Wednesday, 31 December 2008

Nahisi naibiwa-Ushauri.

"Dinah pole na kazi ya kutuelimisha! kwanza nianze na kukushukuru kwa elimu unayotoa pamoja na wadau wengine kwani mengi tumeyajua kupitia blog yako.

Dada Dinah samahani mimi ni mwanaume nina miaka 28, na nakaribia kuoa kama Mungu akipenda mwishoni mwa 2010 au mwanzoni 2011.Tatizo lililo nileta hapa ni kuuliza vitu 61. Kwanini Girlfrend wangu kila akiwa kwenye siku anakuwa mgonjwa kabisa, anatapika haswa, maumivu ya tumbo ndio usiseme huwa anajigaragaza tu chini na dawa ya kutuliza kama diclofenac kameza?

Pia nilimshawishi amuone Doctor kwa hilo anasema ni mara kwa mara kauliza wanasema akizaa mara ya kwanza hilo tatizo linaisha kuna ukweli hapo??


2.Kuna kipindi hakupata siku zake miezi kwa miezi miwili lakini mwezi wa tatu ulipoanza ali-bleed kidogo sana ,mwezi wa nne pia then akaja akaugua vichomi akapelekwa Hospitali yeye anasema Doctor kasema ile damu ya bleed iliganda so akapewa dawa akapona lakini rafiki zake wameni dokeza kuwa katoa mimba nielewe lipi hapa na kama ilikuwa yangu kwanini atoe yaani sielewi kabisa ila yeye akiulizwa anakataa kutoa mimba na anasema hajawahi fanya mapenzi bila kinga. Mimi ni wa kwanza baada ya kupima, yaani sielewi lipi ni lipi!


3. Simu yake mara nyingine hataki niishike, sina kawaida yakuiangalia napenda uhuru ila yangu ruksa sina hiyana. Kuna siku sasa msg iliingia yaani kama machale hivi nikasema huyo lazima atakuwa mwizi wangu ngoja niifungue, kufungua lahaula! ni kama maneno yangu, yaani ni full dear, sijui honey sasa lini tunaonana, nina njaa na vitu kama hivyo.

Siku nyingine msg dear leo nipo Kibaha njoo tulale huku msg hazina majina ni namba tu, nilipo muuliza ni nani akajibu ni jamaa tu anamtongoza ila yeye hamtaki, lakini siku zote nilimwambia nahisi kama naibiwa hivi ila yeye akasema nisiwe na presha wala hana mtu zaidi yangu na kunisifia eti hawezi kumpa penzi mtu mwingine kwani hakuna mwanume kamfikisha kama mimi.


Ila kwa kweli nililazimika kubadili namba yake ya simu aliyokuwa akitumia nikaichukua nikaiweka hewani nilishangaa siku kama 3 simu inaita saa nane au kumi usiku nikipokea anakata nilimpelekea ile namba nikauliza ni ya nani akasema ya baba yake, nilishangaa kwanini baba apige simu muda huo?!


4.Kuna siku alienda kwa shangazi mtu ambako alitakiwa kuangalia watoto wakati shangazi yusafari, aliniambia kuwa uncle mme wa shangazi alimtaka. Mara kuna siku alisahau kufunga mlango wa chumbani uncle kaja na pensi imetuna mboo akimkumbushia kumtaka.


Mimi nikamwambia awe mwangalifu pia amwambie shangazi kuwa kuna hilo limetokea, hakumwambia. Siku nyingine akasema anaumwa akaenda Hospital peke yake uncle akiwa home akatibiwa akarudi.

Si muda mrefu akadai anaumwa tena hiyo siku uncle akampeleka hospital saa 5 asubuhi ,mimi nilipiga simu saa tisa akadai bado wapo hospital?!! saa kumi wapo tangi bovu na huyo huyo uncle wanakula nyama choma yeye akidai mgonjwa!!!?!,vile vile amesema uncle alijituma sana kumletea zawadi hapo home.


Siku nyingine mimi nilikuwa na wasi sana na hilo so nilikuwa napiga simu kila mara. Kuna siku nilipiga simu kuanzia saba usiku mpaka 2 asubuhi hola, haipokelewi, saa nne hivi nakuja kupiga anapokea nikamuuliza hajaona miscalls zangu nyingi nilimpigia akasema hajaona lakini hazikuwa less than 40 na kudai pengine mtoto aliyelala naye kazifuta kwani pengine alishituka usiku na kuchezea simu????!!!!!..


