Tuesday, 29 April 2008

Utajuaje ni "Good in bed"

Hili ni swali nimelipokea kutoka kwa msomaji wangu na linakwenda kama ifuatavyo;

"Dada Dinah nimekuwa nikisikia watu wakisifia wapenzi wao kuwa they are good in bed lakini nashindwa kuelewa ni kitu gani hasa kinapaswa kufanywa ili na mimi niwe good in bed? Amisha."

Amisha asante kwa mail, kuwa mzuri kitandani inategemeana na mpenzi wako ni kama vile uzuri wa sura, upo machoni mwa mtazamaji au mwenye macho sio wote watakao kuona mzuri.

Hali kadhalika ktk ufanyaji wa mapenzi ni hivyo, kuna baadhi ya wapenzi ukuwa unaweza kumfikisha kileleni kila mnapofanya basi wewe ni bingwa, wengine ukiwa unabadili mikao na mitindo kila dakika tano basi wewe ni championi (u dont actually enjoy) lakini ndio hivyo tena kwake ni hakuna kama wewe duniani vilevile kuna wale ambao wanahesabu mara ngapi mmefanyana kwa siku na kwao wewe ni bonge la mpenzi.

Pia wapo wale ukipiga kelele wakati unafika (hajawahi kupigiwa kelele) basi atakuona wewe ni bab-kubwa kunako kitanda, bila kusahau wale kuna baadhi pia ukiwapa ngono ya mdomo, kunywa na kumeza shahawa wanatangaza ndoa hapo hapo........nakadhalika.

Hivyo inategemea zaidi na mpenzi wako japo kuwa sio mbaya ukiwa mbunifu na kuboresha namna ya ufanyaji wako mara kwa mara.

Hebu tuambiane leo (wake kwa waume) unafikiri ni kitu gani mpenzi wako akikifanya wakati mnafanya mapenzi utampa sifa kuwa ni mzuri kitandani?

Mimi nitalianzisha hapa na wewe endelea sio? Poa,
Mimi binafsi nitakuona mzuri kitandani ikiwa utakubali Condom itumike kama kinga ya mimba (japo tumefunga ndoa), unajua tofauti kati ya kungonoka na kufanya mpenzi, vilevile kutumia muda wako na kufurahia kile tunachokifanya, bila kusahau kutowekeana "limit" yaani niachwe niwe huru kushika na kuramba popote.....

Na wewe je?.....karibu.


Monday, 28 April 2008

Mpenzi anaporudi "the old fashion"

Unakumbuka nilikupa maelezo ya mwanamke wa zamani alikuwa akifanya nini pale mpenzi/mume wanapokwenda safari? Nia na madhumuni ilikuwa ni kukupa nafasi wewe kuelewa nini kilikuwa kikitokea wakati ule alafu chukua moja au mbili (jifunze) kisha changanya na yale uyajuayo sasa (ya kisasa). Sasa leo hapa namalizia sehemu ya pili ambayo ni kitu gali kilikuwa kikifanyika mpenzi anaporejea kutoka safari ya mbali.Kitu cha kwanza kilichokuwa kikifanyika ama kufanywa na mwanamke anapomuona mume wake kwa mara ya kwazna tangu walivyotengana (kwenda safari) ni kumsoma kwa macho yuko katika hali gani.....afauraha, ucchovu, hasira, mgonjwa, kukata tamaa n.k. alafu ndio anamlaki mumewe huyo kwa kutegemeana na hali aliyonayo mpenzi wake.Kumbuka kuwa wakatihuo hakukuwa na mawasiliano kama sasa kwamba unajua kama sio kusikia kitu gani kinaendelea kabla hata hujamuona mtu hivyo unakuwa umejiandaa na jinsi ya kumpoke si ndio?Sasa kwa mfano mume hana furaha au mchovu au amekata tamaa mwanamke alikuwa akimlaki kwa furaha lakini sio ile kumkimbilia na kutaka abebwe (jitu lina hasira/huzuni linaweza kukumwaga kwenye majani/chini)....baada ya hapo mume alikuwa akichukuliwa moja kwa moja bafuni/kwenye jiwe/kigoda/stuli kusafishwa kisha anafunikwa na blanketi, shuka au khanga (kaniki) alafu anakandwa sehemu ya pembeni ya kichwa chake kwa kutumia kitambaa kilicholowanishwa kwa maji joto ili kumpunguzia msongamano wa mambo/usumbufu alionao kichwani yaani kumfanya a-relax.Baada ya hapo kilikuwa kikichukuliwa chungu kikubwa au karai leye maji ya joto yaliyochanganywa na mafuta ya karanga alafu unatumbukiza miguu yake humo na kuanza kuikanda nakuikausha mara tu unapomaliza shughuli ya ukandaji.

Mume anaongozwa chumbani kisha alawa kitandani ili apumzike wakati mwanamke unaenda kuandaa chakula (zamani chakula kilikuwa kikipikwa ukiwa nyumbani na sio kabla kwani hakukuwa na vitunza joto/moto) na wakati unaandaa chakula hicho basi unaweza ukawa unaimba nyimbo mbali mbali zinazoelezea unavyojisikia au kilivyokuwa ukijisikia kutokana na upweke au kuonyesha jinsi gani unampenda mumeo.

Pole kwa kukusolemba, tuendelee kama ifuatavyo!

Chakula kikiwa tayari mwanamke humfuata mumewe na kumkaribisha, kwa kuanzia anaweza mlisha tonge mbili-tatu kabla hajakaa na kuanza kula nae. Wakati wanakula ndio wakati wa kuanza kuongea na kuuliza maswali ya huko alikotoka, safari ilivyokuwa na jinsi ulivyotaabika na upweke bila kusaha furaha yako iliyoje kuwa nae tena.

Ulikuwa ukidhaniwa kuwa huu ni muda muafaka kwa vile tayari ameonyesha anamjali, umempunguzia stress na kumfanya awe-relaxed zaidi hivyo atasikiliza na kuelewa kile unachomwambia tofauti na kama angeanza kuwakilisha hoja na malalamiko (ya mama mkwe mfano hahahaha) mara tuu baada ya kumuona.

Pia ulikuwa ni wakati mzuri kuliko kusubiri mpaka mko kitandani, kwani ni wazi kuwa ktk ile nyanja kusikiliza na kumuelewa mwenzio huwa sio rahisi kutokana na wingi wa nyege as you can imagine mtu ndio kajitokea safari lazima mambo fulani yawe mambo.

Sasa baada ya mlo kumalizika ndio unafuata ule wakati wa kujimwaga ktk kufanya mapenzi na kuonyesha ufundi na manjonjo yako uliouongeza wakati yeye hayupo.

Ikiwa narejea akiwa mwenye furaha kabisa yaani yuko kawaida mwanamke alikuwa hajitumi sana kama ambavyo nimeeleza hapo juu.

Friday, 25 April 2008

Uwezo/kuwa na hamu kubwa ya kungonoka!

