Friday, 29 February 2008

Kuchepuka kwa mwanaume!

Ni Ijumaa nyingine nakutana na wewe hapa ktk kupena kaukweli fulani ktk maisha yetu yakimapenzi, ngono na mahusiano.

Kuna sababu kibao kwanini anachepuka(nilisha wahi kuzungumzia baadhi hapo nyuma) nazo ni kupata "attention", Mapenzi, kubadili "play list" hahahaha I mean kufanya mambo mapya ambayo anadhani hujui au ikiwa yeye anajua basi anahisi hutokubali kuijaribu na kuridhisha uanaume wake (biology )......Waingereza wanamsemo wao unaokwenda hivi "Men have strong biological urges to knock on the door of neighbouring huts"....hey I'm not asking you to go and knock on ppl's huts hehehehe utapigwa mshale!

Kuna baadhi ya wanawake huwa wanajisifia kabisa na kujiamini kuwa "mume wangu anaweza kupitisha siku 5 bila kunisumbua kutaka ngono", na wengine wanakwambia hawapendi ngono kwa vile hawasikii utamu au hawapati raha yake na baadhi wanaifanya kila siku lakini inafanywa kama wajibu....kumbuka tu mwanaume (ambae ni open minded ) hafanyi kwa vile anataka kumaliza hamu zake bali anafanya ili kukuridhisha nakukufurahisha, hivyo anategemea mfanye tendo hilo kwa ushirikiano.

Mwanaume mwenyewe mpenzi/mke wake bila kuchoropoka basi ujue ama anaridhishwa kuliko au anapigana sana na hamu yake ya kungonoka nje ya uhusiano wenu kwa vile anakupenda kwa dhati.

Sasa wewe kama mpenzi/mke lazima utakuwa ukimjua mwenza wako kingono-ngono na hivyo kama yeye kitu muhimu kwenye uhusiano wenu ni ngono(sex) basi ni wajibu wako kumrudisha mpenzi wako kwenye mstari kwa kuipa kipaumbele ngono kuliko mambo mengine.

Kama hujui ni vipi basi nione na mimi nitakupa mbinu mbili-tatu za kukusaidia kumrudisha where he belongs.

Mpenzi msomaji nakutakia Mwisho mzuri wa wiki, kuwa mwangalifu ktk kila jambo utakalo lifanya.

Kwaheri kwa sasa.