5. Wakati anatoka huko kwa shangazi siku mbili baada ya ile siku nilopiga simu kuanzia saba usiku hadi asubuhi hakupokea, nilimuomba ngono alikubali round ya kwanza tu niliona hahimili kabisa, na mimi nilitaka ku-prove kama niliibiwa au laa na kawaida huwa naunga sometime bao 2 za kwanza kama round moja, siku hiyo ya kwanza ilikuwa kama 7min,nika unga dakika kama ya 10/13 hivi alilalamika anaumia na kuomba apumzike kitu ambacho sijawahi kukiona ni mwaka na miezi kadha sasa tangu tumekuwa pamoja.


Huwa anahimili round zote vizuri 3-6, sasa hapa nina doubt kuibiwa hii kuchoka round ya 2 tena fupi kabisa! aidha kwa mujibu wa marafiki zake huyo uncle alikuwa anamnunulia hadi pad akiwa period sasa hapa jamani ni sahihi kweli hakunakitu kweli hapa? Yeye nikimuuliza anasema hakuna hawezi share na aunt yake!!!?!


6. Na mwisho kabisa dada D ni kuhusu marafiki,anao wengi wakiume, nikimuuliza oooh nilisoma nao, ndugu, sasa hutaki niongee na wanaume!,aaah wivu umekujaa, kwanza watoto wadogo mimi siwataki unanitosha, unanitafutia visa unataka kuniacha lakini kuna wengine mimi nampunguzia credit halafu yeye anawapunguzia ile nilomtumianaomba msaada wa ufafanuzi wa haya mimi naona hapa kama hakuna kitu ingawa yeye anadai kunipenda sana au ni ya kawaida? nitashukuru
by mdau Baraka.M DSM"

Jawabu:Baraka asante kwa kuungana nasi mahali hapa, baadhi ya watu mnapitia mambo mazito kwenye safari hii ya mahusiano ya kimapenzi lakini mnauvumilivu wa ajabu sana au sijui niseme mapenzi ya dhati!

1-Tatizo la kuumwa tumbo wakati wa hedhi kwa baadhi yetu wanawake ni la kawaida, kwa wengine kama ulivyosema hapo hali hiyo huambatana na dalilizote ambazo mwanamke anakuwa nazo anaposhika mimba(sio wanawake wote wakiwa na mimba wanapitia hatu ahii), lakini vilevile wanawake wengine linaweza kuwa sio tatizo la kawaida la hedhi bali tatizo lingine ambalo labda linaweza likahitaji matibabu au hata upasuaji kutokana na ushauri wa Daktari.


2-Mpenzi anapokuwa mchoyo wa simu yake (wengine wanaweka na password kabisa0 au hata neno la siri la barua pepe yake mara zote huwa kuna kitu anaficha na asingependa wewe ujue. Kwa kawaida wapenzi walio kwenye uhusiano "serious" unaoelekea kwenye kufunga ndoa huwa hakuna sababu ya kutokuwa huru mwenzako ashike au kuangalia simu yako. Hata kama huna tabia hiyo bado mpenzi anatakiwa kutohofia kama wewe utaifungua simu yake n.k.


3-Sasa kutokana na tabia ya mpenzio nadhani ulipoteza ile hali ya kumuamini na ukaamua kufanya ulichofanya na kukutana na kile ambacho ulikuwa ukitegemea kukikuta simuni mwake. Kutokana na mapenzi yako ukabadili namba yake ili kuzuia mawasiliano na huyo "mwizi wako" ktk hali halisi angekuwa mwanaume mwingine angemtibua huyo binti kwa ku-cheat!


Kama hiyo haitosho binti huyo alidiliki kuigawa ile namba mpya kwa mpenzi wake wa nje ya uhusiano wenu, wanasema "a cheater will always be a cheater" na hii imethibitishwa na mpenzi wako huyo baada ya kuwa akipigiwa simu na "baba" usiku wa manane.


4-Watoto wa shangazi yake (binamu) wanaishi na baba yako ambae kutokana na maelezo yako nahisi kuwa ndio "baba" na ndio mwizi mkuu wa mpenzi wako. Sababu ya yeye kuwa kule kwa Shangazi kuangalia watoto haimpi ruhusa kulala kuho huko kwani baba yako anakuwepo usiku. Hivyo ktk hali halisi huyu Mpenzi wako alipaswa kutumia akili akisaidiwa na wewe kimawazo kuwa akae na watoto during the day nakurudi kwake/kwenu usiku badala ya kulala huko huko.


