Saturday, 31 May 2008

Nini cha kufanya, siku ya kwanza!


"Dinah mi nina swali..kama nakutana mara ya kwanza kimwili na mwanaume what should i do n what should i not do??i would really like to makelove to him coz i believe we both love eachother na tumeanza kuwana kahusiano mwanzo wa mwaka huu but we re both very busy n thought we wanted to do it when we can both enjoy n feel ready.

I want to make it special!!coz we trully adore eachother and get along i don want to blow it!postions i should do??viuno??blow job??im planning it to be at ma place ,have a nice home cooked meal,trying to make ma room tempting beemed light,candles,slow music ,wear kinky knickers u know sort of a thing!!looking forward na comments zenu.thanks"

Jawabu: Asante kwa swali lako na pi anaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kwani nilikuwa likizo. Napenda kwanza ukumbuke au utambue kuwa mwanaume siku zote anapenda au anataka kuwa mtendaji mkuu labda niseme kuwa in-control wakati wote hasa hiyo siku ya kwanza ya kukutanisha miili yenu.

Huitaji kujiandaa sana na badala yake jaribu kuwa wewe (be urself) kisha nenda na "flow", ukijiandaa sana unaweza kumuogopesha asirudi tena au akawa anadai ufanye mandalizi hayo kila siku kwa vile ndio uliyoanzanayo so atataka moto uaki pale-pale, sasa siku ukiamua kuwa romantic si jui ndio utafanyaje hehehehehe usijali.

Siku ya kwanza kwa mwanamke na hata kwake yeye mwanaume ni siku ya kujuana miili yenu, i siku ambayo mtu anaweza asi-notice maandalizi yako kwa vile akili yake yote iko kwenye penzi juu yako na jinsi gani atafurahia ku-share mwili wake na wako.

Kwa maelezo zaidi tafadhali nenda kwenye topics za December na saka inayosema "siku ya kwanza". Wachangiaji wengine shukurani za dhati kwa kumuweka sawa mwenzetu.

Kila la kheri!

Thursday, 29 May 2008

Furahia kungonoka bila mshindo....inawezekana!

Kama unauzoefu na vilevile unapenda ngono (sio kungonoka na kila mtu, nazungumzia wewe na mpenzi wako mmoja tu unaempenda) unaweza kufurahia "muunganiko" wa mwili wako na wa mpenzi wako hasa kama wote mnajua miili yenu vema, yaani vipele vilipo....pale ukishikwa au kumshika mwenzio ananyegema au kupata raha fulani hivi ya kimapenzi.

Kumbuka kuwa Ngono ni kitendo cha kukutanisha viungo venyu vya uzazi (mwili) na sio kufika kileleni hivyo kufurahia au kupata raha (sio utamu ni raha hehehehe utamu mambo mengine, nitafute nitakuambia) bila kufikia mshindo inawezekana kabisa....by the path ni kutokana na uzoefu wangu.

Unajua kuwa kuna wakati unafanya ngono/mapenzi au niseme mnapelekana kwa muda wa saa nzima na ushehe na hakuna anaefika kileleni lakini wakati hili likifanyika unahisi kufurahia ile hali ya ukaribu, kushikana, papasana, kubadilishana mate/kubusu, kulambana na muunganiko wa viungo venu vinavyopendana kwa dhati ambapo kwa wakati huo wewe na yeye "manavimuvuzisha" nje-ndani au juu-chini au mduara (kukata kiuno) kama sio huku na kule na baadae ndio mmoja anawahi kileleni au manafika wote.....unauzoefu na hili? Unaelewa sasa na zungumzia nini eeh?

Ila tatizo linalojitokeza kwa watu wengi ambalo linaweza kupelekea watu kupinga ninachokisema hapa ni kuwa, unapokuwa nampenzi wako au unapofikiria swala la kufanya ngono akili yako inakuwa "tuned" kwenye "lazima nimfikishe kileleni mpaka akome au aombe radhi".....kwani umeambiwa ni adhabu? au "lazima tufike mara tatu" na matokeo yake mnapo anza kufanya mnakuwa mme-focus kwenye kufika kileleni na sio kufurahia miili yenu.

Kwa wale wanaume ambao Mungu kawa jaalia kwenda mwenzo mrefu na wanajua tofauti ya "sex na love making" ndio wazuri katika hili ikiwa tu kamuandaa mpenzi wake (mwanamke) nampenzi huyo (mwanamke) anajua kujizuia kufika kileleni na hapo nyote wawili mtafurahia tendo bila kufika kileleni mapaka mtakapochoka "kubilingishana" ndio mnajiachia na kufika pamoja au moja baada ya mwingine.

Ikiwa wewe ni mwanamke ambae kwa bahati mbaya huwezi kufika kileleni ukiwa umeingiliwa (uume kuwa ndani) basi hii ndio inakufaa zaidi kama wewe na mpenzi wako mnajua kuchezeana vizuri na kwa ustadi.

Unachotakiwa kufanya ili kufurahia hili ni kujiandaa kiakili, kimwili na vilevile mazingira....

Nitakuja kumalizia hilo nikifika nyumbani,.....wacha nimalizie kutumikia watu hapa!

Oh hey! ile mbinu ya mwisho ya kumfanya jamaa atangaze ndoa ambayo ili-base kwenye Poll itafuata pia, karibu sana.

Wednesday, 28 May 2008

Dalili ya 3 kuwa anachoropoka nje....

Kwa kawaida kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi hakukosi kutofautiana na matokeo yakutofautiana ni kuzozana, sasa linapojitokeza hilo na kwa bahati mbaya hamjafikia muafaka au mmoja wenu kagoma “kukubali yaishe” au kuwa mjinga ili kutofikia pabaya basi mpenzi wako ambae “anatereza”, anaweza kuibuka na maelezo/sentensi zitakazo ashiria kuwa mnaelekea pande tofauti (ham-elewani) na kama kawaida atakurushia wewe lawama kuwa humuelewi, m-bishi au hata kuwa humheshimu.


Kwa yeye kukusingizia hayo ni wazi kuwa yatakuumiza na kukufanya labda uongeze hasira(hakuna jambo baya kama kusingiziwa jambo) lakini kama nilivyokuonya awali kuwa kukasirika hakuruhusiwi kwani tunachojaribu hapa ni kubadili “mtiririko” au “script” ili kuokoa uhusiano wenu sio.


Maelezo yake yako wazi (kumbuka niliwahi kusema kuwa wanaume most of the time husema kilicho kichwani), sasa hapo anakuambia kuwa uhusiano wenu hauko kama ulivyotakiwa kuwa na anaefanya au kusababisha ni wewe(hata kama ni yeye still atakusukumizia wewe) kwani sote tuna jua kwamba wanawake ndio tunaoweza kurekebisha mambo.....we are mothers, dont forget that!


Sasa ziba/zuia au ondoa hasira zako na anza kuzungumza nae taratibu kwa upendo (kama mama na mwana, yaani jisogeze...mshike panaposjikika namuangalie usoni) na kusema kuwa ungependa nyote wawili muwe kwenye mstari mmoja naje ufanye nini ili kufanikisha hilo. Kisha malizia kwa kusema kuwa utajitahidi kadiri ya uwezo wako ili kumuelewa na kurudisha heshima kwake.

Jichunguze au chunguza kuna kitu gani kimepungua ndani ya uhusiano wenu ambacho kina mfanya ahisi kuwa heshima haipo baina yenu?, kwanini adhani kuwa hum-elewi? n.k alafu rekebisha hizo hitilafu na mambo yatakuwa poa kabisa kwani kinachomtoanje atakuwa anakipata nyumbani.

