Wednesday, 30 January 2008

"Atatembea sana lakini at the end atarudi kwangu" Ukweli..

Mpenzi wako iwe ni mwanaume au mwanamke siku zote anakupa wakati mgumu lakini wewe unamvumilia, inafikia wakati anatoka nje ya ndoa/uhusiano wenu na kujakukuomba msamaha wewe unasamehe kwa vile tu labda unampenda, unawatoto nae na usingependa watoto kumpoteza baba/mama yao au kwenda kulelewa na mtu mwingine ikiwa utamtaliki/acha mpenzio.

Umewahi kujiliza kwanini siku zote akikosa (wakati mwingine anakuacha kabisa) lakini baada ya muda anarudi kwako mbio akikulilia na kuomba misamaha yote kwa kuhapia Miungu yote ajuayo na kukupa ahadi lukuki ili uendelee kuwa nae?

Mpenzi/mwenza mume/mke kama kweli anakupenda au nisema anakupenda kwa dhati na kukuthamini hawezi kwenda kulala nje na watu wengine na pengine kukuacha kabisa kisha ya kimshinda anarudi kwako na wewe kama juha unadhani huko ndio kupedwa, kwamba hapati "penzi" kama lako huko nje ndio mana kila wakati anarudi.

Endelea hapa

Ukweli ni kuwa mpenzi huyo anafanya hivyo kwa vile anajua wewe unampenda kwa dhati na huwezi kumuacha au kumkataa hata akuumize vipi, anahisi kuwa-secured (sio penzi) mikononi/ubavuni mwako...kumbuka usemi usemao "mpenzi akijua unampenda sana anakusumbua" hasa akiwa hana mapenzi na wewe bali yuko na wewe kwa sababu zake binafsi japokuwa alitumia au anatumia neno "nakupenda" n.k.


Sote tunatambua kuwa kuna wakati tunahitaji "mapumziko" kutoka kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi /wenza wetu kutokana na uzito wa matatizo kikazi au kimaisha, kuna wakati mtu unahisi kwamba unataka kuwa mwenyewe bila kelele za watoto au maswali kutoka kwa mpenzi au hata "kupetiwa-petiwa" (hasa kwa wanaume pale mambo yao kiuchumi hayaendi vema).

Hili likitokea(ni tofauti ) haina maana kuwa hupendwi bali mwenzio yuko ktk wakati mgumu akifikiria jinsi ya kuilinda familia yake ikiwa ni pamoja na wewe mpenzi/mkewe na mara zote mwanaume huyo ambae anakupenda kwa dhati hatolala na mwanamke mwingine yeyote mpaka kipindi cha "mpito" kipite then atarudi kwako na kuomba radhi kwa kujiweka mbali na wewe na hata kwenda kwa kaka/rafiki yake kupumzisha akili na kupata maoni ya "kiuanaume" ambayo wewe mama huwezi kumpatia.

Hivyo wewe kama mwanamke ni vema ukaondoa hiyo kasumba au imani kuwa mumeo/mpenzi wako atatembea kote lakini lazima tarudi kwako, kwa yeye kufanya hivyo sio penzi juu yako bali penzi lako kwake ndio linamrudisha kwa vile anatambua wazi kuwa hakuna mtu atampenda kama unavyompenda wewe.

Kumbuka nia na madhumuni ya kusihi hapa Duniani kumtukuza Mungu na kufurahia maisha, hivyo ni vema kuwa kwenye uhusiano ambao nyote mnapendana na kuthaminiana, ukiona/hisi hupendwi ni vema kujitoa badala ya kuwa "unhuppy na lonely in love".

Tafadhali usisite kuongezea maelezo/uzoefu wako ili sote tujifunze....karibu.

Tuesday, 29 January 2008

M'naume M'namke, nani anamuhitaji mwenzie?


Wengi wetu tunazaliwa kisha kukua na kukuta baba na mama pamoja, bibi na babu pamoja, shangazi na mjomba pamoja, baba mdogo/mkubwa na mama mdogo/mkubwa pamoja na kudhani hivyo ndivyo sote tunavyotakiwa kuwa mara tunapokuwa watu wazima n.k.

Tunapoanza au jiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na baadae maisha ya ndoa (milele pamoja) tunakuja kuhisi kuwa hawezi kuishi bila wenza wetu sio kwa vile wanatulisha na kutuvisha bali tunawapenda napengine ni kwavile umri umeenda na unahofia kuwa "nani atanitaka na mikunjo hii".

Sasa wewe kama wewe unafikiri ni nani zaidi anamhitaji mwenzie zaidi?

Endelea hapa.....

