Wednesday, 10 December 2008

Nilihisi, nikahakiki, akabisha sasa nimepoteza mapenzi?-Ushauri

"Hi dada Dinah,
Mimi ni msichana wa miaka 28 nimeolewa na nina watoto waili. Tatizo langu ni kwamba nilihisi mume wangu anatoka nje ya ndoa wakati nikiwa mjamzito wa mtoto wa pili, baada ya kuona anapokea simu za ajabu ajabu na kutwa simu zake alikuwa anaziweka silent au simu zinakaa kwenye suruali tu au kwenye gari.


Siku moja usiku kama saa 4 hivi ilipigwa simu alikua anaoga cha ajabu simu ilikuwa inawaka taa tuu kwa namba hiyo ila kwa namba zingine zinaita kwa sauti ila kwa namba hiyo ndio inawaka taa tu tena bila hata vibration, mi kuona hivyo nikapokea hiyo simu na kukutana na mwanadada bila hata kujua ni mie nikasikia mambo darling, nikamwambia Darling wako anaoga una ujumbe akija nimpe?


Akakata simu mie nikachukua ile namba nikasave kwenye simu yangu na darling wake alipotoka siku mwambia kama alipigiwa simu. Mara tukiwa mezani na watoto tunakula ikapigwa simu ileile akapokea akaanza kubabaika, kidogo kaacha chakula kasema kaitwa na ndugu yake ana matatizo na mie nikamwambia ni bora twende wote maana kama ndugu yake na mie ni wangu pia akakataa na mie nikamwambia hutoki nje ya nyumba hii usiku huu bila mie nikachukua funguo zote za gari nikakaa nazo na nikamwambia ukitoa mguu hapa utajuta.


Basi akaenda chumbani kupiga simu na mie nilijua tuu nikaenda mlangoni nikawa namsikiliza eti anasema naweza kuja ila sina uhakika ila usitegemee sana. Sasa mie kwa hasira Asubuhi nikampigia huyo dem wake kwa private akapokea nilivyokuwa naongea nae akanishtukia akampa mwanaume aongee.


Jioni nikauliza hii namba ni ya nani akaniambia ni ya rafiki yake nikamuuliza mbona sijawahi kusikia kama una rafiki kama huyo nikamwambia mbona ni mwanamke akaniambia kuwa huwa wanashare na mumewe simu nikajua lazima atakuwa kamwambia kuwa nimepiga simu leo.


Nikamwambia huo ni uongo, Basi baada ya hapo nikawa na stress za ajabu mpaka nikapata na matatizo sana mpaka nikaandikiwa Bedrest na ninashukuru Mungu kanijaalia nikazaa salama salmini.


Baada ya kuona nina matatizo akaniambia kuwa huyo dem ni mke wa rafiki yake na anamtaka yeye hana mpango nae na hana tena mawasiliano nao kabisa na sitakaa nisikie simu wala nione sms toka namba hiyo.


Mara akaumbuka ilipoingia sms inamuuliza Vipi leo utakuja??? Mi nikaijibu nikasema siji then nikamwambia kuna msg yako hapa imekuja na nishakujibia, Nikamwambia kama kweli huna mpango nae mpigie simu umwambie amkomeshe na mie nikisikia kama kweli akasema ooh haina haja sijui nini akajitetea na kusema kwakua ndio nilikuwa nimetokakujifungua hata mwezi haujaisha.


Nikaachachana nae nikalala nikaogopa kujipa stress nikakosa Maziwa ya mtoto bure, Asubuhi nikapiga simu ili niongee na yule dada kwa amani yule dada lipogundua ni mimi aliniporomoshea mitusi hata kabla sijaongea nilichotaka kuongea.


Jioni nikamwambia bwana'ake(mume wangu) nikajibiwa sasa na wewe unapigiapigia simu tu watu usiowajua unategemea nini? Sikuamini kama nimejibiwa hivyo nikasema poa nimekoma. Na toka siku izo nikawa sina mapenzi na yeye nikawa namwangalia tuu, niko na watoto wangu tu ila yeye sina stori nae zaidi ya salamu na siku nyingine hata simsalimii ila naumia sana.


Nikakaa kimya nikawa sina mpango nae tuko tuu kama kaka na dada nikiongea nae sawa nisipoongea nae poa, Siku moja nikaamua kumtisha nikamwambia sasa nishamaliza meternity leave namaanisha kuwa mtoto ni mkubwa vya kutosha na sasa na mie naweza kutafuta mtu wa kunipooza moyo niondokane na mawazo nikae na mie na amani moyoni tuwe Ngoma droo.


