Thursday, 25 December 2008

Hana shukrani na a'niponda tu kwa Marafiki-Ushauri

"Pole na kazi dada Dinah. Mimi ni Kijana mwenye umri wa miaka 24, ni mwaka mmoja sasa tangu nimeoa. Nina tatizo ambalo linaniumiza kichwa na sijui nifanye nini, thats why nimeamua kukuandkia hii e mail ili nipate ushauri wako na comments from other people.


Tabia ya mke wangu ni kuchukua mambo ya ndani na kuyapeleka nje, na amekua mtu wa kulalamika everyday, Najitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha anapata kila anachohitaji lakini imekua kazi bure.


Kutokana na kipato changu hua nikipata pesa nanunua kila kitu ambacho ni muhimu kwa matumizi ya nyumbani kuanzia chakula na mahitaji yake mengine muhimu yaani kwa kifupi everything needed I give to her, lakini kwake yeye ni complaint tu.


Na kitu kina choniumiza zaidi ni pale anapokuwa either with my friends or her friends, yaani hakuna stori nyingine isipokuwa ni kuniponda na kusema namtesa, na mnyanyasa sasa sielewi kama kweli ana mapenzi ya dhati na mimi au la.


Na nikimwambia kama vipi akapumzike home hataki anasema nikimpeleka nyumbani nimpe na Talaka. So dada nahitaji ushauri wako nini nifanye? na je ananipenda au hanipendi kwa hali hii?"


Jawabu:Asante kwa kuniandikia. Mkeo ama hana mapenzi na wewe au hapati kile ambacho anakitaka au alitegemea kukipata kutoka kwako mara baada ya kufunga nae ndoa pamoja na kusema hivyo inawezekana huyu binti alilelewa kwenye mazingira ya kutokujua na kuheshimu miiko ya nyumbani kwako, kwamba kinachotokea kwenu kinabaki palepale kwenu, kwa kifupi hana heshima....utoto pia unaweza kuchangia yeye kuendelea kuwa na katabia hako kabaya kabisa.


Kutokana na maelezo yako umesema kuwa unahakikisha kuwa anapata kila kitu anachotaka na unampa mahitaji yake muhimu ndani ya nyumba, hakuna mahali umeelezea kuhusu kumpa mapenzi ya kutosha.....maisha yenu ya kingono yakoje? Unadhani kuwa unamridhisha linapokuja suala la mahitaji yake ya mwili na hisia?


Tatizo la baadhi yenu wanaume mnadhani kuwa mwanamke ukimpa kila kitu in terms of material things na chakula cha kumwaga basi karidhishwa huyo......kuna mahitaji mengine ambayo kwa baadhi yetu wanawake ni muhimu lakini kwenu wanaume hayana umuhimu kwavile ni madogo.


Ninyi mmefunga ndoa mkiwa wadogo sana (ukilinganisha na maisha tunayishi hivi sasa) hivyo mnatakiwa kufanya mambo kama "young couple" more like bf and gf kuliko baba na mama......have fun!


Kitu kama kujenga urafiki kati yako wewe na mkeo hii itasaidia kuwa karibu zaidi na wewe na kukuambia yaliyomsibu au nini hakimfurahishi ndani ya ndoa yenu. Kumuonyesha mapenzi kwa vitendo sio kufanya hivyo only unapotaka kufanya ngono bali fanya hivyo kila unapopata muda....vitu vidogo kama kumshika, kumbatia wakati mnaangalia Tv, kutoka kwa ajili ya matembezi, kumbusu kila unapokuwa karibu yake.


Akikatiza mbele yako kuelekea jikoni mvute na mpe busu mate, mshike tako na vitu kama hivyo, kumuonyesha kuwa unavutiwa nae na unampenda, msaidie kufanya vijishughuli ndani ya nyumba ukipata nafasi sio kila kitu afanye yeye kwa vile tu umeoa n.k.


Hakikisha mnapofanya mapenzi anaridhika kwanza alafu ndio wewe unamalizia, hakikisha unajua uwezo wake wa kungonoka badala ya kuwa unafanya nae kila siku wakati yeye ni twice a week type(hapo lazima atahisi kuteswa ofcoz) au kama yeye ni wale wanaotaka kila siku na wewe ni mtu wa once a week ofcoz utakuwa unamtesa.


