilichotengenezwa kwa ajili hiyo. Makampuni mengi ya bidhaa hzi yanatoa mafuta maalum kabisa kwa ajili ya kukuongezea ile hali ya ulaini amabo unakulinda wewe kwa kuzuia Condom kupasuka/chanikakutokana na ukavu wa Uke na vilevile kumuongezea mwanamke raha ya tendo.


Condoms hazimsababishii mwanamke maumivu bali ile hali ya wewe kumfanya mwanamke mwenye uke mkavu kwa muda mrefu ndio inasababisha maumivu.Ili ufurahie Ngono basi ni vema ukatafuta mwanamke mmoja umpendae na yeye akupende na mfanye tendo kwa ushirikiana na kumbuka ku-focus kwenye kufurahia tendo zaidi kuliko kupiga mabao na mambo yatakuwa bomba kabisa.

Asante na kila la kheri!

Wednesday, 9 July 2008

Ushuhuda wa Mama Rahma! Unakmkumbuka?

"Its me mama Rahma,napenda kumshukuru Mungu kwa afya njema,nilijaribu kwenda kwa Daktari mwingine maana Daktari wangu niliona hayuko intrested kunisaidia nimeamua kutoa Kitanzi sasa nina afya njema najiamini na najitahidi kufanya mazoezi ya misuli ya uke na natarajia kutumia Vinega.

Ushauri wangu kwa wengine ni kuwa waangalifu tunapofanya kitu ambacho Mungu hapendi that's why mtu unapata matatizoada Dinah, sikufichi mapenzi ya mume wangu yalipungua but now he loves me.

Kumbe ile birth control ilinifanya ngozi ya uke iwe laini kiasi kwamba ilipoteza ladha(hali yake ya kawaida) lakini sasa nafurahia tendo kama mwanzo, ty Dada dinah"

Dinah-Mungu ashukuriwe kwa yote, Hongera sana kwa kurudia hali yako ya awali na kufurahia uumbaji wake Mungu. Pia nashukuru kwa kurudi tena nakushuhuida mafanikio yako, karibu tena siku nyingine.

Natafuta Mfundaji!

"Dada Dinah mimi naomba msaada wa kupata mtu wa kunifunda haswaa juu ya haya mambo. Kama ni wewe nitashukuru zaidi au kama si wewe basi nisaidie pata mtu wa kunipa darasa hilo. Mimi nilipata bahati mbaya ya kuzaliwa mjini na kufiwa na mzazi wa kike mapema hivyo kukosa opportunity ya kupewa madarasa haya. Naomba msaada."

Jawabu:Pole kwa kuondokewa na watu muhimu kwako, hata mimi nilizaliwa mjini ila nilibahatika kuishi na Marehemu bibi.

Nasikitika kukuambia kuwa mimi sio Mfundaji lakini nafuraha kusema kuwa naweza kukusaidia ikiwa tu utaniambia wapi unakwama au ungependa kufahamu nini zaidi kama mwanamke ili kuboresha uhusiano wako.

Tafadhali jamani , kama wewe ni Mfundaji au unamjua Mfundaji basi weka mawasiliano yako/yake....mteja mmoja huyo na wengine wengi watafuata. Asante.

****Tahadhari: Kuwa muangalifu unapokwenda watembelea Wafundaji hao, hakikisha unakuwa na mtu mwingine(mwanaume) na Jamaa zako wengine wanajua unakenda wapi, wape details zote kwa Usalama wako.

Onyo: Tangu nimeweka Topic hii masaa matatu yaliyopia nimepokea zaidi ya nambari za simu kumi na tano na anuani za barua pepe sita za Wanaume wanaojiita Rijali, nambari hizo ni za Makampuni ya simu ya Tanzania.

Tafadhali hapa sio mahali pa kutangaza au kutoa huduma za Ngono chafu, wanaokuja hapa wote wanajiheshimu na wako kwenye mahusiano yao na wanataka namna ya kuboresha na sio kufanya ufuska!