Sehemu kubwa ya jamii yetu ya Kibongo hawajui kuwa kuna watu wanauwezo mkubwa wa kufanya ngono au hamu ya kufanya ngono huwa haiwaishi mpaka wafanye zaidi ya mara tatu kwa siku ktk siku saba za wiki yaani mara tatu kila siku. Hiyo hali sio pepo na wala sio kujiendekeza bali nisehemu ya mahitaji muhimu ya mwili wako. Kuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi haina maana kuwa huwezi kuishi bila kufanya kwani wewe sio "addicted" hivyo unaweza kabisa kujizuia.

Wanaume wengi Tz kama sio Afrika nzima wanaamini kuwa mwanaume hawezi kuridhika kingono na mwanamke mmoja na wanawake wanaamini hivyo lakini ktk hali halisi hilo sio kweli kwa vile inategemea zaidi na "libido" yako kama iko juu au chini na sio wanaume pekee wenye uwezo mkubwa wa hamu ya kungonoana bali hata wanawake.

Kuna tofauti kati ya kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya ngono (high sex drive/libido) na kuwa "addicted" na ngono. Unapokuwa "addicted" ni tatizo au niseme utahitaji kupata msaada wa kitibabu au Therapy kama ilivyo kwenye "addiction" nyingine kama vile madawa yakulevya, Sigara, Pombe, Parting au kuwa mpenzi wako.

Unapokuwa "addicted" huwezi kutulizana mpaka upate kile unachotaka na vilevile kuwa sio lazima ufanye mara nyingi kwa siku bali unaweza ukafanya mara moja kila siku na hutoweza kupitisha siku mpaka "ushitue", mtu kama huyu uaminifu kwake huwa zero kutokana na tatizo lake.

Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo na ninakutakia mwisho mzuri wa wiki. C ya!

Thursday, 24 April 2008

"Cheating" inaweza....(mwisho).

Kama nilivyosema awali kuwa “cheating ziko za aina tofauti” na kuna zababu zinazopelekea hilo kutokea. Kuna ile ya bahati mbaya ambayo inaweza kutokea leo n aisitoke tena nakuna zile mbili ambazo ni zaidi ya usiku au siku moja hukua na kukomaa kabisa ambazo huwa tunaita “Affairs”.


Tofauti yake ni kuwa watu wawili wanapendana na wanajua kabisa kuwa mmoja wao au wote wako “commited” na wake/waume zao lakini wanakubaliana kuwa na uhusiano wa kingono na kimapenzi na yanaweza kabisa yakawa ya dhati.


“Affair” inaweza kushamiri, ikapendeza, ikakufunza nini maana yakupenda na kupendwa kama vile hujawahi kupenda ktk maisha yako yote na huenda ikaishia pazuri kabisa au pengine ikwa ndoa ya kwanza kwako na ya pili kwa mwenzio lakini wakati huohuo inaweza ikaharibu, kuumiza, kuchanganya, kukupotezea muda na kukatisha tamaa ya kimaisha/maendeleo, ikakupa upweke hujawahi kuupata ktk maisha yako yote kama sio kubadilisha kabisa ujinsia wako.


Sio kuwa nakubaliana na swala hili ila najaribu kuzungumzia hali halisi na kwa uwazi, unajua hii inapotokea upande mmoja huomba au kulazimisha kama sio kushawishi mpenzi wa mwenzie kuachana na yule aliyeji-commit nae ili waishi pamoja, hii inatokea maranyingi kama mwanaume/mwanamke kaweka wazi kwa mpenzi wa nje kuwa ndoa yake sio yenye furaha kama zamani au kunavitu havimfurahishi huko nyumbani n.k.


Huwa wanajaribu kwa hali na mali kuhakikisha unapata kile unachokitaka ili ubaki nao na usirudi ulikotoka. Kinachosikitisha nakuudhi kwenye hili ni kuwa sio wewe tu utakaeumia (mke/mume) wake bali familia nzima ikiwa ni pamoja na watoto kama mmejaaliwa kuwa nao.


Hali inapofikia hapa kung'atuka huwa ngumu kwa wewe unaeishi maisha ya aina mbili tofauti, unapaswa kuchagua moja ama kumaliza uhusiano wako wa nje kwa kuliweka wazi hilo au kuachana na mke/mume/mpenzi wako ili uwe huru kufanya ufanyalo na yeye awe huru kuishi maisha yake bila kuumizana au kutesana na wakati huohuo kuzingatia nakuthamini maisha ya baadae ya watoto na kujitahidi kuendelea kuwa wazazi japokuwa penzi halipo.


Kumbuka tu kuwa penzi halilazimishwi na kwama ukipenda au kupendwa haina maanakuwa mpenzi wako hawezi kupendwa na watuwengine, unachotakiwa kufanya ni kuboresha penzi lako kila siku na kuzingatia zaidi nini una-offer au uta-offer kwenye uhusiano wenu na sio kutegemea upande mmoja ufanya hivyo kwa vile tu umeoa/olewa au mmeoana.


Uhusiano wa mapenzi hasa ukifikia kwenye ndoa unahitaji kuufanyia kazi na kuwa mbunifu kila siku huruhusiwi kujisahau na hii sio kwa wanawake tu bali wote wake kwa waume kwani “affairs” zinafanywa na jinsi zote mbili.

****Hii ni topic ndefu mmno naomba niishie hapa na wewe ongezea au uliza maswali kutokanana uzoefu wako ktk hili na mimi nitajibu na ktk kujibu kwangu ndio itakuwa muendelezo wa topic hii. Asanteni.

Wednesday, 23 April 2008

"Cheating" inaweza....(II).

Naomba niweke sawa hapa naona nimechanganya baadhi ya watu, nimesema “cheating” inaweza kuokoa uhusiano wako na sio kuwa inaokoa uhusiano wako. Hapo nina maana kuwa ikitokea mpenzi wako ame-cheat haina maana ndio mwisho wa dunia, maisha yanaweza kabisa kuendelea na penzi lenu likawa limesimama imara kama mwamba na hakuna wa kuliharibu/angusha.

Huenda kuwa haijakutokea wewe au mimi, lakini kumbuka hapa hakuna wewe na mimi tu bali kuna watu wengi ambao hili limewakuta kama sio kuwatokea, mimi binafsi siku baliana na tabia hii lakini kama mwandishi wa haya mambo ni vema niangalie pande zote na kusaidia yule au huyu ili sote kwa pamoja tuishi kwa amani na furaha.

“Cheating" inapotokea kwenye uhusiano swala muhimu ni kuzungumzia kilichotokea kama unaweza kufanya hivyo siku hiyo vinginevyo unaweza kuomba nafasi (kutengana kwa muda) ili uweze kuwaza na kuwazua hatua gani uchukue na kufanya uamuzi wa busara.