Mwanaume ni mwindaji na uwindaji huo sio wa kupata kitoweo tu (pesa) bali kukupata wewe mwanamke pia, inasemekana kuwa wanaume wengi wanaamua kuwa “single” au wagumu ku-commite karne hii kwa vile wanawake hawawindiki tena.

Kwamba wanawake wamekuwa rahisi kupatikana (kukubali kirahisi) na hivyo wanaume hawahisi kama unawafaa kama wapenzi wao wa kudumu kwa vile hawakukuwinda bali ulijitega mwenyewe (kutokana na U-feminist a.k.a Ubeijing wa wanawake wengi wakidhani ni Usawa).

Hali hiyo inasababisha wanawake wengi kukata tamaa na wanaume ambao hawa-commite kwenye mahusiano ya kudumu na hivyo kuamua kuwa ile “jamii mpya ya Bi au Lesbo”, Hey sitaki kukupoteza hapa let me go to the Point.

Mwanaume anamuhitaji mwanamke zaidi kama msaidizi wake kuliko mwanamke anavyomhitaji mwanaume na sema hivyo sio kwa kuegemea swala la ngono bali kwenye maswala mengine mengi ya kimaisha.


Inasemekana kwamba wanawake ambao hawajaolewa (spinsters) wanaishi zaidi ukilinganisha na wale walio ndani ya ndoa na Wanaume waliondani ya ndoa huishi maisha marefu zaidi kuliko wale walio nje ya ndoa(bachelors), umewahi kujiuliza kwanini wataalamu wanadai hivo?

***************************************************
My only man @ Belsize area this is for you. Asante for visiting here daily even though You don’t understand much Kiswahili. I love you to death baby!xx

Friday, 25 January 2008

Maji baridi na uzuiaji wa Mimba!

Kuna ile imani kuwa ikiwa hutumii au hujatumia kinga dhidi ya mimba basi mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi kimbilia bafuni na koga/oga/jiswafi na maji baridi na hivyo hutoshika mimba.

Vilevile kuna watu wanaamini kuwa ukifanya mazoezi fulani au kuru-ruka mara baada ya tendo la kufanya mapenzi bila kinga basi hutoshika mimba.

Wapo pia wanao amini kuwa ukikojoa (sio kilele) mara tu baada ya kufanya ngono bila kinga basi bimba hainasi.


Ukweli: Njia pekee ya kuepuka mimba ikiwa umefnya mapenzi bila kinga na unauhakika mpenzi kamalizia Shahawa zote ndani ni kutumia kidonge kinaitwa "after morning pill" a.k.a "emergency contraceptive" ambacho kimepewa 95% kufanya kazi ipasavyo ikiwa kitamezwa ndani ya masaa 24 toka tendo(Shahawa kuwa ndani), lakini kina weza kumezwa ndani ya masaa 72 ambayo ni sawa na siku tatu na ufanyaji wake kazi unapungua jinsi masaa yanavyopungua.


Mfano kikimezwa baada ya masaa 24 utandaji wake wa kazi utakuwa ni mdogo kiasi cha asilimia 58 na uwezekano wa mimba kutengenezeka unakuwa mkubwa.

Unatakiwa kuwa mwangalifu wakati wa kufanya mapenzi hasa kama huna mapango wa kuwa mama au baba kwa sasa, vidonge/kidonge hiki sio njia yakudumu ya kuzuia mimba nikiwa na maana huwezi kucheza peku kila siku ukitegemea kumeza "after morning pill" inamadhara kwa afya yako.

Tumieni Condom ili mfanye kwa kujiamini zaidi.....huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo.

Nakutakia mwisho mzuri kabisa wa wiki hii.
Ty.

Wednesday, 23 January 2008

Pesa kwenye mahusiano ya kimapenzi II


Nakumbuka mama yangu alikua akifanya kazi na baba pia lakini walikuwa hawaishi kuzozana kuhusiana na matumizi yao ya pesa za ziada au niseme akiba (mara baada ya kutimiza mahitaji yote muhimu ndani ya nyumba, Baba alikuwa akizitumia kunywa na wafanyabiashara wenzake wakati mama alikuwa akizitumia zake za ziada kutoa “fungu la kumi” Kanisani.


Migogoro au mizozo kuhusu maswala ya uchumi nikiwa na maana pesa huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika kwa uhusiano wenu. Unatakiwa kujijua umesimama wapi kiuchumi ktk uhusiano wako, nikiwa na maana wewe tegemezi, kipato chako kidogo/kikubwa, kipato kizuri lakini bahili, vipato vyenu wote 2 haviwatoshelezi n.kUkitambua wapi ulipo kiuchumi hakikisha pia unajua tofauti ya haki na wajibu wako ktk uhusiano wenu (wengi huchanganya maana halisi ya haki na wajibu).