Mkiendelea kuleta upuuzi wenu nitawachukulia hatua za Kisheria!

Tuesday, 8 July 2008

Ningependa kufunga Ndoa lakini anaharaka sana-Ushauri!

"Mambo vipi Dinah, Sorry nimejaribu kutafuta e-mail yako bila mafanikio lakini katika kuangalia huku na kule finaly nikaipata.

Mimi nina swali moja ambalo linanitatiza sana kuhusu mpenzi wangu ambae ninataka kumuoa lakini nasita kutokana na vitabia vyake. Hivi wewe binafsi unamchukuliaje mwanamke ambaye yuko very anxious for marriage kiasi kwamba akiona rafiki yake anaolewa basi ujue siku hiyo na wewe utakuwa na kesi.

Pia anakuwa na hasira zisizo na msingi. Yaani kila mara unapokuwa nae basi hakosi kukasirika(sio muda wote) but still anainsist marriage. Mimi natishika na matendo yake kiasi kwamba kila mara najiuliza...hivi nikioa si ndio itakuwa balaa kama kipindi hiki cha mapenzi bila ndoa hakuna kuelewana? bcoz naona hata adabu amepunguza but still anasema ananipenda sana.

In short she is soo aggressive and wants to control me such that anataka anachotaka yeye ndio kifanyike lakini mimi nikitaka jambo hakosi kuweka pingamizi. Nimemwambia nataka kumuoa mwakani (2009) lakini yeye hataki alikuwa anataka this year.

Zamani alikuwa mpole sana kwangu kiasi nikimwambia kitu ananisikiliza lakini siku hizi akinisikiliza basi ni kwa muda. Pia anatabia ya ku-revenge eg. Kama nilisave namba ya mwanamke kwenye simu yangu ambaye yeye hamjui basi ujue na yeye ipo siku atasave namba ya mwanaume na kumchokoza ili ampigie mida ya usiku mimi nikiwa nae, na nikiuliza basi najibiwa "IS MY FRIEND, I THOUGHT IT WILL BE OK WITH YOU BCOZ NA WEWE UNACHUKUA NAMBA ZA WANAWAKE"Naomba ushauri wako Dinah. David"

Jawabu:Asante David, mimi binafsi nitamchukulia mwanamke huyo hajiamini, hajakomaa/kua kiakili na anawivu wa kizembe.

Unajua, Mtu yeyote ambae hajiamini mara nyingi huvaa "wasifu" wa mtu mwingine pale anapoanza uhusiano mpya, kama ujuavyo siku hizi kabla hatujajikita kwenye uhusiano wa kimapenzi huwa tunaanza na kaurafiki fulani hivi kabla ya "date" ili kufahamiana vema sio?, sasa wakati unauliza maswali labda na kuelezea nini unapenda/taka kutoka kwa mwenza, huyo "date" anachukua yale unayopenda zaidi na kujitahidi kuwa hivyo hasa kama anahisi kakupenda au kunakitu anadhani atapata kutoka kwako.

Mfano unaposema "sipendi mwanamke/mwanume mlalamishi, mkaidi, mvivu n,k....napenda kuwa na mwanamke/mwanaume mwelevu, mpole, msafi nje na ndani, asie penda ulevi" n.k basi ujue huyo mwanamke/mwanaume atafanya vile upendavyo ili asikukose.

