Monday, 29 December 2008

Waume za watu wananisumbua-Ushauri

"Da Dinah, mimi na tatizo ambalo ni kama kwa kweli naona nimejitakia. Ni mdada au mama wa miaka 28 na nina watoto japokuwa tumetengana na mume wangu. Sasa unajua tena mijibaba(wanaume) wakishajua kuwa uko single wanaanza kukumendea.


Mimi tatizo langu ambalo lilisababisha kutengana na baba watoto lilikuwa ni uhuni wake, na nikaamua kumwacha ili tusije tukafa na UKIMWI na kuacha watoto. Na nikaapa sitakaa nitoke na mtu aliyeoa au sitakaa niharibu ndoa ya mtu kwa kuingilia penzi.


Sasa tatizo lilikuja hivi, mara nyingi sana mahali ninapofanya kazi waume za watu wanajaribu kunitongoza, na msimamo wangu nimekuwa sitaki kusikia mume wa mtu manake na mimi niliyaonja nilipokuwa kwenye ndoa yangu.


Sasa basi siku isiyoliwa kitu, kuna baba mmoja mume wa mtu kazini amekuwa akinisumbua zaidi ya wanaume wote ili niwe naye kimapenzi. Sasa siku moja tulikuwa na cocktail party na akaja na ushamba wake wa kunitaka kimahusiano, nami(jamani sijui kinywaji kilishaniingia) au ni shetani gani lilonifanya nifungue mdomo.


Nikamwambia kuwa mimi msimamo wangu ni ule ule 'sitaki kuwa naye' lakini kama anataka nimtafutie mtu basi nitafanya hivyo, he took up on the offer na kutokana nilikuwa na rafiki yangu wa kike ambaye ni single nikamwi-introduce.


Na baada ya wiki moja yule rafiki yangu niliyomwi-introduce akaniambia jamaa amenunulia sofa set, halafu mara wanafanya party ' na mara nyingi naona huyu jamaa ndio ana-finance' wananialika na zaidi ya yote inaonekana wamekuwa quite close katika uhusiano wao.


Mimi kama mwanamke ambaye nilishawahi kuolewa najisikia vibaya sana, yaani naji-picture kama mke wa huyu jamaa, naona kweli huyu baba ananyima familia yake upendo na anatoka nje na mimi ndie niliyefanya connection - yaani nimeshajilaaumu saaanaaa, najisikia vibaya kweli, hata kama ndugu wasomaji mkinitukana - kweli I deserve it - lakini yaani sijui jinsi gani yaku-reverse jambo hili. Sasa nimekuwa mbali na wote wawili, wakinialika kwenye party au kutoka nawapa excuse.


Mimi naomba......mnisaidie jinsi ya kufanya, japokuwa najua naweza kutoeleweka ( I risk to be misunderstood) wakadhania labda ni wivu etc, lakini ki ukweli ni kwamba - kujisikia kwangu vibaya ni kwa sababu nilikuwa kisaidizi kikuu kwa kuwakutanisha, na upweke wa mke wa huyu baba (wakati mume anajivinjari na kurudi nyumbani usiku, na uongo anaomwambia ili kuficha kinachoendelea) najua na naona ndio nimeusababisha - mimi naumia sana na mawazo.

Da Dinah - nimeandika kwa ajili ya kutaka tu ushauri wa hali yoyote.
Nitashukuru sana."

Jawabu: Shukurani kwa kuniandikia. Kuna umri fulani mwanamke ukifikia wanaume wanaokutokea wengi wanakuwa tayari wamekwisha oa hiyo haina maana kuwa hakuna wanaume ambao hawana wake/wapenzi la hasha!


Wanawake wengi tunakutana na majaribu hayo. Mimi mwenyewe nakutana sana na vishawishi vya namna hiyo lakini as for me natumia nafasi hiyo kutaka kujua kwanini hasa huyo mume anataka kutoka na mimi hili hali anamke na watoto nyumbani, najitahidi kutafuta namna ya kujua ukweli wa nini anakikosa huko kwake na kutaka huku nje?......akiwa wazi nampa ushauri na ile kunitaka mimi kunabadilika na kuwa rafiki na mara mambo yakiwa mazuri unajikuta unatambulishwa kwa mkewe kama mtu uliyesaidia na sio "the other woman".


