Miaka 5 na mume wa mtu, Hamkunielewa-Ushauri.

"Nashukuru sana da dinah pamoja wachangiaji wote mlioniponda na kunipa ushauri mzuri katika mada yangu Miaka 5 na mume wa mtu!


Kifupi ni kwamba huyu bwana yuko tayari kumpa talaka mkewe ila mimi siko tayari kwahilo. Pili kuhusu kuolewa yuko tayari mda na siku yoyote hata leo ila dini zetu zinaleta pingamizi nami naliona gumu pia kwani siwezi kuwa muislam na yeye alishambadilisha mkewe dini na kumpeleka uislam hivo hawezi kuja ukristo amwache mkewe huko.


Naombeni tena mnisaidie nitumie mbinu gani nitumie katika kuachana na huyu bwana na ni mda gani muafaka wa kutumia katika kulizungumzia hili kwani kila nikijaribu kumtajia hilo tu ni ugomvi na inakuwa kama ndo nimemwambia ahamie kwangu kwani atalala kwangu mwezi mzima bila kwenda kwake.


Kunitambulisha ameshanitambulisha kwao ndugu,wazazi, mkewe, watoto wote wananijua na wamenikubali ila kwangu naona sio kitu hilo kwani siko kwenye nafsi zao hivo uenda ni unafiki au ni ukweli.


Nashukuru sana kwa watakaonisaidia kutatua hili na sio kuniponda.

Kazi na siku njema wote Asanteni. "


Jawabu: Pole kwa kukwazika. Wasomaji wangu ni wazi walipatwa na hasira kwa sababu wasingependa kitu kama hicho kiwatokee wao au hata wanawake wenzao kwa imani kuwa wanawake tunapaswa kushirikiana na sio kuharibiana ndoa.


Mume/mke wa mtu akikutokea mkatae akizidi kukufuata fuata basi nenda kamwambie mkewe hali itakayofanya mke huyo kuwa awear na tabia chafu ya mume/mke wake....hapo utakuwa umesaidia kuokoa ndoa yao, maisha ya watoto wao (ni vema watoto kukua ndani ya ndoa wakiw ana wazazi wote 2) na kuongeza amani kwenye nyumba yao.




Majibu ya wengi yaliegemea kutokana na maelezo yako ambayo sasa umegundua kuwa hayakuwa yamejitosheleza au hayakuwa wazi kwenye points muhimu ambazo ni hizi:-


1-Kumbe jamaa ni Muislamu hivyo anahaki kabisa ya kuoa mke wa pili kwa mujibu wa Imani yake as long as anauwezo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.



2-Wewe hauko na haukuwa tayari kufunga nae ndoa ya kiislamu(hutaki kubadili Dini), which tells me kuwa wazazi wako hawamkubali jamaa kwa vile Dini yake ni tofauti na sio kwa vile ni mume wa mtu.


3-Mkewe, watoto, ndugu na jamaa zake wamekukubali kama mke wa pili lakini wewe ndio unasita kutokana na Imani zenu za Dini kuwa tofauti.


Ungeweka wazi yote haya ingesaidia wasomaji wangu kukupa ushauri tofauti na walivyokushauri mwanzo.*********************************************

Nimefurahishwa na nia yako ya kutaka kutoka kwenye uhusiano huo kama ambavyo wengi walikushauri, kwani ukikubali kuolewa ni wazi kuwa utakuwa umechangia kwa kiasi fulani kuharibu maisha ya watoto ambao tayari wamezaliwa kama matunda ya ndoa hiyo(haijalishi kama dini inaruhusu au la) suala muhimu ni kutokuwa wabinafsi na kuwafikiria watoto hao na maisha yao ya baadae.

Nasema hivyo kwa vile, watoto hao siku zote watakuwa wakichukulia au kuamini kuwa wewe umechukua nafasi ya mama yao na maisha hayatakuwa the same kwao kitu ambacho wengi huwa tunajaribu kukiepuka.

