Ndoa imekuwa Ndoano,nimechoka!-Ushauri

"Hi Dinah, ukisikia la mwenzako utasema afadhali na langu lakini hebu angalia, mume wangu ni wale wasiojua kupendwa nilimuonyesha mapenzi motomoto[ binti wa kitanga] lakini haku appriciate mwisho nikachoka nikawa namuona kama mtu tu ndani ya nyumba mpaka nimesahau wajibu wangu kama kumgeukia tukilala kwani hata umlalie yeye analala kifudifudi ndio maana nami nimeacha.


Tendo la ndoa atake yeye ukitaka wewe hataki tena kwa maneno machafu na kuhama chumba hali hiyo imeni-affect kiasi kwamba akitaka nampa lakini silalamiki simsifii wala mguno wa aina yeyote ile kwani nahisi anadhurumu nafsi yangu.


Sipendi kutoka nje ya ndoa hivyo niliamua kujipiga punyeto wakati nikihitaji na na-enjoy kuliko hata anavyonifanya kwani ni mchoyo akikojoa yeye basi, kwasasa amenitia mimba[miezi 5] nayo kama imetumwa nyege kibao.


Kupiga nyeto Daktari anashauri sio nzuri ukiwa na mimba hivyo nikamueleza mwenzangu akanijibu nifute akilini hawezi nisaidia na tunaenda kwa week mara 1 au mara 2 kwa mwezi. Mimi sasa akitaka namnyima kwa hasira lakini wakati huohuo nina nyege, roho inauma sana.


Kingine sio mtu wa kulea kutokana na hali ya mjamzito anataka nini anaona kama najifanyisha nikimwambia najisikia vibaya,nikitaka matunda napigwa Calender nikimwomba kuichuachua kidogo miguu kwani inailekea kuvimba hataki, yaani sio wa kunisikiliza kwa lolote hatukai tukashauriana anachoamua yeye ndio hichohhicho kiujumla hakuna mapenzi.


Lakini nikimwambia nipe talaka yangu hataki nimechoka kuishi ndoa isiyo na upendo heri nikae mwenyewe, haijawahi kutoke siku akanisifia sifa zote za ubaya ninazo mimi naitwa jeuri, mbishi mchoyo, mchafu.


Wakati mwingine nasema kama ningejua nisingeolewa na tayari tuna mtoto 1 na huyu wa pili na ni wadogo nikae nilee watoto wakue eti wapate malezi ya baba na mama huku kila nikimwona au kusikia sauti yake hasira zinapanda au nikae mwenyewe nilee wanangu kama nitapata tutakae endana nae uongo dhambi nitaishi nae nina miaka 29 tu.

Nitashukuru kwa ushauri wenu na Kiongozi wetu mwana wa Nkibi"

Jawabu:Aisee ni kweli kabisa kuwa ukisoma tatizo la mwenzio unaweza kupata ahueni kuwa lako sio kitu. Lakini ukweli unabaki pale pale sote yunahitaji kuwa na furaha ndani ya mahusiano yetu ya kimapenzi hasa ndoa.

Kabla sijaanza ningependa ufahamu kitu kimoja ambacho wengi huwa hatukitilii maanani pale tunapokwenda kufunga ndoa. Mtu anapotaka kufunga ndoa huwa kuna sababu kwanini anataka kufunga ndoa na wewe haijalishi ni mwanamke au mwanaume.

1-Kutokana na Imani ya Dini tunafunga ndoa kwa vile tumeambiwa kuwa tendo la ndoa kabla ya ndoa ni dhambi, hivyo ni kama vile tunafunga ndoa ili kungonoana kihalali (usininukuu), hapa inawezekana kukawa na mapenzi au matamanio.

2-Kutokana na Imani hizo za Dini pia tunafunga ndoa ili kujenga familia bora inawezekana kusiwe na mapenzi.