Mpenzi tegemezi-Ili kuepuka mzozo wa jinsi gani unatumia pesa unazopewa kila siku ni vema basi ukajifunza kufanya manunuzi ya vitu chee (rahisi) na kinachobaki pale kitunze (weka akiba), kumbuka kuwa ili mpenzi afurahie chakula utakachokipika huitaji kutumia Elfu 30 (tzsh) zote kwa siku na badala yake ongeza ujuzi/utundu ktk mapishi yako….ni mfano tu unaweza ukawa unapewa laki au mia tano kama sio unaagizwa ukaombe chakula kwenu.

Ikiwa wewe mwanaume ndio mwenye kipato basi tambua kuwa ni wajibu wako kumhusisha na kushirikiana na mkeo/mpenzi ktk utengenezaji wa “bajeti” sio kwa vile unazileta basi mambo ya “bajeti” na maamuzi mengine yakiuchumi unatoa wewe.


Kumbuka kuwa unapokuwa kwenye uhusiano mnafanya mambo yote kwa usawa na kuthaminiana sio kwavile masikini (hana kipato) basi ndio hawezi hata kushauri au kutoa wazo kama sio uamuzi wa kufanya jambo Fulani n.k


Vipato vyenu havitoshelezi- Nafikiri unatambua kuwa maisha huwa hayabaki vilevile kila siku, maisha hubadilika na hivyo mtindo wetu wa kuihi hubadilika pia. Mfano nyote mlikuwa mkifanya kazi na mlikuwa “comfortable” na maisha yenu then mke/mpenzi anakuja kuzaa watoto 3 kwa mpigo au mmoja wenu anaachishwa kazi…huwezi kuishi kama mlivyokuwa mkiishi hapo awali, na hakika swala zima la uchumi linabadilika.


Hili likitokea wewe na mpenzi wako mnatakiwa kukubaliana kubadilisha aina ya maisha na kuishi kutokana na majukumu yaliyojitokeza wakati huo, kitu kitakacho wasaidia kuepuka mzozo kuhusu uchumi/pesa.


Mpenzi m-bahili-“dizaini” hii ni ngumu sana kuishi nayo lakini kama kwa bahati mbaya umegundua wakati tayari ushaolewa/oa basi jifunze tu jinsi ya kukabilaiana nae nakuongeza mapenzi yako juu yake.


Ili kuepuka mzozo kuhusu uchumi/pesa ni vema kugawana majukumu, yule mwenye kipato kikubwa basi anafanya yake makubwa na yule mwenye kipacho kidogo basi anafanya yale madogo na hakikisha mnakuwa na “account” moja kwa ajili ya maswala hayo bila shaka mtaishi raha mstarehe bila kuzozana kuhusu pesa.


Mpenzi mwenye kipato kidogo-Jinsi ya kuepuka mzozo hakuna tofauti sana na hapo juu kwamba mwenye kikubwa afanye makubwa na mwenye kidogo afanye yale ya kawaida.


Kumbuka nguzo 2 kati ya 5 ya uhusiano mzuri….Zungumza/Wasiliana na Sikilizana/Elewana.

Mida-mida basi…

Monday, 21 January 2008

Jinsi ya kuzoea kucheza na Shahawa!


My 100th Post....makofi tafadhali(hahahahaha)

Endelea kutoka "shahawa sio Uchafu....."

Mwanamke-Unatakiwa kujifunza taratibu na jinsi siku zinavyokeanda ndivyo ambavyo utakuwa ukizoea, kitu cha kwanza kabia unacho paswa kufanya ni kuziona zinavyotoka hivyo hakikisha unaangalia uume pale ambapo mwanaume anamwaga mahali popote kitandani au hewani.


Pili, mruhusu au ruhusu amwage mwilini mwako, iwe ni kwenye matiti, kwenye makalio, tumboni, kifuani, usoni au juu ya uke wako (akikisha haziteremkii ukeni ikiwa huna mpango wa “kumimbwa”) na zikiwa mahali hapo jaribu kuzishika/chezea kwa mikono yako kwa kuzipaka-paka au kuzisambaza sehemu nyingine ya mwili wako.


Mpaka hatua hii ya Tatu utakuwa umeshazizoea kuzion, kuzishika na kuzinusa nahivyo itakuwa rahisi kwako wewe kujua una “deal” na “kimiminika” kizuri kitokako kwa mpenzi wako mara baada yakufanya tendo “takatifu”.
Tumia kidole/vidole vyako kuchovya Shahawa na kisha zilambe (hakikisha una kinywaji chenye uchachu au tunda lenye uchachu kama vile embe, chungwa, nanasi n.k.) na mara baada ya kulamba kula tunda lako (najua bado ile kasumba kuwa ni uchafu itakuwa inakusmbua hivyo kula kipand cha tunda itakusaidia kuondoa utelezi mdomoni mwako).