Watoto hao watalazimika kukupa heshima ya uoga (kwa vile baba anataka iwe hivyo), lakini mioyoni mwao hautokuwepo kabisa (jaribu kujiweka wewe kwenye their shoes.....ungejisikiaje?).

Hawatokupa upendo sawa na ule walionao kwa mama yao mzazi, hawatokuthamini kama vile wanavyofanya kwa mama yao mzazi hali itakayokufanya utamani kuzaa watoto wako mwenywe kitu ambacho kitaongeza idadi ya watoto na hivyo maisha yanaweza kubadilika kwani huwezi kujua nini kitatokea in 10yrs time.


Kama hao watoto hawatopata matunzo muhimu labda baada ya mama yako kuachika na wakaamua kwenda kuishi na mama (watoto wengi huenda na mama, mama are the best, we have strong bonds na we love mamas) au kushindwa kuendelea na masomo baada ya baba yao (mungu apishe mbali) kuodoka Duniani lawama zote zitakuangukia wewe, labda usingeolewa na baba yao na kuongeza Idadi ya watoto maisha yangekuwa tofauti hata kama Mzee hayupo.....si unajua mambo ya urithi!


Kujitoa kwako kwenye uhusiano na mume wa mtu kutakuwa kumeokoa ndoa ya mwanamke mwenzio, kuokoa maisha ya baadae ya watoto waliozaliwa kwenye ndoa hiyo na pengine litakuwa fundisho kwa mwanaume huyo na hivyo itakuwa mwisho wa kuwa na kimada.


Kuna mchangiaji mmoja kagusia kuhama mji, hiyo ndio njia nzuri na ya pekee ambayo inaweza kuua uhusiano haraka na kukusaidia kuanza maisha upya mkoa/kijiji/kitongoji/mji mwingine. Wakati unaendelea na mipango yako ya kuhama "nchi" humuambii mtu, ukikamilisha wewe unatoweka tu lakini julisha ndungu zako na hakikisha hawamuambii jamaa uko wapi.



Ili basi kumsaidia huyo jamaa, muandikie walaka wa kwanini umeamua kuua uhusiano wenu (usiseme unahamia wapi) na weka points muhimu wazi, Points muhimu ni kuhusu ndoa yake(onyesha kuwa hauko tayari kuharibu ndoa ya mwanamke mwenzio, usigusie suala la utofauti wa dini zenu), watoto na maisha yao ya baade(onyesha unajali maisha ya watoto hao kama vile ambavyo ungejali maisha yako wewe ulipokuwa mtoto).


Mungu atakubariki kwa kuokoa ndoa ya mwenzio na vilevile atakujaalia na utakutana na kijana kama wewe, mwenye nia moja kuwa na wewe kama mke wake.

Sio mwisho wa maisha kum-buti mpenzi, bali ni mwanzo wa maisha yako mapya.

Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
hama mji bila yeye kujua
Anonymous said…
Simple idea dada, kuna muda mwingine inabidi unywe dawa chungu ili upone. hivyo basi nakupa dawa chungu and make unakunywa kama unataka kupona.

Kwanza kabisa chukua muda, kaa chini na jiulize maswali machache. Swali la kwanza jee nipo tayari kuwa mke mwenza? au Jee nikibadilisha dini wangapi wanata support na wangapi watapinga, na jee hao watu wana influance gani kwenye maisha yako? Jee penzi lako kwa huyu bwana litakuwa na kasi na nguvu mmoja mpaka mwisho?

Kama una wasi wasi na jambo lolote kati ya haya, ushauri wangu ni mmoja tuu. MOVE ON. Mwanzoni atasema oooohh ukiniacha nitakuwa chizi, blah blah, lakini that is lies kama kawaida yetu wanaume.