Moja, Jipe muda mbali nae na huko Jiulize je unampenda mpenzi wako? Je unadhani unaweza kumuamini tena? Unafikiri unahitaji maelezo kwanini kafanya alichofanya? Unaweza kuzungumza na marafiki zako ndugu na jamaa kuhusu tukio zima lakini waombe wasikushauru bali wakupoze nakukupa matumaini kwani ushauri wao unaweza kuharibu badala ya kujenga, wakati huu unachohitaji ni kulitafakari hilo wewe kama wewe kwani ndie pekee unaempenda, unaeishi,/uliyeishi na kumjua vema mpenzi wako.


Pili, baada ya kufikiri nakutafakari ukaona mpenzi anastahili kuwa nawe basi nenda na omba maelezo ya kina kwanini kafanya alichokifanya (lazima atakuwa kesha sema mengi by now nakuomba misamaha yote) lakini msamaha kwa tafasiri yangu ni mabadiliko hivyo aliye-cheat atapaswa kuachana kabisa na mwanamke/mwanaume wa nje (unaweza ukamaliza hilo mbele ya mpenzi wako na huyo mtu wa pili), kubadili mawasiliano na kama ikiwezekana basi kazi ubadili kama sio kuhama mtaa.


Mkosaji itabidi atafute namana au njia ya kurudisha umaminifu na mapenzi kwenye ushusiano wenu. Usijilazimishe kufanya mambo amabyo unahisi yanakurudishia kumbu-kumbu ya kilichotokea hata kama hukuona lakini lazima utakuwa na hisia hizo na itakuchukua muda mrefu lakini u'll get over it.


Baadhi huwa wanajilazimishakufanya mapenzi wakihofia kuwa mpenzi ataenda tena nje, ktk hali halisi jambo kubwa kama hili likitokea na ummempa nafasi ya pili mpenzi wako huwa ana-focus kwako tu na si kwingineko.....hivyo jipe muda utakao mpaka utakapo kuwa tayari.
Wewe unaesamehewa (mkosaji) usidhani kuwa mpenzi wako atasahau haraka kama alivyosamehe hivyo unatakiwa kuwa mvumilivu na kufanya kazi ya ziana ili kurudisha uaminifu na mapenzi kwa mkeo/mumeo/mpenzio.


Tatu,Kutokana na maelezo yake ya wazi ya kwanini alifanya alichofanya lazima utahitaji kubadilika. Usibweteke kwa kudhani kuwa kwa vile yeye ni mkosaji basi ni yeye pekee ndie anapaswa kubadilika, hapana kumbuka kwenye uhusiano kunapaswa kuwa na ushirikiano ili kuufanya uhusiano huo kuwa bora (japo kuwa yeye alikuwa mbinafsi na kuchomoka nje hey umesamehe hahahaha sasa move on), wakati yeye anajitahidi ku-re-store uaminifu na mapenzi wewe pia boresha yale ambayo ulikuwa ukizembea au kutoyafanya (inategemea na sababi iliyomfanya achoropoke).


Nne, kama hali ni mbaya na mnahisi hakuna jinsi ya kuendelea na ndoa basi ni vema nyote wawili kama mtaomba msaada kwa Washauri wa ndoa kanisani na popote mnapoamini au mlipofungia ndoa, kama ni ndoa ya kiserikali basi mnaweza kujaribu Therapy ya wanandoa kwa wale ambao hawako ndoani hapa ndio huwa penye uzuri wa kutokufungana pingu za maisha kwani mtu akileta za kuleta na hakieleweki unachukua hamsini zako tu taratiiiibu (sikutumi uwe nje ya ndoa 4 life na wala sipingi ndoa ila nasema ukweli ulio wazi).

PsssT, si wanawake wengi wenye tabia hii ukilinganisha na wanaume, na ikitokea mwanamke ka-cheat mwanaume kusamehe au kuendeleza uhusiano huwa ngumu tofauti na sisi wanawake.

Mada ndefu hii.....nakuja, usichoke kuwa nami.......

Tuesday, 22 April 2008

"Cheating" inaweza kuokoa uhusiano wako.


Umegundua kuwa mpenzi/mumeo/mkeo anatoka nje ya uhusiano wenu au yeye mwenyewe kaamua kusema kuwa hilo ndilo lililokuwa likitokea aukuendelea, unapanic, inakuuma, unakasirika, unalia, unamfokea na kuhoji maswali lukuki kwanini aruhusu hilo kutokea, kitu gani unakosa kwake mpaka ukatafute huko na hata kusema kuwa yule ananini ambacho wewe huna?

Hahahaha wakati mwingine huwa na-miss kugombana na mpenzi ni afya ujue ila sikutumi uka-cheat ili uongeze afya kwenye uhusiano wako.

Kwa kawaida hili huwa linasabaishwa na mambo mengi ambayo nimeshawahi kugusia ktk makala za nyuma na kwa bahati mbaya huwa halitokei mbali au niseme na mtu ambae humjui kabisa mara nyingi huwa ni mtu wa karibu kwa maana huwa unamuona mara kwa mara, kama vile maeneo ya kazini, baa, Salon, dukani/sokoni, mfanya kazi mwenzio.


Mimi binafsi naamini kuwa hili linapotokea huwa kuna na sababu ya msingi kabisa kwa nini mmoja wenu kaamua kwenda nje nasema hivyo kwa vile naamini ktk mapenzi ya kweli na ya dhati, na imani yangu hunifanya nijue wazi kuwa hilo haliwezekani unless kuna mapungufu fulani kati yangu na mpenzi (sio upande mmoja).Lakini kwa bahati mbaya au niseme kwa kibinaadamu hili linapotokea wengi huchukulia tofauti na kujaza lawama wa yule aliyefanya kosa na hatujiulizi wenyewe kwanini ameamua kufanya hivyo towards me.


Baadhi huamua kwenda kuwaadhibu wale waliohusika na tukio zima the other woman/man kitu ambacho mimi sidhani kuwa ni busara.
Natambua hili jambo huwa linauma sana na kukufanya upoteze ile hali ya kumuamini mwenzio japo kuwa unampenda........upendo hauna maana ikiwa hakuna uaminifi, kwambahuwezi kupenda mwenzio kwa asilimia zote wakati huna imani nae tena kutokana na kosa alilofanya.


Najua kuwa kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa wapo watu wameumbwa hivyo kwamba hata ufanye nini watatoka nje tu, ktk hali halisi hilo halipo japokuwa kuna matatizo ya kiakili (Manic Depression a.k.a Bipolar) ambayo yanaweza kumfanya mtu kufanya vitu vya ajabu ikiwa ni pamoja na kufanya ngono ovyo bila yeye kujijua yaani haamui kuwa sasa naenda kulala na fulani bali anajikuta anavutiwa na mtu nakutaka kufanya nae ngono on spot na atafanya hivyo......well hili ni tatizo la kiakili ambalo ni la kurithi na watu wachache sana wanalo.


“Cheating” imegawanyika, kuna wale wanaoafanya hivyo ili kuwa na mpenzi wa pili wa kudumu, kuna wale wanafanya hivyo ili kujaribu kupata mambo fulani ambayo hawayapati kwa wapenzi wao(hii huwa kwa muda mrefu) na kuna wale wanaofanya hivyo kwa bahati mbaya kwa vile kalewa, kashindwa kujizuia baada yakushawishiwa au alikuwa “high” kutokana na matatizo ya kiakili kama nilivyosema hapo juu.