Nne, andaa vipande vya matunda matamu lakini yenye asili ya uchachu kama embe, nanasi au strawberries na kisha mpe mkono (mchue) au mdomo (BJ) mpenzi wako na muombe amwagie Shahawa juu ya vipande vya matunda yako na kisha kula matunda hayo yakiwa na “cream” na ninakuhakikishia utakuwa umemfurahisha mpenzi wako na atahisi kuthaminiwa sana na wewe bila kusahau hisia nyingine za kimapenzi juu yako zitaongezeka.


Hongera kwa kufanikiwa kufikia hatua hii ya Tano ambapo utatakiwa kukinga kinywa chako au kuweka uume mdomoni wakati mpenzi anamwaga Shahawa.
Kama nilivyosema awali hakikisha kuwa pembeni mwa kitanda au mahali mnapofanyia mapenzi kuna matunda yenye asili ya uchachu au kinywaji chochote chenye asili hiyo na kula au kunywa mara tu baada ya kumeza shahawa kwani huwa zina ukakasi Fulani kooni na kwa kula tunda au kunywa kijwaji kitamu na chenye uchachu kitasaidia kuondoa ukakazi huo.


Faida ya Shahawa-Hufanya ngozi yako kunawili na kuwa laini na mororo/nyororo ikiwa utakuwa na tabia ya kuzipaka juu ya ngozi yako kama “cream au Lotion”.

Hasara-Kuwa hatarini au kuambukizwa Magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na UKIMWI.

Utata-Shahawa haziondoi chunusi usono au mahalipengine popote kwa vile ni protini sio asidi lakini inaondoa vipele au ukavu wa ngozi nakuifanya iwe laini, hivyo kama unahcunusi ni wazi kuwa ngozi yako mahali hapo ni ya mafuta kw ahivyo hutakiwiwi kuongeza kitu chenye mafuta au protini.

Asante kwa uvumilivu….
Taraaa!

Friday, 18 January 2008

Ni usawa au Kiburi?

"After thousands of years of male dominance, we now stand at the beginning of the feminine era, when women will rise to their appropriate prominence, and the entire world will recognize the harmony between man and woman". The Rebbe.

Unakumbuka ule Mkutano wa wanawake kule Beijing au unatambua kwanini wanawake wanaitwa "wabeijing"?

Swala la usawa baina yetu wanawake na wanaume lilizua au linaendela kuzua utata kutokanana baadhi ya wanawake ku-abuse maana halisi au nia na madhumuni ya Usawa huo......na matokeo yake wanawake wamekuwa kama wanaume, wamejawa na viburi mbele za wapenzi/waume wao n.k. hii ni kutokanana kutoelewa kwanini hasa wamama wale walikusanyanakule "Beijingi" kudai Usawa.

Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume anataka kuwa au kuoa "mwanaume mwenzie" kwa maana kwamba unatakiwa kubaki mwanamke no matter how much you earn, no matter how educated you are, no matter how tall you are.....having said that sina maana kuwa ndio uwe kila kitu "sawa/ndio bwana/mume wangu" type.


Usawa tunaotakiwa kuutolea mcho ni ule wa kujitahidi ktk elimu, ufanyaji wa kazi kwa bidii (kupata cheo kutokanana uwezo wako sio kwa jinsia yako), kuchangia maendeleo ya familia zetu namaisha yetu kwa ujumla, kuongoza aukushika nyazifa mbali-mbali ambazo awali zilidhaniwa kuwa ni za kiume tu n.k.


Sio kuwa mlevi kwa vile wanaume wanalewa, kuwa na wapenzi wengi wengi kwa vile baadhi ya wanaume wanafanya hivyo, kutongoza kama wanavyotongoza wanaume kwa vile tu "tuko sawa", kula kiasi kikubwa cha chakula kwa vile tu wanaume wanakula kuliko sisi (hushangai kwanini wanaume wanakula sana lakini hawana pot bellies eti?) na mambo mengine mengi ambayo wanaume wanayafanya kwa sababu zao binafsi kwa vile ni wanaume au kulinda ego zao.

Ukikutana na mwanaume ambae anapenda au vutiwa na "kiburi chako" ukidhani ndio usawa ujue huyo ni Player.

Ndio "fact" ya leo......unamchango? swali je?

Mwisho mzuri wa wiki.

