Nampenda mume wangu lakini hani-apreciate!-Ushauri






"Dada dinah mimi sijui hata nifanye nini kwani kila siku najikuta sina raha na mume wangu ndani ya nyumba. Nimeolewa miaka mitatu sasa na nimevumilia wee sasa nimechoka kabisa na tabia yake ambayo mimi sijaizoea. Siokwamba hatuzungumzi mambo ambayo hayatufurahisi, tunaongea sana tu lakini inaonyesha kuwa hawezi kujirekebisha.




Tatizo lenyewe ni hili, mume wangu hajawahi kusema asante nikimfanyia jambo au kitu. Yaani hata baada ya kula asante huwa hamitoki anaishia kusema nimeshiba au chakula kilikuwa kitamu, ile shukurani haipo, hata kama amekinunua yeye si bado jamani anatakiwa kunishukuru mimi kwa kumpikia kama ninavyomshukuru mimi akinipa pesa za matumizi au akija na chakula nyumbani huwa namwambia asante kwa kununua kitu fulani.



Kitu kingine ambacho sina uhakika naomba wewe unisaidie kutokana na uzoefu wako ni hivi, eti kumfulia na kumpigia basi mume wangu ni wajibu wangu wa ndoa? na je nikimfanyia hivyo anatakiwa kunishukuru au inakuwaje hapo.



Alafu tukifanya mapenzi na kumaliza nani anatakiwa kumshukuru mwenzie? na je unamshukuruje mpenzi wako baada ya kufika kileleni?



Dada dinah wengine tuliolewa bila kuwa na bahati kama uliyokuwa nayo wewe, tuliolewa tukijua kusema asante na samahani mengine tunajifunzia humo humo na wakati mwingine unaishia kukasirika tu kwa vile unahisi mpenzi wako hakujali wewe wala yale madogo umfanyiayo.



Nifanye nini ili na mimi nijisikie spesho ndani ya ndoa yangu?"


Jawabu: Kweli umevumilia sana kwa miaka yote mitatu kuishi na mtu ambae unahisi haku-apreciate, kwa kweli inaumiza sana kwa mtu ambae anaelewa umuhimu na thamani ya kuonyeshwa kuwa uko-valued kwenye uhusiano wako na kuwa-appreciated hata kwa kile kidogo unachokifanya.


Nafurahi sana kuwa umelileta hili mahali hapa ili wale ambao labda walikuwa hawajui ni jinsi gani baadhi yetu huwa tunajisikia ikiwa wenza wetu hawaonyeshi shukurani kwa uwepo wetu achilia mbali vile vidogo tufanyavyo.


Mimi binafsi kama Dinah sipendezwi na tabia ya baadhi ya watu na kukufanya wewe ujisikie "unppreciated" ni kama vile unajipendekeza au mpenzi hana habari na wewe (huenda anakujali and all that lakini haisaidii ikiwa sioni, hunionyeshi kuwa unashukuru, unani-value n.k), Kitu kidogo kama kumuambia mpenzi wako "nakupenda" bila kupata ile "nakupenda pia" inaweza kukufanya ujione "msaidizi" badala ya mpenzi wake.


Unatambua, kuna baadhi ya watu (wake kwa waume) wanapokuwa na wewe kama mpenzi/mke wanahisi kukumiliki hivyo chochote unachokifanya kwa ajili yao ni haki yao na "actualy" unapaswa kufanya hivyo kwani wamekuoa au umewaoa kitu ambacho sio kweli na kama ni Imani basi ni potofu kuliko maana halisi ya neno lenyewe.

Kuna wanandoa waliwahi kuja kwangu wakitaka ushuri, nilipozungumza nao niligundua kuwa hawafanyi vile vitu vidogo ambavyo wengi tunavidharau bila kujua umuhimu wake kwenye maisha yetu kama wapenzi, Mume alikuwa anadai kuwa anahisi kuwa hamridhishi mkewe kitandani kwavile mkewe huyo hajwahi kuonyesha shukurani kila wanapofanya mapenzi........sasa unaweza kugundua umuhimu wa shukurani kwa baadhi ya watu.