3-Tunafunga ndoa ili kuwa na heshima mbele ya jamii (Africa zaidi) au kuondoa mkosi, hapa tutafunga ndoa bila mapenzi.

4-Tunafunga ndoa kwa vile tunalazimika kufanya hivyo kutokana umri, hapa vilevile mapenzi hakuna.

5-Tunafunga ndoa kwa vile tumeelewana kuwa kwenye uhusiano na kugundua tunapendana na kutaka kuishi maisha yetu yote pamoja (Kisasa).

6-Tunafunga ndoa kwa vile wazazi wanataka ufanye hivyo, hapa utafunga ndoa na yeyote atakaejitokeza bila mapenzi, nasikitika kusema tena kuwa hapa mapenzi hayapo.


7-Tunafunga ndoa kwa ajili ya kupata sifa, umeoa/olewa na mtu kutoka kabila/nchi fulani, mtoto wa fulani, mzuri, maarufu n.k. mapenzi hakuna.

8-Tunafunga ndoa kwa vile marafiki zetu wote wamefanya hivyo na wewe unahisi kuwa nio pekee umebaki bila mume/mke, hakuna mapenzi.

9-Tunafunga ndoa ili kupata msaidizi, iwe ni kupikiwa au kujikimu kutokana na ugumu wa maisha, hapa mapenzi ni sufuri,......kama kunamengine unaweza kuongeza.

Ili ndoa iwe nzuri, yenye amani na upendo inatakiwa ijengwe kwenye misingi ya mambo mengi (inategemeana na ninyi wenyewe) lakini muhimu zaidi ni mapenzi mliyonayo kati yenu ninyi watu wawili.

Sina uhakika ( hujanipa maelezo) ya uhusaiano wenu ulivyokuwa kabla hamjaamua kufunga ndoa, mlikuwa kwenye uhusiano kwa muda gani kabla ya kufunga ndoa na vilevile ngono ilikuwaje?......


Sasa pale uliposema kuwa wewe ni "mtoto wa kitanga" ni wazi kuwa ulimaanisha ni mjuzi wa mambo ya kuridhisha, liwaza na kufurahisha mpenzi si ndio? lakini pamoja na ujuzi wako na bidii kwa mumeo huyo hakuna kilichobadilika na badala yake hali inazidi kuwa mbaya na yeye kukutenga.


Inawezekana kabisa kuwa "maujizi" unayompa sio yale ambayo yeye anataka kutoka kwako, sasa badala ya kumfanya afurahie unamfanya ajisikie ovyo na huenda anashindwa kukuambia kwa vile anaogopa kukukatisha tamaa kama sio kukudhania kuwa wewe ni "mwingi wa khabari" (Malaya) kwamba unajua mengi ukilinganisha na umri wako.....si unajua baadhi ya wanaume wa kibongo? Bado wanamavumbi (not open minded)


Lakini kitendo cha yeye kufanya ngono anapotaka na kuhama chumba ikiwa wewe unataka ngono inanifanya nihisi kuwa huyu bwana (mumeo) hana mapenzi kabisa na wewe na anapongonoka na wewe ni kwa vile anahitaji kupunguza nyege yaani unatumiwa kama "chombo" cha kumalizia tamaa zake za mwili au kama wanavyosema "kiburudisho".


Ikiwa huyu bwana hana mapenzi na wewe ni wazi kuwa hawezi kukulea, bembeleza wala kujali hisia zako, chochote utakachohitaji kwake itakuwa ni usumbufu.


Kama unampenda (najua umechoka lakini.....) kuomba Talaka kabla hujajua tatizo linasababishwa na nini na kujaribu kulitatua sio jambo la busara, Suluhisho ni kuzungumza nae (Wasiliana) na wewe kama mwanamke kuchukua jukumu la kumfanya mwanaume huyo akupende au awe na mapenzi na wewe kwani mwanamke ndio mtu pekee anaeweza kujenga maisha bora na mazuri ya ndoa au kuyabomoa.