Nini cha kufanya-Kaeni chini na mzungumzie tofauti zenu, weka wazi kuwa hupenzi tabia yake ya kwenda kueleza watu maisha yenu binafsi, mwambie kama kuna tatizo lolote au kuna kitu hakifurahii ungependa akuambie wewe moja kwa moja ili ujirekebishe.


Anza kwa kumuambia akueleze kwa uwazi vitu gani unafanya havipendi tangu mmekuwa pamoja, akivisema basi hakikisha unajirekebisha na kuwa mume bora kwake. Mawasiliano ndio ufunguo wa kurekebisha mambo na kuondoa tofauti ndani ya uhusiano wowote wa kimapenzi kwani ni njia pekee itakufanya wewe na yeye kujua tatizo liko wapi na lilekebishwe vipi.


Mwambie yeye ndio mama mwenye nyumba na yeye ndio anaweza kuibomoa au kuijenga nyumba yenu na kuwa bora zaidi na mfano kwa wanandoa wadogo wengine.


Shirikianeni ili muweze kuishi kwa amani na upendo, kwani mnasafari ndefu sana ya kuendelea kuishi pamoja since wote ni wadogo ndani ya ndoa. Kumbuka ili ndoa iwe bora inahitaji kufanyiwa kazi, Uhusiano wa kimapenzi sio lelemama ni hard work.

Kila la kheri!


***Dinah anawatakia usherekeaji mzuri wa sikukuu ya Noeli, nawapa pole wale wote wanaouguliwa na wale waliofiwa, Mungu awapeuponaji wa haraka wagonjwa na kuwapa moyo wa uvumilivu wafiwa kipindi hiki......Mungu awe nanyi!

8 comments:

Anonymous said...

Well
kwanza nakutakia nawe sikukuu njema,then back to ya issue,mi
nadhani unahitaji kukaa na mke wako na kuongea nae kuhusu vitu anavyovifanya na akuambie tatizo ni nini,then umueleze tu ukweli kwamba anavyofanya kuwambia rafiki zako mambo ya maisha yenu u dont appreciate.
Kitu kingine badala ya wewe kununua vitu vya ndani ni vizuri kama ungekua unampa mkeo ndo afanye hivyo may be she like to do shoping herself, i know wasichana wengi wanapenda kufanya shopping za nyumba zao wenyewe na si mwanaume kumnunulia.

Anonymous said...

pole sana kaka kwa yote yanayokukuta katika ndoa yako ki ukweli huyo dada
hana tena mapenzi na wewe na wakati haujafunga nae ndoa je alikuwa na tabia kama hizo?wanawake kama kama hao hiyo ndyo inakuwa hurka yao kiasi kwamba kuja kuacha inakuwa kazi sana dawa ni moja andika taraka talaka anayosema mrudishe kwao atzidi kukutia aibu na hila kwa jamii nzima.ni hayo tu its mlimbwende

Anonymous said...

WEWE MUACHE HUYO MKEO KWANI TABIA KAMA AMEANZA KUACHA SI RAHISI; MPE HIYO TALAKA AITAKAYO: NAAMINI WW BADO KIJANA PIA BADO HANDSOME WAPO WATAKAO PITAPITA MBELE YAKO WAKIJUA UMEMUACHA ESPECIAL HAO HAO MASHOGA ZAKE; ACHANA NAE HUYO HANA SHUKURANI:SIKU UKIKOSA KABISA ATAANDIKA BANGO KWENYE MILANGO:

MAMA LAO:

Anonymous said...

Habari dada dinah, samahani kwa kuwa nje ya mada shost, pole kwa kazi ya kutuelimisha ss. Dada tatizzo langu mm sijui kuweka mbombo wazi kama wenzangu, nimejaribu kutafuta e-mail yako yote nimeshindwa. je nitokeje mbele kama wenzengu? maana shost nina madukuduku kibao, napenda ushauri kama wenzangu.asante, au yeyote mwana ambaye anaelewa haya aniandikie kwenye e-mail anitaantonya@yahoo.com asanteni

Anonymous said...

Hello mchangiaji wa hapo juu,usikurupuke mno kusema hana mapenzi na huyo bwana na kusema ambpe talaka.Mambo ya ndoa hayako hivyo vinginevyo hakuna mtu ambaye angedumu katika ndoa.

