Monday, 8 December 2008

Ananiacha kwavile tu mimi sio kabila lake!-Ushauri

"Habari za kazi Dinah, nimeona niankuandikie baada ya kuisoma ya mwenzangu na kuona watu wengi wamemshauri vizuri.Habari yenyewe inaanza mwaka 1998 Novemba baada ya kuhamia Arusha tukitokea DSM baada ya baba yangu aliyekuwa Askari jeshi kuteuliwa kuwa Katibu Tarafa mkoani Arusha na kuhamishia makazi huku.


Kwenye nyumba tuliyofikia alikuwa akiishi msichana moja anaitwa Agness Meliyo(Totoo)kabila ni Muarusha alikuwa akiishi na mama moja aliyeamua kumsomesha msichana huyo na kumsaidia kazi ndogondogo baada ya kutoka shuleni, sasa kipindi hicho mimi nilihamia nikiwa darasa la sita na kuhamia shule hiyo aliyokuwa akisoma msichana huyo yeye akiwa darasa la nne.


Kipindi hicho hakuna kati yetu aliyemtamkia mwenzake kuwa anampenda kwa kuwa bado tulikuwa shule ya msingi mwaka 1999 baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba wao walihama katika kitongoji cha Sakina na kuhamia katika Kitongoji cha Majengo kwa kuwa mama huyo aliyekuwa akimlea alikuwa akinipenda nilimsaidia kuhamisha baadhi ya vitu na kuniomba nikalale kwake alipohamia nilifanya hivyo na kipindi hicho ndicho tulianza rasmi mapenzi yetu na Agness.


Baada ya kukubaliana nakuona kila moja mwenzake anampenda tulianza mahusiano naye mwaka 1999 Desemba nikiwa mimi tayari nimemaliza darasa la saba na nikajiunga na kidato cha kwanza mwaka 2000 nikiwa kidato cha pili baada ya miaka miwili kuanza shule yeye akiwa darasa la sita tulishirikiana kingono na kwa kweli nilimkuta na usichana wake ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kukaa miaka miwili pamoja.Kwa kweli mapenzi yetu yalikuwa ni mazuri huku kila moja akijitahidi kumpenda mwenzake kwa nia ya siku moja kuoana na uhusiano wetu ulikuwa ukijulikana na wazazi wake wa kumzaa ambao nao tunaishi nao hatua chache kutoka tunapoishi sisi pamoja na mama yake mlezi.


Baada ya mimi kumaliza kidato cha nne mwaka 2003 nilisoma baadhi ya kozi hapa Arusha na mwaka 2005-2007 nilikuwa DSM nikisome katika chuo cha Rayol college of Tanzania nikisomea Uhandishi wa habari muda wote tulikuwa tukiwasiliana na kupeana ahadi nyingi ya baadaye kuja kuishi pamoja,na kipindi chote alikuwa anakuja nyumbani na anamsaidia mama yangu kudeki,kupika na kuosha vyombo yani kila mtu alikuwa akielewa uhusiano wetu.


TATIZO LENYEWE.
Baada ya kumaliza kidato cha nne mchumba wangu huyo aliamua kusome Ualimu wa awali(chekechea)kwa muda wa miaka miwili na kipindi fulani akikaribia kumaliza chuo alikuwa akidaiwa Ada jumla ya Tsh.Laki moja na mama yake mlezi alimweleza kuwa kipindi hiki yeye hana fedha kwa hiyo amfuate mama yake mzazi amlipie Ada hiyo naye mama yake hakuwa nayo ikabidi amweleze mama yangu ambaye alimpatia fedha hiyo na kwenda kulipa Ada hiyo na kufanikiwa kumaliza lakini hivi sasa ndio wapo kwenye mitihani ya mwisho huku akiwa amepata field katika moja ya shule mkoani Kilimanjaro.


Msichana huyu kwa kweli ndugu zangu nilikuwa nampenda sana ni ilikuwa kuanzia mwakani tuanze kuishi pamoja kwa sababu ndio alikuwa amemaliza masomo yake.

Tumeishi na msichana huyo tangu mwaka 1999 akiwa ni mwanafunzi wa darasa la nne hadi leo 2008 Novemba eti ndio ananieleza niachane nae kisa ni hivi.Msichana huyo yeye ni Muarusha na kabila hilo huwa halitaki kuoana na kabila tofauti eti mama yake amemtishia kumlaani ili aweze kuachana na mimi wakati tangu muda mrefu wazazi wake walikuwa wakipinga na yeye alisema hawasikilizi.