Maana kama yeye kaoa na anatongoza basi na mie nimeolewa na nitatongozwa na akijaribu tu namkubali hata kama sijampenda ilimradi na mie nipoze moyo .Kumbe ilimuiingia na akajua naweza kufanya kweli akaanza kujidai anarudisha mapenzi kwa kasi kubwa mara ananiongelesha hata kama sitaki kuongeleshwa mara hivi mara vile.


Ila mie nikawa tu kama jiwe sijali ndo kwanza najidai simwoni niko Busy na simu kutwa nachat na rafiki zangu nacheka yani hata nikiwa na rafiki zake au ndugu zake mie busy na simu yangu tuu wala siwaoni.


Siku moja nilikuwa nimelala akaniamsha eti naomba kuongea na wewe nikamsikiliza akaniambia eti kuwa vile nilivyokuwa navihisi ni kweli alikuwa na mahusiano na huyo dem ila ni mahusiano tu kama rafiki yake tu wa kuongea nae tuu na kunywa tuu lakini hajawahi kufanya nae chochote hata kiss hajawahi miezi yote zaidi ya 7.


So mie nikitaka kufanya nitalipiza itakuwa ni kuwaumiza watoto tu cha kufanya tuelewane na tupendane kama zamani maana yeye hajafanya chochote cha ajabu ni kukaa tu na kuongea na huyo dada.


Nikamuuliza kama kweli kwanini ulishindwa hata kuniambia kama una rafiki wa design hiyo? Na kwanini siku aliyonitukana kama ni rafiki wa kawaida kwanini asimchukulie hatua yeyote au kwanini huyo dada anitukane kama hatembei na mume wangu??


Mi nikamsikiliza alivyomaliza nikamwambia haya nimekusikia nikaendelea kulala maana nilijionea ananizingua tuu mie nausingizi na nasubiri niamke kumnyonyesha mtoto ye ananiletea habari zake za kijinga ambazo mie zimegoma kaminika na kichwa changu.


Sasa naomba mniambie kwa story hiyo ni kweli kua hajawahi kufanya chochote au kaamua tu kuniambia hivyo kwakuwa nimemtishia na mie kutoka nje ya ndoa au kurudisha amani ndani?


Mie bado nipo vilevile kama jiwe vile simjali kwa chochote najijua mie na wanangu tuu yeye namwona kama picha ya ukutani tuu."

Jawabu: Asante sana kwa ku-share tatizo lako mahali hapa, nakupa pole kwa yote unayokabiliana nayo lakini wakati huohuo nakupa hongera kwa kusimama Imara dhidi ya emotional "abuse" kutoka kwa mumeo.

Hili ni tatizo sugu kwa wanaume wengi wa Kiafrika, mwanamke anapokuwa mjamzito au kujifungua wanadhani wamepatiwa nafasi ya kwenda kutembeza "viungo" vyao nje ya ndoa zao. Kutokana na maelezo haya ni wazi kuwa mumeo hakuwa akikuthamnini na wala hana haeshimu ndoa yake.

Hawajui kuwa Mwanamke anahitaji ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa mume mara baada ya kujifungua, sio kuanza kusumbuliwa kiakili na kihisia.


Mumeo ameongopa ili wewe usiende kufanya kama alivyofanya yeye(Mkuki kwa Nguruwe) lakini ukweli (kutokana na maelezo yako) amefanya mambo ya kimapenzi mengi tu na huyo "rafiki yake".


Kinachoshangaza nikuwa, pamoja na kukubali urafiki ulikuwepo bado hajaonyesha kuwa anajutia makosa yake kwani hajakuomba msamaha, kitu kinachonifanya mimi (Dinah) nihisi kuwa mumeo huyu anakiburi, anajivunia alichokifanya na hana mpango wa kubadili hiyo tabia yake chafu.


Naelewa kabisa uamuzi wako wa kumtenga mumeo na itachukua muda mrefu sana mpaka utakapomuamini tena, kumtamani tena, kumtaka tena na kujisikia kutaka kufanya nae mapenzi.


Inawezekana kila ukiwa nae karibu au anapokufanyia jambo/mambo fulani picha ya yeye kumfanyia yule mwanamke mwingine inaweza kukujia na kuua "mood", yaani hata kama ulikuwa na hamu inakuishia ghafla.


Nini cha kufanya-Kama tangu umejifungua hujafanya mapenzi na mumeo itakuwa vema akienda kuangaliwa kama yuko salama kutoka VVU, lakini kama ulikuwa ukifanya mapenzi wakati unahisi kuwa "anatereza" nje basi ni vema kama wewe, yeye na mtoto mkaenda kuangaliwa damu ili mjue kama mko salama kutoka VVU.


