Hivi huyu anampango na mimi au myeyushaji tu-Ushauri!

"Dada Dinah mimi naomba kupost tatizo langu, naliombea ushauri. Mimi ni mdada wa miaka 27, nimekuwa na boyfriend wangu kwa muda wa miaka 2 na miezi tisa sasa na ndani ya uhusiano huo tumejaliwa kupata mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja sasa.


Kipindi chote hicho mwenzangu hakuwa tayari kwa ndoa na mimi sababu kubwa ikiwa haniamini juu ya mahusiano ya mapenzi niliyokuwa nayo zamani kabla ya kukutana naye. Hapo nyuma niliwahi kuwa na relationships na watu wengine, ila tangu nilipokuwa nae sijawahi kuwa na wengine.


Ila wakati wa mwanzo kabisa wa uhusiano wetu aliwahi kukuta message kwenye simu yangu kutoka kwa ex boyfriend japo haikuwa ya mapenzi. All my ex boyfriends hatukugombana na kuachana kwa shari so huwa tunaweza wasiliana kama casual friends.


Alinieleza kuwa hapendi na mimi nikaacha. Ila nadhani hakunisamehe kwa hilo toka moyoni. Tumekaa na akatafuta access kwenye email yangu na kusoma mails zangu akakuta email toka kwa ex boy friend ikinipa hongera ya kuwa na mtoto, alikasirika sana na sasa akaamua kuwa uhusiano wetu ufe kabisa.


Ila mimi sababu nampenda sana nikamuomba afikirie upya uamuzi wake, mwanzo alikataa kabisa. Baadae akakubali nimpe muda japo wakati huo aliweka masharti juu ya uhusiano wetu, kuwa mawasialiano naye yawe juu ya mtoto tu.


Niliamua kujifunga mkanda na kuvumilia kipindi hiki, ni kama miezi miwili sasa tangu kianze, mwanzo nilikuwa nalia sana ila sasa nimeizoea hali, na pia hata yeye sasa anaonekana anapenda tuanze kuwa karibu, imeshatokea hata mara kadhaa tumefanya mapenzi.


Niliamua kubadili emails na hata kubadili namba ya simu ili kupunguza namna ya watu kuweza kunipata au kuwasiliana na mimi. Tatizo langu ni kwamba, sielewi kichwani kwake kweli anamapenzi gani na mimi na ana mpango gani na mimi.


Je ananiadhibu ili nijifunze somo au ananikomoa au anataka nikate tamaa sielewi. Amenifanya uwezo wangu kikazi na hata mahusiano yangu na marafiki na ndugu na hata watu wengine kuwa magumu na bado anasema anahitaji muda kuendelea kufikiri, je niendelee kusubiri au? maana kumpenda nampenda sana, kuishi bila yeye itawezanigharimu hata kuhama nchi. Naomba ushauri"

Jawabu:Pole kwa kuwekwa njia panda na baba wa mtoto wako.Kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi, pamoja na mambo mengine muhimu kuna nguzo kuu tano za kufanya uhusiano huo kuwa bora. Nguzo muhimu ambayo wengi huisahau au kutoilia maanani ni "mawasiliano".


Mawasiliano ninayozungumzia sio yale ya kuulizana hali zenu,mtoto au jinsi gani mnapendana kama sio matatizo uliyokumbana nayo kazini bali ni kuelezana na kupeana habari kuhusiana na mambo muhimu kwenye uhusiano wenu, kuweka wazi nini kinakukera, kuhoji uhusiano wenu unapokwenda, msimamo wenu na uhakika na hisia zenu, kuweka sawa mipango ya maisha yenu ya baadae (je ipo au haipo) n.k.


Asilimia kubwa ya wanadamu tunapokutana, kupendana na kukubaliana kuanzisha uhusiano huwa tunakuwa na mzigo wa maisha yetu ya awali ya kimapenzi kabla hatujakutana na wapenzi wa sasa. Hii inapaswa kutambulika na niwajibu wenu ninyi kama wapenzi kutambua kuwa ile "Past" ni sehemu ya historia ya maisha yako na haiwezi kufutika kamwe!