Mtu kama wewe (muuliza swali) asante kwako ni muhimu na inakufanya ukose amani ndani ya ndoa yako(this is serious), si ajabu unajihisi mpweke wakati mwingine kwa vile unahisi kuwa mumeo haku-appreciate.

Wengi tunatofautiana kimalezi kwani tumlelewa ktk mazingira tofauti, baadhi yetu tulifundishwa umuhimu wa kuomba msamaha, kuomba ikiwa unahitaji kitu na kushukuru unapopewa au fanyiwa jambo lakini wapo ambao vitu kama hivyo havikuwepo kabisa (msome m3 kwenye Comment).

1)-Kweli kabisa mumeo anapaswa kushukuru kwa kumpikia na kumuandalia chakula hata kama yeye kakinunua, unapompikia mume wako mara nyingi unapika kwa mapenzi yako yote, utamu wa chakula au uchaguzi wa nini kiliwe siku hiyo unatoka moyoni mwako na unafanya hivyo ili mume wako akirudi nyumbani afurahie chakula hicho. Sasa asiposema kuwa kakipenda na kushukuru kwa kweli inakatisha tamaa na inauma mno.

Kule kwetu tunaambiwa/fundwa kuwa hakikisha mumeo hali chakula cha mwanamke mwingine(hata kama ni mama yake), ikiwa anapenda kula kwa mama'ke au kwa rafiki yake (mkewe kapika) au Hotelini basi hakikisha unajifunza mapishi hayo......got the point eeh?

2)-Kitu chochote unachokifanya ndani ya ndoa yako kwa ajili ya mpenzi wako sio wajibu wako wa ndoa ni mapenzi yako juu yake, kumjali na kuhakikisha kuwa anakuwa msafi na anapendeza wakati wote bila kusahau kumsaidia labda kutokana na shughuli zake nyingi za kikazi. Lakini kama wote mnafanya kazi basi mnapaswa kufua pamoja au mmoja wenu kufanya hivyo akipata nafasi......ndoa ni ushirika hivyo mnatakiw akushirikiana na kusaidiana ktk kila jambo ndani ya nyumba yenu.

Bila shaka ikiwa atakuta nguo zake zimefuliwa na akunyooshwa basi anapaswa kuonyesha kuwa ameona hili na anashukuru kwa kufanya hivyo....."mke wangu asante kwa udobi" sio sentensi ngumu na wala hulipii kodi japokuwa kwa mwanamke inathamani kubwa sana.

3)-Ku-appreciate baada ya kufanya mapenzi au hata wakati mchezo unaendelea inategemea na wahusika wenyewe, unaweza ukawa unasema jina lake na kumwambia kiasi gani unapenda anachokifanya na mengine yatakayokujia wakati huo unaposikia raha/utamu.

Vilevile unaweza ukamkumbatia kwa nguvu na kwa mapenzi yako yote na kumbusu kabla "hajang'atuka" mwilini mwako, pia unaweza ukasema asante na kumuambia jinsi ulivyofurahia "the moment" na kama amekufanya ktk mtindo tofauti au leo umehisi kichw akikubwa zaidi kuliko jana mwambie......na yeye akafanya hivyo kwako.

Ufanye nini basi ili aanze ku-appriciate-Ondoa hasira na anza kuwa unamshukuru kila anapokufanyia kitu hata kama ni kukukata ukucha, mwambie asante na mpe kibusu shavuni au mshike kuonyesha shukurani yako. Hilo mosi.

Pili, Mwambie ukweli tu jinsi unavyojisikia, mwambie kwa upole na kwa upendo kuwa unahisi "unappreciated" na inakunyima amani kabisa moyoni mwako.