Pamoja na kuwa mumeo anaonyesha mapenzi kuliko mlivyokutana hapo mwanzo, hakikisha hu-give in mpaka aombe msamaha na kuahidi kutorudia tena kosa alilolifanya (msamaha maana yake ni mabadiliko kwa vitendo), hivyo hiyo itakuwa nafasi yake pekee ya kubadilika.


Kamwe usimwambie ukweli kuwa ulikuwa unamtishia kuwa utaenda kulalwa nje ya ndoa yako, iache kama ilivyo.......najua siku moja atataka umhakikishie kama kweli ulikuwa na mpango huo au hata kama tayari umelala na mwanaume mwingine (hapo alipo linamuuma kweli kweli sema hana jinsi ya kuliweka wazi......hakuna mwanaume anapenda kutombewa mwanamke wake, hasa yule mwenye tabia hiyo.


Akitaka kujua muambie ukweli kuwa hukufanya lakini ulikuwa ukisukumwa kufanya hivyo kutokana na tabia yake ya kwenda nje ya ndoa yenu...kwa maana nyingine ni kuwa, huwezi ku-cheat ikiwa yeye hato-cheat, aki-cheat anakuhamasiha na wewe kufanya hivyo. Hii itakuwa adhabu tosha kwake japokuwa wewe unajua moyoni huwezi ukafanya hivyo bali ulikuwa ukimtishia tu.

Kitu kingingine ambacho ni muhimu sana ni kuwekeana Sheria, ni mume wako, mnapokuwa pamoja inamaana mnaunda ushirika fulani ambao unapaswa kufuata Sheria fulani na ni mwiko kabisa kuzivunja.

Kwa Mf-Simu yake ni yako, rafiki zako awafahamu na wewe uwafahamu wake, Namba zote ziwe-saved kwa majina unayoyajua kutokana na ulivyotambulishwa, kama kuna shughuli za kifamilia wote 2 mnashiriki, hakuna safari za usiku unless mnatoka wote, kuambizana kwa uwazi kama kuna kitu kimepungua kwenye uhusiano wenu na kupeana mikakati ya kukirudisha, kuwa na muda wenu kama wapenzi na sio kama baba na mama, kutumia kinga dhidi ya VVU mpaka utakapo hisi kumuamini tena (kama utaamua kufanya mapenzi na mumeo).


Kumbuka kwenye ndoa yenu kuna watu wadogo wawili hivyo ni muhimu kuwafikiria watoto wenu zaidi na maisha yao ya baadae kuliko kujifikiria ninyi zaidi. Hawa watoto wanahitaji mapenzi yenu nyote wawili, baba na mama mliopendana hapo mwanzo na kufunga ndoa.....hivyo ni vema kuonyesha mapenzi mbele ya watoto wenu na tofauti zenu kuziweka pembeni machoni mwao.


Ukiona unashindwa ku-recover kutokana na "Emotional abuse" basi unaweza kwenda kupata msaada kwa wataalamu, kama nilivyosema itakuchukua muda mrefu lakini kutokana na ushirikiano wa mumeo (kubadili tabia) utakuwa sawa na kufurahia ndoa yako.

Wewe ni mwanamke tofauti kabisa na wale tuliowazoea hapa Bongo akina "ndio bwana", ni mfano wa kuingwa na wanawake wengine, kisa chako kinaonyesha kuwa huitaji mwanume bali unamtaka mwanaume.........Safi sana.

Mimi na wachangiaji wengine tunakutakia kila la kheri.

21 comments:

Anonymous said...

hahahaaaaaaaaaaa,ww kiboko.nimependa staili yako.ok hapa cha kufanya huyo ni mumeo kaachini zungumza naye mwambie nataka uniambie ukweli wa moyo wako,kama umelala na huyu mwanamke,pili nendakapime tena ngoma asije kulata balaa mkaacha watoto yatima,tatu akikataa kusema kalala na hilo jinamke lake mwambie poa msamehe ila kuanzia sasa simu yake na yako zote ziwe zenu hakuna siri.
da siti

Anonymous said...

pole sana dada we jasiri kweli mashalaaaa!kaza moyo mama usivunje ndoa ajili ya hayo tuu,mkapime vvu,msamehe,jengeni uaminifu tena.ila mwambie mshenzi sana mtakufa muache watoto kwa ajili ya upuuzi wake na tamaa zake bila kufikiri.