Jambo linapojitokeza unapaswa kulizngumzia wakati huo (itakubidi ujifunze kuzuia hasira), sio unaacha siku moja au mbili zinapita alafu unarudi nyuma.....kwa mwanaume itakuwa "unapenda kulalama kila wakati" wakati kwako itakuwa "nilihitaji muda kufikiria na kupanga maneno yangu".

Panua uwezo wako wa kiakili au niseme upeo ili uweze kufikiri haraka na kupangilia maneno cha-chap on spot, suingonjee kesho utakuta mwana sio wako.

Huu ni mwisho wa mfuatano wa jinsi ya kugundua kuwa Mpenzi anatereza/toka nje ya uhusino wenu wa kimapenzi/ndoa.
Endelea kuwepo.

Monday, 26 May 2008

Dalili ya 2 kuwa anatereza nje...

Sema wewe, vipi mambo?
Naendelea na sehemu ya pili ya dalili za kukufanya wewe utambue kuwa mpenzi wako anakucheza shere.

Akishuhudia tukio lolote linalohusisha uterezaji (cheating) kutoka kwa marafiki zenu au ndugu na jamaa lenye kuhusisha swala zima la kutoka nje ya uhusiano na pea husika wanataka kuachana 4 good......atasema kwa sentensi fupi tu yenye maana kuwa "kamwe sitoweza kukufanyia hivyo" alafu kamaliza.

Najua utafurahi na kuamini kinachotoka mdomoni lakini anaweza kabisa akasem ahivyo akimaanisha kuwa kamwe hutogundua anachokifanya kwa kujifunza mapungufu yaliyotokea kwenye tukio zima.....kama nilivyosema unachotakuwa kufanya hapo ni kubadili mtiririko mzima kwa kuanzisha maongezi yatakayohusisha tukio lililotokea/linalotokea bila kujenga hasira/ukali.


Kwa vile kasema kuwa yeye kamwe hatokufanyia hivyo (hatokuumiza) basi mwambie jinsi gani unampenda na namna gani utaumia au penzi lenu kusumbuka ikiwa mmoja wenu akitereza na kisha sema hutoruhusu hilo litokee kwa vile usingependa kupoteza penzi lenu.


Alafu malizia kwa kusema, lakini ikiwa mmoja wetu kashawishika na katereza nihakikishie kuwa tutalizungumza kwa uwazi na kutafuta ufumbuzi/muafaka.......hapo utakuwa umebadilisha "script" yake na wakati huohuo wewe unatakiwa kuangalia kitu gani kimepungua kama sio hakipo kwenye uhusiano wenu na hivyo anza kuki-restore taratibu ili Uhusiano usiharibike.

Pamoja na kuwa sote kazi zetu za kila siku zakutuingizia kipato ili tuendelee kuishi, kumbuka kuwa uhusiano wa kimapenzi unahitaji kufanyiwa kazi ili kuwa mzuri na wenye afya.....usitegemee penzi pekee kufanikisha hilo, unahitaji kujishughulisha kila siku ili usijisahau.(keep the fire).

Endelea kuwepo kwa dalili ya tatu, lakini kama unanyongeza ktk hili basi usisite kuongezea. Karibu.

Saturday, 24 May 2008

Nina mimba ya miezi 8, salama kungonoka?

"Hello dada dina nakupongeza sanaa kwa kazi nzuri haipiti siku moja mimi bila kuangalia blog yako kiasi kwamba nisipokuta updates naskia hasira...anyways dada dinah mi nina tatizo moja.

Mie ni msichana wa umri wa miaka 23,nimepata ujauzito wa rafiki yangu wa kiume wa miaka takribani 5, tulianza kufanya mapenzi mwaka jana tu yani baada ya miaka minne ya uhusiano wetu sasa maswali niliyonayo ni haya:kwanza sijafanikiwa kuskia utamu wa ku-come nikitombwa mie huskia kama nililambwa kisimi tu ntaanzaje kuskia hivo?

Nimefanya mapenzi mara tatu tu! ya tatu ndo nimepata ujauzito na sijafanya tena kwakuwa boyfriend alikuwa kikazi marekani ila anarudi jumatatu hii na tutafanya mapenzi.

Nina mimba ya miezi 8, je is it safe kufanya mapenzi?na style gani zitamchengua?nikivaa shanga je ntachemsha na mtumbo wangu?Nipo freshi kiafya sina matatizo ya ujauzito...nashukuru ukinijibu hayo. asante sana-KOKU".

Jibu: Awww umeshika mimba kabla hujautambua na kuujua mwili wako vizuri, kwanini hukutumia Condom? Usijali wala kujisikia vibaya kwani hatuwezi kubadili kilichotokea lakini naamini kabisa mara tu baada ya kujifungua na Mpenzi wako akiwa karibu utafanikiwa kuujua utamu wa kufanya mapenzi/ngono.

Kwa kuanzia mpenzi wako akija mwambie akupe ngono ya mdomo (akushukie chini) na kucheza na kisimi hakika utapata utamu wa ngono ukoje.......kwa maelezo zaidi mwambie aje kusoma Topic ya Zamia sasa hili ni kwa swali lako la kwanza.

Ikiwa Dakitari au Mkunga wako hajasema kama unamatatizo yeyote basi utakuwa salama kabisa kufanya mapenzi japokuwa unapaswa kuwa mwangalifu usije ukakorofisha au kushitua mambo mengine kabla ya wakati. Miezi nane ni mingi au niseme tumbo lni kubwa sana na hata wewe mwenyewe utakuwa umejichokea kiaina hivyo mikao utakayohitaji kufanya mapenzi ni ile ya ku-relax zaidi kama "spoony".

Ambapo baada ya kuandaliwa unalalia ubavu (natumaini ndivyo unavyolala kutokana na ukubwa wa tumbo) kisha yeye mpenzi wako analala kwa nyuma,kisha wewe unapanua mguu ili aweze kuingiza uume kisha rudisha mguu juu ya mguu mwingine (kama ulivyokuwa) na yeye anaendelea kukufanya taratibu mpaka wote mtakaporidhika au maliza haja zenu.

Vilevile mnaweza mkafanya kifo cha mende wewe ukiwa juu (kama umekaa vile) na hakikisha anakupeleka taratibu ikiwa huwezi ku-ride au kifo cha mende wewe juu lakini mpe mgongo (inaitwa doggie lakini sio hatari kama ile ya kuinama/bong'oa) nautazame miguu yake.

Kamwe suifanye mikao au mitindo mingine kama "doggie" zaidi ya hii mitatu. Have fun on Monday na all the best kwa kupokea mtoto mpya.

Friday, 23 May 2008

Mke wangu akerwa na Kitumbo......Ushauri!


"Dada Dinah. Naomba niweke swali langu tena hapa.Mimi nina tatizo kidogo nahitaji kusikia ushauri wako na wa wasomaji wote wa ukumbi huu mzuri.

Nina ndoa yangu kwa miaka sita sasa tuna mtoto mmoja na tunategemea mwingine Mungu akijaalia mwaka huu. Baada ya uja uzito wa kwanza tumbo la mke wangu halikurudi katika hali ya mwanzo, yaani alikuwa na kitumbo kinamna fulani. Lilipungua lakini si katika hali ya mwanzo au tuseme ya kawaida.Tumejaribu kutafuta tight ya tumbo lakini haikusaidia, ingawa labda haikuwa nzuri sana.

