Saturday, 13 December 2008

Rafiki kaua ndoa ya mshikaji'ke, afanye nini-Ushauri!

"Kuna jambo nataka mnisaidie nini nifanye,
Mim ni mwanaume, kuna lafiki yangu ambaye ni mtu mzima amabe ana mke na watoto. Huyu rafiki yangu ana rafiki yake kipenzi na wamekua kama familia moja, kibaya zaidi huyu jamaa (rafiki yangu) amefanya kitendo kibaya sana cha kumtongoza mke wa rafiki yake na hatimaye kufanya naye vitendo ngono.


Mie nikiwa kama msiri wake mkubwa aliponiambia mambo yale nilimkatalia kabisa na kumwambia ache mambo hayo kwani yatakuja mletea shida baadae lakini hakusikia na kuendelea na mambo yale.


Sasa kilicho kuja kutokea ni mume wa huyo mwanamke Rafiki yake) kuja kujua huo mchezo wao mchafu,alipobanwa mwanamke alikili kuwepo ukweli wa jambo hilo na uadui kuanzia hapo baina ya mumewe na huyu jamaa yangu ambae pia alikuwa rafiki yake.


Kibaya zaidi huyo jamaa kamwacha mke wake kwa sababu hiyo na kumtaalifu mshikaji kuwa amemwacha mke kwa sababu yake. Sasa amenirudia mimi nimsaidie,binafsi sijui nini cha kumshauri na kwa sababu nilimkataza mambo hayo mapema hana cha kunilaumu.

Sijui Dinah na watu wangu mna nini cha kusema juu ya hili. "

Jawabu:Hata mimi sijui cha kumshauri honestly! Rafiki yako hana utu hata kidogo, alijua ni mke wa rafiki yake na bado akatongoza na mpaka kufanya nae ngono, huyo mwanamke ambae ni mke wa rafiki yake pia ni mshenzi na hafai kuwa ktk jamii tena hana hulka kabisa. Kitu gani hasa kilimfanya akubali kutoka na rafiki ya mume wake akiwa ndani ya ndoa?Natambua wanawake wakati mwingine tunapenda "attention", ukijua kuwa kuna wanaume wengine wanakutamani na kuku-chat up unajisikia raha na mwenye nguvu fulani kama mwanamke, kutongozwa ni kawaida kwa baadhi yetu, kwani kuolewa haina maana kuwa hatutamaniwi na wanaume wengine.

Lakini hiyo haina maana kuwa umkubali kila anaekutongoza na kuanzisha uhusiano ukijua uko ndani ya uhusiano mwingine na mtu unaempenda na ulieahidi kuishi nae maisha yako yote!

Uhusiano wa rafiki yako na mke wa rafiki yake ukoje? bado wanaendelea baada ya mwenye mke kuacha? Je wanadhani kuwa wanapendana?......kama uhusiano wao mzuri basi waendelee lakini kama jamaa alikuwa anataka kuharibu ndoa ya mwenzie kutokana na tamaa au wivu basi akamuombe rafiki yake msamaha alafu ajitenge nae (yaani urafiki ufe), asijaribu kuendeleza urafiki na jamaa baada yakumtombea mkewe.

Ushauri wangu ni wewe kumaliza urafiki na huyo mharibifu wa ndoa ya watu kwani ni wazi kabisa na wewe ukioa ataweza kufanya exactly alichokifanya kwa rafiki yake nakusababisha ndoa yako kufa.


Watu kama hawa, wanapaswa kutengwa na jamii, kwani wanasababisha watu hasa vijana kuhofia suala zima la kufunga ndoa, wanaifanya ndoa kutokuwa na thamani tena.Kila lililojema!

9 comments:

Anonymous said...