Anonymous said...

pole dada yangu kwa hayo yote, hapo ni kwamba huyo mke mwenzio sio demu sijui nani ni mke mwenzio, coz haiji akilini rafiki akutukane, and possibly ni mtu anayekufahamu na anaweza kuwa rafiki yako, jaribu kumueleza muelewane kufanya kosa sio kosa kurudia kosa ndio kosa, mkinuniana hapo utampa muda huyo mke mwenzio kutanua na mme wako, mida kama hii kwa mumeo ni mkuafaka coz umesema watoto wakubwa, so it is obvious ana miss utamu wako wewe unafikiri kwanini alikuoa wewe, utamu huo dadaa hahhaha.ok kuwa siriaz uko kwenye ndoa bila shaka ushakuwa mama wa watoto lazima uwe siriaz ktk hili kwani linaweza kuwa htari ktk maisha yako ya watoto, na huyo mmeo, so pigania it doesn't make sense urafiki wa karibu mwanaume na mwanamke kulingana na maelezo yako, huyo dada mwingine anakusaidia kuimeza hiyo mboo ya mmeo'' wanasema ile kitu inamesa mwenzie, so anamesa hiyo ya mr wako''=maasai version....ila umfanye ajue kwamba wewe umemind hadi mwisho, ila kununiana sio suluhu, by the way anachotaka kwako nimeshakwambia na ame miss,wanaume wengi siku hizi ni ovyo lkn hii hutegemea zaidi back ground, pia kipindi kama hiko wewe hukuweza kata kumpa mkono mzee unategemea nini wakati unajua hana pakuachia nguvu zake? kuwa mbunifu mama, usiache kamwe mboo ya mumeo ikizagaa ovyo itumie ni haki yako, unakaa nayo ndani how mtu mwingine aitumie? ndo kusema wewe unashindwa kuifanya isisimame akiwa nje ya hapo home?. ok Dina will conclude this. pole sana maana inauma sana, mimi huwa nafikiri nikija kujua kama kuna man ananitombea my lovely yf, nisijue mpaka nife maana natamani huyo jamaa abaki bila mboo maana ndo inayo mpa kiburi kuiba wanaweke wawenzie,yf wangu anajua ndio maana huwa hapendi kutoa background anajua nilivyo na wivu na hiyo tamu yake! so na wewe pigania mboo yako hata kama unaumia, ila kununa sio suluhu.
by lajk@ymail.com

Anonymous said...

Mmmmmmmmmmmmmm huu!!! Pole dada.Maisha ya unyumba ni safari ndefu sana, inatufunza mengi.

Kwanza kabisa nakupongeza kwa ujasiri wako ambao ulimuonyesha mumeo katika hilo,hasa kule kujitunza mwenyewe wakati wa uja uzito maana ungeharibu mengi.

Pamoja na hayo pia umeendelea kukaa naye na kujaribu kucheua lipi liwe jambo lenye kuleta maana katika mahusiano yenu ya ndoa.Nafurahi kwamba hujachukua uamuzi mzito wowote zaidi ya kujaribu kuweka mambo kwenye mizani.

Wangu ushauri dada ni kwamba, mpaka hatua hiyo uliofikia, tayari umeishamwonyesha na kumthitishia mumeo kuwa umeyajua yote yaliokuwa yanatendeka, na hivyo hata yeye anajua hilo,japo anajibaraguza tu.

Jambo moja ambalo wanaume daima wanalo(hata mimi ni mwanaume)ni kujifanya hawawezi kusema NIMEKOSA. Tunatumia njia nyingine ambazo hazileti muafaka haraka.Anaposema kwamba hakufanya mapenzi naye, ni mwongo,ila tu dada uelewe kwamba alifanya na amekirijapo hilo la kusema nimekosa unisamehe linakuwa gumu au linakuwa na kigugumizi.

Nakuomba dada jaribu kupiga picha nyuma tangu mumeanza uhusiano hadi kuoana kama amewahi kusema dhahiri mbele yako kukiri kosa(naam ninaamini amewahi kukosa).Hapo unaweza kuwa na hakika kuwa neno hilo halitutokei vinywani mwetu.Kwa sasa rudisha tu ule moyo wako wa upendo wewe msamehe na mwambie nimekusamehe licha ya kuwa huraki kusema nisamehe.

Usijaribu kurefusha/kudumisha hali hiyo iliyopo sasa ya mahusiano yenu kwani italeta madhara mengine.Tafadhali ushinde ubaya kwa kutenda wema.Kosa lilitokea na sasa huna haja ya kuliwekea shari.Yaliyopita sindwele na tugange yaliyopo na yajayo.