Wanaume kama mume (samahani Kaka zangu) huwa wanadai kuwa wao ni kama watoto wanahitaji kubembelezwa wakati mwingine, sio kubembelezwa tu bali kufundishwa, kuelekezwa, kuambiwa na kuongozwa na anaeweza kufanikisha hayo yote sio mama yake bali ni wewe mkewe. Kama unamapenzi ya kweli kwake basi pigania penzi lako, sio unaachia kirahisi hivyo wakati uwezo wa kuweka sawa mambo uko mikononi mwako.


Baada ya kujaribu hayo na kushindikana hapo ndio linapokuja suala la kutafuta "ustaarabu mwingine" iweni ni kumpa nafasi (kutengana) au kuchukua kilichochako (Talaka)...



Nini cha kufanya-Muonyeshe mapenzi ya hisia na sio ya mwili, jitahidi kuwa karibu nae na kuzungumza nae kwa kumuangalia machoni (ana kwa ana) kuhusiana na unavyojisikia juu yamapenzi yako kwake (sio kulalamika), Muulize kama alipofunga ndoa na wewe hakuwa tayari au hakuwa na mapenzi ya dhati juu yako.

Sema wazi kuwa kama alikuoa kwa sababu nyingine na sio kwa mapenzi unaelewa anavyojisikia na hata kama ingekuwa wewe ungejisikia hivyo ajisikiavyo yeye......lakini wewe unampenda sana, (hapa mmwagie misifa zinazokaribia na ukweli)........sio kumuambia yeye mzuri hapana, sifa kutokana na utendaji wake kitandani, uongeaji wake, muonekano wake, busu zake, mwendo, misuli yake ya kiume n.k tena fanya hivyo ukionyesha ashiki lakini usipitilize, kumbuka unaonyesha mapenzi ya hisia na sio ya mwili hapa.

Hoji kwa upole na upendo kama kuna tatizo lolote ambalo labda wewe hulijui akueleze na mtafute suruhisho kwa pamoja kama familia, husisha watoto kwenye maongezi hayo, kuwa wanahitaji kukua kwenye mazingira ya upendo na amani utokao kwa wazazi wao ambao ni wewe na yeye.

Mawasiliano hayo yatasaidia kumfanya awe huru kutoa yaliyouaza moyo wake (inategemea na utakavyo muanza na jinsi utakavyo m-bembeleza na kumshawishi kwa mapenzi ya hisia, wanawake tuna uwezo huo)......ikiwa alikuoa wewe bila mapenzi yake anaweza kueleza hilo, kama ni "maujuzi yako" yanam-put off atasema (kumbuka unatafuta suluhisho), sasa hata akikuku-offend wewe chukulia kawaida.

Baada ya hapo utakuwa umejua ukweli kwanini amekuwa na tabia ya ajabu, hapo atakuwa amekupa mwanga wa kuweka mikakati madhubuti kurekebisha mambo. Usimtenge, endelea kumuonyesha mapenzi ya dhati. Siku akitaka ngono mmpe kwa mapenzi yako yote na wewe i-tune akili yako kuwa unafanya mapenzi na mumeo ili uweze kufurahia.

Ikitokea wewe unataka usimuambie moja kwa moja kuwa unataka kutiwa na badala yake fanya vitendo vitakavyomfanya awe-relaxed......kabla hujalianzisha, na unapolianzisha sio unakimbilia kufungua zipu na kumnyonya "abdala kipara" na badala yake cheza na zile kona za kumnyegesha mwanaume kwa kutumia ulimi au mikono na vidole.

Nasikitika kusema kuwa mwanaume anapokuambia mambo fulani na kuyarudia mara kwa mara tambua kuwa kati ya hayo moja au mawili ni kweli, hivyo ni wajibu wako kufanya mabadiliko. Sasa angalia kwa undani haya yafuatayo ambayo nitayafafanua ili unielewe vema.