Duh what hell?,bulshit! huyo hahitaji ushauri mfukuze tu fala huyo.yaani nina hasira naye utafikiri kaniibia mimi,tena na wewe take care atakuibia na wako.ivi watu wa hivi wana roho gani jamani?, hata huyo mwanamke malaya tu hana ishu, huyo ni changu tu how comes ampe rafiki wa mmewe. duh yaani nina hasira hata nashindwa kuandika sana ila jamani wadau tuwe na utu hii iwe changa moto kwa wote wenye tabia kama hizi,wasichana wengi wamejaa kwanini uchukue mke wa mtu?,inakera sana na ni aibu huyo hahitaji ushauri ni mpumbavu akafie mbali huko loo?!! jamani mmh,ivi mtu kama huyu akiibiwa yeye atajisikiaje mana usimfanyie mtu mwingine kitu ambacho hupendi ufanyiwe, inauma sana.

lajk@ymail.com

Yassin said...

Mimi naona kwamba jamaa ana makosa lakini ibilisi alimuingia,,,,,,Pia jamani tukae tujue kwenye mapenzi siku zote hakuna kusikia kabisa ila mpaka uone yamekuharibikia ndio unaanza kujuta sasa na kusema kwamba laaah!!ningejuwa nisingefanya na ukiangalia labda jamaa alikuwa anakula na TI-G sasa hapo anaweza kusikia la nani???Mimi naona hapo kama jamaa kaaribu ndoa ya watu ilikuwa ni bahati mbaya ila pia ni mchezo mchafu kwa nini umuingilie mke wa mtu na kumtongoza??Na kwa nini kama amefanya hivyo mara moja akarudia mara ya pili mpaka mme wa yule mwanamke akagundua jamaa anaonekana bado mshamba wa mapenzi ila sasa ndio maji yakimwagika hayazoleki....ila nadhani DH atakupa maelezo kwa kirefu zaidi na ushauri mzuri zaidi.

Anonymous said...

I hope uliyechangia hapo juu ni mr.ujue kuna mapenzi yale labda useme mtu yupo na mpenzi wa kawaida sio mke wa mtu ukasema jamaa hasikii sawa lkn mke wa mtu!!! mm nilikuwa na rafiki yangu alikuwa na mpenzi ambaye kwa mujibu wa wanaye mfahamu upande wa binti walisema kuwa yule binti ana kashfa ya ngoma lkn huyo rafiki yangu alishauriwa kumuaacha ilishindikana kabisa hapo nakubali kuwa ukiwa kwenye dimbwi la mapenzi unakuwa kama kipofu, lkn hainipi maana kwa case ya mke wa mtu, how can you dare? mke wa mtu!!!!!!!! kaka hapo juu haijakutokea wewe hiyo kitu,inauma sana tena sana, na kumbuka ambacho hupendi kufanyiwa usimfanyie mtu mwingine, imagine hii imekutokea wewe kwa yule love wako umpendae kuliko vyote, naupo tayari kufa kwaajili yake halafu kuna rafiki yako ana share nawe kwa mkeo utajisikiaje? unless tell me kwamba ni binti wa kula nae tu good time sio mkeo, na hujamuoa, na unao wengi so yeye ni substitute tu. wife? asikwambie mtu hata huyo aliyeiba akifanyiwa yeye itakuwa songo mbingo hapo, labda kama alifanya for fun, revenge na vitu kama hivyo lkn hivihivi inauma sana., hasa kama jamaa alikuwa anampenda huyo bibie aliye muacha, aidha utamu wa mapenzi unategemea kiasi gani mnapendana na mkeo/GF/BF. na huo in my view haukuwa urafiki ni umbea tu, urafiki gani hadi kumla wife? huo ni upumbafu, narudia kusema huyo hahitaji ushauri ni mpumbavu tu hana maana,haya wala aibu coz alijua nini anafanya, na alishauriwa kuto fanya hivyo sasa hapa anataka ushauri wanini? wakati ashaboromga tayari,hata hao jamaa wakirudina trust kati yao itatoweka, so cheating na visasi itakuwa ndo mchezo, na siku zote huwezi ishi maisha mazuri kama mwanzo kwani uaminifu utakuwa umepungua hata kama mme apende vipi atakuwa na kinyongo cha kimya kimya moyoni. its maddiness and dubious!, juzi juzi kuna mfanya biashara maarufu kariakoo, kwa kiburi cha pesa zake na kurubuni wake za watu ameishia kuvunjwa miguu alifumwa na mke wa mtu, nayeye aangalie ataja afanyiwe kitu ambacho kitamuumiza maisha yake yote, na inaonyesha ni mzoefu wa kuiba wake za watu ataja akutwe na wenye uchungu na wake zao atazaa dagaa hiyo siku.