Naelewa ni ngumu kuachia haraka,lakini umeishafanya sehemu kubwa zaidi ya kilichobaki, hivyo MSAMEHE ili muendelee kupanga mipango mingine ya kuijenga familia yenu.Ukiliendeleza hilo litaleta gharama kubwa na ufa mkubwa zaidi.Hivyo ziba ufa usije ukajenga ukuta. Kukosa si kosa bali kurudia kosa.

Nakuatakia kila lililo jema ili muafikiane na mrudie hali yenu ya mahusiano.Japokuwa umemjaribu kumwambia sasa unatafuta na wewe wako pembeni, wakati mwingine unaweza kuona hilo linajenga moyo kabisa.Basi Limalize dada ili uanze nawe kupata haki yako kutoka kwa mumewe.

Anonymous said...

Nimesoma hii habari huku nikishusha punzi taratibu kabisa. Nikiwa kama mwanaume naona ni jinsi gani wanaume wa Tanzania wanavyo wachezea faulo kina dada. Kwanza Dada yangu pole sana, pili nadhani niende kwenye red meat moja kwa moja. Nadhani uhusiano wenu upo mikononi mwako, wewe ndio wa kuokoa ndoa au kuitia motoni.

Wanaume wengi wasio na msimamo hujikuta wakishawishika kutembea nje pindi wake zao wanapokuwa wajawazito. Nadhani hili limemkumba mzazi mwenzio, na kama amesha acknowledge kwamba alikosea basi hiyo ni one step ahead.

Nadhani kutokana na ufupi wa maelezo yako, inaonyesha nyote wawili mlikuwa na health relationship mpaka ulipokuwa mjamzito, na kwa sasa hali ni tete. Hivyo ni jukumu lako kuamua kama unataka ndoa iendelee au ife. Kama unataka pendo liendelee basi nadhani ni muda muafaka wa wewe kuchukua action mara moja. Mapendekezo

1. Muombe mumeo date ya maongozi, make sure watoto wasiwepo, na kama hauko comfortable kuyaongelea nyumbani kwako then tafuta somewhere else.

2. Akikubali, then weka argument yako bayana kwamba unaamini alichofanya ni makosa na upo willing kumsamehe kama atakubali makosa na ata change direction. Lakini weka bayana kwamba hili liwe la mwanzo na la mwisho, na ikitokea tena, divorce won't be the option it will be the choice. Hii itamuweka wazi kujua kwamba this time anajua kitakacho mkumba akirudia makosa.

3. Impose new policy, ambayo inabidi aikubali nayo ni zero tolerance kuhusu kupokeleana simu. Mwambie kwamba yeye ana haki ya kupokea simu yako, na wewe una haki ya kupokea simu yake. Wewe una haki ya kumwambia nani alipiga likewise yeye.

4. Wewe kukubali kusahau yaliyo tokea na kuhaidi hauta kuja kumuhold accountable sababu ya hiyo issue. You will never mention huyo mwanamke no matter how worse the situation happen kati yenu.

Nadhani hizi ni good step za kurudisha uhusiano mahara muafaka. Kumbuka kusema ukasake na wewe sidekick sio solution, bali unaongeza mafuta ya taa kwenye moto. Kuamua kwamba unamyima unyumba sio solution kwani nae itafika muda ataamua vingenevyo.

Dawa ni kutafuta muafaka, kama wote wawili mnapendana then bora mtatue, na kama mmoja wenu hayupo willing kuresolve hili tatizo, then i think hakuna litakalowezekana.

Mdau namba 1

Anonymous said...

Yaani hii story imenigusa!!strength of woman!!nimekupenda mpenzi..natamani wanawake wote tungekuwa ivi!You know what mamii you know your value. Sasa ni ivi huyo mwanamme ni mwongo,sema tu anajaribu kujitetea ili urudi chakufanya ni ivi mpenzi kaa nae muongee mambo yenu aweke wazi mean awe mkweli kwake coz wewe ni mkewe,then jaribu kumsamehe mpenzi na usali na kurudisha feelings zako kwake hayo ndo maisha mpenzi, ila kabla hamjarudiana vizuri mwambie mkapime kwanza for the sake of you and your kids. Kitu kingine ni ivi kuwa mrembo yaani zidisha kuwa mrembo ili umwonyeshe kuwa your still hot!na watu huko njee lazima wanakutolea macho but dont go for other guyz!go out with your friends and kids have good time life is short.
Hawa wanaume wasituzeeshe hapa!nimependa sana ulivyo strong!even me nimeolewa but siwezi kuwa weak kwake hata siku moja!though nampenda sana

Anonymous said...