Baada ya kuja tuhuma kuwa Mjomba anamtokea, yeye kama binti muaminifu alipaswa kutumia akili na kutokuwepo pale nyumbani usiku (asilale pale), yule ni mjomba ambae hana uhusiano kidamu na mpenzi wako hivyo attraction inaweza kabisa kujitokeza na watu wakapendana......watu wataamua kutoendelea kwa sababu ya kuheshima kuwa ni mume wa shangazi ambae ni dada wa baba......(kwenye jamii nyingine wapwa ni marufuku kuwa karibu na wajomba walio oa dada wa baba yako).


Badala ya kumuambua awe muangalifu ulitakiwa kumshauri asiwe akilala pale kwa mjomba kama nilivyoeleza hapo juu. Nasikitika kusema kuwa kisingizio cha kutokupokea simu na kupokea baadae na kudai kuwa "labda mtoto alichezea" hakina nguvu ya kushawishi ukweli ndani yake.


Kuhusu swala la yeye kuumwa mara kwa mara linatia wasiwasi, hebu mshauri akaangalie afya yake kwa ujumla na zaidi VVU, pia wewe mwenyewe kaangaliwe afya ili ufahamu mapema kama uko huru dhidi ya VVU na kama ni matibabu yaanze haraka na vilevile suala zima la kubadili mtindo wako wa maisha(Lishe, matumizi ya madawa, kuwa muangalifu zaidi kuhusu swala zima la ngono inategemeana na majibu).


5-Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa siku hiyo ya mwisho walikuwa wakifanya "kamuagano" nahuenda alichoka sio kutokana na ngono ya mjomba bali pia hali yake ya kuumwa (natumaini ulitumia kinga siku hiyo).....ila na wewe una moyo wa ajabu!!

Kununuliwa pads sio kitu cha ajabu, hata baba/kaka anaweza kukununulia pads kwani anajua kabisa kuwa unazihitaji kama mwanamke hasa kama huna kipato (hufanyi kazi).


6-Hata kama ingekuwa mimi nisingeweza kuamini rafiki zake wengine wenye jinsia tofauti na yeye. Maelezo yako yameweka wazi tabia halisi ya mpenzi wako kuwa sio muaminifu, sio kwamba unahisi tu bali ushahidi unao kuwa "anachezea hisia zako" kwamba hajatulia hivyo ni ngumu sana kuamini chochote anachosema au kukuambia.


Nini cha kufanya-Nenda kaangalie afya kujua kama una VVU au huna. Majibu utakayoyapata yachukulie kuwa ni ufunguo wa wewe kuanza maisha mapya. Baada ya majibu yako, mshauri na yeye akafanye hivyo (ikiwezekana muende pamoja ili kusiwe na rushwa, mana'ke wengine hulipa ili majibu yabadilishwe).


Ikiwa wote mko safi kiafya au mmeathirika na unahisi kumpenda na unaamini kuwa atabadilika kitabia basi zungumzieni yote na hofu yako juu ya uhusiano wenu, jaribu kuhoji kitu gani anakitaka kutoka kwako ambacho anakwenda kutafuta huko kwa "mjomba". Mawasiliano hayo yatakusaidia wewe kujua mapungufu yako wapi na kuyarekebisha.


Baada ya kukubaliana kuwa mjaribu tena uhusiano wenu basi ni vema kuweka miiko/sheria/rules ndani ua uhusiano wenu na itekelezwe na ninyi wote (mf. kuwa huru kutumia simu zenu, kutokwenda kwa "mjomba" peke yake, kupunguza marafiki wa kiume ambao sio muhimu kwake,n.k.) kisha mpe muda (trial) wa kubadilika bila kuharakisha ndoa.


Vinginevyo (ukihisi hutaki tenakuendelea nae) wewe endelea tu na maisha yako na siku moja utakutana na binti mzuri, mwenye haiba ya kike na mwenye kuthamini penzi.

Heri ya mwaka mpya na kila la kheri!

23 comments:

Anonymous said...

Yaani Kaka, MBONA UNAKUBALI KUFANYWA MJINGA HIVYO. SASA UNATAKA UKWELI AU UHAKIKI WA KIVIPI!!!! YAANI ACHANA NAYE KABISA, KIMBIA, UTAKUJA KUPATA NGOMA UKIANGALIA.

Anonymous said...