Hivyo wote mnapaswa kujua namna ya kukabiliana na "maisha ya awali" mnapokuwa kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi. Sio wapenzi wote wanaoachana kwa vita na chuki, kuna wengine wanaamua kuachana tu kwa vile mmoja anataka ndoa mwingine hayuko tayari kuolewa au kuoa, wapo wanaoachana kwa vile hawaridhishana kingono, wengine wanaachana kwa vile wamegundua penzi halipo n.k.


Hizo sababu nilizozitaja haziwezi kuwafanya watu hawa walio-share sehemu ya maisha yao pamoja kuachana 4 good, wengi wetu huwa tunapaenda kubaki marafiki mpaka mmoja wetu anapokuwa na mpenzi hapo ndio huwa tunapunguza ukaribu na tunabakiza salamu tu zile za kujuliana hali kama unauhakika mpenzi wako mpya atakubali hilo liwepo n.k.


Ni kweli wewe (muomba Ushauri) unampenda mzazi mwenzako na ndio maana umekua radhi kufanya yote ambayo alitaka ufanye ikiwa ni pamoja na kupoteza marafiki zako, kubadili nambari ya simu na anuani yako ya barua pepe, lakini huyo mpenzi wako bado halioni hilo kutokana na ubinafsi alionao.


Kuna matatizo machache ninayaona kwenye uhusiano wenu (kutokana na maelezo yako)kama nilivyodokeza hapo juu ni kuwa hakukuwa na hakuna mawasiliano, mpenzi wako hajiamini hali inayopelekea yeye kuwa "control freak" na mwisho kabisa ni kuwa hana uhakika na hisia zake juu yako.


Kitendo cha yeye kuonyesha anataka kurudiana na wewe mimi nadhani ni kwavile unampa ngono, isijekuwa anakuja hapo kwa ajili ya mwili wako lakini hana mpango na wewe kama mpenzi wake wa kudumu.

Kuona ujumbe wa kukupa Hongera ya kujifungua kutoka kwa Ex sio kosa kubwa la kumfanya ahitaji muda wa kufikiri, anafikiri nini kisichofikirika kwa muda wa miezi zaidi ya miwili? Ingekuwa amekukuta na mwanaume mwingine ningeelewa kuwa nahitaji muda hata wa miezi sita kufikiri na kujitahidi kukusamehe na kusahau lakini barua pepe tu!.....anawalakini huyo.

Nini cha kufanya-Sitisha uhusiano wa kingono na yeye tangu anahitaji muda kufikiri basi aendelee kufikiri na akimaliza nakuamua kurudiana na wewe moja kwa moja ndio Ngono itapatikana. Muambie kuwa huwezi kufanya ngono nje ya uhusiano kwa vile unahofia afya yako na ya mtoto kwani hakuna sababu ya kupewa mapenzi ya mwili wakati yeye hakupi mapenzi wala amani moyoni, vilevile hujui anafanya nini huko anakotumia muda wake kufikiri. Hilo mosi.

Pili, Rudisha uhusiano kwa marafiki na ndugu zako na tumia muda wako mwingi na watu hao hali itakayokusiaidia kuondokana na mawazo juu ya mwanaume asiye muelevu na wala hajui kuthamini hisia za mtu anaempenda kwa dhati ambae ni wewe mama wa mtoto wake.

Kitendo cha kuwa karibu na watu hao (ndugu na marafiki zako) kama ilivyokuwa zamani itasaidia kuboresha utendaji wako wa kazi nakuongeza furaha kwenye maisha yako, kumbuka kuwa unajukumu lingine ambalo ni mtoto. Hakikisha huruhusu matatizo yako ya kimapenzi kuathiri utendaji wako wa kazi ili usije fukuzwa kazi.

Jitahidi kutumia muda wako mwingi na watu hao pale unapopata nafasi, ikiwezekana badilisha kabisa mtindo wa maisha yako na mtindo wa kimavazi na jinsi unavyokuwa ukijiweka wakati uko na huyo "mzee wa kufikiri". Kumbuka wewe bado Kijana, Mzuri, unapendeza na kuvutiaa sasa muonyeshe kuwa unamtaka kwa vile unampenda lakini humuhitaji (Unaweza kuishi bila yeye) ikiwa hana mpango na wewe......hapo humuambii unamuonyesha kwa vitendo, kutokana na utakavyokuwa ukijiweka, sawa?