Baada ya kupata nafasi ya field huko Moshi alikuja nyumbani siku moja nikijaribu kuongea naye anakuwa na hasira hakutaka kuongea na mimi kabisa sasa kuna rafiki yake ambaye hupenda kumueleza mambo yake na yangu hata yale ya siri,nikawa nimestuka hali hiyo nilimweleza dada huyo ambaye huuza pombe katika kibanda na nyama ya nguruwe kuwa anayoyataka yatatimia kwa kuwa alikuwa akiongea baadhi ya mambo kinyume nyume kinachohusiana mimi na mchumba wangu tena mambo yenyewe yakiwa ni siri kati ya mchumba wangu na mimi.Basi siku moja alikuja kutoka Moshi akamweleza rafiki yake huyo ambaye mimi nahisi ndiye mnafiki kuwa eti ana mazungumzo na mimi nilimfuta nyumbani kwao saa za jioni akaniambia ni kweli anataka kuongea na mimi lakini kwa muda huo alikuwa akitoka akielekea Ngaramtoni kwa rafiki yake nikaachana nae nikarudi kwa huyo dada na kumuuliza ni kitu gani anachiotaka kuongea.


Agness akaniambia kuwa eti anataka kuachana na mimi na alishamweleza kila kitu dada huyo na kesho yake aliporudi kweli akanielezea kusudio lake na nilipomuuliza sababu yeye alisema kuwa ameamua tu na kwa sababu ya mama yake kumkataza eti jamani baada ya miaka tisa nikiwa naye tena nilianza naye akiwa ni mtoto kabisa.


Lakini siwezi kuwaficha kitu chochote juu ya huyo binti ila nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu nilimuita msichana huyo chumbani kwangu ni ilikuwa ni kujaribu vipi kuhusu ahadi yake na mimi baada ya mambozii fulani nilimweleza kuwa nilikuwa nataka kuachana naye kwa kweli alistuka sana na aliponiuliza ni kwa sababu gani sikumweleza kitu chochote na akaamua kuondoka chumbani kwangu.


Asubuhi ilipofika alinitumia barua kwa mdogo wake na ndani ya barua hiyo alikuwa amesema kuwa hawezi kuishi bila yangu hivyo ameamua kujinyonga na akasema tukio hilo atakwenda kulifanyia chumbani kwangu kwa kweli nilimsihi sana asifanye hivyo na akanielewa baada ya kumwita na kuongea naye kuwa nilikuwa nataka kujua msimamo wake katika uhusiano wetu na alinielewa tukarudia kama zamani tena kwa upendo zaidi hadi kilichotokea hivi ajuzi.


Hivyo ndugu zangu wadau naomba ushauri wenu maana nimeshindwa kuvumilia kwa sababu ninampenda sana na tumeishi naye kwa muda mrefu tangu wote naweza kusema tulikuwa wadogo maana mimi nilikuwa ndio nimemaliza darasa la Saba na yeye akiwa darasa la Tano mwaka 1999 mpaka leo ameamua kuachana na mimi je? nifanyaje."

Jawabu:Pole sana kwa yaliyokutokea, nashukuru kwa ushirikiano wako.
Wewe na Agness mmekuwa kwenye uhusiano tangu mwaka 1999 alipokuwa darasa la nne katika hali halisi akiwa mtoto mdogo asiejua nini hasa maana ya kupenda.


Binti yeyote ktk umri mdogo ambae amekua au anaelekea kukua (kubalehe/vunja ungo) huwa anakuwa na hisia fulani za kutaka kuwa karibu na jinsia ya kiume (ndio maana baadhi ya wazazi Tanzania huamua kuwafuga watoto wao ktk kipindi hicho cha ukuaji ili kuepusha wasianze ngono).
Katika harakati hizi za ukuaji wa mtoto wa kike hufikia wakati anasikia raha kuguswa au kushikwa na mwanaume na vilevile hujitokeza vijitabia vingine kama kujichekesha, kukuangalia kwa "kutamani", kuvaa mavazi fulani kupata "attention" n.k. hii yote ni kutokana na mabadiliko ya homono mwili mwake.....ni kipindi kigumu sana kwa wasichana na wanahitaji kuwa karibu na wazazi wao ambao wanaweza kuongea nao kwa uwazi kuhusu mabadiliko yao na jinsi yakukabiliana nayo.


Huyu binti alipokuwa akionyesha kukutaka haikuwa mapenzi bali ilikuwa zile hisia zake za ukuaji wake, japo kuwa yeye na wewe mliamini kuwa ni mapenzi. Huyu binti jinsi anavyokuwa ndivyo anavyozidi kubadilika na kung'amua au ku-discover ujinsia wake, "attraction" kwa watu wengine n.k.


Sasa wewe kuwa na Agness tangu alipokuwa mdogo haina maana kuwa ndio mizizi ya uhusiano bora au mapenzi madhubuti, inawezekana kabisa wewe ni muhimu sana kwenye historia ya maisha ya ke ya ukuaji hasa kwenye suala la ngono kwa vile ndio akuanz ana wewe lakini hiyo hamfanyi yeye kukupenda wewe kama unavyompenda yeye(ulimpenda ukiwa Kaka mkubwa kabisa).