jamani wanawake hivi ni lini tutaishi kwa amani katika ndoa zetu. Dear ninakuonea huruma sana kwa kuwa hata mimi yalisha nikuta hayooo tena mume wangu aalini-cheat kwa house girl kwa kuwa nilikuwa nimepangiwa kazi mji mwingine nje kidoogo to ya pale tulipokuwa tunaishi. Iliniuma sana, lakini no way, Mme ninampenda, ndoa ya kanisani, hakuna talaka.
USHAURI.
Usimlipize kisasi mumeo utawatesa watoto bure na wewe mwenyewe kimawazo. Hata kama utaamua kutoka nje ya ndoa bado moyo wako umeshaumizwa! huwezi kutibu kwa kutafuta mpenzi wa nje, believe me, nilijaribu na HAIKUNISAIDIAA.
Msamehe mumeo na zidi kumuombea sana, abadilike. Hata kama akikukutanisha na huyo dada dear mapenzi hayaishagiii mweeee! uwiii!

Anonymous said...

Ooohhh.....you sound so strong good gal!! To be honest that man anakuzingua tu!!!Ukweli ni kwamba atakuwa anatombana na wanawake wengi sana.Ni huyo tu umebahatika kumbamba.Chamsingi usimrudishie kisasi maana ukirudisha kisasi itakuwa kama vile umekubali anachokufanyia that man is right!!! Wewe muweke sawa na umwambie aache hiyo tabia na muwekeane mikakati ya kuchunguzana!!!

Anonymous said...

Pole sana tena sana dada, jamani mara nyingi wanaume huwa wanatoka nje wakati mke au hata girlfriend akiwa mjamzito, ni tatizo kwa familia nyingi hi basi tu watu hawasemi. Dada najua kitendo hicho kimekuuma sana ... lakini jinsi ulivyosema ... angalia watoto wako ...kweli wajisemee wazungu... usijibu kosa kwa kufanya kosa... kama mwanamme ameshaunja nje ameshaonja ..wengine wanabadilika na wengine ndio unakuta wanakwama huko, na kuanza kuwabadilisha au kuwa na magirlfriend wengi. Mimi nakuomba sana, huu ni muda wa kujiangalia kimaendeleo, kama wewe ni mfanyibiashara au umeajiriwa kazania mafanikio zaidi na zaidi au elimu yako haikufika kiwango ... basi ni wakati wa kujikakamua ujiendeleze maana hawa wanaume wanaweza kukujeuka dakika yoyote. Mi muhimu kumsamehe, lakini usidanganywe kitu, ukishaonja nje, ni vigumu kuacha. Ataaacha mpaka mambo ya poe halafu aanze upya na atakuwa amehitimu style au namna ya kukuingiza mjini, na hutakaa umbambe. Na ajisemee R-Kelly.... when the woman is fed up! Lakini kwa sababu ndoa yenu bado ni changa sana labda unaweza kusahau na kumpa chance ingine. Lakini kumbuka pia mwezi akifanya kosa hilo .... na magonjwa kibao siku hizi ni ... ameamua kuwa really really selfish. I think you really need to weigh your judgment. Maana hata ukimnunia ni tu kama umemfukuza, itafika kipindi wote wawili mtachoka kufanya actions halafu watoto wakiendelea kukuwa itazidi kuwa ngumu. I wish you luck

Anonymous said...

jamani,
Nilidhani tatizo hili ni langu tu. Kumbe tuko wengi. Mimi dada nimeamua kusamehe lakini naona kuna kitu hakitoki rohoni. kIola mara kinanibana sana na ninalia. Hata hapa nimesoma ujumbe wako huku machozi yakinitiririka.
Kwa ujumla anakudanganya. Hakuna mwanaume anayekubali kwamba alimtomba "maimuna wake". Mimi pia hadi kesho anasema kuwa hakufika mbali. Yaani stori yako ni kama yangu na nimesoma nikadhani niliandika mwenyewe bila kujua.
Siku hizi nimegundua kwamba kusamehe ni kazi sana. Sijui kama kuna kusahau katika kusamehe. Mpaka naogopa nikifikiria maisha ya baadae. Mungu atusaidie. Tukio hili linaumiza saaaana. Mtu asikudanganye na usithubutu kusema kitu kama hajakukuta. Ni rahisi sana kusema lakini kutenda kazi.
Wangu nilishaamua kumpa unyumba kwa vile niliona najitesa na kujikosesha raha bure. Jambo lingine nililofikiria ni kwamba siku hizi hakuna wanaume waaminifu, nitampata nani mwaminifu kama hata huyu wangu katoka? Hata nikiamua ku-cheat haisaidii, kwanza siyo tabia yangu. Nitakuwa najifunza masomo magumu tu na kujikosesha amani.
Sasa nafanya naye kama sehemu ya kupunguza stress. Maana jamani, inaumiza moyo kupita kawaida.
Biblia inasema Wivu ni mbaya sana, unawaka kama mwali wa moto.
Naommba niachie hapa ili tuendelee kupata ushauri na mawazo ya wengine.
Mwathirika wa mapenzi.