Sasa tukafikiri na kuona labda kabla hajajifungua safari hii tujaribu kupata utaalamu wa jinsi gani tunaweza kupunguza na ikiwezekana kurudisha tumbo lake katika hali ya kawaida, maana hata yeye mwenyewe inamnyima raha kiaina. Sasa ni njia gani nzuri za kutumia zisizokuwa na madhara kwa afya? Nitafurahi mno kusikia ushauri na kama tutafanikiwa katika hili."
Jibu: Napata matumaini kuona kuwa wewe mwanaume unaungana na tatizo linalo mkera mkeo na kutafuta namna ya kumsaidia ili ajisikie anavutia tena baada ya kujifungua (wanawake wengi hujihisi kuwa hawavutii tena) kitu ambacho ni muhimu ili kumrudishia Mkeo kujiamini kwake akiwa mtupu hali itakayo pelekea ninyi wawili mfurahie miili yenu kwa uhuru zaidi.
Upangiliaji wa mlo (diet) na mazoezi kwa ruhusa ya Dakitari wake ni muhimu kutegemeana na alivyojifungua kwamba amejifungua kwa kawaida (asilia) au kwa upasuaji.
Pamoja na kuwa kufanya mazoezi kuna-sound rahisi mama wengi hushishwa kuyafanya kutokana na uchovu au kuwa na shughuli nyingi zinazohusiana na swala zima la kuwa mama.
Kabla hajaanza mazoezi ya kupunguza na kulikaza tumbo lake baada ya kujifungua atapaswa kulifunga (kiasili au kibongo-bongo) na vilevile kujitahidi kupunguza unene ulioongezeka kutokana na ujauzito na anaweza kufanya hivyo kwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba, kutembea haraka-haraka n.k alafu baada ya kupunguza unene ndio afanye mazoezi niliyoyaelezea kwenye topic hii Mazoezi ya tumbo. Kila la kheri ktk kumpokea mtoto mpya.

Thursday, 22 May 2008

Dalili 1 kuwa anatereza/toka nje...

Habari za sasa mpenzi msomaji wangu, ni siku nyingine tena nakutana na wewe kujifunza mawili matatu, lakini kabla sijaendelea ningependa ku-share na wewe kitu kilichonitokea jana (D'hicious kutimiza mwaka) nilitolewa kwa ajili ya Mlo wa jioni (Dinner) na Pea mbili tofauti ambazo zimefaidika na kuboresha maisha yako ya kimapenzi hasa upande wa ngono na maelewano. Pea moja iligundua D'hicious na kuitambulisha kwa pea nyingine na matokeo yake D'hicious ikapata watu wanne zaidi ambao wanafaidika na Blog hii.


Kwa hiyo ilikuwa kind a party kwenye mgahawa wa kichina ambapo tulipata chakula kizuri na kubadilishana mambo mawili matatu na ofcoz kujibu maswali kiasi kuhusiana na mambo fulani which was fun kwa vile ni topic ambayo niko comfy sana kuizungumzia so tulikuwa na wakati mzuri sana na kama mnasoma hapa sasa.....kutoka moyoni nasema asanteni sana kwa kuonyesha mnajali.
************************************************************************

Bila shaka unakumbuka mwanzo wa mada hii, ikiwa hukumbuki basi pitisha macho hapo chini kwenye sehemu ya kwanza ya ili tuende sambamba. Unapogundua mabadiliko fulani ambayo yanahashiria kuwa mpenzi anatereza hupaswi kukasirika wala kujenga chuki na mumeo/mpenzi bali unatakiwa kuiandika upya kama sio kuibadilisha "script" kwa vile hakuna mwanaume anatoka nje bila kujua nini anakifanya, faida au hasara zake na jinsi ya kukuficha/danganya na kujitetea ikitokea atabambwa.


Kumbuka wanaume wanzungumza kama ambavyo sisi wanawake tunafanya (hasa wakiwa hawajaoa) na swala la kutereza (cheat) linapojitokeza wote hufuata mtiririko (Script)ule ule ila wanabadili kwa kukwepa/kutofuata yale yaliyopelekea wenzao kushitukiwa kama siokufumaniwa.


Dalili ya kwanza-Anapopunguza "attentions" na kutumia muda wake mwingi kufanya mambo mengine ndani ya nyumba na kukufanya ujihisi/sikie "lonenly in love" na unapoliweka hilo wazi anakulaumu wewe kwa kutokuwa na muda nae na wala halalamiki (najua utakavyojisikia lakini kumbuka nimesema hakuna kukasirika wala kuwa mkali) na badala yake jieleze kistaarabu kuwa huenda kufanya kwako kazi masaa mengi, kuangalia watoto au kufanya kazi nyingi ndani ya nyumba kuna kufanya uchoke sana na hivyo kutopata muda wa kuwa karibu nae lakini hiyo haina maana kuwa penzi limepungua au kuisha kwani unampenda kama mwanzo mlipokutana.


Kisha muulize ni kitu gani ambacho mlikuwa mnakifanya awali kwenye uhusiano wenu na sasa anakikosa......akimaliza kusema aku kuorodhesha basi mwambie hata wewe unakosa yote hayo na ungependa mambo yawe kama yalivyokuwa awali.

Na kuanzia hapo anza kujirekebisha na kufanya mambo ya fulani kama mpenzi na sio mume/mwenza au mama fulani. Hapa utakuwa umegundua anatereza na wakati huohuo umezuia asiendelee kwa kumpatia kilichokuwa kikimpeleka nje (usiulize kuhusu the other woman just show him how lucky he is to have u as a wife/mwenza).

Kila la kheri na endelea kuwepo kwa dalili ya pili.

Wednesday, 21 May 2008

D'hicious.....a Year on!Shukurani za dhati kwako wewe msomaji kwa ushirikiano wako, Rafiki zangu wote walioiweka D'hicious kwenye site zao kwa moyo mkunjufu na wenye furaha nasema Mungu awabariki sana kwa kuthamini mchango wangu ktk jamii ya Kitanzania "mtandaoni".

Katika safari hii ya miezi 12 nimekumbana na vishawishi vingi as you can imagine, nimekutana na kutengeneza mafariki wengi kutoka sehemu mbali mbali za Dunia, nimejifunza mengi kutoka kwa watu wengine na hata kukabiliana na "bullies".

Nisingekuwa nakiburi cha kuvuka miezi 12 na kusema nilichokisema leo hii bila ya Rafiki yangu mpenzi na wa Siku nyingi, Geeque aambae mimi huwa napenda kumuita "Jiikyuu" au GQ ambae siku zote usiku na mchana alikuwa pale kwa ajili yangu, huyu bwana ni kimbilio, nguzo na shujaa ktk maisha yangu "mtandaoni" ambayo time to time nilikuwa napata wakati mgumu kutokana na vitisho, abuse na vishawishi.

GQ unaja kabisa kuwa bila wewe D'hicious ingekuwa hadithi.......Asante kwa yote na Mungu akubariki sana.


Tuesday, 20 May 2008

Utajuaje anatereza/toka nje?

Mwisho wa wiki iliyopita nilikuwa BR having some fun nikaulizwa swali kuwa utatambua vipi kuwa Mume wako sio mwaminifu? Maelezo niliyoyatoa nadhani yalitosheleza swali husika.

Sipendi sana kuzungumzia mabaya yanayotokea kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini kwavile ni hali halisi au sehemu ya maisha ya baadhi ya watu wengine hali inayofanya baadhi kuhofia na pengine kujaribu kutafuta mbinu ya kuzia hilo lisitokee.

Natambua wazi kuwa hata wewe kuna siku huwa unahisi ungependa kujua kama Mpenzi wako hatoki nje ya uhusiano wenu, sio lazima iwe kimwili kama ambavyo wengi wanaamini ukweli ni kuwa uaminifu wa mwenza wako sio lazima uegemee kwenye Ngono tu bali inaweza ikawa kihisia, kiuchumi, au kimawazo n.k.