Ni kweli ulifanya kosa kubwa sana kuunganisha mume wa mtu kwa mwanamke mwingine ukijua wazi kuwa mwanaume huyo ana mke na watoto. Kama mwanamke mwenye maadili mema na mwenye kujali maisha bora kwa mwanamke mwenzio na watoto (ukizingatia kuwa wewe ni mama na sidhani kama ungependa watoto wako siku moja wateseke) ungemshauri mume huyo kutulia na mkewe.


Wakati mwingine unaweza kuokoa ndoa ya mwanamke mwenzio kwa kutoa ushauri kwa mwanaume anaekutaka au kumwambia mkewe kwa namna yeyote ile hata kama ni ku-form urafiki wa kizushi (sio kwenda na kudai mumewe anakutaka, hapana) bali kumtahadhalisha kuwa awe muangalifu na mwenendo wa mume wake na kama kuna kitu kinakosekana ndani ya nyumba kama vile romance,amani, upendo, ngono, n.k. basi ajaribu ku-restore vinginevyo ataletewa magonjwa, ikiwezekana mfundishe, muelekeze nini cha kufanya......najua mwanamke mjinga-mjinga atadhani unataka kumuibia mumewe lakini mwanamke muelevu atakuelewa na kukushukuru.

Kwa bahati mbaya umechelewa na hakuna kitu unachoweza kukifanya ili rafiki yako na mfanyakazi mwenzio ambae katika hali halisi ni Fuska ili waachane bila kukudhani kuwa wewe unawaonea wivu kutokana na wanavyopendana nakufanyiana mambo ambayo wewe umeona ni muhimu na kuyataja kama vile party, vifaa vya ndani n.k.


Nini cha kufanya-Kaa chini na rafiki yako na mueleze ukweli kuhusu huyo Baba (mfanya kazi mwenzio) kuwa ametelekeza familia yake kwa ajili ya huyo rafiki uliyemuunganishia......unaweza kusema ulimsakizia kwa vile wewe hukutaka kuendelea kusumbuliwa na huyo mwanaume lakini hukutegemea kama wangeanzisha uhusiano nakufikia hatua ya huyo jamaa kutelekeza mke na watoto wake.


Kwa vile unauzoefu na ndoa, familia yenye watoto uliowazaa mwenyewe na Talaka unajua wazi maumivu anayopata mke ikiwa atagundua mumewe anatoka nje ya ndoa, hofu ya watoto kuishi bila baba yao....hivyo pamoja na maelezo mengine muhimu tumia uzoefu wako huo kufikisha ujumbe kwa rafiki yako juu ya kutembea na mume wa mtu.....omba radhi kwa kuwaunganisha ikiwezekana.


Itakuwa ngumu na itamchukua muda mrefu kwa rafiki yako kuachia ngazi ikiwa amejenga mapenzi ya kweli na huyo mwanaume, inawezekana kabisa akamshawishi jamaa amuache mkewe ili amuoe yeye na hapo ndio utakapojisikia vibaya zaidi. Kwani itakuwa sio tu umesababbisha wawe wapenzi bali pia watakuwa mke na mume na wakati huohuo utajisikia unahatia kuwa umevunja ndoa ya mwanamke mwenzio kwa kumrusha mume wa mtu na rafiki yako.


Baada ya kuweka wazi kwa rafiki yako achana nao waendelee na mambo yao, Yeye kama mtu mzima atakuelewa, atatafakari na kufanya uamuzi wa busara. Endelea na maisha yako na watoto wako bila kuonyesha chuki juu ya uhusiano wao ambao sio halali.

Mungu akubariki na kila lililo jema!

12 comments:

Anonymous said...

huyu sst kinachomsumbua hapa sio dhamira kumsuta ,bali ni wivu kuona ka vitu vingekuwa vyake, kwani huyo dada kapanga kuishi single maisha yake yote, wangapi anona mtaani wanasalitiana. yeye atulie kivyake,huwezi jua ndani ya nyumba ya mh. huyo kunani. inaonyesha mh. hakumtaka kitani bali alitaka pumziko la pili. namshauri huyo dd,amrudiye bwana yake,vinginevyo hakuukimbia ukimwi,bali ameufuata huko anakoishi single.