Ujeuri-Kutokana na kukosa ngono ipasavyo ni wazi kuwa huna raha na inakusababishia hasira hivyo chochote mumeo atakacho kuuliza au kukuambia unaweza kumjibu kijeuri, pengine sio yeye tu bali kila mtu aliye karibu na wewe. Badilika.

Uchafu-Pamoja na kujiswafi kwako na kuoga, huenda manukato unayotumia (waoga maji ya hiriki au marumba-rumba, wajifukiza udi, mafuta uzuri yatokanayo na mkaratusi etc) ambayo Bibi alikuambia humvutia mwanaume huyu mumeo yanamchefua.

Unajua harufu za manukato (hata kama ni Oganza) zikijichanganya na harufu asilia ya mwili inaweza kutoa harufu mbaya mmno na harufu ya mwili ni bonge la pu-off. Vilevile inawezekana jinsi unavyoiweka nyuma, iweke nyumba ionenkane kuna mwanamke, jipende, badilisha mpangilio wa vitu kila baada ya miezi 3-6, ipambe lakini isiwe too much.

Pia isije kuwa jinsi unavyovyaa.....mwanamke kujipenda na kuvutia, hivyo sio unatilia mavazi mazuri ukienda harusini tu bali mvalie mumeo vizuri ili avutiwe na wewe. Badilisha mtindo wako wa kimavazi na jinsi unavyoiweka nyumba yako.

Uchoyo-Kutokana na hasira, kutokuwa na furaha, inawezekana unapika chakula cha aina moja au hupiki kabisa kumkomoa au kutuma ujumbe kuwa wewe ni muhimu, lakini yeye halioni hilo bali anakudhania kuwa wewe ni mchoyo. Vilevile inawezekana anapokuja na wageni na wewe huonyeshi kufurahi (kutokana na matatizo yako ya ndoa), lakini wageni hao na mumeo wanahisi kuwa hupendi waje kwako kula, ukidhani wanakuja kula n.k.

Ubishi-Unayokumbana nayo kwenye uhusiano wako yanaweza kuwa ni matokeo ya wewe kujaribu kupigania haki yako, mumeo anapokuambia kitu au kuomba kitu unabisha kukifanya kwa vile yeye huwa hafanyi lolote unapohitaji. Kumbuka nimekuambia onyesha mapenzi ya hisia, basi acha ubishi.

Baada ya yote haya mumeo haonyeshi kubadilika hata robo? Girl go for the Talaka, tunafunga ndoa ili kuwa na furaha, kupata ushirikiano ktk nyanja zote lakini wewe huzipati, kisa cha kuwa single mum with a husband??

Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
Wao,its so sad story i real sorry
for you.
Anonymous said…
pole sana dada,pole tenapole haswaaaaa,nina maswalikabla yakutoa maoni yangu
1.mlipokuwakwenye uchumba hukuona hayo yote?au labda ulilazimishwa kuoana naye

2.ulipoingia kwenye ndoa mtoto wa kwanza uliona hivyo ikawaje ukaachia wapili?au alikubaka