Mara nyingi hii sehemu ndogo ya jamii hufanikiwa kuwa na huo uhusiano lakini baada ya muda fulani mhusika (mwanamke/mwanaume) anachoka kule ku-"pretend/act" au kuvaa wasifu ambao sio yeye na badala yake anakuwa yeye kama yeye na hapo ndio utakapoanza kuona mabadiliko makubwa sana kama ulivyoshuhuida kwa mpenzi wako huyu.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa mpenzi wako anataka kufunga ndoa kwa vile rafiki zake tayari wamefungandoa yaani anafuata mkumbo kwa kujiona kuwa anaachwa nyuma, mtu kama huyo hafai kwani baadae atakusumbua sana, pili huenda anahisi kapoteza sana muda kuwa na wewe na hivyo anahofia ukimuacha hatopata tena mtu wa kuji-"commite" kwake kama wewe (ndio maana nikasema hajiamini) hivyo anatumia nguvu (ukali, ujeuri, kisirani, visasi n.k.)

Mimi naamini kuwa swala la ndoa ni maamuzi ya watu wawili hasa ukizingatia maisha tunayoendsha hivi sasa, ofcoz kimila na kidesturi mwanaume ndio anachumbia lakini baada ya hapo ninyi wote wawili ndio mnapanga,shirikiana na kuelewana lini mfunge ndoa na hiyo inategemeana na aina ya maisha mnayoishi/endesha na aina ya ndoa (sherehe) mnayoitaka.

Kuna wale wanaopenda "simple" lakini bab-Kubwa (hapa unahitaji kipato cha maana na miezi kama mitatu mpaka sita hivi kujiandaa) alafu kuna wale wanapenda kubwa na bab-Kubwa(utahitaji zaidi ya miezi sita inategemeana na kipato), wengine hutaka ndogo na ya kawaida (hii inachukua siku saba tu kitu na box).

David ulivyotoa maelezo yako hakuna mahali umegusia wewe kumpenda yeye, sito kulaumu kama ile hali ya kumpenda inapungua kutokana na matendo yake ambayo ni ya aibu sana kama mwanamke (mambo ya usawa hayo), hata hivyo kitendo chako cha kutunza namba za wanawake wengine bila kumshirikisha yeye sio kitu kizuri (wewe hapo ulikosea pia).

Lakini kama unampenda na nia yako ni kufunga nae ndoa basi nakushauri mfanye maswasiliano....zungumzeni na mwambie wazi kuwa anahitaji kubadili mwenendo wake vinginevyo uhusiano wenu utakuwa hadithi, mwambie wazi tu kuwa unampenda lakini vitendo vyake vinakukatisha tamaa na unahofia kuwa ukifunga nae ndoa bado utakwenda kutafuta amani nje....Mikwara yenye ukweli ndani yake huwa inafanya kazi.

Kisha msikilizie, kama anakupenda kwa dhati ataomba radhi na kujitahidi kubadili tabia yake mbaya, maana ya kuomba radhi ni kubadilika, kama hubadili matendo basi hakuna sababu ya kuomba msamaha.

Kila la kheri!

Monday, 7 July 2008

Nataka kuacha Nyeto?-Ushauri!

"Dada Dinah nakushukuru kwa kazi ya kuelimisha jamii unayoifanya kupitia mtandaoni. Well done. Maana siku zinavyozidi kwenda mambo yanazidi kubadilika teknolojia inakua kwa hiyo tuko zaidi kwenye computers na mambo ya ukunga na jando yanapungua kutokana na mabadiliko ya jinsi tunavyoishi.


Sasa kwenye mada ambayo naileta kwako, mimi ni kijana wa kiume mwenye miaka 28, nimekuwa nikipiga punyeto tangu nikiwa na miaka 21 mpaka sasa, sio kwamba sina mpenzi la hasha nimekuwa na wapenzi mbalimbali (one at a time)mpaka hivi sasa ninaye na panapo majaliwa atakuwa mke wangu. Nataka sana kuacha hii punyeto.

Naomba unieleze madhara yake naikiwezekana unipe na materials nyingine za kusoma na msaada wa kimawazo jinsi ya kuachana nayo.

Wasalaam AD "

Jawabu: AD asante kwa kutambua machango wangu mahali hapa vilevile nashukuru kwa ku-share tatizo lako. Kuacha punyeto ni uamuzi tu kama ilivyo kwenye mambo mengine kama vile Umalaya, Ulevi, Uvivu n.k. japokuwa inategemea na ulivyoathirika Kisaikojojia, huenda ukahitaji msaada wa Tiba ya "Therapy".