NDO TATIZO LA KUPENDA MABINTI NANYI MMEZEEKA. KWA TATIZO LA KWANZA LIPO KWA MABINTI WENGI,LAITWA DYSMINORRHEA,NI KWELI MABINT HUTESEKA SANA WANAPOKUWA KATIKA HEDHI,MAUMIVU MAKALI,SABABU NI AIDHA ZA KIMAUMBILE AU ALISHAWAHI KUTOA MIMBA AU KUUGUA UGONJWA WA ZINAA. DAWA NI MEFTAL P 500, IKISHINDWA AMWONE DR ALIYESOMA ,SIO WA MTAANI.NINGEMTIBU KA ANGETAKA.

PILI,HUYU BWANA ANAMAPUNGUFU, HUYU BINTI NI KWELI NI KICHECHE, ALIKINI SABABU NI WEWE, KWANINI USHIKE SIMU YAKE,UTAFUTE MSG,UPIGE SIMU 40,NA MENGINE, YOTE HAYO UDHAIFU. MWANAMKE MPE SHUGHULI,USIMWONYESHE HOFU,ATAKUTESA.KAZI KWAKO,
MWISHO HUYU DADA MPIGIE KAZI, HUWEZI PIGA CHINI,SIO SAIZI YAKO, KIPESA NA KIMAPENZI. ANATAKA VYOTE NA UMESHINDWA KUMPA.
POLE SANA,MADUME HATUKO HIVYO.

Anonymous said...

kaka mchumba ako sio mwaminifu hiyo ni kwa maelezo yako hapo juu,taadhari usilazimishe penzi na usiogope kuachana kisa utaumia.Please mimi kama mimi sijawahi kuteseka na penzi kwa kiasi hicho unachosema.Cheki out kuna ukimwi na hao wanaume wa watu wasio waaminifu ndio wanaosambaza ukimwi.Chukua taadhari mapema na kama unaweza achana nae na jipe muda utapata mchumba ambaye atakuwa ametulia.Pia inawezekana anakushikilia wewe may be anakutegemea kwa kipato ila kupitia maelezo yako mchumba ako sio mwaminifu hata kidogo.chukua taadhari mapema.

Anonymous said...

baba jibu unalo,kama unayosema ni kweli basi "no doubt" UNAIBIWA,la maana achana naye kwani huyo anayekuibia ni mume wa mtu so hawatadumu,na kama unampenda atarudi tu ila usionyeshe uzaifu wa sana!

Anonymous said...

Sijui kwa mtazamo wako,lakini kwa mtazamo wangu hapo huna mtu,hata kama unampenda vipi atakuja kukuumiza siku moja,kwa maelezo yako huyo dada sio mwaminifu na hayuko muwazi,siku hizi hata wanawake wamekuwa vimeo pia so sishangai kwako,ila kabla hujachukua maoni yetu fanya uchunguzi zaidi ili kupata uhakika ila kufanya mapenzi na mume wa shangazi yako?haiingii akilini lazima atakua amechanganyikiwa au huyo uncle ndo anamfikisha safari yake

Anonymous said...

Wao
thats so bad,pole sana but what i can see mpenzi wako anaonekana sio mkweli ,Lakini ungejaribu kutafuta ukweli zaidi kwa kuchunguza kabla ya ku judge mengine yanaweza kuwa uongo na mengine ni kweli,but mi nacho kushauri ungekaa uchunguze kama hayo unayoyahisi ni kweli ana yafanya au la.
Usije ukamuacha mpenzi wako kisa mjomba au marafiki zake wa kiume ambao may be hana mahusiano nao then ukaja kujuta baadae

Anonymous said...

mmmhh pole sana kaka yangu...
kwa kweli happo wizi mtupu...huyo hakufai unaibiwa kaka yangu
wewe kaa nae chini mweleze how u fill kwamba hupendi kufanyiwa mambo kama hayo.hayo mambo bwana yanaumiza sana tena wewe ni mvumilivu sana.bwana hapo demu wako anagawa lazzzzzzzima

Anonymous said...

pole sana kaka.ki ukweli huyo demu .ni kicheche na huyo uncle anaesema ni mume wa shangazi yake tayari kashatembea nae.na hao wanaompigia sim anadai wanamtongoza wameipataje anmba yake kama sio kawapa.watakuwa walanzia mbali hadi wakapeana namba za simu.na kuhusu hilo tumbo ni kweli linaweza likawa linamsumbua sio wote wanaoumwa sana nqa matumbo siku ya period basi wametoa mimba hapana na hao amrafiki mda mwingine sio wa kuwaamini sana.mi nakushauri muweke chini huyo demu wako na umueleze hali halisi ya maisha ya sasa.anaweza apewe mimba haya si atailea je akipata huo ugonjwa nao ataufanyaje.cha umuhimu we muelekeze ukiona mambo bado hayaeleweki huna budi kuachana nae.kwani utakuja kupata shida hata katiak hiyo ndoa yenu mnayotarajia kufunga.its isha