Wednesday, 16 January 2008

Pesa kwenye mahusiano ya kimapenzi

Pesa muhimu sana ktk maisha yetu, pesa ni sabuni ya roho (well mapenzi pia ukiyapata yale ya kweli), Pesa husababisha penzi kufa, kunawili, kukomaa, kukua n.k.

Haijalishi pesa inatoka wapi, iwe pande zote mbili au kwa ushirikiano as mnabiashara/Kampuni as family/pea a.k.a couple au inatoka upende mmoja as kwa mwanamke au mwanaume tu.

Hivi wewe na mpenzi wako huwa mnafanikiwa kujadili maswala ya uchumi (pesa) ndani ya uhusiano wenu bila vita? Well, I mean kuzozana?

Je mpenzi wako ni mbahili? unakabiliana vipi na ubahili wake?

Hebu nipe uzoefu wako kisha naja na maelezo kutokana na uzoefu wangu na vilevile kutokana na uchunguzi wangu wa kienyeji.

Karibu!

Monday, 14 January 2008

Shahawa sio uchafu

Ktk swala zima la kufanya mapenzi/ngono na mpenzi huwa tunajikuta tunafanya vijimambo vya ajabu sana ambayo ukimuelezea mtu anaweza akakuona "wewe namna gani?" lakini ktk hali halisi tunayafanya hayo mambo kwa mapenzi yetu yote na pengine tunapata raha fulani ktk kufanya hivyo vijimambo.

Sasa kwenye hivyo vijimambo vingi tuvifanyavyo kula hiki kimoja nimekichagua ambacho ni kitamu sana (sio kama pipi au asali bali utamu ule wa kimapenzi) na kitakachokusogeza karibu zaidi na mpenzi wako nacho ni kuthamini Shahawa za mpenzi a.k.a cum a.k.a manii a.k.a maziwa a.k.a krimu (as cream) kwa kuzichezea, kuziramba, kuzipaka mwilini n.k.

Natambua kuwa wengi hushindwa kuwa huru kucheza na "kimiminika" hicho kutokana na harufu yake kali au kwa vile wanaume wenyewe wanaziona/chukulia Shahawa zao kama uchafu. Skia, chochote kinachotoka mwilini mwa mpenzi wako unaempenda kwa dhati kama matokeo ya kufanya mapenzi (jasho, "cum", mate n.k.) sio uchafu.

Nitakupa maelezo mafupi ya nini chakufanya ili Shahawa zako zisiwe na shombo kali wewe mwanaume na kwa mwanamke nitakuambia namna ya kujifunza kucheza, kulamba na hatimae kujaribu kumeza shahawa bil akusahau faida ya Shahawa.

Mwanaume-Unapaswa kuangalia lishe yako na nini unakunywa(kama utaweza achana na bia na badala yake kunywa maji mengi zaidi) ili kuondoa shombo ya Shahawa na hivyo iwe rahisi kwa mpenzi wako kucheza nazo, onyesha unazijali nakuzipenda ili mpenzi wako azipende pia (ukidhani ni uchafu na zinatoka kwako...mtu mwingine atafanya nini?).

Acha kabisa tabia yakukimbilia bafuni kuoga au kusafisha "kiungo" au kukimbilia kitambaa/tissue kila baada ya mzunguuko na badala yake baki hapo na onyesha unazithamini kwa kuzishika na kuzipaka juu ya ngozi yake (pale ulipomalizia).

Mtakapo maliza mizunguuko yenu na mmetosheka ndio mnakwenda kuoga/safisha wote......mpango wa kuoga kila baada ya kumwaga sio tu unamkosha mwanamke haki yake kitandani bali pia kunamjengea dhana potofu kuwa Shahawa ni uchafu.

Mwanamke- utaanzia wapi ili uweze kulamba na hatimae kuzimeza?


Naja, Boss leo mood mbaya....
Friday, 11 January 2008

Unaharaka ka' bao la kwanza?!

Mambo?

Ni Ijumaa nyingine tena imewadia ambapo kama kawaida natoka na "fact" na leo ni ukweli kuhusu bao la kwanza.

Ni ruska kuliachia liwahi na huwa linautamu wake wa zaiada kutokana na kuwahi kwake kuja hivyo usinune na usimuite mwenzio "one min man" hilo moja.

Pili bao la kwanza huwa lina nguvu sana na la moto pia lina afya na usipokuwa makini unaweza ukapasukiwa Condom au Condom kusukumwa ndani (mbele zaidi) hali itakayosababisha ibaki ndani baada ya uume kutolea nje ya uke (yaani condom inabakina uume unatoka mtupu) hali inayoweza kupata faida na hasara hapo.