Kwa vile hujaweka wazi hiyo nyeto u naipiga wapi, nikiwa na maana kuwa unafanya hivyo kwavile huwezi kumaliza uume wako ukiwa ndani? Unafanya hivyo kwa vile unahisi ndio unasikia utamu zaidi kuliko ukiwa ndani ya uke wa mpenzi wako?, Je Unajichua baada ya kumaliza na mpenzi wako kwa vile hajakuridhisha? Naomba uweke wazi hapa ili niweze kukupa jawabu la uhakika.

Pole kwa kuchelewa kukujibu, hii ni kutokana na shughuli za hapa na pale. Asante!

Saturday, 5 July 2008

Kunatofauti za ukataji kiuno?

"Dada D mambo yako nimeyakubali,ila naomba kuuliza kitu kimoja...Kwanini wale kina dada wanenguaji(stage show) wanakatika sana wakiwa jukwaani hadi mtu unapandwa na midadi,wengi wao ni wachovu katika minenguo ya kitandani?"

Jawabu: Asante san akwa swali lako, ukataji wa kiuno wa jukwaani na ule wa kitandani unatofauti kubwa sana. Umenikumbusha, kuna mdada mmoja aliwahi kunilalamikia kuwa mpenzi wake huwa anamlazimisha amzunguushie kiuno kama Feni kitu ambacho kinawezekana ikiwa mwanaume anaume mrefu kisha mwanamke akaning'inia na kuzuunguuka hehehehhe natania hapa! Ila kukizunguusha sana inawezekana lakini hakitompa mwanaume au mwanamke raha inayokusudiwa na ukatikaji wakati wa kungonoana.

Mwanamke akikata kiuno kile cha kucheza jukwaani ni wazi kuwa huwezi kukisikilizia kwa ndani "unless" umashikilie kiunoni, lakini mwanamke anaekikata kile cha kitandani utahisi uume wako ukibanwa na kuachiwa kama vile mwanamke anavyobana misuli ya uke a.k.a Endiketa!

Nitakupa mfano kidogo hapa; kiuno cha ngono (kitandani) hukatwa kwa chini zaidi na kikikatwa makalio ya mwanamke hukaza tofauti na kile cha jukwaani ambapo ni kiuno tu ndio kinazunguuka.

Kunamikao ambayo humfanya mwanamke ashindwe kukata kiuno ipasavyo hasa kama maumbile ya wanaume yako kinamana, Mfano mwanaume mwenye uume mfupi akimfanya mwanamke ktk mkao wa "doggie" ya kulala ambayo mwanamke huwa huru zaidi kukizunguusha hufanya ashindwe kukatika vilivyo kwa vile itachomoka-chomoka.

Vilevile mwanaume mwenye kitambi kikubwa akifanya ktk mkao wa kifo cha mende ni wazi kuwa hatomlalia mwanamke hivyo ule uhuru wa mwanamke kukikata kilekiuno cha kungonoka inakuwa ndogo sana.

Asante kwa ushirikiano wako.
"Hi Dinah,Hope you're fine and chillin. Dina hI'm compilling together a book, it's an EROTIC novel based on a sexually corrupted journey of a couple (wife+hubby). The issue is, i'm in need of guy who knows better erotic matters, a person who may help me in the editing process.

As I can see, you're more than star in the area and your advice is highly sought. I wish for you to be the editor and top critic of my book n help makin it perfect. Do you have time for that? please, I need you! I may send first 1-2-3 chapters to you for a review if you're ok with it. Good day... Bony."

Jawabu: Habari Bony, asante kwa kuthamini machango wangu mahali hapa, hakuna matata kabisa. Sasa wewe nitumie hizo Sura tatu za mwanzo ili nione tutakavyosaidiana katima hilo. Siku njema.