Anonymous said...

pole sana kwa hilo kaka.Kwanza kabisa nataka nikuambie hivi huyo mpenzi wako sio mwaminifu,anatembea na mjomba wake lazimaa,na hata ukija kumuoa lazima atakuwa anaendelea na auncle wake.Sasa wewe cha kufanya make sure amemwambia shangazi yake kuhusu mume wake,tena mpe muda maalumu asipo mwambia aunt yake basi wewe chukua jukumu la kumweleze aunt wewe binafsi,maana huo ni ufirauni ndio hawa hawa tunawapa sitiri majumbani kwetu wakati wanatafuta maisha ,then wanatembea na waume zetu,mwambie shangazi yake,na ikibidi achana nae,we baba gani atakae kupigia simu saa nane usiku,na kwanini hakupokea basi,kimalaya hicho bado hajajua awe na nani,umewekwa kama spare hivi,atakapo make decision awe na nani kama sio wewe utaumia sana baraka.
Mwisho stop kusex nae kwanza,au uwe unatumia condom wakati huu unapomfanyia uchunguzi,na ukimaliza uchunguzi wako mkapime kwanza ndio muendelee.Nakuambia hivi kwa sababu kuna mwanaume ameambukiza ukimwi mama na watoto wake watatu,(mmoja alitoa nje maana aliona ni kudhalilishwa)yote hayo ni mabinti wametokewa na mpenzi wa mama yao halafu hawakumweleza mama yao,kumbe angemwambia mama yake kuwa huyu mwanaume wako ananitaka huenda mama yake angemwambia an vvu,hivyo angeponea na wenzie pia wangepona,tatizo walifanya siri,kila mtu anaona mapesa yanamwagika anaona loo nakaa kimya mama hatajua,kumbe wanazungukwa wote,Na hivi sasa jamaa amewaacha wote,ye kazi yake ni kutanua tu na watoto wazuri maana anajua ameshachafuka.Yani inauma sana binti anatakwa ma mumeo halafu hasemi,anagawa tu,na wadau jamani hii ni kwa wote,iwe fundisho mambo ya kumkomesha mwanamke mwenzio unatembea na mumewe,mtagawiwa virusi mpaka!!
mdau jgn

Anonymous said...

Baraka..!!!

Kuwa mwerevu kidogo na urudi kwenye dunia ya kawaida utoke kwenye dunia ya kupenda. Hapo unaibiwa na ni wizi mtupu...!!

Kwa maelezo yako huyo Uncle mnashirikiana. Kwa desturi na mila zetu watanzania uncle hawezi kukununulia pads mtoto wa kike sana sana atakupa hela ukanunue mwenyewe.

Na mimi nahisi alitoa mimba komaa na hiyo topic atasema tu.

Hilo la simu pia nalo linantia wasi wasi anaficha nini hapo ???

Muhimu: Mweke chini mueleze unavyo fikiri kuhusu uhusiano wenu kwa kujiamini na mweleze jinsi usivyokuwa na imani naye na umfanye aamue kama ni wewe au kila mtu aendelee na maisha yake. La sivyo atakupeleka peleka hivyo hivyo mpaka utamuoa.

Ni hayo tu

DD

Anonymous said...

pole sana yani we hadi mda huu hujajua tu kwa yote haya mbona ushahidi unao kama wa msg na hizo cm zinazopigwa, umenichekesha eti baba yake anapiga cm sa 8 za usiku na wewe ukaamini mbona we mjinga hivyo na kila kitu kiko wazi? unataka ushahidi wa nini tena? na je aunt yake anajua kuwa huyo uncle ananunulia pads? na kwa nini wewe ukimkataza kitu anakuwa mbishi? navyoona mimi wewe unampenda huyu msichana na hata tukushauri vipi huwezi mwacha ila HIV ndo itakufunza kwanza msichana mwenyewe hajui kuvaa condom kila mwanaume anampa kavu na wee unakubali tu kupita peku peku MAISHA NI YAKO KIJANA usiendekeze ujinga ukafa bila kutimiza ndoto zako, wnawake wapo wengi tulia na kama mungu alikupangia huyo basi atakuwa wako ila huyo ANAKUIBIA tena LIVE.kama kweli anakupenda hiyo sana angeacha upumbavu wake BE LIKE A MAN usipende kijinga jinga ingawa mapenzi yapo na kupenda ni upofu.