Mimi binafsi naamini kuwa unapokuwa na mume/mpenzi ni wazi kuwa mtakuwa mnajuana vizuri sana na mabadiliko yakijitokeza inakuwa rahisi wewe kufahamu kuwa kuna kitu kinaendelea.....wengi hutegea kuona "dozi" zimepunguzwa lakini ikimbukwe kuwa sio wanaume (hata wanawake) wote wanapunguza "dozi" za kungonona kwani inategemea zaidi na uwezo wake wa kutiana.

Kutambua mpenzi wako anacheza nje unatakiwa kuwa "smart" na hata kama umegundua "anatereza" hupaswi kuhoji kwa ukali bali ibua mazungumzo kuhusiana na tukio lingine (inaweza kuwa hata la kwenye movie" as long as ni "kutoka nje".

Nikirudi nitakupa vijimambo ambavyo mwanaume akivielezea/sema ni wazi kuwa anatereza. Usicheze mbali!

Monday, 19 May 2008

Mam'mkwe hanipendi je niolewe?...Ushauri

kelly said..."Habarini za saa hizi wadau wote wa dinah.... mimi jamani nina jambo linanitatiza ningependa dinah na wadau wengine mnisaidie, kama nimetoka nje ya mada basi mnisamehe bure.... mimi nina mchumba uhusiano wetu mpk leo unamiaka minne,mwaka wa tatu nilivalishwa pete sasa tatizo ni kuwa mchumba wangu hataki nionane na mama yake kwa madai mama yake mkorofi ila ndugu wengine wote nawajua nawananijua na wanataka tuoane hata kesho,kwetu pia anajulikana.

Yeye anaishi kwao na mimi naishi kwetu na kila siku tunaonana na weekend tunashinda wote.... ila linapokuja swala la mama yake yupo sehemu fulani basi hatutaenda hiyo sehemu ili tu nisionane na mama yake.... sasa wadau kama jamaa anataka niwe mkewe itakuwaje hapo?


Nilishaambiwa na wifi zangu kuwa mama yake hanipendi,na yeye ndio kipenzi cha mama yake,siku moja nilimwambia kama mama yako akikataa tusioane itakuwaje akasema ooh atake asitake mimi nikishajipanga nakuoa yeye shauri yake.

Kwa upande wangu mimi sitaki kuoana nae kama mzazi wake huyo hatokuwa radhi na pia sikotayari kumpoteza kwa vile nampenda sana..... wadau na dinah naomba msaada wenu wa mawazo kama nitakuwa sijaeleweka niulizeni nitawafafanulia pale ambapo hamjanielewa nawapenda wadau wote wa dinah "

Thursday, 15 May 2008

Shahawa zinaniwasha....


Mpendwa Waridi, samahani kwa kuchelewa kukujibu....

Uliniuliza kuwa kwanini Shahawa zinakuwasha? Ukaeleza kuwa tatizo hilo umekuwa nalo tangu umeanza uhusiano wa kimapenzi which means sio kitu kilichojitokeza sasa kwa jinsi nilivyoelewa mimi.

Jibu:Kwa kawaida Shahawa haziwashi au hata kusababisha muwasho unless hupatani nazo yaani uwe na aleji(Allergy to Semen/Sperm), kitu nitakachoweza kuhisi kuhusiana na tatizo lako ni maambukizo ya Fangazi/si au wengine huiita “Yeast” kitaalamu inajulikana kama “Candida Albicans” ambapo ule ukakasi/uchachu (unategemea na lishe ya mpenzi wako) unapoingia kwenye vijipasuka/vipele vilivyopasuka kwa ndani husababisha muwasho.
Nakushauri unamuone Daktari ili akupime (atahitaji mkojo au swab ya majimaji huko ukeni) kisha atakushauri na kukupa matibabu kutegemeana na tatizo alilotambua kwenye vipimo vyake.

Afya ya uke ni muhimu sana kuliko hata kinywa au uso wako na unatakiwa mwangalifu wakati unatumia sabuni, maji (chemsha ili kuwa na uhakika), vifaa unavyotumia kujisafishia ukiwa Gym au kama unaishai nyumba za kupanga zenye Kopo/bomba moja chooni, choo kwani kuna vyoo vimejaa kiasi kwamba ukichutama sehemu zako nyeti zinatishia kugusa vinyesi vya watu wengine, taulo la kujifutia na hata uchangiaji wa nguo za ndani (hata kama unafua kwa Jick) still unakuwa kwenye hatari ya kuambukizwa bila kujijua.


Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa usijisikie vibaya kwenda kumuona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kike kwa ushauri wa kitibabu hali kadhalika dawa, kwani dawa zinapatikana kwa wingi na nyingine zinaozea stoo kwa vile wanawake wanaona aibu kwenda kuomba ushauri ili kupata matibabu.

Magonjwa ya ngono kwa wanawake ukiachilia yale makuu kama kisonono, kaswende, UKIMWI n.k. yapo mengine madogo madogo ambayo sio lazima uyapate kwa kufanya ngono bali kwa njia nyingine zitokananzo na mitindo ya maisha tunayoishi, kutokujua/kutokujali afya ya uke, mabadiliko ya homono hasa kama wewe ni mtumiaji wa madawa ya kuzuia mimba n.k.

Kila la kheri na asante kwa ushirikiano wako.

Kelly jibu lako litafuatia soon.....endelea kuwepo tafadhali!

Utachumbiwa lini.......? Make him(II)

White Gold & Diamond!
4-Ni mwiko kuwa tegemezi, hakikisha unafanya kila uwezalo kuonyesha kuwa unaweza kufanya mambo yako kivyako bila kuomba-omba (vibomu) unless umekwama kweli kweli yaani malipo yamechelewa au biashara hajaenda vema mwezi huu na mwenye nyumba anatishia kukuweka nje, hakikisha tukio hilo halijirudii mara kwa mara.

Kumbuka kuzungumzia malengo yako ya baadae (sio ndoa) malengo yako kimaisha kwamba ungependa unatafuta kiwanja ili ujenge nyumba hata ya chumba kimoja Mungu akikujaalia, ungependa kununua shamba mahali na kufanya kilimo cha mboga-mboga n.k.

Sahau au usithubutu mambo ya kisistaduu uchwara ya ningependa kufungua duka la kuuza nguo, kufanya pati kubwa ya kuzaliwa kwangu au kununua Prado.....haitosaidia kwani ni kama vile unamwambia akupe mtaji.....zungumzia vitu vikubwa vya kudumu.....atakuona una akili ya kimaendeleo na unafaa kua wa milele Daima.


Sisemi kuwa usipokee zawadi au "mshiko" aki-offer si kajitolea bwana.....hiyo bomba lakini kale ka mchezo ka' kumfanya mpenzi wako kitega uchumi sio njema kwani kila mtu anamajukumu yake ujue! Mwanaume akionakuwa unaweza kujitegemea bila kuwa na kiburi (uswawa kwa sana)anakuwa na uhakika na maisha yenu ya baadae kama familia, na hivyo kusogeza swala la ichumbana ndoa karibu zaidi kuliko alivyopanga kuwa mpaka ajenge nyumba, kumiliki biashara kubwa n.k.


Kwani atajua wazi kuwa mtashirikiana na kufanikisha mambo haraka zaidi ikiwa mko pamoja kama mke na mume......ni kweli ukiwa mwenyewe kufikia malengo inachukua muda mrefu sana (kutokana na uzoefu wangu) lakini mkiwa wawili ktk ndoa malengo yanafikiwa chap-chap....kumbuka usemi usemao umoja ni nguvu na...........!

Hivyo mwanamke usibweteke fanya bidii ktk shughuli zako na onyesha kuwa unaweza kuweka tofauti ktk maisha yenu (ikiwa mtafunga ndoa) hali itakayomvuta mpenzi kutangaza ndoa.