Thursday, 3 July 2008

Kungonoka sana ni Ugonjwa?-Ushauri!

"Asante dinah kwa kutuweka wazi, leo mimi nasema nilikuwa nashindwa kuelezea mbele ya wanawake wenzangu kuhusu jinsi ninavyopenda kitendo cha kungonoka/sex. Walikuwa wakihadithia na kuonyesha mshangao kwa wale watu ambao wanafanya ngono siku 7 za wiki bila kupumzika?

Mimi nilikuwa nawashangaa sana, kwani mimi na mume wangu tulikuwa tunafanya kila siku na hata baada ya kutengana na mume wangu nikapata wapenzi wawili tofauti; mmoja ana high sex drive km mume wangu na mwingine alikuja kukopu na jinsi nilivyokuwa napenda mimi.

Je huu ni ugonjwa? sijijui km ni normal au vipi? lakini hapohapo km sipi kwenye mahusiano na uwezo wa kujizuia ht miezi 6. (ila piga p.....nyeto) mara kwa mara. namaanisha si lazima nipate mboro tuu.sijui nimejieleza vzr?mimmy "

Jawabu:Hali ya wewe kutaka kungonoka sana ni ya kawaida kwa baadhi ya wanawake, kuna wale ambao wamejaaliwa kufanya ngono zaidi ya mara tatu kwa siku nahufany akila siku, yaani kwa wiki wanaweza kufanya zaidi ya mara Ishirini na moja (hii ni kutokana na uzoefu) yaani the more unafanya the more unataka tena na tena.

Hali hiyo tunaiita "high libido" sio ugonjwa na wala sio "addiction" Mungu kakuchagua hehehehehe(bahati) lakini uzurio wake ni kuwa unaweza ukajizuia na usifanye kabisa kwa mwaka mmoja ndio maana nikasema kuwa sio "adictive".

Sasa ikitokea mpenzi wako hayuko kama wewe yaani "libido" yake ni ya kawaida unaweza kujizuia ili uendane nae lakini mara moja mora ukaomba "mizunguuko zaidi" ili kuridhika hivyo ni vema kuliweka wazi hilo kwa mpenzi wako kabla hajafika mbali. Ikiwa mpenzi ni "low libido" sidhani kama mtawezana aisee bora kuishi mwenyewe, mambo ya mara moja kwa wiki nani anataka? hihihihi).

Mimmy uko salama na Mshukuru Mungu kwa hilo. Siku njema.

Kutoa mimba ni sahihi?-Ushauri!

Bonyeza hapa kuona Picha inaonyesha kiumbe (mtoto) kilichotolewa, kilikuwa na umri wa wiki nane tumboni ambazo ni sawa na miezi miwili.
"Natoka nje ya mada kidogo naomba mitizamo yenu Dinah na wadau wengine katika suala la abortion/utoaji mimba je ni sahihi kwa wapenzi kutoa mimba baada ya kuingia bila kutarajiwa?kama hawajajiandaa na pia kuwa tayari kwa mtoto kifedha na hata kindoa-TEITEI".

Mtazamio wangu:Teitei nashukuru sana, hili swala bado ni nyeti sana kulizungumzia japo kuwa linafanyika sana ktk jamii nyingi hapa Duniani ikiwa ni pamoja na hapa nyumbani Bongo, ni kama ilivyo kwenye kuzungumzia ngono kwa uwazi/adharani.

Maelezo nitakayoyatoa ni ya wazi pia ni hali halisi, lakini kusema nitakacho sema sio kwamba naunga mkono swala zima la utoaji mimba. Mimi binafsi naamini kuwa utumiaji wa madawa ya kuzia mimba hasa ile "Morning after" ni utoaji mimba, lakini hili watu hawalioni au kulizingatia mpaka mimba ijengeke ndio wanaona "big issue", lakini katika hali halisi kuzuia mimba (unaruhusu iingie lakini isijengeke) na kutoa mimba (unaruhusu iingie na ijengeke kisha unatoa) kwangu mimi ni mauaji ya viumbe visivyo na hatia.