Hasara yake ni kuambukizwa gonjwa la zinaa au kupata mimba bila kukusudia/panga.

Faida ni kumimbika kirahisi kama unampango huo.

Hivyo wewe kama muoga wa "kumimba" au "kumimbwa" basi ni vema au muhimu kuliepuka bao la kwanza kwa kukubaliana na mwenza kulimaliza nje kama vipi liishie kwenye "ngono ya mdomo" alafu mengine ya fuatie mumo kwa humo.

Sikutumi ukafanye bila kinga baada ya bao la kwanza hapo! Najaribu kukuambia tu kuwa ni bao pekee lenye afya, nguvu na muhimu sana kama mnasaka kumimbana kirahisi......

Hakika mabao mengine pia unaweza kupata mimba ila sio kirahisi sana kama lile kwa mwanzo, nazungumzia bao la kwanza baada ya kutotombana kwa muda mrefu like 3days to miaka fulani hivi.

Mwisho mwema wa wiki.

Cya.

Thursday, 10 January 2008

Nini kiswahili kwa "affectionate"


Kwa wanawake wengi wa Kibongo hawajui au hawajali umuhimu wa kuwa “affectionate” as long as anapatiwa pesa za chakula na manunuzi mengine binafsi kila siku, sina hakika kuwa hawatilii maanani hii kitu kwa vile wanaume wetu wa kibongo wengi sio “affectionate” kwa sababu zao binafsi au kudhani kuwa ni sio kitu muhimu sana au “sio utamaduni wetu”(hata denda sio utamaduni wetu lakini mbona tunakulana tu eti?)


Katika hali halisi ni muhimu sana japo mpenzi wako hajui jinsi ya kuomba au akijaribu kukupa “affection” anakatishwa tamaa au kushushuliwa (told off) kuwa anadeka mno au “hukui tu” au hajiheshimu n.k. labda kwa vile wamekuwa pamoja muda mrefu au tayari kawa mama.


Nimeshuhudia baadhi ya wanaume wakilalama kuwa wapenzi wao hawaonyeshi shukurani kwa yale mwengi ambayo wanawafanyia wake/wapenzi wao lakini wanashindwa kuelewa kuwa mtu hawezi kushukuru kwa vitu au mambo unayomfanyia wakati hayaitaji au kwake sio muhimu sana kama yale ambayo anayahitaji ambayo wewe mwanaume huyafanyi.


Au ni kweli unayafanya lakini jinsi unavyo yawakilisha hayo uyafanyayo kama “affection” kwa mpenzi wako ni tofauti na vile mpenzi wako anataka au angependa na kwa bahati mbaya hasemi au hakuambii vile anataka na matokeo yake nyote wawili mnakuwa hamna raha au amani mioyoni mwenu japo kuwa mnapendana kwa dhati.


Ni wazi kuwa kila mmoja wetu anamahitaji yake ktk swala zima la uhusiano wa kimapenzi ambayo ni tofauti kabisa “no matter how compatible you might be”, hivyo ni jambo la muhimu sana kuyaweka wazi mahitaji yako(sio chakula, maladhi na matibabu bali mambo ya kushikana, busu, outings, ukaribu, mazungumzo, ngono, kuwa pale kwa ajili yake n.k.) kwa mwenza wako ili aweze kuyatimiza.


Kumbuka kuwa hakuna mtu anazaliwa anajua kila kitu bali sote tunajifunza kila siku, na nafasi nzuri ya kujifunza ni kumzoea (bila kumshushia heshima) mpenzi wako kama rafiki,mpenzi na mwenza….ondoa au acha kabisa heshima ya uongo (Uoga) na badala yake be youself ili akupende 4 who u are sio who u pretend 2 be.


Huwezi kuamini kuwa baba mtu mzima hawi-affectionate kwa mkewe aliyeoa miaka ya 80s lakini anakuwa “very affectionate” kwa binti mke mdogo anaetoka nae a.k.a kimada……I don’t real get it?


Jamani mapenzi hayana ukubwa wala udogo, mapenzi hayazeeki, mapenzi huendelea kuwepo bila kujali mmekuwa pamoja kwa muda mrefu kiasi gani…..mapenzi ni hisia zilizo ndani yako na hazina uhusiano na kuzaliwa kwa watoto au kuzeeka hivyo sote hatuna budi kuyaonyesha kwa uwazi kwa wenza wetu


Muonyeshe mwenzio jinsi unavyompenda kwa vitendo sio kwa kungonoana kwani huko sio kupenda kwa vitendo bali ni hitaji lingine linalojitegemea ambalo nalo ni muhimu pia kwenye uhusiano (sio zamu yake leo).