Agness alikuzoea wewe kama mwanaume unaempa mambo fulani, unamsaidia anapokuwa na matatizo sasa basi inawezekana kabisa ulipomuambia kuwa unaachana nae mapema mwaka huu (kama ulivyosema) ulimsaidia ku-search moyo wake na akagundua kuwa hana mapenzi juu yako.
Kutokana na maisha tunayoishi hivi sasa sidhani kama Kabila ni kigezo cha watu kutofunga ndoa, nadhani anatumia sababu hiyo ili wewe u-give up on her kwa vile hutokuwa na jinsi zaidi ya kumuacha aende kuolewa na mtu wa kabila lake kwa kuogopa radhi ya mama yake(kutokana na Imani yake).
Nini chakufanya-

Nakuja....endelea kuwepo!

4 comments:

Anonymous said...

pole sana mdau kwa hilo, mm mtazamo wangu hapa kuna mawili anaweza kuwa kapata mtu mwingine so wewe ni kiraka, by the way kuanza nae sio tija kwani huenda kampata mwingine ambaye yupo smart ktk mambo na pia kujali hadi kuweza kunteka fikra vizuri,aidha jua kuwa wasichana wapo very adaptive to change so kama hukumuweka vizuri katika kumjali/kutomba vizuri/vizawadi. majisifa ya kutosha basi ndio imetoka hiyo ninachojua ni kwamba wasichana wanakuwa driven na hisia so inawezekana bado hukumteka kivile sana, maisha ya sasa sidhani kama bado kuna ukabila kiivyo, lkn pia inanipa shida kujua ilikuwaje ikachukua muda hivyo ikiwa wazazi wa pande zote walikuwa wanajua?, pioa wazazi wa huyo binti ndo kusema wanataka mtafutia bwana au inakuwaje?
pili anaweza kuwa anawasikiliza wazazi lkn hapa ni asilimia ndogo sana ingawa hapa ina make sense if and only if this statement is correct and strict enough'' ni waarusha na huwa hawakubali kuolewa na kabila lingine'' of which for the time being that to a large extent does not hold water, mambo ya kuchaguliana wachumba yanaishia sasa hv ni mixer tu ndio maana hata wabena wanaoa wachagga hahhahah joke!, lkn kweli zamani ilikuwa ngumu mnyalu kuoa mhagga lkn now ni full mixin, mm nataka nioe maasai hahah!.
so from there you can justify your position by making sense of the two debatable concepts regarding your case.however you still have to invistigate more ili ujue mchawi wako yu wapi,siku hizi gals have bcome very unrealistic, even men, so you yourself could have been with her partially, you probably didnt agree whether you get married/ is just for fun actually it is very confusing especially when mtu unajua una mtu wa kuoa halafu inatokea kama hii.namini humu utatoka na jambo ambalo litakusaidia kutoka kwa wadau mbalimabli, kwa dada yetu Dinah ambaye kwakweli anbaye atasema hayupo smart ktk sector ya malavi daviatakuwa na lake jambo,hata hivyo hata kama kuna vitu anakosea ni kawaida kwani yeye si malaika,haya tusikie michango ya wadau wengine na conclusion ya sister Dinah
by lajk@ymail.com

Anonymous said...

Ulipomjaribu kwa kusema unaachananae labda akaenda kufikiria akaona humfai kwani utamuacha wakati wowote. Wanawake wengine hawataniwi wala kupimwa. Pole sana mshikaji wewe kubali tu kuachwa utakutana na mwanamke mwingine atakupenda zaidi ya huyo.

JayJay said...

Rafiki yangu huyo demu ata ukija kumua ni matatizo tu. Tafuta mwanamke mature ambae utampenda ukiwa na wewe mwenyewe mature, hayo mambo ya tulipendana toka shule ya vidudu wakati mwingine ni kujitesa na kujidanganya. Muache aende na wewe nenda kivyako na maisha yanaendelea kama kawaida, tena na hivi mnakaa mbali mbali ndio bomba kichizi wangu.

Anonymous said...

WEWEW KIJANA! Kwanza ulimfanya huyu binti akose hata mwelekeo kwa kuanza naye mapenzi akiwa mtoto asiye na maamuzi yoyote ya busara.Ulimbikiri huyu binyi akiwa dara la sita?? wewe jeuri kabisa!!

Je, ungemjaza mimba mambo yangekuweje?

Kwanza wewe mwenyewe ulianza kwa kusema huhitaji kuendelea na uhusiano naye,kibao kimegueka kwako ssa unalialia nini kama ulifikiri mazuri kwa mwenzio?

Unaonekana bado ni mtoto kifikra. hebu kwanza achana na mtoto wa watu na wewe nenda zako.msichana wa watu kajitahidi kuwa nawe, halafu wewe ukaanza ujeuri ulitazamia nini?

Nataka kukwambia kwamba sasa amekuwa na ana uamuzi wa busara, ameisha jua ukweli wa mambo.Mambo ya utoto yameisha huwezi kumdanganya hata kidogo.Pia ameona wengi na ameona mengi, hivyo duara lile ulilomzungushia amelikata baada ya kutoka nje ya eneo husika.Ulimfundisha ngono mwenyewe akiwa mtoto, sasa amekuwa anaijua mwenyewe kuitafuta na kuicheza.Sahau kurudi kwako kwani ulijikokea moto mwenyewe kuuzima huwezi.