Anonymous said...

Baraka naona visa ya bibie ni vingi mno.Na kama una wasiwasi kiasi hicho, sidhani kama unaweza kuja kumwamini hata ukimuoa

Anonymous said...

Baraka nakushauri huyo mrembo hakufai tayari amesha onyesha tabia mbaya hafai ni mama huruma huyo achana nae usije ukapata mardhi bure wanawake wapo wengi hata kama unampenda vp atakusababishia uishi maisha mafupi ni bora ubullshit.
Jito

Anonymous said...

Mkubwa mi nakushauri paki kushoto mshushe na msubiri abiria mwingiune baada ya kupitia SUMATRA ya afya zenu ili uwe na uhakika wa safari yako.Pole sana mkubwa,maisha ni safari

Anonymous said...

Duh unajuwa si vizuri kutenganisha watu ila naamini sababu bado hamjaona mungu apendi mpaka muoane, KWAHIYO KAKA UNA MUDA MZURI WA KUTOMUOWA ATAKUARIBIA HASA MKIJA KUZAA PAMOJA PLZ MUELEZE SHANGAZI, NINI KILICHOKUSIBU NA SABABU ZA KUMUACHA SI KAMA UNAMUHARIBIA SHANGAZI UNAMFUNGULIA NA SHANGAZI UKIMWI MBAYA USIJE KUWAKUTA. Pole Muombe mungu ipo siku utapata wamaana. atakujak ujuta PESA inaonesha pia ndio inamsumbuwa.

Anonymous said...

pole kaka. mie kwa mtazamo wangu ni kwamba unaibiwa mzee. huna haja ya kuteseka na bibi, wako tele ila cha msingi ukitaka mke mtangulize mungu atakuchagulia MKE MWEMA. usiangalie sura mzee, mie ilishanikumba kama yako lkn mungu amenipa mke mzee. siku hz hii kitu ya kawaida mkuu kwa pande zote.

jaba

Anonymous said...

Baraka,
Una wivu mno kakangu. Hapo acha kabisa. Ila ukipata m wingine usiendekeze wivu wa hivyo. Jitahidi kuishi na mtu kwa kumwamini. Kwa mfano umeeleza suala la kuumwa tumbo, siyo umalaya wala nini. Ni matatizo ya kawaida kwa wadada. Nil;ipokuwa sec kuna mtu alikuwa anaumwa hadi tunakusanyika wote. Sasa wewe hata hilo umemtilia shaka.
Mii kwa upande wangui naona hata wivu unao mkubwa sana. Unachunguza sana. Hapo tu bado mchumba, ukimwoa je! Unatakiwa ujirekebishe.
Kuku ukimchunguza sana huwezi kumla. Pili, wewe u-mwaminifu kiasi gani????
Usimsakizie sana dada wa wtu. Ni msichana na bado anachokozwa na wengi. Ukimuoa atajenga heshima na kujitunza tu.
Wengi unaoona wametulia kwenye ndoa walikuwa viruka njia haswa enzi za usichana. Kwa hiyo, suala la kwamba atakutesa mimi siliamini sana. Tena ndio anaweza kuwa mamamzuri.
Ila kwa kuwa una wivu sana na umeshamjengea mashaka, nahisi ukimuoa utamtesa sana na ndoa yenu inaweza isidumu na utakuwa umempotezea muda na maisha yake.
Cheer!

Anonymous said...