Tatu, Ji-keep busy na mambo yako na mtoto, lakini siku akitaka kuja kumuona mtoto usimkatalie lakini hakikisha kuna kuwa na "limit" ya yeye kuwepo hapo kwako na vilevile anapokuwa na mtoto wewe endelea na shughuli zako nyingine, yaani usimpe muda wa kuongea na wewe au kulianzisha zali la kutaka ngono.

Ukiendelea kumsubiri utakuwa unajipotezea muda, unajinyima amani na uhuru wa kuwa karibu na ndugu, jamaa na marafiki na vilevile kukataa wanaume wengine wanaokutokea na wanakupenda kwa kudhani kuwa baba mtoto wako anafikiria na siku moja atarudi. Siku hazitokusubiri wewe, zinasonga mbele kama ifuatavyo.......


Nne,(ukifikia hatua hii kama anakupenda kweli na anampango nawe, ataomba mzungumze), akiomba mazungumzo na wewe usikubali haraka haraka, mpe muda......mwambie leo unashughuli nyingi hivyo muonane keshokutwa na siku ya siku ikifika usisahau kujiweka ktk hali ya kupendeza na kuvutia kwa maana ya "sexy".

......na kabla hajaanza muwahi na muambie jinsi gani umejitahidi kufanya yale yote ambayo alitaka uyafanye, ulijiweka mbali na marafiki, ndugu na jamaa kwa ajili yake, umebadili nambari ya simu na anuani ya barua pepe ili Ex wako asiwasiliane na wewe kwa vile hukutaka kumuumiza hisia zake.

Kisha muambie msimamo wako na unachokitaka kutoka kwake, iwe ni commitment au unataka kujua uhusiano wenu na mtoto unakwenda wapi na mengine unayodhani ni muhimu na unayataka kutoka kwenye uhusiano wenu huo......alafu mpe nafasi aseme alichotaka kusema!

***Lakini baada ya kufanya yote hayo bado hajaonyesha dalili ya kutaka mazungumzo ili kurudisha "majeshi", basi ujue alikuwa anakutumia kwa ngono kila anapokuja kumuona mtoto wake. Achana nae na keep sexy, keep happy, work hard na siku moja utakutana na mwanaume anaejiamini, atakae kupenda kwa dhati na kukuthamini.

Wewe bado mdada mdogo na kumbuka penzi halilazimishwi.

Kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
Mdogo wangu pole kwa anayokusibu,
Wanaume walio wengi huwa hawapendi kujua/kusikia kama una mawasiliano na mwanaume mwingine zaidi yake. Nimesoma kwa umakini hii habari ila nionavyo mm huyo jamaa hana mapenzi ya kweli kwako, na uamuzi wakukuoa ama la hauhitaji hata siku mbili kuamua. Ukweli anao kichani kwake ila anashindwa kukwambia wazi kwakuwa anaona itakugharimu na mtoto bado ni mdogo, pia anaogopa kesi na kutoa matumizi kilazima therefore anakuvutia kasi mtoto asogee. Be careful.
Bubbles~~~
Anonymous said…
Mahusiano hasa ya urafiki, uchumba hadi mke na mume yanapitia kwenye mlolongo wa vikwazo. Haya yanatokea, nikawaida, na huenda ni vipimo vya kuliweka pendo lake mahala pake. Kama kweli unampenda mwenzako hutakata tama, unatakaiwa umpiganie kwa upendo na subira.
Unajua katika mahusiano ya awali lazima kutakuwa na kutokuaminiana, hasa ikitokea kuwa wewe ulikuwa na marafiki kabla yake. Na yeye pia huenda alikuwa nao. Haya ndio maisha ya wengi. Uhusiano huu hujichuja na hatimaye unabakiwa na yule ambaye unaweza kumuita `mke, au mume wangu’
Wakati wa kujichuja, ni kama huo, na hapo unatakiwa kuwa mwangalifu, kwanza kwa kumsoma mwenzako anapenda nini,na kipi hakipendi. Na kama wewe umeshaamua huyo ndiye anakufaa, inabidi uanze kukata mahusiano na wengine. Inakuwa vigumu kwani wengine unataka kuachana nao bado wanakuhitaji, kwa wema au kwa kukuharibia.
Hatua uliyochukua ya kubadilisha namba na e-mail address ni njema, na ilitakiwa ufanye hivyo mapema, ili kuondoa walakini. Lakini hata hivyo hujachelewa. Muhakikishie mwenzako kuwa yeye ndio chaguo lako. Kaa na yeye usione aibu, mueleze ukweli kuwa sasa wewe ndio chaguo langu, wengine hawana nafasi.
Hapa ofisini tulikuwa na majadala wa kwanini tunasomeana meseji zetu, yaani kwa mke na mume au wapenzi. Wengi wanasema, simu hazitakiwi `kushare’ Kama mume ana simu yake na mke yake, basi hakuna haja ya kusoma meseji za mwenzako.
Wengine wamesema nyie mume-kuwa kitu kimoja kwahiyo mambo ya kufichana sio mazuri, kwani mkianzia kwenye simu, mtaendelea kwenye mambo mengine. Ni vyema vitu kama hivyo viwekwe wazi, kwani mnafichana nini, kama mnaficha basi kuna kitu kinaendelea ambacho ni kinyume na makubaliano ya ndoa, au uchumba wenu.
Ni kweli kama mumesha-oana ni heri makawa wawazi, nyie sasa ni kitu kimoja, inakuwaje simu inalia unaogopa kuipokea kwasababu ni ya mume wako au mke wako. Ndio wakati mwingine sio vyema kupekuapekua meseji za mwenzako, lakini tunafichana nini? Hapa nahisi kama tunafanya hivi kuna sitofahamu miongoni mwetu. Sijui haya ni maoni yangu na siri ya mtu ni mtu mwenyewe.
Mimi
emu-three
Anonymous said…
Dada nitakufundisha kitu kinachoitwa man pyscology 101. Kwanza kabisa unatakiwa ujue kusoma alama za nyakati kwa mwanaume. Jee huyu bingwa kweli anakupenda? au? Mimi kwa muono wangu nadhani hapa hakuna penzi, labda kuna jingine.

Nadhani kama kweli anakupenda basi hakutakiwa akuweke kwenye probation eti kisa umeongea na ex wako...

Solution.
Muite na ukae nae chini, mwambie kwamba umeshakaa gereza la mapenzi kwa muda mrefu na sasa unadhani ni muda wako wa kuachiwa. Hivyo inabidi akuambie kama yupo radhi kuendelea au laa?

Dada kitu kimoja nitakacho kushauri, kamwe usiingie kwenye ndoa au relationship na huyo mpenzi wako kwa sababu ni mzazi mwenzio... Hilo litakuwa kosa utakalo jutia maisha yako.