Ni wazi kuwa hili linapotokea uamuzi wa kwanza kabisa na haraka ni kuachana na mpenzi wako, Lakini je unaweza kuendelea kuishi na mpenzi wako? Je utaweza kumuamini tena? Utaanzaje kufanya nae mapenzi? Itakuwa kama zamani au itabadilika n.k.

Pssst: Mpenzi anaekili kuwa ka-cheat mara nyingi huwa na mapenzi ya dhati, anajuati akosa lake na pia anaumia kama unavyoumia wewe au pengine zaidi kwa kile alichokifanya na uwezekano wa yeye kurudia kosa ni mdogo sana kwa vile hatotaka kuumua au kukuumiza tena na that's love! Lakini yule anaeficha mpaka umekujakugundua affair imekuwepo kwa zaidi ya miezi kadhaa au miaka hana tofauti na muuaji na ni wazi kabisa hana mapenzi ya dhati na wewe......

Endele akuwepo, nitakapo rudi nitakupa maelezo na mbinu za ku-cope na hilo na vilevile nitagusia kilichokuwa kikifanyika miaka ya akina bibi kwani cheting sio kitu cha karne hii. Usicheze mbali.

Friday, 18 April 2008

Maambukizo ya HPV

Human Papilloma Virus (HPV) ni maambukizo yanayotokea sana wanawake na huambukizwa kwa kufanya ngono, unapata maambukizo haya hata ukitumia kinga (Condom). Baadhi ya maambukizo haya huweza kusababisha Saratani iitwayo "Cervical" au Saratani ya Kizazi ambayo inaweza kusababisha usiweze kushika mimba/zaa ktk maisha yako yote au maambukizo mengine huko ukeni ambayo sio yale ya Ngono tunayoyajua nakutajia kila siku.

Hakuna dalili zozote za Saratani hii ya kizazi lakini ukiwahi kujua kuwa unayo kwa kufanya kipimo kiitwacho "Smear" basi unakuwa umeokoa maisha yako kwani Saratani hii inaua wanawake sambamba na ile ya Matiti.

Mwanamke anaeanza ngono mapema (chini ya miaka 21) anakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata Saratani hii na wale wanaoanza Ngono ndani ya miaka 20 huwa x2 kwenye hatari ya kupata Saratani hii.

Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo kwa maelezo zaidi Muone Dk bingwa wa magonjwa ya kike, Madaktari hawa wanapatikana kila Hospitali kuwa Nchini.

Mwisho mzuri wa wiki.

Thursday, 17 April 2008

Unapotengana na mpenzi

Siku hizi watu tunaachana na wapenzi wetu sio kwa kwenda kufanya kazi mjini au kijiji cha pili bali nchi ya mbali bonge la hatua eeh?

Kutokana na maendeleo ya Tekinolojia na ukaribu wetu na familia tumekuwa "relaxed" pale wapenzi wetu wanapokwenda mbali nasi kwa muda mrefu tofauti na miaka hiyo, kwa mujibu wa marehemu bibi yangu (Mungu amrehemu). Zamani mwanamke ukiolewa inakuwa wewe na mumeo tu sasa anapoaga kuwa nakwenda kijiji cha pili kikazi mke anakuwa ktk hali ya huzuni na kutafuta mbinu za kumshawishi mpenzi ama waende wote au asiende kabisa huko alikoagizwa.

Na hiyo huwa nafasi pakee kwa mwanamke kuonyesha kwa mpenzi wake huyo ni jinsi gani hawezi kuishi bila yeye, jinsi nakiasi gani anamhitaji mumewe na kwamba hatoweza kabisa ku-cope na upweke.

Wakati huo mwanamke alikuwa akionyesha "affection" kwa mume wake zaidi ya siku zote pale inapojuliakana lini hasa anapaswa kuondoka na siku chache kabla mpenzi hajaondoka mwanamke akipaswa kumshawishi mume/mpenzi kutokubali kusafiri au waende wote kwa kutishia kujiua (kupanda juu ya mti....sio mrefu sana na kujiachia uanguke), kulia kila siku, kususa kula nakadhalika, lakini yote hayo yakishindikana basi mwanaume anaahidi kufupisha safari yake ili awahi kurudi kuwa na mkewe/mpenzi wake.

Mume anapokuwa mbali (kasafiri) mwanamke anajitenga kwa kutokuoga mara kwa mara, kutojipamba/remba, kutokuvaa vizuri na vilevile kutotembea/toka nje bila sababu ya msingi, yote hayo ilikuwa ni mapenzi juu ya mume wake nakujaribu kuepuka kuvutia wanaume wengine na yeye mwenyewe kushawishika na ku-cheat.

Wakati huo wote mwanamke anakuwa anajifunza mbinu mbali-mbali za kumfurahisha mume/mpenzi wake au mazoezi ya jinsi ya kumpa raha mume atakaporudi, mazoezi hayo sio kukata kiuno ktk mtindo tofauti tu bali, kucheza mbele ya mume wake (strip dance sio Umagharibi ulianza miaka ya zamani Tz),mapishi, kuimba na wakati huohuo mwanamke hutumia muda wake kuomba Dua ili mume wake arudi salama.

Wanawake wa sasa hatujishughulishi sana kwasababu tofauti kama sio wengiw etu hatujui au hatujaambiwa, vilevile ukaribu wetu na familia na maendeleo ya Tekinolojia vinachangia kutufanya tujisahau na kutokuwa wapweke as much as bibi zetu were!

Nitaendelea......

Hivi Limbwata kweli Ipo?

"Mimi dada Dinah, leo nataka kuja na mpya, huenda ikawa ni kero au nikuomba msaada. Si mpya kwamba ni jambo ambalo halipo, ni mpya katika uwanja huu wetu. Na huenda si mpya, umeshaligusia, ila hatukulipa kipaumbele kwasababu ni jambo lakukosa `elimu’. Na huenda sio kukosa elimu tu kwani wapo wenye elimu zao wanaliendekeza.


Tuliite ni Imani za watu fulafulani.Yupo jirani yetu ambaye tunaweza kumuita `womenizer’ au mhuni au mume mwenye pepo wa ngono. Jamaa huyu hakikatizi kitu, kila amuonaye kwake ni mzuri, na alivyo na kisimite, huwa akiomba hakosi.


Alikuwa akitamba kuwa wake kwake ni kama shati, hataki wamtawale milele ingawaje kaoa. Na cha ajabu alienda kupima ngoma hana! Mke wake ni mpole, mke toka kijijini, katulia home, kimya (kaziba masikio kwa pamba). Sasa mke wake akawa analalamika, baada ya mambo kumzidi na bahati alikuja hadi kwa my wife kuomba ushauri.