1.Nianze kwa kuwashukuru wadau kwa kutoa michanngo yenu mizuri imenifungua,Mungu awabariki.
2.Niseme mapenzi upofu so nilkuwa vitu vingine sioni ama naona kama ni sahihi au sio sahihi.
3.kuna mdau amezungumzia swala la pesa kuwa ni tatizo, nisingependa kuongeza chumvi lkn fedha kwa ke sio tatizo na supply effectively coz nina uwezo mzuri kiuchumi in general.
4.Kuhusu mapenzi namkojoza sana hadi aseme basi, nipo na stamina sana ktk hilo na ufundi wa kutosha yy huwa anasema hajawahi pata man kama mimi ktk sector hiyo.kiufupi kwenye sector hii ya mapenzi gwaride lake huwa ana choka yeye mimi nikiwa bado,naweza kwenda round more than 6, fupi 2 za mwanzo inclusive.
5.kuhusu kumwambia aunt,actually muda mimi nilionana nae ilkuwa siku kama 4 aunt alirudi,hakupewa taarifa japo mimi nilishinikiza sana apewe taarifa lkn pia huyo uncle wake ndo alikuwa wa kwanza kulala mika kwa mkewe kwamba binti alikuwa anavaa nguo zinazo mtega so amuonye yy hiyo tabia hapendi, lkn si mara ya kwanza huyu uncle kumtongoza mara ya kwanza alitongoza aunt aliambiwa , na hata wakati huyu binti naenda mara ya pili alipewa onyo kuwa kwakuwa anajua alishatongozwa na uncle hajatulia anatakiwa kuwa mwangalifu. kwahiyo baada ya kuambiwa hivyo aunt alimfuata binti nakumpa wosia mkali hadi kutaka kupiga na ni no salamu now and then.[sitaingilia mambo ya ndugu]
6.Aliyesema wivu ni kweli nina wivu sana, coz nampenda na pia sina wivu usolazima ingawa napenda uhuru sipendikufichwa kitu ambacho najua kinaweza nidhuru, napenda mwanamke awe huru lkn pia nipo sensitive kujua kama kuna kitu kinaendelea chini ya kapeti,so napenda plain and simple. binafc napenda uhuru lkn na yy awe huru, na hakuna kitu nachukia kama cheating so hapa ningebaini ilikuwa ni no mjadala.
7.Nitayafanyia kazi mawazo yenu ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa haja na kama hamtojali majibu nitayaleta hapa black/white, a-z.ikiwezekana na kutoa full contacts ili ikiwezekana nipate mchumba mpya kupitia hii blog sijui dada D atakubali?! ..nahisi takubali kwani nitanunua kwake pete ya uchumba....hapo je D... coz kwasasa nipo busy sana tena sana na nipo nje ya nchi kwa muda, so nahisi hivi itachukua muda kutulia kuanza kutafuta mtu...hii nahisi itachukua muda mrefu zaidi.
8.Aliyesema nimezeeka ananionea jamani bado nadai,28 tu duh kumbe nioe nitakuwa babu lol sikujua,mimi nilifikiri nitaambiwa muda muafaka,kama ni hivyo shame on me! lkn pia nina sababu za msingi ktk swala zima la elimu, so nilipunguza jukumu la kuwa na mwenza kwanza.

Niwashukuru tena na HAPPY NEW YEAR AND MUCH LOVE TO YOU ALL.

B.M

Anonymous said...

Maisha ya ndoa yanahitaji kuaminiana na kuwa na "peace of mind" baina yenu. Sasa kama umeshaanza kupata "signs" ambazo ni viashiria vizuri kabisa katika kupata wasi wasi ama kutokumuamini mwenzako, nakuhakikishia hata ukimuoa hakuna raha utakayoipata zaidi ya kuwa na wasi wasi muda wote.Na hii inaweza kukupelekea kushindwa hata kufanya mambo yako ya msingi ya kimaendeleo (uta-lose concentration). Unajua kuolewa siku hizi ni deal sasa huyu kwakuwa anajua hawezi kuolewa na huyu mtu anaejificha naye, so ni lazima akunganganie wewe uli uje umtoe kimasomaso naye awe katika kundi la "walioolewa". KAka yangu hapa changanua mwenyewe kutokana na viashiria uvionavyo halafu amua lile litakalokuletea raha kwenye maisha yako. Kumbuka ndoa ni "life commitment baina yenu". Asante na kila la kheri. Heri ya mwaka mpya kwako na wadau wote wa blog bila kumsahau host wetu "dada dinah"

Gumegume said...

Nakushauri uachane na huyo demu. Ila wa hivyo wakati mwingine ndio huwa wanatulia kwenye ndoa. Mimi nimeshawahi kuona watu wameoa viruka njia lakini akiolewa anapata kubano na anatulia.
Angalia ustaarabu.

Ila pia inaonekana mshikaji wangu ni mnoko sana. Kwanza wakati nasoma nilishangaa kuona umeandika unauliza kuhusu vitu 61 kumbe ni sita. Halafu inaonekana wewe ni mgumu kusameme au unasamehe lakini husahau. Umewezaje kutunza hayo yote kifuani muda wote huo!?
Ndo haiko hivyo. Labda umri pia unakusumbua. Ila wivu acha, wewe ni mwanamme.
Gumegume.

Anonymous said...