Just quit, and things will work out.
Anonymous said…
Wanaume wakitaka kuwaacha wake zao, huwa wanawafanyia visa. Na wewe unaweza kuanza kumfanyia visa, unamwogopa nini? Unajifanya mstaarabu. Unadhani siku akikuchoka atakuacha kistaarabu? atakuacha unalia. Sasa na wewe anzisha tabia za ajabu ajabu, mwenyewe akiona umebadilika ataghairi hata kukuoa, na utakuwa huru. Ahsante
Anonymous said…
Dada,
Pole kwa kuwa njia panda na kwa kutokueleweka vizuri na wachangiaji,ambao wengi wao mbali ya kutokukuelewa walikushambulia ikiwa ni ishara nzuri kuwa sasa jamii imeanza kubadilika na kuona kuwa mtu anayechukua mume/mke wa mtu anafanya kitendo kibaya na hivyo basi anapaswa akemewe.
Hii ni ishara njema na nafikiri tuko katika muelekeo sahihi,baada ya muda fulani huko mbele,watu watakuwa wanaishi na wake/waume zao bila ya kutoka nje ya ndoa zao.
Mimi ninakushauri uandae mazingira mazuri ya kufanya kikao na watu wa karibu,wenye hekima na busara.Huyu jamaa kwanza usimfahamishe,yeye aje kufahamishwa na wazee.
Waalike kiongozi wa dini yake,na kiongozi wa dini yako,upande wa familia yako mualike kiongozi wa familia,na kutoka familia yao mualike kiongozi,pia kama kuna rafiki yake wa karibu basi mualike.Watu hawa wote wawe ni wale wenye msimamo wa kuunga mkono mahusiano ya dani ya ndoa,wawe wenye hekima na busara.
Pia wawe wenye kutunza siri. Kama kutakuwa na mtu huru,yaani hana uhusiano na pande yoyote kati yenu lakini anamjua mmoja wenu na unahisi anaweza kuwa na mchango ambao utasaidia katika kikao hicho,basi mualike ilimradi ana sifa nilizozungumzia hapo juu.
Nataka kutoa angalizo kuwa si viongozi wote wa dini wana busara na hekima na si viongozi wote wa familia wana busara na hekima,hivyo basi kuwa makini sana na aina ya watu utakaowaalika. Waeleze dhumuni lako na mipango yako, na kikao kilenge zaidi kwenye kutafuta suluisho na si kutafuta chanzo cha tatizo(witch hunting)na sio kutoa lawama.
Kiongozi wa dini wa upande wake ndio umpe jukumu la kwenda kumpa taarifa ya kikao hicho,na kumualika katika kikao.
Pia muombe MUNGU sana na kwa kuwa yeye ni muaminifu na haruhusu/hakubaliani na kuchukua wake/mume za watu basi ATAKUSAIDIA.
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com
Anonymous said…
Habari Da Dinah,
Nashukuru sana kwa mchango wako pamoja na wachangiaj wote kwa kuchangia mada yangu miaka 5 na mume wa mtu.

Ushauri wenu nitaufanyia kazi sana kama ambavyo mmenishauri na pia namuomba Mungu mpaka ifikapo 15/01/09 niwe nimeshaachana na huyu jamaa.

Swala la kuhama mji litakuwa gumu kidogo coz ajira siku hizi zinasumbua na hapa nilipo sina hata miaka 2 kwenye hii ofisi sasa nikihama mji itakuwa vigumu kutafuta tena kazi kama mnavojua kwa sasa ni vigumu sana kupata kazi ila nitakachojitahid ni kuhama ninapoishi sasa na kuhamia mtaa mwingine nikifanikiwa kupata chumba pia.

Pili kuwaita viongoz wa dini kabila pia naliona gumu coz weng wao hawajui uhusiano wetu nitakachofanya mimi nikuwaeleza ndugu zake wote na marafiki zake kuwa kwa sasa siko na jamaa tena na nitamweleza akamweleze mkewe akigoma nitamueleza pia ili hata likija kutokea la kutokea nisiwe lawaman kweli jambo hili limeniumiza kichwa kwa mda mrefu sana ila nashukuru sana Da Dinah kuweka blog hii ya jamii kwan imenisaidia kutatua jambo langu japo sijalitatua bado ila ushauri wenu ni msaada tosha.

Asanten sana kwa ushauri wenu Mungu Awabariki na Kazi njema nyote