5-Kamwe narudia tena kwamwe usiruhusu amalizie manii yake ndani hakikisha na ni mwiko kutumia madawa ya kuzuia mimba (kisa cha kubadili mwili/maumbile yako) kwa mwanaume ambae hajakuchumbia, hakikisha manatumia "condom".....Kwanza hurushisiwi kabisa kufanya ngono lakini kutokanana mfumo wa maisha wa sasa, wadada tunabaki shuleni kwa muda mrefu tofauti na miaka ile na kuizuia nature inakuwa ngumu hivyo inabidi tu ufanye ngono nje ya ndoa.

Sasa kama huruhusiwi kufanya Ngono b4 ndoa kwanini unamruhusu mwanaume akumwagie ndani wakati unajua kabisa uhusiano wenu sio "commited" kwa sasa....nina maana hakuna pete ya uchumba? Ukimimbika je?Kumbuka unafanya ngono kabla ya ndoa ili kufurahisha mwili na sio kujenga familia (which is the Main reason ya kukutanisha miili yetu kwamujibu wa Sayansi na Dini)......kama anakupenda kweli, yaani kafika mwisho wa Reli lakini unamzuia kumalizia ndani ni wazi kuwa ataharakisha mambo ya kutangaza ndoa ili apate uhuru.......wenyewe wanasema "kumiliki mwili wako nje na ndani".


Baada ya kufanya yote haya na mengine ya kumfurahsiha na kumridhisha kitandani na nje ya kitanda ktk mwaka mmoja na bado hajatangaza ndoa? Aaaah lazima kuna kipengele nimekiacha, sasa hebu niambie mpenzi wako anapenda nini zaidi yaani kama vipi anaweza hata ngono akaiweka pembeni ili amalize anachokipenda na ikiwa hakijaenda alivyotaka basi ngono inakuwa "out of the window".

Nikipata majibu yako then nitakupa Mbinu ya mwisho (nitaweka ktk mtindo wa Polls kulia kwa site hii) na baada ya hii (mbinu ya mwisho) ndoa haijatangazwa basi no matter how much you love the guy ujue you are not enough to be his wife acha kupoteza muda, tafuta ustaarabu mwingine, maisha mafupi atii!

Kila la kheri.

Tuesday, 13 May 2008

Utachumbiwa lini.......? Make him!

Wengi tunaamini kuwa matunda ya mapenzi ni ndoa na sote tunatambua kuwa ndoa ni jambo zuri, la heshima (wengi wanafeli hapa), busara na chanzo cha familia bora (japo kuwa mimi siamini sana hapa). Kinachosikitisha ni kuwa huu uamuzi huwekwa wazi na mwanaume na sio mwanamke hata kama wewe ndio unataka kuolewa yaani umefika bei n aunajua kabisa Haruna ni the one lakini Haruna mwenyewe khabari hana (well kama haruna (muislamu) na haja adopt tamaduni ya watu na yuko karibu au juu ya miaka 25 lazima atatangaza ndoa kwa mujibu wa dini yake) hivyo bora nitumie jina la Jonathan hahahahaha.

Nimeona hapo chimi M3 anasema wanawake tuwe wagumu kutoa K kwani akisha onja hataki tena, nasikitika kusema kuwa swala la ndoa M3 ni zaidi ya K na vilevile swala hili linachanganya kiaina. Wakati mwingine mimi huwa naamini kabisa kuwa ndoa ni mapenzi na uamuzi (labda kwa vile kila nilietoka nae kama mpenzi alitangaza ndoa), wengine wanadai kuwa ni bahati na baadhi wanasema ni lazima kama ilivyo ktk kuzaliwa na kufa, si unakumbuka sherehe 3 hapa duniani kuwa ni kuzaliwa, kuolewa/oa na kufa.

Watu nitakao walenga ni wale ambao wako tayari kwenye uhusiano na wanapendana lakini wanataka wapenzi wao wawasapuraizi kwa pete ya uchumba au hata kwenda kutambulishwa kwao kuwa wao ndio wapenzi wa kudumu.

Mpenzi akifika bei unamjua tu, wala huitaji vithibitisho si ndio jamani? Lakini mapenzi yake kwako sio tiketi ya yeye kukufanya wewe wa milele hivyo suibweteke nakusubiri siku akijisikia atangaze ndoa wengine mpaka uwaonyeshe kuwa "U can live with or without them" ndio wanajisogeza zaidi, sasa fuata haya yafuatayo:-


1-Ni mwiko kumkutanisha/tambulisha kwaa wazazi wako au kumpa namba ya simu ya nyumbani kama sio ya baba na mama (ya wazungu waachieni wenyewe) haruhusiwi kuwazoea bila kuji-commit. Kumbuka kuwa mwanaume anatakiwa kulifanyia kazi hili na kuhakikisha kuwa anakutana na wazazi wako nakujitambulisha ikiwa tu pete iko kidoleni na mnakwenda huko kutambulisha uchumba rasmi nakufuata taratibu nyingine za mahari, barua n.k. sio mmekutana leo kesho yuko sebuleni angalia Tv au kucheza na wadogo zako kama sio kuwapeleka kwenye manunuzi pale soko mjinga au kwenye maonyesho ya saba-saba.


Kama kwa bahati mbaya tayari amekwisha kutana na wazazi wako kabla ya makala yangu hii basi hakikisha hapati tena nafasi hiyo,mpaka kuwepo na pete au hata yeye kuandika barua nakulipa mahali nusu na robo (mana'ke sio wote wanaamini ktk pete).


Ikitokea shughuli kubwa kwenye Ukoo wenu kama vile sherehe za ndoa au Msiba hakikisha unakwenda mwenyewe bila yeye, ofcoz unamwambia nini nimetokea (msiba)au kinakwenda kutokea(ndoa) na akiomba kushiriki au kwenda na wewe mwambie ungependa awepo lakini hudhani kuwa ni wazo zuri kwani utakuwa busy sana (hutokuwa na muda wa kuwa pamoja kama wapenzi) na sio hivyo tu bali unajaribu kum-save na too much hassle.....hapa atakuona wewe ni wa maana sana nakuna uwezekano mkubwa siki za karibuni akataka uwe wake wa daima milele(Daima).....Usisahau kuwa hayuko pale kupendwa na ndugu zako na wala haitaji kupenda na kuzoea nyumbani kwenu.

2-Kamwe aah ni marufuku kuhamia kwake au yeye kuhamia kwako ikiwa kila mmoja wenu anajitegemea (anaishi kwake), wengi hukimbilia ku-move in wakihofia wapenzi wao kuchukua watu wengine na kulala nao.....skia wewe, achakuwa tegemezi kihivyo (emotional) utakimbiwa, kila mtu anahitaji nafasi yake time to time, swala la kulala na mtu mwingine kama lipo basi anaweza na mtu huyo hotelini, nyumba za kulala wageni au hata ofisini wakati kila mtu katoka....swalamuhimu ni mapenzi ya dhati na uaminifu.


Ikiwa ulihamia kwake ili ukamuonyeshe umuhimu wako kama "mke" yaani kupika, kusafisha, kupiga basi, kumpangia nguzo shati na tai nzuri kwa ajili ya kazini n.k. na bado Njemba haina dalili yakutangaza ndoa basi ni wakati wa kuhamia kwako peke yako kama sio kurudi kwa dada/wazazi, na kumbuka unapo hama bakiza kachupi kako kadogo ambako anakapenda kukaona maungoni mwako.


Ukihamia kwa mpenzi wako kabla ya kuchumbiwa, itamafanya ajisahau navilevile atakujua kwa sana yaani mambo mengine ulitakiwa uyafanye baada ya miaka 5 yandoa wewe unayafanya kabla hata ya uchumba na nina kuhakikishia ndoa haitoangazwa unless baba na mama'ke wamwambie "hey bwan' mdogo unataka tufe kabla hatujamuona mkwe na mjukuu "ndio atatuma posa? Yaleyale......!