Kwa mujibu wa Imani zetu za kidini utoaji mimba sio sahihi na huesabika kama mauaji ambayo ni dhambi, lakini wakati huohuo mama anaweza kulazimika kutoa mimba kutokana na matatizo mbali mbali moja likiwa ni matatizo ya kiafya ambapo Daktari hupendekeza hilo, hili hufanyika kwa kufuata hatua za kisheria na vilevile kuzingatia maamuzi ya mama na baba wa mtoto, kwamba wako radhi mtoto afe mama abaki au wote wawe hatarini kufa ikiwa mimba haitotolewa.


Swala lingine ambalo ni la pili linaweza kufanya/sababisha pea/wenza watake kutoa mimba ni kutokuwa tayari kwa hilo kama ulivyosema hapo juu, kwamba mimba imeingia kwa bahati mbaya bila ninyi wawili kupanga, kwamba hamko tayari kuwa baba/mama au mnajua wazi kuwa hamtomudu malezi ya mtoto atakae zaliwa.

Natambua unataka kuuliza "kama ulijua hukua tayari kwanini sasa ulingonoka?" hebu tuwe wazi na nafsi zetu, ni wangapi hufikiria mimba au kuzaa pale tunapokwenda kufanya mpenzi au pale tunapovutiwa na wapenzi wetu? Mimba ni matokeo ya kungonoana na ni wajibu wetu (wake kwa waume kuwa waangalifu) lakini wakati huohuo tutambue kuwa kuna bahati mbaya ambayo husababishwa na watu kutojua kikamilifu kile wanachokifanya (ngono) kutokana na swala zima la ngono kuwa siri miongoni mwetu.

Tatu ni mwanamke "kumimbwa" na mwanaume aliyem-baka, kutokana na tendo lenyewe ambalo ni la kikatili na limefanywa na mtu ambae humjui, humfanya mwanamke kuathilika kisaikolojia na kiakili nakutaka kutokuwa na kumbu-kumbu ya mkatili huyo na njia pekee ya kuondokana na hilo ni kutozaa mtoto wake (m-bakaji) ambae akizaliwa ofcoz itakuwa kumbukumbu mbaya na ya maumivu makuu.

Kwa nchi zilizoendelea kunavituo vyakuwalea/angalia wanawake waliobakwa namimba zao na mara tu watakapijifungua watotow aliozaliwa huchukuliwa na kutafutiwa familia amabzo zinahitaji watoto, na kipindi chote hicho mwanamke huyo huenda kozi kali ya ushauri nasaha mapaka atakapo jifungua.

Kutokana na mfumo wa maisha tunayoishi sasa swala zima la utoaji mimba (kwa nchi zilizoendelea) limeachwa kwa mwanamke husika, kuwa yeye ndiye mwenye uamuzi wa nini kifanyike juu ya mwili wake na kabla hilo halijafanyika ni lazima mama huyo apatiwe ukweli wa athali/madhara na hatari za kutoa mimba, anatakiwa kufanya hivyo wakati gani, aina gani ya utoaji wa mimba anaitaka kisha wanakupa muda ukafikirie kabla hujaendelea na utoaji mimba.

Ukirudi baada ya muda waliokupa na ukawa na msimamo uleule wa kuendelea na uamuzi wako basi unapewa ushauri nasaha na unaelezwa tena nini kitafanyika, athari na matuzo baada ya huduma kukalimika alafu ndio wanaendelea....kutokana na maelezo yangu utatambua kuwa wenzetu wamelikubali na kuliweka wazi ili kuepusha utoaji mimba ambao sio wa kitaalam.

Asante.

Wednesday, 2 July 2008

Akianza kuingiza inauma-Ushauri!