Anonymous said...

FATAKI FATAKI TUPU!
HII NDIYO INAYOSEMWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KILA SIKU KWENYE MATANGAZO.
MTAFUTIE RAFIKI ZAKE WAMSHAURI VIZURI.

Anonymous said...

Kwanza Pole sana dadangu kwa matatizo yaliyokufika. Pili nakupongeza kwa ujasiri wako Mungu akuzidishie.
Ushauri wangu, kama walivyoshauri wengine haina haja kuendeleza kununiana, na cha msingi ni kutafuta njia bora ya kutatua matatizo yenu na muishi vizuri, huyo fisadi kiwembe atakimbiana wenyewe, usijali na Mungua atakusaidieni

1. Nendeni mkapime kama mko salama nyote.
2. Ukihakikisha mko salama basi anza majamboz. Unakumbuka ule mkao wa kununa aliofundisha dada Dina, basi anza na ule. Vizuri iwe wikiendi.
3. Mkiamka asubuhi sasa fungua kitabu cha kuelezana ukweli na kupeana mawaidha.
Nakutakia kila la kheri

Anonymous said...

Mimi pia nimewahi kufanya hivyohivyo. Nilikuwa na demu ambaye alimjibu kunya mke wangu, lakini nimemuacha. Yaani alimtukana kishenzi. Sasa tatizo lenyewe lilikuwa ni mke wangu. Hebu chunguza vizuri, kama wewe si tatizo, basi jamaa nae ameacha kukupenda. Mimi mai wife nampenda sana, ila kuna kitu ilibidi nikatafute nje. sasa hivi kipo mle mle ndani ndo maana nimeacha ujinga. unaweza kumbadilisha mmeo.

Anonymous said...

Loo, wewe dada mbona unamminya mumeo hivyo?Unafikiri angefanya nini wakati wewe ukiwa mjamzito na mchezo labda haukukufaa muda huo na jamaa alikuwa nduki na mihemko??Huoni kama huyo mdada kakusaidia kumzimia jamaa kashikashi ya mwili?

Hebu acha sasa kujibaraguza eti unamjaribu na wewe unataka kutafuta wa kwako?? Huoni kwamba unaongeza shida juu ya shida huyo jamaa yako ataendelea kutafuta nje?

Kwanza si ajabu kweli umetafuta hapa unatuzingua tu!!! una maana wewe huhitaji tangu umejifungua hadi sasa?Mihemko yako unaipeleka wapi?Mpe mumeo haki yake nawe akupe haki yako muendeleze mchezo hayo mengine yalikuwa ya kujibinafasi tu baada ya kukosekana the right person to play with.

Ukiendelea kuminya, ujue kuwa donda dugu hilo halitapona dada.Wewe meza tu ndo zetu wanaume huwa tunachepuka mambo yakituzidi mno.Sameheaneni tu yaishe muanze na moja mbili tatu.Kwaza hata wewe sasa hivi minyege imekupanda sana maana ni muda mrefu ingawa unajidai kama vile huhitaji, la sivyo na weqwe umeishaibua lijamaa.Kwani ungangali huo mimi unanipa shaka sana.Haya basi yako maamuzi.

shamim a.k.a Zeze said...

LOL!! leo nimeamini msemo usemao " KIBOKO YA MWANAUME NI MWANAUME MWENZIE" hapo mamy cha kufanya as yeye amejirudi na kukiri kosa, thats mean amejitambua kuwa alikuwa anachemsha...sasa cha kufanya mkae chini nae na kama ulivyoambiwa na wadau hapo mkapimishane ngoma...msije acha watoto yatima ...kama mambo fresh ..basi muendeleze yenu mapenzi ukumbuke we ni mkewe na 4 the sake of the baby...si wajua kosa moja haliachi mume..na ukizingatia shost ndo ivyo ulikuwa na uja uzito labda hakua anapata huduma zote...ili mradi kajirudi nawe jirudi muendeleze gurudumu

Ni hayo tu!!

Anonymous said...