sasa kimawazo yangu naona umeolewa na ngumbaro"mtu wa miaka 47"hajui kupenda wala kupendwa.cha kufanya usivunje ndoa tulia lea watoto,akitaka uchi mnyime mwambie nikokwenye siku mpaka achoke kama anakupenda atakuuliza siku haziishi?hapo ndo mweleze yano kusibumwaga yote.ukiona haja kuuliza jua hana mpango naww kabisa alioa kuondoa mikosi tuu huyo,kama ukiachana naye utapa amani,fanya moyo wako unavyokutuma. siku njema......
Anonymous said…
pole sana dada yangu kwa hayo na nikupe pongezi kwa kuwa mwanamke muaminifu, keep it up, sio wanawake wote wanaweza fanya hivyo ukilinganisha na ukame wa mambo ya utamu,umenikosha hapa ''Sipendi kutoka nje ya ndoa hivyo niliamua kujipiga punyeto''.
Kwa mtazamo wangu upande mmoja, unaonyesha kuwa wewe ndio chanzo ''nilimuonyesha mapenzi motomoto'' which means umeacha, ni big mistake! maelezo yanaonyesha umstarabu sana kujali lkn ulishindwa kumwambia ukweli kwanini haonyeshi response kwa unayo mfanyia?,the essence of communication between lovers! love inahitaji ubunifu kuiweka iendelee kuwepo.pia mambo ya usafi lazima ukae mkao wa kumvutia husband for ever, hata kama umezaa, kuna wengine huwa wanakuwa wachafu hawatamaniki, kisa analea!!mara 1 au 2 kwa mwezi, duh hiyo kali hapo kuna jambo gumu mtoto wa tanga umechemsha!.


kwa upande mwingine japo hujasema umri wa mzee, nina wasi na hilo yaani kama kibabu hv! am serious on this sorry!! pia kazi anayaofanya pengine anachoka sana na misosi sio supportive kupata nguvu,pia pengine ana low sexual drive, so ur not matching for that case.aidha anaweza kuwa ni mtu mwenye stress muda mwingi [ubunifu zaidi unahitajika hapa kwani mtu wa hivi anahitaji zaidi kufarijiwa na kiburudisho aka wife na vitu kama hivyo kwani mind yake inakuwa haipo kwenye constant move kazi hapo ipo kumtoa huko na kumleta kwenye akili ya mapenzi]
kumbuka ulikuwa unalea, mapenzi yalikuwa zaid kwa mtoto, baba alisahaulika si haba pengine unasaidiwa na small hausi.
na kwakuwa upo namsimamo mzuri kabisa ktk wanawake na upo siriaz na hili,nilifikiri ungempeleka apate ushauri hata kwa huyo Dr alokwambia nyeto sio mwafaka ktk kipindi hiki, pia ndugu jamaa na marafiki watumike ukishindwa ww mwenyewe na punguza hasira kama ni muelewa atajirudi tu hasira mara nyingi huwa ni hasara,jaribu kusoma mood yake then ongea nae huyo sio hawara lazima ajue kiasi gani unahitaji ushirikiano wake.pia usisitishe ushirikiano wako kwake hapo hujui pengine unasaidiwa, ukibana small hausi itapata chance zaid. ni hayo tu kwa leo,