Mueleze kuwa unapompikia chakula huwa unakipika kwa mapenzi yako yote, na huwa unasikia raha ikiwa anaonyesha kukipenda lakini unahisi "special" zaidi ikiwa atasema asante kwa chakula kitamu n.k

Ni mumeo na hakika anakupenda, ikiwa alikuwa hajui kuwa "shukurani" ni muhimu sana kwako basi atataka kujua zaidi vitu gani akifanya unahisi kuwa na wewe ni "special wife" kwake na ataanzia hapo, taratibu lakini surely na atazoea na maisha yako ya ndoa yatakuwa mazuri na kwa vile utakuwa na unahisi spesho kama ulivyosema na vilevile hutokuwa na hasira tena.

Mungu ailinde ndoa yenu, kila la kheri!

Nakuja......

Comments

Anonymous said…
Samahani kwa hili ninalotaka kushauri- kama mimi lakini. Unajua katika hali zetu za kimaisha tunatofautiana sana kutokana na malezi yetu au mahali na mazingira tuliyokulia nayo.
Kwahiyo mnapokutana, uwe umekutana na rafiki au maofisini,kijweni, kwenye ndoa, nk, usikimbilie kulaumu hili au lile. Kwasababu maisha tuliyokulia yanatofautiana na kila mtu ana mtizamo wake.

Baada ya kusema hayo, mimi nakushauri kuwa, ujaribu sana kukwepa kujiwekea vikwazo, ambavyo vinaweza kukusononesha. Vikwazo kama `kwanini yeye hafanyi hivi, kwanini yeye haniambii hivi nk..’ Hivi ndivyo ambavyo vinasababisha sasa hivi kulegalega kwa ndoa zetu.

Jambo la muhimi ni kuchukulia kama ilivyo(take it easy), huku unatafakari kwa hekima jinsi gani ya kuliondoa hilo tataizo kama linawezekana. Lakini ukijisononesha utakonda, utapata vidonda vya tumbo, presha nk, wakati mwenzako haelewei kwanini.

Ni vizuri kila unapofanyiwa iwe wema au jambo lolote kutoa `ahsante’,kama ilivyo kutoa shikamoo kwa mkubwa. Lakini wapo ambao kusema ahsante kwao ni vigumu,sio kwa mumeo pekee. Wapo ambao hawajui kusema `naomba' hata kama ankuomba kitu chako, atasema `nipe', kama vile ni kitu chake.
Hali hii inatokana na jinsi tulivyolelewa toka utotoni. Na hii ni changamoto kwako wewe kama mzazi kumzoesha mtoto wako kusema `naomba' au kusema`ahsante' kila anapofanyiwa kitu.

Unapofikia utu uzima kama hukuzoea kusema ahsante, mara zote ulimi wako utakuwa mgumu kutamka neno hilo. Na mnapooana mnazoeana kisi kwamba hata kama mlikuwa mnapeana shikamoo kabla hali hiyo inafutika. Kwahiyo wewe kama mwenzake unatakiwa ulichukulie kibusara. Na ni vyema wewe ukawa uanasema ahsante kwa niaba yake mwishowe naye atakumbuka kusema hivyo.

Kuhusu swala la mahusiano, swala kubwa lakujiuliza ni hili. Je wakati mnangonoana, ni nani alikuwa anapata raha kutoka kwa mwenzake? Jibu ni moja wote mlikuwa mnapata raha, na sidhani kwamba wewe ulikuwa umakaa kamagogo,au yeye alikuwa amekaa kama gogo huku akipokea raha fulani kutoka kwako au wewe kutoka kwake.
Kwa hivyo basi kwa hulka kama ileile niliyoieleza awali,usiogope kumwambia mwanzako ahsante, na wakati mwingine ongezea `namimi naomba ahsate yangu, au ahsante kwa niaba yako na vitu kama hivyo.
Vipo vitu vidogovidogo katika mahusiano yetu ambavyo mtu mwingine asipofanyiwa vinamkera mwenzake, wakati huo mwingine anaona ni kitu cha kawaida, au havina umuhimu au nikupoteza muda nk.

Kwa mfano mtu mwingine akiwa anakula kitu hata kama ni kidogo namna gani au hata kama hakifai kuchangia lazima amwambie mwenzake `karibu' au sio.