*Sasa hebu leo mwambie mpenzi wako ni nini hasa hupendi akufanyie na nini hasa unapenda afanye kuonyesha “affection” kwako.


Natambua kutokana na utamaduni wetu kuna mambo mengine huwa tunashindwa kuyafanya kwa kuhofia jamii itatudhaniaje…..who cares….hawakulishi…..hawakuvishi na kila mtu anaishi kimtindo wake na kufurahia maisha kivyake hivyo wewe ukihisi unataka kuonyesha penzi kivitendo mkiwa marikiti au kituo cha daladala just do it! sio mpaka mfike uchochoroni!


Kuwa "affecionate" ni muhimu sana pia ikiwa wewe na mpenzi wako hamlingani kiuwezo ktk kubilingishana.......kuna watu kungonoka sio muhimu sana kwao kutokana na sababu zao mbali-mbali lakini hiyo haina maana hawahitaji kupendwa au kupetiwa-petiwa.

Siku njema.

Tuesday, 8 January 2008

Chupi, "briefs" au Bukta/boxer!
Mimi binafsi nikiuona mwanaume ndani ya chupi huw anaona kama vile sio mwanaume kamili na pia huni-put off lakini nikiona "boxer" (zipo kama kaptura pana na za kubana) au zile wanaita "briefs"(ni chupi lakini zimekaa vema kwamba zinafunika makalio ya m-baba) imefunika "vifaa" vya mwanaume nahisi kuvutiwa, kwa kifupi sipendi kuona mwanaume kavaa chupi yaani bora utoke "Comando" kuliko univalie chupi aisee.


Kuna mtu kanikumbusha kitu kimoja muhimu sana ambacho nadhani wengi huwa hatukifikirii au hatukitilii maanani sasa nimekumbuka nimeona ni vema niki-share na wewe msomaji wangu.


Kuna baadhi ya wanaume ndude zao zimepinda kuelekea upande mmoja. Mboo ya aina hiyo huwa inauma kiaina kwa vile inapoingia hailengi katikati na badala yake huingia kwa kugusa nguzo ya uke (kule mboo ilipoelekea/pindia) nguzo hiyo kwa wakati huo inakuwa haijachanganya kwa utamu (kuta huchukua muda kuwa tayari tofauti na kisimi au mwanzo wa uke natumai unalijua hilo).


Sababu kuu ya "mpindo" huo ni ukubwa na udongo wa kende/pumbu, kama ujuavyo kuwa wanaume wote mna pumbu mbili na baadhi moja ni ndogo kuliko nyingine sasa uume huwa na tabia kugeukia/fuata kule kudogo (sijui huwa inajaribu ku-balance uzito hahahahaha) ikiwa pumbu ziko sawa basi mboo inakuwa imenyooka tu kama kawaida.


Na sababu nyingine ya pili(sio kuu) ni tabia ya kuvaa bukta/boxer pana ambazo mara zote hufanya "bidhaa" kuning'inia tofauti na chupi, briefs au boxer za zilizoborehwa ambazo huzikusanya pamoja kama furushi.


Sasa ikiwa kende/pungu zako ziko tofauti (kubwa na ndogo naunavaa bukuta au bokisa ni wazi kuwa mboo "itajimuvuzisha" kule kwingine ili ku-balance uzito hali itakayo fanya ipindie huko na ukivaa chupi hali hiyo ya kuegemea upando mmoja hupungua kwavile unakuwa umekusanya zote pamoja.


Hivyo ni vema kwa mwauanume kuvaa nguo ya ndani ambazo zinakusanya bidhaa zako pamoja kuliko zile boxer pana au bukta ili kuepuka "mpindo".

Una nyongeza? Nitashukuru ikiwa nitapata mchango kutoka kwa wanaume ambao ndio walengwa wangu hapa.....
*1st Pic ni Boxer za kisasa na 2nd ni brief.
Ty.

Monday, 7 January 2008

Nani mwenye uwezo wa juu wa kungonoka?


Kuna ile dhana au niseme imani kuwa wanaume ndio pekee wenye kutaka ngono mara nyingi na ndio maana wanahitaji mwanamke zaidi ya mmoja ili kuridhika kikamilifu.


Napenda utambue kuwa dhana hiyo haina ukweli wowote kwani hali ya kutaka sana ngono inategemea na maumbile ya mtu nikiwa na maana jinsi mtu alivyo umbwa japokuwa kuna aina ya magonjwa mbayo tiba zake huongeza hali hiyo (tutalizungumzia hilo siku nyingine).


Kuna mama mmoja aliwahi kuniambia kuwa anatafuta wanamaombi ili wamuombee ili hamu yake yakufanya mapenzi/ngono ipungue kwanu mumewe hawezi kumudu na humfanua mume huyo kuwa hoi hali inayomfanya mwanamama huyo kuhisi guilt.