lajk@ymail.com
Anonymous said…
Pole sana dadaangu,najua kumeza unashindwa,kutema pia unashindwa,mie ni mwanamume 28 yrs,kweli cjapenda vitendo vya mumeo,ndoa haiwi hivyo,hata kama ana vimwana nje hatakiwi kukutesa na kukunyima uhuru wa ww kufanya unachopenda kwake.mke ni mtu wa kwanza kucare kwa wanaojua lakini. Mi nasema kwenye wanandoa kuna mambo mengi sana,ikitokea kama hayo jaribu kuwa mvumilivu kidogo,na jiweke vizuri na sema nae,njia iliyo bora kufikia muafaka wa jambo lolote ni mazungumzo,na kutaka ushauli kama ulivyofanya. Dinah yupo na wadau wapo,wackilize wanasema nn. Mi naondoka mdogomdogo,niache nafac.nikipata wasaa ntarudi niongeze kitu.
Anonymous said…
pole mdogo wangu. Wanaume baadhi ndiyvyo walivyo hawajui mapenzi tena ukiwa mja mzito unakuwa na utamu wa kipekee lakini kwa kuwa hajaribu atasikia tu kwa wengine. Kwanza nakushauri ukumbuke una uja uzito sometimes uja uzito unakufanya uwe na hasira na mood ambazo hukuwa nazo subiri vumilia ujifungue na uangalie tena. Ukiona hali inaendelea hivyo nakushauri utoke. Gone are the days-ni siku za kale ambapo wanawake walilazimika kukaa na wanaume eti kwa kuwa watoto wanahitaji baba na mama. Iwapo baba hayupo for you his woman atakuwepo kwa ajili ya watoto? Iwapo unajipima unaona uwezo wako uko poa songa mbele dada na wala usihadaike kwamba huwezi kumpata mtu mwingine wa kukupa raha au hata kukuoa. Wanaume wastaarabu nao wapo japo wachache. Unachohitaji sasa ni kuwa mvumilivu ujipangie mkakati wa kumudu maisha yako bila mumewe. Jiulize maswali muhimu kama utaweza kuishi maisha ya kuwa alone tena? Na kuhusu punyeto-haina shida mdogo wangu kinachomatter hapo utumie kifaa kizuri ambacho hakitakuchubua wala kufika kwenye cervix yaani iwe kwenye G spot. Usihadaike wanawake wengi wameolewa lakini hawapati raha kwenye sex kwani wanaume wengi wanajifikiria wenyewe na wanaona kwamba kuongea kuhusu sex ni kazi ndiyo maana asilimia kubwa wanaamua kuchukua machangu kwani hawahitaji discussion. Wewe ni mwanamke wa heshima. Unastahili the best. subiri jifungue pina na jipange kisha uachane naye mwanamme ambaye unakaa naye tu kama pambo ndani ya nyumba. Usikate tamaa na usimfanye huyo mume kuwa Mungu wako. Kuna maisha zaidi ya hapo na ukijipangilia utapata.
Anonymous said…
Yaani kabla sijachangia, mdogo wangu wewe umenichekesha kweli jinsi unavyoandika! yaani nimecheka hapa sina mbavu.. utafikiri mazuri hayo unayofanyiwa.
Eti mimba kama imetumwa.. nyege kibao! ha haaaa jamani nitarudi baadae kuchangia.
Anonymous said…
Pole sana dada kwa shida inayokupata ndani ya ndoal. Lakini dada katika mazingira magumu kama hayo, kwa nini uliamua kubeba mimba na unajua mume hana mapenzi na wewe? hili ni kosa kubwa umefanya kwani utaendelea kupata shida hizo hizo pengine na zaidi. jaribuni kuwashirikisha wazazi labda wanaweza kumshauri akabadilika. Otherwise we leo mimba yako hivyo hivyo kininja ninja mpaka utakapojifungua.