Uchunguzi zaidi unatakiwa hapa ingawa mtazamo wa haraka haraka kuna tatizo tena kubwa ukizingatia dunia yenyewe yasasa ishaharibika, pamoja na mambo mengine kuna haja ya kucheki afya zenu, kwa maana hiyo from now kama alivyosema mdau mmoja tumia kondom kwanza au siitisha hadi ufumbuz upatikane, lkn pia hili ni swala ambalo kwasasa ni tatizo kwa pande zote mbili uaminifu umepungua kwa kiasi kikubwa.wengine ishakuwa mazoea so hawawezi tulia na mmoja kwa sababu zao mbalimbali kama tamaa ilozidi uwezo,mazoea ya kufanya,limbukeni,kutojiamini na uliyenae, kuendelea kutafuta perfect match,kuimarisha uchumi [hasa mabinti vyuoni, mashuleni-sio wote lkn] na wengine ni starehe tu ya ladha wanazo dhani ni tofauti.
Binafsi nina wivu ila ni muwazi ktk hili na nikiona kuna dalili ya wasiwasi kama ni simu lazima nii cheki tena kwa makini.aidha swala la tumbo kuuma hata wangu analo ni la kawaida na yy kaambiwa akizaa linaweza pungua, so tunasubiri kama kuna ukweli,lkn ngoja ngoja ngoja yaumiza matumbo.... mheshimiwa uliye taja dawa hapo juu kama kweli umesema unaweza tibu basi tuwasiliane maana shida anayo pata huwa naona huruma sana.

Kuhusu marafiki, kuwa makini sana coz inategemea hao rafiki anaishi nao vp so kuna uwezekano wa kumharibia kwako i.e kama anajigamba na wewe ili umuache wakidhani wana mkomoa or wajiweke wao.

mwisho kabisa abiria chunga mzigo wako kuna, kuna wasichana wengine no hawajui isije kuwa mojawapo,chunga ukimwi upo na kimtazamo umedanganywa vya kutosha uamuzi ni wako lkn fanya uchunguzi makini wa kina kubaini ukweli si blah blah, ni hayo tu.

lajk@ymail.com

mimi said...

OMG ...Bee ur 1 in a million man..afu yeye anakuchezea....mi sidhani kuwa umezeeka wanakuonea tu n pia..na pia wivu unahitajika kwani ni moja ya mapenzi..my bf checks ma fon evrytym we meet n i don hv a prob coz i aint cheatin on him(my bf name z Baraka M too..mh)....na mi sijui nikuelezeeje ila du mshua huyo sista ni noma..i understand watcha goin thru...kwani ukipenda n ni vigumu kuamini ukweli hata kama unaujua..maana accroding 2 ur msg ..we ukweli unaujua its jst dat ur heart stil wit her..its kul..ukiumia utapona..ukiwmi hauponi...wanawake wapo kibao...u ll get 1 soon..move on now o u ll neva b able too...trust me i kno wat im tokin abt..n kuhusu period nadhani majibu ya above yanajitosheleza....heri ya mwaka mpya 2 u oll +Dada d
hey Bee folow ur heart bt don ignore ur mind...ur da ril man...a gud man..i wish my man was so tru lik u

Anonymous said...

Duh nimefumaniwa nini? [mimi 5:09:00 PM, try to find me at (barakam@ymail.com)i'm always straight and if you r my lady please learn from the comments given and critique where necessary coz sijaficha na sijaongeza chumvi kwani lengo lilikuwa ni kupata msaada wa mawazo kwa wadau ili kupata ufafanuzi ulio mzuri na kama ulivyoona maoni hapo yaweza kuwa ni changa moto kwako if and only if ur the targeted, if ur not nashukuru kwa majibu au maelezo yako yamenivutia sana, na watu kama nyie huwa hampatikani kirahisi..!'i mean in this one?!!'.
Pia ikibidi nitahitaji watu kama nyinyi kumuelimisha mwenzenu, mimi najua wanawake wapo wengi kazi ni kumpata yule mnae endana nae na zaidi hata kama mimi naachana na mwanamke ni vema akajua kuwa anaachika kwa uzembe wake wa kuto thamini hisia zangu kwake,kupuuza ushauri,kukanusha tu ukweli,kutojali,kucheza na hisia za mwenzio, mimi hii huwa naita kuchezewa akili''with time i'l never tune to the dance i cant even nod''.

Pia nikushukuru Dada Dina kwa maelezo yako mazuri,kuhusu kupima VVU nilishapima mara nyingi na afya ni njema, hata mimi niliwahi fikiri hivo nikapima sana lkn hakuna kilichokutwa.

Asanteni wote kwa maelezo yenu.

B.M