Kuhamia kwake kunaruhusiwa ikiwa tu ametangaza ndoa na maandalizi ya ndoa yameanza (tunaita trial), alafu mwezi mmoja kabla ya ndoa unarudi kwenu....sio kwako....kwenu kwa wazazi au ndugu.

3-Ni mwiko kujifananisha ninyi na pea inayo au iliyofunga ndoa hivi karibuni, yaani wewe unatakiwakua "nunda" when it comes kwenye maswala ya ndoa au uchumba wa watu wengine, hasa kama yeye anaonyesha kutokuwa na habari (kawaida wanaume huwa hawana habari wala wivu) basi na wewe kuwa kama yeye.


Siku umeenda kumtembelea Mpenzi amabe kafika bei ila swala la ndoa halipo eti mpaka ajenge nyumba......lini? (kumbuka hakuna kuishi pamoja mpaka achumbie)ukiwa unaongea na rafiki yako amabe kafunga doa hakikisha unasema sentensi za kuponda ndoa kwa sauti ili mpenzi asikie tena kwa kunogesha muulize "hivi inakuwaje unaweza kuishi na mtu yuleyule kila siku iendayo kwa Mungu?" Mimi sidhani kama nitaweza, nahisi itakuwa boring"......hehehe kwa yote unayomfanyia nakumridhisha kitandani, kwa jinsi unavyompenda na kumjali alafu anasikia hivyo.....yaani akili itamjia Njemba nyingine zinaweza niwahi hapa......ataenda itafuta pete ktk siku zijazo, wewe subiri tu.

Hakikisha unayasema yote hayo kuwa unajua kabisa anakupenda kwa dhati na maisha bile wewe ni bora kifo.....mana'ke ukisema haya kwa player ujue kashinda na atakung'ang'ania na pete usiione alafu anaenda kuoa mtu mwingineee.

Nakuja...kumalizia....acha nitengeze vijiseti vya kusukuma mwezi.

Monday, 12 May 2008

Jinsi ya kumfanya Mpenzi atangaze ndoa!

Pete: White Gold,Diamond & Aquamarine.
Najua wengi mtakimbilia hapa mana'ke wanawake na ndoa ni kama vile inzi na kipindu-pindu au kashata na gahawa/kahawa anyway sitokuhakikishai kuwa nitakachokuambia kitafanya kazi kwani inategemea zaidi na mpenzi wako, malezi, mazingira,akili yake (yaani how open minded he is) na aina ya maisha yake.

Nakumbuka siku moja nilikuwa na marafiki zangu fulani (well wadada nafanya nao kazi) mmoja akasema kuwa "James lazima nimfanye anioe" nikajiuliza kwa sauti kuu huku na cheka (kidhani ni utani) unamfanyaje mwanaume atangaze ndoa? Ninavyojua mimi ni kuwa mnalizungumzia swala zima kisha mnasikiliziana kama nyote mna nia moja then siku moja mpenzi (mwanaume ndio anatangaza ndoa/posa) si ndio....hiyo kisasa.

Ya kizamani ilikuwa binti unajitahidi kuwa masafi na mwenye tabia njema kisha mwanaume anakuona kuwa wewe ni "ndoa type" then anakuja kwa wazazi wako kuposa kama sio wazazi wake wanakupenda kisha wanawashawishi wazazi wako wakubali uolewe na mwana wao wa kiume alafu from there ndio unaanza kujifunza kama sio kujilazimisha kumpenda aukumzoea kama mume wako ajae.

Kwa bahati siku hizi tunakuwa kwenye mapenzi na mapendo, kisha tunafanya nusu na robo kama sio yote yanayofanywa kwenye ndoa lakini jamaa halitangazi ndoa wala nini na wewe unahisi siku zinakwenda na huna mpango wa kuzaa nje ya ndoa.

Mwenyewe unajitahidi kumpena na kumuonyesha mapenzi yako, unaongeza ubunifu kitandani, unampa uhuru/nafasi yake anapohitaji kwenda kulewa (humfuatilii), mnakwenda kwenye sherehe za ndoa una-comment jinsi ambavyo siku moja ungependa naninyi mfanye hivyo.....yaani unampa dalili zote kuwa wewe ni a good wife, lakini Njemba haitangazi ndoa....!

Inaweza ikafikia wakati ukahisi uvumilivu umekushinda na umechoka kupotezewa muda na hivyo kuchukua uamuzi na kumwambia kama kweli unanipenda ungefunga ndoa na mimi siku nyingi so ama unanioa ktk wiki moja au uhusiano umekufa......hapo lazima atatangaza ndoa ili asikupoteze ikiwa kweli anakupenda au anajua unampenda na hakuna mtu atakae mpenda kama wewe ila tatizo la hii kitu ni kuwa wewe mwanamke ndio unaonekana Desperate kuolewa hivyo unakuwa umelazimisha......ni bonge la noma!


Nikirudi nitakupa mbinuz za kumfanya mshikaji atangaze ndoa na kuifanya itokee sio mnakuwa wachumba kwa miaka 3 wakati tayari mmeishi pamoja kama wapenzi kwa miaka 5.....it's boring bana.

Usicheze mbali.

Thursday, 8 May 2008

Nimekeketwa je kuna dawa....

Swali via mail linakwenda kama ifuatavyo:-
"Dear Dinah, Hope you are doing well, Samahani nina tatizo ambalo naona waweza kunisaidia mawazo, mimi ni mwanamke ambaye nimekeketwa nilipokuwa mdogo, kutokana na mila za kwetu kipindi kile. Katika kufanya mapenzi na mpenzi wangu huwa nacum na siku zingine huwa sifiki, siku akiniandaa vizuri huwa naenjoy na huwa nacum hata mara 2 kwenye mzunguko mmoja. Tatizo langu ni kwamba naamini kuwa wenye vinembe huwa wanafaidi mapenzi zaidi na zaidi kuliko tuliokeketwa, je kuna njia yeyote ya kitaalamu ama dawa yeyote inayoweza kurudisha kinembe kilichokatwa? Please nisaidie maoni. Ahsante kwa kutuelimisha kwenye blog yako. Its me Victim"

Kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa kuwa wazi ktk kulielezea swala lako. Ni jambo la kumhsukuru Mungu kuwa pamoja na kukeketwa bado unaweuwezo au niseme umejaaliwa kupata utamu wa kufanya ngono/mapenzi kwenye kona nyingine za uke wako hasa ndani ambwako wanawake wengi hawajui utamu wake.

Napenda nikuhakikishie tu kuwa utamu wa kwenye kisimi (kinembe) haufikii kabisa ule wa ndani ya uke hasa kama umejaaliwa kusikilizia/kupata utamu huo kisimini na ndani ya uke. Kwa mwanamke ambae hajawahi kabisa kupata utamu wa kungonoana (juu kwa juu au ule wa ndani) kwa sababu tofauti kuanzia mpenzi hataki au hajui kucheza namwili wako mpaka matatizo mengine ya kiafya basi Kisimi ni njia pekee na rahisi ya kumfanya apate uzoefu au idea ya utamu wa ngono ulivyo.

Kwa wewe kufanikiwa kufika kileleni ukiwa huna kisimi nadhani unafaidi zaidi kuliko yule ambae anakisimi lakini hafiki kileleni uume ukiwa ndani ya uke.

Nasikitika kusema kuwa hakuna dawa ya kurudisha kisimi/kinembe kwani kisimi sio kiungo kinachokua siku hadi siku na vilevile pale mahali hapo palipokuwa na kisimi palikuwa jeraha ambalo limepona na kuwa ni kovu na juu ya kovu huwa hapajitokezi/kua kitu hata kipele huwa hakioti juu ya kovu.