Mdau #1
Anonymous said…
Dada, Pole sana na wakati mgumu ulionao.
Kuna watu wengine ikatokea katika mapenzi wakaumizwa au kudanganywa basi itakubidi ikugarimu sana kuwarudishia imani. Huyo jamaa yako ni mmoja wao,nawe sasa inakugarimu kutokana na mawasiliano uliyokuwa nayo na mpenzi wako wa zamani.
Nakushauri umueleza kwamba yaliyotokea ni kwa sababu wewe wanaume ulioachana nao hamkuachana kwa ubaya/kashfa hivyo basi huwa mnasalimiana kama kawaida lakini kwa sababu yeye hapendelei,umeacha na umuakikishie kuwa hautarudia tena.
Hali hii mimi naona ni nzuri kwa sababu wakati mwingine ukiwa na mawasiliano na wapenzi wa zamani taratibu unaweza kutekwa nao na kurudiana,au msiridiane lakini kila wakati mmoja wenu akipata na nyege anamtafuta mwenzake na mambo yanaendelea lakini inakuwa haina nguvu sana mwanzoni kwa kuanzia na baadae ushika kasi,wenyewe wanasema "kukumbushia koloni"
Hao wanaume uwafahamishe hali halisi na kama inawezekana umkutanishe na mmoja wao na mpenzi wako wa sasa nae kama mtu wa kuelewa atarudisha imani yake kwako.
Pia njia zako zote za mawasiliano ziweke wazi kwake,kwa mfano mruhusu awe na uhuru wa kuangalia sms au kupokea simu yako,password ya e-mail zako zote mpe,n.k.
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com
Anonymous said…
hapo tatizo lipo kwako mwenyewe dadangu!wewe kama upo na mtu ambaye hadi umezaa nae na unategemea aje kuwa mumeo kwanini uwape nafasi hao max zako kuwa karibu na wewe kwa namna moja au nyingine?lazima utambue kuwa ni ngumu kwa sisi wanaume kuweza kuamini kuwa mtu ambaye umewahi kukis nae na hata kufanya nae mavurugu(sx)anaweza kuwa rafiki wa kawaida,(sikusemi vibaya)ila najaribu kukuonyesha facts na wewe mwenyewe uchuje!hebu jiweke ndani ya viatu vyake kama dakika kumi tu(jaribu kufikiri ungekuwa wewe ndio yeye)na unagundua kuwa bado anawasiliana na wasichana ambao aliwahi kuwanao kimapenzi,halafu akwambie ni rafiki wa kawaida,itaingia akilini?so me ningekushauri uchague moja,kuamua kuwa na mzazi mwenzio au hao jamaa ambao wanakwambia ´´i miss u´´lakini hawaleti nepi za mtoto wala maziwa!na lazima uwaweke wazi kuwa unamalengo na maisha mapya sio ule usichana tena,kumbuka wewe ni mama sasa!nafikiri nimekusaidia kiasi mpenzi!babu zetu walisema "tatizo dawa yake ni kutatua sio kulikimbia"so kubadilisha namba ya simu na email na kila kitu(labda hadi nyumba)haitasaidia kama hutowaweka wazi hao jamaa kuwa u need to kuwa na maisha mapya na heshima kama asilimia sabini tu hivi,muombe msamaha jamaa na achana na hao jamaa wa zamani!
nilikuwepo!
Anonymous said…
Dada pole sana hadi hapo ulipofikia, lkn mm mtazamo wangu haupo siriazi na huyo mpnz/mzazi mwenzio, ww ndio unaweza kujenga/kubomoa uaminifu kwake.umepata huyo ambaye sijui kama mlipanga kuzaa au iliingia bila plan za kuona!!. ivi hata kama ungekuwa wewe yy akwambie kuna x wake wanawasiliana sana ungemuelewa kama ni mawasiliano tu au kuna kitu kina endelea kweny black box? try to be siriaz ukiona mume hakuamini means kuna possibility kuwa kuwa wewe una matukio yanayo onyesha kuwepo uhusiono mwingine, au huan mapenzi ya dhati kwake so yy anaona wewe hutambui umuhimu wake, kama una mpenda show it, kama huonyeshi kama unampenda yy sio malaika kujua kama unampenda au laa,kufanya mapenzi sana/kuzaa naye sio maana kuwa anakupenda/wewe kumpenda, yy unaweza kuona alikuwa anakusoma tu akili yako unamwelekeo gani?, upo siriazi kiasi gani?,unajali vipi?, unamtegemea kvp?,unamshirikisha kvp? na vitu kama hivyo lazima um match interest zake, some time you can surrender non critical interests,possibly ulipo kuwa naye aliona kama hujaridhika na yeye so bado ulikuwa unaangaza angaza macho bado kwa vidume vingine, na pengine umeanza kuwa siriaz baada ya mimba hatimaye mtoto so yy anaweza kuwa amekusoma sana hadi hapo, so its you kujiweka/kujirekebisha na kumuelewesha kuwa ur dead serious on him.Some time wanaume wana lalamikiwa kwa makosa au kukosa uaminifu wa wake/wachumba/wapenzi wao. however it depend ww ndo unamjua huyo jamaa u've been with him for so long now, huwezi niambia kama hukuweza msoma kama mtumiaji tu au amefika? be siriaz dada, mm huwa nawakubali wazungu kwa kipengele kimoja tu, nacho ni kuwa siriaz katika jambo ambalo amekusudia kuli fanya kama kweli ni mpenzi ana stick to u kama samaki na maji,kitu ambacho wengi wetu hatukifanyi wewe unakuwa upo upo tu jamaa ataona wewe mzembe tu atakuzalisha then hakuoi, siku hizi access to women ni kubwa tofauti na zamani, mwanume au mwanamke anaweza oa au asioe kwani anachotaka kama anapata any time,i.e kupikiwa,utamu mpaka home,kufuliwa nguo, usafi home, n.k anaweza pata hata kama hajaoa zamani hii kitu ilikuwa ngumu, imeenda ikibadirika hadi now unakuta njemba zinakujaoa/kuolewa uzeeni. hahha.....watu hawataki kujibana solution ni kutooa/kuolewa mapema ili aendelee kuwa huru of which huwa ina impact kubwa kwa wanawake kwani umri ukieenda sana kuolewa inakuwa ngumu kidogo.
kingine pia ni maandalizi kuoa/kolewa ni vitu vinavyohitaji maandalizi so jamaa pengine hajajiandaa/muda sio mwafaka kuwa na wife home but its you na yy kuongea vizuri kufikia mwafaka kama hataelewa jua tu alikuwa mpita njia hana true love nawewe, na usijilazimishe kuolewa nae utajuta the whole life maana atakuwa anafanya anavyotaka naww itakuuma lkn ndio ushafika utafanyaje1! ni hayo tu kwa leo sema naye, i wish u gud luck!