Kabla hajapewa ushauri alishakuwa na nia moja ya kwenda kutafuta `dawa ya mapenzi’-limbwata au love potion, alimwambia mke wangu ana nia hiyo.Hutaamini, kumbe licha ya mke wangu kumshauri vinginevyo, kuwa `ndoa’ ni kuvumiliana na hakuna dawa ya mapenzi inayoweza kusaidia, na huenda ikaharibu kuliko kusaidia.


Alipewa mifano ya watu mbalimbali ambao inasemekana waliwafanyia waume zao na matokeo yake yakawa kinyume chake. Lakini hakuelewa, alienda kwao mikoani na aliporudi, ndipo tulipoona mabadailiko. Hutaamini lakini ndivyo ilivyotokea.

Yule bwana akawa habanduki nyumbani, yule jamaa akawa hazungumzi na watu hasa wanawake. Hata marafiki zake ambao walikuwa wakikesha naye kwenye bar wakaanza kutilia mashaka. Kulikoni mwenzetu huyu vipi! Jamaa hutaamini hata kazi yake ya udereva wa masafa marefu akaamua kuiacha na alinzisha biashara ndogondogo karibu na nyumba yake.


Wengine waliofika kwake wanasema kawa mume-bwege. Jaribu kufikiria mtu alivyokuwa awali na sasa utafikiri ni watu wawili tofauti.Sasa dada Dinah, sio vizuri kuchimba sana undani wa huyu jamaa na mkewe, ila ndio nimekuja na hili swali jipya, huenda kuna watu wana uzoefu nalo. Huenda kuna watu ya mewakuta au jamaa zao.


Huenda hata wewe mwenyewe umeshawahi kuona, kukuta, hatuwezi kupata maoni ya jambo hili ili kuboreshana kimahusiano, kuonya au kupeana ushauri?What is `love potion’ Limbwata au neneo gani jingine sijui. Hiki ni kitu gani hasa, je kipo,? Je kinasaidia, je nini madhara yake kwa wanandoa au wapenzi? Je kinafanywaje kwa wale wanaojua, na wengi wanaoendekeza hili ni akina mama, twaomba msaada jamani." Mimi Emu-three

Jawabu: Well, mimi sina uzoefu na hili ila nimesikia na hata kuulizwa dawa ya mapenzi na nini na siku zote jibu langu ni kuwa mapenzi hayana dawa ni hisia za mtu juu yako, hazilazimishwi.

Limbwata kwa ufahamu wangu ni ushirikina na inafanyakazai kama ambavyo nguvu za giza/ushirikina unavyofanya kazi inategemea zaidi umenuia vipi (nia yako ni nini hasa when doing it).


Sasa unapomwendea mpenzi wako kwa mtoa Limbwata ni wazi kuwa humpendi na unataka kumbadilisha utakavyo wewe kwani atakapofanyiwa Limbwata atakuwa na "characture" nyingine kabisa na hatoonyesha mapenzi kwako bali atakuwa mjinga kwa kutofanya vitu ambavyo "real man does" hachezi mbali na wewe/nyumbani, haishi kukuzungumzia na kukusiafia mbele ya watu wengine, kulia nakuomba msamaha kila manapozozana, kufanya kila unachoamuru afanye n.k.


Hayo sio mapenzi kwa vile sio hisia zake juu yako na anafanya vitu sio kutoka moyoni kutokana na hisia zake ju yako bali kichwani kutoakana na ulivyo/alivochezewa/changanywa/blackmailed.
Mara nyingi hali hii inapomuishia mtu aliye-Limbwatika huwa hana mapenzi kabisa na mpenzi wake, yaani hali inakuwa mbaya kuliko ilivyokuwa awali.


Wanawake wengi wanaofanya hivi ni ama waliolewa kwa vile wanatabia njema kama wake lakini waume zao hawakuwapenda, wanawake ambao hawajiamini kiuchumi au kuendesha maisha bila mume/mwanaume, wanawake wanao Imini kuachika au kuomba Talaka ni aibu kwa jamii hivyo anaamua ku-stick kwenye ndoa yake n.k.


Hili lipo, linafanya kazi kama nguvu nyingine za giza na hufikia muda nguvu hizo zinaisha.Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu ni kujiamini na kutolazimisha penzi, kwani hata ukim-limbwata mwenzio atafanya utakavyo lakini wewe unajua moyoni kuwa hakupendi.


Vilevile ni vema kuzingatia msemao wa kale usemao "mpende akupendae na asie kupenda achana nae".Hata kama uko kwenye ndoa na unaona wazi kuwa ndoa yako doesnt work pamoja na kujaribu kwako kote, usilazimishe omba Talaka endelea na maisha yako ukiwa huru.....mambo ya kung'ang'ania penzi wakati unajua hupendwi ni uzamani. Kunafaida gani ya kuwa mpweke ndani ya uhusiano/ndoa?

Wengine wataendelea.....Asante M3

Wednesday, 16 April 2008

Nikimshukia mume wangu hataki nim-busu!

"Jamani mimi nina kero ambayo sijui nitaimalizaje. Naombeni msaada wenu jamani wa mawazo na ushauri. Ninaomba ushauri wenu kwa mambo haya mawili ambayo kwangu yamekuwa ni kero lakini ufumbuzi sina.1. Nimeolewa na nina miaka 10 sasa kwenye ndoa.


Napenda sana kujifunza na kuboresha ndoa/ngono kupitia blog kama hizi na mengineyo. Sasa basi, ninapenda sana kumshukia mme wangu, kule chini na kwa kweli huwa anafurahia sana. Lakini ikitokea nikamshukia hatujabusiana au kunyonyana ndimi vya kutosha, hataki tena mdomo/ulimi wangu niugusishe na mdomo/ulimi wake. Ananionea kinyaa na kwa kweli huwa najisikia vibaya sana na inanibidi siku nyingine nisimlambe kule kunako. Na kuna wakati kweli ananiomba nimlambe.


Lakini nikishamfanyia hivyo tu, hataki hata nimbusu karibu na mdomo wake. Jamani hii ni nini? Au mnanishaurije jamani?2. Nimekuwa nikitamani sana kulambwa kisimi changu, maana sijawahi na ninatamani pia anilambe. Ila ndio hivyo, mwenzangu hajisikii kufanya hivyo. Naishiwa nguvu kweli.

Halafu kama mjuavyo, kuna majamaa huko nje ni mataalam sana, kuna siku hata kazini tunakuwa tunataniana, mnajua watani wa jadi tulivyo, basi nikitaniana na jamaa akanigusia kunilamba huko chini huwa nasisimuka sana.

Mpaka nimefikia hatua natamani nipate mmoja tu anifanyie hili. Mnanishaurije hili? Au niache tu nivumilie? Kusema kweli sijawahi kufanywa na mtu mwingine tangu nizaliwe zaidi ya huyu nimpendaye ninayeishi naye. Naombeni mnisaidie kero zangu hizi.

Maana naona dada Dina ametoa kero na ufumbuzi huenda akanipatia ufumbuzi wa hilipia. emu-three na wengine mpo?!Wamama na wadada kazi kwenu mnisaidie ndugu yenu, dada Dina nakutegemea dadangu. Naubiri."