Kuna njia ya kitaalamu (Plastic Surgery) ambapo huumba/tengeneza kisimi cha bandia (kutokana na sehemu ya nyama mwili mwako) kisha wanaunganisha na mabaki ya "nerves" za kisimi (kwenye jeraha) lakini inategemea zaidi na walivyokiondoa, inasemekana baadhi huwa hawaondolewi sana na wengine wanakwanguliwa kabisa. Upasuaji huu unagharimu millions za kitanzania, maelfu ya Kimarekani na Uingereza.

Wednesday, 7 May 2008

Mpenzi hataki kushukiwa, je ni kwanini?

Ni swali nililopokea sikuc hache zilizo pita kwa mail na linakwenda kama ifuatavyo:-
"Dinah, mimi ni mwanamke ambae nimekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa miezi tisa sasa, tangu tumekuwa pamoja nimegundua mpenzi wangu sio mtundu kama ambavyo wanaume wengine hivyo siku moja niliomba anishukie chumvini na akafanya hivyo bila shida na tangu siku hiyo kila tukitaka kufanya mapenzi lazima anishukie.
Lakini cha kushangaza nikitaka kumshukia yeye anakataa, hasemi kuwa sikaki ila unaona tu anakwepa kwa kuanzisha kitu kingine amabcho kinanifanya nishindwe kumfikia kule chini na kama ulivyowahi kusema kwenye makala zako za nyuma kuwa kama mtu hataki kufanya jambo tusimlazimishe, je wewe unafikiri ni kitu gani kinamfanya akwepe kushukiwa?Ash."


Jibu langu:
Ash asante kwa swali lako ngoja, swala muhimu la kuzingatia ni kuheshimu matwaka yake nakutojisikia vibaya kwa vile hataki umpe mdomo (ajabu kweli wanaume wengi wanapenda kushukiwa lakini kushukia wake/wapenzi wao huo mbinde), huyu wako anahitaji pongezi kwa kujali hitaji lako na kukuridhisha.


Unajua baadhi ya wanume pia huwa hawajiamini kimaumbile kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake, sote tunatambua kuwa swala la kupena midomo huko chini ni "intimate" sana hivyo mtu mpaka anakuruhusu kuweka mdomo au hata kuangalia tu anahitaji kuhakikishiwa kuwa sehemu yake inavutia, nzuri, safi, kubwa (hata kama ndogo sema tu kubwa auinakutosha au unapiepnda kama ilivyo) mana'ke wanaume ni "insecure" linapokuja swala la uume.

Yaani akijihisi kuwa "mzigo" wake ni mdogo au aliambiwa na mpenzi wake wa awali kuwa "abdalah kichwa wazi" hafiki popote hata kama sio kweli still mwanaume huwa ana-mind na kupoteza kujiamini kwake.


Sasa basi, huenda hajiamini kuwa uume wake ni mkubwa wa kutoshwa kunyonywa hilo moja, pili inawezekana kabisa ikawa anahofia "kucheka" a.k.a kumwaga kabla hujafika popote (kwa wanaume wengi hili ni tukio la aibu sana), tatu labda anajua kuwa uume wake hauvutii kwa vile labda anangozi chafu, au makovu/mabaka kutokana na mapele (kumbuka kuna magonjwa ya ngozi na ya zinaa).


Swala muhimu na la kuzingatia ni kuzungumza kuhusiana na jinsi gani ungependa kuonja uume wake, onyesha kuwa unapenda kufanya hivyo zaidi kuliko kurudisha kile anachokufanyia (kulipa), hakikisha unazungumzia hilo wakati mmepumzika tu hamna mpango wa kwenda kungonoana na wakati unaongea jaribu kuweka mkono wako juu ya "mtuno" wa kaptura/suruali yake na kumpapasa.


Jambo lingine muhimu ni kujifunza kusifia maeneo yake hasa "kiungo" chake, njia rahisi ni kuoga pamoja ili iwe rahisi kwako kuuona uume wake, unaweza ukamkanda "full body" lakini kwa kuanzia mapajani akiwa kalala chali kwani akilala kifudi-fudi(lalia tumbo) itakuw angumu kwako kumkanda uume wake. Tafadhali rejea jinsi ya kukanga kwenye makala za nyuma.


Ikishindikana basi usilazimishe kwani sio lazima, kila mtu anafurahia na kuridhika kivyake sio lazima umfanyie vile anakufanyia wewe.

Tuesday, 6 May 2008

Ngozi yako...
Hatuwezi tukazungumzia swala la kungonoana bila kuhusisha ngozi, Ngozi laini, safi na isiyo na mabonde, mikwaruzo wala ukavu huvutia sana sio tu kwa kuiangalia bali hata kuishika na kuichezea. Miaka ya nyuma bibi zetu walikuwa wakitumia pumba za mahindi, Unga wa liwa na machicha ya nazi kusugua miili yao na pia binti/mwanamke alikuwa akipaswa kukaa ndani kwa muda fulani wakati “treatment” hiyo ikiendelea ili kuwa na ngozi nzuri, laini na yenye kuvutia kabla hujaolewa/funga ndoa.


KUWA na ngozi laini au ngozi nzuri wakati umri wako ni mkubwa (miaka arobaini na kuendelea) si rahisi kama ulivyokuwa awali hivyo unahitaji kufahamu ni vitu gani vinavyoweza kusababisha uharibifu wa ngozi (kukunjamana/ukavu) na hivyo kuchukua hatua madhubuti za kuepukana navyo. Vilevile nitakupa njia za kiasili na za kisasa za kukabiliana na hali hiyo, lakini kabla napenda nieleze yafuatayo.


Baadhi ya wanawake (hata wanaume) wanapofikia umri huu ngozi huaanza kuwa kavu, nyepesi, mistari hujitokeza sehemu ya juu ya uso (paji), kuzunguuka midomo, macho (juu na chini), vilevile ngozi hupoteza rangi yake ya awali usipo kuwa mwangalifu na kuijali ngozi yako..
Hali hiyo husababishwa na kutoondolewa haraka kwa chembechembe zilizokufa chini ya ngozi na kufanya ngozi yako kupoteza vitu vifuatavyo:-

-Mosi, hali ya kujibadilisha/kujitengeneza upya na kurudia katika hali yake ya awali ikiwa itahathirika.
-Pili, hali ya kujikunjua ,
-Tatu, hali ya kuhifadhi maji na kusababisha ukavu na matatizo mengine ya ngozi.
-Nne, ngozi haitaweza kudhibiti miale ya jua ijulikanayo kwa kitaalam kama “UVA” na “UVB” kwani haitakuwa na chembechembe ziitwazo “melanin” ambazo huilinda ngozi.


Yote hayo kwa kitaalamu hujulika na kama “melanocytes”, hivyo ni vyema ukafahamu kuwa jinsi umri unavyozidi kwenda ndio uwezekano wa kuwa na ngozi mbaya unaongezeka ikiwa hutoiepusha ngozi yako dhidi ya miale ya jua.


Vilevile mwanamke unapofikia umri mkubwa zaidi na kuelekea kwenye mabadiliko ya mwisho ya mwili wako ambayo husababishwa na kwenda mwisho wa hedhi au kukoma Hedhi (MENOPAUSE) ngozi yako wakati huu itahitaji matunzo maalum au ya ziada ili ibaki katika hali nzuri yenye afya na kuvutia, unapaswa kuacha kabisa vitu vifuatavyo:-


-Unywaji wa pombe ( aina yoyote ya kilevi) kwani huuwa vitamini A,B na C ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi.

-Epuka matumizi ya sabuni zenye au zilizotengenezwa kwa acid kwani hukausha ngozi.