Wanasema ukichunguza sana asali inavyotengenezwa utasema mmh, lakini kwa utamu wake ulivyo, hakuna ambaye anaweza kuicha! Labda uwe mgonjwa. Hii ni kama mapenzi ndani ya ndoa. Ukiyachunguza sana unaweza ukasema hapa nimeukwaa mkenge, lakini bado tunapenda tuishi katika ndoa kwasababu kubwa ya upendo, kwasababu kubwa ya je huyo nitakayempata atakuwa hana udhaifu huo.
Ulichofanya ni kizuri,kutafuta ukweli, baada ya kugundua `kulikoni' lakini wengi wanashauri tusipende kupekenyuapekenyua meseji za simu za mabwana zetu au mabibi zetu kwani unaweza ukakutana na meseji ikakupa ugonjwa wa moyo.
Wapo watu maofisini wanapenda kuitana wapenzi,mashosti lakini kiundani sivyo kama wanavyotaniana. Kuna wengine utani wa ofisini wanaweza wakajisahau wakaupeleka hadi nyumbani bila makusudio au wengine wakiwa na nia mbaya ya kuharibu mahusiano yenu. Kwahiyo wewe kama mwenza unatakiwa kuwa mwangalifu.
Ni vizuri kulinda chako,kama ulivyofanya, unaweza ukaweka geti kali, lakini lisivuke mpaka, kwani wapo waume ambao kuridhika kutulia kwao ni mwiko, lakini mwiko huo unaweza kuuondoa mwenyewe kinamna nyingi ikiwemo mwenyewe kuhakikisha kile kinachomvuta nje unaweza ukakifanya.
Labda mtasema nasemahivi kwasababu ni mwanaume, lakini wapo wanawake hawataki kuboresha mapenzi yao kwa wanaume wao, kama walivyo wanaume. Lakini no bora wewe mwanamke ukaboresha zaidi maana hali halisi itakuumiza wewe zaidi.
Kuhusu ushauri wangu naona kwa vile mwenyewe amekubali kosa,undelee kumweka sawa, kwani unaweza ukavuka mkoja ukakanyaga…
Tukubali tusikubali, hali hizo zipo sana, na wakuzimaliza ni mimi na wewe. Mfano mzuri ni wakuelezana ukweli, na wa pili ni wa kuboresha mahusiano yetu kwani huenda yakawa ndio chanzo na watatu nikuwa Karibu na mwanza wako, usimpe nafasi ya kupata vishawishi.
Tusubiri ushauri wa dada Dinah
Mimi
emu-three

mbelembele2008@yahoo.com said...

pole sana dada yangu.hayo ndio maisha yalivyo.muombe mungu tu akusaidie.huyo mumeo ndio amenogewa na K ya nje .yaani mpaka aje akae sawa itachukua muda sana.angekuwa hajakuoa ningekuambia uachane nae.lakini mvumilie tu kwani wanaume huwa tunajirekebisha sie.usimlipe kisasi kwani magonjwa ni mengi sana.vumilia tu hadi utakapoona mwisho wake.ikiwezekana nenda ukamshitaki kwa wazazi wenu.

Anonymous said...

dada hapo juu uliekuwa cheated tunaomba story yako izi story zinatufundisha sie tunaotaka kuolewa dada dinah je ni vipi unaweza kumdhibiti mwanaume asicheat?why do men cheat lkn jamni hamridhiki na mapenzi ya wake zenu na matamu wanayowapa na kuwalelea watoto kuwatunzia familia u shameless morons!!

Anonymous said...

kweli men are morons ur right mdada hapo juu

Anonymous said...

mi namuunga mkono mdau namba 1 kwa asilimia 100% coz mi ni mwanaume nilishawahi kuteleza kihivyo lkn demu alipompigia simu mke wangu ndo ulikuwa mwisho wangu kwake,na mke wangu alinielewa kwani sikumficha kitu,na sasa nipo nje ya nchi na simu yangu anayo mke wangu,inabidi upiganie kiburudisho chako mama hakuna mwanaume mwenye nafuu na videmu vya nje vinajua kuhandle waume za watu,so be careful usije wewe ukawa ndio mwanamke wa nje kwa mtu mwingine!

Anonymous said...

Ulichofanya ni kizuri bt usiendelee as long as ameshakubali kosa. Usicheze na ndoa mama watu wanazililia. Tulia na mumeo, jitahidi upendeze si kwa vile unanyonyesha basi unajiachia kama mzee. Na jaribu kujiuliza kitu gani kimemtoa nje, inawezekana sababu ni wewe. Rudisha mapenzi motomoto. Ila mkapime kwanza. Nakusisitiza usicheze na ndoa, ukiachwa wewe utarudi kwenye blog kuomba msaada wa kumrudia mumeo. All the best ktk ndoa yako.