lajk@ymail.com

Anonymous said...

hapa hakuna ushauri kama mtu unajali maisha yako huwezi huwezi kufanya upuuzi wa hivyo kwanza una risk maisha yako na ya wengine,how sure hao wanandoa walikuwa free from diseases?. labda umshauri akapime kama yupo salama na kama alikuwa nao masikini atakuwa kawaambukiza hao wana ndoa kwani huo mchezo unonekana ulikomaa kabisa hadi mwenye wake kaja kugundua. mm binafsi sina huruma hata chembe kwa mtu ambaye ataniibia wife kwani huyo anachezea kamali roho yangu so ni dili naye vizuri ili ajue kuwa alichokifanya hakifai ktk jamii, pia kama angekuwa rafiki yangu ndo kafanya huo upuuzi wala asijaribu kuja kuomba ushauri maana ataumia, au zaidi sitamsaidia kwa lolote hana maana ktk marafiki.ni muuaji tu, pengine hata urafiki mimi na yeye ukaisha., nina hasira na huyo jamaa japo simjui looo!!

lajk@ymail.com

Anonymous said...

mshenzi tuu,hana lolote yaani best wako na mke wa jamaa wote ziroooo huna la kumshauri mwambie asubiri 40 yake na yeye,kama haitafika na yeye atafanyiwa na mtu kama hivyo.maana kila mtu atalipwa hapa hapa duniani.

Anonymous said...

yaani leo nina hasira za kufa mtu,bf wangu ana mwanamke mwingine naamekwenda naye kwenye sendoff ya rafiki yake wa huko kazini kwao,hasira zikisha nitaomba ushauri ila sasa nashukuru nachangia mada ya huyu k za wanawake hazibadiliki,kama anakupenda kweli atanyevuka akikuona ni maumbile yake,kumuandaa kila saa mkifanya huo ni uongo anakutumia huyo msichana wako.

Anonymous said...

Huu ni mtihani mkubwa, kwani visa kama hivyo vinatokea sana katika jamii zetu. Tumeshakumbana na maswala kama hayo, unaona kabisa jirani yako anaibiwa na mtu unayemfahamu au narafiki yako, unaogopa kumueleza jirani yako, ukichelea kukosana na rafiki yako.
Swala la kujiuliza je kama wewe ungefanyiwa hivyo ungefurahi? Leo anafanyiwa huyo kesho utafanyiwa wewe hata kama sio huyo rafiki yako,anaweza akafanyiwa na mtu mwingine.
Naona haya machafu yakionekana ni vyema tukayaweka wazi, bora uvunje urafiki kuliko kuona uchafu unafanyika. Bora uwe mpenzi wa Mungu kuliko msindikizaji wa shetani. Ni bora ukose rafiki kabisa kuliko kuwa na marafiki wengi wanaoangamiza jamii.
mimi
emu-three

Anonymous said...

anony wa saa 7:31 A.M, naona una hasira hadi umechangia pasipo penyewe loo punguza hasiara cha kufanya nikuongea nahuyo BF wako vizuri ajue kuwa wewe hupendi hicho kitu ukubaki tu na hasira hujamwambia atajua wewe ni easy woman,au wewe ndo unajipendekeza which means huwezi muacha hata kama wayajua madhambi yake, try to be serious kuna magonjwa chungu nzima haina mantiki yoyote kumpenda mtu anaye hatarisha maisha yako, like wise huyu aliyevunja ndoa hana haya kabisa.
Aidha sijakuelewa unaposema kumuandaa my sweet kila round ni uongo ananitumia! kivipi sijaelewa pls come again! sina uzoefu na wanawake wengi so nilitaka kujua kama hiyo kitu ipo au haipo na sababu zake.
by lajk@ymail.com

Anonymous said...

Dah! kweli huyu dada aliyeporwa na mwanamke mwenzie ana hasira, mpaka kakosea hata mchango wake kachangia sio penyewe duh! taratibu dada utaua, nimecheka sana unaposema una hasira ya kufa mtu, pole sana dada yangu.