Ni kutoka kwa anony @ 9:12:00 PM, kwenye topic hapo chini.

Tuesday, 15 April 2008

Huwezi kuboresha hivi

Natumaini unakumbuka siku chache nilizungumzia swala la kuboresha utendaji wa mpenzi wako na nikasema kuwa kuna vijimambo vingine hukera lakini hakuna jinsi ya kuviboresha na badala yake unatafuta njia mbadala kukabiliana navyo.

Kujikunja au kubadilika kwa sura wakati anafikia mshindo/kilele, ikiwa hii inakukera basi fumba macho au angalia kwingine, pia unaweza kuangalia jinsi Manii inavyotoka (inategemea na mmejiweka vipi).

Kupika kelele/kutukana-Ikiwa mpenzi wako ni mmoja kati ya wale wanapiga kelele au kusema “maneno matamu/matusi” mpaka mtaa wa pili wanasikia au nyumba ya pili hasa kama mnaishi kwenye “attached houses” ambazo ukuta wake sio wa Tofali chapa ya Simba au paa limetenganishwa na mbao tu na hiyo inakukera kwa vile inakufanya uone aibu mbele ya majirani/ndugu basi hakikisha kila anapofikia hapo unampa denda hali itakayo zuia ukelele kwenda mbali, usithubutu kumzima mdomo unaweza kuua bila kukusudia.

*Kupitiwa kwake na usingizi mara tu baada ya kumaliza/kumwaga, hii hukera hasa kama hujamaliza. Sasa ili kuepuka maumivu ya kuachwa njia panda hakikisha unaliweka wazi hilo mapema ili ajue nini cha kufanya (unaweza kumueleza) na pia kumwambia mara ngapi unataka kufika kabla yeye hajaachia, ili akifika na kulala fo-fo-fo usinune au kunung'unika.

Vilevile unaweza ukaanza mwenyewe kujiandaa (jichue bila kufika kileleni) bila yeye kukuona mana'ke akikuona unaweza kumuongezea nyege na akamaliza mapema kuliko sikunyingine zote.

......Kama kuna vitu unadhani vinakukela na unajua kabisa huwezi kuvibadili ongezea maelezo yako hapa....karibu!

Monday, 14 April 2008

Lina, unataka nini kwenye uhusiano wa kimapenzi

"Habari da dinah,mimi naitwa lina ni msichana mwenye umri wa miaka 25. Sikuwahi kuwa na relationship ya kudumu kwani huwa sibahatiki kumpata nimpendaye aidha nitampenda mimi afu yeye hanipendi au yeye atanipenda lakini unakuta simpendi hivyo huwa nakata tamaa na ilishatokea mmoja ambaye nilidhani tumependana akanitaka nifanye naye mapenzi lakini sikuwa tayari akaniacha.

Nilikuwa lonely kwa muda mrefu sasa lakini nimepata mwingine anayenipenda na mimi nampenda na sasa ni zaidi ya miezi miwili niko nae na yeye anataka nifanye nae mapenzi naogopa kumkatalia asijekimbia kama yule wa mwanzo kwani umri nao unakimbia ila ninaogopa kwa sababu sijawahi kufanya mapenzi namaanisha am still a virgin hizo staili zote mi sizijui sasa sijui itakuwaje. Pliz naomba ushauri wako nakuaminia..naomba usitoe email yangu hadharani..asante"

Friday, 11 April 2008

Uhusiano wa maji na Ngono

Sote tunafahamu kuwa unywaji wa maji ni muhimu kwa afya zetu ndani na nje ya miili yetu. Kunywa maji kwa wingi sio tu hufanya ngozi yako kuwa nyororo, hukuongezea nguvu, husaidia kifuko cha mkojo kufanya kazi yake vema na kuepuka maambukizo yasiyo ya lazima kama vile "urine infections" n.k.

Unywaji huo wa maji pia hupunguza shombo ya sehemu zako nyeti hasa kama wewe ni mpenzi wa kushukiwa chini (wake kwa waume). Unapokunywa maji ya kutosha mkojo wako huwa msafi kama vile maji na huwa hauna harufu kali lakini ukinywa maji kidogo (si vyakusosha) mkojo wako huwa na harufu mbaya na kali.

Swala muhimu ni kujifunza kunywa maji kwa wingi kuliko vinjwaji vingine, na kwa wale wenye tabia ya kunywa bia au saoda kila wanaposikia kiu inabidi wabadili mwenendo huo ikiwa wanapenda kuwapa wapenzi wao harufu -free wakati wanawashukia kule mahala au kunywa na kumeza Shahawa.

Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo, nakutakia mapumziko mema ya mwisho wa wiki.

Thursday, 10 April 2008

Jamani mambo ya mapenzi acha tu!

"Mimi nina umri wa miaka 40, tangu nianze mapenzi nikiwa na umri wa miaka 19 sikuwahi kufika kileleni, mpaka nikaolewa nikazaa watoto wawili bado nilikuwa sijafika kileleni. Cha ajabu nilipoachana na mume wangu nikapata mwanaume ambaye sio mzuri, wala hana pesa, yaani ni mtu wa kawaida tu.

Ajabu mara tu kufanya naye ngono nikafika kileleni na mpaka leo kila nikifanya naye mapenzi ananifikisha na tuna mtoto ana miaka 8 bado tunapendana, ajabu nilijaribu kwa mwanaume mwingine sikupata orgasm. Sasa najiuliza je huyu bwana hana nini ? Mbona tangu zamani hadi sasa sipati kwa mwanaume mwingine ila yeye tu ? au nina matatizo au anatumia kimzizi ? Yaani sielewi."

Ni anony @ 2:50:00 PM; kwenye Topic ya "lete uzoefu wako"

Kama una maelezo unadhani yatamsaidia basi unganisha hapa....karibu.

Tuesday, 8 April 2008

Boresha utendaji wake kitandani

Kuna vijimambo huwa vinakera sana wanawake wa kati wa kufanya mapenzi, baadhi nimekutana navyo mwenyewe na vingine ni malalamiko kutoka kwa wanawake wenzangu.


Kijambo kama kumaliza hara, kutokujua kubusu (mtu badala akubusu kwa ulimi anakupaka kama siokukumiminia mimate......jamani kwani mwenzi kasema anakiu?), kuongeza “speed” kabla mambo hayajachanganya (anza taratibu mpaka uambie ongeza mwendo ndio uongeze vinginevyo unaumiza mwenzio), kulazimisha kushukiwa chini wakati yeye kubusu kisimi hajawahi achilia mbali kukilamba, kutojishughulisha vya kutosha, kutonyonya chuchu kiusahihi.....mtu anyonya kama mtoto (ataka maziwa yatoke), kuacha afanyacho nakupokea simu, akimaliza tu kakimbilia bafuni au kwenye friji au sigara n.k.