Nikamwambia hilo sio pepo ni hali ya kawaida na anachotakiwa kufanya ni kuzungumza na mumewe na kutafuta njia mbadala bila kuumizana hisia au yeye mwanamke kuwa mwelevu na kuelewa kuwa uwezo wa mumewe ni mdogo….angekuwa mwanaume angetafuta kimada siku nyingi..

Ni wazi kuwa kuna baadhi yetu tunafanya mapenzi zaidi ya mara tano kwa siku na kila mzunguuko mmoja unafika kileleni mara mbili hivyo kwa ujumla mwanamke unafika kileleni mara kumi kwa siku ndio unajisikia kweli umefanya leo…..na asubuhi yake ikifika unahisi kama vile hujafanya kwa siku nyingi na unataka tena…..


Hii hutokea kwa vile mwanamke kama umejifunza kufurahia ngono/kufanya mapenzi na unafurahia au unauwezo mkubwa wa kufanya hivyo basi the more unafanya the more utataka kufanya…yaani hamu huongezeka maradufu tofauti na wanaume wao jinsi wanavyofanya ndivyo hamu inavyowapungukia


Utafurahia zaidi ikiwa mpenzi wako nae anauwezo kama wako au zaidi lakini kumbuka kuwa mwanaume hawezi kufika mara zote hizo kwa siku, ataishia 3-4…..siku zote mwanamke huwa juu kwa vile tunamaeneo tofauti ya kupata utamu wa kufanya ngono/mapenzi tofauti na wanaume,


usikatishwe tamaa ikiwa mpenzi wako wa mwanaume anakufanya na ukifika yeye hatoi kitu sio kuwa hafurahii bali hakuna cha kutoa lakini kufika kwako humpa yeye raha kuwa anauwezo wa kukufurahisha 2 the maximum…mambo ya ego hayo.


Kutokana na maelezo yangu ya awali utagundua kuwa ni muhimu kuwa na mpenzi ambe mko sexually compatible ili kuepuka mambo ya kutafuta wapenzi njeya uhusiano wenu kuwafikisha vile mtakavyo.


Tujaribu kujifahamu na kuwa wazi pale tunapoanza uhusiano, pamoja na kuwa umevutiwa na unapenda mambo Fulani kutoka kwa mwenzio weka wazi kuwa ngono kwako ni kitu muhimu hali hiyo itasaidia nyote wawili kufanya uamuzi wa busara kabla uhusiano haujakomaa….


Nikisema uamuzi wa busara sina maana kumkimbia mwenzio kwa vile unadhani hawezi hapana……unaweza kujitolea mhanga na kuishi bila kuridhika kimapenzi/kingono 4 love inawezekana eti?


Kiasilia au kimaandiko nia na madhumuni ya mke na mume au wapenzi kuwa pamoja ni kungonoana haya mambo mengine tunajiongezea tu….wewe unasemaje?

Friday, 4 January 2008

Malaya!

Ni Ijumaa nyingine tena imewadia na kama kawaida naibuka na “fact” na leo napenda utambue maana halisi ya neno "Malaya" ambalo ni neno asilia linalotumika au tumiwa kumshushia hadhi au kumtusi mwanamke (Kama ambavyo baadhi yenu mnanitusi).

Hali ya kupenda na kufurahia ngono na mpenzi wako sio tabia (Umalaya), uwezo mkubwa wa kufanya mapenzi/ngono (high sex drive) sio tabia (Umalaya) ailimradi tu unafanya hivyo na mpenzi wako mmoja.

Uvaaji wa mitindo fulani ya nguo sio tabia (Umalaya),ujuzi au utundu ktk kufanya mapenzi sio tabia (Umalaya), kuelezea au kufundisha mambo fulani kuhusu ngono/mapenzi sio tabia (Umalaya) na vilevile kujiingiza kwenye uhusiano mpya mara baada ya mke/mume/mpenzi kufariki au kuachana nae sio tabia (Umalaya).

Malaya ni mwanaume au mwanamke mwenye tabia au hulka ya kujumuika kimwili/fanya ngono na zaidi ya mtu mmoja (kulala/tombwa/tomba/tombana ovyo) iwe yuko kwenye uhusiano au nje ya uhusiano.

Jichagulie mpenzi mmoja, jifunze kupenda, kuwa mwaminifu, jali, thamini na utafurahia kama ambavyo wengine tunafurahi.

Nakutakia mwisho mzuri wa wiki hasa ukizingatia ni ya kwanza ktk mwaka 2008.

Ty.