"Hi Dinah mimi ni msichana mwenye umri wa miaka28 namshukuru Mungu kanipa mpenzi nimpendaye sana. Naomba unisaidie kwenye hili tatizo langu na samahani sana kwa usumbufu, kila ninapokutana na mpenzi wangu faragha napata maumivu sielewi tatizo nini hasaila nanyevuka vizuri kabisa.

Kuna wakati nilikuwa nafikiri ni kwa sababu ya kukaa kipindi kirefu bila kukutana ila kuna kipindi tulikaa pamoja kama wiki nzima hali yangu ikawa hivyo hivyo napata maumivu kila anapoanza kuingiza uboo wake kwenye uke wangu na hii hali hutokea kila tunapoanza tu bao ila baada ya hapo siyasikii tena.

Naombeni ushauri wenu kwenye hili jambo maana huyu mwanaume anataka tuoane sasa naogopa isije ikawa nina matatizo ikawa aibu kwangu je me nipo kawaida au nini matatizo?tafadhali naomba nisaidie dada yangu "

Jawabu: Asante, hakuna haja ya kuomba msamaha kwani hakuna usumbufu wowote niupatao ktk kujaribu kusaidia wasomaji na watembeleaji wangu wote, nafarijika kutambua kuwa unathamini uwepo wangu hapa kwa kutaka ushautri wangu.

Hiyo hali hiyo ya maumivu inaweza kusababishwa na mambo machache tofauti ikiwa ni pamoja na uume kuwa mkubwa, uke kuwa mdogo, anaingia kwa fujo, wasiwasi wako wa kupata maumivu (itakuwa imekuathili Kisaikolojia, kwamba wakati mwingine wala huumii ila kwa vile kichwani kuna swala la kuwa unaumia kutokana na uzeofu wako basi wewe unahisi maumivu ambayo hayapo).

Vilevile inawezekana kabisa kuwa ulijeruhiwa hapo mwanzo wa uke sasa kila akiingia anakuwa anakutonesha na kusababisha maumivu au pengine huwa huna unyevu wa kutosha, unaweza kuhisi kunyevuka lakini ute unakuwa hautoshi kusukuma uume ndani hivyo unahitaji kilainisho cha ziada kama vile mate au K-Y Jel.

Hilo lisikutie hofu au wasiwasi kuwa unatatizo/kasoro, napenda utambue kuwa ni hali ya kawaida kwa baadhi ya wanawake na kama nilivyosema hapo awali kuwa huenda linasababishwa na ukubwa/udogo wa viungo vyenu vya kufanyia mapenzi.

Alafu kumbuka kuwa mtu akifika bei (akikupenda) hakuna kasoro anaiona kwako yaani kwake wewe ni "perfect"! Ondoa hofu na furahia maisha na kila lililo jema ktk kukamilisha mipando ya ndoa.

Tuesday, 1 July 2008

Nimefiwa na baba, Mpenzi kaniacha pia-Ushauri!

"Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka thelathini na tano niimeachana na mpenzi wangu karibu miezi miwili sasa, kilichopelekea tuachane ni mimi kutokuwa karibu nae pia kutofanya nae mapenzi kwa vile sikuwa najisikia kufanya hivyo na nilikuwa naona kama Dunia imenilemea kutokana na kuondokewa na Baba yangu Mzazi. Tatizo nililonalo hivi sasa ni kwamba bado nampenda na ninataka turudiane nifanye nini?"

Jawabu: Pole sana kaka yangu ka hilo lililopelekea wewe kuniandikia mimi. Nimefurahishwa na uwazi wako ktk hili. Niliposoma maelezo yako nikahisi kwamba ulikuwa unasumbuliwa na mawazo mengi kutokana na kuondokewa na mmoja kati ya watu muhimu sana ktk maisha yako, hali hiyo ilipelekea wewe kuwa na aina yua "Depression".