-Uvutaji wa sigara amabazo hutokana na tumbaku (hii ni kemikali) huchafua damu kwa kuikosesha “oxygen” hali ambayo husababisha ngozi kujikunja .

-Usipende kutembea au kukaa juani kwa muda mrefu,wengi hupendelea kuota jua la asubuhi ambalo ndilo husababisha mikunjo kwa asilimia Themanini.

-Epuka madawa makali ya kuchubua ngozi a.k.a Mkorogo.

-Usipende kujiweka katika wimbi la mawazo kwani hali hiyo pia husababisha uharibifu wa ngozi, jitahida kuwa na furaha ( hata kwa kujifanya) wakati wote ilimradi tu sikunjaeuso wako.

-Usipake vipodozi vingi na ikiwezekana paka unapohitaji na isiwe kama sehemu ya muonekano wako.

-Acha au punguza kunywa kahawa, pia usile vyakula vyenye mafuta yasio ya asili (vyakula vya kukaanga).

Vitu muhimu vya kuzingatia ktk utunzaji wa ngozi yako.
-Krimu na vifaa vyote vya urembo vilivyopo duniani havitaweza kukusaidia ikiwa wewe mwenyewe hukuijali ngozi yako tangu mwanzo lakini ulaji wa mboga-mboga, matunda na mazoezi vitakupa/kukuongezea chembechembe zote zilizokufa na kunyoosha ngozi yako kuliko krimu ya usiku ambayo ni ghali.

-Kuwa na lishe nzuri/bora (mara 3kwa siku) na kila ukiandaa usikose kuweka mbogamboga na matunda, pia hakikisha kuwa chakula chako kina virutubisho vyote vya vitamini A, B ,C na E, vilevile iron, magnesium, potassium,zinc n.k. ambavyo mara nyingi hupatikana kwenye vyakula vikavu.

-Safisha ngozi yako mara kwa mara na vilevile isugue kwa kutumia machicha ya nazi (kwa vile yanamafuta asilia ambayo nadhani yana vitamin E na usione noma hakuna atakae kuona) unaweza hata ukaomba mwanao au mumeo akusaidie sehemua mabzo huwezi kuzifikia kama vile ktk ya mgongo n.k.

-Unaweza pia ukaongezea vyakula vyenye vitamini B1 ,2 ,6,12 ,vilevile unapaswa kunywa maji kwa wingi ili kuongeza “oxygen” kwenye damu, hulainisha ngozi, huimarisha homono .nk.

-Mazoezi ya kawaida (sio yale ya “shape up”) huimarisha ngozi kwani hufungua vijitundu vidogovidogo na kuruhusu “oxygen” kuingia kwa urahisi kwenye kila chembechembe (cell) za mwilini, kwenye “hormone” ambazo hulisha ngozi na kuongeza “OESTROGEN” ambayo husaidia kuifanya ngozi kuwa katika hali ya Ujana (kunyooka).

Nikirudi nitakupa njia za kisasa ambazo zitawafaa wale amabo wanaishi sehemu amabzo hakuna machicha ya nazi.......nakuja!

Friday, 2 May 2008

Hatubadiliki bali tunakua/pevuka

Sote huwa tunasikia kama sio wewe unauzoefu tayari wa kulalamikiwa na mpenzi kuwa tumebadilika. Utasikia mkizozana kidogo mwenza wako anasema "siku hizi umebadilika sana, zamani hukuwa hivi" anaweza hata akakupa mifano hai lakini wewe unaweza ukabisha kwa nguvu zote na kushangaa au kujiuliza umebadilika nini? Mbona uko vilevile tu kitabia na kimuonekanao.


Lakini katk hali halisi huwa kuna kuwa na mabadiliko makubwa sana(ukuaji), wewe huyaoni kwavile ni sehemu ya ukuaji wako hivyo unabadilika automatically bila wewe kutambua. Ukiangalia nyuma ulipokuwa teen ni tofauti na sasa ambapo uko kwenye early 20s na unapofikia late 20s utakuwa na tabia tofauti na hapo awali hali kadhalika unapofikia miaka 30, 40 na kuendelea.


Wenza wengi hugombana na kutofautiana kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa vile huwa wanategemea wapenzi wao waendelee kuwa vilevile walivyo kutana nao miaka 6 au 15 iliyopita. Hawajui kuwa inategemea zaidi umekutana nae akiwa na umri gani, ukikutana na mpenzi yuko kwenye late 20s au early 30s huwa hakuna mabadiliko......lakini kama ulioa/olewa nyote mkiwa watoto au mmoja wenu ni chini ya miaka 27 basi mimi hapo wala sina la kuongeza!

Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo? Unanyongeza? basi nafasi ni yako.....

Mwisho mzuri wa wiki. XXX

Thursday, 1 May 2008

Vijana wa sasa wanaharaka sana

Tofauti na zamani vijana sasa wamekuwa wakihofia zaidi kukutana na "the one" mapema zaidi ktk maisha yao kuliko kufanya bidii na kuzingatia masomo ili ufike mahali fulani kielimu au kimaisha (kazi/biashara), natambua kufaulu mitihani sio kufaulu maisha na kufeli mitihani sio kufeli maisha ni wewe tu na mipangilio yako si ndio jamani au?


Sina hakika ni nini hasa kinapelekea mfumuko wa hawa Dogo wengi kutaka kufunga ndoa au kuwa na wapenzi ktk umri mdogo badala ya kuzingatia masomo au pengine kufurahia maisha yao kabla ya kuongeza majukumu mengine kabla hata miili na akili zao hazijakomaa.


Sio kwamba na pinga kuwa na mpenzi au kwamba huyo "the one" hayupo au hapatikani hapana, unastahili kuwa nampenzi kutokana na matakwa ya mwili wako lakini sio kwa kumsaka na kupoteza muda mwingi kwenye "sites" za kutafutia wenza, wachumba au mahusiano ya kimapenzi au maeneo ya vilabu vya usiku, hotels kubwa, maeneo mengine ya starehe.


Katika hali halisi penzi huwa halitafutwi bali hujitokeza lenyewe tu ikiwa moyo wako utampenda mhusika, sasa kitendo cha kuanza kwenda kujiandikisha kwenye hizo "sites" kutafuta wenza ktk umri wa miaka 17-24 mimi binafsi nahisi kuwa ni kujipotezea muda na kujiongezea "stress" ambazo sio za msingi kabisa kwenye maisha yako ktk umri huo mdogo.


Baadhi yao wanajitosa kwenye "dating sites" au "maeneo ya starehe ya wanaojiweza" ili kukutana na wanaume/wanawake ambao tayari wamejijenga ili yeye akiingia kwenye uhusiano huo aweze kutumia vile ambavyo mwenzake amevihangaikia na kuvitolea jasho ili mtaani wamkome, sisemi kuwa huna haki ya kutumia mali (nyumba, gari, pesa) ya mume/mke au mpenzi wako kama anakuruhusu kufanya hivyo lakini huitaji ku-focus kwenye kutafuta mpenzi mwenye aina fulani ya maisha kwani kwa kufanya hivyo sio haki.

Sasa imefikia hatua hapa nyumbani (bongo) kuwa na boyfriend au girlfriend ni lazima kama vile kula au kuoga kama sio kuvaa chupi, unakutana na vitoto vidogo ndio kwanza vimemaliza shule ya Sekondari vinahangaishana mtaani na kwenye kumbi za starehe kama sio online kutafuta "the one".

Achana na swala zima la kuhaha huku na kule kutafuta mpenzi ktk umri huo mdogo na badala yake zingatia kitabu au kazi, tunza mapato yako na furahia maisha yako na huyo "the one" muda ukifika utakutana nae tu.


Wewe unasemaje kuhusu hili?......karibu.