Naomba nikuulize swali, je wewe na mumeo mna umri sawa, mara nyingi mume anakuwa na umri mkubwa kama sikosei, je wewe unamwamkia mume wako Shikamoo? Mara nyingi ukila kama nilivyosema juu tuna tabia ya kukaribisha watu, hata kama unamumunya pipi Je wewe wakati mnangonoka na mumeo akaja mtu nje unaweza kumwambia `karibu', jibu lipo dhahiri. Ni hekima kidoogo tu.
mimi
emu-three
Anonymous said…
jamani neno asante,samahani nakupenda ni muhimu sana katika maisha ya kawaida kabisa,
kwa kweli hata mimi hua naumia kw amtu yeyote yule asiyenambia kua asante.
halafu kingine kuhusu mapenzi bwana wote mnatakiwa mseme asante kama mmeridhishana hata wewe bibie unatakiwa useme asante,mi naona wote mnatakiwa kusema asante
Anonymous said…
Dinah Habari za kazi?

nashukuru mwenzangu katangulia kuliongelea hili. Mimi pia nina tatizo kama la huyu dada lakini mimi huyu ni boifriend wangu, Dinah huyu kaka ninampenda sana tu ninamfulia nguo zake kumpikia na hata usafi wa nyumba yake ni juu yangu lakini mwenzangu hata asante hana, na pia tukimaliza kufika kileleni ni mimi ndie ninaemshukuru kila nikimuuliza mwenzangu labda haujaridhika anasema anafurahia kuwa na mimi lakini neno asante halipo mdomoni kiasi najihisi vibaya kila wakati. nisaidie Dinah
Anonymous said…
We dada acha kuiga mambo yatakushinda.Neno asante lisikufanye ukasirike kiasi hicho.Kuna mambo ya msingi.Kama umeshagundua huo ni udhaifu wake, tatizo ni lipi sasa.Tulia na ndoa, utaenda kwa mwanaume mngine, atataka akule tigo sasa, sijui utasemaje sasa.Mi naona bomba tu kwani udhaifu wake umeshaujua, hivyo sio suala la kukasirika tena.
Anonymous said…
Dadangu kwanza pole sana!
Nimekipata vizuri sana unachosema na kwa kweli ninaki-feel kabisa.
Wapendwa wanablog wenzangu, kwa mtu ambaye hajui maana ya asante hawezi kumwelewa huyu dada kabisa na anaweza kumwona kama mtu ambaye hajapatwa na matatizo makubwa na sasa analalamika kwa vitu vidogo.
Naomba mtambue kwamba katika maisha haya tuna watu wa aina mbalimbali. Na kila mtu ana kitu anachokijali na kukithamini sana na akifanyiwa hicho huona kwamba anapendwa saaaaana!
Nilipoolewa nilikuwa pia sijui maana ya asante lakini mme wangu alikuwa anajali sana na kwa kweli huwa anajisikia vizuri sana ukimshukuru na unaweza kupata hata kilichofichika kwa kumshukuru tu. Sasa kwangu mimi nimejifunza na siku hizi nashukuru sana/nasema asante mara kwa mara, na hata kwa watu wengine pia.
Tatizo lako ni kama langu pia japokuwa mimi nimejifunza kuliacha. MImi napenda na kujali sana kadi (i.e. Greeting, love, birthday cards nk). Na nilikuwa naona kwamba akiniletea kadi amenijali sana. Mme wangu yeye manjonjo hayo hana. Nakumbuka tangu tuoane amewahi kunipa kadi 2 tu na sasa tuna miaka 9 katika ndoa. Hebu fikiria katika hali hiyo.