Anonymous said...

kweli dunia imeisha kila msichana/mama ninaye ongea naye mambo ya kazini katongozwa,sijui kahongwa,mara mke wa fulani anatembea na yule kaka. ivi kweli tutapona?? mimi we dada sijui mama nimekuheshimu tu lakini hujanifurahisha na nina wasiwasi ndoa yako umeivunja mwenyewe ni mtazamo wangu na pia hapo kuna jambo umetuficha sema wewe unamtaka huyo mzee this should be black and or white ''wanafanya party,sofa set'' hapa kuna kijiba cha roho lol

Aidha kuna haja ya ku share xperience za makazini ni namna gani zina affect ndoa au Dinah na wadau mnasemaje? jamani tuliopo makazini tujaribu kuwa makini vinginevyo hali ni mbaya, mind you wafanya kazi wanahama hama sana so kama kuna vikoloni humo mwote what do you think?
mwisho kabisa huna kosa kuwa karibu na binti huyo mwingine kosa lako ni ku facilitate mme wa mtu kupata kiburudisho, hii hata wewe ingekuuma in case ungesikia kuna mwanamke kam support husband wako kupata smll hausi, its such a hell lkn ndio hali halisi makazini trust me, si wana wake si wanaume, lkn washawishi wakubwa in most cases ni wanaume hata kama wameoa.pia wadada wenyewe mnavyovaa siyo kabisa some time, kumbuka ofc nyingi kuvaa ni suruali kitambaa tena unachomekea[kwa wanaume] sasa vinguo mnavyo vaa akina abdala kule chini hali ya hewa huwa sio nzuri unaweza shindwa simama kuchukua file mteja anasubiri hapo lol
Pia hapa wanawake naomba majibu yenu utafiti nilioufanya unaonyesha hamkatai kwa mwanume aliye oa kwa kiasi kikubwa[ sio wote lkn].kweli wanaume popote mlipo mnatakiwa kubadilika, msitumie vyeo kuwa rubuni wanawake, na wanawake muwe makini kazi mnazopeana kama pipi hizo mwisho wake huwa unakuwa ndo huo utamu kolea utapo ombwa utakataa ikiwa yeye ndo anapitisha CV yako?
matarajio makubwa kupita kipato na kuridhika na uliye naye! from xperience men/women nimeona hasa waliosoma wanapenda uhuru sana kujiachia au hata kukumbushia past relations to them is not a big deal so wewe dada una dalili hizo, tulia tafuta wako, kama kweli ulimtosa huyo jamaa hongera ingawa siamini sana kwanini ikuume hivyo!?

tubadilike, women mkiwa na msimamo hata maambukizi ya VVU yatapungua ila kwa wanaume in my opinion imeshindikana,imagine huyo jamaa alokuwa anakusumbua, sijui alijua kama wewe ni mke wa mtu au ulimficha? kuna watu wengine hawasemi [men/women] unakuta jitu kubwa kabisa linasema mimi sina mtu, kweli wapo lkn 2 kwa 100, tubadilike jamani hali ni mbaya lkn kama tunasema maisha mafupi so tujiachie sawa ila ndo yatakuwa mafupi zaidi.

Lajk.

Anonymous said...

Jamani, mimi ndio liniondika kutaka ushauri,

i) Kazini mimi nimefanya kwa muda sasa miaka 3 na nusu, kila mtu anafahamu kuwa mimi ni single na nina watoto.

ii) Mungu amenibariki ninaprofession nzuri ambapo,imenisaidia kujimudu kwa kila aina,kwa hivyo wivu (And Iam saying this from the bottom of my heart) its not part of me writing begging for advice.Ningependa, ushauri ambao ningeweza kuutumia kuwaonyesha hawa wapendanao kuwa wanalofanya ni kosa. Lakini kutokana na kitu kama hichi(illicit love) ni kawaida katika jamii yetu, naonekana kituko au mwenye wivu.

iii)Ndio ni kweli mimi bado nasubiri mwenzi atakae nipenda 'AMBAYE NI SINGLE' atakae nipenda mimi na watoto wangu. Kwa hivyo kutokana na nimeshajua ninachotaka katika maisha yangu. NDIO SABABU AMBAYO IMENIFANYA SITAKI KURUKIA AU KUINGILIA PENZI.