by lajk@ymail.com
Anonymous said…
huyu kaka hapa juu nimempenda sana! maelezo yake ni mazuri mno, na nakubaliana nae. mimi pia nishagombana sana na fiance wangu kuhusu mambo ya x na mie nilikwua na keep contacts nao na ni kweli at times mnakumbushana kwa jokes lakini sio kimatendo mambo yale ya zamani. sio vizuri especially mtu kama umezaa unakuwa mama u have to be focused and mov on wit ur life . kubadilisha email namba haisaidii cha kufanya ni kuwa push away hao ma x wako. mtu mliye vuliana chupi au kukiss au kuwa kwenye mapenz (hata km kukiss/kufanyana hakukuepo) huwezi kumkeep kama rafiki hata km hamkuachana kwa shari. hio ni fact! better thing uache mawasiliano nao ila ikatokea mkakutana barabarani ukiwa na mumeo unaweza kumsalimia tu basi yakaisha ila mambo ya hadi kutumiana email ni NO NO dada yangu! cha kufanya, muombe mpenzio msamaha(kwa vitendo) muonyeshe kuwa hukuwa na nia mbaya na mpe muda usimlazimishe jamaa anakupenda. believe me ila ameumia. inauma kweli. all the best.
Anonymous said…
hana mpango na ww, nyie mko kwenye game ambayo ukiendekeza haitaisha.mtabaki kuumizana mioyo.
Anonymous said…
hey mama ake huyo uliezae nae sikufichi ameshakuona kuwa huna msimamo hivyo mlee tu huyo mtoto lakini hapo hakuna mapenzi, ww mwenyewe ndio umeharibu ushinde moyo wako tafute yule aliyetayari kuwa nawe hapo utajiumiza kichwa mama ake
Anonymous said…
pole sana dada kwa yaliyokukuta,napmba ujue kuwa mtoto sio ndio dada yangu, vijana wengi siku hizi wana watoto waliozaa na wasichana lakini sio wanaowaowa, huyu mwanaume wako naona ameshabadili nia ya kutaka kukuowa, ndo maaan anatafuta visingizio visivyo na maana, huwezi jua ana plan gani na maisha yake, ila kukuambia anaona aibu hautamuelewa, angalia sana dada asije akakakufunga ukapoteza muda wko bure.
Panga maisha yako bila ya kumtegemea, na pia mwambie kama kweli anakuhitaji uoni haja ya kusubiri, lakini kama anaendelea na msimamo wake tafuta utaratibu mwingine dada yangu.
Wengi wamezaa na wanaume lakini wamewaacha kwenye mataa bila hata sababu zinazoeleweka.
pole sana ila fanya maamuzi mapema usije chelewa na kujuta baadae.
Anonymous said…
Mdogo wangu huyu jamaa si mtu mzuri,ukiona mtu ambaye hapendi ushirikiane na ndugu na marafiki zako kwanza hajiamini na ana wivu wa kupitiliza.Mtu kama huyu hafai kuolewa naye kwakua atakua mbaya zaidi na anaweza kukudhuru au kukuacha na watoto hata 5 bila sababu za msingi.jiondoe mapema utapata mzuri zaidi.