Sasa kabla sijakushauri nini cha kufanya ningependa ufahamu kuwa hali hiyo sasa imekwisha yaani umebadilika au niseme umepona na umekuwa wewe kama hapo awali na ndio maana swala la kutaka kutafuta suluhisho au njia ya kurudioana na mpenzi wako limekujia na umetambua kuwa wewe ndio ulikuwa sababu ya yeye kuondoka!

Ni wazi kuwa mpenzi wako hakujua kuwa wewe ulikuwa unasumbuliwa na "Depression" na kwa mawazo ya mwanamke wa kawaida ndani ya Bongo alihisi labda humpendi tena na ndio maana akaamua kujitoa kitu ambacho ktk hali halisi hakupaswa kukifanya na badala yake alipaswa kuwa mvumilivu, kukupa ushirikiano kwenye "nyanja" nyingine na sio ile ya kimwili tu.

Unajua watu tunapokea na kuchukulia matatizo kitofauti sana, kuna wale ambao wakikumbwa na tatizo kama lako huwa haliwapigi/shitua kama ilivyokutokea wewe, na hiyo inategemea zaidi na ukaribu/uhusiano kati yako na mpendwa wako ambae ni Mzee (baba'ko).

Ushauri wangu kwa kuanzia ni kujenga hali ya kujiamini tena kwa kuanza kujichanganya na marafiki (outing), jiunge "gym" au anza kufanya mazoezi ya viungo mepesi (kukimbia, push-ups n.k), soma sana vitabu vya "challenges", angalia funny movies (usiguse zinazohusu mapenzi au huzuni) au jishughulishe na mambo ya shamba, bustani hata kama ni ya maua, usafi n.k (kuwa-busy) na kamwe usipende kukaa peke yako ama kumtembelea mama yako kila wakati (atakurudisha nyuma yaani utakuwa na uzuni zaidi).

Ikitokea uko peke yako basi jitahidi kusikiliza muziki uliochangamka Mf ule wa Mr blue na Chillah wa "Nipo, nilikuwepo na nitakuwepo" au Fiesta wa Ray C au hata ule wa Ngoma zetu sijui kaimba nani au za Mr Ebbo kwanizitakuchekesha kimtindo......those kind of songs na kwa sauti ya juu (usisumbue majirani lakini).

Wakati unaendelea na utaratibu huo anza kwa kuwasiliana na mpenzi wako mara moja/mbili kwa siku (ni salamu najisni gani unamkosa na kumpenda, tafadhali usithubutu ukagusia tatizo lako) Kisha mambo yakiwa "swafi"(baada ya wiki mbili mpaka tatu utakuwa umerudisha kujiamini kwako) na hapo ongeza "gia".

Pendekeza kuwa ungependa kuonana nae kwa ajili ya kinywaji mahala fulani (sio nyumbani kwako/kwake) ikiwa ni mpenzi wa maua basi si vibaya "kuibuka" na "bunch" la maua tafadhali yasiwe ya "plastic" (wanawake wengi tunapenda maua lakini si wote tunathamini maua), ili ushinde basi nunua hereni nzuri kwa ajili yake.

Natambua kuwa mkikutana utapenda kumwambia "nakupenda sana na ninataka turudiane na tupendane kama zamani" ni maneno mazuri lakini sio mwanzo mzuri, nakushauri uzungumzie mambo ya kawaida tu kama siasa, movie, muziki, jamii n.k, mtegee aanze yeye.

Mpenzi wako akijaribu kugusia mambo fulani mliyokuwa mnafanya pamoja kama wapenzi, hapo ujue umeshinda na ndio atakuwa amefungua mlango wa wewe kuomba msamaha na kumueleza ni nini haswa kilikuwa kinakufanya uwe mbali na yeye hasa pale kunako uhondo (kitandani)!

Nakutakia kila la kheri na mafanikio katika safari hiyo ya kurudiana na Mpenzi wako umpendae