Pamoja na kero hizo za mwanaume wako ndani ya shuka/kitanda au sita kwa sita ambazo zinaweza kurekebishika/badilishwa/boreshwa kwa msaada wako wewe mwanamke kuna nyingine huwa hazirekebishiki na huwezi kubadili na hivyo ni vema ukajifunza kuvumilia au kutafuta njia mbada kukabiliana nazo (nitakutajia kadiri tunavyoendelea hapa).


Ikiwa mpenzi wako sio bora katika utendaji wake kitandani (sizungumziii kukufanya kwa zaidi ya saa nzima bali kujua afanyalo na kwa usahihi au vile wewe unapenda), atahitaji msaada wako ili kuboresha utendaji wake kwenye sekta hii.

Tafuta siku ambayo unatambua wazi kuwa utakuwa na muda wa kutosha kumpa somo mwenzio (siku nyege sio nyingi sana....siunajua tena) na wakati huohuo kumpa nafasi ya kujaribu vile wewe unapenda au unafahamu kuwa ndivyo inavyopaswa kufanywa.


Utajua kiurahisi kuwa mpenzi wako sio “bora” kitandani ikiwa wewe tayari umekwishakuwa na Ex ambae mambo yake yalikuwa bomba. Sikutumi umfananishe/linganishe mpenzi wako wa sasa na yule Salumu...hapana bali najaribu kusema uzoefu wako utakusaidia kuboresha utendaji wa mpenzi wako na hivyo atakuwa bora ktk utendaji wake ili nyote mfurahie uumbaji wake Mola.


Pamoja na kutumia uzoefu wako ktk kumfanya mpenzi awe bora hakikisha unazigatia kulinda “ego” yake kama mwanaume, hakikisha hutomsababishia maumivu ya hisia zake hivyo hakikisha unapotoa somo usijiweke ktk mazingira ya kutoa somo na badala yake jiweke ktk mazingira ya kujifunza (wote wawili), kuwa wazi waza wakati unawakilisha hoja lakini ktk hali ya utani kidogo japo kuwa moyoni unajua nini unakifanya.


Mfano-Akiingiza basi ni mwendo mdundo, mwambie kuwa anachokifanya ni poa lakini wewe husikii raha yeyote (mwanaume anajali wewe ufurahie, sasa ukisema hupati raha inakuwa rahisi kusikiliza unataka akufanyeje) ila akipunguza mwenzo na kufanya taratibu ndio unasikia utamu/raha na kuwa utamwambia ikiwa unataka “speed” iongezwe.


Mf.2-Ikiwa hajui kubusu....muulize anajua aina ngapi za kubusu kwa ulimi(atasema) kisha mwambie akubusu akiwakilisha ujumbe kuwa kachoka, anatakakungonoana, anakupenda, n.k. akikosea (kwa vile wewe wajua) mbusu vile inavyopaswa kubuswa/kubusiwa/kubusu aah kiswahili utata mtupu chagua sahihi.


Nikirudi nitakueleza kero ambazo huwezi kuzibadili/boresha......enedele akuwepo

Monday, 7 April 2008

Mazoezi ya tumbo

kiwa wewe hujawahi kuzaa nitakushauri ufanye mazoezi ya kukimbia kisha malizia na “sit-ups” mia moja kwamba hamsini asubuhi na hamsini jioni. Hakikisha unaanza mazoezi asubuhi kabla hujala kitu kinaitwa kifungua kinywa (muda mzuri kuanza ni alfajiri au asubuhi kati ya saa moja na mbili) na muda mzuri kwa mazoezi jioni ni kuanzia saa kumi, kumi namoja na saa moja kabla hujala mlo wa jioni.

Siku ya kwanza itakuwa ngumu siku ya pili mpaka wiki utapatwa na maumivu ya misuli sehemu ya tumbo, hiyo ikitokea inamaana kuwa misuli inafanya kazi na hupaswi kupumzika au kuacha

Kwa wale mama wapya; ndio umejifungua hivi karibuni ni vema ukafuata maelekezo ya Mkunga wako na watu wengine lakini kumbuka tu kuwa unakula chakula cha kukutosha wewe na sio kula kwa ajili yako na mtoto (kiasi cha maziwa kinatoka kilekile hata kama utakula mlo wa watu wanne).

Unachopaswa kuzingatia ni kula mlo kamili wenye virutubishao vyote (balance diet) kama vile wanga, mafuta, protini n.k. Pia kumbuka na kukaza tumbo lako kwa kulifunga khanga nyepesi au kitambaa chepesi ili kusaidia kurudisha tumbo lako la uzazi na kuwa kama lilivyokuwa awali kabla hujawa mjamzito.

Nashauri mazoezi haya yafanywe wiki sita au mtoto anapotoka Arobaini (kwa waislamu) baada ya kujifungua kwa njia ya kawaida na sivinginevyo, vilevile yafanywe hatua kwa hatua. Mfano leo unafanya hatua ya kwanza, kesho ya pili n.k, hivyo ni vyema kama utaandaa ratiba yako ambayo itakusaidia au kukumbusha zoezi linalofuata .

*Hatua ya kwanza ni zoezi liitwalo “maombi”na lina sehemu mbili( hukaza misuli ya tumbo na kuondoa uvimbe).

Mosi, lala chali, kunja miguu yako, hakikisha kuwa unyayo uko sambamba na sakafu. Tenganisha kidogo mapaja yako na uweke mikono yako katikati huku viganja vikiwa vimekutana, kasha nyanyua kichwa na sehemuya juu kidogo ya kifua na kurudi chini mara kumi.

Pili, ukiwa umelala hivyohivyo jitahidi kuinua kichwa hadi sehemu ya mgongo na kurudi chini mara kumi.

*Hatua ya pili nayo imegawanyika katika sehemu mbili na zoezi lenyewe linaitwa “uti” (huimarisha mgongo, hupunguza tumbo, makalio na mapaja).

Mosi, lala chali,kunja miguu yako, smbaza mikono yako huku na huko na viganja vyako vikiangalia juu.

Hakikisha miguu na magoti vimetengana kama inchi tano hivi. Vuta pumzi (usitoe) geuza kichwa chako upande wa kushoto , huku magoti, miguu na makalio vikiwa upande wa kulia. Kaa hivyo kwa dakika tatu.

Pili, Rudisha kichwa mahali kilipokuwa mwanzo na upumue, rudia tena kama awali kadri uwezavyo lakini kumbuka kubana pumzi na kutoa pumzi sehemu ya pili ya zoezi hili.

*Hatua ya tatu ni zoezi liitwalo “kunja nyonga” vilevile limegawanyika katika sehemu mbili na hukaza misuli ya tumbo na kulipunguza .

Mosi, lala chali, inua miguu juu huku mikono yako ikiwa huku na huko na viganja vikiangalia juu, kaa hivyo kwa dakika moja na kisha nenda sehemu ya pili.

Pili, Peleka miguu yako (ikwa imeinuka juu) hadi kwenye kichwa na uhakikishe kuwa makalio yako yameinuka na ukae hivyo kwa dakika mbili kisha rudisha miguu yako chini na urudie tena mara ishirini.