Msomaji
Anonymous said…
Wanaume bwana, labda anamtu nje, jaribu kuchunguza, maana sababu halisi ya ufirauni huo haueleweki - hebu jaribu kuchunguza vitu kama simu yake, wakati gani anapenda kulala kifudifudi, na mida anayorudi nyumbani kutoka kazini.Lakini, mimi nakushauri kuwa una point either ukae hivyo hivyo mpaka uzee na yeye kutotaka kubadilisha tabia au utafute utulivu wa mawazo, maana kama unasikia hasira ukisilia sauti yake tu, basi inamaana kuwa wakati mwingine itakuwa unajikuta unafoke watoto au hata kuwapiga kwa ajili ya hasira ambayo inakumaliza moyoni. Jamani NDOA NI KWA WOTE WAWILI NA KASUMBA ZILE ZA MIAKA 40 INABIDI ZIISHE ILI BABA NA MAMA WOTE WACHANGIE KUBORESHA NDOA YAO!!!
Anonymous said…
Wanaume wengi wa kibongo wako kama huyo mume wako ndio maana wanawake wengine wanaamua kutoka nje ya ndoa zao hivihivi.
Anonymous said…
Anony wa 9:45pm nashukuru kwa kulieleza hili jambo waziwazi. Hii kwa kweli imekuwa ni kasumba ya wanaume 80% ya wabongo. They really dont care.
USHAURI WANGU.
Vumilia lea mimba yako maana huo ni msalaba wako. Ukijishaua kuondoka sasa hivi na Bongo ilivyo ngumu nani atalea mimba na mtoto/watoto wako? Unless una kazi nzuri na familia yako wapo tayari kukupa support. THINK TWICE.
Bubbles.
Anonymous said…
muomba ushauri. hatukulazimishwa tulipendana ila kwa muda mfupi,na hali ilianza tangu tuanze maisha nilidhani nitamlekebisha lkn hiki ni kisiki ingawaje sasa imezidi, aliponitundika ya 2 tulikuwa tunaelewana nami nilijua sasa ananipenda ndio nikampa yote kama watu wanavyosema usikaze kwa sana akatoka nje,asanteni kwa ushauri wenu
Anonymous said…
Pole mpenzi kwa maswahiba yanayokupata. Usiondoke ktk ndoa yako, vumilia. Watoto wawili kuwalea mwenyewe si kazi ndogo. Jitahidi kuwa msafi, mpole, mkarimu, hata akikasirika jitahidi mpenzi, ndo wanaume wa kibongo wanataka hivyo. Hata mimi nilikua na matatizo kama yako, nikaacha hasira, nikaanza kupendeza na kumpenda sana ingawa wakati mwingine najilazimisha, Mungu mwema imesaidia sasa nafurahia ndoa yangu. Usikate tamaa, muweke Mungu mbele pia huku ukibadilika, trust me! it will work out.

For Dinah!
Dinah I don know you, bt kwa jinsi ulivyo na ushauri mzuri na busara nimekupenda sana. Kip it up mummy!
Anonymous said…
Hello wachangiaji, jambo moja ambalo naomba msiwe so biased, ni kwamba karibu kwa silimia mia hamjajua nini kiko kwa huyo mama ambacho yamkini kinachangia nsana matatizo aliyoyaeleza hapa.Nina maana kama ingetokea huyo mwananume wake akaeleza ya kwake bika shaka mngekuwa na nafasi nzuri sana ya kuyapima matatizo yao.

Eleweni kwa makini yanayoelzwa na huyu mama.Kama wao walipendana na amesema kwa muda mfupi,lakini kwa kuridhika naye,bila shaka kuna mambo mengine ya zaidi kwa upande wake.Mimi nawashukuru wale ambao wamemsihi avumile kwani ni yeye hASA ANAYEMJUA MUMEWE hivyo ni yeye atakayejua zaidi nini afanye.Lakini ukisema achana na mume huyo!! Wahenga walisema "Mkimbia tope hukanyaga mavi"

Jambo lingine wengi wamesema "wanaume wa bongo wengi wako hivyo" Hilo ni jumlisho la ajabu mno.Sijui mumewahi kuolewa na wanaume wa west?, wa Europe?, asia? india? Russia? au skandinavian? mkaona wako tofauti? ninayesema hapa niko nje ya nchi na nimezunguka katika nchi kadhaa hapo juu ambazo giant.Labda mmetumia njia hiyo kama kumpherapitise na kusympathatize na huyo mlalamikaji.

ushauri wangu wewe dada jukumu liko kwenye roho yako na kwenye uelewa wako maana hapa hatujui mumewe ana nini ndani yake kinachomsibu juu yako.La muhimu kama walivyoshauri wengine,kaa katika makao wa kuleta amani ndani ya nyumba yako.Kama wewe ni mkristo basi tafuta ushauri wa pamoja na mumewe kwenye uongozi wenu wa kanisa.Unapoleta hapa wewe kama wewe tu utachanganywa na baadaye utajuta.Ni vizuri wote wawili msikilizwe ili ufumbuzi wa tatizo hilo upatikane mkiwepo wote wawili.Nakutakia kila lililo jema katika hatu nzuri utakazochukua kwa hilo linalokusibu.