Ninachotaka kusema ni kwamba dadangu, maisha ni kuchukuliana. Mmeo hajui maana ya asante na hata yeye ukimshukuru ni sawa na nhujashukuru. Hapa simanishi kwamba uache kumshukuru, endelea kumshukuru ila kwako wewe uchukulie kama umepoteza tu. Yaani jiweke sawa na mtu aliyedondosha milioni moja njiani na akaitafuta bila mafanikio. Natambua pia kwamba kadri mnavyoendelea anaweza kujirekebisha kama utakuwa unamwambia kwa lugha na mazingira mazuri kuhusu tatizo lako hili.
Pili, nadhani pia ana mambo mazuri pia. Jaribu kujifunza hayo anayopenda kukufanyia (mazuri) na uyajali na kuyathamini ili yachukue nafasi ya asante unayotaka. Hii itakusaidia kujitibu kisaikolojia ili isikuumize sana.

Mimi binafsi baada ya kuona hakuna kadi, nikaanza kutafakari mambo mengine anayonifanyia mazuri. Niliyatathmini kuanzia kitandani hadi... Nikagundua kuna mengine pia yanayonifariji japo kiu tya kadi huwa naipata wakati mwingine. Hasa nikiona watu wanapeana kadi n.k.
Naona sasa nataka kuandika gazeti. Lakini natumaini haya yatakusaidia.
Ubarikiwe ndugu yangu.
Anonymous said…
wewe dada tulia na mumeo binadam tumetafautiana, kama huyo mtoa maoni wa kwanza alivyokueleza,hilo sio jambo la kuyumbisha ndoa yako kama linakuuma sana kaa kitako na mpenzi wako zungumza nae mueleze tatizo lako au yapuuzie fanya kama huyaoni mradi mnaelewana na mumeo basi,unajua ni tabia ya wanaume sio wote wanaozoea kufanya hivyo unajua kuna wanaume mkikosana hata kama mkosa yeye hawezi kusema sorry na kawaida hata akijiona yeye ni mkosa basi atakutolea ya zamani ilimradi akufanye wewe ndio mkosa mwisho wake atakwambia yamekwisha nyamaza lakni samahani ni mwiko kukwambia,

shosti kaa utulie na mumeo kama usijiudhi bure kwamambo madogomadogo, bora huyo mwenye tabia hiyo kuliko mwenye tabia ya ulevi na kukuletea nyumba ndogo, ukitoka hapo eti ukatafute mwengine kwaanae jua kusema asante utajuta maana utakayokuta huku mungu anajua,

kuhusu kumfulia mume au kumpigia pasi hayo ni mapenzi ya mtu na mumewe kwani hata kazi ndogondogo za ndani ya nyumba ni zenu wote anatakiwa napopata mda nae azifanye lakni sisi wanawake imani zetu na mapenzi yetu kwao mambo yote tumejibebesha ndio utakuta mwanaume tayari ameshajiwekea kwamba haya anatakiwa afanye mwanamke hivo sivyo mapenzi yenu ndani ya nyumba mnavoishi ndio zinawanya mgawane kazi au kusaidiana kwamba nyote niwajiobu wenu kufanya ikiwa ni kupiga pasi hata yeye anapopata mda wa kufua na kupiga pasi anatakiwa akufanyie hivyo au mkae wote pamoja mnafua na kupiga pasi huku maongezi yanaenda mnajikuta mapenzi yanazidi. kazi za ndani ni mapenzi ya mtu sio kwamba ni mwanamke anatakiwa afanye hichi afanye kile, ni mapenzi yako yako na ulivyomzoesha.
Anonymous said…
Mhhh sasa hapo kazi ipo inaonekana katika maelezo yako dada unapenda sana kupewa asante lakini ndio inavyotakiwa...katika upande wa mapenzi sioni kama kuna sababu ya kupeana asante kwa sababu wote mlikuwa mnafurahishana....ila kwenye chakula hata mimi kama nimenunua lazima nimpe asante yule aliyenipikia....Pia kama upo kwenye ndoa ni lazima wewe ufue nguo za mume wako na kumpigia pasi maana yeye anakwenda kutafuta hela ya kula sasa wewe unataka arudi kazi amechoka aje na afue nguo????Nadhani majibu kamili DINAH anakuja nayo!!