Friday, 4 April 2008

Wajua mikao na mitindo ya kungonoana, Namna je?

Mambo?

Ukweli wa Ijumaa ya leo ni kuwa mikao na mitindo ya ufanyaji wa mapenzi/ngono ni vitu viwili tofauti na vilevile kuna namna ya kufanya mapenzi/ngono kitu ambacho ni kitu kingine kabisa ambacho kinajitegemea na hutegemea zaidi nia yenu ninyi wawili au wewe peke yako siku hiyo, ndoa/uhusiano ulipo/unapokwenda, matatizo ya kimaisha, n.k.

Sote tunajua na kufanya aina tofauti za mikao na mitindo ya kufanya ngono/mapenzi ili kufurahia utukufu wake Mungu aliotujaalia lakini sidhani kama ulikuwa ukijua kuwa mikao na mitindo hiyo ina namana yake ya kujiandaa na kuifanya kwa vile ukiifanya yote hakika utaishiwa (kwa wale wenzangu ambao wanajipatia mizunguuko kila siku) na matokeo yake maisha ya kingono kwenye uhusiano wako yanamuwa "boring".

1-Namna ya kwanza ni ile ya kutopoteza muda sana ambayo inamchanganyiko wa kungonoka na kufanya mapenzi at the same time. Mikao yake ni kifo cha mende na mitindo yake, "doggy" na mitindo yake, kusimama na mitindo yake, "spooning" na mitindo yak....n.k. nia na madumuhi ya hii namna ni kuridhishana kingono, yaani hapa kilele/vilele ni muhimu.

2-Namana ya pili ni kufanya mapenzi ki-"sensual" ambapo mwanamke au mwanaume anakuwa kaandaa mazingira mazuri ya kuvutia, udi/manukato, mishumaa, maua aina ya fulani ya nguo ndogo(chupi/sidiria/kijigauni/khanga/mtandio n.k.) ya kuvutia, matunda, kinywaji kama vile champagne, kioo,....mara nyingi hii huwa tunaifanya kwenye fungate ya pili(kukumbushana mlipotoka na kuwa bado unampendamwenzio hasa kama mmekaa muda mrefu ktk ndoa au ni busy ppl) au ktk kusheherekea miaka fulani ua ndoa/uhusiano wenu. Wakati mnafanya mapenzi mnayafanya taratibu na kujaribu kujifunza na kufurahia kila kona ya miili yenu kabla hamjamalizia kilele.......hapa huruhusiwi kukimbilia mshindo au ku-focus kwenye kilele......wewe furahia maumbile ya mwenzio, haraka za nini?

Mikao mizuri ni kipepeo, kumi na moja, kumi na saba,kifo cha mende, spoony.....buni yako kivyako ila sio ile ya sulubu/migumu.

Kutokana na ufinye wa muda sitoweza kuandika namna nyingine za kufanya mapenzi ambazo sio mikao wala mitindo siku za mbeleni....endelea kuwepo.

Nakutakia mwisho mwema wa wiki.

Thursday, 3 April 2008

Jinsi ya kuangamiza kitumbo dida!

Kufuatia maombi mengi ya wasomaji wa D'hicious kuhusu mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo ambayo nilidokezea kwenye topic ya “kukaza musili ya uke” kwa kusema kuwa ni mazoezi ambayo mimi nimekuwa nikiyafanya kwa miaka mingi na kuwa ni zoezi pekee ambalo unaweza kuanza kuona matokeo yake ktk siku tano (only kama utafafanya kwa usahihi).


Inasemekana mzoezi haya huchukua muda mrefu kutoa matokeo utakapo fikia umri wa miaka 30 au uko kwenye kungi la miaka hiyo nakuendelea, ugumu huo hauna maana kuwa tumbo lako halitokaza/oungua na kukufanya upendeze na kuvutia nakujiamini unapovalia mavazi yako upendayo.


Kabla hujaanza mazoezi haya unatakiwa kwanza kuangalia lishe yako kwa maana kuwa unatakiwa kula kwa kufuata muda (mfano kila baada ya masaa manne) na kuepuka vilevi(kunywa maji au mtindi), kuepuka kula wanga baada ya saa moja usiku(na badala yake kula matunda..sio ndizi though, salad), kuepuka kunywa vinywaji vyenye sukari ya kuongeza kama vile aina za soda/juice(na badala yake kunywa maji mengi au juice ya kutengeneza mwenyewe/asilia), epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi (kula mchemsho zaidi), kamwe usiruke mlo kwani kwa kufanya hivyo kutajaza hewa tumboni hali itakayofanya tumbo litune pale utakapo kula kitu kidogo, mtuno huo utafanya misuli ya tumbo lako kutanuliwa na kitu kitakachosababisha uchelewaji wa kulipunguza tumbo hilo.


Wakati unajizoesha na utaratibu huo mpya wa mlo a.k.a diet utatakiwa pia kuandaa mwili wako kuzoea mazoezi na wakati huohuo kusaidia kupunguza “fat” mwili mwako, ili ufanikishe hilo basi unatakiwa kwa kufanya mazoezi ya kawaida tu kama vile kuruka kamba. Kukimbia, kutembea mwendo mrefu n.k.


Baada ya kama wiki hivi toka uanza hii suluba ndio unapaswa kuanza mazoezi yakukaza tumbo ambayo yako ya aina nyingi ila mimi nitakupa maelezo ya yale ambayo ninauzoefu nayo na nimekuwa nikiyafanya mara kwa mara nakupata matokea mazuri kabisa kama mnavyoniona well kwa wale walioniona hehehehehe.


Mazoezi haya yako ktk sehemu mbili amabzo ni kuondoa tumbo baada ya kujifungua a.k.a Bulge na lile la kuondoa tumbo la uzembe hujawahi kushika mimba wala kuzaa lakini unakitambi fulani hivi...
Nakuja nikiwa full loaded....endelea kuwepo.

Wednesday, 2 April 2008

Ushuhuda kutoka

Poleni kwa kuwaacha solemba kwa takiribani masaa 36 hivi kapajatop kangu kaliumia kidogo sasa nikakapeleka sipitali, kamerudi few min ago. Ktk kupitia comment nimekutana na ushuhuda huu, wengi huniandikia mail lakini naona huyu kaja kushuhudia hapa kwa faida ya wote...anasema,

"dinah mpenziilike 6-7 months ago nilikuandikia msg naomba ushauri nifanyaje niweze kuingia kwenye relation tena maaana i was betryaed by my ex niliyezaa nae!!ushauri wako ume work i met a nice guy we trully love eachother,anampenda mtoto wangu pia na inshallah mungu akisaidia tunampango wa kuhalalalisha relation yetu.he adores me n adore him we re in love dinah ,im in love at last hehhehe.endelea kushauri wengi kama mimi ..i took my time n he came along .thanksmamiii"
ni anony @ 5:07:00 PM ipo kwenye topic hiyo hapo chini.

Hongera sana nakila la kheri ktk maisha yako na familia yako.