Mpendwa mlalamikaji, naungana kabisa na mchangiaji wa kwanza kwamba ni vema,

Ukae naye mzungumze pamoja juu ya hali hiyo inayojitokeza ili mshauriane na yamkini kuontana.Mwambie athari za kupeleka mambo ya ndoa yenu nje kwa watu na mengineyo.

jambo lingine ni lile ambalo mchangiaji wa kwanza amesema jaribu kubadili mfumo wa ununuzi wa mahitaji yote ya nyumbani,yaani badala ya wewe kuzurura kwenye shoppinh, basi mpe nafasi hiyo mkeo.
Jambo lingine, ni vizuri kama pia mke wako na wewe mtakaa pamoja kuangalia makadirio ya matumizi yenu nyumbani kulingana na kipato mnachopata kwa mwezi, na kwa umahiri mzuri mpe nafasi huyo mkeo kupanga makisio ya matumizi yenu na kila kitu.halafu fanya tathmini baada ya muda fulani katikati kuona jinsi kila kitu kilivyokwenda.

Ni kweli sa ingine wanaume huwa tunawanyima na kwabania nafasi zao wake zetu kiasi kwamba sasa mke anabaki kwenye dilema kuwa sasa kazi yake ni ipi?Je, awe wa kupokea tu na kupika?hapana anayo nafasi ya kufanya yale yote ambayo hata mume anafanya, muhimu tu ni kujaribu kushirikishana na kugawana majukumu kutegemeana na nafasi zenu mlizonazo.

Amini usiamini, ukimpa nafasi yeye vizuri ataacha kusema mambo yenu nje. Unajua watu huwa hasemi mambo wanayofanya wenyewe kwa watu,ila huwa watu ni wepesi kusimulia visa vya wengine.Kumbuka msemo wa wahenga" Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu uchungu"

Mpaka hapo bika shaka utabadili mfumo huo na utakusaidia.Usiwe na haraka ya kusema mke huyo hakufai, hiyo haitakusaidia.Kama ulimwoa ulimkubali na kuridhika naye, basi fanya chini juu kuchukuliana naye na kuzungumza naye kwa upendo uleule ulioonyesha wakati wa kumtongoza na kumzhawishi mpaka akakubali kuolewa nawe, nina imani hata katika hili utafanya ushawishi zaidi ili hiyo tabia aimalize.

Nakutakia kila la heri katika hilo ili mwaka mpya uanze na mabo mapya katika ndoa yenu.

Dinah said...

Anony @ 7:51:00 PM, kama ulivyoweka comment yako unaweza kuweka maelezo yako kw anjia hiyo au angalia upande wa kuli mwa ukurasa huu utaona anuani yangu ya barua pepe inayokwenda kwa bongo.radio@yahoo.com

Asante kwa ushirikiano.

Anonymous said...

kaa naye mkeo ongea naye, wewe ndo unmjua vizuri mkeo sisi hatujui yupoje na ana akili gani ,kwani wewe hujamuuliza tatizo ni nini? mambo mengine hayo yanaweza kumalizwa na nyinyi wenyewe,pengine hakufanyiwa kitchen party,kufundwa na vitu kama hivyo.

kingine mjomba mambo ya sokoni kama yeye anataka ndio aende mbona ruksa kwanza uta babmbikwa hata nyanya zenyewe, kama vipi shopping mwende wote kama unapenda. hapa inaonekana swala lipo kwenye kodi ya mezani yaani haipo, sasa unafikiria nini? solution unayo mwenyewe ila nina wasiwasi na hiyo talaka anayodai ameona labda alivyotegemea sio so anataka akacheki ustaarabu mbele.

Zaidi ukiona hakuelewi,jaribu kutumia wazee kumwelekeza, pia nina wasiwasi an umri wa huyo binti kama wewe ni 24 yeye je? possibly ana akili bado ya kitoto but take tht seriously,unatakiwa kuwa firm hayo ni baadhi ya mambo ya kwenye ndoa usikurupuke, shirikiane kufanya maamuzi, pssibly wewe ni mbabe humshirikishi so yeye anakusema kwa friends akijua msg sent utazipata tu, ukishindwa sikio la kufa halisikii dawa lkn jitahd kufanya maamuzi yalo sahihi/ kilala kheri

lajk.

Anonymous said...

Mdau mwenye e-mail anitaantonya@yahoo.com kumuandikia dada Dina tuna e-mail bongo.radio@yahoo.com