Anonymous said...

Wacha wivu mami. Umenena kuhuzu sofa set, party etc. What I see here you entered into a feeling that "that suppose to be me. I was there first. Ni ujinga wangu that I dont benifit. You know what kili dhambi if you're genuine and live with what you did.

EVARIST said...

Mbona mie sijaona tatizo liko wapi hapo?Hooking up someone na mtu mwingine sio kosa as such unless kwenye mambo ya dini (na we know watu wa dini hawana hizo).Nadhani ingekuwa kosa kama ungemficha rafikio kwamba huyo bwana ni mume wa mtu kisha rafikiyo akaanguka ktk mahaba na mume wa mtu pasipo yeye kujua.Wewe umeshatimiza kazi yako,yatakayoendelea huko mbele kazi yao japo huwezi kukwepa kuwa sehemu ya equation hiyo!Take it easy,dada.Ndio maisha yetu ya kila siku.

Anonymous said...

lol..dada micjakuelewa vizuri hapo, wanaume wa watu wanakusumbua au wivu?? je ni kweli uliacha na mume wako kwa tabia zake mbaya??km unajua madhara ya mume kutembea nje ya ndoa kwa nini ulimuuunganishia huyo shoga yako kwa mume wa mtu? why didnt u tell ur friend kuwa huyo mwanamume ni mume wa mtu?
wewe pia unasupport watu wanaotoka nje ya ndoa zao, nahisi hukumpenda tuu huyo jamaa au ulimuona mchovu sasa best ako kawekwa vizuri roho inakuuma watamani ingekuwa weye sio! wacha wivu.
lily.

Markus Mpangala said...

kusumbuliwa? je uliwajuaje kama ni waume za watu? uliwafahamu lini? sijui, labda dada Dina atatoa jawabu hapa. nimepita kukusalimia ndugu yangu maana siku nyingi sana

Fita Lutonja said...

Hii kazi kweli sina mchango zaidi ya kushangaa!!!!!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Kama umewakutanisha halafu huyo jamaa humtaki mbona unafatilia sana? ooh sofa,ooh parties.Kama walivo sema wengine unamtaka huyo mtu na unahisi ulikosea kumunganisha na shoga'ko.Unavodai eti waume za watu wanakufatafata kama una msimamo watachoka wenyewe na utapata wako wa pekeyako lakini kama hata huyu bado unammezea mate utaishia kuwa nyumba ndogo dalili zinavonyesha.

Anonymous said...

Dada hapo kweli mm nakuunga mkono kuwa ulikosea sana kumpigia pande huyo mwanaume wa mtu huku wewe kipo kitu kinacho kutenganisha na mme wako kama hiki kwa huyo mwanaume mkwale.
Basi dada aangu naona mimi na wewe tuna share charactor naomba tuwasiliane kwa email hii...
jitonyile@yahoo.com

Anonymous said...

Mie Hapo naweza Jamani nikaona kwanini huyo mtu ana mke na watoto anataka nje inatokea na wamama wengine wengi mume akirudi hajatulia wanaanza mara hiki atapiga makelele kitandani atataka kidogo tu. kwahiyo mume stress zake anatakak umalizia nje, ila muhimu anatakiwa Familia yake ajue kila tatizo analitatuwa vipi kwak uita mama na watoto kwa pamoja na muda mwengine kutoka out. wanawake ambao kama WAKE za watu wao wanakuwa Tamaa na Hasa kama mume mbahili alafu anakuwa anapenda kazi 2 much hata akirudi yeye anamudak idogo tu na familia yake na hao pia wanafanya Mke awe na tamaa.

Anonymous said...

Dadangu kama kweli dhamira inakusuta na unakubali ulifanya kosa kumuunganisha mume wa mtu na shoga'ko andika barua ukisema fulani ana nyumba ndogo anaitwa fulani na anakaa sehemu fulani tafuta mtoto mdogo ampelekee mkewe huyo fedhuli,hapo sasa mke atajua la kufanya na wewe kidogo utakua umefuta angalau kidogo upuuzi uliofanya.